Amapiano vs Singeli

nasrimgambo

JF-Expert Member
Jan 10, 2017
981
1,000
Yote ni aina ya muziki wa kiafrika kutoka mitaani wanakoishi Waafrika wa hali ya kawaida.

Amapiano nasikia inatokea mitaa kama Soweto, Katlehong, Vosloorus ama Mamelodi huko Afrika Kusini.

Tena ulionekana muziki wa watu wa mitaani. Lakini hatimaye huu mziki umekubalika na kuigwa na watu wa mataifa mengine
ila umebakia utambulisho wa wasauzi kwasababu huu mziki unapendeza zaidi ukiimbwa kwa lugha na lafudhi za huko huko Afrika Kusini na jinsi ya kuucheza wenyewe wasauzi ndio mahodari zaidi, yani hata tuige vipi amapiano ikichezwa na msauzi ndio inapendeza zaidi.

Tukirudi singeli huu muziki nao umeanzia mitaani kabisa, ambapo tunaambiwa asili yake ni ma-emcee wa mitaani walipoanza ku 'play' isha nyimbo za taarabu kwa kasi ili zichezeke kisha wakaongezea na mitindo inayofanana na mchiriku na mdundiko.

Moja ya nyimbo zilizoinua muziki huu ni ulikuwa wimbo wa msanii msaga sumu ulioitwa Lowassa, ambao ulikuwa ni wimbo wa kampeni ya uraisi wa muheshimiwa Edward Lowassa back in 2015.

Nao kama ilivyo kwa Amapiano, singeli imekuja kuwa maarufu na sidhani kama kuna watu wa nchi nyengine wanaiwezea kuliko sisi. Japo kwenye kucheza naamini mtu wa asili yeyote anaweza icheza labda wasio Waafrika ndio watachekesha wakicheza singeli.

Ila amapiano na singeli zinaenda njia tofauti

Amapiano imeanza kuvuka toka kuwa mziki wa mitaani na kuwa mziki unaoheshimika na kuigwa kimataifa, ila singeli bado haijaanza kuigwa. Pia mashairi ya singeli yanazidi kuipoteza.

Hivi nani atachukulia serious nyimbo zinazoimba juu ya mtu anayeheshimu madanga ya mke wake kuwa ndio yanampa kula, yani uma"""lay$&a wa mke mume anajivunia.

Ama nani atachukulia serious nyimbo yenye mashairi ya kishangingi kama vile wimbo wenye mashairi ya mwanamke nyumba ndogo anayeenda kwa mke mkubwa kujitambulisha na mabendibati

Ama wimbo wa mwanamke anayeimbia juu ya ex wake huku anamtambia mwanamke mwengine kuwa kama yeye mume kwake (huyo mwanamke mwengine) basi naye ni danga lake.

Kama haitoshi singeli ya siku hizi ni video za makalio makalio makalio yani ni mata__k__ooo tu na kukata viuno nyimbo zikitoka total class less

Halafu ndio hii singeli ndio itashindana na amapiano ambayo ni mziki unaoweza imbwa, tazamwa na kuchezwa kokote na hauna mashairi na video za Konsepti za hovyohovyo

Safari ya tanzania kuwa na utambulisho wetu kama taifa ina vikwazo vingi ikiwemo hili la wasanii kukosa ubunifu na kuimbaimba mashairi ya kukenulisha meno ila in long run yanafanya miziki ionekane haina class huku ubunifu wa nje ukiendelea kuonekana kuwa ni bora kuliko wa hapa kwetu nyumbani.
 

T14 Armata

JF-Expert Member
Mar 7, 2017
4,260
2,000
Singeli watu waliichukulia kama uhuni ila ndio ilikuwa njia yetu ya kutokea. Yani tumebaki kuwaona wasanii wetu wanapepea kila staili inayoibuka nao wanaidandia, walianzia Nigeria wakaiga mpaka uongeaji wao baadae South Africans walivyochukua tuzo kimataifa wabongo wakaibukia kule. Sahivi wanajifanya wanaimba kama wamezaliwa SA

Singeli ingeboreshwa ikaongozwa na wenye exposure kidogo wakajua kufanya modifications alafu waimbaji wakaachwa wale wale kina Dogo Nigga ingetambulika. Ila yale mauno siyapingi, sijaona nchi duniani wanakata mauno wamelala chini hii ni kitu kingine kabisa mradi isitafsiriwe vibaya

Singeli au zile style za macharii wa ara zitapotea hivi kizembe. Nenda Arusha au Moshi utaona wazungu wanavyozipenda, hata Maasai rap ilipotea ya kina rip faza_nelly
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom