nkuwi
JF-Expert Member
- Feb 11, 2013
- 4,801
- 5,344
Polisi wetu sijui mnaenda(GA) kusomea ujinga ktk mafunzo yenu?
Hivi inawezekana kweli kuwa mtu mmoja tena aliyedhoofu kiakili na kimwili mnashindwa kumshika na kumuweka chini ya ulinzi hadi mmpige risasi ya miguu na kichwa?
Tena askari zaidi ya 7 bunduki na mabomu yenu kweli?
Habari ilikuwa hivi, kijana aitwaye "Muungano Muyanji" wa Ikungi Singida ni mgonjwa wa akili kwa muda sasa. Jana asubuhi aliamka kichaa kikiwa kimepanda, alileta fujo nyumbani kwao na kumjeruhi mke wake na mama mwingine aitwaye mama Gire kwa kisu!
Baada ya tukio Hilo kutokea watu waliofika walimkabili na kumdhibiti kwa kumnyang'anya kisu alichosema nacho, na kumfunga kamba.
Polisi walipewa taarifa zote wakati tukio linafanyika ila walichelewa kufika, walipofika baaadaye tukioni walikuta mtuhumiwa (Kichaa) wamemfunga na kumdhibiti cha ajabu walipofika tu wakampiga risasi mbili za mguu kabla ya kumpiga nyingine ya kichwa na kufa hapo hapo! As if wanaua kenge fulani hivi!
Wananchi walichachamaa na kureact juu ya kitendo hicho! Polisi waliendelea kuwatishia wananchi wengine bunduki pia.
Walichofanya polisi waliuchukua mwili na kuupeka kituo cha afya Ikungi kabla ya wananchi kwenda kuuchukua mwili na kuuacha Barabara ya kituo cha polisi, hali hii mkuu wa wilaya aliingilia kati na mwili ulipelekwa hospitali ya mkoa Singida kuhifadhiwa.
Mpaka sasa hali sio nzuri, mwili umesuswa huko hospitali!
Waziri wa mapolisi Mwigulu Nchemba hawa vijana wako vipi?
Huku ndio kwenu kiongozi mtu hawezi kuuawa kishenzi namna hiyo as if mnaua paka mla nyama jikoni!
Chukua hatua!
========
Mtu mmoja amepigwa risasi na kufariki papo hapo ,baada ya kuwajeruhi watu zaidi ya wanne kwa kisu mkoani Singida.
Mkazi mmoja wa ikungi mkoani singida amepigwa risasi na kufariki papo hapo ,baada ya kuwajeruhi kwa kisu watu zaidi ya wanne akiwemo mke wake na kuhatarisha maisha ya askari polisi wanne kwa kutaka kuwachoma kisu wakati wakitaka kumkamata.
Akitoa taarifa kwa waandishi wa habari kamanda wa polisi mkoa wa Singida ACP Debora Magiligimba,amemtaja aliye pigwa risasi na kufariki marehemu Herman Joseph miaka thelasini na mbili mkazi wa Ikungi madukani, baada ya kubishana na mke wake alitoa kisu na kumchoma makalioni , na watu walipo fika kutoa msaada aliwachoma kisu watu wengine watatu.
Kamanda Magiligimba amesema baada ya skari kufika marehemu Herman alifanya jaribio mara mbili la kutaka kuwachoma kisu askari licha ya askari kupiga risasi hewani ,lakini askari mmoja katika jitihada za kukwepa kisu alianguka na maremu kumlalia askari huyo kwa kutaka kumchoma kisu kifuani,ndipo alipo fyatua risasi kwa kuokoa maisha yake na wengine na kusababisha kifo.
Kutokana na tukio hilo la marehemu kuchoma watu visu kamanda Mgiligimba alipoulizwa na ITV alisema kuwa marehemu alikuwa na matatizo ya akili ambayo huwa yana tokea na muda mwingine ana kuwa katika hali ya kawaida,pia amesema jeshi lake bado lina endelea na uchunguzi zaidi kubaini ukweli wa tukio hilo.
Chanzo: ITV