Simulizi ya ujasusi: Do not shout (Usipige kelele)

SIMULIZI RIWAYA

JF-Expert Member
Feb 19, 2022
415
1,275
DON'T SHOUT

(usipige kelele)


Sehemu ya...............01
Mtunzi: Saul David
Tel : +255756862047
E-mail: saulstewarty@gmail.com
****

EPISODE 01...

"Moto, moto, jamani motooooo"
"Moto, kuna mtu ndani, motooooo"

Sauti hizi za makelele zilipasua anga zikitokea katika chuo kimoja kikubwa kilichojengwa kisasa pembezoni mwa jiji la Dar es salaam.

Wingu kubwa la moshi lilikuwa limetanda hewani kutokana na moto mkubwa uliokuwa ukiunguza jengo moja chuoni hapo, wanafunzi waliokuwa katika hostel zao walikurupuka na kuanza kutoka nje kwa kasi, huku wengine wakichungulia kutoka juu ghorofani kuangalia kilichokuwa kikiendelea.

Wote walishuhudia namna jengo moja la maktaba lilivyokuwa likiteketea kwa moto mkali.

"Jamani msaidieni Sophia alikuwa humo ndani hajatoka msaidieniii " alizungumza mwanafunzi mmoja wa kike hali akionyesha wasiwasi mkubwa aliokuwa nao.

Wanafunzi wa kike wenye moyo mwepesi waliaanza kupiga kelele zaidi huku wakiita jina la Sophia, na wengine wakiangua kilio.

Wanafunzi wa kiume nao walibaki katika hali ya kujiuma uma hakuna aliyethubutu kunyanyua mguu wake kujitoka katikati ya lile jengo lililokuwa tayari limeshika moto pande zote, wote walihofia usalama wa maisha yao.

Wanafunzi walizidi kukusanyika huku taarifa za kuwemo kwa Sophia mle ndani zikizidi kusambaa kwa kasi. Kelele zilizidi mara alipofika mwanafunzi mmoja wa kiume ambae ndiye haswa alikuwa na mahusiano ya kimapenzi na Sophia pale chuoni aliitwa john

"Shem John njoo Sophy yuko ndani atakufa jamaniii" mwanamke mmoja alipiga kelele huku akimkimbilia john na kuanza kumvuta mkono.

John alipigwa na butwaa kwa sekunde kadhaa hali akionyesha kushitushwa na habari hizo.

"Sophia, Sophia yupo humu ndani" aliuliza
" ndiyoo, alikuwa humu ndani"

Wanafunzi wote waligeuka na kuanza kumtazama john huku kila mmoja akiwa na matumaini kuwa ni lazima angefanya jambo kumsaidia mpenzi wake.

John alipiga hatua taratibu kusogea kwenye lile jengo lililo kuwa likiteketea kwa moto. Jonh aliutazama ulemoto ambao ulikuwa ukiwaka haswa, kisha akageuka kutazama nyuma akaona wanafunzi wote wamenyamaza kimya wanamuangalia hasa wanafunzi wa kike.

Akageuka tena na kuutazama ule moto
" Aah hapana nitakufa bure" John alijisemea kimoyomoyo kisha akageuka na kuanza kurudi.

"Hebu subirini, kwani mm..mm..mmeshapiga simu zimamoto"
Aliuliza john hali akipatwa na kigugumizi cha ghafula.

"Ndiyo walisema wako njiani lakini tunashangaa mpaka sasa hawajafika bado"
"Kwa hiyo...." Alisema john lakini kabla hajamalizia sentensi yake mara alipita mtu mmoja kwa kasi akiwa amejifunika blanket nzito akakimbia na kujitosa moja kwa moja ndani ya ule moto akaingia ndani ya jengo la maktaba.Kelele za hapa na pale zilisikika huku kila mmoja akisema lake.

Wanafunzi karibu wote wa chuo hicho walikuwa wakitazama tukio hilo, wakati huo ving'ora vya magari ya zimamoto vilianza kusikika jirani kabisa na chuo hicho na punde magari manne ya zima moto yalifika na haraka shughuli ya kuzima moto ilianza.

Baada ya dakika Kama mbili hivi yule mtu aliyejitosa kwenye moto alitoka akiwa amembeba Sophia mgongoni na kujifunika lile blanket lake ambalo lilikuwa limeshika moto kDa chini.

Wale zimamoto walimpokea na kuanza kumpa huduma ya kwanza na kwa bahati nzuri binti huyo mrembo Sophia hakuwa ameungua ila tu alizidiwa kwa kushindwa kupumua kutokana na moshi mwingi uliokuwamo mle ndani.

"Yusto, Yusto, Yustoooo"
"Jamani we kaka asantee"
"Mmmh wewe kweli mwanaume"
"Muangalieni anaonekana jasiri hadi raha jamani"

Hizi zilikuwa ni sifa kutoka kwa wanafunzi wa kike zilizokuwa zikimwendea mwanafunzi mwenzao Yusto aliyejitosa kumsaidia Sophia.

Sifa hizi zilikuwa ni mwiba mkali kwa John aliyekuwa bado ameduwaa baada ya kushindwa kumsaidia mwanamke wake, alijihisi amedhalilishwa kupita kiasi na hii ingemtengenezea skendo kubwa hapo chuoni.

John alikuwa ni mtu mwenye majivuno
John alikuwa ni mtu mwenye majivuno makubwa chuoni hapo alikuwa na pesa na alipenda sifa na kujifanya yupo juu kuliko wanafunzi wengine wote, pesa zake zilimpa jeuri na kumdharau kila aliyekuwa mbele yake, alifanya matukio mengi ya ajabu na wala hakujali.

John aliondoka kinyonge huku akimtazama Yusto kwa macho makali Yusto nae alimuangalia bila kupepesa macho kisha akatabasamu kitendo kilichomfanya John akasiriki zaidi.

"Subiri nitakuonyesha, masikini mkubwa wewe mimi ndio Master Joo sijawahi kushindwa" alisema john kwa sauti ya chini huku akiuma meno yake kwa hasira akaondoka.

*****

Yusto alionekana akitembea taratibu baada ya kutoka kwenye tukio la moto sasa alikuwa akirejea chumbani kwake, Mara simu yake iliingia ujumbe mfupi wa maandishi akaufungua na kuusoma.

"NIMEKUONA YUSTO NI WEWE, ASANTE KWA KUNISAIDIA LAKINI KWA NINI UNANITESA HIVI YUSTO KAMA HUNIPENDI KWA NINI UMEKUJA KUNISAIDIA"

Huu ulikuwa ni ujumbe kutoka kwa Sophia, Yusto alisimama kwa dakika kadhaa huku akitafakari ajibu nini. baada ya sekunde chache akaandika meseji kumjibu

"HAKIKISHA UMEPUMZIKA, ALAFU JOHN HAJAPENDA SIJUI UNATAKA MPAKA ANIUWE, SI UNAMJUA LAKINI"

aliituma sms hiyo kisha akarudisha simu mfukoni na kuanza tena kutembea lakini mara alisita na kusimama ni kama vile aliona kitu, akaanza kupiga hatua akielekea kwenye darasa moja akaingia ndani.

"Wewe umekaa humu inamaana hujasikia kama nje kuna moto" Yusto aliuliza kwa ukali kidogo huku akimuangalia mwanamke mmoja aliyekuwa amekaa mbele yake na kumpa mgongo.

Yusto alimuangalia juu hadi chini, mwanamke huyo alikuwa mrefu kiasi rangi yake kama chotara si mwafrika si mwarabu, kichwani alikuwa na nywele ndefu zilizofika mgongoni.

Sehemu kubwa ya mgongo wake ulikuwa wazi kutokana na nguo aliyokuwa ameivaa, hivyo Yusto aliweza kuishuhudia vizuri ngozi laini ya mwanadada huyo aliyekuwa pia amevaa sketi fupi iliyokaa vizuri kwenye hips zake na kubana kwenye kiuno chake chembamba.

Mapaja ya mwanadada huyo yalikuwa wazi kwa sehemu kubwa jambo lililomfanya Yusto kutaka kuiona sura ya mwanadada huyo ambae hadi dakika hiyo hakuwa amezungumza wala kugeukaa.

"ii..ina..inamaana hunisikii" Yusto aliuliza tena kwa mara ya pili lakini safari hii akionyesha kupatwa na kigugumizi kiasi.

Yule dada aligeuka taratibu kisha akatazama na Yusto uso kwa uso. Yusto alijikuta mapigo yake ya moyo yanaanza kwenda kasi ghafula sura nzuri ya mwanamke huyo ilizidi kumuweka kwenye wakati mgumu alikuwa ni mrembo, mrembo kupindukia, ni kweli chuoni hapa kulikuwa na warembo wengi lakini hakuna hata mmoja aliyewahi kumshitua Yusto kwa kiwango hicho hii ilikuwa ni mara yake ya kwanza hadi yeye mwenyewe alijishangaa.

"Nini hiki, Huyu mwanamke ni nani?" alijiuliza Yusto, ni kweli ilikuwa ni mara yake ya kwanza kukutana na mwanafunzi huyo mgeni.

Yule dada alimtazama Yusto kuanzia juu hadi chini na alipofikisha macho yake kwenye kiuno cha Yusto akatabasamu na kumtazama Yusto usoni.

Yusto aliweza kuuona mwanya ambao ulizidi kuupambamba uzuri wa dada huyo mrembo.

Yusto hakuelewa nini kimemfanya dada huyo atabasamu taratibu aliinama na kujitazama ndipo alipogundua kuwa zipu ya suruali yake ilikuwa wazi.

Aliduwaa kwa sekunde kadhaa kisha akamtazama tena yule dada ambae alikuwa bado ametabasamu.

"Hi" alisema yule dada.

DON'T SHOUT
(Usipige kelele)

Sehemu ya......................02

Mtunzi: Saul David
Tel: +255756862047
Email: saulstewarty@gmail.com

Episode 02
UTANGULIZI (kwa wasomaji wapya)
Moto mkubwa unawaka na kuunguza jengo la maktaba ndani yake akiwemo binti mmoja mrembo anaeitwa Sophia, John ambae ndiye mpenzi wa sophia anashindwa kufanya lolote kumsaidia mpenzi wake lakini anatokea kijana mwingine(Yusto) anaejitosa katikati ya moto huo na kumsaidia Sophia jambo linalomkasirisha sana John anajikuta anaweka kisasi kizito kwa Yusto.

Baada ya purukushani hizo kuisha Yusto akiwa chuoni hapa anakutana na mwanamke mrembo kupindukia ambae hakuwahi kumuona kabla.

ILIPOISHIA...
Yusto hakuelewa nini kimemfanya dada huyo atabasamu taratibu aliinama na kujitazama ndipo alipogundua kuwa zipu ya suruali yake ilikuwa wazi.

Aliduwaa kwa sekunde kadhaa kisha akamtazama tena yule dada ambae alikuwa bado ametabasamu.

"Hi" alisema yule dada.

SONGA NAYO...
"Hi, mambo vipi" alijibu Yusto huku akitazama pembeni kwa aibu kisha akafunga zipi ya suruali yake haraka haraka. "Poa, pole ulikuwa unazima moto?"

" Aah hapana tulikuwe tu pale tunaangalia"
"Mimi naogopa sana moto ndo maana sijaenda hata kutazama" Alisema yule dada huku akimuangalia Yusto kwa macho ya kumdadisi, macho hayo ya kudeka yalimfanya Yusto ashindwe kujiamini akabaki katika hali ya kujiumauma wala hakujua azungumze nini na mrembo huyo, mara simu yake iliita.

Akachukua na kutazama jina la mpigaji

'FRANK'
haraka akaipokea
" Uko wapi wewe, boss yupo hapa nje ya geti anatuita njoo haraka" ilikuwa ni sauti ya Frank akizungumza upande wa pili kisha akakata simu.

Taarifa hii ilimshtua kidogo Yusto haraka akatoka bila hata kumuaga yule dada.

Yusto alitembea upesi hadi alipotoka nje kabisa ya chuo hicho mbele yake aliona gari nyeusi ikiwa imepaki pembeni ya barabara, gari hiyo haikuwa ngeni machoni kwa Yusto, aliifuata taratibu akafungua mlango wa nyuma akaingia.

Ndani ya gari hilo alimkuta tayari Frank rafiki yake amekwisha ingia nakukaa siti ya nyuma, mbele alikuwepo dereva pamoja na mzee mmoja aliayevaa suti nyeusi uso wake ukiwa umekunjamana.

"Hivi ninyi mnataka kazi hamtaki" aliuliza yule mzee kwa sauti ya kukwaruza.

"Tunataka bosi" Yusto na Frank walijibu kwa pamoja hali wakionyesha unyenyekevu wa hali ya juu.

"Sasa kwa nini mmekuwa wazembe, tumewaleta hapa kama walinzi wa siri ndani ya hiki chuo mnatakiwa kufanya kazi, hii ni biashara inaushindani kama biashara nyingine

hiki ni chuo kikubwa Tanzania nzima mmiliki wa hiki chuo anamaadui kibao ambao hawataki kuona akifanikiwa, wanamtafuta kila kona ili waharibu sifa ya hiki chuo, angalia tarehe 9 wanafunzi wote wameumwa matumbo wakaharisha tatizo ikaonekana ni chakula, tarehe 15 maji yalikata ghafula, tarehe 21 kukatokea short ya umeme vitu vya wanafunzi vikaungua na wengine kidogo wafe, leo tena maktaba imeungua vitabu na vitu vyote vya muhimu vimewaka moto na ninyi mpo mshahara manachukua hivi mnafikiri haya matukio yote yametokea bahati mbaya tuu" Alifoka yule mzee.

"Hapana bosi"
"Sasa kama hapana ninyi kazi yenu ni nini, mko hapa kama walinzi wa siri kulinda usalama sasa matukio yote haya yanatokea ninyi mnakuwa wapi, au mnapenda kusoma?, kama ndio wewe Yusto nasikia kunamtihani gani sijui umekuwa wa kwanza hii ndo kazi iliyokuleta hapa?"

" Hapana bosi ila tulipoanza kazi tulikuwa tunafeli sana ikabidi tukazane pia kusoma wasije kutushtukia lakini pia tungefeli zaidi tungefukuzwa hata chuo"

"Acha wendawazimu wewe sisi wenyechuo ndio tumekuleta hapa nani anaweza kukufukuza, hebu fanyeni kazi pelelezeni mjue nyuma ya haya matukio yote kuanzia tarehe 9 kuna nini sawa"

"Sawa bosi"
"Msisahau kwamba hii ni vita, tuliwaweka kambini miezi 8 mkapata mafunzo sio kwamba tulikuwa tunapoteza mda, haya shika hii"
Alisema yule mzee kisha akachomoa bastola ndogo mbili akampa Yusto moja na Frank moja.

"Hatutaki ujinga tena, nimetumwa kuja kuwapa onyo la mwisho sasa tusikie tena tukio la ajabu, nawapa siku 7 tu mnipe report ni nani yuko nyuma ya haya matukio kwa heri".

Walimaliza mazungumzo kisha Yusto na Frank wakashuka kwenye gari na kuondoka wakawa wanarejea chuoni huku kila mmoja akiwaza namna atakavyoanza kukabiliana na majukumu hayo.

"Unajua Yusto ni kweli tumejisahau sana haya matukio yamefuatana yani ni ndani ya mwezi huu mmoja sio bure, mbona mwanzo hali ilikuwa shwari tu eti kunani jamaa?"

"Tumepewa siku saba tu, nategemea utaniambia tuanzie wapi acha maswali ya kijinga?" Alisema Yusto hali akiwa amekunja sura yake.

Wakati wamefika kwenye geti la kuingia chuoni kwa mara nyingine tena Yusto akamuona yule dada waliyemkuta darasani anakuja upande wao, sasa aliweza kumuona vizuri namna mwanamke huyo alivyoumbika kuanzia juu hadi chini, alikuwa na shepu nzuri ya kuvutia na alitembea kwa madaha sana.

Walikutana na mwisho wakapishana bila hata kusalimiana, harufu ya marashi mazuri aliyopulizia dada huyo ndiyo iliyobaki kwenye pua za Yusto na Frank.

"Oya huyu ni nani?" Aliuliza Yusto
"Haa! inamaana humjui huyu demu anaitwa Caren, ni femas sana hapa chuoni kila mtu anamjua, nakwambia wanaume wanajigongagonga hapo lakini anawatolea nje, hadi Master Joo kachemka"
"Eeh John huyu mpenzi wa Sophia?"
"Sasa je, si ndo maana anataka kumtema Sophia kisa Caren, lakini Caren nae kakaza sijui ana nini huyo dada"

"Mmh unajua John anamtesa sana Sophia, kwanza umesikia leo kashindwa kumchomoa kwenye moto mle maktaba"
"Nimeskia kamanda wewe ndo ulimtoa sophia mle kwenye moto hongera, naona bado unamuelewa sana fanya mpango basi au unamuogopa John"
"Aah wapi hiyo sio sababu"
" Dah nasikia John kazuia mwanaume yoyote kumsogelea Caren yani kashakuwa demu wake tayari na hajampata, yule jamaa bangi zinamuharibu wallah"
"Kwani huyo Caren katokea wapi na anamda gani hapa chuoni"
" Amehamia tarehe 7 mwezi huu anawiki kama 3 tuu"

Alijibu Frank kauli iliyowasha taa nyekundu kwenye kichwa cha Yusto akasimama
" umesema tarehe 7?"
"Ndio kwani vipi?" aliuliza Frank akiwa haelewi Yusto ameshanganzwa na nini lakini mara akaelewaa.

" Aah kweli Yusto, inamaana baada ya Caren kuja ndo haya matukio yameanza kutokea hapa chuoni kuanzia hiyo tarehe 9, mmmh inawezekana kweli akawaa..." Alisema Frank huku akitafakari zaidi.
" Nakata uniletee taarifa za huyu mwanamke sasa hivi utanikuta room kwangu" Alisema Yusto
*****

Dakika 10 baada Yusto alikuwa ndani ya chumba chake amekaa, na Mara mlango ukafunguliwa akaingia Frank.

"Vipi umepata" Yusto aliuliza kwa bashasha
"Ndiyo huyu dada anaitwa Caren Pius Mwanandota, anamiaka 20 alikuja hapa chuoni tarehe 7, anaishi floor ya pili chumba namba 59, anatabia ya kutoka nje ya chuo mara kwa mara akiwa peke yake hata sasa hayupo amewaaga marafiki zake anaenda shopping hizo ndo taarifa nilizopata mpaka sasa" alisema Frank na bila kupoteza muda Yusto alichukua koti lake lenye rangi nyeusi akalivaa kisha akatoka nje kwa kasi akawa anaelekea upande zilipokuwa hostel za wanawake.

Frank alitoka nje na kumsindikiza kwa macho.
" aah huyu jamaa nae hatuliagi, anakurupuka tuu" alisema Frank kisha akageuka kuingia ndani lakini mara alishtuka na kugeuka tena nyuma.

"Mungu wangu Caren kurudi" alisema Frank huku akimuangalia Caren aliyekuwa anatembea kwa kasi kidogo kuelekea kwenye vyumba vyao.

JE, NINI KITAFUATA?
CAREN NI NANI?
VIPI KUHUSU JOHN, SOPHIA?
NINI HATIMA YA CHUO HIKI?
 
DO NOT SHOUT
(Usipige kelele)

Sehemu ya....................03

Mtunzi: Saul David
Tel: +255756862047
E-mail: saulstewarty@gmail.com


UTANGULIZI {kwa wasomaji wapya}
Vijana wawili Yusto na Frank wapo kwenye jukumu zito la kulinda usalama wa chuo kimoja cha kisasa nchini Tanzania wakiwa kama walinzi wa siri wanaojifanya kama wanafunzi wa kawaida. Chuo hicho kinakumbwa na mfurulizo wa matukio yanayoibua sintofahamu kwa wanafunzi wa chuo hicho jambo linalopelekea Yusto na Frank kuanza kupeleleza chanzo cha matukio hayo wakianza na kumtilia shaka mwanafunzi mmoja mgeni ambae ni mrembo kupindukia anaejulikana kwa jina la Caren.

ILIPOISHIA...
"Mungu wangu Caren kurudi" alisema Frank huku akimuangalia Caren aliyekuwa anatembea kwa kasi kidogo kuelekea kwenye vyumba vyao.

SASA ENDELEA...
Frank alijua wazi kuwa Yusto alikuwa akienda kukichunguza chumba cha Caren, hivyo ilikuwa ni hatari kama Caren ataingia na kumkuta Yusto ndani ya chumba chake.

Alichukua simu yake haraka na kumpigia Yusto lakini simu ikawa inaita bila kupokelewa.
"Ooh! come on Yusto" alisema Frank hali akihisi kuchanganyikiwa asijue afanye nini kumsaidia rafiki yake.
Hakuwa na namna nyingine ya kufanya, akaandika ujumbe wa maandishi kisha akatulia kusubiri kitakachotokea.
****

John maarufu kwa jina la MASTER JOO alikuwa amekaa akipata kinywaji katika eneo moja maalum la kupumzikia ndani ya chuo hicho hali akitafakari mambo mawili matatu.

Tukio lililotokea siku hiyo la yeye kuaibika mbele ya wanafunzi wenzie baada ya kushindwa kumsaidia mpenzi wake Sophia kwenye ajali ya moto lilimchanganya sana, akajikuta anamchukua sana Yusto akawa anawaza namna atakavyo muadabisha kijana huyo ambae tayari alilichafua jina lake.

John alikuwa mtu mwenye pesa kuliko wanafunzi wote chuoni hapo aliishi kwa majigambo makubwa na alikuwa akiogopwa na baadhi ya wanafunzi na hata wakufunzi pia kutoka na hadhi ya maisha aliyokuwa akiishi, mara zote alikuwa akitembea na marafiki zake walioendana kitabia ambao yeye aliwaita wafuasi wake.
Wakati John akiwa amezama kwenye mawazo mara marafiki zake wawili walifika eneo lile kwa kasi.

"Kaka mkubwa tumemuona Yusto anaelekea kwenye mabweni ya wasichana kule" alisema mmoja wa wale vijana.
"Nini? wee kweli'
"Ndiyo ni yeye"
"Safiii, nmemnasa huyu mpuuzi, sasa dogo fanya kazi yako chukua ile Camera yako mfuatilia kila atakakoenda urudi napicha zaidi ya mia moja hapa, nataka nimuaibishe chuo kizima zaidi ya yeye alivyonifanyia Leo, namtengenezea bonge la skendoo, atatamani kuhama chuo" alisema John huku akitabasamu.
*****

Yusto alikuwa tayari kwenye ghorofa la wasichana akawa anasoma namba za vyumba kimoja baada ya kingine.
Katika chuo hicho hakukuwa sheria iliyokuwa inawazuia wanafunzi wa kike kuingia hostel za wanaume au wanaume kuingia hostel za wanawake hii iliruhusiwa isipokuwa kulala tu.

Yusto alitembea kwa kujiamini hali akiwa ameinamisha kichwa chake chini hakutaka kila mtu amuone, lakini hakujua kuwa nyuma yake tayari kulikuwa na kijana wa John anamfuatilia na kumpiga picha.

Mwisho alifika chumba namba 56 kama alivyoelekezwa na Frank kuwa humo ndimo alimokuwa akiishi Caren binti mgeni na mrembo kuliko wote chuoni hapo.

Yusto alitazama huku na huku akahakikisha hakuna mtu anaemuona akaingiza mkono mfukoni akachomoa visindano viwili vidogo mno akachokonoa kitasa cha mlango huo hazikupita sekunde 5 kitasa kikafunguka, kwa tahadhali kubwa akasukuma mlango na kuingia ndani.

Yusto alipokelewa na harufu nzuri ya marashi uliyomfanya akumbuke kwa mara ya kwanza alipokutana na malkia huyo, Yusto akajikuta anatabasamu hii ilionyesha wazi kuwa taribu moyo wa Yusto ulikuwa umeanza kunasa kwa binti huyo mrembo Caren.
Hakukuwa na vitu vingi sana chumbani humo, Yusto aliangaza macho yake huku na huku kisha akasogea kwenye kabati la nguo akalifungua.

Macho yake yalitua kwenye koti moja nzuri jeusi lililokuwa limewekwa peke yake upande mmoja wa kabati.
Yusto alilikagua juu hadi chini kisha akalifunua kwa ndani.
Mara ghafula alipatwa na mshtuko mkubwa baada ya kuona kitu ambacho hakutarajia kukiona. upande wa ndani wa koti hilo kulikuwa na mifuko mingi iliyochomekwa visu vidogo vidogo vingi mno zunguuka pande zote za koti.

Hili lilimshangaza sana Yusto akawa anavitazama vile visu vyema makali pande zote, wakati akiwa katika hali ya kuduwaa macho yake walitua mezani ambako nako aliona kitu kingine kilichomfanya asogee na kutazama zaidi.

Ilikuwa ni karatasi ya ramani moja kubwa iliyochorwa kwa ustadi mzuri.

"Hii ni ramani ya hiki chuo chote, yes ni yenyewe, huyu mwanamke hapana, sio bure"
Alisema Yusto huku akichukua simu yake na kupiga picha ile ramani,
Akiwa bado ameshika simu hapo aliweza kuona 'missed call' mbili na meseji zilizotumwa na Frank muda mfupi uliopita haraka akafungua na kuisoma.

'OYA CAREN KARUDI MWANA, TOKA HUMO NDANI MSALA HUO'

Yusto hakuwa na sababu ya kujiuliza mara mbili mbili, haraka alifunga lile kabati akaanza kuelekea mlangoni kwa kasi lakini alisimama ghafula mara baada ya kuhisi mlangoni kunamtu,
Ni kweli mlango ulianza kufunguliwa taratibu huku Yusto akiwa ametoa macho akili yake ikienda kasi kuangalia namna ya kujitetea
*****

Yule kijana aliyepewa kazi ya kumpiga picha Yusto aliendelea kuifanya kazi hiyo kwa ustadi mkubwa hadi pale Yusto alipoingia ndani ya chumba cha Caren.

Alitulia kwa muda kisha na yeye akanyata hadi mlangoni akasimama kwa sekunde kadhaa huku akiwa ametega sikio lake pale mlangoni.
Baada ya kuona kupo kimya akaanza kuufungua mlango huo taratibu huku mkono mwingine akiitanguliza camera yake ndani tayari kupiga picha.
*****

Wakati Yusto akiwa ameduwaa, alishangaa kuona mtu akitanguliza mkono wenye camera.
"Shit" alisema Yusto na bila kuchelewa aliudaka ulemkono na kuubamiza ukutani kisha akafungua mlango kwa kasi akiwa bado ameshika ule mkono akaruka na kumsindikiza kwa mateke mawili mfurulizo yaliyompata yule kijana kifuani akaanguka kwenye korido kama gunia huku akikohoa na kulia kwa maumivu, camera ikadondoka chini.

Haraka Yusto alifunga mlango kisha akawa anaiwahi ile camera lakini yule kijana hakutaka kukubali kirahisi nae akamlukia Yusto na kumvaa mzima mzima, purukushani ikaanza upya kila mtu akitaka kuiwahi ile camera.

Haukupita muda wasichana wa bweni hilo walianza kukusanyika wakishangazwa na vidume hao wawili waliokuwa wakigombana kwenye mabweni yao.

Punde Caren nae alifika, akasimama ghafula baada ya kuona jambo ambalo hakulitegemea kuliona karibu na mlango wa chumba chake, alipatwa na mshangao mkubwa zaidi baada ya kuona Yusto kijana aliyekutana nae darasani mda mfupi uliopita ndiye aliyekuwa akipigana na mwenzake.

Wakati huo Yusto nae aligeuka na kukutanisha macho yake na Caren wakabaki wanatazamana huku mioyo yao ikionekana kuzungumza.

ITAENDELEA.....
 
DO NOT SHOUT
(Usipige kelele)
Sehemu ya....................04
Mtunzi: Saul David
Tel: +255756862047
E-mail: saulstewarty@gmail.com


⭐⭐⭐
ILIPOISHIA...
Wakati huo Yusto nae aligeuka na kukutanisha macho yake na Caren wakabaki wanatazamana huku mioyo yao ikionekana kuzungumza...


SASA ENDELEA...
Wakati Yusto anazidi kutazamana na Caren hii ilimpa mwanya yule kijana aliyekuwa anampiga picha kwa siri kuanza kukimbia na kamera yake. Yusto anaposhtuka tayari yule kijana alishafika mbali lakini hakutaka kumruhusu aende, kwa kasi ya ajabu alianza kumfukuzia.

Caren ambae alikuwa bado anashangaa kuona wanaume hao wawili wakipigana ndani ya bweni la wanawake, mbaya zaidi walikuwa Karibu na mlango wa chumba chake alibaki amesimama huku akimfikiria zaidi Yusto ambae pindi wanatazamana alihisi ni kama moyo wake unaenda kwa kasi sana hakujua nini sababu.

Yule kijana alikimbia akifuata uelekeo zilipokuwa ngazi za kushuka gholofa ya chini, Caren akiwa amesimama mbele ya kijana huyo aliyekuwa anakuja kwa kasi, akajikuta anapatwa na msukumo wa kumsaidia Yusto aliyekuwa anajaribu kumkimbiza kijana huyo ambaye tayari alimuacha umbali mrefu.

Yule kijana alipofika karibu na Caren, Caren alimpisha na kusogea pembeni lakini kwa makusudi akautega mguu wake njiani, yule kijana bila kutegemea alijikuta anajikwaa kwenye mguu wa Caren nakuanguka chini kwa kishindo huku akitoa kelele za maumivu makali aliyoyapa, punde Yusto akawa amefika na kumkamata akamnyang'anya ile camera.

Kijana aliumia vibaya mno hivyo haikuwa rahisi tena kwake kukabiliana na Yusto.
Caren alijikausha na kuondoka kama vile hajafanya jambo lolote akaenda na kusimama mbele ya mlango wake akaendelea kutazama kama wanafunzi wengine wa kike ambao sasa walikuwa wameongezeka na kuwa wengi.

"Najua aliyekutuma nani, kuwa kama mwanaume basi acha kuishi hapa chuoni kwa kumtegemea mwanaume mwenzio, kumbuka zile hela sio zake nizawazazi wake" Yusto alisema kwa sauti ya chini akiwa amechuchumaa pembeni ya yule kijana aliyekuwa anahangaika kujinyosha mkono wake.

Baada ya kusema hivo Yusto alisimama na kuanza kuondoka akiwa ameshika ile kamera mkononi, baada ya kupiga hatua kadhaa alisimama na kugeuka nyuma akatazama wale wanawake waliokuwa wamekusanyika wanawashangaa lakini macho yake yakatua kwenye uso wa Caren wakawa wanatazamana.

Walitazamana kwa zaidi ya sekunde 30 mwisho Yusto akajikuta anatabasamu ni kama vile alijua msaada alioutoa Caren baada ya kumuangusha yule kijana.
Caren nae alijikuta akitabasamu huku akiinama chini kwa aibu kama ilivyokuwa desturi kwa watoto wa kike, alipotazama chini mara akaiona simu ya Yusto chini ya malango wa chumba chake, akaiokota lakini kwa bahati mbaya tayari Yusto alikuwa amekwisha terekemka kwenye ngazi na kuondoka.

Yusto hakutaka kuendelea kupoteza muda aliondoka na taratibu kumbukumbu ya vitu alivyoviona ndani ya chumba cha Caren ilimjia.

"Visu,ramani ya chuo, vya nini huyu mwanamke, huenda akawa ametumwa?, ila ametumwa na nani? mmh hapana mbona hata hafanani, mtoto mlaini vile" Yusto alikuwa akijiuliza na kujijibu mwenyewe.
*****

John alitazama saa yake ya mkononi, sasa zilikuwa zimepita dakika 20 tangu alipomtuma kijana wake amfuatilie Yusto na kumpiga picha.

"Mbona kachelewa huyu dogo" alisema John huku akichukua simu yake kwa lengo la kumpigia kijana wake.
Akiwa ameweka simu sikioni mara alimuona Yusto anakuja eneo lile hali akionekana mwenye jazba.
John alitaharuki kidogo huku akikata simu yake ambayo haikuwa na maana tena akajua tayari mambo yalikuwa yameharibika.

Yusto alifika na kuipigiza ile kamera juu ya meza ambayo john alikuwa ameweka chupa yake ya bia, ikadondoka chini na kupasuka.

" hivi wewe unajikuta nani hapa chuoni?, unafikiri Kila mtu atakuogopa eti kisa unapesa, how dare you?"
"Hahahah come on Yusto, pesa ndo kila kitu hapa duniani, pesa inafanya mambo ambayo hayawezekani kuwa rahisi, nlimchukua Sophia kutoka kwenye mikono yako sababu ni nini, si pesa hahahaha haukuwa na uwezo wa kumuhudumia ndio maana akakuacha" John aliongea kwa dharau.

"Siku zote umekuwa unajidanganya hivyo John, Sophia alikuwa kama mdogo wangu na bado ataendelea kuwa mdogo wangu na hajawahi kuwa na mahusiano ya kimapenzi na mimi, nlimruhusu aje kwa mpuuzi kama wewe kwa sababu moyo wake ndo ulitaka, nisingepinga"
" Hahahah eti mdogo wako, msitufanye wajinga basi kwani nani hapa chuoni ambae hajua kama Sophia anakupenda, ananisumbua kila siku kwa ajili yako, na leo kidogo mfe wote kwenye moto"

" Okay anyway hilo sio lililonileta hapa, John nimekuja kukuonya kwa masuala mawili muhimu
moja acha kabisa kunifuatilia, mbili acha kumtesa Sophia kwa sababu ya pesa zako, unajijua wewe ni malaya basi muache aende" Yusto aliongea kwa ukali kisha akachomoa memory inayotuza picha kwenye ile kamera na kuondoka.
"Unacheza na mdomo wa mamba Yusto, nitahakikisha unajuta maisha yako yote" John aliongea kwa hasira lakini Yusto hakugeuka wala kumjibu chochote akaenda zake.
Wakati akiondoka mara pembeni yake akatokea Caren anakuja huku akitembea kwa kasi, John alikuwa wa kwanza kumuona, akashtuka kidogo.

"We kaka, we kaka, kakaaa" Caren alikuwa akijaribu kumuita Yusto lakini Yusto hakusikia akaendelea kutembea na mwisho akapotelea kwenye jengo la mabweni ya wanaume.
Caren alibaki amesimama huku ameshika simu ya Yusto asijue la kufanya,
"Vipi Caren wangu, unashida gani na huyo jamaa nikusaidie" Caren alisikia sauti ya mtu kutoka nyuma yake akageuka.
"Aah John kumbe ni wewe, mambo yah nina shida na huyu kaka"
"Shida gani?" Aliuliza John huku akimkazia macho Caren
"Aah ni ishu private kidogo" Caren alijibu huku akiuficha mkono wake ulioshika simu ya Yusto kwa nyuma.

"Powa naweza kukupeleka kwenye chumba chake anachoishi kama hutojali"
" sawa basi tunaweza kwenda" Caren alijibu haraka haraka jibu lililomshangaza sana John, kwa anavyomjua Caren alijua ni lazima angekataa.
Sasa hakuwa na budi zaidi ya kumsindikiza Caren kilipokuwa chumba cha Yusto, wakawa wanatembea taratibu huku kila mmoja akiwa kimya akiwaza lake kichwani.

"Lakini Caren hivi nitakusubiria mpaka lini kwa nini hutaki kuamini kama mwenzio nakupenda, niamini Caren sema chochote mimi nitakupa" John alivunja ukimya.

"Ooh! umeanza porojo zako kama hutaki nisindikiza rudi" Caren aliongea kwa ukali kidogo, John akawa kimya na mwisho wakawa wanakaribia mlango wa chumba cha Yusto chumba namba 103.
*****

Baada ya Yusto kumchimba mkwara mzito John, aliondoka kwa jazba na hii ilimfanya asisikie pindi Caren anamuita.

Yusto alifika na kuingia moja kwa moja chumbani kwake akafunga mlango na kuwasha taa kwani tayari giza lilikuwa limeanza kuingia. Mara alishtuka kumuona mtu akiwa amejilaza kitandani kwake.

"Sophia umefuata nini humu ndani" Yusto aliuliza kwa mshangao hakutegea kabisa kumkuta Sophia ndani ya chumba chake wakati huo, haikuwa kawaida yake.

"Yusto baba nimekuja kukupa zawadi kwa kuyaokoa maisha yangu kwenye ajali ya moto" alisema Sophia huku akisimama pembeni ya kitanda,
Sophia alikuwa amevaa dera jepesi lililo uchora vizuri umbo la mwili wake, jambo lililomfanya Yusto kuanza kuchanganyikiwa, Sophia alikuwa mrembo haswaa na siku zote alikuwa ni rafiki mkubwa wa Yusto pale chuoni na wengi waliamini watu hao wawili walikuwa na mahusiano ya kimapenzi hadipale John alipoingilia na kuwavuruga akafanikiwa kuwakosanisha.

"No, Sophia sasa hivi ni....." Alisema Yusto lakini kabla hajamalizia sentensi yake Sophia alifungua kamba za dera kale kikadondoka chini na kumfanya abaki na nguo za ndani tu.

"Hata kama hujawahi kuwa na hisia na mimi Yusto lakini naomba kwa leo tu" alisema Sophia kwa sauti iliyojaa mahaba mazito na bila kuchelewa alikimbia na kumvaa Yusto kisha akaanza kumwagia mvua ya mabusu.
****

" Hicho ndo chumba cha Yusto namba 103" Alisema John huku akinyoosha kidole kumuelekeza Caren.
"Asante" Alisema Caren huku akiachia tabasamu lililozidi kuutesa moyo wa John.

ITAENDELEA...
 
DO NOT SHOUT
(Usipige kelele)

Sehemu ya....................05
Mtunzi: Saul David
Tel: +255756862047
E-mail: saulstewarty@gmail.com


⭐⭐⭐
ILIPOISHIA...

"Hata kama hujawahi kuwa na hisia na mimi Yusto lakini naomba kwa leo tu" alisema Sophia kwa sauti iliyojaa mahaba mazito na bila kuchelewa alikimbia na kumvaa Yusto kisha akaanza kumwagia mvua ya mabusu.
****

" Hicho ndo chumba cha Yusto namba 103" Alisema John huku akinyoosha kidole kumuelekeza Caren.
"Asante" Alisema Caren huku akiachia tabasamu lililozidi kuutesa moyo wa John.

SONGA NAYO...

Yusto alibaki ametulia tu asijue la kufanya, wakati huo Sophia alikuwa amekazana kummwagia mvua ya mabusu mdomoni na shingoni huku akihema kwa nguvu, alionyesha dhahiri kuwa alikuwa amepania kufanya kile alichokusudia kufanya, alipitisha mikono yake na kuanza hufungua vishikizo vya shati la Yusto mwisho akaona kama anachelea akalivuta kwa nguvu akang'oa vishikizo vyote vikaanguka chini, sasa akawa na kazi moja tu kucheza na mwili wa Yusto.

Wakati huo wote Yusto alikuwa ametulia tu, kumpa ushirikiano alishindwa lakini kusema hapana pia alishindwa, alijua ni kiasi gani angeujeruhi mara mbili zaidi moyo wa mwanamke huyo mrembo ambae alikuwa tayari amechoshwa na tabia za mwanaume wake aitwae John,
Siku zote Yusto alimchukulia Sophia kama mdogo wake na rafiki wa kawaida lakini kwa Sophia ilikuwa ni tofauti, yeye alimpenda mno Yusto lakini mwisho ilibidi akubali matokeo baada ya Yusto kumueleza uhalisia wa moyo wake, Sophia alikubali kubaki kama mdogo wake na walipendana sana wakaishi hivo kwa muda mrefu hali kila mtu chuoni hapo akiamini Yusto na Sophy walikuwa ni wapenzi, hali hiyo iliendelea kwa muda mrefu hadi pale Sophy alipojikuta anaangukia kwenye penzi la John mwanaume ambae alikuwa ni mtu wa kuutesa moyo wake Kila kukicha.

⭐⭐⭐
Sophia alizidi kuushika shika mwili wa Yusto kwenye maeneo ambayo alijua ni lazima angemshtua mwanaume huyo na taratibu Yusto alijikuta anaanza kupatwa na msisimko mkali wa mapenzi kiasi cha kushindwa kuvumilia, Sophia aliligundua hilo nae bila kuchelewa alishusha mkono wake na kakafungua mkanda wa Yusto taratibu.

Yusto alitoka mguno kwa mbali huku akimshika Sophia kiunoni na kumsogeza karibu yake zaidi hali wakiendelea kupeana mabusu moto moto na safari hii Yusto alionyesha ushirikiano wa kutosha jambo lililomfanya Sophia kuanza kuregea kadri muda ulivyokwenda.
⭐⭐⭐

" Hicho ndo chumba cha Yusto namba 103" Alisema John huku akinyoosha kidole kumuelekeza Caren.
"Asante" Alisema Caren huku akiachia tabasamu lililozidi kuutesa moyo wa John.

Caren alisimama kwa sekunde kadhaa bila kuzungumza chochote.
"Aah basi mimi naweza kwenda" alisema john baada ya kujishtukia kuwa Caren alikuwa akisubiri aondoke
"Poa asante John" alijibu Caren, John aliondoka hali akionekana mnyonge, alijikuta anazidi kumchukia Yusto zaidi na zaidi, roho yake ikazidi kumfurukuta akaahidi kufanya jambo zito kwa Yusto.

Baada ya John kuondoka Caren alianza kupiga hatua kusogea kwenye mlango wa chumba cha Yusto lakini kabla hajafika mara Frank akafika eneo lile nae alionekana anaelekea ndani ya chumba cha Yusto rafiki yake.

Frank alipatwa na mshituko kiasi baada ya kugonganisha macho na Caren mwanamke waliyekuwa wakimtilia mashaka kuwa ndiye aliyekuwa anahusika kwenye matukio zaidi ya matatu yaliyotokea chuoni hapo siku chache baada ya Caren kulipoti.

"Ma..mambo mdada" alisema Frank
"Poa vipi" alijibu Caren
"Safi mbona upo huku kwenye mambweni ya wanaume"
"Yeah kwani ajabu nini, nina shida na huyu kaka wa chumba hichi"
"Hichi?, unamaanisha Yusto?"
"Yeah bila shaka anaitwa Yusto"

Frank alibaki katika hali ya kuduwaa hakujua ni shida ipi ilimleta Caren kwani hawakuwa hata na ukaribu wowote na Yusto , watika akizidi kushangaa ndipo alipoiona simu ya rafiki yake Yusto ikiwa mikononi mwa Caren, hapo akakumbuka si mda mrefu Yusto alikwenda kwenye chumba cha Caren kumpeleleza na hakuwa na taarifa nini kimetokea kule.
Wakati akiwaza nini afanye kwa mbali Frank alimuona John na vijana wake watatu wamesimama wanawatazama, hili nalo lilikuwa ni tatizo jingine, Frank aligeuka na kuutazama mlango wa chumba cha Yusto ulioonyesha kuwa umefungwa kwa ndani hakuna aliyekuwa akijua kinachoendelea ndani kati ya Yusto na Sophia...

JE, NINI KITAFUATA!?
NINI KITAENDELEA KWA SOPHIA ANAETESWA KIMAPENZI NA JOHN, NA SASA SOPHIA ANAAMUA KUJITOA KWA YUSTO RAFIKI YAKE HALI ANATAMBUA HANA HISIA NA YEYE?
JE ITAKUWAJE KWA JOHN NAE AMBAE KWA SASA HAMJALI TENA SOPHIA, ANAAMISHIA MAJESHI YAKE KWA BINTI MGENI CAREN, WAKATI HUO CAREN NAE ANAONEKANA KUVUTIWA NA KIJANA YUSTO, LAKINI PIA
CAREN NI NANI HASA
KWA NINI CHUMBANI KWAKE ANA VISU NA RAMANI YA CHUO HICHO?
JE, WALINZI HAWA WA SIRI (YUSTO NA FRANK) WATAWEZA KUIFANYA KAZI YAO IPASAVYO CHUONI HAPO?
JOHN KIJANA MWENYE PESA ZAKE ATAMKABILI VIPI YUSTO?

MAJIBU YOTE HAYA UTAYAPATA KWENYE MUENDELEO WA SIMULIZI HII YA DON'T SHOUT, HAKIKISHA HAUKOSI HATA SEHEMU MOJA YA SIMULIZI HII...



ITAENDELEA LEO JIONI
 
DO NOT SHOUT
(Usipige kelele)
Sehemu ya...............06
Mtunzi: Saul David.
Whatsapp: 0756862047


UTANGULIZI(kwa wasomaji wapyaa).
Wanafunzi wawili Yusto na Frank wakiwa ndani ya chuo kimoja chenye hadhi kubwa nchini Tanzania kama walinzi wa siri wa chuo hicho, kibarua chao kinaingia dosari baada ya matukio kadhaa kutokea chuoni hapo. Wanapewa jukumu la kutafuta na kubaini chanzo ndipo wanapo mtilia shaka mwanafunzi mmoja mgeni Caren ambae ni mrembo kupindukia, wanahisi huenda akawa anahusika kwani baada ya kuja kwake ndipo matukio hayo yalianza kutokea mfurulizo na baada ya kumpeleleza wanabaini vitu ambavyo vinazidi kuwafanya waamini fikra zao. Lakini wakati hayo yakiendelea Katika isiyotegemewa Caren na Yusto wanajikuta kuanza kupendana taratibu. Wakati huo pia Yusto yuko kwenye changamoto kubwa ya kimapenzi dhidi ya mwanamke anaemchukulia kama rafiki chuoni hapo anaitwa Sophia.

ILIPOISHIA...
Wakati akiwaza nini afanye kwa mbali Frank alimuona John na vijana wake watatu wamesimama wanawatazama, hili nalo lilikuwa ni tatizo jingine, Frank aligeuka na kuutazama mlango wa chumba cha Yusto ulioonyesha wazi umefungwa kwa ndani hakuna aliyekuwa akijua kinachoendelea ndani kati ya Yusto na Sophia...
⭐⭐⭐


SASA ENDELEA

"Aah sijui ulikuwa na shida gani maana Yusto yupo kule juu chumbani kwangu" Frank alidanganya.
Caren alitulia kwa muda, alijikuta anatamani sana kuonana na Yusto, lakini sasa mazingira yalionekana kuanza kuwa magumu.

"Nina simu yake hapa aliidondosha kule bwenini kwetu naomba utampa" alisema Caren huku akimkabidhi Frank simu ya Yusto. Frank aliipokea ile simu huku akimtazama Caren usoni, alionekana kuwa mnyonge.

Baadae Caren aliondoka na kumuacha Frank amesimama nje ya mlango wa kuingilia chumba cha Yusto,
Baada ya kuhakikisha Caren ameondoka, Frank aligeuka upande mwingine akawatazama John na vijana wake ambao nao walianza kuondoka.
Frank alisogea karibu na mlango wa chumba Cha Yusto, akaanza kubisha hodi kwa nguvu.
⭐⭐⭐

Sophia na Yusto ambao walikuwa bado wakishikana shikana huku kila mmoja akianza kuzama taratibu kwenye ulimwengu wa huba walishutushwa na kelele za mlango ulokuwa ukigongwa kwa nguvu.

Walitulia kimya kwa muda lakini mlango uliendelea kugongwa tena na tena na safari hii alisikika frank akiita kwa nguvu.

"Yusto, Yusto, fungua basi umelala saa hizi?"

Hatimae Sophia aliamua kumuachia Yusto hali akionyesha kukasirika kiasi, akavaa nguo zake kisha akawa anatembea kuelekea mlangoni.

Wakati huo wote Yusto alikuwa amesimama anamtazama mwanamke huyo ambae alikuwa amejeruhiwa na mapenzi baada ya John kuuchezea moyo wake, Yusto alijua ni namna gani amekasirika lakini hakujua ni vipi angeweza kumsaidia.

"Sophia..." Aliita Yusto

"It's okay, naelewa" Sophy alijibu kwa kifupi akimtaka Yusto asizungumze ziadi, akatembea hadi mlangoni akafungua na kutoka nje akaondoka zake bila hata kuzungumza lolote na Frank ambae alibaki amesimama mlangoni katika hali ya mshangao huku akimsindikiza sophy kwa macho.

"Ni nini hii Yusto" aliuliza Frank huku akifunga mlango akawa anamtazama Yusto ambae alikuwa bado yu kifua wazi.
"Siku zote unasemaga Sophy ni kama mdogo wako hii ni mnafanya"

"Unajua kila kitu Frank, sikuwa na chaguo lingine, huyu mwanamke kaumizwa vya kutosha sikutaka kumuumiza zaidi ni heri kumpa anachokitaka, kwani shida iko wapi" Yusto aliongea kwa kujiamini

"Oh! Come on Yusto unakosea, you are a gentleman, kwa nini ujirahisishe kihivyo kwa mwanamke huoni kama unajivunjia heshima".

"Frank, Frank tafadhali... Mimi namuelewa sophy kuliko mtu mwingine yoyote hapa chuoni, najua lipi ni jema na baya kwake. Kwanza shida iko wapi mimi ni mwanaume naweza kudate nae nikitaka,"

"Mmh isiwe ni kweli kama watu wanavyo sema mnajiita kaka na dada kumbe mnakulana kisiri Siri hahahah"

"Unacheka nini sasa hebu achana na hizo stori hakuna tulichokifanya hata hivyo nashukuru kwa ujio wako"
Alisema Yusto huku akihangaika kupekuwa pekuwa kwenye mifuko ya suruali yake ni kama vile kuna kitu alikuwa anakitafuta bila mafanikio

"Simu unayoitafuta hii hapa" alisema Frank.

"Eee.. umeipata wapi" Yusto aliuliza kwa mshangao huku akijaribu kutafakari ni wapi aliidondosha simu yake.

"Ooh nilidondosha wakati napigana na yule kijana wa kamera" alisema Yusto na hapo akamsimulia Frank namna alivyokuwa anapigana na yule kijana aliyetuma na John kumfuatilia pindi alipoingia bweni la wanawake.

"Unajua Yusto unakaribia kuanzisha vita nyingine na John yule bwana anaweza kukufanyia lolote baya, kumbuka mwaka jana aliuwa kimasihara tu na ushahidi ulikuwepo ila akashinda kesi kwa kuhonga, sasa wewe naona unakatisha kwenye kumi na nane zake" alisema Frank

" kivipi"
"Hujui, kwani humu ndani si ulikuwa na Sophia na unajua anamahusiano na John, haya saa hizi John anamfuatilia Caren lakini tayari huyo Caren anataka kujenga ukaribu na wewe"

"Aah wapi hilo haliwezi kutokea, Caren hanijui simjui, mimi sio type ya yule mwanamke, simuwezi kwanza"

"Unakataa nini Yusto hii simu ameleta Caren, amekuja hadi hapa nje akiwa pamoja na John alitaka kuingia humu ndani mimi ndo nimemzuia,"

"Unasema nini wewe, Caren huyu huyu aje huku kwenye mabweni ya wanaume, no haiwezekani,"

"Ooh mimi ndo nakwambia, hebu nambie upelelezi wako umeendaje kunakitu chochote umekigundua kwenye chumba cha Caren"

"Mmmh bwana wee, ukweli huyu mwanamke anaweza akawa sio mtu wa kawaida, chumbani kwake nimekuta kuna ramani ya hiki chuo chote, pia anakoti moja kubwa limechomekwa chomekwa visu vingi vidogo vidogo kwa ndani yaani kama mafia hivi, nina wasi wasi sana na Caren tena sana" alieleza Yusto

"Kwa hiyo tunafanyaje, si uajua tumepewa wiki moja tu na bosi, mi napenda kazi ndugu yangu" alisema Frank baada ya kutafakari kwa muda.

"Inabidi tumpeleleze Caren tena, kwanza tutege camera zetu za siri hiki chuo chote hadi kwenye mlango wa Caren hii kazi tuifanye usiku wa leo"
Alisema Yusto wazo lililoungwa mkono moja kwa moja na Frank.

"Ooh kuna sms imeingia kwenye simu yako hapa, ila wakati mwingine kuwa makini sijui kama Caren hajaipekuwa pekuwa hiyo simu yako, demu mwenyewe naona kama anakupenda hivi, hahahaha"

"Acha utani basi, unajua kabisa huyu anaweza kuwa adui yetu namba moja na leo usiku tunakazi ngumu kwa ajili yake, anaanzaje kunipenda" alisema Yusto huku akipokea simu yake na kuifungua ile meseji kutoka kwenye namba ngeni.

'HELLOW YUSTO MAMBO,
CAREN'


Yusto alibaki ametoa macho kwa mshangao, huku akirudia rudia kuisoma ile meseji kichwani akawa anaitengeneza taswira mwanamke huyo mrembo kupindukia.

"Oya vipi mbona umeduwaa, meseji ya nani ni Sophia nini, anataka tena" aliuliza Frank huku akimtazama Yusto kwa macho ya udadisi.
Yusto hakujibu chochote, ujumbe wa Caren ulimchanganya.
"Yap ni sophy ananiomba ladhi kwa kilichotokea" Yusto alidanganya
"Dah ila mna drama nyie" alisema Frank wakati huo wala Yusto hakuwa akimsikiliza, alikuwa bize kujibu sms ya Caren.


NAMBIE CAREN ASANTE SANA KWA KUNILETEA SIMU, SIJUI NIKUPE ZAWADI GANI

Alijibu na kukaa kwa hamu kusubiri Caren atajibu nini lakini hadi dakika 45 zinakwisha Caren hakuwa amejibu chochote. Wakati wote Yusto alikuwa ameshikilia simu yake akisubiri ajibiwe.
⭐⭐⭐

Baada ya Caren kurudi chumbani kwake alijikuta moyo wake unauma sana kwani alikuwa na hamu kubwa ya kuonana na Yusto kijana ambae taratibu alikuwa akimwingia moyoni, kila alipo mfikiria alijikuta anatabasamu mwenyewe.
Mwisho uzalendo ulimshinda kwa kuwa tayari alishaichukua namba ya Yusto akamtumia ujumbe mfupi wa maandishi akajilaza akiwa anasubiria majibu kwa hamu kubwa.
Mara sms iliingia akaruka na kuichukua simu yake lakini tofauti na alivyotegemea ilikuwa ni Sms kutoka kwa John.

CAREN MWANAMKE MREMBO KULIKO WOTE NILIOWAHI KUWAONA NITAFANYA CHOCHOTE KUHAKIKISHA NAKUPATA, MIMI SIO MTOTO NISHAJUA UNAMPENDA YUSTO SASA KWA USALAMA WA MAISHA YAKE KAA MBALI NAE.

Ilikuwa ni sms iliyoambatana na vitisho kutoka kwa John, lakini cha ajabu Caren hakuogopa badala yake akacheka kwa dharau na punde ikaingia sms kutoka kwa Yusto akimtaka achague zawadi baada ya kumupelekea simu.

Caren akiwa anatabasamu aliwaza ni jibu gani nzuri angemjibu Yusto.

Mwisho alipata jibu lakini kabla hajatuma ujumbe wowote mara iliingia sms nyingine kutoka kwenye namba aliyoisave Boss G meseji hiyo ilibadilisha kabisa mudi aliyokuwanayo Caren.

NAOMBA TUWASILIANE SASA HIVI

Haraka alichukua kompyuta yake ndogo akapanda kitandani na kukaa, akaifungua kisha akabonyeza vitufe kazaa, sura ya mwanaume mmoja mzungu ilijitokeza kwenye kioo cha kompyuta yake wakawa wanawasiliana kwa njia ya video kitalamu inajulikana kama mtandao wa Skype.

"Hello Diana habari yako"
Aliongea yule mzungu kwa kiswahili dhaifu huku akimwita Caren, Diana.
"Ni nzuri bosi"
"Hongera umefanya kazi mzuri sana leo kwa kusababisha moto mukubwa maktaba, leo ushiku tunataka ufanya kazi ingine, hakikisha from tomorrow i mean kesho kusiwe na umeme hapo chuoni hadi week iishe sawa Diana"
"Sawa bosi nimeelewa" Caren aliitika kwa unyenyekevu mkubwa.

"Ramani ipo, vifaa ipo, you have everything you need so make sure unafanya kazi muzuri, see you" Alisema yule mzungu kisha akatoweka kwenye kioo cha kumpyuta ya Caren/ Diana.

Caren alibaki ametulia kwa muda, wala hakukumbuka tena kumjibu Yusto sms, alifunua godoro na kuchomoa bastola iliyokuwa chini ya kitanda akawa anaitazama huku akifikiria jambo, sura yake ya kirembo ilionekana kubadilika hakuwa Caren yule wa kawaida, aliishikiria bastola huku macho yake makavu akijitazama kwenye kioo.

⭐⭐⭐
Yusto nae baada ya kukaa muda mrefu bila Caren kumjibu aliweka simu pembeni na kuanza mandalizi ya kazi kubwa wanayotakiwa kuifanya usiku wakiwa kama walinzi wa siri wa chuo hicho chenye hadhi kubwa kuliko vyuo vyote nchini TANZANIA.

Je nini kitafuataa
ITAENDELEA TENA KESHO
 
DO NOT SHOUT
(usipige kelele)

Sehemu ya.............07
Whatsapp: 0756862047

Mtunzi: Saul David


ILIPOISHIA....
Yusto nae baada ya kukaa muda mrefu bila Caren kumjibu aliweka simu pembeni na kuanza mandalizi ya kazi kubwa wanayotakiwa kuifanya usiku wakiwa kama walinzi wa siri wa chuo hicho chenye hadhi kubwa kuliko vyuo vyote nchini TANZANIA.

SASA ENDELEA...

MIAKA MINNE(4) ILIYOPITA...
NCHINI BURUNDI....


Umaskini, njaa, ukabira,vita vya wenyewe kwa wenyewe, maafa ya hapa na pale ni changamoto kubwa zilizokuwa zikiendelea kuwakumba kabila la Watusi waliokuwa wakiishi katika kijiji kimoja cha Nzintao nchini burudi kilichokuwa karibu na mpaka wa TANZANIA.

Maisha ya watu hao yalikuwa ni ya taabu mno, hakuna aliyekuwa anawatazama au kujaribu kuwasaidia, kufa kwa njaa kwao ilikuwa ni tukio la kawaida, hakika hali yao ilitisha mno.

Diana alikuwa ni binti mdogo yapata miaka 16 hivi nae alikuwa miongoni mwa familia masikini zilizokuwa zikiishi maisha ya dhiki kali katika kijiji hicho, Diana alikuwa akiishi na mama pamoja na mdogo wake wa kiume ambao kwa wakati huo wote walikuwa ni wagonjwa mno wakisumbuliwa na maradhi mbalimbali ya mwili.
Baba yake Diana alifariki miezi 6 iliyopita akiwa vitani hivyo jukumu la kuilea familia hiyo lilibaki mikononi mwa binti mdogo Diana ambae nae hakuwa na lakufanya kutokana mazingira ya kijiji hicho, zaidi ya kusubili miujiza.
Mama na mdogo wake walikuwa wanashinda ndani wamelala hakukuwa na matumaini kabisa ya wao kupona, Diana ndiye aliyekuwa akihangaika angalau kuwatafutia angalau mlo mmoja kwa siku, hali ilitishi mno.

Siku moja Diana akiwa nje ya kibanda chao, aliona gari zuri jeupe likisimama mbele yake mara wakashuka watu wanne waliokuwa wamevalia suti nadhifu zenye rangi nyeupe.

"habari Diana mama hajambo" aliongea mwanamke mmoja wa watu wale huku akiachia tabasamu nzuri na kushikashika shavu la Diana kisha akampatia biskuti.

Diana aliitikia huku akipokea ile biskuti kisha akaachia tabasamu lililofanya sura yake nzuri iliyokuwa imefichwa na ugumu wa maisha kuonekana.

"Tupo hapa kwa ajili ya kukusaidia wewe mama yako na mdogo wako, tutawatibu wote watapona sawa mtoto mzuri"alisema yule mwanamke.

"Daktari aliwahi kunambia mama na mdogo zangu hawawezi kutibiwa kokote kule tofauti na India" Diana aliongea kwa unyonge.

"Hilo sio tatizo Diana, kama utakubali kuondoka na sisi basi tutabadilisha maisha yako, nishike mkono twende wote" alizidi kuongea yule mwanamke hali tabasamu lake likiwa kwenye viwango vya juu.

"Twende wapi" aliuliza Diana huku akimuangalia usoni.

"Tanzania, twende wote Tanzania"

Diana alibaki ametulia kimya kwa sekunde kadhaa akageuka na kuitazama nyumba yao mbovu ambayo ndani yake alilala mama na mdogo wake wakisubiri kufa, akageuka tena na kuwatazama wale watu ambao wote walikuwa na nyuso za furaha.

Diana alijikuta akinyoosha mkono na kuushika mkono wa yule mwanamke, hii ilikuwa ni ishara tosha kuwa Diana amekubali kuondoka nao.

Bila kuchelewa watu hao waliingia ndani wakamchukua mama na mdogo wake Diana pamoja na Diana mwenyewe wakaingia ndani ya gari na safari ya kuelekea nchi Tanzania ikaanza.
****


Masaa 12 baadae Diana alikuwa ndani ya jengo moja kubwa la kifahari, huko alikutana na watoto wengine wa kike wa lika lake akaunganishwa nao na hapo akajikuta anaingia kwenye maisha mapya ambayo hakuwahi kuyawaza.

Diana na wenzake walikuwa wakipema mafunzo maalum ya kupambana pamoja na matumizi ya siraha pamoja na vitu vingine vingi vikuhusu maisha ya kawaida, ulikuwa ni kama vile kambi ya jeshi.

Tangu aiingizwe ndani ya jengo hilo Diana na wenzake 21 hawakuwahi kutoka, kuna baadhi ya siku Diana alikuwa akichukuliwa na kuingizwa kwenye chumba maalum cha mawasiliano huko aliwasiliana na mama yake mzazi pamoja na mdogo wake ambao walikuwa nchini india wakiendelea na matibabu, afya zao zilionekana kuimalika sana na walionekana kuwa watu nyenye furaha mda wote jambo lililompa faraja kubwa Diana akajikuta anaapa moyoni kujitoa kuwatumikia watu hao kwa namna yoyote ilimdradi tu mama na mdogo wake waishi.

Aliendelea kubaki ndani ya ngome hiyo huku uzuri wa sura na umbo lake vikiendelea kujidhihirisha siku hadi siku, si hivyo tu bali Diana alikuwa akijitoa sana katika mazoezi kuzidi wenzake wote, uwezo wake pia ukawa ni mkubwa zaidi jambo hili liliwafurahisha zaidi waalimu wake na kumuona kama mwanafunzi bora kuliko wengine.

Siku zilizidi kwenda hatimae mwaka wa kwanza wa pili wa tatu na hatimae wa nne,
Sasa Diana akawa na umri wa miaka 21.
⭐⭐⭐

"Diana umefika wakati wa wewe kufanya kazi zetu nje na hapa, kazi yako ya kwanza pamoja na wenzako ni kumuangusha kiuchumi huyu bwana anaejiita Mark Moon, tutashambulia biashara zake zote hadi tuhakikishe anaporomoka ki uchumi, Diana wewe tunakutuma katika chuo chake kimoja kipo Dar es salaam chuo hicho ni kipya, Mark Moon amekijenga kwa gharama kubwa na wanafunzi wanaosoma pale ni wenye hadhi ya juu, wewe utaenda pale kama mwanafunzi wa kawaida lakini tutakuwa tukikuelekeza vitu vya kufanya, lengo letu ni kuharibu kabisa sifa ya chuo hicho."

Hayo yalikuwa ni maelekezo aliyopewa Diana ikiwa ndio kazi yake ya kwanza kuifanya.

"Huyu anaitwa Dr Gavin, yeye ndo atakae waongoza kwenye hii kazi, Diana tunakwamini sana hakikisha unafanya kazi kwa usahihi, pia kabla hujaondoka hakikisha umewasiliana na mama na mdogo wako"

Baada ya taratibu zote kukamilika team ya wanawake wanne ikiongozwa na mtu mmoja mzungu aliyeitwa Dr Gavin ilitoka nje ya ngome hiyo kubwa na kuingia mtaani katika oparesheni ya kumdondosha ki uchumi tajiri mmoja mkubwa maarufu kama Mark Moo.

"Diana nakukumbusha wewe utaitwa Caren Onyango kene chuo hichi usishahau hilo, nikutakie kazi mzuri" alisema Dr Gavin huku akionekana kusumbuliwa na lugha ya kiswahili.

Diana/Caren aliingia katika chuo hicho huku uzuri wa sura na umbo lake ikiwa ni sifa iliyotetemesha karibu chuo kizima, Diana alianza kazi yake kama alivyokuwa akielekezwa na hadi sasa alikuwa amekamilisha matukio kadhaa ambayo taratibu yalianza kushusha hadhi ya chuo hicho
Leo ilikuwa siku ya Diana/Caren kupewa kazi nyingine.
⭐⭐⭐

"Hello Diana habari yako"
Aliongea yule mzungu(Dr Gavin) kwa kiswahili kibovu.
"Ni nzuri bosi"
"Hongera umefanya kazi mzuri sana leo kwa kusababisha moto mukubwa maktaba, leo usiku tunataka ufanya kazi ingine, hakikisha from tomorrow i mean kesho kusiwe na umeme hapo chuoni sawa Diana"

"Sawa bosi nimeelewa" Caren aliitika kwa unyenyekevu mkubwa.

"Ramani ipo, vifaa ipo, hakikisha unafanya kazi muzuri, vinginevyo utaingiza ndugu zako yote matatizoni" Alisema yule mzungu kisha akatoweka kwenye kioo cha kumpyuta ya Caren/ Diana.

Caren alibaki ametulia kwa muda, wala hakukumbuka tena kumjibu Yusto sms, alifunua godoro na kuchomoa bastola iliyokuwa chini ya kitanda akawa anaitazama huku akifikiria jambo, sura yake ilionekana kubadilika hakuwa Caren yule wa kawaida.
Yusto nae baada ya kukaa muda mrefu bila Caren kumjibu aliweka simu pembeni na kuanza mandalizi ya kazi kubwa wanayotakiwa kuifanya usiku wakiwa kama walinzi wa siri wa chuo hicho chenye hadhi kubwa kuliko vyuo vyote nchini TANZANIA kilichokuwa kikimilikiwa na tajiri mkubwa bwana Mark moon.

ITAENDELEA.....
 
DO NOT SHOUT
Sehemu ya...........08
Mtunzi: Saul David
Email: saulstewarty@gmail.com

ILIPOISHIA...

Walinzi wa siri wa chuo ambao wanajifanya kuwa ni wanafunzi Yusto na Frank wanajiandaa kwenda kufanya kazi ngumu usiku huo ya kumpeleleza binti mmoja mgeni katika chuo hicho Caren ambae ametumwa kufanya matukio yatakayo kiharibia sifa chuo hicho maarufu nchini Tanzania. Usiku huo huo Caren nae amepanga kwenda kufanya tukio lingine chuoni hapo kama alivyoagizwa..

SASA ENDELEA...

Ukiwa ni usiku wa saa saba Yusto alikuwa anamalizia kujiandaa mara mlango wa chumba chake ulifunguliwa ghafula akaingia mtu ndani kwa kasi na kufunga mlango. Yusto alishtuka akachukua bastola yake aliyokuwa ameiweka kitandani akaificha upesi kwa kuichomeka nyuma kiunoni.

"We vipi bana unashindwa kubisha hodi" Yusto alifokaa baada ya kugundua mtu aliyeingia alikuwa ni rafiki yake Frank.
"Saa hizi ni usiku bro hodi za nini unataka kila mtu atusikie" alijibu Frank.

Walitumia dakika 15 kujadilia jinsi watakavyotekeleza jukumu lao usiku huo na mwisho walikuwa tayari kuanza kazi wakatoka taratibu kuelekea kwenye mabweni ya wanawake wote wakiwa wamevalia makoti meusi marefu na kuziba nyuso zao kwa vitambaa.
Walipofika mahali kila mmoja alielekea upande wake, Frank alikuwa na kazi ya kwenda kukata umeme chuo kizima wakati huo Yusto yeye alielekea kwenye chumba cha Caren, hivi ndivyo mpango ulivyokuwa umekaa.
⭐⭐⭐

Saa sita na nusu usiku Caren alikuwa tayari ameshatoka chumbani kwake kwenda kutekeleza jukumu alilopewa.
Hakuwa Caren yule binti mrembo mlaini aliezoeleka chuoni hapo, huyu alikuwa ni Caren mwingine kabisa.
Akiwa na mavazi yale yale sawa na waliyo vaa Yusto na Frank aliingia kwenye jengo moja ambalo lilikuwa linatunzwa samani mbali mbali za chuo zilizo chakaa ama kuharibika.

Dakika mbili baada ya Caren kuingia jengo hilo mara umeme ukakata chuo kizima. Upesi alionekana anatoka kama upepo akapotea na kutokomea bwenini kwao, alikuwa mwepesi mno na aliifanya kazi yake kwa ustadi mkubwa.
⭐⭐⭐

Frank aliyekuwa anaelekea ilipokuwa main switch ya kukata na kuruhusu umeme chuoni hapo alishangaa umeme unakata hata kabla yeye hajafika. Alibaki ameduwaa kwa muda, hasa baada ya kugundua maeneo jirani na chuo hicho yalikuwa na umeme kama kawaida hii ilimaanisha chuoni kwao tu ndipo hapakuwa na umeme.
Akiwa katika hali ya kutahamaki kwa mbali alimuona mtu anakimbia kwa kasi na kuingia kwenye mabweni ya wanawake, jambo lililo mshangaza zaidi mtu huyo alikuwa amevalia mavazi kama waliyo vaa yeye na Yusto.
"Shiiit" alisema Frank hali akiuma meno yake. akawa anapiga hesabu afanye nini.
⭐⭐⭐

Yusto akiwa tayari ndani ya mabweni ya wanaweke alikuwa amesimama nje ya mlango wa chumba cha Caren alipoutazama vizuri mlango aligundua kuwa umefungwa kwa nje.

"Inamaana ametoka?, Kaenda wapi" Yusto alijiuliza mwenyewe bila ya kuwa na majibu na taratibu alisogea hadi karibu kabisa na mlango huo lakini kabla hajafanya lolote mara umeme ulikata.

"mmh kijana yuko shapu huyu"

Alisema Yusto huku akiamini kabisa Frank rafiki yake ndiye aliyekata umeme, lakini kumbe haikuwa hivyo, hii ilikuwa ni kazi ya Caren.
Kama kawaida yake Yusto aliingiza vipini flani kwenye kitasa na mara mlango ukafunguka, akaingia ndani kwa tahadhali na kufunga mlango.

Aliwasha tochi ya simu yake, kuangalia kitandani palikuwa patupu hakuna mtu, akakagua sehemu zote chooni na bafuni kulikuwa kimya kabisa.

"nilishasema huyu mwanamke sio wa kawaida" alisema Yusto huku akizidi kukagua.
Lakini wakati akiendelea kufanya hivyo mara alisikia vishindo vya mtu anakuja kwa kasi,
alizima tochi yake upesi na kutulia kimya.
Sekunde chache baadae vishindo vilisikika karibu kabisa na mlango na mara mlango ulianza kufunguliwa.

"Caren" Yusto aliongea kimoyomoyo huku akiwa ametoa macho na haraka alinyata na kungia bafuni akafunga mlango na kutulia kimya.
Ni kweli alikuwa ni Caren mwenyewe, aliingia taratibu akafunga mlango kisha akawasha taa yake maalum ya sola. akaanza kuvua nguo zake za kazi taratibu na kuzipanga kwenye droo ya kabati.

Yusto akiwa bafuni alitulia kwa zaidi ya dakika mbili na mwisho akainuka taratibu kuchungulia.
Mlango ulikuwa umezibwa kwa chini lakini juu ilikuwa ni kioo hivyo Yusto aliweza kuona upande wa pili.
Macho yalimtoka hasa baada ya kuona kitu ambacho hakukitegemea, ndo kwanza Caren alikuwa anazidi kuvua nguo zake taratibu, alivua kila kitu na sasa alibaki na sidilia pamoja na chupi basi.

Alisogea kwenye kioo na kuanza kujitazama huku akizunguuka zungukaa, wakati huo Yusto alikuwa akimshuhudia hali akiwa ametoa macho, aliushuhudia uzuri wa mwanamke huyo kwa karibu kabisa, mapigo yake ya moyo yalianza kubadilika kadri muda ulivyokwenda.

Caren alifungua kabati na kuchukua radio yake ndogo akabonyeza vitufe kadhaa mara mziki laini ulianza kusikika kwa sauti ya chini.
Caren alianza kucheza na kuimba mziki huo laini wa kirundii wenye asili ya burundi.
Hakika Caren alikuwa ameumbika, alikuwa na kila sifa ya kuitwa mwanamke mrembo,ukiachilia mbali sure yake nzuri, mwili wake ulikuwa umejikata vizuri kiunoni, laini,kitovu cha kudumbukia, mapaja yake yaliyo jaa na kuzifanya hips zake zibambe saawia.
Hali hi ilimfanya Yusto kujisahau kabisa akasimama nakuendelea kumtazama...

Hali akizidi kucheza Caren aliikumbuka simu yake, akaisoma tena ile sms alotumiwa na Yusto ndipo akakumbuka hakumjibu.
Akiwa bado anacheza Caren aliandika ujumbe kumjibu Yusto huku akitabasamu

'Vp umelal, samahn kw chlew nlikuw bze kdg, mmm hyo zawad nikkuomb utanpa dady😉😉'


ITAENDELEAA....
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom