Simwelewi rafiki yangu anataka nini kwangu

Simwelewi rafiki yangu anataka nini kwangu

Hivi nyinyi mnafikiri mimi nimetoka chekechea jana? Mpaka nimeanzisha uzi mbinu zote zimeshindikana na jamaa bado mshiji kwa sana tu.
Duuu.. wewe huhisi kumfeel??
binafsi hiyo kitu ilwai nitokea, kuna mwanamke nlimtamanigi sana nikajenga urafiki nae, sasa nikahisi kama urafiki umenoga kuliko mapenzi so nkampotezea tukawa washkaji tu kumbe naye ananipenda, nilikua kupiga baada ya miaka 2 sema penzi alikudumu sana now tupo washkaji tu na huwa mara chach sana tukikutana tunakumbushia
 
Habari za kutwa waungwana,

Nina rafiki tumefahamiana miaka minne iliyopita, kufahamiana kwetu tulikutana kwenye sherehe na tulikaa viti vya karibu na tuliongea na kucheza mziki pamoja. Wakati sherehe ikiendelea nilianza kufikiria usafiri wa kunirudisha nyumbani, nilianza kumuuliza jinsi nitakavyopata tax, aliniuliza kuelelekea wapi? Hapo ndipo niligundua ni jirani yangu kabisa.

Tulichukua tax moja, na baada ya pale tulibadilishana namba za simu.
Kesho yake alinipigia simu, alinialika niende kanisani kwao, nililipenda lile kanisa, niliendelea kusali pale kwa muda. Nilikuja kufahamu huyu kaka ni mlokole wa kufa mtu, mara nyingi ananipigia simu tunachat, mazungumzo mengi ni current affairs, dini, na mara nyingine ananipa offer za dinner.

Kuna wakati nilimwambia nitakwenda nyumbani kuwaona wazazi, aliniambia nisiondoke bila kumuaga, siku ninaondoka alikuja na bahasha nzito. Niliifungua nikiwa njiani, aliniwekea mpunga wakueleweka. Nilimtumia message ya asante, alinijibu asante na karibu. Nilivyorudi nilimfahamisha nimerudi basi. Hajawahi kunisimulia habari ya girl friend, wala hajanitongoza ni mwaka wa nne huu.

Simuelewi huyu rafiki yangu nisaidieni ndugu zangu.
Utongozwe mara ngapi?Nothing goes for nothing. Kwa hayo yote mjibu i love you too
 
Huu ni mtongozo wa slow motion si mwendo kasi.
 
Mmmh ulivyosikia bahasha iliyotuna tu roho imechachamaa! Si ulisema unakwenda kulima siku ile? Vp kilimo hakilipi?
[emoji100] [emoji125] [emoji125] [emoji125] [emoji125]
Watoa hela kama huyo ndo mzuri sasa. Nifanyie makeke nitakupa pasu basi nawe
 
Huyo ni domo zege ila amekufa kaoza, kwa upande wa pili inaonekana ulitaka uwe umeshampa dudu kama asante. Mpetu wanaume hatufanani.
 
Back
Top Bottom