Maamuzi magumu: Mume wangu hanijali kwa chochote, nataka kuachana naye

Bi dentamol

JF-Expert Member
Feb 1, 2014
987
1,912
Nataka nifanye maamuzi magumu ya kuachana na huyu Mwanaume, nahofia kitu kimoja

1) Ukweni kwangu pamoja na mume wangu hawana dini yaani ni waganga sana. Je watanibakiza?

2) Nilitolewa mahari mil 1.6 bi mkubwa ameshakula na taratibu za kisukuma ukiolewa kama haujazaa mahari inarudi na faini juu, nafanyaje?

3) Jamaa nampenda japo simuhitaji nitaweza kusahau na kurudi katika hali ya kawaida?

Sababu za kumuacha
1) Sielewi nina roho mbaya au vipi lkn nahisi hii hali imenichosha.Mume wangu hajali sana kuhusu mimi wala maitaji yangu wala mahitaji ya familia lkn 90 anajali ndugu zake.

Before sijaishi nae nilikuwa nina kipharmacy changu ambacho kilikuwa kinanitosha tu kwa mahitaji yangu baada ya kunioa kimila ikabidi nimfuate mkoa mwingine na duka kuajiri mtu ambapo huwa naenda kukagua biashara baada ya mwez 1 japo mapato yamepungua Sana.

Kinachoniuma nimemuomba sana mume wangu anifungulie biashara huku nilipomfuata kutokana na fani yangu amekuwa mgumu sana ananiambia kaa tu kwanza so nimekuwa mtu wa kukaa tu ndani sina kipato chochote zaidi ya hicho kidogo nachopata nacho nakuweka kwenye ac ya familia.

Nina mtoto ambae nilizaa before yupo kwa mama angu nashindwa hata kutoa matumizi nyumbani kwetu kipato Sina,
Kinachoniuma mtaji sipewi lkn jamaa kila kitu anahudumia kwao tu.

3) Tangu mwaka Jana mwez wa 11 afya yangu sio nzuri naumwa mambo ya kizazi nimetibiwa hospitali za wilaya bila mafanikio ameshindwa hata kunipeleka kwa madaktari bingwa wa wanawake najua mwenzangu hana hela leo nimeshika simu yake nimeumia sana kuona salary ya mwezi huu imeingia mil 2 .3

Anajenga kwao hata kunipeleka hospital za maana hakuna kweli jaman?

Tangu kanioa hajaninunulia hata chochote juzi nipo nyumbani nilikuja kimatibabu mama akanipa hela nikanunua nguo jamaa nimemwambia kafurahi tu.

Kilichoniuma zaidi Leo, mwaka Jana tulilima mpunga kwa ajiri ya kuongezea tununue kiwanja tukapata magunia Kama 20 tu lao yameuzwa hela zinaweka milango kwao hata kupewa elf 50 ya nguo hakuna Wala kupewa tu taarifa hamna nimeumia Sana.

Yaani 15% tu ya kipato chake anatoa katika familia lkn 75% ya kipato chake anapeleka kwao.

Jamaa ni mhanisi TANESCO lkn ndani tunakalia viti na meza vya baa ukimwambia tununue kitu kwa ajiri ya ndani hataki.

Binafsi naona napoteza muda tu acha nikapambane kivyangu.

Naombeni ushauri namuachaje?
 
Usinukum TU Kuna kitu, umri, familia kuna vitu vingi ila Sasa serious nimeamua

Jaribu kupitia thread moja moja, soma comments zote ukiwa umetulia, mwisho kabisa utapata jibu la nini ukifanye.

Ni misuse of resources kukaa tunarudia yaleyale kwa mtu ambaye hafati.

Acha tuutumie muda na mawazo kwa watu ambao wako serious.

Thread 11+ ni nyingi sana kwa same problem.
 
Wamesha mtengeneza kwao, siku anakaa sawa hana kazi vizazi vyenu shida tupu.

Chamsingi usimuache ila fight kwa Aina yako na usimshilikishe kwa chochote.

Na vizuri ukafight jirani na mama yako maana mama atakupa moyo kila hatua ngumu kwako.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Toa ushauri mkuu, hayo mengine ni arrangement za kwao. Maana naamini wakati wanaingia kwenye kuoana kila kitu kiliwekwa mezani.
Istoshe zijasema hanipi matumiz ya mtoto ...mzazi mwenzangu keshatangulia mbele za haki
Mwanangu yupo kwa mama angu kanikuta nina biashara zangu namsomesha mtoto wangu medium lkn Sasa nimeolewa nimeacha biashara Sina kipato chochote mtoto namleaje?
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom