Simulizi ya ujasusi: Do not shout (Usipige kelele)

DO NOT SHOUT
Season 2
Sehemu ya.........12
Mtunzi: Saul David
WhatsApp: 0756862047

ILIPOISHIA....
Brandina anafanya jitihada kubwa na mwisho anafanikiwa kumuokoa Yusto kutoka kwenye mikono ya madam Jane mama yake.
Upande wa pili Caren anafika eneo la tukio baada ya Revocatus kumuomba msaada.

SASA ENDELEA....

" Revo nakuuliza Yusto yuko wapi?"
"Maji maji, naomba maji kwanza tafadhali"
"Hebu acha masihara Revo, maji natoa wapi mimi"
"Kwenye gari yapo mle kwenye gari yangu"
"Haya inuka twende"
Alisema Caren huku akimsaidia Revocatus kusimama

"Aiii Aaah! taratibu sana Caren unaniumiza"
"Kwani umefanyaje mbona kama umepigwa Revo"
"We acha tu ninywe maji kwanza please"
Alisema Revocatus, wakakokotana hadi pale alipokuwa amepaki gari yake, wakaingia ndani.

Revocatus alitafuta maji yalipo na kuyafakamia kwa kasi sana akanywa kopo zima akamaliza.
Caren alikua akimuangalia tu akisubiri atulie kwanza.

"Haya nambie nini kimetokea, imekuwaje upo huku?"

"..aah ni Yusto, Yusto alitwekwa akaletwa huku nilifuata kuja kumsaidia"

"Nini? unamaana gani kusema alitekwa yuko wapi sasa kwa nini hukusema mapema"

"Caren ilikua ni ghafula tu, kila kitu kilitokea ghafula sikupata wazo la kukutafuta mapema, lakini usijali Yusto yuko salama"

."salama kivipi, mbona hauko nae"

"kuna mtu mwingine kaja kamsaidia, hata simjui lakini inaonekana anafahamiana vizuri na Yusto, ni mdada hivi mzuri mzuri"

"Katoka wapi huyo mtu"
"Hata sijui kwa kweli wakati mimi nahangaika kumuokoa Yusto akatokea tu ghafula Kama malaika wake wa ulinzi, akamchukua na kuondoka nae"
"Revo unamasihara sana alafu hili ni jambo serious"
"Kivipi Caren si nakueleza ilivyokuwa au"
"Sasa malaika wa ulinzi kaingiaje"
"Aah namaanisha huyo mdada alivyo yani alikuja ghafula tu hatujui alikotoka kafikaje, akamchukua Yusto akapaa nae kwenye ukuta wakatoweka"

"Ona sasa, eti akapaa"

"Ona nini ndo hivo Yusto kaokolewa na mrembo huko"
"Unajuaje, vipi kama huyo mtu akawa amemteka tena"
"Hapana, nina uhakika na hilo, huyo mwanamke na Yusto wanafahamiana"

Kimya kilitawala kwa sekunde kadhaa, Caren akawa anatafakari maelezo ya Revo, kwa kiasi roho yake ilitulia baada ya kuambiwa kuwa Yusto wake yuko salama hakujua kama baadhi ya maelezo kutoka kwa Revocatus yalikua ni ya uongo.

"Kwa hiyo ni nani basi alimteka Yusto"
Caren aliuliza swali jingine.

"Mmh sijui, kwa kweli sijui" Revocatus alidanganya, hakutaka kuweka wazi suala la madam Jane na ile ngome yake.

"Okay basi tuondoke hapa, Yusto anaweza kuwa amerudi mjini atanitafuta nina imani"

"Umekuja na usafiri gani hapa Caren"
"Pikipiki yangu, haipo hapa we twende nitakuonyesha" alisema Caren huku akihamia kwenye usukani wa gari.
."aah hebu subiri kwanza Caren, Darubini yangu, pale uliponikuta nimelala nimeidondosha pale"

Caren hakusema neno, akashuka upesi akafika hadi pale alipoelekezwa ni kweli aliikuta Darubini ya Revo, akaichukua na kuanza kurudi.

Lakini mara akasita na kusimama, ni kama vile kuna kitu alikiona, akageuka na kutazama tena.
Ni kweli, kwa mbali sana Caren aliiona ile ngome ya madam Jane.
Alibaki ameduwaa kidogo inakuwaje kwenye msitu kama huo kukawa na nyumba tena kubwa,
akageuka na kumtazama Revo ambae alikua bize akinywa kopo jingine la maji, alitamani kumuliza lakini akasita.

Aliweka ile darubini machoni kisha akaanza kuikagua ile ngome kwa umakini.
Caren aliweza kuona kila kitu, hatimae aliliona hadi lile ghorofa lililojengwa katikati ya ngome hiyo.

Caren alilitazama jengo hilo kuanzia chini hadi juu.
Mara Caren alionyesha mshtuko wa hali ya juu baada ya kumuona Madam jane akiwa amesimama dirishani ndani ya chumba kimoja cha juu kabisa katika ghorofa hilo.

"Bosii?, Madam Jane?" Caren alijiuliza huku akizidi kuibua maswali mengi kichwani kwake yasiyo na majibu.
Hapo akajaribu kuunganisha matukio na kupata majibu ya baadhi ya maswali aliyokuwa akijiuliza.

"Bila Shaka madam Jane ndio aliyemteka Yusto na kumleta huku, lakini kwa nini amteke, au kajua nina mahusiano ya kimapenzi na Yusto? hapana hawezi au kajua Yusto ni mwanae kamwita kumuhoji, mmh hapana, sasa kwa nini, alafu pia mwanamke gani kaja kumuokoa Yusto huku, atakuwa ni Sophia?, hapana"

Caren akawa anajiuliza na kujijibu mwenyewe.
Kwa mbali akamuona Madam Jane akichukua simu yake akaibonyeza na kuiweka sikioni.


Madam Jane alionekana akiwa ndani ya chumba chake cha kupumzika katika lile ghorofa.
Alionekana mtu mwenye mawazo sana mkono akiwa na ile picha aliyoichukua baada ya yusto kuidondosha.

Nae alikuwa na maswali mengi yasiyo na majibu akilini mwake. Kwanza hakuacha kumfikiria Yusto kijana aliempa kashikashi nzito ndani ya ngome yake na kisha kutoroka.
Japo wakati huo alikua bado akiandamwa vikali na walinzi wake kuhakikisha wanamkamata tena.
Taswira na maneno ya Yusto hayakufutika akilini kwake.

"Kaingia humu ndani kaziona picha zangu za siri, lakini kwa nini akaamua kuichukua hii picha moja niliyopiga na Zubeda? Kwa nini hii picha na sio nyingine"
Madam jane aliwaza huku taa nyekundu ikiwaka kwenye akili yake, akaona sio bure.
Akachukua simu yake akapiga namba ya Caren kisha akaiweka simu sikioni.


Caren akiwa bado anaendelea kumtazama Madam Jane kupitia ile Darubini, mara simu yake ikaita, haraka akaipokea. Ilikua ni simu kutoka kwa madam Jane mwenyewe.

"Hallo bosi"
"Caren, uko wapi sasa hivi"
"Aah, nipo chuo madam"
"Vipi umefikia wapi kwa kazi niliyokupatia"
"Aa..ee.. nimeshajua alipo Zubeda naanda mazingira ya kifo chake ambayo hayatakua na utata bosi"

"Sawa vizuri, jaribu kuangalia pia kama kuna mtu yoyote anaonekana kuwa karibu na Zubeda kisha nipe taarifa, nilisikia pia alitekwa nataka kujua nani alifanya hivyo kwa sababu gani" alisema madam Jane, kisha akakata simu.

Caren aliendelea kumtazama madam Jane jinsi alivyoonekana kuwa na mudi mbovu wakati huo.

"Bila shaka ameshaanza kuhisi kuwa mtoto wake Yusto yupo hai, lakini bado anataka nimuuwe Zubeda nani sasa atamthibitishia Yusto ni mwanae wa kumzaa" Caren alilaumu.

"We mwanamke hiyo Darubini huioni au unataka nifie humu kwenye gari huoni kama nina hali mbaya jamani"
Revocatus alipaza sauti huku akimchungulia Caren kwenye vioo vya gari (site-mirrow).
Caren alitembea haraka akaingia kwenye gari akaiwasha na kuondoka.
"Vipi uko sawa, au bado unamuwaza Yusto"
"Niko sawa acha maswali ya ajabu" alisema Caren

ITAENDELEA...
Je, caren atautatua vipi mtihani ulio mbele yake?
Vipi hali ya Yusto na Brandina?

USIKOSE SEHEMU INAYOFUATA..
 
๐๐€๐Š๐ˆ ๐๐€ ๐Œ๐ˆ๐Œ๐ˆ
(Stay with me)
๐ฌ๐ž๐š๐ฌ๐จ๐ง 2
Sehemu ya..............13

Mtunzi: Saul David
WhatsApp: 0756862047

ILIPOISHIA....
Revocatus anapata msaada kutoka kwa Caren anaemchukua na kuondoka nae, wakati huo upande wa pili bado Brandina na Yusto wanaendelea kuandamwa na vikosi vya ulinzi kutoka kwenye ngome ya madam Jane.
Wakati huo pia madam jane anajikuta kwenye wakati mgumu na mawazo mengi mara tu baada ya kukutana na Yusto.

Je, nini kitafuata?

SASA ENDELEA...

Akiwa bado ni mtu mwenye mawazo mengi madam Jane alikaa kitandani huku akijaribu kuwaza ni nini afanye.

Tayari alishamtuma Caren ahakikishe anammaliza Zubeda lakini bado hisia zake zilimbeba mbali mno na kujikuta anamkumbuka mwanae Yusto ambae alimtelekeza angali akiwa na miezi sita tu, akaendelea na biashara yake ya ukahaba ya kujiuza, ndipo alipojikuta anaokota dodo kwa kupendwa na tajiri mark moon, lakini uwepo wa mtoto wake Yusto ukawa kikwanzo cha ndoa yake na tajiri huyo mwisho akajikuta anaachana na mark moon kwa sababu hiyo licha ya kujitahidi sana kumficha Yusto.
Madam Jane akajikuta anamchukia Zubeda na Yusto akawachukia kiasi cha kutoa agizo wauwawe, akiamini wao ndo sababu ya kuharibu bahati yake.

Madam jane alikumbuka yote haya akiwa amekaa pale kitandani, akamkumbuka hadi mtu aliyempa kazi hiyo ya kumuuwa Zubeda na Yusto kipindi hicho yeye akiwa Dubai, mtu huyo aliitwa Azizi.

Baadae Azizi akamtaarifu kuwa amefanya kazi yake ipasavyo, Zubeda amepata ajali mbaya ya gari, ajali ya kutengenezwa, amekua kichaa na hawezi kukumbuka chochote Yusto nae alikufa pale pale kwenye ajali hio.
Hivyo ndivyo alivyoelezwa na Azizi.

"Yes sikua na kosa mlistahili kufa ninyi wote mlistahili kufa, kwa nini mliharibu ndoto zangu, niwaza kuwa malkia wa Dunia nzima lakini badala yake mkanifanya niaibike na kugeuka kituko Dunia nzima, hasa wewe Zubeda wewe ambae hadi leo unaishi, pengine mwanangu hakuwa na kosa alikua ni malaika yule, lakini kwa sababu yako Zubeda kwa sababu yako nikamuua hadi mwanangu Yusto aaaah!"

Madam Jane alikua akiongea mwenyewe ndani ya kile chumba kama mwenda wazimu, akili yake haikua imetulia kabisa.

Wakati akiwaza hayo mara taswira ya yule kijana Yusto alieleta kashikashi nzito mda mfupi uliopita katika ngome yake alimjia tena akili mwake.

"Aah, nini hiki nawaza hawezi kuwa mwanangu yule, kivipi ani, mwanangu alikufa, sina mtoto mwingine zaidi ya John mimi, sinaa"
Madam Jane alijisemea huku akijaribu kuifuta taswira ya kijana huyo akilini mwake lakini ikawa ngumu, sura na sauti ya Yusto vilimganda, akajikuta anakumbuka jinsi Yusto alivyopigwa risasi mbele yake, moyo wake ukamuuma tena.

"Kwa nini naumia sasa aaaah aaaah" madam Jane alijilaumu huku akipiga piga kichwa chake kwa hasira hapo akachukua simu yake na kupiga namba aliyoi-save Osman Azizi.
Mtu aliyempa kazi miaka mingi iliyopita, kuwauwa Zubeda na Yusto.

Simu iliita mara ya kwanza bila kupokelewa, akapiga tena mara ya pili na ya tatu hapo ikapokelewa.

"Janeth, ni muda umepita tangu nione simu yako" sauti nzito ya kiume iliyojaa kitetemeshi ilisikika upande wa pili.

"Pengine unaweza ukawa umeshajua sababu ya mimi kukupigia simu" Madam Jane aliuliza.

"Nitajuaje sasa, okay let me guess, unataka gari kutoka Japan au China"
Azizi aliongea kwa kiburi, hakuwa Azizi yule aliekua akifanya kazi chini ya madam Jane miaka kama 20 iliyopita, sasa alikua ni mtu anaejitegemea mwenye pesa zake, anamiliki kampuni kubwa ya kuuza na kununua magari.

"Ni kuhusu mwanangu" madam Jane alijibu
"Mwanao, yupi, kafanyaje" Azizi aliuliza akijaribu kumuelewa madam Jane.

"Nakuja tuongee"
"Aah niko bize kwa sasa usijali nitakutafuta mwenyewe nikipata muda" alisema Azizi kisha akakata simu.

"Hallo...halloo...mjinga mmoja wewe, unanikatia mimi simu, hunijui Azizi, ole wako kama ulicheza na akili yangu"


Upande wa pili Azizi mzee wa makamo mwenye asili ya kiarabu hivi alionekana anatabasamu mara tu baada ya kumalizia kuzungumza na Madam Jane.

"Sasa muda umewadia, muda niliousubiri zaidi ya miaka 20, sasa ni wakati wa kupiga pesa, pesa ndefuuu" alisema Azizi kisha akacheka kwa sauti tena sauti kubwa.


Madam Jane alichukua koti na mkoba wake akavibebe kisha akatoka nje ya kile chumba akateremsha ngazi na kutoka hadi nje kabisa ya lile jengo.
Akakutana na Kindoki, kiongozi wa ulinzi ndani ya ngome yake.

"Vipi" aliuliza madam Jane huku akimuangalia Kindoki usoni.

"Hatujawapata bosi, wamepotelea msituni lakini bado vijana wanaendelea kuwafuatilia" Kindoki alitoa taarifa ya namna opareshini ya kuwafuatilia Brandina na Yusto ilivyokuwa ikiendelea.

"Helkopta iko wapi"
"Ilienda huko pia kuongeza nguvu kama ulivyosema Madam"
"Mpigie rubani arudi hapa mara moja kuna sehemu nataka kwenda"
"Sawa bosi"
"Sasa hivi"
"Sawa"

Kindoki alifanya kama alivyo agizwa muda mfupi baada helkopta ilifika na kutua, madam Jane akapanda, na kuondoka.


"Aaaiiiggghh" kelele za manung'uniko zilisikika kutoka msituni pembezoni mwa mto.
Watu wawili walionekana wamekaa chini ya mti mmoja akiwa ameuma kipande cha mti mdomoni huku akilalamika kwa maumivu na mwingine alikua akihangaika kuichomoa risasi iliyokuwa imezama kwenye bega la mwenzake kushoto, hatimae akafanikiwa kuitoa.

Walikua ni Brandina na Yusto.

Baada ya Brandina kufanikiwa kuitoa risasi iliyokua imezama kwenye bega la kushoto la Yusto, alichana kipande cha nguo yake nyepesi aliyokua amevaa ndani ya koti, akamfunga Yusto eneo alilo jeruhiwa.

"Vipi umeshaangalia kama hawatufuati tena" aliuliza Yusto

"ee hawapo tumeshawaacha mbali hawawezi tena kutuona, helkopta yao pia imerudi"

"Dah afadhali, ila Brandina ulijuaje niko huku yani umefikaje"
"Hilo sio la muhimu kwa sasa, labda nikulize wewe inakuwaje madam Jane akakuteka, mnajuana"
"Ataa, eti kwa sababu nlichoma mwanae John na mkasi"
"John yupi, yule wa chuoni, ni mtoto wa madam Jane?"
"Ee ndiyo, mimi pia nimejua leo"

Wakati wakiendelea na mazungumzo hayo Brandina aliitumia nafasi hiyo pia kumuelekeza Yusto kazi waliyokuwa wamepewa na bosi wao mark moon ya kumfuatilia huyo madam Jane.

Hapo ndipo Yusto akakumbuka zile picha alizoziona chumbani kwa madam jane, akatamani kujua zaidi.

Hapo Brandina akamueleza kila kitu anachokijua kua Madam Jane aliwahi kuwa mke wa bosi wao Mark Moon lakini ndoa yao haikudumu kwa muda mrefu wakaachana.

"Waliachana kwa shari hivyo mark moon anahisi kuwa huenda madam Jane akawa ni adui yake anaemtafuna kimya kimya ukizingatia Sasa hivi biashara zake nyingi zinaandamwa" alieleza Brandina.

"Vipi unajua nini kuhusu madam Jane huyu kwenye picha hapa unamfahamu pia"
Alisema Yusto huku akiingiza mkono mfukoni kuchukua ile picha ambayo aliichukua kwenye chumba cha madam jane.

"Mwanamke gani?" Aliuliza Brandina huku akimuangalia Yusto aliekua ameduwaa baada ya kugundua kuwa alishaidondosha ile picha.

"Aaa..eee..unajua... Sema nini madam Jane aliwahi kuwa na rafiki au ndugu yake hivi mwanamke amenaniliii yanii.. " Yusto alieleza kitu ambacho hata yeye hakuelewa.

"Sikiliza Yusto niliyokweleza mimi ndio hayo ninayoyafahamu, kumbuka kipindi wanafunga ndoa ni zamani sana pengine mimi nilikua hata sijazaliwa hayo maswali yako majibu yake tutayapata wakati tunaendelea kufanya hii kazi aliyotupa bosi" alieleza Brandina huku akivua koti lake kubwa akamvisha Yusto baada ya kubaini alikua akitetemeka kwa baridi.

"Asante" alisema Yusto huku mawazo yake yakimbeba mbali sana akaona kuna kila sababu ya kuifanya kazi hiyo kwa nguvu zote ili kujua ni vipi madam Jane alipiga picha akiwa na mama yake mlezi Zubeda.

"Yusto uko sawa?"
"Yaa niko sawa Brandina"
"Tutalala hapa hadi kesho asubuhi, angalau hali inaweza ikawa imetulia"
Alisema Brandina huku akimtazama Yusto kwa macho yaliyoregea.

"Tulale hapa?"
"Yah hawa watu wapo kila mahali bado wanatutafuta, sio salama kuondoka mapema"
"Mmh! tunalalaje sasa hapa Brandina"
"Aah jamani unauliza kama sio kamanda vile, subiri nitakuonyesha"
Alisema Brandina huku akisimama akasogea karibu na ule mto wa maji yaliyokua yakienda kwa kasi ndogo.
Akanza kuvua nguo zake mbele ya Yusto bila aibu yoyote akabaki na nguo za ndani pekee, kisha taratibu akaingia ndani ya maji kwenye ule mto.

Yusto alibaki akimtazama mwanamke huyo aliyejaaliwa kwa kila idara, akawa anawaza ni jinsi gani atakabiriana na jaribu hilo lililokua mbele yake.

"Aah! ndio usiku kucha jamani, sasa itakuwaje" aliwaza Yusto.

Je, nini kitafuata?

Vipi kuhusu sakata jipya la madam Jane na Osman Azizi?
Osman Azizi ni nani hasa?
Vipi kuhusu Revocatus na Caren?
Nini kitatokea, ukizingatia Brandina anampenda sana Yusto?

*USIACHE KUFUATILIA,
ITAENDELEA....

0756862047
 
๐ƒ๐Ž ๐๐Ž๐“ ๐’๐‡๐Ž๐”๐“
๐ฌ๐ž๐š๐ฌ๐จ๐ง 2

Sehemu ya.............14


Mtunzi: Saul David
WhatsApp: 0756862047

ILIPOISHIA...
Brandina na Yusto wako msituni wamejificha baada ya kufanikiwa kutoka kwenye ngome ya Madam Jane. Brandina anamtaka Yusto walale hapo hadi asubuhi ya siku nyingine kwa ajili ya usalama zaidi.

SASA ENDELEA....

Brandina aliingia kwenye maji akiwa na nguo za ndani pekee, hali ya hewa ya eneo hilo ilikuwa na ka ubaridi kiasi lakini hakujali, akawa anajirushia maji taratibu kuuosha mwili wake laini.

Yusto alikua akimtazama kwa kuibia ibia akawa anamshangaa mwanamke huyo ambae hakuonyesha hata chembe ya aibu.

"Labda kwakua ni jasusi, kashazoea" aliwaza Yusto.

Mara Brandina aligeuka akagonganisha macho yake na Yusto, Yusto akazuga kama vile alikua hamtazami yeye, akaangalia pembeni.

Lakini Brandina aliweza kumgundua, akatabasamu, kisha akatoka kwenye maji taratibu na kuanza kumfuata Yusto pale chini ya mti.

Yusto alimtazama Brandina wakati anakuja. Akamkagua kuanzia juu hadi chini, alikua ni mwanamke aliyeumbika haswa.
Mwili wake uliojaa na kujikata vizuri kiunoni, ki sura chake kizuri ukichanganya na vijinguo alivyovaa wakati huo vilimfanya kuonekana kama wale wadada wa kibrazili wakiwa beach.

Yusto alijikuta anamiss Caren wake, hawakupishana sana uzuri na Brandina.

"Vipi mbona unaniangalia sana"
"Nani mimi"
"Ee ndio wewe" alisema Brandina huku akichuchumaa mbele ya Yusto.

"Aah..ha..hapana mimi nawaza yangu tu hapa" alisema Yusto huku akimkagua Brandina aliyekua amechuchuma na kupitisha mikono katikati ya mapaja yake mazuri.
Licha ya kufanya hivyo lakini Yusto aliweza kumchungulia kwa ndani kabisa akaona chupi iliyokua imetuna kiasi kwa mbele.

"Ooh mungu wangu huku sasa kutesana" aliwaza Yusto huku akikwepesha macho yake haraka na kutazama kwingine.
Lakini macho yake yalitua kifuani kwa Brandina, napo hali ilikua ni ile ile ya kumtesa. Chuchu zake za duara zilizotuna zilikua zimebanwa vizuri na sidiria yake.

"Vipi twende basi tukaoge pale mtoni"
Alisema Brandina.

"Ah hapana nahisi baridi harafu si unaona nina kidonda na bado sijakihudumia vizuri hakitakiwi kiingie maji kabisa"

"Aah sema unaogopa baridi Yusto"
"Wala hata, niko fresh mbona"
"Sasa na purukushani yote hii iliyotokea leo utalala hivo hivo bila kujimwagia maji angalau"

"Mmmh"
"Usigune bana wewe njoo uoge utakuwa makini usikitie maji hicho kidonda"

Yusto alijikuta hana ujanja wa kuendelea kubishana.
"Haya poa basi naja"
Alisema Yusto huku Brandina akimtazama kwa macho fulani hivi maregevu.
Wakawa wanatazamana na Yusto, kisha wakatabasamu kwa pamoja.

"Haya tangulia basi nakuja" alisema Yusto, Brandina hakuwa na kizuizi akatembea kwa madaha kama kawaida yake akarudi tena ndani ya maji yaliyokua yanamfika juu kidogo ya kiuno.

Yusto alitoa nguo zake akabaki na bukta na singrendi pekee taratibu akasogea tayari kuingia kwenye ule mto.

Brandina aligeuka na kumtazama huku akijihisi mapigo yake ya moyo kwenda kasi, ilikua ni siri yake na moyo wake namna alivyokua akimuelewa na kumpenda mwanaume huyo.
Japo tayari alikua anajua kuwa moyo wa Yusto umejaa mazima kwenye penzi dhidi ya Caren lakini haikua sababu ya yeye kuacha kumpenda.

Yusto aliingia ndani ya maji taratibu huku wakiwa bado wanatazamana na Brandina.

"Vipi mbona kama unaogopa, au maji ni ya baridi sana?"
"Aah yani we acha tu kama barafu hivi"
"Acha kujiregeza we mwanaume banaa"

"Hata kama ila sio kwa baridi hii hahaha"
Alisema Yusto na kucheka.
Mara Brandina akachota maji kiasi kwenye kiganja cha mkono wake na kumrushia Yusto.

"Aaaa wewee" Yusto akilalamika
Brandina akafanya hivyo kwa mara nyingine tena ya pili na yatatu na baadae akaanza kuyarusha maji kwa mikono yote miwili huku akicheka.

"Brandina acha basi.. aaaah" alisema Yusto huku akijivuta kwenye maji akasogea karibu na Brandina akamshika mikono yote miwili kumzuia lakini Brandina akawa anapambana ajinasue hapo Yusto alimgeuza na kumkumbatia kwa nyuma akambana kwa nguvu huku akiwa bado amemshika mikono akicheka pia.

Hakujua kufanya hivyo alikua anazalisha tatizo kubwa kwa Brandina, ile hali ya kukumbatiwa na Yusto ilimfanya mapigo yake ya moyo kuongezeka kasi zaidi na zaidi, akatamani Yusto aendelee kumkumbatia asimuache.

Kulikuwa na baridi kali wakati huo lakini mwili wa Brandina ulianza kuwa na joto taratibu.

"Vipi mbona umetulia hivo" Yusto aliuliza kwa sauti ya chini jirani kabisa na sikio la Brandina.

"Yustoo" Brandina aliita huku akigeuza shingo na kumtazama Yusto.

Yusto alishangaa namna ambavyo macho ya Brandina yalikua yameregea, ilionyesha wazi hakua kwenye hali nzuri hata kidogo
hakuwa Brandina yule aliyemtembezea kichapo kikali Revocatus masaa machache yaliyopita.

"Yes nambie" Yusto aliuliza hali akiwa bado amemkumbatia Brandina.

Brandina akawa kimya akashindwa kabisa kuzungumza.

"Mbona kimyaa.."
"Mmmh"
"Umeniitaa"
"Yes, najiuliza vipi kama wangekuuwa ningefanyaje mimi"
"Mmh unamaana gani"
"Unajua najisikiaje ukiwa karibu na mimi kama hivi"
"Hapana, ila bila shaka unajisikia vizuri si ndiyo"
"Yustoo.."
"Yes tell me"
"I know you're takken, najua moyo wako upo kwa Caren lakini unaweza angalau kua na mimi kwa leo tu, najua unajua nini namaanisha" Brandina aliongea bila kupepesa macho.

Yusto alijikuta anapata kigugumizi cha ghafula, alishagundua kitambo sana kuwa Brandina anampenda lakini hakujua kama ipo siku atakuja kutamka maneno kama hayo waziwazi,
Yusto alijikuta kwenye wakati mgumu na istoshe alikua amezama penzini na msichana wa ndoto zake Caren, tena penzi lao lilikuwa bado ni jipya kabisa.

"You know what nakutania bana, usichukulie serious, its just joking" alisema Brandina baada ya kuona Yusto amekaa kimya kwa muda akajua wazi ilikua ni ngumu kwake kufanya hivyo, akawa hatamani kusikia jibu la kuumiza moyo wake kutoka kwa Yusto.
Brandina alijikuta akijilaumu kwa alichokifanya ilikua ni kama kujidharirisha mbele ya mwanaume yeye kama mwanamke anaejielewa.

"Yah hata mimi nilijua tu unatania," alisema Yusto huku akimuachia Brandina ambae alianza kuondoka,
Yusto akawa anamuangalia akiona kabisa alichokua anakisema Brandina ni tofauti na uharisia
"Lakini ameyasaidia maisha yangu, anastahili hata zaidi ya hili" aliwaza Yusto huku akijihisi kumkosoea Brandina.

"Oga upesi basi niku....."

Alisema Brandina lakini kabla hajamalizia sentensi yake mara alishikwa mkono na kuvutiwa tena ndani ya maji.
Kufumba na kufumbua alijikuta yupo kifuani kwa Yusto. Wakawa wanatazamana uso kwa uso.

Bila kuchelewa Yusto alianza kumpiga mabusu ya hapa na pale jambo lililomfanya Brandina kuwa kwenye wakati mgumu.
Akaanza kutoa miguno, huku na yeye akiuchomeka mguu wake katikati ya miguu ya Yusto.
Akaingiza mkono kwenye maji akamshika Yusto tumboni na kisha akaanza kuushusha chini taratibu.


ITAENDELEA....
๐Œ๐š๐ฅ๐ข๐ณ๐ข๐š ๐ฏ๐ข๐ฉ๐š๐ง๐๐ž 20 ๐ฏ๐ข๐ฅ๐ข๐ฏ๐ฒ๐จ๐ฌ๐š๐ฅ๐ข๐š ๐ค๐ฐ๐š ๐“๐ฌ๐ก ๐ž๐ฅ๐Ÿ 1๐ญ๐ฎ๐ฎ

WhatsApp 0756862047
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom