Sina chuki nao, ila mishahara ya wabunge ni 'too much'

Shocker

JF-Expert Member
Sep 15, 2012
1,942
3,818
Huo ndio ukweli mishahara ya au mshahara wa mbunge na mapochopocho wanayokwapua au kulipwa ni mishahara hatarishi kwa Taifa letu ambalo linajikongoja.

Ajira ya ubunge sasa imekuwa ni ya kufa na kupona. Hivi kazi hii kweli mmeifuatilia na kipimo cha mtu anachokwapua, wengi huwa wanachomekea tu lakini ukweli hii kazi ni ya kupata hela kiulaini kabisa, wewe upige meza tu na kuunga mkono kila jambo, inatosha kabisa kuwepo salama kwa muda wote.

Kuna haja sasa mishahara yao iangaliwe upya inawadhalilisha wengine kuna watu wapo tayari kupoteza roho zao kwa kulinda nchi hii, kuna wanaofanya kazi hatarishi za kupambana na majangili na majambazi ambao roho zao zipo nje ndani wakati wa utekelezaji, inakuwaje hawa wapiga meza na blah blah wanalipwa hela iliyovuka mipaka?
 
Hiyo ni roho mbaya, kutaka wenye kingi kipunguzwe si sawa, wewe komaa upate kama wao
 
images (43).jpeg
images (49).jpeg


Picha hizi mbili zitoshe kutupa majibu.

Ni nchi moja ambayo kiongozi anapiga full tank magari ya kifahari kwenye mikutano ya kampeni.

Watoto wa wanaopiga kura wanakaa chini! Zaidi ya hapo wanaambiwa ufaulu umeongezeka ila ikifika January wanaambiwa wasubiri madarasa yajengwe na huku kuna watu wanavuta 15M mfukoni kwa mwezi na gari la 200M+ kiyoyozi muda wote huku watu wakiambiwa ni wanyonge na wamepata mtetezi!

"HUO NDIO UKWERI , NASEMA UONGO NDUGU ZANGU? HII NCHI IMECHEZEWA SANA.
 
Huo ndio ukweli mishahara ya au mshahara wa mbunge na mapochopocho wanayokwapua au kulipwa ni mishahara hatarishi kwa Taifa letu ambalo linajikongoja...

Mkuu nisiache kutia neno hapa:

".....,inakuwaje hawa wapiga meza na blah blah wanalipwa hela iliyovuka mipaka ?"

Kimsingi wao ndiyo wenye kuwapangia na kuwahoji wapanga mishahara ya kuwa nani alipwe nini, wakiwamo wao.

Wabinafsi wale kama walivyo, siku wakiamua wawe wanalipwa wao tu, au hata kidogo chetu pia waongezewe wao, ndiyo itakuwa imetoka hiyo!

Kwa hakika ni wawamba ngozi (au ngoma) wazuri kuliko maelezo.
 
Huo ndio ukweli mishahara ya au mshahara wa mbunge na mapochopocho wanayokwapua au kulipwa ni mishahara hatarishi kwa Taifa letu ambalo linajikongoja...
Hawa hakuna haja ya kupunguza mishahara yao, posho zao zipunguzwe kwa 25% maana posho ni mara 500% ya mshahara
 
Huo ndio ukweli mishahara ya au mshahara wa mbunge na mapochopocho wanayokwapua au kulipwa ni mishahara hatarishi kwa Taifa letu ambalo linajikongoja. Ajira ya ubunge sasa imekuwa ni ya kufa na kupona...
Wabunge wa Bunge la Kenya wako tatu bora ya Wabunge wanaolipwa pesa nyingi zaidi duniani! Wabunge wa Tanzania hata mia moja bora hawamo! Kuwalalamikia ni wivu tu!
 
Na ukumbuke hawakatwi kodi yaani ni kitonga tu, au museleleko tu hakuna mlima, halafu wanasema wana inchi tulipe kodi ya uzarendo, pamoja na makato yote tunayo kumbana nayo wao wanaona hayatoshi watukamue mpaka tone la mwisho kabisa.
 
Huo ndio ukweli mishahara ya au mshahara wa mbunge na mapochopocho wanayokwapua au kulipwa ni mishahara hatarishi kwa Taifa letu ambalo linajikongoja...
Nadhani ni standard ya mabunge ya Jumuiya ya Madola (the Commonwealth) ambayo Tanzania ni mwanachama.
 
Hiyo ni roho mbaya, kutaka wenye kingi kipunguzwe si sawa, wewe komaa upate kama wao
Ingekua wanavyanzo vyao vya mapato tusingewaonea wivu .kinachotuumiza Ni hizi Kodi tunazolipa sisi wajasiriamali wadogo Tena kwa kuvuja jasho mno wao wanachukua kiulaini Sana .Bora izo pesa zingeenda kufanya miradi ya maendeleo kuliko kulipaa watu Kama Hawa ambao wanajiwakilisha wao tu uko bungeni.
 
Back
Top Bottom