Sina raha

Misguided

Member
Apr 11, 2011
32
13
Mimi ni mwanamke mwenye umri wa miaka 29.Nimeolewa na nina mtoto mmoja. Juzi nimegundua kwamba mume wangu anatembea na mmoja wa marafiki zangu. Nilimsindikiza rafiki yangu kumuona shangazi yake mgonjwa,tukiwa pale nikataka kumkumbusha mume wangu kununua baadhi ya vitu ambavyo tulikua tunahitaji nyumbani. Nikaazima simu ya rafiki yangu kwakua yangu ilikua imeisha chaji,akanipa. Nikadial namba za mume wangu bila wasiswasi,baada ya kuandika zote nikaona kwenye screen imeandikwa mpenzi. Nikajua labda nimekosea maana nilikua natoa namba kichwani kwahiyo nikadial upya,matokeo yale yale.Nikaona nipige,ikapokelewa "mambo darling" sauti ya mume wangu bila ubishi. Kigugumizi nilichopata sikuweza kutoa neno zima.Akaishia kusema "mpenzi unakatakata ngoja ntakupigia" simu ikakata. Nilichofanya nilifuta namba nilizodial alafu nikadial simu ya dada wa kazi.

Kuchungulia msg box naona zinazotoka na kwenda kwa mpenzi zimesheni. Nikamrudishia na pale pale nikaaga.Sijamuuliza yeyote kati yao wala sijaongea na rafiki yangu since.Nafikiria nini cha kufanya.Naombeni ushauri.
 
Ungeongea naye 2 ukijidai wewe ndo hy rafiki yk hlf mwisho umjulishe kuwa wewe ni mkewe na umeshagundua mahusiano yake na rafiki yako! HAPO MUVI NDO LINAANZA SASA
 
Pole sana na hayo madhila Da'Misguided. Mkalishe chini huyo mumeo uongee naye halafu umsamehe muendelee na maisha yenu.
 
sasa hukumuuliza shosti yako kwa nini? Ulipaswa kukata mzizi wa fitna! Shoga yako anajua kuwa huyo anayemuita mpz ni mumeo? Kama anamjua na wewe umelifumbia macho hilo swala una tatizo wewe. .

Halafu wanaume mbona hamna haya wala adabu?wanawake wote waliojaa mpaka utembee na shoga wa mkeo?
 
mwelezo kwa upole ili ajue kuwa umejua. Kisha endelea na life kama kawaida bila kumwonyesha hasira. Jitahidi kupendeza na kutabasamu kila mara.
 
pole sana dada kwa yaliyokukuta,mushukuru mungu kwa kila jamboCha msingi kaza maombi kama mungu kapanga kuwa huyo ni mmeo wa maisha, atazunguka kote lkn atarudi kwakoPunguza hasira kwa sasa subiri mda upite kidogo then chukua simu ya mmeo uone kama kna msg zake anazochati na huyo rafiki yako muulize kwan utakuwa na uthibitisho la sivyo utazua ugomvi mwingine na mmeo
 
Huyu dada alipata mfadhaiko hakuamini yote aliyoona kwa simu na kwa sauti ya mumewe. Inatokea hivyo na ni bora alinyamaza akaondoka. Ama mwenye kosa zaidi ni shoga mtu maana bila shaka yy ndiye aliyemuibia mwenziwe mpenzi. Wanawake wana vitimbi sana wanaweza kukuweka kwa vizuri na usikurupuke. Ushauri wangu ongea na mumeo bila shaka atajisikia vibaya umsamehe muendelee na maisha yenu. Duniani kuna mitihani mengi.
 
Una akili kama mchwa, ulifanya jambo la busara kutomuuliza
Mke hagombani na kimada wa mumewe
Kaongee na mmeo, na ukabe hadi penati kuanzia sasa.

Kuwa na rafiki kama huyo huhitaji adui.
 
mwelezo kwa upole ili ajue kuwa umejua. Kisha endelea na life kama kawaida bila kumwonyesha hasira. Jitahidi kupendeza na kutabasamu kila mara.
YN AMSAMEHE KIRAHISI NA TABASAMU ZITO KESHO ATATEMBEA NA NDUGU WA MKE WAKE! wanaume sijui mkoje
 
Pole sana na hayo madhila Da'Misguided. Mkalishe chini huyo mumeo uongee naye halafu umsamehe muendelee na maisha yenu.
Asante ndugu yangu.
Sasa huo msamaha nitoe hata nisipoombwa?
Ungeongea naye 2 ukijidai wewe ndo hy rafiki yk hlf mwisho umjulishe kuwa wewe ni mkewe na umeshagundua mahusiano yake na rafiki yako! HAPO MUVI NDO LINAANZA SASA
Ujasiri ndugu yangu ujasiri.
Yani niliishiwa nguvu kabisa.
sasa hukumuuliza
shosti yako kwa nini? Ulipaswa kukata mzizi wa fitna! Shoga yako anajua kuwa huyo anayemuita mpz ni mumeo? Kama anamjua na wewe umelifumbia macho hilo swala una tatizo wewe. .

Halafu wanaume mbona hamna haya wala adabu?wanawake wote waliojaa mpaka utembee na shoga wa mkeo?
Ni rafiki yangu wa karibu sana kwahiyo wanafahamiana kupitia mimi.Sio kwamba nimelifumbia macho ila nafikiria ntawauliza vipi wakati sina ushahidi mkononi?Si wataishia kuruka futi kumi kwamba sio kweli?
mwelezo kwa upole ili ajue kuwa umejua. Kisha endelea na life kama kawaida bila kumwonyesha hasira. Jitahidi kupendeza na kutabasamu kila mara.
Ahhh hata sijui nini kinawezekana na nini hakiwezekani tena. Hapa nilipo natamani hata angekua katembea na mtu mwingine na sio rafiki yangu.Kweli kua uyaone.
 
Ukimwi ukimwi ukimwi, ongeeni yt lakini kumbukeni njia mojawapo ya kuambukizana ukimwi ni kutokuwa mwaminifu.
 
pole sana dada kwa yaliyokukuta,mushukuru mungu kwa kila jamboCha msingi kaza maombi kama mungu kapanga kuwa huyo ni mmeo wa maisha, atazunguka kote lkn atarudi kwakoPunguza hasira kwa sasa subiri mda upite kidogo then chukua simu ya mmeo uone kama kna msg zake anazochati na huyo rafiki yako muulize kwan utakuwa na uthibitisho la sivyo utazua ugomvi mwingine na mmeo
Asante mwaya. Simu yake ina password, hua hapendi niguse hata kama nataka kumpigia mtu na yangu haina salio.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom