Sio siri mashekhe wa uamsho wamekamatwa kwa tuhuma za kuupinga Muungano wa Tanzania

Shocker

JF-Expert Member
Sep 15, 2012
1,946
3,820
Sio siri mashekhe wa uamsho wamekamatwa kwa tuhuma za kuuping Muungano wa Tanzania kuwa sio wa haki na unafaa kuangaliwa au kuvunjwa ni tuhuma zilizowapelekea kusota mahabusu au jela za Tanganyika aka Tanzania Bara(TZB).

Kuna kundi liliibuka la waTanganyika na kuja juu sana ndani ya bunge na kufikia kuwepo kwa kundi lililojulikana G58 kama sikosei na hatua zake zilifika mbali katika kutaka kuuipapatua Tanganyika ndani ya jinamizi la Muungano,bahati nzuri au mbaya Raisi wa wakati ule akalikanyaga lile kundi na kuzima harakati zao,hatukusikia kukamatwa wala kuitwa na kuvishwa kosa la ugaidi.

Je ni kwanini Mashhe waliokuwa ndani ya Taasisi iliyosajiliwa kisheria ya UAMSHO kukamatwa au kutekwa mmoja mmoja toka ilikuwa siri mpaka ikajulikana wametekwa, wakawekwa Unguja na si muda mrefu wakapelekwaTanganyika aka TZB eti wanahusika na mikakati ya kigaidi ,jambo ambalo hadi leo halijapatiwa ushahidi, tunajua ushahidi uliotolewa kiharakaharaka ulikwama mahakamani kwa kuwa uongo ulikuwa umevuka mipaka na kukosa mashiko.

Suali mbona wale kundi la wabunge wa bara hawakushitakiwa kwa kosa la ugaidi ?
 
Binadamu Mwenye nia njema hawezi shawishi nchi igawanyike bali irekebishe mahala anapoona kuna kasoro
Ni kweli ikiwa jibu lako limesibu suali lakini angalia vizuri ulete jibu muafaka sio unakurupuka. Hao wabunge wao walitaka nchi igawanyike au irekebishike ndio nikasema angalia suali?

Mashekhe wa uamsho ukiangalia mikutano yao utaowa walitaka Nchi irekebishike na sio bla bla walikuwa na hoja nzito dhidi ya haki na usawa katika Muungano,unajua kama Zanzzibai inaidai Serikali ya muungano?

Ikidai muzilipe ni ugaidi na kero ni nyingi tu,hivi wewe ukibeba kilo tano za sukari toka Dar kwenda Mtwara unazilipia iweje ukitoka Zanzibar iwe ni kesi ya uhujumu uchumi ?
 
Sio siri mashekhe wa uamsho wamekamatwa kwa tuhuma za kuuping Muungano wa Tanzania kuwa sio wa haki na unafaa kuangaliwa au kuvunjwa ni tuhuma zilizowapelekea kusota mahabusu au jela za Tanganyika aka Tanzania Bara(TZB)...
Wabunge hawakutaka kuvunja Muungano, walitaka Muungano wa serikali tatu.

Serikali ya Tanganyika, ya Zanzibar na ya Muungano.

Hili jambo hata Jaji Mkuu Mstaafu Francis Nyalali alilipendekeza katika ripoti yake, hivyo si jambo ambalo liko nje ya kuzungumzika au sheria.

Wangetaka kuvunja Muungano wangepewa kesi ya uhaini.
 
Sasa kama lengo lilikuwa ni kuukataa Muungano, kwa nini hawakuwashawishi nyinyi wafuasi wao kutumia njia sahihi za kujitenga na huo Muungano? Mfano kuandika Petition, nk.

Na badala yake wakahamasisha kuwafanyia vurugu watu wa imani tofauti! Ikiwemo kuwamwagia tindikali na kuchoma nyumba zao za ibada?
 
Ni kweli ikiwa jibu lako limesibu suali lakini angalia vizuri ulete jibu muafaka sio unakurupuka. Hao wabunge wao walitaka nchi igawanyike au irekebishike ndio nikasema angalia suali...
Sijakurupuka nimekujibu kwa kuzingatia kuna vitu vingi havijulikani wazi ktk hao mashekhe na serikali na haviwezi kuwekwa wazi, Hata hao wabunge wenyewe wanajua vitu Vidogo sana, ndio maana miswaada ikipelekwa kwao wanapitisha baadae wanakuja kulalamika tena kwa wananchi na wamepitisha wenyewe.

Hakuna raia mwenye uhakika na hayo madeni, na kama yapo kwanini Maraisi wasitatue na wako pamoja? kuna kodi ni kero kwa nchi nzima na watu wamekua wakilalamika kwa miaka mingi, hilo tatizo ni la Kitaifa na Raisi amesema analiondoa.

Ushirika siku zote ni mzuri kuliko utengano, ila kama hawana kosa wanapaswa kuachiwa, ndio maana watu wanadai kuondolewa kwa sheria kandamizi na zisizojali haki za watu,
 
Sio siri mashekhe wa uamsho wamekamatwa kwa tuhuma za kuuping Muungano wa Tanzania kuwa sio wa haki na unafaa kuangaliwa au kuvunjwa ni tuhuma zilizowapelekea kusota mahabusu au jela za Tanganyika aka Tanzania Bara(TZB)....
Hao ni magaidi ingawa siyo wa dhati ila wa kutafuta pesa kutoka nje kwa jina ka uislam.
 
Sio siri mashekhe wa uamsho wamekamatwa kwa tuhuma za kuuping Muungano wa Tanzania kuwa sio wa haki na unafaa kuangaliwa au kuvunjwa ni tuhuma zilizowapelekea kusota mahabusu au jela za Tanganyika aka Tanzania Bara(TZB)...
Kwani uliona mzenj yoyote kumwagiwa tindi kali wala wageni watalii? Mbona toka wameshikwa hali ni SHWARI. SIKU NYINGINE USIJITOE UFAHAMU.
 
Sio siri mashekhe wa uamsho wamekamatwa kwa tuhuma za kuuping Muungano wa Tanzania kuwa sio wa haki na unafaa kuangaliwa au kuvunjwa ni tuhuma zilizowapelekea kusota mahabusu au jela za Tanganyika aka Tanzania Bara(TZB)....
Kuweka rekodi sawa,G55 ilifanikiwa kulishawishi bunge kuazimia iundwe serikali ya Tanganyika.Aliyezima azimio hilo hakuwa rais bali mwalimu Julius K. Nyerere kwa hoja kwamba hiyo,haikuwa sera ya CCM.
 
Sio siri mashekhe wa uamsho wamekamatwa kwa tuhuma za kuuping Muungano wa Tanzania kuwa sio wa haki na unafaa kuangaliwa au kuvunjwa ni tuhuma zilizowapelekea kusota mahabusu au jela za Tanganyika aka Tanzania Bara(TZB)...
Mkuu jua unaongea haya kwa sababu ya serikali ya muungano, bila serikali ya Muungano hakuna Zanzibar bali kutakuwa na Unguja na Pemba na kwa tabia zenu ugomvi wenu utakuwa hauishi na matokeo yake itakuwa kutusumbua tena wabara kwa kutujazia wakimbizi.

Bila Muungano musingejazana huku bara, kama unaona Muungano hauna faida waambie viongozi wako wawachukue wazanzibar wenzenu waliorundikana bara na si ajabu hata wewe mwenyewe unaishi Tandika wakati kwenu ni Pemba.

Je, umeona wabara wangapi wanaishi huko kwenu?
 
Sio siri mashekhe wa uamsho wamekamatwa kwa tuhuma za kuuping Muungano wa Tanzania kuwa sio wa haki na unafaa kuangaliwa au kuvunjwa ni tuhuma zilizowapelekea kusota mahabusu au jela za Tanganyika aka Tanzania Bara(TZB)....
Wabunge hawakuhamasisha kuwauwa wazanzibar wakati wanadai serikali ya tanganyika.

Sent from my TECNO RA7 using JamiiForums mobile app
 
Sio siri mashekhe wa uamsho wamekamatwa kwa tuhuma za kuuping Muungano wa Tanzania kuwa sio wa haki na unafaa kuangaliwa au kuvunjwa ni tuhuma zilizowapelekea kusota mahabusu au jela za Tanganyika aka Tanzania Bara(TZB).

Kuna kundi liliibuka la waTanganyika na kuja juu sana ndani ya bunge na kufikia kuwepo kwa kundi lililojulikana G58 kama sikosei na hatua zake zilifika mbali katika kutaka kuuipapatua Tanganyika ndani ya jinamizi la Muungano,bahati nzuri au mbaya Raisi wa wakati ule akalikanyaga lile kundi na kuzima harakati zao,hatukusikia kukamatwa wala kuitwa na kuvishwa kosa la ugaidi.

Je ni kwanini Mashhe waliokuwa ndani ya Taasisi iliyosajiliwa kisheria ya UAMSHO kukamatwa au kutekwa mmoja mmoja toka ilikuwa siri mpaka ikajulikana wametekwa, wakawekwa Unguja na si muda mrefu wakapelekwaTanganyika aka TZB eti wanahusika na mikakati ya kigaidi ,jambo ambalo hadi leo halijapatiwa ushahidi, tunajua ushahidi uliotolewa kiharakaharaka ulikwama mahakamani kwa kuwa uongo ulikuwa umevuka mipaka na kukosa mashiko.

Suali mbona wale kundi la wabunge wa bara hawakushitakiwa kwa kosa la ugaidi ?
Huu ndio ukweli unaofichwa
 
Hao magaidi walishindwaje kujiongeza wakaenda huko Calbo Delgado kwa mazezeta wenzao
 
Kuweka rekodi sawa,G55 ilifanikiwa kulishawishi bunge kuazimia iundwe serikali ya Tanganyika.Aliyezima azimio hilo hakuwa rais bali mwalimu Julius K. Nyerere kwa hoja kwamba hiyo,haikuwa sera ya CCM.
Uko sahihi, nakumbuka 1993 pale IFM ndipo kikao kilifanyika chini ya Mwalimu Nyerere na akazima hoja ya G55 na ndio sababu ya JKN kumchukia PM Malecela.

Sent from my TECNO RA7 using JamiiForums mobile app
 
Tuwaachie mahakama waamue,its too late kutuletea uzi kama hui kipindi hiki.
Tumetoka kwenye stress za LUKU,tuache kwanza kidogo tupumzike.
 
Back
Top Bottom