Gari la Dossa Aziz Austin Morris Alilompa Julius Nyerere Wakati wa Kupigania Uhuru wa Tanganyika

Mohamed Said

JF-Expert Member
Nov 2, 2008
20,920
30,261
GARI LA DOSSA AZIZ ALIYOMPA JULIUS KAMBARAGE NYERERE WAKATI WA KUPIGANIA UHURU

Ilikuwa mwaka wa 1946 Ally Sykes akiwa katika meli iliyokuwa inawarudisha askari Waafrika kutoka Vita Vya Pili Vya Dunia pamoja na kaka yake Abdul meli ilipofunga nanga Mombasa yeye akatoroka melini kuelekea Nairobi kumtafuta rafiki yake Peter Colmore.

Akiwa Nairobi Ally alifanya urafiki na Mkikuyu mmoja kwa jina James Kariuki.

Kariuki alikuwa mwanaharakati wa Mau Mau.

Kariuki alikuwa dereva wa teksi wakati wa mchana na askari wa Mau Mau wakati wa usiku.

Kariuki alipogundua hisia za kizalendo za Ally, alimkaribisha kwenye mikutano ya Mau Mau iliyokuwa ikifanyika usiku na kwa siri.

Mikutano hii ilikuwa ikifanyika Limuru na Ngong Hills, nje ya Nairobi.

Ilikuwa katika mikutano hii ndipo Ally alipojifunza somo lake la kwanza katika ustadi wa kuficha siri na upinzani dhidi ya Waingereza.

Hii ilikuwa mwaka 1946 na Ally Sykes alikuwa na umri wa miaka 20.

Wakati wote alipokuwa Nairobi Ally Sykes alipanga Central Hotel.

Mara nyingi katika mazungumzo yake na Tom Mboya.

Mboya alimuhimiza Ally kurudi nyumbani Tanganyika kuongoza harakati za uhuru.

Dossa Aziz alipokwenda Nairobi mwaka wa 1946 alimkuta Ally, kijana maarufu na mwenye shughuli zake pale mjini akijulikana na takriban kila mtu.

Dossa Aziz alikuwa amekwenda Nairobi kufanya usaili wa mafunzo ya urubani.

Kulikuwa na vijana wawili kutoka Tanganyika, wote watoto wa matajiri.

Dossa Aziz alikuwa katika usaili na mtoto wa Mwarabu mmoja tajiri, Ally Mmanga.

Dossa Aziz alikataliwa kufanyiwa usaili kwa kuwa alikuwa Mwafrika.

Waingereza walidai kuwa Waafrika hawakuwa tayari kufundishwa urubani.

Dossa Aziz alifadhaika sana.
Alimpigia simu baba yake huku akilia na kumpasha habari hizo.

Ili kumliwaza mwanae, baba yake Dossa, Aziz Ally, alimtumia fedha anunue gari kama kifuta machozi.

Gari hili lilikuja kuwa ndiyo chombo cha kwanza cha usafiri kwa TAA, TANU na Julius Nyerere.

Ally alimpeleka Dossa Aziz kwenye mkutano wa KAU ambao Kenyatta ilikuwa ahutubie.

Wajaluo wakiwa kabila hasimu na maadui wao Wakikuyu, kabila ya Kenyatta, walikuwa wakipita huku na kule katika mkutano ule wakimtukana Kenyatta.

Jambo hili lilianzisha mapigano kati ya Wajaluo na Wakikuyu.
Mapigano yalifuatia pande zote mbili zikitupiana mawe.

Askari wa kuzuia fujo wakiongozwa na maafisa wa Kizungu waliitwa kutuliza fujo.

Waliizingira River Road, mahali ambapo mkutano ulikuwa ukifanyika na wakaanza kushambulia kwa virungu Mwafrika yoyote waliyemwona.

Dossa Aziz alishuhudia mambo haya yote kwa mshangao mkubwa.

Baada ya kununulia gari, Dossa Aziz alikaa na Ally siku chache kisha akarudi nyumbani.

Alirudi Dar es Salaam akiendesha gari yake mpya Austin Morris A 40 Vanguard.

Harakati za TANU zilipopamba moto Dossa Aziz aliitoa gari hii kumpa Mwalimu Nyerere kwa ajili ya shughuli za TANU.

Gari hii ipo Makumbusho ya Taifa.

(Kutoka kitabu cha Abdul Sykes)

337158905_6265316983529358_1004270831049132930_n.jpg

337228218_677592860805430_7652877109277477305_n.jpg

Dossa Aziz​
 
Kumbe hali hii ya kutaka kufahamika watanzania tukiwa ugenini(kwamba Wewe nani ) kumbe jambo la kihistoria
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom