Simulizi za Kusisimua: Nyerere alipoingiwa huruma Mwana-TANU Mwenzake kukosa Nauli...

Maggid umeguswa na suala la nauli badala ya kuhoji kwa nini Dossa Aziz na wengine hawasomeki katika historia ya nchi?

Hawakuwa na vigezo vya kuwa viongozi hasa wakilinganishwa na nani?

Kwa nini kabla ya uhuru walikuwa matajiri na wanaonekana kufilisika baada ya uhuru na hata vizazi vyao havisikiki?

Mabinti,vijana,na wajukuu wao wako wapi? kwa nini familia ya Bibi Titi haisikiki?

Nini kiliikumba familia ya kambona? ina maana hakuna mwana familia ya kambona aliye excel hata kielimu?

watu tunahoji mambo trivial badala ya kujiuliza maswali magumu
Mkuu unamaanisha historia ipi ?maana watz wengi tunawajua hao watu akina Dosa ,Sykes, Aziz n.k kama wapigania Uhuru Wa nchi hii.Je, labda wewe ungependa waandikweje ?

Umesema hao watoto wa wapigania Uhuru kama akina Bibi Titi ,Kambona hawasikiki.Je, ulitaka wasikike vipi? Wawe magavana ,mawaziri au ?Mkuu, hii nchi ni ya watanzania wote ,Fanya bidii tafuta fursa utasikika tu.Au mkuu ungependa labda wapewe vyeo vya bure bila jitihada kwa kuwaenzi baba/mama zao ?

Kama ulitaka hivyo,utakuwa umepotoka hatuwezi kuijenga nchi yenye usawa ikiwa tutawapendelea watu kwa majina yao/koo zao.Tukifanya hivyo tutatengeneza koo za watawala na koo za watwana.

Asante.
 
Ni kweli Maggid lakin mzee alikuwa analalamikia kiasi cha malipo ya uzeeni aliyokuwa anapokea,kwamba ilikuwa kidogo sana.Nilipomuuliza kuhusu kifo cha Sokoine,mzee alisema ,,,,aaa wapi,kawawa wanamsingizia tuuu,aliyemuua bado yuko serikalini na ni mtu mkubwa tuuu.Nilijitahid kumdadisi lakin wap mzee hakuniambia aliyekuwa anamaanisha.
Mwanga moja hiyo, nafikiri utakuwa umenielewa
 
Hapana,usimlaumu Majjid,huenda alitaka kuonesha jinsi mzee Dossa alivyotumia nguvu na mali zake na uhuru ulipopatikana hakuna aliyemjali akaishia kuwa fukara na akakutana na mnufaika wa juhud na mali zake,akaishia kumpa tuu nauli na kumnunulia gari ya kutembelea.Unajua kila jambo lina angle zake kadhaa ambazo mtu mmoja hawezi kuziona zote.
Mkuu wewe ungekuwa Nyerere ungemfanyia nini Dosa ili iwe sahihi ?
 
Niko karibu na mjukuu wa mzee chaurembo baada ya uhuru hawakuambulia chochote zaidi ya nyumba yao ya gorofa iliyo barabara ya msimbazi kutaifishwa na nyerere
 
Mkuu wewe ungekuwa Nyerere ungemfanyia nini Dosa ili iwe sahihi ?
Ningetaka maoni yake kuhusu nini angehitaji kufanyiwa.Kama cheo au biashara,kilimo au mengineyo.Ningemtengenezea mazingira ambayo yasingemfanya afe kwa majuto.Kwa ujumla tu kwamba ningemlipa fadhila kwa aliyonitendea binafsi,chama na hata nchi.Zaidi ya hayo,ningehakikisha anaingia katika vitabu vya historia ya nchi yake.
 
Hiyo sentesi ya mwisho hiyo habari yake sijawahi kuiona kwenye mabandiko aliyo'akiyaweka mzee Mohammed Said...sasa sijui hakupatapo kulijua hili!?but soon atakuja hapa nadhani atalitolea ufafanuzi kama sio kulipinga.
 
Wewe hata tu nishani ya heshima kwa hawa wazee kutambua mchango wao hakuna hivi we jiulize ulipo kua unasoma shule kunakitabu chochote ulisha soma kikakuonyeha watu walo changia mchango mkubwa kupata uhuru wa nchii hii zaid ya nyerere
Kwa kawaida historia haipatikani katika nyaraka moja.Mara nyingi historia hujengwa na mkusanyiko wa nyaraka nyingi tofautitofauti.

Hawa wazee wengine tumewafahamu kupitia maandiko mbalimbalia ambayo kwa pamoja yanajenga historia ya nchi yetu.

Sasa kama wameandikwa na historia inawatambua.Tatizo liko wapi!

Leo hii hata familia ya Nyerere haisikiki kwa kuwa hakutaka kuwa mbinafsi na kujipendelea yeye na familia yake eti kisa alipigania Uhuru na kuwa Rais wa kwanza.
 
Mkuu unamaanisha historia ipi ?maana watz wengi tunawajua hao watu akina Dosa ,Sykes, Aziz n.k kama wapigania Uhuru Wa nchi hii.Je, labda wewe ungependa waandikweje ?

Umesema hao watoto wa wapigania Uhuru kama akina Bibi Titi ,Kambona hawasikiki.Je, ulitaka wasikike vipi? Wawe magavana ,mawaziri au ?Mkuu, hii nchi ni ya watanzania wote ,Fanya bidii tafuta fursa utasikika tu.Au mkuu ungependa labda wapewe vyeo vya bure bila jitihada kwa kuwaenzi baba/mama zao ?

Kama ulitaka hivyo,utakuwa umepotoka hatuwezi kuijenga nchi yenye usawa ikiwa tutawapendelea watu kwa majina yao/koo zao.Tukifanya hivyo tutatengeneza koo za watawala na koo za watwana.

Asante.

Kaka asante kwa Reply nzuri juu ya bandiko hapo juu, na mimi niseme hivi, mleta bandiko ameanza vizuri sana kwa kuelezea namna mwasisi wa taifa hili alivyokuwa na upeo mpana na wa mbele sana katika kupambanua mambo, ubinafsi haukuwa sehemu yake, upendeleo ulikuwepo na kuwatanguliza wengine alikuweka mbele hakuwaacha nyuma Watu wote waliokuwa chachu ya uhuru wa nchi yetu,

Ila alikuwa na akili sana yakujua wapi ni muweke nani na wapi nisimweke, ukitaka kuangalia kwa undani sana wanaharakati wote walioasisi uhuru wa nchi hii familia zao hazijabeba Legacy walioacha wazazi wao hata familia ya Nyerere yenyewe haijafanikiwa kwenye hili, nadhani nikwasababu ya filosofi iliyokuwepo wakati ule ambayo ilibebwa na kufuatiliwa vizur na wazazi wao, ilibadilika sana mbeleni kiasi kwamba watoto hawakuweza kuendana na kasi ya mabadiliko....

Sababu nyinginine pia, viongozi wengi waliofuta katika utaawala wa Tanzania, Ubinafsi, kujipendeza, madili na ufisadi vimetawala hawakumbuki mtu ila mfumo uliowaweka madarakani. Ndio maana matabaka na kubaguana vimekuwa moto unaotutafuna kimyakimya. Ila mimi binafsi bado nahusudu namna ya utaawala na approach aliyokuwa anaitumia Mwalimu, katika kuyakabili matatizo na kutatua changamoto na namna alivyokuwa akiyaangalia mambo

Mungu adumishe Uhuru wa Tanzania katika Amani, umoja na Ushirikiano thabiti na madhubuti. Amen
 
Ningetaka maoni yake kuhusu nini angehitaji kufanyiwa.Kama cheo au biashara,kilimo au mengineyo.Ningemtengenezea mazingira ambayo yasingemfanya afe kwa majuto.Kwa ujumla tu kwamba ningemlipa fadhila kwa aliyonitendea binafsi,chama na hata nchi.Zaidi ya hayo,ningehakikisha anaingia katika vitabu vya historia ya nchi yake.
Kwa hiyo hao wazee walipigania Uhuru kwa maslahi yao binafsi na sio nchi ?

Mbona Nyerere kafa maskini, isingekuwa Jeshi kumjengea nyumba angekufa kama mtu masikini mwingine.

Nepotism ndiyo inaharibu nchi hii ,Nyerere angekumbatia kundi dogo la watu eti kisa walipigania Uhuru nchi hii ingekuwa na matabaka ya koo za watawala na watwana.
 
Hapana,usimlaumu Majjid,huenda alitaka kuonesha jinsi mzee Dossa alivyotumia nguvu na mali zake na uhuru ulipopatikana hakuna aliyemjali akaishia kuwa fukara na akakutana na mnufaika wa juhud na mali zake,akaishia kumpa tuu nauli na kumnunulia gari ya kutembelea.Unajua kila jambo lina angle zake kadhaa ambazo mtu mmoja hawezi kuziona zote.
Balibabambonahi,
Asante, uko sahihi, na moja ya shida ya baadhi ya wachangiaji ni kukurupuka. Baadhi pia huona baya kwa kila kinachoandikwa na mtu wanayemchukia. Hao wapo mpaka mwisho wa dunia.
Maggid
 
Maggid umeguswa na suala la nauli badala ya kuhoji kwa nini Dossa Aziz na wengine hawasomeki katika historia ya nchi?

Hawakuwa na vigezo vya kuwa viongozi hasa wakilinganishwa na nani?

Kwa nini kabla ya uhuru walikuwa matajiri na wanaonekana kufilisika baada ya uhuru na hata vizazi vyao havisikiki?

Mabinti,vijana,na wajukuu wao wako wapi? kwa nini familia ya Bibi Titi haisikiki?

Nini kiliikumba familia ya kambona? ina maana hakuna mwana familia ya kambona aliye excel hata kielimu?

watu tunahoji mambo trivial badala ya kujiuliza maswali magumu
Whose task to make such a history? Tusiingize udini tu maana mtoa mada ameleta hoja murua
 
9 Reactions
Reply
Back
Top Bottom