Barikiwa sana mkuu,umenena yaliyo ya kweli.Mungu ibariki Tanzania.Kaka asante kwa Reply nzuri juu ya bandiko hapo juu, na mimi niseme hivi, mleta bandiko ameanza vizuri sana kwa kuelezea namna mwasisi wa taifa hili alivyokuwa na upeo mpana na wa mbele sana katika kupambanua mambo, ubinafsi haukuwa sehemu yake, upendeleo ulikuwepo na kuwatanguliza wengine alikuweka mbele hakuwaacha nyuma Watu wote waliokuwa chachu ya uhuru wa nchi yetu,
Ila alikuwa na akili sana yakujua wapi ni muweke nani na wapi nisimweke, ukitaka kuangalia kwa undani sana wanaharakati wote walioasisi uhuru wa nchi hii familia zao hazijabeba Legacy walioacha wazazi wao hata familia ya Nyerere yenyewe haijafanikiwa kwenye hili, nadhani nikwasababu ya filosofi iliyokuwepo wakati ule ambayo ilibebwa na kufuatiliwa vizur na wazazi wao, imebadilika sana kiasi hawakuweza kuendana na mabadiliko....
Pia viongozi wengi waliofuta katika utaawala wa Tanzania ubinafsi, kujipendeza, madili na ufisadi vimetawala hawakumbuki mtu Ila mfumo uliopo. Ndio maana matabaka na kubaguana Ndio moto unaotutafuna kimyakimya. Bado nauhusudu namna ya utaawala na approach aliyokuwa anaitumia Mwalimu katika kuyakabili matatizo na kutatua changamoto na namna alivyokuwa akiyaangalia mambo
Mungu adumishe Uhuru wa Tanzania katika Amani, umoja na Ushirikiano thabiti na madhubuti. Amen