Simulizi za Kusisimua: Nyerere alipoingiwa huruma Mwana-TANU Mwenzake kukosa Nauli...

Nimesoma maoni ya wengi ila maoni ya huyu ni utaahira mtupu,sasa Kenya ni nini mpk lazima wafanyacho na ss tufanye?

Hlf acha udini,kumbuka wapigania uhuru walikuwa watu kutoka Pwani ambao hat Jk alipokelewa nao,so ni lazima walikuwa waislam ss issue cyo udini ila historia ya nchi lazima iwatambue mashujaa wake wawe waislamu au wakrist cyo muhimu,babu yako kumbuka hakuwa anajua chochote kule kwenu Miliman hata kusoma hakusomaga,nchi zingine ukienda makumbusho hata sanamu zao mashujaa wetu tungeziona..we unaropoka tuu wakat hata ukimtumia mtu vocha unamuuliza umepata unataka asante wakati jina lake lilisoma ktk simu yako kuwa amefikiwa na salio . Na hata mchango wa maafa bukoba hukutoa hlf unadhani kujitoa kwa ajili ya watu usiowajua ni kitu kidogo .
Tena ss hv upo Dar kwann usirud kwenu ukawa mzalendo kutengeneza uhuru wa mawazo wa wanakijiji wenu mkaukomboa tuu mji wenu uwe unadhalisha ili uje kuwa mji huru kiuchumi na vizazi vyenu vikafaidi,ila kwakuwa ni mbinafsi unang'ang'na na jiji ili kuikomboa familia yako tuu,thamin walichofanya wale wazee,ww huwez hata uish milele
watu mnapotoka nje ya mada na kuanza kutema povu kama mmemeza OMO.
 
Huu mtindo wa kulialia na kulalamika nauchukia sana, okay it happened, tufanyeje sasa au tuendelee kulia. Huyo Nyerere keshakufa hata tukilalamika atatusaidia nini?
Yatubidi turekebishe makosa aliyoyafanya,tuyape majina yao hadhi stahiki,historia yetu iandikwe upy,tuanzishe foundations za majina yao zisaidie palipo na upogo wa kimaendeleo.
 
Yatubidi turekebishe makosa aliyoyafanya,tuyape majina yao hadhi stahiki,historia yetu iandikwe upy,tuanzishe foundations za majina yao zisaidie palipo na upogo wa kimaendeleo.
Ni bora kufanya hivyo kuliko kumlalamikia Nyerere kila siku.
 
Mzee Mohamed heshima yako, nakumbuka tukiwa pale Tanga Port, ukifanya kazi bandarini na mimi nikifanya kazi kampuni mmoja ya usafirishaji wa makontena ya mchanga maalum uliokuwa unakwenda Japan na China.

Mara nyingi tukikutana kwenye lift ya Bandari House, au kwa port manager ghorofa ya juu kabisa. Sikujua kwamba wewe ni mweledi kwenye masuala ya historia na uelimishaji wa jamii. Baadhi ya vijana wanakukejeli kwa sababu ya malezi potofu ya kisasa lakini unachokifanya ni chema sana kwa kizazi cha leo na cha kesho.

Ni wachache ambao hutumia muda wao kwa ajili ya kuhifadhi historia, wengi huyakebehi maandiko ya kihistoria kwa sababu ya kupofushwa na elimu za kisasa.

Nakutakia wiki njema na maisha yenye afya nzuri. Mungu akubariki.
Philipo,
Ahsante sana kwa kunikumbusha Tanga na kazi zetu za kutafuta maisha.
Ingia katika hii blog yangu: www.mohammedsaid.com kiuna mengi.
 
Huu mtindo wa kulialia na kulalamika nauchukia sana, okay it happened, tufanyeje sasa au tuendelee kulia. Huyo Nyerere keshakufa hata tukilalamika atatusaidia nini?
Fakalava,
Muhimu ni kuiweka historia mahali pake panapostahili.

Kutoa uongo katika historia hii na kuuweka ukweli ili
wanaostahili heshima wapate heshima zao hata kama
wameshatangulia mbele ya haki.
 
Fakalava,
Muhimu ni kuiweka historia mahali pake panapostahili.

Kutoa uongo katika historia hii na kuuweka ukweli ili
wanaostahili heshima wapate heshima zao hata kama
wameshatangulia mbele ya haki.
Mzee Mohamed, unaona ni heshima hipi wanayostahili? Je, ni kuanzisha Foundations zenye majina yao kama mdau alivyopendekeza hapo awali?
 
Fakava,
Niwie radhi nakujibu swali lako kwa kuuliza swali.

Kiliwapata nini serikali kuwapa medali Abdul na Ally Sykes mwaka wa 2011
katika kuadhimisha miaka 50 ya uhuru wa Tanganyika ilahali medali nyingi
zilitolewa na ndugu hawa wawili hawakutunukiwa heshima ile?

Wametoa medali hizo kwa lipi kubwa khasa ambalo Abdu na Ally walilofanyia
nchi hii?
 
Kabokocastory,
Njama ilikuwa ni kufuta kabisa historia ya TANU kwa kuhofu
kuwa historia ya uhuru wa Tanganyika ni historia ya Waislam
wa Tanganyika.

Mwaka wa 1988 gazeti la Africa Events (London) lilipochapa
makala yangu ''In Praise of Ancestrors,'' ambamo ndani niligusia
mchango wa Abdul Sykes katika kuunda TANU na mchango
wa Waislam katika kupigania uhuru wa Tanganyika, toleo zima
lilikusanywa na kutolewa katika mzunguko,

Yapo mengi.
Kwa sasa tusimame hapa kwanza.
Historia ikishajiandika huwa ni ngumu sana kufutukia bro na kwa bahati mbaya wale wanopambana kuendelewa kuiweka hai historia kama hizi hukumbana na changamoto nyingi. Kwa mi naamini kwa faida ya wengi na ili kuendelea kuweka historia ya hawa mashujaa wetu katika vinywa vya kizazi cha sasa ni vizuri sasa na muda umefika kuiweka katika machapisho, nakala mbali mbali na hata kwenye jukwaa za kuelimisha kama hizi
 
Nyerere alikua mbinafsi sana, haiwezekani wazee walio leta uhuru wakaishi maisha ya kishenzi. Sifa zote alibeba yeye na waliopambana wakaachwa kwenye giza. Tukiacha unafiki nyerere alikua na roho mbaya, Mbinafsi na mpenda sifa.
 
Ndugu zangu,

Leo Ni Tisa Disemba. Ni Siku yetu kuu kusheherekea Uhuru wetu. Tumetimiza miaka 55 ya uhuru. Tuna kila sababu za kusheherekea.

Nitapenda niweke hapa simulizi ya kihistoria yenye kusisimua, na kuelimisha pia.

Kwenye andiko lake lililojenga nadharia ya kisiasa. ' The Prince' kwa maana ya Mwana Mfalme, Mwanafalsafa Machiavelli anazungumzia juu ya kiongozi aweje. Machiavelli anamtaka kiongozi kuwa makini na tabaka la waliomsaidia kuingia madarakani na hata wenye kumzunguka. Kwa mujibu wa Machiavelli, hutokea kwa Mwana Mfalme "kuwajeruhi" waliomsaidia kuupata utawala.
Hii ni kwa kutowatimizia yote yale waliodhani kuwa ni haki yaokutimiziwa.

Badala yake, Mwana Mfalme huwaingiza kundini wawe kama wengine.
Katika manung'uniko yao, Mwana Mfalme hawezi kutumia dawa chungu dhidi
yao kwa vile hujihisi ana deni kwao. Lakini, cha msingi kwa MwanaMfamle ni kuzingatia ukweli, kuwa, hata kama atakuwa na maaduiwachache, katika kuchukua nchi, muhimu ni kuwaridhisha walio wengi, nahapa ni wananchi.

Huwezi kutawala kwa amani bila upendo na utashi wa walio wengi. Ni kwa sababu hizi, Mfalme Louis XII wa Ufaransa aliweza kwa kasi ya ajabu kuitwaa Milan na kwa kasi ya ajabu kuipoteza Milan.

Hakukidhi matakwa na matarajio ya wananchi walio wengi waliomfungulia
milango.Mtawala aliye mbali na asiyejali maslahi ya watu wake walio
wengi ni mtawala mwenye hofu. Na mtawala mwenye hofu zaidi na watu
wake kuliko adui wa nje, basi, hujijengea kasri ama ngome imara ya
kujihifadhi ingawa hilo halitamsaidia kuzuia nguvu za umma za
kumwondoa madarakani. Kwa mtawala, kasri ama ngome iliyo imara ni
kuepuka kuchukiwa na wananchi, kuacha ubinafsi na kujali maslahi ya
wengi.

Ni katika hili, kuna ambao walimtarajia Julius Nyerere kuwapendelea wale waliomsaidia kuingia kwenye mamlaka. Lakini, Nyerere aliwaacha waingie kwenye kundi kuu, kwa maana wawe miongoni mwa wananchi. Wafanye kazi ya siasa lakini si kwa kupewa vyeo vya juu, kwa vile tu, walikuwa ni miongoni mwa wale 17 waliounda TANU.
Hapa nawazungumzuia watu kama akina Chifu Kunambi na Dossa Aziz. Chifu Kunambi alitoa hata eneo lake kwa maekari ili kijengwe Chuo Kikuu. Chifu Kunambi amekufa miaka kadhaa iliyopita akiwa anaishi maisha ya kawaida pale Ubungo Msewe.

Na kuna , Julius Nyerere alimuonea huruma sana Dossa Aziz alipokutana nae kule Kizota , Dodoma. Dossa Aziz alikuwa ni MwanaTanu mwenye kadi nambari 4. Ni Dossa Aziz aliyetoa Landrover yake itumike na TANU, ndio gari aliyotumia Nyerere kuzunguka vijijini kwa wananchi kuitangaza TANU. Ni Dossa Aziz na wenzake waliomchangia Julius nauli ya kwenda UNO kudai uhuru wa Tanganyika.

Lakini, pale Kizota, Dodoma, miaka ile ya 80 mwishoni, Julius Nyerere alimwona Dossa Aziz aliyechoka sana. Julius akaambiwa, kuwa hata nauli ya kwenda Dodoma, Dossa Aziz alisaidiwa na rafiki yake na classmate wake wa tangu Kitchwele School, Ally Sykes.

Julius Nyerere aliingiwa na huruma. Inasemwa, kuwa Julius, kwa fedha zake mwenyewe, alimnunulia Dossa Aziz gari la kutembelea.

Naam, simulizi ni nyingi...

Maggid Mjengwa.
0688 37 36 52 ( Whatsapp)
0754 678 252

Hiyo picha ina uhusiano upi na gari alilotoa Dosa Aziz kabla ya Uhuru?
 
Kwa hiyo hao wazee walipigania Uhuru kwa maslahi yao binafsi na sio nchi ?

Mbona Nyerere kafa maskini, isingekuwa Jeshi kumjengea nyumba angekufa kama mtu masikini mwingine.

Nepotism ndiyo inaharibu nchi hii ,Nyerere angekumbatia kundi dogo la watu eti kisa walipigania Uhuru nchi hii ingekuwa na matabaka ya koo za watawala na watwana.

Wewe unaandika hayo lakini mwanawe Marehemu Mzee Nyerere Andrew Nyerere humuhumu JF aliwahi kuandika kuwa wao wanaishi ki "Royal Family".

Tumuamini nani? Wewe au mwanawe Nyerere?
 
Habari za akina Dossa Aziz na wengineo zinapatikana kwenye vitabu vya historia. Kama hatusomi vitabu hilo ni tatizo lingine.
Tupe majina ya hivyo vitabu vyenye "Habari za akina Dossa Aziz" tuvitafute. Maandiko pekee yaliyowakumbuka akina Dossa Aziz ni ya Alama Mohamed Said. Nje ya hapo sijawahi kukumbana nayo, tusaidie majina ya hivyo "vitabu vya historia" tukawasome wazee wetu.
 
Hiyo picha ina uhusiano upi na gari alilotoa Dosa Aziz kabla ya Uhuru?
Kama hilo linalosemwa ni kweli, Dosa alitoa zaidi ya Mwalimu, Dosa alitoa akiwa mwananchi wa kawaida, Mwalimu alitoa akiwa mtawala au aliyekwisha kutawala
 
Tupe majina ya hivyo vitabu vyenye "Habari za akina Dossa Aziz" tuvitafute. Maandiko pekee yaliyowakumbuka akina Dossa Aziz ni ya Alama Mohamed Said. Nje ya hapo sijawahi kukumbana nayo, tusaidie majina ya hivyo "vitabu vya historia" tukawasome wazee wetu.
Maalim Faiza,
Nimesoma kila kitabu kinachohusu historia ya TANU na uhuru wa Tanganyika.
Nimesoma kila kitabu kilichoandikwa kuhusu Mwalimu Nyerere.

Ikiwa kuna vilivyonipita vitakuwa vichache sana.

Katika vitabu vya historia vilivyoandika historia inayokaribia ukweli ni cha Judith
Listowel,
''The Making of Tanganyika,'' (1965).

1136953

Vitabu vyote vilivyobakia hakuna kitu.

Lady Judith Listowel alikuwa mke wa Lord Listowel aliyekuwa Gavana wa Gold
Coast kutoka 1957 - 1960.

Huyu mama alitaka kuandika kitabu kuhusu Tanganyika kwa hiyo akamwomba
Peter Colmore amuunganishe na wapigania uhuru wa Tanganyika wamsaidie
katika utafiti wake.

Peter Colmore na Ally Sykes walikuwa marafiki wakubwa sana na mapatna
katika biashara na walifahamiana Nairobi toka mwaka wa 1942 wakati wa WWII
wote wawili wakiwa wanajeshi vijana katika KAR.

Siku zile Waingereza wote walikuwa wakitaka kufanya jambo Afrika ya Mashariki
mtu wao wa kuwafagilia njia na kuwafungulia milango alikuwa Peter Colmore.

Colmore alikuwa anaushawishi mkubwa sana kwa viongozi wa Afrika ya Mashariki
na alikuwa rafiki wa karibu sana wa Kabaka Edward Mutesa.

Colmore alikuwa na urafiki na viongozi wengi wa Afrika ya Mashariki ila Mwalimu
Nyerere
licha ya juhudi ya Ally Sykes kumkutanisha Colmore kwa kumpeleka
nyumbani kwa Mwalimu, Magomeni.

Colmore alipata mwaliko wa kuhudhuria sherehe za uhuru wa Tanganyika December
1961 kupitia mgongo wa Ally Sykes.

Kabaka Mutesa alisoma darasa moja na Abbas Sykes, King's College Budo.

Nimeuleta huu mukadama, yaani utangulizi mrefu ili uweze kujua ilikuwaje Listowel
aliweza kuingia Tanganyika na kufanya mazungumzo na wapigania uhuru wengi
na kupata ukweli wa historia ya TANU.

Hapa Tanganyika Colmore mwenyeji wake alikuwa Ally Sykes na ndiye alikuwa mtu
wa kwanza kuzungumzanae kuhusu harakati za uhuru wa Tanganyika.

Hii ndiyo sababu kwenye kitabu chake Dossa Aziz katajwa pampja na wazalendo wengi
kama Dr. Luciano Tsere, Dr. Vedasto Kyaruzi, Sheikh Suleiman Takadir, Schneider
Plantan
kwa kuwataja wachache.

1136924

Ally Sykes na Peter Colmore, Paris 1963
 
Ndugu zangu,

Leo Ni Tisa Disemba. Ni Siku yetu kuu kusheherekea Uhuru wetu. Tumetimiza miaka 55 ya uhuru. Tuna kila sababu za kusheherekea.

Nitapenda niweke hapa simulizi ya kihistoria yenye kusisimua, na kuelimisha pia.

Kwenye andiko lake lililojenga nadharia ya kisiasa. ' The Prince' kwa maana ya Mwana Mfalme, Mwanafalsafa Machiavelli anazungumzia juu ya kiongozi aweje. Machiavelli anamtaka kiongozi kuwa makini na tabaka la waliomsaidia kuingia madarakani na hata wenye kumzunguka. Kwa mujibu wa Machiavelli, hutokea kwa Mwana Mfalme "kuwajeruhi" waliomsaidia kuupata utawala.
Hii ni kwa kutowatimizia yote yale waliodhani kuwa ni haki yaokutimiziwa.

Badala yake, Mwana Mfalme huwaingiza kundini wawe kama wengine.
Katika manung'uniko yao, Mwana Mfalme hawezi kutumia dawa chungu dhidi
yao kwa vile hujihisi ana deni kwao. Lakini, cha msingi kwa MwanaMfamle ni kuzingatia ukweli, kuwa, hata kama atakuwa na maaduiwachache, katika kuchukua nchi, muhimu ni kuwaridhisha walio wengi, nahapa ni wananchi.

Huwezi kutawala kwa amani bila upendo na utashi wa walio wengi. Ni kwa sababu hizi, Mfalme Louis XII wa Ufaransa aliweza kwa kasi ya ajabu kuitwaa Milan na kwa kasi ya ajabu kuipoteza Milan.

Hakukidhi matakwa na matarajio ya wananchi walio wengi waliomfungulia
milango.Mtawala aliye mbali na asiyejali maslahi ya watu wake walio
wengi ni mtawala mwenye hofu. Na mtawala mwenye hofu zaidi na watu
wake kuliko adui wa nje, basi, hujijengea kasri ama ngome imara ya
kujihifadhi ingawa hilo halitamsaidia kuzuia nguvu za umma za
kumwondoa madarakani. Kwa mtawala, kasri ama ngome iliyo imara ni
kuepuka kuchukiwa na wananchi, kuacha ubinafsi na kujali maslahi ya
wengi.

Ni katika hili, kuna ambao walimtarajia Julius Nyerere kuwapendelea wale waliomsaidia kuingia kwenye mamlaka. Lakini, Nyerere aliwaacha waingie kwenye kundi kuu, kwa maana wawe miongoni mwa wananchi. Wafanye kazi ya siasa lakini si kwa kupewa vyeo vya juu, kwa vile tu, walikuwa ni miongoni mwa wale 17 waliounda TANU.
Hapa nawazungumzuia watu kama akina Chifu Kunambi na Dossa Aziz. Chifu Kunambi alitoa hata eneo lake kwa maekari ili kijengwe Chuo Kikuu. Chifu Kunambi amekufa miaka kadhaa iliyopita akiwa anaishi maisha ya kawaida pale Ubungo Msewe.

Na kuna , Julius Nyerere alimuonea huruma sana Dossa Aziz alipokutana nae kule Kizota , Dodoma. Dossa Aziz alikuwa ni MwanaTanu mwenye kadi nambari 4. Ni Dossa Aziz aliyetoa Landrover yake itumike na TANU, ndio gari aliyotumia Nyerere kuzunguka vijijini kwa wananchi kuitangaza TANU. Ni Dossa Aziz na wenzake waliomchangia Julius nauli ya kwenda UNO kudai uhuru wa Tanganyika.

Lakini, pale Kizota, Dodoma, miaka ile ya 80 mwishoni, Julius Nyerere alimwona Dossa Aziz aliyechoka sana. Julius akaambiwa, kuwa hata nauli ya kwenda Dodoma, Dossa Aziz alisaidiwa na rafiki yake na classmate wake wa tangu Kitchwele School, Ally Sykes.

Julius Nyerere aliingiwa na huruma. Inasemwa, kuwa Julius, kwa fedha zake mwenyewe, alimnunulia Dossa Aziz gari la kutembelea.

Naam, simulizi ni nyingi...

Maggid Mjengwa.
0688 37 36 52 ( Whatsapp)
0754 678 252

Asante kwa historia murua Hakika Nyerere ni Baba wa Taifa na aliyetenda haki Kwa wote
 
Back
Top Bottom