SINGELI: Fahari ya Tanzania, tuienzi

Mchumi90

JF-Expert Member
Mar 16, 2015
1,089
1,297
Habari za jioni wanadarisalama na wenzetu wote mlio nje ya jiji la Makonda.
Hapa town (darisalama-in Mbowez voice) mziki wa singeli umekuwa maarufu na umetokea kupendwa kwa kasi kubwa sana. Imefikia hadi baadhi y radio stations kuipa airtime ya kutosha (pongezi kwa E Fm). Nadhani huu mziki una asili ya hapa kwetu kabisa na hatujacopy sehemu tofauti na aina nyingine za mziki. Wito wangu, ni wakati muafaka wa kuuenzi mziki huu hata kwenye tuzo za Killi kuwe na category yake kabisa.
Nasema pole pole....hauna
Pole Dada......hauna
++++++++++++
Mida ya kubeti....
++++++++++
Mama Amina
++++++++++
Mwaga maji

Baadhi ya collection ya Singeli.
 
Hata east Africa radio huwa wanaupiga kwenye vipindi vya supamix na planet bongo
#nyumban kwanza
 
Ukienda kwenye music wa singeli wanaimba

oyoo mjinga kaingia mama shingili
kabla ajazinduka na kupaa piga kabari
msichelewe machizi, machizi majita


ukistuka umeshapigwa kabari, mfukoni watu wamekwisha ondoka na vyao
 
Msaga Sumu
Manfonga
Dogo Nigga
Hawa wahuni wanasogeza gurudumu la singeli hapa wale "Kanye & Kim wanna be" hawawezi kukuelewa maana wanauchukia huu muziki kinoma.
 
Nkisikiaga tu mama aminaaaaaaa........... roho nyeupe
linafuatia bonge la tusi ndo raha zetu wa uswazi watuachie starehe zetu......ila tahadhari ukisikia nyimbo hizi mida ya saa 10 alfajiri usipite karibu maana kitachokupata
 
Msaga Sumu
Manfonga
Dogo Nigga
Hawa wahuni wanasogeza gurudumu la singeli hapa wale "Kanye & Kim wanna be" hawawezi kukuelewa maana wanauchukia huu muziki kinoma.
well said ila nahisi muziki wa msaga sumu ni kategori tafauti.wao walianza na kigodoro ulikuwa kama wataratibu flani hivi refer (mama wakambo,rafiki wa kweli),then ikaibuka hii singeli yenye miondoko ya kuchangamka hivi (up tempo) hizi za akina man fongo.ni kama dancehall ilivyozaliwa kutoka kwenye reggeae
 
Mkuu kweli kabisa, singeli ipo vzr...... kama mimi nikisikiaga wimbo wa chura hata kama napovu lzm nitoke bafuni!
 
Huu muziki muzuri sana hata mchiriku.
Zungusha we mama Zungusha watoto wa Ubungo, Manzese, Kinondoni, mwananyamala, mbagala, kigogo, mbagala na ilala. Inatakiwa serikali itambue huu mziki
 
naskia hainaga ushemeji tunakulaaa
naskia hainaga ushemeji tunakulagaaaa

naskia hainaga ushemeji tunakulaaa
naskia hainaga ushemeji tunakulagaaaa

wanangu zamu ya nani leo
zamu ya man fongo
zamu yako itakuja kesho
usijali baharia wangu

zamu ya nani leo
zamu ya man fongo
zamu yako itakuja kesho usikonde baharia wangu
 
ila naona msaga sumu kama anapotezwa vile na madogo maana yeye amebaki kuubadili wimbo huo huo mmoja
naipenda simba shabiki wa damu
nampenda lowasa shabiki wa damu
saivi tena eti anaipenda jangwani shabiki wa damu ....
 
Back
Top Bottom