Maisha sio mstari mnyoofu, kona zisikufanye utoke mchezoni

Feb 4, 2024
67
206
Kinachotutesa wengi ni kuishi kwa imani kuwa maisha ni mstari mnyoofu na hili sio tu tumelijenga sasa la hasha! Bali hata mifumo ya malezi inachangia hilo.

Kuna ambao wamelelewa kwa kuaminishwa kuwa vitu hupatikana kwa wakati ule watakao hivyo kufanya ukubwani watu wapate shida sana pindi wanapokutana na uhalisia wa maisha kuwa maisha sio mstari mnyoofu.

Utotoni tuliamini kwa ambao wamefika shule wengi waliamini shule ikiisha tu leo basi kesho wanapata ajira na wakipata ajira tu tayari wananunua nyumba, gari, kuoa/kuolewa na kufurahia maisha.

Hii nadharia ambayo inaonyesha kuwa maisha ni mstari mnyoofu lakini tukija kwenye michakato ya maisha ni wachache sana wanaopitia mstari mnyoofu na hata kama mambo yako yatakunyookea kwenye jambo moja basi kwenye jambo la pili mambo hayakuwa na unyoofu.

Utotoni ilikuwa kila ukililia kitu unapewa kwa wakati na hapa ndio mwanzo wa imani hiyo kuwa maisha ni mstari mnyoofu ilipoanzia ambayo ipo kinyume na uhalisia wa maisha.

Maisha sio mstari mnyoofu na kuwa hivi haimaanishi kwamba ni changamoto bali ndio uhalisia wenyewe ambao unatakiwa kupambana nao na sio kujiona mtu mwenye mikosi kwa sababu tu umemaliza shule na kukaa mtaani miaka mitano bila kazi, umeachika kwa mchumba uliyempenda au umeanza kazi tu unataka kila kitu ununue kwa mshahara mmoja hilo haliwezekani na ukitaka liwezekane basi utajikuta gerezani.

Kuna ambao wanaanza mahusiano yao ya kwanza na yanageuka ndoa ila kuna wengi ambao wanapitia dhoruba kadhaa za kuachika ndio baadaye zinakuja ndoa.

Kuna muda maisha
yanakupitisha sehemu ambayo hapo zamani ulijua wanaopitia humo wana dhambi kumbe ni mapito tu kuwa maisha sio mstari mnyoofu bali kuna kona nyingi za kukomaa nazo.

Kuna wanaomaliza vyuo na kupata ajira ila kwa zama hizi kuna mtu mpaka kasahau kuwa na yeye alisoma chuo kwa sababu ana miaka mingi mtaani. Kumaliza chuo na kukosa ajira haimaanishi kuwa maisha ndio yamefikia ukomo bali hiyo ni kona ambayo unafaa ukomae nayo na hapo ndipo ujuzi wako wa udereva unapimwa.

Dereva mzuri haogopi kona za bara bara, ukiona dereva anataka tu apite barabara tambarare na kukwepa kila barabara yenye kona basi kuna shida kwenye ujuzi wake tena cheti chake kichunguzwe na vivyo hivyo hata kwenye harakati za maisha kama unataka kila jambo lako lisiwe na kona basi haya maisha yatakushinda kwa sababu kuna muda utajua kesho utapata ila unakuja kupata kesho kutwa .

Makala hii imeandikwa na Mwanasayansi Saul kalivubha.
 
MAISHA SIO MSTARI MNYOOFU, KONA ZISIKUFANYE UTOKE MCHEZONI.

Kinachotutesa wengi ni kuishi kwa imani kuwa maisha ni mstari mnyoofu na hili sio tu tumelijenga sasa la hasha! Bali hata mifumo ya malezi inachangia hilo.

Kuna ambao wamelelewa kwa kuaminishwa kuwa vitu hupatikana kwa wakati ule watakao hivyo kufanya ukubwani watu wapate shida sana pindi wanapokutana na uhalisia wa maisha kuwa maisha sio mstari mnyoofu.

Utotoni tuliamini kwa ambao wamefika shule wengi waliamini shule ikiisha tu leo basi kesho wanapata ajira na wakipata ajira tu tayari wananunua nyumba, gari, kuoa/kuolewa na kufurahia maisha.

Hii nadharia ambayo inaonyesha kuwa maisha ni mstari mnyoofu lakini tukija kwenye michakato ya maisha ni wachache sana wanaopitia mstari mnyoofu na hata kama mambo yako yatakunyookea kwenye jambo moja basi kwenye jambo la pili mambo hayakuwa na unyoofu.

Utotoni ilikuwa kila ukililia kitu unapewa kwa wakati na hapa ndio mwanzo wa imani hiyo kuwa maisha ni mstari mnyoofu ilipoanzia ambayo ipo kinyume na uhalisia wa maisha.

Maisha sio mstari mnyoofu na kuwa hivi haimaanishi kwamba ni changamoto bali ndio uhalisia wenyewe ambao unatakiwa kupambana nao na sio kujiona mtu mwenye mikosi kwa sababu tu umemaliza shule na kukaa mtaani miaka mitano bila kazi, umeachika kwa mchumba uliyempenda au umeanza kazi tu unataka kila kitu ununue kwa mshahara mmoja hilo haliwezekani na ukitaka liwezekane basi utajikuta gerezani.

Kuna ambao wanaanza mahusiano yao ya kwanza na yanageuka ndoa ila kuna wengi ambao wanapitia dhoruba kadhaa za kuachika ndio baadaye zinakuja ndoa.

Kuna muda maisha yanakupitisha sehemu ambayo hapo zamani ulijua wanaopitia humo wana dhambi kumbe ni mapito tu kuwa maisha sio mstari mnyoofu bali kuna kona nyingi za kukomaa nazo.

Kuna wanaomaliza vyuo na kupata ajira ila kwa zama hizi kuna mtu mpaka kasahau kuwa na yeye alisoma chuo kwa sababu ana miaka mingi mtaani. Kumaliza chuo na kukosa ajira haimaanishi kuwa maisha ndio yamefikia ukomo bali hiyo ni kona ambayo unafaa ukomae nayo na hapo ndipo ujuzi wako wa udereva unapimwa.

Dereva mzuri haogopi kona za bara bara, ukiona dereva anataka tu apite barabara tambarare na kukwepa kila barabara yenye kona basi kuna shida kwenye ujuzi wake tena cheti chake kichunguzwe na vivyo hivyo hata kwenye harakati za maisha kama unataka kila jambo lako lisiwe na kona basi haya maisha yatakushinda kwa sababu kuna muda utajua kesho utapata ila unakuja kupata kesho kutwa .

Makala hii imeandikwa na Mwanasayansi Saul kalivubha.
 
Kwel bwana, kuna kona moja nimepigishwa leo daah!!! Yan ndio j3 naingia mzigon nakutana na bonge ya bad news toka kwa mteja ofis nzima hoi!

Sema ndio vile nishakuaga sugu siku hiz, nikawaita vijana nikawaweka chini nikawambia sikiliza hii kitu ya kawaida tu anataka sawa hataki okay, lets focus.

Ila moyon roho inauma nahisi kuchanganyikiwa sema ndio hivyo huwez kuonyesha umepagawa mbele ya vijana wako unapiga hesabu how to recover from the situation

Mwanangu!!! Noma nomaaaa.

Ukiwa soft lazima utoke tu mchezoni 😂😂😂
 
Back
Top Bottom