Simulizi za polisi kuua gaidi Arusha

Simulizi za polisi kuua gaidi Arusha

Polisi siku hizi simwamini hata angekuwa baba yangu mzazi nisingemwamini,naona wanaongoza kwa uongo!!
 
MTUHUMIWA WA UGAIDI KUUAWA ARUSHA inasikitisha sana, japo sina undugu na uhalifu wa aina yote. Polisi kama kawaida wanajitahidi kueleza, pamoja na dai la interijensia ya kisasa, ni waongo na wakiukaji wa haki za binadamu wakubwa! Bahati mbaya tume ya haki za binadamu tz ipo ipo tu, haina la maana inalofanya kuangalia na kukemea maovu wanayotendewa wananchi na dola! Hebu jiulize mtuhumiwa tangu ashikwe mpaka anauliwa na polisi siku zote hizo kwa nini hakupelekwa mahakamani?
 
Huyo jamaa alikuwa noma balaa.Nasikikia walitumia siku kadhaa kumkamata baada ya kuzingira nyumba alimokuwa
 
Ama kweli huyo jamaa ni noumaaaaa! pamoja na pingu mikononi na miguuni na gari ikiwa kwenye speed tena usiku katikati ya maasikari tena gari iliyofunikwa iliweza aliweza kuruka!
kali zaidi risasi ya mkuuni na matakoni imemuua hapo hapo wala hata hakuwahi kufikishwa hosipitalini!
mara alipue mashekh mara makanisa (the same person, contradicting), mara akalipue mikutano ya chadema mara akalipua mabar mara akamwagie mashekh tindikali (the same man)!
to me, it rising many answers than questions!

polisi wasitufanye sisi watoto kwa maelezo yao yasiyo na mantiki
 
Swali ni je alichokisema kamanda Sabas ni kweli au ameudangaya umma?amesema huyu jamaa alikua anakimbia ,lakini ukiangalia amepigwa risasi na mtu aliyekua mbele yake
Alisema amepigwa kiunoni ni kweli hapo ni kiunoni?

Hii ni stori nyingine,ila ni stori ISIYO na tofauti kabisa na ya wafanyabiashara wa Ifakara waliouawa na mapolisi huko Sinza.
 
Ipo siku atakufa kiongozi wa ccm mkubwa watu wataingia baribarani kushangilia..
 
kama polisi katika intelijensia yao wanaamini kwamba Mwangosi aliuwawa na chadema kwa kutupiwa kitu kutoka kwa mashabiki wa chadema,unafikiria hapo tutaambiwa hadidhi gani zaidi ya kudaganywa? ili kuepukana na haya mabo ni lazima wananchi wakubali kuitoa serikali ya ccm madarakani,tatizo ni baadhi ya waislamu pamoja na kufanyiwa haya yote bado wanaikumbatia ccm kwa kuambiwa tu eti chadema ni chama cha wakiristo
 
Swali ni je alichokisema kamanda Sabas ni kweli au ameudangaya umma?amesema huyu jamaa alikua anakimbia ,lakini ukiangalia amepigwa risasi na mtu aliyekua mbele yake
Alisema amepigwa kiunoni ni kweli hapo ni kiunoni?

Mkuu hata kama risasi za polisi zina uwezo wa kukata kona hapo alipopigwa sio kiunoni.
 
Najiuliza, saa 5.30 usiku walimlengaje kwa risasi mguuni na makalioni?

Vv
 
Habari za Tanzania zinatia kichefuchefu. Na ukizifuatilia utajikuta unapata presha kali sana kutokana na kupandwa na hasira. Kila uchao kila kiongozi anatoa utumbo tu.
 
...huyu mkubwa ndiye anafuga ugaidi...inakuwaje magaidi wanakuwa waislam tuuuuuuuuuu,mie sielewi hapa.Kote ni wao tuuu hii inakuwaje?.Kwa nini kipindi huyu bwana ndo mabomu mabomu,mapadri risasi risasi?


Uzuri haya mambo yanaenda kwa awamu leo raia anauawa kwa tuhuma tu ambazo hazijathibitishwa na mahakama mnaleta majibuya kejeli. Endeleeni kushangilia kwa vile mnaona jamii fulani ndo inaumia, lakini nina uhakika mwakani mauaji kama haya yatawakuta wanasiasa. Na sisi kelele zenu tutazijibu kwa kejeli.
 
Bahati yake mbaya marehemu. Kuna kitu kipo ila ngumu kukigundua kwa haraka maana ni siri ziko kwenye makablasha ya vyombo vya usalama. Inawezekana alikuwa ni liability....how, I dont have any idea. Vijana wenzangu tuwe makini sana na haya mambo ya kujiingiza kwenye vikundi ambavyo hatujui vimebeba nini ndani yake...kutumika halafu kuishia kienyeji kama huyo jamaa inasikitisha sana. Imagine baada ya wiki mbili tu za kukamatwa ametangulia mbele ya haki akiruka judo/karate kupigana na risasi. What a movie.

Tujikite katika kufuata sheria na taratibu za nchi kuepukana na maswahiba yasiyo na tija kama ya huyu jamaa.
 
Ama kweli huyo jamaa ni noumaaaaa! pamoja na pingu mikononi na miguuni na gari ikiwa kwenye speed tena usiku katikati ya maasikari tena gari iliyofunikwa iliweza aliweza kuruka!
kali zaidi risasi ya mkuuni na matakoni imemuua hapo hapo wala hata hakuwahi kufikishwa hosipitalini!
mara alipue mashekh mara makanisa (the same person, contradicting), mara akalipue mikutano ya chadema mara akalipua mabar mara akamwagie mashekh tindikali (the same man)!
to me, it rising many answers than questions![/QUOTE

Mkuu umesahau kuwa tumeambiwa alikuwa bingwa wa karate na judo? Lazima alitokea kwenye paa. Yaani hii hadithi imefanya niamini kuwa kumbe Jack Chan sinema zake sio fiction!

Ama polisi wametuweza na story yao!
 
sina imani na hili jeshi la polisi...
Wazungu husema ukiwa muongo jitahidi uwe na kumbukumbu nzuri.. "Liars must have a good memory"

Jeshi la Polisi nchini limetoa taarifa ya kuuawa kwa kijana Yahaya Omary mtuhumiwa wa milipuko ya mabomu Arusha. Polisi wanasema wamemuua kwa kumpiga risasi mguuni na kwenye ---- alipokua akijaribu kukimbia.

Lakini picha ya marehemu iliyoonekana baadae inaonesha kupigwa risasi ya tumbo. Sasa kwanini Polisi wamedanganya ni mguu na ----?? Wanataka kuficha nini?

Bila shaka Polisi walidhani picha ya mtuhumiwa akiwa kauawa haitaonekana.. hivyo wakaamua kudanganya ili kuhalalisha mauaji. Lakini hatimaye picha imeonekana akiwa kapigwa risasi ya tumbo, Polisi wameumbuka.

Pili, hivi mtu anayekimbia anapigwaje risasi ya tumbo? Alikua anakimbia kinyumenyume au? Maana kama kweli alikua anakimbia angepigwa risasi kwa nyuma si tumboni.

Lakini hii si mara ya kwanza jeshi la Polisi kuingia kwenye tuhuma za kuua watu wasio na hatia na kushindwa 'kujustify' mauaji hayo.

Mwaka 2006 aliyekua kaimu RPC wa mkoa wa Dar, Bw.Abdalah Zombe aliorganize mauaji ya wafanya biashara wa madini kutoka Mahenge Morogoro na kusingizia ni majambazi. Akafika mbali zaidi na kudai walikua wanarushiana risasi na Polisi.!

Lakini ripoti ya Tume ya Jaji Kipenka ikawaumbua Polisi maana ripoti ilionesha watuhumiwa wote walikua wamepigwa risasi visogoni. Ikabainika pia si kweli kuwa walikua wakirushiana risasi na polisi.

Huwezi kurushiana risasi na Polisi then upigwe risasi kisogoni.. Jaji Kipenka akawaumbua Polisi kwa kueleza kuwa wafanyabiashara wale walifungwa kamba mikono na miguu, kisha wakafungwa vitambaa vyeusi machoni ndipo wakapigwa risasi.

Halafu baada ya kuhakikisha wameuawa Polisi wakawapora jumla ya sh. mili.200 na madini waliyokua nayo. Kisha Zombe akaita mkutano na waandishi wa habari akasema kuna majambazi yameuawa yakijaribu kurushiana risasi na Polisi.

Ukatili, ukatili, ukatili wa kiwango cha kutisha. Yani uwakamate watu wasio na hatia, uwafunge vitambaa usoni, uwapige risasi, kisha uwapore mali na fedha walizonazo.. halafu bado uwasingizie ujambazi.. Kwa kweli Mungu wetu ni wa huruma sana lakini hii dhambi sijui kama inasameheka.

Mazingira ya kuuawa kwa wafanyabiashara wale yanafanana na mazingira ya kuuawa kwa kijana Yahya Omary anayedaiwa kulipua mabomu Arusha.

Kwanza inadaiwa alikua anakimbia, lakini risasi kapigwa tumboni. How comes? Mtu anayekimbia tulitegemea apigwe risasi mgongoni au maeneo ya nyuma ya mwili lakini si tumboni. Huu ni uongo wa kitoto kabisa.!

Polisi wanadai eti mtuhumiwa alikua mcheza karate na judo, hivyo alitumia mbinu zake za karate ili kuwakimbia Polisi.

Cha ajabu mtuhumiwa alikua hajafungwa Pingu mikononi wala miguuni. Hivi unaweza kumkamata mtuhumiwa wa kulipua mabomu tena anayejua kucheza "karate na judo" halafu umsafirishe bila kumfunga pingu? Hizi ni hekaya za Abunuasi.!

Halafu Polisi wanasema eti alitoroka akiwa chini ya Ulinzi mkali.. Hivi Ulinzi mkali ndo kumsafirisha mtuhumiwa bila pingu?? Uongo wa kitoto kabisa huu.!

Nashauri Rais Kikwete aunde tume kuchunguza mauaji ya kijana huyu kama alivyounda Tume ya Jaji Kipenka kuchunguza mauaji ya wale wafanya biashara wa Mahenge. Huenda kijana huyu ameuawa ili kupoteza ushahidi.!

Huenda Polisi wanamjua mhusika wa mabomu ya Arusha, na labda ni "kigogo mkubwa" ambaye hawawezi kumgusa.. Hivyo wameamua kumuua kijana Yahaya ili kupoteza ushahidi.

Nimeona vyombo vingi vya habari vikiandika habari hii kwa ushabiki. Vingi vimeonesha kufurahishwa na mauaji ya kijana huyu. Gazeti moja limeandika "ALIYELIPUA MABOMU ARUSHA AUAWA".

Hili gazeti sijui kama lina Mhariri, maana hii si habari. Huwezi kusema "aliyelipua mabomu arusha..." wakati haijadhibitika kama ni kweli alihusika au lah.!

Yahaya alikua mtuhumiwa tu na angefikishwa mahakamani ukweli ndio ungejulikana. Huenda si yeye aliyehusika na mabomu na labda hata hajui lolote kuhusu mabomu.. Labda Yahaya alikua na ugomvi na kiongozi wa serikali ndo akaamua kumbambikia hii kesi.

Na chombo pekee cha kusema ukweli ni mahakama.. Lakini serikali kwa kujua kesi ikienda mahakamani wataumbuka na itajulikana Yahaya hakuhusika na mabomu ya Arusha wakaamua kukatisha maisha.

Wakamuua kikatili kabla kesi haijaenda mahakamani. Wawakamsingizia eti alijaribu kukimbia. Kivipi alijaribu kukimbia wakati kapigwa risasi ya tumbo.?

Lakini magazeti yamemhukumu.. yamemuita muuaji.. mrusha mabomu.. mengine yamemuita jambazi sugu..

Nayaogopa magazeti ya Tanzania. Ni magazeti hayahaya yaliyowahukumu wale wafanyabiashara wa Mahenge waliouawa na Polisi wa Zombe. Magezeti yakaandika "MAJAMBAZI KUTOKA MORO YAUAWA DAR."

Lakini ilipokuja kubainika hawakua majambazi magazeti hayohayo yakaandika "KASHFA NZITO JESHI LA POLISI; WADAIWA KUUA RAIA WASIO NA HATIA NA KUWABAMBIKIZIA KESI YA UJAMBAZI"

R.I.P Yahaya Omary, binafsi siwezi kukuhukumu kama magazeti yanavyofanya, maana sijui kama ni kweli ulihusika na mabomu ya Arusha au lah.

Labda mahakama ingeweza kutuambia ukweli.. lakini kwa kuwa umetangulia MUNGU pekee ndio anajua ukweli.

Pumzika kwa amani Yahaya.. Hata waliokuua ipo siku nao watakufuata. Duniani sote tunapita.. hakuna atakayeishi milele.. ipo siku ukweli utafahamika na itakuwa kilio na kusaga meno kwa wote walioshiriki mauaji haya ya kinyama dhidi yako.!

JIPU LIMEPASUKA, SIWEZI KUWA ADUI KWA KUSEMA UKWELI.!
source
Malisa GJ || Your Partner in Critical Thinking.!
 
imeniacha hoi hii stori. yaani mtu mwenye pingu miguuni na mikononi halafu kazungukwa na polisi ndani ya gari iliyofunikwa kwenye speed barabara ya lami na ukiangalia hiyo risasi imepigwa kwa mbele wala sio kwa nyuma. ni usanii na maigizo kwa kwenda mbele.


Ama kweli huyo jamaa ni noumaaaaa! pamoja na pingu mikononi na miguuni na gari ikiwa kwenye speed tena usiku katikati ya maasikari tena gari iliyofunikwa iliweza aliweza kuruka!
kali zaidi risasi ya mkuuni na matakoni imemuua hapo hapo wala hata hakuwahi kufikishwa hosipitalini!
mara alipue mashekh mara makanisa (the same person, contradicting), mara akalipue mikutano ya chadema mara akalipua mabar mara akamwagie mashekh tindikali (the same man)!
to me, it rising many answers than questions![/QUOTE

Mkuu umesahau kuwa tumeambiwa alikuwa bingwa wa karate na judo? Lazima alitokea kwenye paa. Yaani hii hadithi imefanya niamini kuwa kumbe Jack Chan sinema zake sio fiction!

Ama polisi wametuweza na story yao!
 
Nimemsimulia mwanangu mdogo stori hii akaniona na mimi mwongo!!
 
Habari za Tanzania zinatia kichefuchefu. Na ukizifuatilia utajikuta unapata presha kali sana kutokana na kupandwa na hasira. Kila uchao kila kiongozi anatoa utumbo tu.
kula LIKE..Mimi ndomaana sina muda na magazeti ya tz na habari zozote za tz coz zimejaa shaka sana na haziaminiki vilevile zimelalia upande mmoja.
 
Back
Top Bottom