Sio kila busu linamaanisha upendo, mengine yanawakilisha usaliti

Mr George Francis

Senior Member
Jun 27, 2022
186
212
BUSU ni ishara moja wapo inayoonesha upendo, mahaba salamu au heshima.

Kama neno la Mungu linavyosema..
"Salimianeni kwa busu la upendo. Amani na iwe kwenu nyote, mlio katika Kristo. Amina."
1 PETRO 5:14

Na watu wengi huwa tunajiskia raha na kuwa na furaha tunapopata BUSU kutoka kwa watu tunaowapenda.

Kupigwa BUSU raha jamani! Sulemani anasema,
"Kubusu na anibusu kwa kinywa chake. Maana pambaja zako zapita divai."
WIMBO ULIO BORA 1:2

Lakini sio malazote BUSU linamaanisha upendo, wakati mwingine linaweza kubeba dhana ya USALITI.

USALITI ni kitendo cha kukosa uaminifu kwa makusudi. Yaani mtu au watu wako wa karibu unaowaamini kutoa siri jambo lako la siri kwa adui.

Upo usaliti baina ya marafiki, mpenzi (mume/mke), ndugu, wafanyakazi wenzako au watu wowote wa karibu.

Mtu unayelala naye au kula naye chakula anaweza kukusaliti.
Neno la Mungu linasema..
" Naye alipokwisha kusema hayo, Yesu alifadhaika rohoni, akashuhudia akisema, Amin, amin, nawaambieni, Mmoja wenu ATANISALITI."
YOHANA 13:21

Yesu anaendelea kusema,
"Basi Yesu akajibu, Ndiye mtu yule nitakayemtowelea tonge na kumpa. Akatowelea tonge, akalitwaa akampa Yuda, mwana wa Simoni Iskariote."
YOHANA 13:26

Hapa tunaona kuwa Yuda ambaye alikuwa mwanafunzi anayeaminika anatajwa kuwa atamsaliti Yesu.

Neno linasema,
"Basi alipokuwa katika kusema, tazama, mkutano wa watu, na yule aitwaye Yuda, ambaye ni mmoja wa wale Thenashara, amewatangulia. Akamkaribia Yesu ili KUMBUSU.

Yesu akamwambia, Yuda, wamsaliti Mwana wa Adamu kwa KUMBUSU?
LUKA 22:47-48

Hivi ndivyo ilivyo hata katika maisha yetu ya kila siku. Kuna watu tunaishi nao kwa muda mrefu kama ndugu, mpenzi au rafiki kumbe moyoni mwake anapanga kukusaliti na kukuumiza.

Ishi na watu vizuri lakini KUWA NAO MAKINI. Lakini laana ya USALITI haitakuacha salama kama ilivyomtesa YUDA hadi kuamua kujiua.

Neno la Mungu linasema,
"Akavitupa vile vipande vya fedha katika hekalu, akaondoka; akaenda, akajinyonga."

USALITI unaweza kupoteza kabisa hatima yako njema katika dunia.

Jifunze kuwa mwaminifu kwa Mungu na kwa watu wote.

NENO LA BWANA.

#No_learning_No_earning
So we have to Learn

Prepared By
Mr George Francis
Contact: 0713736006
Email: mr.georgefrancis21@gmail.com
 
Back
Top Bottom