Sio fair, Wanaoshinikiza Rais Mama Samia afikiri kama Magufuli sio uungwana

Azizi Mussa

Verified Member
May 9, 2012
8,789
2,000
Nashukuru Mungu kwamba angalau Tanzania ya hoja kwa hoja inarejea taratibu.

Kumeibuka kundi la watu linaloshinikiza Mhe. Rais Mama Samia afikiri kama Hayati magufuli. Haieleweki vyema kwa nini wanafikiri hivyo ila kimsingi sio fair kabisa.

1. Mzee Mwinyi hakufikiri kama Nyerere, Mzee Mkapa Hakufikiri kama Mwinyi, Mzee wetu Kikwete hakutumia akili ya Mkapa, Hayati Magufuli hakutumia akili ya Mzee Kikwete, sasa kwa nini tufikiri Mhe. Rais Mama Samia anatakiwa kufikiri kama Magufuli? Sio fair kabisa yani.

2. Kila mtu huzaliwa na uwezo wake wa kipekee na 'purpose' maalum kwenye hii dunia. Kwa lugha nyingine, Mungu kamleta kila mtu kwenye dunia hii ili kutimiza jukumu fulani na amempa uwezo unaomuwezesha kutimiza jukumu husika. Ndio maana tunatofautiana busara, hekima, uvumilivu, uungwana roho nzuri na mbaya e.tc. Hivyo kutaka Mh. Rais Mama Samia afikiri kama Magufuli sio fair Kabisa!

3. Kila mtu huzaliwa 'original'. Hivyo ili mtu aache 'legacy' ni lazima abaki kuwa 'original' wakati wote. Kutaka Mhe.Rais Mama Samia afikiri kama Hayati Magufuli, ni kutaka kushinikiza asiwe 'original ' na hiyo sio fair kabisa.

4. Moja ya kitu kibaya sana duniani ni utumwa. Na utumwa mbaya zaidi ni wa kifikira, yaani kutumia misimamo ya mtu mwingine balada ya kutumia experience na utashi kufikia conclusion binafsi. Sasa kwa nini Mhe. Rais Mama Samia ashinikizwe asiwe anatengeneza conclusion kutokana na utashi na experience yake mwenyewe? Hiyo sio fair kabisa

Hitimisho;

Tumpeni nafasi Mhe. Rais Mama Samia afanye vitu kulingana na dhamira, experience na utashi wake. Afikie conclusion zake yeye kama yeye maadam havunji katiba, sheria au kudhulumu mtu. Huo ndio uungwana.

Mungu alimuweka Hayati Magufuli ili afanye aliyoyafanya na yatokee yaliyotokea kwa sababu maalum. Kadhalika, Mungu kamuweka Mama Samia kuwa Rais ili atimize 'role' fulani muhimu kulingana na mipango ya Mungu. Ni vizuri akapewa nafasi ili atimize 'role' hiyo, badala ya kumshinikizwa ageuke kuwa copy ya mtu mwingine. Huo ndio uungwana.

Katika kipindi cha uongozi wake, atahukumiwa kwa atakayoyafanya yeye kama yeye, ataacha legacy kwa yale atakayoyafanya yeye, na mbele ya Mwenyezi Mungu ataulizwa yeye kama yeye kuwa alichunga nini hapa duniani wakati wa uongozi wake.

Tuweni waungwana, tusimpotoshe Mama. Mama ni mtu mzima, mwerevu na muungwana. Aachwe awe yeye kama yeye maadamu havunji Katiba,sheria wala kudhulumu mtu.

Ramadhan Njema.
 
Nyendeke

JF-Expert Member
Jul 21, 2013
1,531
2,000
Daaaa.., kwani kuna Jambo gani linaendelea huko au ndio mnatafuta namna ya kujiposition kwa Bi Mkubwa, mbona Mnazoza sana Bandugu???
 
Azizi Mussa

Verified Member
May 9, 2012
8,789
2,000
Daaaa.., kwani kuna Jambo gani linaendelea huko au ndio mnatafuta namna ya kujiposition kwa Bi Mkubwa, mbona Mnazoza sana Bandugu??
Mkuu, kwenye hii dunia, mtu hawezi kukumbukwa kwa kuimba wimbo ulioimbwa na msanii mwenzake. Hiyo haijalishi wimbo huo ni mzuri au mbaya. Labda kama anaimba kwa lengo la burudani tu lakini sio kuacha 'legacy'

Ili kuacha legacy inabidi kutunga na kuimba wako, hata kama unasema tu 'yoyoyoyo....." Lakini maadamu ni wako, watu watakukumbuka hivyo.

Ukiona wewe ni muimbaji halafu watu wanataka urudie nyimbo ambazo zishaimbwa na mtu mwingine, chukua tahadhari.
 
Waaai

JF-Expert Member
Jan 14, 2021
1,300

Mama ataacha legacy yake.
 
Ni kweli Mkuu.., lakini huyu Muimbaji wa sasa si ndio alikuwa anaimba chorus na bridge kwenye Wimbo aliokuwa anaimba Mtangulizi wake?
Sasa iweje unataka Wimbo ubadilike ikiwa yeye nae alikuwa sehemu ya Wimbo huo? Hapo kitakachobadilika ni Mahadhi ya Sauti tu ila Alaa na mapigo ya vyombo yatabaki kama yalivyo, yeye atakuja na Wimbo wake mwenyewe kuanzia 2025 hapo ndio tutajuwa Utunzi na uimbaji wa Mama sasa!!!
 
Hapana mkuu, Hata kama kama jambo lenye utata, sio haki kumlaumu mtu ambaye sio mwamuzi wa mwisho kwenye mazingira flani. Hata kwenye ndege mwenye mamlaka ya mwisho ni captain in command
 
dndagula

JF-Expert Member
Jul 24, 2016
543
500
Mkuu, kwenye hii dunia, mtu hawezi kukumbukwa kwa kuimba wimbo ulioimbwa na msanii mwenzake. Hiyo haijalishi wimbo huo ni mzuri au mbaya. Labda kama anaimba kwa lengo la burudani tu lakini sio kuacha 'legacy'

Ili kuacha legacy inabidi kutunga na kuimba wako, hata kama unasema tu 'yoyoyoyo....." Lakini maadamu ni wako, watu watakukumbuka hivyo.

Ukiona wewe ni muimbaji halafu watu wanataka urudie nyimbo ambazo zishaimbwa na mtu mwingine, chukua tahadhari.
Jinsi itakavyokuwa pia huwezi kumgombanisha mama na Ilani ya uchaguzi ya CCM hata kama mbinu za utekelezaji atazibuni kwa kadri atakavyoona inafaa. Falsafa ni ile ile ya Magufurism with a difference in approach.KAZI IENDELEE.
 
Nyendeke

JF-Expert Member
Jul 21, 2013
1,531
2,000
Hapana mkuu, Hata kama kama jambo lenye utata, sio haki kumlaumu mtu ambaye sio mwamuzi wa mwisho kwenye mazingira flani. Hata kwenye ndege mwenye mamlaka ya mwisho ni captain in command
Ni kweli Mkuu.., lakini unataka afanye lipi ikiwa na yeye alikuwa sehemu ya Ilani hii inayotekelezwa kwa miaka hii Mitano?
Kimsingi kwa kipindi hiki hawezi kutoka nje ya Ilani waliyokuwa wanaenda nayo sema approach zake na Vipaumbele ndio vinaweza kuwa tofauti na Mwendazake!!!
 
VAPS

JF-Expert Member
Jul 10, 2012
4,896
2,000
Mama Samia katu hawezi kuwa Magu!!! Ile mbegu haikuwa Tz asilia, hakuna Msukuma mwenye roho ya kimaskini vile.Niwakarimu, makini na waungwana sana
 
Azizi Mussa

Verified Member
May 9, 2012
8,789
2,000
Jinsi itakavyokuwa pia huwezi kumgombanisha mama na Ilani ya uchaguzi ya CCM hata kama mbinu za utekelezaji atazibuni kwa kadri atakavyoona inafaa. Falsafa ni ile ile ya Magufurism with a difference in approach.KAZI IENDELEE.
Tanzania hatujawahi kuwa na tatizo la ilani bali personalities na tabia ya mtu na mtu. Au wewe ushawahi kuona shida kwenye ilani?
 
Mmawia

JF-Expert Member
Aug 20, 2013
104,725
2,000
Hao wanao jifanya kumshauri mama yetu ni wale waliokuwa wananufaika namwendazake ili wakumbukwe nao wapate teuzi.

Ni kundi hatari sana kwa ustawi wa taifa letu
 
Azizi Mussa

Verified Member
May 9, 2012
8,789
2,000
Hongera sana ndugu Nape kwa kukazia hoja hii bungeni.

'Mama apewe nafasi aandike kitabu chake'
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom