Sio siri wanawake wanaongea sana

Sio siri wanawake wanaongea sana

Melki Wamatukio

JF-Expert Member
Joined
May 3, 2022
Posts
6,328
Reaction score
11,463
Kutokana na msongo wa mawazo nilionao, nikaona wacha nikajichanganye na watu ili kuepusha kujitundika kitanzi

Nimejikuta naweka kituo kwenye kijigenge kimoja kidogo dogo. Kulikuwa na bodaboda watatu ila mmoja wao alikuwa na tabia zisizo za kuigwa na mwanaume wa aina yoyote ile duniani. Maake pikipiki lake alilifunga vijiredio vidogo vidogo vinavyolia nyenze, yaani ni full makelele na muziki unaopigwa ni muziki wa uswazi. Boda mwingine anaongea na mpenzi wake kwa sauti ya juu, mwingine yuko busy kusogeza mbele boda lake, mara alirudishe, mara aliegemee, mara atake kuswaga watu miguu yao. Dah!

Pembeni yake kulikuwa na kijibanda cha vitafunwa (na ni jioni hapo), kulikuwa na wanawake watatu. Wanawake hao walizungumza kama wamepachikwa External Hard Disc kwenye koromelo zao. Yaani ni vururu, mwendo wa vuta nkuvute. Cha ajabu wao wanaelewana, plus zile nyenze za redio, wakafanania watu wanaotaka kugombana. Huwezi amini, hadi kufikia saa 2 usiku, muda naondoka pale still walikuwa kwenye mazungumzo tena ya kupayuka. Mazungumzo yasiyo na vituo, mpaka nikawa najiuliza, sasa hawa wanawake wameolewa na nani?

Leo ndo nimepata jibu la swali la hivi ni kwanini wanaume walio wengi wenye ndoa zao wanakesha bar
 
Anazidi kunipendeza huyo!, mkuu we nipe huyo utatafuta mwengine!
ntakutafutia mwingine huyu nataka nifike nae mbali.

Nilitaka kusahau, na haombi hela, hajawai niomba hela hata tangu tuwe marafiki maana tulianzia urafiki.
 
raha ya nyumba upate wakukuchangamsha ukirudi jioni unapewa pole,wajilia vyako afu unapewa ubuyu wa mtaa mzima ukitoka hapo lazima unenepe😂😂😂😂
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom