Nyani Ngabu
Platinum Member
- May 15, 2006
- 92,239
- 113,612
Toka Freeman Mbowe atoke jela/ gerezani, ameshakutana na Rais Samia mara kadhaa sasa.
Bado sijui na sielewi kwa nini hasa wamekuwa wakikutana kutana.
Ni kweli kuwa Mbowe alikamatwa na kufungwa kimakosa.
Mtu yeyote aliye na chembe ya akili kwenye ubongo wake analijua hilo.
Kwenye nchi zilizostaarabika, mtu anayekamatwa na kufungwa kimakosa huwa anastahili kulipwa fidia ya usumbufu alioupata na muda alioupoteza.
Lakini nchi yetu hii iliyo ni jamhuri na ndizi, hakuna cha fidia. Unaswekwa jela kwa amri ya Rais, unatolewa kwa amri ya Rais. Halafu baadaye Rais huyo huyo anakuita nyumbani kwake ukanywe juisi na kutafuna karanga na biskuti, na wewe unaenda. Ngoma inaisha.
Kwa watu tulio wahalisia wa mambo na tusiopenda kuyafanya mambo marahisi yawe magumu, mara nyingi huwa tunapenda kufuata taratibu zilizopo.
Kwa msingi huo, mimi sioni sababu wala tija yoyote kwa hawa CHADEMA kukutana kutana na Rais mara kwa mara.
Kinachohitajika kwa sasa ni Rais na chama chake kilichopo madarakani kufuata tu katiba iliyopo, basi.
Kama katiba inayotumika sasa inaruhusu vyama vingi vya siasa viwepo na inaruhusu vyama hivyo kufanya shughuli zake nchini kwa mujibu wa sheria, basi na viachwe vifanye hizo shughuli.
Hakuna haja wala sababu ya kuvizuia. Katiba inaruhusu. Kwa nini wewe uende kinyume na katiba na kuvizuia?
Yaani kuna mambo mengine ni marahisi tu lakini baadhi ya watu hupenda kuyafanya yawe changamani.
Fuateni katiba. Acheni kuonea watu. Ni hivyo tu.
Lipi lililo gumu katika hayo?