Getrude Mollel
JF-Expert Member
- Apr 26, 2022
- 259
- 353
Serikali imetenga Bil 150 kugharamia ruzuku ya mbolea itakayotolewa kwa wakulima nchini kwa ajili ya kupunguzwa makali ya bei ya mbolea. Rais Samia Suluhu Hassan anatarajiwa kuzindua mpango wa utoaji wa ruzuku ya mbolea katika kilele cha maonyesho ya Nanenane, yatakayofanyika mkoani Mbeya.
Mkurugenzi Mtendaji wa Mamlaka ya Udhibiti wa Mbolea Tanzania (TFRA) Dkt. Stephen Ngailo, alisema ruzuku hiyo, itasaidia wakulima kuongeza uzalishaji wenye tija kwenye kilimo. Pia ruzuku hiyo itasaidia wakulima kuimarisha usalama wa chakula na kuongeza upatikanaji wa malighafi za viwanda vya ndani.
Mbolea ambazo zitatolewa kwa ruzuku ni kwa ajili ya kupandia na kukuzia, aina nyingine za kupandia na kukuzia, zitahusishwa katika ruzuku kulingana na mahitaji ya soko.