fasiliteta
JF-Expert Member
- Jul 2, 2014
- 2,165
- 3,655
Ukitaka kuijua CCM-A na CCM-B,paguse hapo kwenye mshahara.Huo ndio ukweli mishahara ya au mshahara wa mbunge na mapochopocho wanayokwapua au kulipwa ni mishahara hatarishi kwa Taifa letu ambalo linajikongoja.
Ajira ya ubunge sasa imekuwa ni ya kufa na kupona. Hivi kazi hii kweli mmeifuatilia na kipimo cha mtu anachokwapua, wengi huwa wanachomekea tu lakini ukweli hii kazi ni ya kupata hela kiulaini kabisa, wewe upige meza tu na kuunga mkono kila jambo, inatosha kabisa kuwepo salama kwa muda wote.
Kuna haja sasa mishahara yao iangaliwe upya inawadhalilisha wengine kuna watu wapo tayari kupoteza roho zao kwa kulinda nchi hii, kuna wanaofanya kazi hatarishi za kupambana na majangili na majambazi ambao roho zao zipo nje ndani wakati wa utekelezaji, inakuwaje hawa wapiga meza na blah blah wanalipwa hela iliyovuka mipaka?
Hawakuachi salama.
Hebu ona mdee na kundi lake pamoja na kuitwa Kamanda miaka nenda Rudi,wametia mpira kwapani na pamba masikioni.
Mcheki Mbowe uchaguzi serikali za mitaa alivyoupotezea ila uchaguzi mkuu wa ubunge kajisahulisha.No kususa