Wengi wanaotaka wake zao wasifanye kazi wana upeo mdogo wa kufikiri halafu ni wabinafsi

Robert Heriel Mtibeli

JF-Expert Member
Mar 24, 2018
21,340
51,895
WENGI WANAOTAKA WAKE ZAO WASIFANYE KAZI WANAUPEO MDOGO WA KUFIKIRI ALAFU NI WABINAFSI

Anàandika, Robert Heriel
Mtibeli.

Chizi sio lazima uokote Makopo, kuna Chizi Fresh ambao ndio wengi wapo kundi hili tena wengine wasomi. Alafu kuna ambao ni Chizi Maarifa hawa wengi ukiwaona kwa mbali unaweza kudhani wako timamu lakini ukiwatazama kwa ukaribu ni wendawazimu.

Unakuta kajamaa kametoka familia Maskini, kameoa kutoka Familia Maskini. Kanafanya kazi iwe kwa kuajiriwa au kujiajiri lakini pato lake kwa mwezi hata Milioni moja halifiki.
Lakini ukikasikiliza mawazo yake kuhusu uchumi na mahusiano utabaki kuona kalivyo na upeo mdogo.

Yaani kisa umenunua mwanamke kwa bei ya jumla(kutoa mahari) labda shilingi milioni nne. Basi Mwanamke huyo ambaye sasa ataitwa mkeo unasema asifanye kazi kisa umemuoa.

Ukiulizwa kwa nini asifanye kazi? Huna hoja ya maana hata moja zaidi ya kutokujiamini, ubinafsi na ukandamizaji kama sio unyanyasaji.

Unamwambia mkeo asifanye kazi au asimiliki kipato kingi tena inafikia hatua kwa uzuzu wako unamhujumu mkeo na kumuwekea vikwazo ili asifanikiwe. Ati unaogopa atakunyanyasa ati atakuwa jeuri. Chizi weeeh!

Mkeo asifanye kazi, unapesa za kumhudumia mahitaji yake yote?
Alafu wengi wenye mtazamo kama huu unakuta Wake zao hata mafuta ya kupaka hawana, nguo wanazovaa mtumba, tena bora mtumba lakini ziwe nyingi. Lakini hata pesa ya kuwanunulia wake zao nguo walau kila mwezi nguo moja au mbili hawana. Mke kapauka, kazeeshwa. Yaani hatamaniki tena. Kila siku kumlisha mkeo Maharage kazi kujambajamba. Alafu unakuta jitu linasema linahudumia mke. Alafu halitaki mkewe afanye kazi. Ili angalau pesa ya kubadilisha chakula hapo nyumbani iwepo sio kila siku ugali na mchicha au maharage. Nyama na samaki mpaka sikukuu. Familia inapitisha Wiki hata maziwa hakuna. Alafu ulivyo chizi unaona sawa tuu. Alafu ukijaribu mtandaoni huku ooh! Mwanamke asifanye kazi utadhani umemudu mahitaji yake. Mwehu wewe!

Watoto wako ada zenyewe zinakusumbua, lishe yenyewe hawali. Utapiamlo na kifaduro kinawasumbua. Watoto mpaka imefikia hata uwezo wa kufikiri hawana Kwa sababu kila siku unawalisha chakula kingi cha wanga kama ugali, mihogo, maandazi na maujiuji ya nafaka. Ilhali kiafya watoto chini ya miaka 20 wanatakiwa kula protein nyingi kuliko kundi jingine la chakula ili miili yao ijengwe vyema. Vyakula vya protini ambavyo vinatakiwa viwe vingi katika mlo wenu hapo nyumbani ni Samaki, nyama, maharage, maziwa, mayai n.k.
Lakini kwa vile kipato chako ni duni huwezi kuhudumia hivyo. Alafu kwa vile tayari unakifaduro cha ubongo huoni kama unahitaji usaidizi na kwa ubinafsi wako unataka watoto wako nao wakose lishe kama wewe ulivyokosa. Ati mke asifanye kazi au asikusaidie majukumu. Kwa huduma gani unazotoa mwehu wewe!

Haya, mshahara wako wenyewe haukutoshi kutunza Wazazi wako.
Alafu hutaki mkeo asifanye kazi. Hivi unafikiri wazazi wake mwanamke watahudumiwa na kutunzwa na nani kama sio huyo mke wako. Mbuzi wewe.

Pesa yako hata milioni moja haifiki kwa mwezi. Unataka wadogo wa mkeo wahudumiwe na nani?
Unataka ile nyumba ya wazazi wa mkeo ifanyiwe ukarabati na nani kama sio mkeo.

Alafu haya machizi Fresh hapohapo unayasikia yakisema, usijenge Ukweni, mara Usitoe pesa Ukweni. Alafu hapohapo unayakuta yanazuia Wake zao wasifanye kazi. Hivi kama sio Ushetani na laana hizo ni kitu gani? Hivi kuna ubinafsi na ukatili wa kutisha zaidi ya huo?

Bado umfulishe na kumfanyisha makazi mengi bila kumpa lishe bora. Zaidi ya hapo umpige kisa ameona mambo sio mambo na umemgeuza msukule wake hapo.

Embu acheni Upumbavu wenu.
Ni mara elfu Mwanamke asioelewe au awe single Mother alee Watoto wake kitabutabu kuliko kuishi na mwanaume mwenye Ushetani wa namna hiyo.

Mwanaume elewa kuwa kama wewe unavyopenda na kuhitaji kuhudumia Wazazi wako ndio hivyohivyo mkeo naye anataka wazazi wake wahudumiwe.

Na ndio maana Watibeli Hawatoi Mahari kwa sababu inaharufu ya manunuzi au biashara ya binadamu kwa visingizio vya kishetani.

Hutaki mkeo afanye kazi alafu ukiombwa pesa ya kuwasomesha wadogo zake unapiga yowe na kulalamika. Wewe mwehu nini.

Na mimi nawaambia Wanawake hasa Watibeli ni lazima wafanyekazi. Kufanya kazi ni amri ya kila kiumbe ili kiwe huru na kujitegemea chenyewe. Binadamu asiyefanya kazi ni mfu.
Mtu mwenye akili na Mwanamke kamili na mke mwema hujisikia aibu na fedheha kumtegemea mumewe kwa kila kitu.

Mimi nimemaliza.

Robert Heriel
Taikon wa Fasihi
Kwa sasa Dar es salaam
 
Mwanamke ni pambo hatakiwa kufanya kazi yeyote zaidi yakumburudisha mume wake.

Ukishamuoa mwanamke amebadili koo, kutoka ukoo wao kuja upande wa mume, ndio maana wengine hubadili mpaka majina ya wazazi wao.

Baada yakumuoa apaswa kufata Sheria na taratibu za upande wa mumewe, hayo yakuhudumia ndugu zake sijui wadogo zake nimambo ya ziada. Mnapooana jukumu kubwa nilakuangalia familia yenu nyinyi wawili nakujenga mpango mkakati wa watoto wenu baadae waishije. Kila mtu akianza kuhudumia nakutoa kipaumbele kwao hapatakua na familia tena.

Kila mtu ajenge kwao, Kila mtu awe anatuma hela kwao, kwenu nyie wawili mtapajenga lini?.

Mwanamke akikubali kuolewa basi ajue na atambue anaenda kufata taratibu na Sheria za mumewe kama hayupo tayari basi asikubali kuolewa.

Sisi wengine tunaamini hata kama niko wrong basi mwanamke anafaa kunisikiliza na kutii nilichokisema.

Ndio maana Koo nyingine wanaume hawali chakula sehemu Moja na wanawake jiulize Kwa nini?. Hili nikuwafunza watoto wakiume na kike Kila mtu kujua majukumu ya baba yake na mama yake niyapi , na namna mwanamke anavyopaswa kumtii na kumuandalia chakula mumewe.

Majukumu yamwanamke ndani ya nyumba yanafahamika na majukum ya mwanamme ndani ya nyumba yanafahamika, Sasa ukitaka kila upande uingilie majukumu ya nwenzake hapatotosha, ndio maana familia nyingi zinaparaganyika Kwa Kila upande kuona unaweza kuhimili kufanya majukumu ya mwenzake.

Kila mtu aishi nakufanya yale ambayo anatakiwa kufanya nakutekeleza majukumu yake.

Nakipindi unaoa au kuolewa basi mwenzi wako ajue lengo ni nini hasa, mimi nikitaka kuoa basi lengo nimke wangu aagalie watoto basi, mengi kama yakija basi niyaziada. Lakini lengo kuu lazima hata yeye alifahamu Kwa mantiki kwamba anaolewa kuja kuwa mama wa nyumbani.
 
Usiwalaumu Mkuu,tatizo ni matokeo mabaya yanayokuja baada ya mwanamke kufanya kazi......wengi Juan za kutokusikiliza mume,kiburi,kujilinganisha,kumshusha thamani mume na kurudi home muda atakao

Ipo sababu ya wao kufanya hivyo.
Wanaume waliowengi wake zao wakifanya kazi huanza kujiona duni. Na kuanza kuleta chokochoko kwa Wake zao. Ni kama wanamiliki mtu mwingine wakati ni Watu wawili huru walioamua kuungana tuu.

Wewe mwanaume ambaye hajielewi utaweza kumheshimu?
 
WENGI WANAOTAKA WAKE ZAO WASIFANYE KAZI WANAUPEO MDOGO WA KUFIKIRI ALAFU NI WABINAFSI

Anàandika, Robert Heriel
Mtibeli.

Chizi sio lazima uokote Makopo, kuna Chizi Fresh ambao ndio wengi wapo kundi hili tena wengine wasomi. Alafu kuna ambao ni Chizi Maarifa hawa wengi ukiwaona kwa mbali unaweza kudhani wako timamu lakini ukiwatazama kwa ukaribu ni wendawazimu.

Unakuta kajamaa kametoka familia Maskini, kameoa kutoka Familia Maskini. Kanafanya kazi iwe kwa kuajiriwa au kujiajiri lakini pato lake kwa mwezi hata Milioni moja halifiki.
Lakini ukikasikiliza mawazo yake kuhusu uchumi na mahusiano utabaki kuona kalivyo na upeo mdogo.

Yaani kisa umenunua mwanamke kwa bei ya jumla(kutoa mahari) labda shilingi milioni nne. Basi Mwanamke huyo ambaye sasa ataitwa mkeo unasema asifanye kazi kisa umemuoa.

Ukiulizwa kwa nini asifanye kazi? Huna hoja ya maana hata moja zaidi ya kutokujiamini, ubinafsi na ukandamizaji kama sio unyanyasaji.

Unamwambia mkeo asifanye kazi au asimiliki kipato kingi tena inafikia hatua kwa uzuzu wako unamhujumu mkeo na kumuwekea vikwazo ili asifanikiwe. Ati unaogopa atakunyanyasa ati atakuwa jeuri. Chizi weeeh!

Mkeo asifanye kazi, unapesa za kumhudumia mahitaji yake yote?
Alafu wengi wenye mtazamo kama huu unakuta Wake zao hata mafuta ya kupaka hawana, nguo wanazovaa mtumba, tena bora mtumba lakini ziwe nyingi. Lakini hata pesa ya kuwanunulia wake zao nguo walau kila mwezi nguo moja au mbili hawana. Mke kapauka, kazeeshwa. Yaani hatamaniki tena. Kila siku kumlisha mkeo Maharage kazi kujambajamba. Alafu unakuta jitu linasema linahudumia mke. Alafu halitaki mkewe afanye kazi. Ili angalau pesa ya kubadilisha chakula hapo nyumbani iwepo sio kila siku ugali na mchicha au maharage. Nyama na samaki mpaka sikukuu. Familia inapitisha Wiki hata maziwa hakuna. Alafu ulivyo chizi unaona sawa tuu. Alafu ukijaribu mtandaoni huku ooh! Mwanamke asifanye kazi utadhani umemudu mahitaji yake. Mwehu wewe!

Watoto wako ada zenyewe zinakusumbua, lishe yenyewe hawali. Utapiamlo na kifaduro kinawasumbua. Watoto mpaka imefikia hata uwezo wa kufikiri hawana Kwa sababu kila siku unawalisha chakula kingi cha wanga kama ugali, mihogo, maandazi na maujiuji ya nafaka. Ilhali kiafya watoto chini ya miaka 20 wanatakiwa kula protein nyingi kuliko kundi jingine la chakula ili miili yao ijengwe vyema. Vyakula vya protini ambavyo vinatakiwa viwe vingi katika mlo wenu hapo nyumbani ni Samaki, nyama, maharage, maziwa, mayai n.k.
Lakini kwa vile kipato chako ni duni huwezi kuhudumia hivyo. Alafu kwa vile tayari unakifaduro cha ubongo huoni kama unahitaji usaidizi na kwa ubinafsi wako unataka watoto wako nao wakose lishe kama wewe ulivyokosa. Ati mke asifanye kazi au asikusaidie majukumu. Kwa huduma gani unazotoa mwehu wewe!

Haya, mshahara wako wenyewe haukutoshi kutunza Wazazi wako.
Alafu hutaki mkeo asifanye kazi. Hivi unafikiri wazazi wake mwanamke watahudumiwa na kutunzwa na nani kama sio huyo mke wako. Mbuzi wewe.

Pesa yako hata milioni moja haifiki kwa mwezi. Unataka wadogo wa mkeo wahudumiwe na nani?
Unataka ile nyumba ya wazazi wa mkeo ifanyiwe ukarabati na nani kama sio mkeo.

Alafu haya machizi Fresh hapohapo unayasikia yakisema, usijenge Ukweni, mara Usitoe pesa Ukweni. Alafu hapohapo unayakuta yanazuia Wake zao wasifanye kazi. Hivi kama sio Ushetani na laana hizo ni kitu gani? Hivi kuna ubinafsi na ukatili wa kutisha zaidi ya huo?

Bado umfulishe na kumfanyisha makazi mengi bila kumpa lishe bora. Zaidi ya hapo umpige kisa ameona mambo sio mambo na umemgeuza msukule wake hapo.

Embu acheni Upumbavu wenu.
Ni mara elfu Mwanamke asioelewe au awe single Mother alee Watoto wake kitabutabu kuliko kuishi na mwanaume mwenye Ushetani wa namna hiyo.

Mwanaume elewa kuwa kama wewe unavyopenda na kuhitaji kuhudumia Wazazi wako ndio hivyohivyo mkeo naye anataka wazazi wake wahudumiwe.

Na ndio maana Watibeli Hawatoi Mahari kwa sababu inaharufu ya manunuzi au biashara ya binadamu kwa visingizio vya kishetani.

Hutaki mkeo afanye kazi alafu ukiombwa pesa ya kuwasomesha wadogo zake unapiga yowe na kulalamika. Wewe mwehu nini.

Na mimi nawaambia Wanawake hasa Watibeli ni lazima wafanyekazi. Kufanya kazi ni amri ya kila kiumbe ili kiwe huru na kujitegemea chenyewe. Binadamu asiyefanya kazi ni mfu.
Mtu mwenye akili na Mwanamke kamili na mke mwema hujisikia aibu na fedheha kumtegemea mumewe kwa kila kitu.

Mimi nimemaliza.

Robert Heriel
Taikon wa Fasihi
Kwa sasa Dar es salaam
Mlete mkeo afanye kazi ofisini kwangu
 
wanaume wengi tusichojua ni kwamba hawa wanawake hasa walio ndani ya ndoa Mungu hajawahi kuwaacha wana bahati za biashara wanaijua mipango na mikakati ya kutoboa.....
ukipata mtu sahihi hutajutia ukiwekeza biashara itatiki akiajiriwa utaona kipato chake kinavyoleta mae deleo watoto wako hawatateseka..... mimi kuna muda ninacharara ila cha ajabu wife nakuja kuweka mambo sawa nabaki kisema Mungu asante maana msipokua na vipato ukajitegemeza mwanaume tu kuanguka ni rahisi na muda mwingine wanaliwa kwa kukosa uhuru wa kuchangia kwenye familia....

mpe pesa kama ana akili atazifanyia cha maana na tukumbuke akili za mwanamke zinaakisi ubora na uimara wa mwanaume...

kamwe ukikita mtu anamkataza mkewe kufanya kazi angalia maisha yake kuna raha fulani haipati.

nb: sikulazimishi kukubali mkeo afanye kazi angalia mazingira uliompata kama ulimpata kwa kuhonga na kutumia nguvu nyingi pima akili yake sio kila mwanamke ana utha iti na misimamo muangalie wako je anajiweza au anagombewa kama mpira wa kono....
 
Kwani akifanya kazi hawezi kuwa pambo au kumburudisha mumewe?

Kuna wanawake wanaofanya kazi na bado ni warembo kuliko wanaokalizwa nyumbani.
Hoja yako haina mashiko
Hoja inamashiko vizuri, ukitaka lakini wewe unaamua kutoipa mashiko, ukitaka muishi vizuri na mkeo basi muishi Kwa kufata maandiko hasa kama mnaamini katika Imani. Mambo mengine yakimaisha ni Qadar tu, mnaweza kupambana wote lkn still mklala njaa.
 
wanaume wengi tusichojua ni kwamba hawa wanawake hasa walio ndani ya ndoa Mungu hajawahi kuwaacha wana bahati za biashara wanaijua mipango na mikakati ya kutoboa.....
ukipata mtu sahihi hutajutia ukiwekeza biashara itatiki akiajiriwa utaona kipato chake kinavyoleta mae deleo watoto wako hawatateseka..... mimi kuna muda ninacharara ila cha ajabu wife nakuja kuweka mambo sawa nabaki kisema Mungu asante maana msipokua na vipato ukajitegemeza mwanaume tu kuanguka ni rahisi na muda mwingine wanaliwa kwa kukosa uhuru wa kuchangia kwenye familia....

mpe pesa kama ana akili atazifanyia cha maana na tukumbuke akili za mwanamke zinaakisi ubora na uimara wa mwanaume...

kamwe ukikita mtu anamkataza mkewe kufanya kazi angalia maisha yake kuna raha fulani haipati.

nb: sikulazimishi kukubali mkeo afanye kazi angalia mazingira uliompata kama ulimpata kwa kuhonga na kutumia nguvu nyingi pima akili yake sio kila mwanamke ana utha iti na misimamo muangalie wako je anajiweza au anagombewa kama mpira wa kono....
Nina mifano hao miwili nakuunga mkono...Father mdogo idea za biashara zake kapewa na mkewe sasa ni billionaire,nina brother nae anamsikiliza sana mkewe kweny biashara yupo mbali sana..

Wanawake ukiwashirikisha mipango yao tena yule mke halali kuna 80% chance ya kufika mbali ...Hata mzee wangu alijenga kupitia mama kwa biashara ndogo ndogo

Tatizo ,mifumo ya familia nyingi upande wa mume wanamfanya mke kama adui wao ,hawataki awe sehemu ya mipango ya mtoto wao(mume) japo kuna ndoa...

Hilo suala naunga mkono hata ukifuatilia matajiri wengi ndio wamefanikiwa hivyo ndio ule msem " Nyuma ya kila mwanaume aliyefanikiwa kuna mwanamke"
 
Back
Top Bottom