Sina hisia na mume wangu nisaidieni

Sina hisia na mume wangu nisaidieni

Habari waungwana!

Nimekuwa sina hisia na mume wangu kwa miaka 5 sasa. Chanzo cha yote haya ni jinsi anavyoishi nami, amekuwa hanijali, ananichukulia kama mleaji wa wanae basi. Yaan amekuwa anajali kampani za marafiki zake kuliko mimi.

Jaman nimechoka nahitaji msaada wa utabibu. Hali hii imenichosha najihisi kama nabakwa nahisi akili imeshachoka.

Tafadharini nishaurini, sihitaji kebehi. Am fed up!
Pole sana mamii!
Ila nahisi pia elimu yako sio ya juu, nyie watu huwq mnakubali kuburuzwa maana hamna pa kujishikia wenyewe! Namanisha uko tegemezi kwake na yeye ametambua kuwq ana hiyo silaha!!
Ushauri: Kaa nae chini umueleze, mawasiliano mazuri ni kitu muhimu sana ktk kuboresha uhusiano, watu wanachukulia mawasiliano poa poa tu!! Ongea nae na funguka!!
 
kaa nae chini mwambie ukweli kuwa unahitaji kudekezwa na kubembelezwa+caring zaidi ya mtoto aliyebemendwa.......

asipokuelewa kuna mstari upo ivi

NJOONI KWANGU MNAOSUMBUKA NA KUELEMEWA NA MIZIGO NAMI NITAWAPUMZISHA


nashukur kwa ushauri !asante
 
Mumeo ana hulka ya "Love possessiveness"
Watu wa aina hii, hawapendi uhuru kwa wenzi wao, huwachagulia marafiki wenzi wao, kifupi huwa na mipaka kwenye kila jambo. Tiba yao hutegemea mtu na mtu.
 
umemweleza mumeo matatizo yake? je amelipokeaje?
Kuna mengine huwa tunawaonea tuu hawa wenzetu.

Hivi kweli mwanaume mwenye mke na watoto unapaswa kuelezwa na mtu kuwa unapaswa kuijali familia yako?

Kwamba kutoa hela ya chakula, ada na mahitaji mengine ndo basi unaijali familia?

Sasa mwanamke anaweza kuwa kweli amechoshwa na kutokujaliwa kwa familia yake ingawa mwanaume alikuwa na tabia za kujali pengine hata kabla ya ndoa, lakini pia mwanaume anaweza kuanza tabia hiyo baada ya ndoa au baada ya kupatikana watoto. All in all, mwanamke anaweza jifunza toka kwa jirani, rafiki n.k akiona kule mtu anapewa attention zote hata kama jamaa anchepuka, atatamani angalau mwanaume wake angekuwa hivyo.

Matatizo yatukute kwa bahati mbaya, tusiyatafute! Usimpe mtu sababu ya kuongea au kutenda kinyume na makusudio yake.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom