Magufuli kiboko ya masikini; Mtetezi wa Matajiri

Robert Heriel Mtibeli

JF-Expert Member
Mar 24, 2018
21,337
51,858
MAGUFULI KIBOKO YA MASIKINI, MTETEZI WA MATAJIRI.

Na, Robert Heriel

Kuna watu hawamuelewi Mhe. Rais na hawatakuja kumuelewa kabisa. Leo nitakupa mbinu ndogo sana ya kumuelewa Mhe. Rais ambayo huenda ulikuwa huijui. Mbinu hiyo ni; Usimpende sana magufuli yaani usiwe na mahaba niue naye, pia usimchukie sana Magufuli yaani usiwe adui yake kindaki ndaki" Hiyo ndio siri ya kumuelewa huyo jemedari anayelisukuma taifa kwenda mbele.

Mhe Rais anakauli yake moja hupenda kuisema, nitainukuu; Mimi ni Rais wa wanyonge" Nadhani hata wewe uliwahi kumsikia Mhe. Rais akisema maneno hayo. Pengine kila mmoja ameielewa kwa namna yake. Lakini leo nitaenda kuielezea kinagaubaga kuwa Mhe. Rais akisema hivyo huwa anamaanisha nini.

Kuna watu wanafikiri kuwa Magufuli akiongea hivyo anamaanisha yeye ni Rais wa masikini, thubutuu! Kama ulikuwa umemuelewa hivyo umechemka, Rais Magufuli hajawahi na hatawahi kuwa Rais wa masikini.

Hakuna watu anaowachukia Mhe. Rais kama masikini, pengine utaniuliza kwa nini, mimi mwenyewe sijawahi kumuuliza, lakini sababu nitakupa zilizoshiba. Ila itoshe kusema kuwa Mhe. Rais anawachukia Masikini sana. Lakini baadaye nitaulizwa kwani masikini ni nani? Huenda ni mimi na wewe? Heeh! Yaani nachukiwa na Rais, kwa nini? Nitakuambia kwa nini.

Awali niseme kuwa hakuna anayewapenda masikini, tokea dunia iumbwe masikini hajawahi kupendwa, moja ya sababu kuu ni kuwa masikini hapendeki. Kama Mhe. Rais angewapenda masikini angekua mtu wa kwanza duniani kuwapenda masikini, hii ingeandikwa hata kwenye vitabu vya rekodi za dunia.

Si ajabu kwa Mhe. Rais kutowapenda masikini kwani hata Mungu muumba wa Ulimwengu hajawahi kuwapenda masikini na hatakuja awahi kuwapenda, unajua kwa nini Mungu hawapendi masikini, nitakueleza baadae. Masikini ni watu wa hovyo wanaochukiza sana, zamani baadhi ya viongozi waliazimia kuwaua masikini wote. Loooh!

Rais anaposema yeye ni Rais wa wanyonge hurejelea watu wanaoonewa wanapokuwa kwenye harakati zao za kutafuta riziki, watu wanaoonewa wanapokuwa kwenye majukumu yao, hao ndio wanyonge kwani huonewa na wenye nguvu wanaowakwamisha. Wala sio Rais wa Masikini wasio na akili nzuri.

Ili mtu awe masikini itambidi awe mjinga sana, awe mzembe, awe mvivu, awe amekufa, awe hana akili sawasawa, awe mtegeaji yaani masikini lazima awe na sifa mbaya zote. Hakuna masikini aliyewahi kuwa na sifa njema. Subiri kwanza, naona nimetaka kuongeza sauti kabla ya muda.

Masikini huwa wanashangilia pale wanapoitwa wanyonge hiyo ni tabia ya masikini, wakati kiukweli masikini hajawahi kuwa mnyonge. Siku Magufuli akisema yeye ni Rais wa wanyonge jaribu kuangalia watakaoshangilia, utashangaa mwenyewe.

Masikini ni imani kama ilivyo imani nyingine. Masikini ni kama dini, wanataratibu zao, wanamiungu yao, Umasikini ni dini ambayo kila siku ni siku ya ibada. Bado usijue kwa nini Magufuli hawapendi Masikini, bado hujanipata tuu. Kama bado subiri utaelewa tuu.

Masikini anafikiri kuwa kuna mtu yupo kwaajili yake na yeye hayuko kwa ajili ya mwingine. Yaani ni tegemezi. Huwategemea watu, huitegemea serikali, hutegemea misaada ya nchi kubwa, masikini ni tegemezi. Sasa ole wako usimpe kile alichokuomba, atakulalamikia mpaka uzimie, yaani kila siku ni manung'uniko, utadhani wewe ni baba yake uliyemzaa. Siku moja Magufuli uvumilivu ulimshinda akawajibu kidizaini kuwa; serikali sio Baba yenu, fanyeni kazi. Labda nimesahau, anyway nimekumbuka, serikali haitawapa chakula, limeni, ardhi ipo, mvua ipo alafu niwaletee chakula. Sileti. Hahahaha! Haki ya nani nilicheka sana.

Unajua hakuna kitu kibaya kama kukutana na masikini, masikini anaomba omba kila muda. Hata Mungu hapendi majitu yanayoombaomba kila muda, hayana muda wa kupumzika kila kukicha kuomba, wakiamka kuomba, kazi hayataki, yao yanataka yaombe tuu. Thubutu! Mungu alichoka maombi ya masikini maelfu ya miaka huko nyuma siku moja akayatolea uvivu akayaambia; asiyefanya kazi asile. Imagine Mungu anasema hivyo, ubaweza ushindwe kujua alikasirika kwa kiasi gani. Ni kwamba hakutaka tena makelele ya masikini waombaji. Akaona ni kheri wasiofanya kazi wafe tuu kuliko kusumbua watu na kumsumbua yeye.

Mungu aliwahi kukaa kikao na masikini lakini walimvuruga mno, hawakuelewana, Mungu alipoona Masikini wanaakili moja na nusu, akawaagiza wamfuate mdudu aitwaye chungu ati wakajifunze kwake. Unajua masikini wengi ni wavivu, hupenda kulala kama maiti, utawakuta wanalala tangu saa mbili usiku mpaka kesho asubuhi saa tatu saa nne. Hivi hapo kuna nini, Bado hujajua kwa nini Magufuli hawapendi masikini?

Masikini waliwahi kufukuzwa hekaluini siku moja na Mungu. Imagine Mungu anafukuza watu hekaluni, pengine hadithi hizi huzijui lakini leo nimekujuza. Mungu hawapendi masikini kwa sababu wengi sio watiifu, wazembe na wasiojijali wao wenyewe. Masikini amefika kanisani hana sadaka wala zaka, dooh! alafu hata aibu hawana, Mungu akawauliza, mbona hamkuja na sadaka wala zaka, je wiki hii mlikufa, hamkuwa mnapumua, hamkuwa na nguvu, au je mlikuwa mnaumwa? Masikini hana cha kujibu kazi blah! blah! Mara mambo magumu, sawa hata mia tano ulikosa, kimya. Masikini akaulizwa sasa umekuja kufanya nini, akajibu nimekuja kuabudu, Mungu akamuambia masikini, umeshindwa siku sita kuniabudu huko nje kanisani, utaweza leo siku moja. Dooh! Kumbe masikini hakujua kuwa kanisani watu huenda kumshukuru Mungu kwa yote yaliyofanyika wiki nzima, hivyo matoleo ni moja ya vithibitisho kuwa uliabudu kwa siku sita. Mungu akawafurumusha masikini akawaambia msije kwangu mikono mitupu. Bado Magufuli awapende? Thubutuu!

Masikini ikiwa hawatoi sadaka kwa Mungu wao, wataweza kulipa kodi? Hahahahahah! na hapo ndipo chuki za wazi za Rais zitakapo jitokeza. Masikini hawataki kufanya kazi, niambie taifa litapata wapi kodi, yaani Magufuli ashindwe kulipa watumishi wake mishahara kwa upuuzi wa watu wajinga wasiotaka kufanya kazi, magufuli miradi yake haiendi vizuri kisa Masikini wasiofanya kazi hawalipi kodi, bado awapende. Mimi sidhani kama hilo litawezekana.

Ajabu Masikini hata kwenye makanisa, misikiti, na mambo ya kijamii, ni wavivu, hawatoi michango lakini watakavyojazana utadhani sisimizi. Kama ni kwenye harusi utashangaa watakavyojaa, michango hawajatoa wasubirie kwenye malalamiko, mara wali mdogo, sijui pilau haina nyama, sijui vinywaji havijatosha yaani masikini ni watu wa shari. HAHAHAAH!

Kodi hawatoi wasubirie wakifika hospitalini, ooh! hakuna madawa, ooh! vifaa sijui vimefanyaje yaani ilimradi watasema. Wakute shuleni, ada hawajaalipa lakini wao ndio wakwanza kuwatukana walimu, mara hajafundisha, mara sijui,,,,,,,,! Khhhah!

Masikini akija kwenye biashara yako, kiatu shilingi ngapi, atakuuliza. Utamjibu elfu 50, atakavyohamaki na kukitolea maneno ya shombo, muulize unashilingi ngapi, atakuambia elfu nane. Haaa! utashangaa kidogo, kisha mwambia haya leta hiyo nane tumalize kazi. Utashangaa wala hautaamini. Atakupiga chenga basi tuu ilimradi.

Masikini wanapenda mambo rahisi, wanapenda miujiza, wanapenda maisha ya kamari. Masikini dini yao inawaambia kuwa wao wataenda mbinguni na matajiri watachomwa moto.

Hivi Magufuli atakuwa Rais wa watu wa bahati nasibu, watu wa miujiza wasiotaka kazi, ahhahaha! Thubutuu!

Kitu pekee ambacho Magufuli na viongozi wakubwa duniani wanchokiogopa kwa masikini ni wingi wao. Masikini ni wengi mno hivyo njia rahisi ya kuwapumbaza ni kuwachekea na kuwasifia kwa ujinga wao. Usipofanya hivyo hawatakuchagua, nani asiyependa kuchaguliwa. Thubutuuu!

Usishangae Magufuli akiwatukana matajiri kwa maneno machafu, mara majizi, mafisadi na majina mabaya ya namna hiyo. Lengo lake ni kuwachota masikini akili kwa maana ni wajinga. Hata hivyo hao matajiri hawana muda na Magufuli, wao wanawaza kazi zao, wakati Masikini wakimsubiri Magufuli aje awaletee maisha mazuri.

Yesu aliwahi naye kuwachota masikini akili akawaambia ati ni rahisi kwa ngamia kupenya kunako tundu la sindano kuliko tajiri kuuona ufalme wa Mungu. Acha Masikini washangilie. Yesu ilipofika jioni yule akaingia kwa Zakayo akala chakula cha jioni, ndivyo ilivyo hivyo,

Masikini wajenge Kanisa la matope, nani akubali, viti vibovu nani akubali, hakuna vyombo vya muziki wala kwaya haina sare nani akubali, masikini ni kama nyani ukimuendekeza utavuna mabua. Njia bora ya kumsaidia masikini ni kumdhulumu ili akili zimkae sawa. Ukimsaidia utajichimbia kaburi lako mwenyewe.

Sasa Magufuli ni kiboko ya masikini, kwa maana umasikini ni tabia kamailivyo kwa utajiri. Na tabia hujengwa na mazoea. Mazoea a uvivu, uzembe, anasa, ngono zembe huleta umasikini. Magufuli kuwaambia watu wachape kazi ni pigo kuwa kwa masikini kwani wao ni wavivu kwa sehemu kubwa.

Falsafa za magufuli ni bakora kwa masikini, lakini ni kete muhimu kwa matajiri. Kwani moja ya sifa za matajiri ni kuchapa kazi na kujitegemea.

Nipumzike sasa.

Robert Heriel
Taikon wa fasihi
0693322300
 
Ni kweli, halafu maskini habebeki... mfano mzuri uchebe
Mie ndo maana nasemaga moyoni Vanessa mdee amejua kutufunda wanawake....! HAIWEZEKANI uachane na nuhu then urukie kinyesi Kama uchebe. Check Vanessa alivyotunyoosha waja...kaachana na jux kajitupa Mambele huko...! Yaan hako kauchebe kamenikerekta
 
Mie ndo maana nasemaga moyoni Vanessa mdee amejua kutufunda wanawake....! HAIWEZEKANI uachane na nuhu then urukie kinyesi Kama uchebe. Check Vanessa alivyotunyoosha waja...kaachana na jux kajitupa Mambele huko...! Yaan hako kauchebe kamenikerekta
mapenzi mama mapenzi
 
Back
Top Bottom