Singida: Amuua mke baada ya kuombwa ada ya mtoto

Analogia Malenga

JF-Expert Member
Feb 24, 2012
5,007
9,873
MWANAMKE mmoja Moshi Mkimbu (40) mkazi wa Kijiji cha Ndulungu Tarafa ya Ndago Wilaya ya Iramba mkoani Singida ameuawa kwa kupigwa na kitu chenye ncha kali na mume wake aitwaye Juma Shabani.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Singida Kamishna Msaidizi (ACP) Stella Mutabihirwa akizungumza na waandishi wa habari leo aamethibitisha kutokea kwa tukio hilo ambalo lilitokea Julai 18, 2021 katika kitongoji cha Misughaa na kuwa mtuhumiwa alikamatwa na atafikishwa mahakamani kujibu shitaka lake.

Mutabihirwa alisema kuwa uchunguzi wa awali wa Jeshi la polisi umebaini kuwa chanzo kikubwa cha mauaji hayo ni ugomvi wa kifamilia pamoja na ulevi baada ya marehemu kudai pesa za mahindi yaliyouzwa kwa ajili ya ada ya mtoto shuleni, ndipo mume wake huyo alianza kumshambulia kwa kumpiga na fimbo na kitu chenye ncha kali na kusababisha kifo cha mke wake.

Michuzi Blog
 
Uchunguzi wa awali wa Jeshi la polisi umebaini kuwa chanzo kikubwa cha mauaji hayo ni ugomvi wa kifamilia pamoja na ulevi baada ya marehemu kudai pesa za mahindi yaliyouzwa kwa ajili ya ada ya mtoto shuleni
 
Umasikini tu ndio unatuandama, unauaje mtu kwa kukuomba ada ya mwanao, kweli huu uchumi wa kati ukichanganya na hizi tozo za miamala ya simu basi ni balaa tupu
 
Haya ndio madhara ya kutumia nguvu badala ya akili.
Kukosa elimu na umasikini.

Ona sasa unakwenda jela kizembe kisa ada ya mtoto wako mwenyewe.

Hakuna tofauti na waliotumia nguvu kwenye kongamano la jana, wote kutokea juu hadi chini kabisa kwa corporal chapa nyau chapa vumbi.
 
Huyu muuaji wacha apelekwe jela akaliwe tigo.

Mtoto wake mwenyewe anataka alipiwe ada na nani au yeye kazi yake ni kujaza manii kwenye papuchi?

Akili za watanzania wengi ni tishio zaidi ya Korona.
 
Back
Top Bottom