Mr George Francis
Senior Member
- Jun 27, 2022
- 186
- 212
Mwanaume unayetarajia kuoa au ambaye umeshaoa, pamoja na majukumu mengi uliyonayo, lakini unapaswa kukumbuka kuwa wazazi na ndugu zako bado wanaishi.
Neno la Mungu linasema,
MWANZO 2:24
"Kwa hiyo mwanamume ATAMWACHA baba yake na mama yake naye ATAAMBATANA na mkewe, nao watakuwa MWILI MMOJA."
MATHAYO 19:5
"Akasema, Kwa sababu hiyo, mtu ATAMWACHA babaye na mamaye, ATAAMBATANA na mkewe; na hao wawili watakuwa MWILI MMOJA?"
MARKO 10:7-8
"Kwa sababu hiyo mtu ATAMWACHA babaye na mamaye, ATAAMBATANA na mkewe;
na hao wawili watakuwa MWILI MMOJA; hata wamekuwa si wawili tena, bali MWILI MMOJA."
WAEFESO 5:31
"Kwa sababu hiyo mtu ATAMWACHA baba yake na mama yake, ATAAMBATANA na mkewe na hao wawili watakuwa MWILI MMOJA."
Neno 'KUWAACHA' wazazi wako haina maana kwamba 'UWATELEKEZE' wazazi wako wala ndugu zako.
Mwanaume unapotimiza jukumu lako la kwanza kwa mke na watoto wako, usisahau pia kusaidia wazazi na ndugu zako.
Neno linasema,
"......, na wajifunze kwanza kuyatenda yaliyo wajibu wao kwa jamaa zao wenyewe, na kuwalipa wazazi wao. Kwa kuwa hili linakubalika mbele za Mungu."
1 TIMOTHEO 5:4
Upendo wako kwa wazazi na ndugu zako uendelee kudumu siku zote.
Neno linasema,
"Upendo wa ndugu na udumu."
WAEBRANIA 13:1
"Yeye ampendaye ndugu yake akaa katika nuru, wala ndani yake hamna kikwazo."
1 PETRO 2:17
Usiwaache wazazi na ndugu zako wakiteseka kwa njaa, eti kwa kigezo kuwa shida zao hazikuhusu. Hapo utamkosea Mwenyezi Mungu.
Ndoa yako itajawa na baraka kama itakuwa ni kiunganishi kizuri cha undugu kati ya upande wa mume na upande wa mke.
Na nyote mkiishi kwa upendo, furaha na amani. Mtu awaye yote asiwe sababu ya utengano kati yenu.
Kama ilivyo kwa mwanaume, mke pia uyashike mafundisho haya. Majukumu ya familia yako, yasikufanye usahau kuwa wazazi na ndugu zako bado wanaishi.
Mungu awabariki sana.
#No_learnig_No_earning
So we have to Learn.
Prepared By
Mr George Francis
Contact: 0713736006
Email: mr.georgefrancis21@gmail.com