Na itakuwa hivyo
Maisha ya mjini kipindi nimepanga nilichoshwa na zile fujo, barabara ilipojengwa nilifurahia lakini ikageuka kero, magari yanapaki nje ya nyumba, mtaro mchafu, gari kubwa ikipita kuna mtetemo, n.k.
Kuna kiwanja cha karibu iligeuza kuwa gereji yani mafundi nyundo ni tabu juu ya shida
Omba sana kanisa la kilokole au msikiti ukajengwa maeneo ulipo, utaijua maana ya noise polution
watu wengi wanahama, wanauza nyumba zijengwe biashara, kuna iwezekano mdogo wa kuwa na jirani mlieishi zaidi ya miaka 20.
watoto kutoka nje zaidi ya kwenda shule kuna usalama mdogo wanalazimika kuwa Geti kali