Simulizi za Kusisimua: Nyerere alipoingiwa huruma Mwana-TANU Mwenzake kukosa Nauli...

TEWA SAID TEWA MEMBER WA ''WEDNESDAY TEA CLUB,'' TAA, MUASISI WA TANU, RAIS WA EAMWS, WAZIRI SERIKALI YA KWANZA, BALOZI, MBUNGE NA KIONGOZI WA WAISLAM WA TANGANYIKA
Anaandika mwandishi wa historia Mohammed Said

Picha hizi (hapo chini)zinatoka katika Maktaba ya Said Tewa mtoto wa marehemu Tewa Said Tewa ambae kwa miaka mingi amekuwa akiishi Denmark. Said anasema ameniletea picha hizi baada ya kuona juhudi zangu katika kuhifadhi historia ya Tanzania na viongozi wake baba yake akiwa mmoja wao iliyokuwa karibu ipotee. Hayo maandishi, ‘’caption,’’ katika baadhi ya picha ni mwandiko wake mwenyewe Mzee Tewa. Picha nilizopokea ni nyingi sana zikimwonyesha Tewa Said Tewa katika mengi lakini nimeona nichukue hizi chache ambacho zitamuunganisha yeye na matokeo muhimu zaidi katika historia ya Tanzania na katika nafasi yake kama kiongozi wa Waislam akiwa Rais wa East African Muslim Welfare Society upande wa Tanzania. Binafsi nimejifunza mengi kutoka kwa Mzee Tewa tukiwa tumekaa sisi wawili tu nyumbani kwake Magomeni Mikumi akinihadithia historia ya uhuru wa Tanganyika.

Msikilize Mzee Tewa:

Tewa Said anakumbuka siku kabla ya uchaguzi pale Ukumbi wa Arnatouglo, Abdulwahid alikwenda nyumbani kwake jioni. Wakati huo Tewa alikuwa akikaa mtaa huo huo wa Aggrey na Swahili, si mbali sana kutoka nyumbani kwa Abdulwahid. Abdulwahid alimwambia Tewa maneno haya kuhusu mabadiliko ya uongozi ambayo waliamua kuyafanya katika TAA:

‘’Tewa, kesho tunakwenda kumpa huyu mtu, Nyerere, mamlaka ya kuendesha nchi hii. Kuanzia hapo, mara tu tutakapomchagua kutuongoza hakuna namna tena ya kumnyangíanya madaraka tuliyompa. Hatumfahamu vizuri sana lakini natumaini kila kitu kitakwenda sawa.’’

Mengi kuhusu Tewa Said Tewa unaweza kuyasoma hapo chini:
Mohamed Said: Tewa Said Tewa Mmoja wa Waasisi wa TANU 1954
asante sana mkuu
 
Imesemwa kua maisha ya mbeleni ni kwa walioyaandaa. Hawa wapigania uhuru kama hawakuandaa maisha ya baadae kwa watoto na watu wao wa karibu sioni ni kwa jinsi gani watakumbukwa. Mfano sasa viongozi na watu wenye nafasi wamekua mstari wa mbele kuwapa elimu nzuri vijana wao, na hii imepelekea kuona majina yao mengi yakijirudia kwenye nyanja za siasa na uongozi kwa ujumla.
Nikirudi kwenye historia ya nyuma ya kina mzee Sykes, Abdulwahid, Dossa Aziz na wengineo, kwa jinsi ilivotolewa hapa na ndugu Majjid kisha Mohamed Said inaonekana kama kuna aina fulani ya kutengwa au kutotendewa kwao haki na mfumo uliokuwepo. Walijitahidi kuweka misingi ya ile walioamini inafaa kwao, walianzisha taasisi mbalimbali za kiislam za kielimu na kadhalika, nadhani lengo kubwa ilikua ni kustawisha na kuendeleza imani ya kiislam. Nimeona kwamba malengo yao hayakufanikiwa kwanza kwa sababu ya migogoro baina yao, sijui chanzo ni nini, pili ni kuhamishwa kwa bwana Tewa kwenda nje ya nchi ilififisha nguvu yao, pia inaonekana kama kulikua na nguvu nyingine iliyokua inapingana nao. All in all naona walikua na agenda ya kuusambaza uislamu na kuwapa nguvu waislamu kielimu na kifikra kitu ambacho sio kibaya, ni kwama wakristo wanavofanya kwa kua na taasisi mbalimbali za kielemu na nyinginezo.
Lakini kushindwa kwao hasa labda kuna agenda nyingine ambayo labda hatuifahamu au imefichwa kwetu. Kwa nini taasisi za kikristo zilistawi ila za kiislam zilisua sua? Je sera za taasisi za kikristo zilikua bora sana na zenye matokeo chanya kuliko za kiislam? Je kuna sababu nyingine iliyowaangusha waislamu na taasisi zao toka kipindi kile cha wapigania uhuru? Nashindwa kubase popote maana sina info kutoka upande wa pili hasa tukirefer msemo aliosema mzee Tewa kua siasa ni mchezo mchafu, maana hapo kuna kitu kilifanyika au walifanywa au walifanya na hakikufanikiwa, na kitu hicho kilihama kutoka kwenye dini kikajihusisha na siasa, au vyote viwili dini na siasa.
 
Mwenyekiti nakufuatilia sana makala zako ww ni mwandishi nguli kwa hyo kwenye historia sensitive kama hizi ni wajibu kujiridhisha sio kukusanya kukusanya kama barza

Bafa,
Shukran mjumbe wangu, Mwenyekiti wako sina hulka ya kukusanya kusanya. Shida baadhi ya wachangiaji huchangia huku wakifikiri badala ya kufikiri na kuchangia.
 
Tusalmie mapacha mwenyekiti
 
Maggid umeguswa na suala la nauli badala ya kuhoji kwa nini Dossa Aziz na wengine hawasomeki katika historia ya nchi?

Hawakuwa na vigezo vya kuwa viongozi hasa wakilinganishwa na nani?

Kwa nini kabla ya uhuru walikuwa matajiri na wanaonekana kufilisika baada ya uhuru na hata vizazi vyao havisikiki?

Mabinti,vijana,na wajukuu wao wako wapi? kwa nini familia ya Bibi Titi haisikiki?

Nini kiliikumba familia ya kambona? ina maana hakuna mwana familia ya kambona aliye excel hata kielimu?

watu tunahoji mambo trivial badala ya kujiuliza maswali magumu
Umenena kwa mapana sana mkuu na nadhani tulifanye kama challenge kwa ndugu Maggid arudi uwanjani (field) akafande akafanye dodoso tena na ikibidi atuletee taarifa zaidi kwa faida ya wengi haswa vijana. Kimsingi kizazi cha sasa hivi kina taarifa finyu na uelewa mdogo sana wa hawa mashujaa wetu sababu kubwa ikiwa ni wao kutowekwa katika kumbukumbu nzuri (maandishi) ambayo itafanya kila kizazi kijacho kiweze kufahamu mchango wao
 
Habari za akina Dossa Aziz na wengineo zinapatikana kwenye vitabu vya historia. Kama hatusomi vitabu hilo ni tatizo lingine.
 
Imesemwa kua maisha ya mbeleni ni kwa walioyaandaa. Hawa wapigania uhuru kama hawakuandaa maisha ya baadae kwa watoto na watu wao wa karibu sioni ni kwa jinsi gani watakumbukwa. Mfano sasa viongozi na watu wenye nafasi wamekua mstari wa mbele kuwapa elimu nzuri vijana wao, na hii imepelekea kuona majina yao mengi yakijirudia kwenye nyanja za siasa na uongozi kwa ujumla.
Nikirudi kwenye historia ya nyuma ya kina mzee Sykes, Abdulwahid, Dossa Aziz na wengineo, kwa jinsi ilivotolewa hapa na ndugu Majjid kisha Mohamed Said inaonekana kama kuna aina fulani ya kutengwa au kutotendewa kwao haki na mfumo uliokuwepo. Walijitahidi kuweka misingi ya ile walioamini inafaa kwao, walianzisha taasisi mbalimbali za kiislam za kielimu na kadhalika, nadhani lengo kubwa ilikua ni kustawisha na kuendeleza imani ya kiislam. Nimeona kwamba malengo yao hayakufanikiwa kwanza kwa sababu ya migogoro baina yao, sijui chanzo ni nini, pili ni kuhamishwa kwa bwana Tewa kwenda nje ya nchi ilififisha nguvu yao, pia inaonekana kama kulikua na nguvu nyingine iliyokua inapingana nao. All in all naona walikua na agenda ya kuusambaza uislamu na kuwapa nguvu waislamu kielimu na kifikra kitu ambacho sio kibaya, ni kwama wakristo wanavofanya kwa kua na taasisi mbalimbali za kielemu na nyinginezo.
Lakini kushindwa kwao hasa labda kuna agenda nyingine ambayo labda hatuifahamu au imefichwa kwetu. Kwa nini taasisi za kikristo zilistawi ila za kiislam zilisua sua? Je sera za taasisi za kikristo zilikua bora sana na zenye matokeo chanya kuliko za kiislam? Je kuna sababu nyingine iliyowaangusha waislamu na taasisi zao toka kipindi kile cha wapigania uhuru? Nashindwa kubase popote maana sina info kutoka upande wa pili hasa tukirefer msemo aliosema mzee Tewa kua siasa ni mchezo mchafu, maana hapo kuna kitu kilifanyika au walifanywa au walifanya na hakikufanikiwa, na kitu hicho kilihama kutoka kwenye dini kikajihusisha na siasa, au vyote viwili dini na siasa.
Edger...
Nimeleza yote nini kilitokea katika kitabu cha Abdul Sykes.

Sehemu hiyo ni sehemu ya tatu ya kitabu nimeiita: Njama
Dhidi ya Uislam.

Hayo ambayo wewe huyajui mimi nimeyaleza kwa kuwataja
hadi majina wahusika wakuu.
 
Umenena kwa mapana sana mkuu na nadhani tulifanye kama challenge kwa ndugu Maggid arudi uwanjani (field) akafande akafanye dodoso tena na ikibidi atuletee taarifa zaidi kwa faida ya wengi haswa vijana. Kimsingi kizazi cha sasa hivi kina taarifa finyu na uelewa mdogo sana wa hawa mashujaa wetu sababu kubwa ikiwa ni wao kutowekwa katika kumbukumbu nzuri (maandishi) ambayo itafanya kila kizazi kijacho kiweze kufahamu mchango wao
Kabokocastory,
Njama ilikuwa ni kufuta kabisa historia ya TANU kwa kuhofu
kuwa historia ya uhuru wa Tanganyika ni historia ya Waislam
wa Tanganyika.

Mwaka wa 1988 gazeti la Africa Events (London) lilipochapa
makala yangu ''In Praise of Ancestrors,'' ambamo ndani niligusia
mchango wa Abdul Sykes katika kuunda TANU na mchango
wa Waislam katika kupigania uhuru wa Tanganyika, toleo zima
lilikusanywa na kutolewa katika mzunguko,

Yapo mengi.
Kwa sasa tusimame hapa kwanza.
 
Maggid,
Hakuna hata kitabu kimoja cha historia kilichowataja akina Dossa.
Ikiwa kipo naomba nifahamishe jina la kitabu.
Mwalimu wangu Mohammed,
Nina hakika jina la Dossa Aziz limeandikwa vitabuni kama kumbukumbu ya kihistoria. Bahati mbaya niko Dar na mbali na maktaba yangu iliyo Iringa. Ingawa hivyo, kwa haraka nakutumia link ya kitabu hiki ambacho kinapatikana mtandaoni..Nyerere and Africa
 
Ndugu zangu,

Leo Ni Tisa Disemba. Ni Siku yetu kuu kusheherekea Uhuru wetu. Tumetimiza miaka 55 ya uhuru. Tuna kila sababu za kusheherekea.

Nitapenda niweke hapa simulizi ya kihistoria yenye kusisimua, na kuelimisha pia.

Kwenye andiko lake lililojenga nadharia ya kisiasa. ' The Prince' kwa maana ya Mwana Mfalme, Mwanafalsafa Machiavelli anazungumzia juu ya kiongozi aweje. Machiavelli anamtaka kiongozi kuwa makini na tabaka la waliomsaidia kuingia madarakani na hata wenye kumzunguka. Kwa mujibu wa Machiavelli, hutokea kwa Mwana Mfalme "kuwajeruhi" waliomsaidia kuupata utawala.
Hii ni kwa kutowatimizia yote yale waliodhani kuwa ni haki yaokutimiziwa.

Badala yake, Mwana Mfalme huwaingiza kundini wawe kama wengine.
Katika manung'uniko yao, Mwana Mfalme hawezi kutumia dawa chungu dhidi
yao kwa vile hujihisi ana deni kwao. Lakini, cha msingi kwa MwanaMfamle ni kuzingatia ukweli, kuwa, hata kama atakuwa na maaduiwachache, katika kuchukua nchi, muhimu ni kuwaridhisha walio wengi, nahapa ni wananchi.

Huwezi kutawala kwa amani bila upendo na utashi wa walio wengi. Ni kwa sababu hizi, Mfalme Louis XII wa Ufaransa aliweza kwa kasi ya ajabu kuitwaa Milan na kwa kasi ya ajabu kuipoteza Milan.

Hakukidhi matakwa na matarajio ya wananchi walio wengi waliomfungulia
milango.Mtawala aliye mbali na asiyejali maslahi ya watu wake walio
wengi ni mtawala mwenye hofu. Na mtawala mwenye hofu zaidi na watu
wake kuliko adui wa nje, basi, hujijengea kasri ama ngome imara ya
kujihifadhi ingawa hilo halitamsaidia kuzuia nguvu za umma za
kumwondoa madarakani. Kwa mtawala, kasri ama ngome iliyo imara ni
kuepuka kuchukiwa na wananchi, kuacha ubinafsi na kujali maslahi ya
wengi.

Ni katika hili, kuna ambao walimtarajia Julius Nyerere kuwapendelea wale waliomsaidia kuingia kwenye mamlaka. Lakini, Nyerere aliwaacha waingie kwenye kundi kuu, kwa maana wawe miongoni mwa wananchi. Wafanye kazi ya siasa lakini si kwa kupewa vyeo vya juu, kwa vile tu, walikuwa ni miongoni mwa wale 17 waliounda TANU.
Hapa nawazungumzuia watu kama akina Chifu Kunambi na Dossa Aziz. Chifu Kunambi alitoa hata eneo lake kwa maekari ili kijengwe Chuo Kikuu. Chifu Kunambi amekufa miaka kadhaa iliyopita akiwa anaishi maisha ya kawaida pale Ubungo Msewe.

Na kuna , Julius Nyerere alimuonea huruma sana Dossa Aziz alipokutana nae kule Kizota , Dodoma. Dossa Aziz alikuwa ni MwanaTanu mwenye kadi nambari 4. Ni Dossa Aziz aliyetoa Landrover yake itumike na TANU, ndio gari aliyotumia Nyerere kuzunguka vijijini kwa wananchi kuitangaza TANU. Ni Dossa Aziz na wenzake waliomchangia Julius nauli ya kwenda UNO kudai uhuru wa Tanganyika.

Lakini, pale Kizota, Dodoma, miaka ile ya 80 mwishoni, Julius Nyerere alimwona Dossa Aziz aliyechoka sana. Julius akaambiwa, kuwa hata nauli ya kwenda Dodoma, Dossa Aziz alisaidiwa na rafiki yake na classmate wake wa tangu Kitchwele School, Ally Sykes.

Julius Nyerere aliingiwa na huruma. Inasemwa, kuwa Julius, kwa fedha zake mwenyewe, alimnunulia Dossa Aziz gari la kutembelea.

Naam, simulizi ni nyingi...

Maggid Mjengwa.
0688 37 36 52 ( Whatsapp)
0754 678 252

Maggid,
Inaelekea huna habari kamili za Dossa Aziz.
Dossa
alikwenda Dodoma akifuatana na Abbas mdogo wake Ally Sykes.

Hapakuwa na suala la nauli kwa safari ya Kizota.

Alichonunuliwa Dossa ni nguo na viatu na aliyemnunulia ni Abbas Sykes
na ndiye aliyemlazimisha kuhudhuria mkutano ule kwani ingawa alialikwa
Dossa hakutaka kwenda.

Huoni ''similarities,'' kati ya uandishi huu na uandishi wangu
''style,'' ''content...'' katika baadhi ya sehemu?

Nakijua kitabu hiki.
Lete kitabu kingine hiki hakifai.
 
Mbona hao watu tunawafaham na tunatambua michango yao kama wapigania uhuru. Katika hutuba zake Nyerere amewataja hao watu mara kadhaa kutambua michango yao. MATAIFA HUWA HAYAJENGWI kwa kuwagawia watu vyeo na mali. Kuna wapiganaji wetu walipoteza maisha katika Vita ya Kagera mbona hatusikii familia zao zikilalamika. Kuhusu mchango wa Waislam Nyerere ameeleza wazi kabisa katika hotuba zake; mlitaka afanye nini zaidi?
 
Ndugu zangu,

Leo Ni Tisa Disemba. Ni Siku yetu kuu kusheherekea Uhuru wetu. Tumetimiza miaka 55 ya uhuru. Tuna kila sababu za kusheherekea.

Nitapenda niweke hapa simulizi ya kihistoria yenye kusisimua, na kuelimisha pia.

Kwenye andiko lake lililojenga nadharia ya kisiasa. ' The Prince' kwa maana ya Mwana Mfalme, Mwanafalsafa Machiavelli anazungumzia juu ya kiongozi aweje. Machiavelli anamtaka kiongozi kuwa makini na tabaka la waliomsaidia kuingia madarakani na hata wenye kumzunguka. Kwa mujibu wa Machiavelli, hutokea kwa Mwana Mfalme "kuwajeruhi" waliomsaidia kuupata utawala.
Hii ni kwa kutowatimizia yote yale waliodhani kuwa ni haki yaokutimiziwa.

Badala yake, Mwana Mfalme huwaingiza kundini wawe kama wengine.
Katika manung'uniko yao, Mwana Mfalme hawezi kutumia dawa chungu dhidi
yao kwa vile hujihisi ana deni kwao. Lakini, cha msingi kwa MwanaMfamle ni kuzingatia ukweli, kuwa, hata kama atakuwa na maaduiwachache, katika kuchukua nchi, muhimu ni kuwaridhisha walio wengi, nahapa ni wananchi.

Huwezi kutawala kwa amani bila upendo na utashi wa walio wengi. Ni kwa sababu hizi, Mfalme Louis XII wa Ufaransa aliweza kwa kasi ya ajabu kuitwaa Milan na kwa kasi ya ajabu kuipoteza Milan.

Hakukidhi matakwa na matarajio ya wananchi walio wengi waliomfungulia
milango.Mtawala aliye mbali na asiyejali maslahi ya watu wake walio
wengi ni mtawala mwenye hofu. Na mtawala mwenye hofu zaidi na watu
wake kuliko adui wa nje, basi, hujijengea kasri ama ngome imara ya
kujihifadhi ingawa hilo halitamsaidia kuzuia nguvu za umma za
kumwondoa madarakani. Kwa mtawala, kasri ama ngome iliyo imara ni
kuepuka kuchukiwa na wananchi, kuacha ubinafsi na kujali maslahi ya
wengi.

Ni katika hili, kuna ambao walimtarajia Julius Nyerere kuwapendelea wale waliomsaidia kuingia kwenye mamlaka. Lakini, Nyerere aliwaacha waingie kwenye kundi kuu, kwa maana wawe miongoni mwa wananchi. Wafanye kazi ya siasa lakini si kwa kupewa vyeo vya juu, kwa vile tu, walikuwa ni miongoni mwa wale 17 waliounda TANU.
Hapa nawazungumzuia watu kama akina Chifu Kunambi na Dossa Aziz. Chifu Kunambi alitoa hata eneo lake kwa maekari ili kijengwe Chuo Kikuu. Chifu Kunambi amekufa miaka kadhaa iliyopita akiwa anaishi maisha ya kawaida pale Ubungo Msewe.

Na kuna , Julius Nyerere alimuonea huruma sana Dossa Aziz alipokutana nae kule Kizota , Dodoma. Dossa Aziz alikuwa ni MwanaTanu mwenye kadi nambari 4. Ni Dossa Aziz aliyetoa Landrover yake itumike na TANU, ndio gari aliyotumia Nyerere kuzunguka vijijini kwa wananchi kuitangaza TANU. Ni Dossa Aziz na wenzake waliomchangia Julius nauli ya kwenda UNO kudai uhuru wa Tanganyika.

Lakini, pale Kizota, Dodoma, miaka ile ya 80 mwishoni, Julius Nyerere alimwona Dossa Aziz aliyechoka sana. Julius akaambiwa, kuwa hata nauli ya kwenda Dodoma, Dossa Aziz alisaidiwa na rafiki yake na classmate wake wa tangu Kitchwele School, Ally Sykes.

Julius Nyerere aliingiwa na huruma. Inasemwa, kuwa Julius, kwa fedha zake mwenyewe, alimnunulia Dossa Aziz gari la kutembelea.

Naam, simulizi ni nyingi...

Maggid Mjengwa.
0688 37 36 52 ( Whatsapp)
0754 678 252

Maggid,
Nimefanya kipindi kuhusu kumbukumbu ya uhuru wa Tanganyika:
Mohamed Said: KUMBUKUMBU YA UHURU WA TANGANYIKA 9 DESEMBA 1961 KIPINDI MAALUM RADIO KHERI 104.10
 
Maggid,
Inaelekea huna habari kamili za Dossa Aziz.
Dossa
alikwenda Dodoma akifuatana na Abbas mdogo wake Ally Sykes.

Hapakuwa na suala la nauli kwa safari ya Kizota.

Alichonunuliwa Dossa ni nguo na viatu na aliyemnunulia ni Abbas Sykes
na ndiye aliyemlazimisha kuhudhuria mkutano ule kwani ingawa alialikwa
Dossa hakutaka kwenda.

Maggid,
Huoni ''similarities,'' kati ya uandishi huu na uandishi wangu
''style,'' ''content...'' katika baadhi ya sehemu?

Nakijua kitabu hiki.
Lete kitabu kingine hiki hakifai.

Mwalimu wangu Mohammed,

Taarifa za Dossa Aziz wenye kusimulia yumkini hutoa tafsiri zao kulingana na matakwa yao. Kwenye hili la kitabu Mwalimu wangu Mohammed unasema hakifai, sasa mie niulize tu, hakifai kitabu ama mwandishi mwenyewe? Labda ungetusaidia kwa kutueleza kwanini wewe unadhani hakifai.
Natanguliza shukran kwako Mwalimu wangu Mohammed Said.
 
Sasa hizo nadhani ni chuki binafsi,hujui Pinda alikuwa nani nchi hii!!??Pinda analipwa kwa mujibu wa Sheria na Nyerere alikuwa Rais wa nchi hii.Yaani wewe ulitaka wagimbea Uhuru wote wawe marais au ulitaka wawe wanalipwa mshara.

Acheni propaganda ,nchi hii imekomblewa kwa harakati za maelfu ya watu na sio tu hao wachache ambao ninyi mnawapigania kwa kigezo cha dini zao.

Hao akina Sykes na Nyerere sio watu pekee walipigania Uhuru wa nchi hii.Hao walikuwa viongozi tu lakini kuna wengine pia walipata madhara mengine mbali na kifirisika.

Hata leo hii CHADEMA ikitwaa madaraka akina Mbowe watasomeka kwenye historia lakini vijana walipigwa mabomu Arusha wanaweza wasitajwe japo wamemwaga damu kupigania Demokrasia .Kuna watu leo hii wanazihakiwa kuwa "wanywa viroba" na bodaboda lakini ndio kundi kubwa lenye hamasa katika kupigania demokrasia.

Kwa hiyo tukisema kila aliyepigania Uhuru wa nchi hii wapewe heshima sawa hata Mimi na yule tunaweza kutaja babu zetu ambao nao walichangia mapambano ya Uhuru.tuache hisia potofu za kuona tunatengwa ilihali historia inawatambua wazee hao,labda kama walitegemea madaraka na kuwa first class citizens kitu ambacho sio sahihi katika kujenga nchi yenye usawa.
Wewe mtu nakushangaa,huachi kutaja dini na chuki binafsi,hayo yanakujaje hapa? Lakini nakusamehe bure kwani hata uandishi wako unaakisi akili yako,kwa mfano mshara ni kidudu gani? Kuzihakiwa ni nini? Any way ukimkimbiza kichaa kisa kakutukana,utakuwa ni kichaa zaidi yake.
 
Habari za akina Dossa Aziz na wengineo zinapatikana kwenye vitabu vya historia. Kama hatusomi vitabu hilo ni tatizo lingine.
Zaidi ya kitabu cha Maalim Mohamed Said nitajie kitabu kingine.Hata hicho chenyewe kinapigwa vita,miaka minne nyuma nilikuwa nafanya interview Pale Duce,kwa ajili ya TA history,profesa mmoja alikituhumu kuwa ni uandishi wa historia ya udini pale nilipokisite kuwa latest history book nilichokuwa nimesoma.Ina maana kwa mtazamo huo bado hao mashujaa wanapigwa vita.
 
Naelekea kukuamini wewe kwa hili kuliko maelezo ya comrade Mjengwa hili....eneo la chuo kikuu ni kubwa sana...sipati picha kama kweli mzee kunambi alimiliki lote hilo...
Siku zote hua nasema Tanzania hatuna waandishi wa habari ila tuna wana udaku. Si mjengwa wala mayalla. Hawana tofauti na Sisi watoa mada hapa japo hatuja someauandishi. Mtu anaandika kitu alichosimuliwa kijiweni anashindwa hata kuwafuata ndugu ama rafiki wa karibu wa Kunambi
 
Yeye alihusika kuyakamata na kukimilikisha chuo,raia wengi waliyaachia bure tuu,na wengine walipewa fidia kidogo.Mzee Kunambi alidai ni chuo cha pili duniani kuwa na eneo kubwa kikizifiwa na chuo kikuu kimoja kipo Canada. Nilikuwa na rafiki yangu Chambanenge sjui yuko wapi siku hizi.
Chuo cha pili kwa kuwa na eneo kubwa nyakati zile au?
 
Back
Top Bottom