Sindano za vichaa zimenifanya niwe mchungaji

bushland

JF-Expert Member
Joined
Mar 6, 2015
Posts
7,015
Reaction score
4,998
Habari wanabodi,
Jamani hakuna linaloshindikana mbele za Muumba wetu. Baada ya kumpiga mwanaume chini tena bila kurudi nyuma na kuamua kuchoma sindano za vichaa ili nijiepushe na anasa, nimepata muda mzuri wa kumtumikia Mungu.

Nipo katika harakati za kuwashawishi vijana wanaohangaika usiku na mchana na mambo ya anasa, kuacha Mara moja mambo hayo na kumgeukia Muumba wetu kwani yeye ndo kila kitu. Hata yule jirani yangu aliekuwa akiteswa na mwanaume nikamshauri aachane nae sasa tunamtumikia Mungu na tuna furaha isiyo ya kawaida katika maisha yetu.

Huwa tunaamka saa kumi alfajiri kwenda kanisani tunaomba hadi saa mbili asubuhi na kweli tumefunuliwa mengi sana. Tumeonyeshwa wadada wengi wakiwa na shida kubwa ya uhitaji wanaume wa kuwaoa, ushoga nao umeongezeka kwa kiwango cha kutisha na mambo mengine mengi ambayo tumeonyeshwa tupo katika maombi makali ya ukombozi.

Wanajf wenzetu tunaomba mtuendelee kutuombea tuweze kusonga mbele.
Tumeenda pia kule wanakojiuza wakinadada tumeweza kupiga maombi huko huko wanakofanyia kazi zao na wamekiri kumpokea Yesu na biashara ile wameacha na sasa tupo nao huku kanisani wanamtumkia Mungu.
 
Kichwa cha mada ni irrelevant na mada.

Saa 10 alfajiri mpaka saa 2 mnaombea nini?

Btw: Ni uamuzi mzuri kabisa
 
Aseeee, kazini mnaenda saa ngapi? Tanzania ya viwanda tutaipata kweli
 
JF siku hizi imekuwa ya habari za kutunga
 
Hamna lolote n stress znawasumbua tuu,n najua zkiisha mtalud kulekule.
 
Sasa kwanini umechoma sindano za vichaa kama Mungu anaweza kukusaidia?
 
Kwa hiyo unatushauri na sisi tukachome hio sindano ya vichaa, vipi siku ikiisha nguvu?

Nawaza.
 
Kumtumikia Mungu kwa kujidunga sindano ya VICHAA?
 
Duh! Where as I thought I know everything, new things unfolds to me.. Hili la sindano za vichaa nalo ni jipya kwangu...
 
bado nina shaka na imani yako, kujitoa kwa Mungu ina maana kujitesa yaani kuukatalia mwili tamaa zake na kuzishinda na ndo kuamua kumfuata Bwana pekee, ila wewe umeruka hilo kwa kujichoma hiyo sindano ya vichaa, yaani mwili umeutolea hali yake ya kawaida ya mihemko kwa sindano zako hivyo ukawa huru huna kishawishi cha kukishinda na ndo ukaamua kumfuata Bwana. hapo haupo sawa, hata mapadre kwa kanisa katoliki ijapokuwa hawaoi ila hakuna anayeruhusiwa kwenda upadre akiwa si mkamilifu, sasa wewe huoni kama uwezo wako wa kushinda vishawishi haupo ktk imani bali ktk sindani!
 
Habari wanabodi,
Jamani hakuna linaloshindikana mbele za Muumba wetu. Baada ya kumpiga mwanaume chini tena bila kurudi nyuma na kuamua kuchoma sindano za vichaa ili nijiepushe na anasa, nimepata muda mzuri wa kumtumikia Mungu.

Nipo katika harakati za kuwashawishi vijana wanaohangaika usiku na mchana na mambo ya anasa, kuacha Mara moja mambo hayo na kumgeukia Muumba wetu kwani yeye ndo kila kitu. Hata yule jirani yangu aliekuwa akiteswa na mwanaume nikamshauri aachane nae sasa tunamtumikia Mungu na tuna furaha isiyo ya kawaida katika maisha yetu.

Huwa tunaamka saa kumi alfajiri kwenda kanisani tunaomba hadi saa mbili asubuhi na kweli tumefunuliwa mengi sana. Tumeonyeshwa wadada wengi wakiwa na shida kubwa ya uhitaji wanaume wa kuwaoa, ushoga nao umeongezeka kwa kiwango cha kutisha na mambo mengine mengi ambayo tumeonyeshwa tupo katika maombi makali ya ukombozi.

Wanajf wenzetu tunaomba mtuendelee kutuombea tuweze kusonga mbele.
Tumeenda pia kule wanakojiuza wakinadada tumeweza kupiga maombi huko huko wanakofanyia kazi zao na wamekiri kumpokea Yesu na biashara ile wameacha na sasa tupo nao huku kanisani wanamtumkia Mungu.
Kama wadada wengi wanahitaji kuolewa.. Mbona tukiwatongoza wanaringa ringa hivyo? Au wanatujaribu?
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom