MamaSamia2025
JF-Expert Member
- Mar 29, 2012
- 10,221
- 22,295
Kwenye ahadi za mwanaCCM kuna ila inayosema, fitina kwangu mwiko na nitakuwa mkweli daima. Nikiwa kama mwanaCCM mwenye kadi iliyolipiwa ada nakataa kabisa mambo ya kinafiki na kudanganyana.
Miaka ya hivi karibuni kumejitokeza watu wengi sana wahamasishaji wa mafanikio (Motivational Speakers) ambao naona wanachofanya ni jema sana na ni msaada kwa nchi. Ila pia kumejitokeza mambo mengi yenye ukakasi kwenye shughuli za hawa watu.
Wengi wao pia ni jobless wanaoongea kwa kukopi wahamasishaji wa marekani hali ambayo inakosa uhalisia kwa mazingira ya nchi yetu. Hali ya maisha, utamaduni na mfumo wa maisha ya Tanzania una tofauti kubwa na kule USA hivyo mhamasishaji wa USA hawezi kuwa sawa na wa Tanzania.
Sasa shida inakuja mhamasishaji anapokuja na maneno ya kina Kiyosaki, Ben Carson na kuwaambia vijana wa Nanjilinji. Mwisho wa siku inakuwa sio hamasa bali kuwavuruga zaidi vijana.
Kilichonisukuma zaidi hadi kuandika uzi ni hii tabia ya kila Motivational Speaker kudai alipitia maisha magumu sana hadi kufika alipofika.
Tena wanaokera zaidi ni wale ambao kiuhalisia bado wana maisha magumu na kujikweza. Nitatoa mifano michache ya watanzania maarufu ambao motivation zao zimejaa utata na kukosa uhalisia.
1. MAJIZO: Huyu bosi wa EFM huwa anadai alikuwa anakosa hata hela ya kula enzi akiwa DJ ila akapambana na kufungua redio. Nikipiga thamani ya uwekezaji wake pale EFM na muda aliotumia kutoka U-DJ hadi kuwa mmiliki wa redio kubwa nchini hesabu zinakuwa zinakataa. Na kama ingekuwa hivyo basi Aboubakar Sadik aliyekuwa nae Kwafujo DJs angekuwa nae kashafungua redio au kitega uchumi kikubwa.
2. FRED VUNJABEI: Huyu kijana nae analeta ukakasi sana. Anadai ELIMU tu alichopewa na baba yake ambaye pia ni mfanyabishara mwenye mafanikio kwa ngazi ya Iringa. Lakini katika hali ya kushangaza anatuambia kabla ya kuuza nguo alikuwa mwajiriwa kama mhasibu huku akianza biashara za kwenda China wakati akiwa mwajiriwa. Pia anatuambia alishawahi kuwa muuza magari na kusafiri nchi nyingi. Katika hali ya kushangaza zaidi anadai alikuwa na mtaji mdogo sana ikabidi amchangie rafiki yake aanze kwanza biashara ambaye baada ya kufanikiwa ndo akampa Fred 20m. Huyu kijana nae aachane na mambo ya kusema alipambana sana.
3. MABINTI MAARUFU WENGI; Hili group lina watu wengi ndo maana nimeona niwataje kama group. Wengi wao wanashinda hotel za kitalii wakila bata na kuudanganya umma kwamba wamepambana sana kufikia hapo.
Nashauri Motivational Speakers wakaiga mfano wa Sugu, Mzee Mtei, Marehemu Mengi na Ruge ambao stori zao zimejaa uhalisia na kweli wanahamasisha.