Simulizi ya kusisimua

Simulizi ya kusisimua

SEHEMUBYA 40
NA GAOOH
SIMU 0654387935
TULIPOISHIAAA SEHEMU ILIYOPITA..
Japo sikuwa nikijua sana ila majina ya somoe
sidhani kama ni watu tabora kama john
alivyonambia kuwa msichana atatokea tabora, aah
sikujali sana nikaamua nifunike tu kombe
mwanaharanu apite, tulimuonesha chunba chake
cha kulala..
SASA ENDELEAAA..
Tulianza maisha na somoe akiwa kama mfanya kazi
wa ndani, Alizifanya kazi vizuri hukua akinisaidia
kazi huku ujauzito wangu ukiendelea kukua siku
hadi siku.
"Mke wangu umeona sasa somoe ni binti mzuri
sikuamini kama ataweza kufanya kazi vizuri namna
hii,"
"Kwann hujutegemea,?"
"Rafiki yangu niliemuomba anitafutie mdada wa kazi
aliniambia yuko busy sana hivyo ikabidi.." Kabla
hajamaliza nikamkatisha.
"Ikabidi nimwanbie mtu mwengine najua
ningekuanbia siku ya kwanza kabla hajaja basi
ungekata, ndio mana nilimleta alafu nikasubiri
akianza kufanya vibaya ndio nimfukuze, ila kumbe
binti wa wawatu ni mtulivu na anafanya kazi zake
kwa bidii NIMEMPENDA KWA KWELI,"
"Ndio umefanya nini sasa hivi John?, utakuja
kuniletewa wachawi kwenye nyumba," nilisema.
"Usijal mke wangu ilikuwa ni lazima nikuletee mtu
wa kusaidia kazi,matarajio yangu yalikuwa ni
kuletewa na rafiki yangu ila ameshindwa sasa
ningefanyaje nisamehe kama nimekosea ila
nakuahidi kama Somoe atafanya kosa lolote
nitamtiamua." John alihitimisha sikutaka kuifanya
iwe mada nilimkubalia john tu wakati huo somoe
alikuwa chumbani kwake na sisi tulikuwa chumbani
kwetu.
Asubuhi kama kawaida Mume wangu aliamka kisha
akaniamsha na kisha kujiandaa kwa ajili ya kwenda
kazini alijiandaa hapo nikaamka na kwenda nje
kumuandalia chai, nilijua pengine somoe hajaamka
bado ila nilipoamka nilikuta amekwisha amka muda
huo alikuda anadeki ndani.
"Shikamoo dada,"aliniamkia huku akiinamana kama
mtu anaetaka kupiga magoti.
"Marahaba umeamkaje,"
"Salama dada sijui wewe na shemeji,"tuliongea
machache nikaenda jikoni kuandaa chai ya Mume
wangu kisha akatoka nilimtengea akanywa wakati
huo Somoe akiendelea na usafi John alipo maliza
kunywa chai nilimuweka shati lake vizuri kisha
nikamtoa mpaka nje kwenye gari nilimbusu na yeye
akanibusu kisha akaingia ndani ya gari yake
akaniaga na kuondoka.
Nilirejea ndani na kuelekea chumbani kwangu kulala
tena.
Kitendo cha kulala na kupita dakika kadhaa nilijihisi
sipo pale nikipolala ila nipo sehemu nyengine yenye
majani mengi ya mti yaliodondoka na kujikusanya
sehemu moja kisha mimi nikalala juu yake nilijihisi
kutokuwa na fahamu kwavile nilikuwa nimelala huku
yule msichana niliekuwa nikimuonaga ndotoni ndio
alikuwa pembeni yangu na wenzake wakiwa na visu
tena vikiwaka moto walifika mpka nilipokuwa kisha
alikuta peke yake yule msichna hapo akachoma kisu
tumboni kwangu sikuwa na nguvu za kuamka wala
kupiga kelele kuzuia kile mwili wangu ulikuwa kama
uliopooza pia cha kushangaza hata maumivu
sikuyasikia kisu kiliingumia tumboni kwangu na
mtoto walimtoa baada ya kumtoa walianza kuimba
nyimbo zao nyimbo ambazo nilizikumbuka vyema
za kule hekaruni tofauti ni kuwa sikuwahi kuzielewa
maana yake ila nilijua tu huwa zinaibwa kwa ajili ya
nini, zipo za kushegherekea na zipo za huzuni hasa
mmoja wetu akifa bila ya matakwa yetu kipindi kile.
Hizi walizoimba zilinikumbusha kuwa ni nyimbo za
sherehe, waliimba huku wakinizunguka nikiwa
nimelala pale pale chini, nyimbo zile waliimba huku
mtoto wangu wakimuweka juu juu baada ya kufanya
vile wakamuingiza ndani ya chungu ambacho
kilikuwa kimewekwa juu ya kichuguu niliweka, zoezi
hiki pia nililikunbuka kuna kipindi tulikuwa tukipata
vichanga tuna vitia ndani ya chungu ambacho kina
damu kisha tunavichinja na kuvila nyama, ni kweli
na wao walifanya vile vile nilishuhudia kwa macho
yangu pimaa mwanangu wakimtafuna pia wasivyo
na adabu walinioneshe nyama za viungo vyake hasa
mguu walinionyeshe niliumizwa na kitendo kile,
baada ya kumalza kula mwili wa mwanangu ndipo
walipokuja na kwangu walishika mguu wakitaka
waunyofoe kwenye mwili wangu kitendo hiki ndio
kilinifanya niogope zaidi nikistukaaa nikiwa nahema
juu juu.
"Umefikaje huku ndani," nilishangzwa na uwepo wa
Somoe chumbani kwangu, tena alikuwa amenishika
mguu.
"Nakuuuliza Somoe kipi unafanya chumbani
kwangu,?"
"Nisamehe dada, nilikuwa nakutafuta huko nje
nikakukosa ndio nikaingia ndani ila nilipofika nje ya
chumba chako nikakikuta kipo wazi ikanibidi niingie
nikuamshe dada"
"Unasemaje Somoe, unaingiaje chumbani kwangu
bila taarifa yoyote,"Nilimfokea somoe kitendo kile
hapo nikabadirika kabisa nikimwambia achukue
nguo zake arudi kwao ndoto ile ilinitesa sana akili
yangu na kustuka kumkuta somoe ndio niliumia
zaidi.
"Nisamehe dada, nisamehe sina kwa kwenda Dada
nilipotoka kuna shida nimefanya kuondoka walitaka
kuniodhesha dada nakuomba usinifukuze sitarudi
tena dada"aliongea huku akilia tena machozi
yakimserereka kwenye mashavu yake, kuona vile
huruma ilinikaa nilimuonea huruma Somoe, hapo
nikajiona nafanya dhambi,dhambi ya kumhisi mtu
vibaya ikiwa sio yeye wala hausiki na chochote.
"ondoka zako, kafanye kazi zako, toka chumbani
kwangu,"nilimfokea akaamka alipokuwa amepiga
magoti kisha akaondoka chumbani kwangu akilia
kwa kufina fina,baada ya Somoe kuondoka hapo
niliingia bafuni kuoga nilihisi uchovu mwili mzima
akili haikunipa niliioga maji nikiwa na mawazo
"Somoe ni nani?, Somoe ni nani,?"Sauti kubwa
iligonga kichwani kwangu ikitaja jina la Somoe,
nilipotoka bafuni nilitamani kumpigia simu Mume
wangu ila niliwaza nitamwambia kitu gani ikiwa
nilimficha hapo mwanzo asijue chochote kuhusu
mapito yangu.
Nilifunika tena kombe nikatoka nje ya chumba
changu kisha nikikaa mezani nikihisi tumbo langu
likihitaji chakula zaidi, nilichukua chupa ya chai
kisha kujiwekea chai hapo nikaanza kunywa, huku
mikate ikiwa mezani.
"Somoee somoe," nilimwita kwa sauti kubwa, nae
alikuja akiwa na wasi wasi alikuja akiwa mpole
zaidi huku uso wake ukibeba hisia zake, kutokana
na machozi yakiokuwa yakimtoka, pia mikono
akiiweka nyuma.
"Nisamehe dada,"ndio neno la kwanza alilosema
tena akipiga magoti.
"Amka yashaisha yale," nilimwambia akaamka pale
na kusimama hata uso wake aliuinamisha chini
asiniangalie machoni.
"Nenda chumbani kwangu kuna nguo pale chafu
nataka uzifue,"
"Sawa dada,"alisema kisha akaondoka, nikaendelea
kunywa chai, saa zilisogea mpaka pale giza
lilipomea usiku ndipo john wangu aliporudi
nilimkumbatia kisha nikairegeza tai yake,
nikamkaribisha ndani tukaongozana muda wote
niliuhisi upweke hivyo john alivyokuja ni kama faraja
kwangu, Muda wote Somoe alikuwa kwenye sofa
akituangalia tu mi na john alionekana kama mtu
anaetuwaza sana, sikumjali nikaingia na john
chumbani huku nimeshika mkoba wake tulipoingia
ndani, akaingia bafuni kuoga nikakaa nikimsubiri
mpka alipotoka tukaelekea mezani kwa ajili ya kula
chakula cha usiku.
"Somoe yuko wapi?" John aliuliza.
"Alikuwa amekaa pale anaangalia tivi,"
"Yeye amekwisha kula au,?"
"Hata sijui John, ila amekula kama angekuwa hakula
basi angekuja hapa!,"nilimjibu john kisha mada ile
tukaipotezea tukianza kuongea kuhusu kazi
zake,alizungumzia changamoto zake za siku hii
alizokutana nazo niliishia kumpa pole John wangu
mana niliamini anatafuta kwa ajili ya Maisha yetu na
watoto wetu.
Tulimaliza kula john alijinadi kuchoka hivyo niliacha
tu vyombo pale nikaingia ndani na john wangu kwa
ajili ya kulala hata mimi nilihisi uchovu hivyo
tulivyojilaza kitandanj tukapitiwa na usingizi, kifuani
kwa john nikilala huwa nahisi amani zaidi hivyo hata
nilipolala nilipitiwa na usingizi, nikiwa usingizini
nilistushwa na sauti ambazo nilizisikia, nje.
Nilipata ujasiri ambao sikujua ulipotoka kiasi
kwamba niliamka kitandani ila nilipoamka sauti zile
zilikata, niliingia chooni kwavile nilihisi kubanwa na
mkojo hivyo nikingia chooni nilipotoka chooni
nikiona mwanga chini ya mlango hapo nikajua ni
mwanga wa taa hivyo nikichofanya nikafungua
mlango wa chumbani bila woga na kukuta taa ikiwa
haijazimwa. "Inamana huyu Somoe hakuamka?"
Nilijiuliza bila majibu, hapo ikabidi nianze kupiga
hatua kuifata switch ya umeme ili nikazime taa,
kitendo cha kupiga hatua ili nikazime taa ndipo
likazuka jambo la ajabu, mlango wa chumba cha
Somoe ndio nilipokomea Sauti za ajabu zikisikika
ndani humo nikiogopa kupiga hatua, kwani kelele na
milio isioeleweka ilisikika ndani mwa Somoe.
 
Riwaya nzuri sana tafadhali weka nyingine bioto keyaa
 
SEHEMU YA 41
NA GAO
SIMU 0654387935
TUNAENDELEA TULIPOISHIAA
Nilijiuliza bila majibu, hapo ikabidi nianze kupiga
hatua kuifata switch ya umeme ili nikazime taa,
kitendo cha kupiga hatua ili nikazime taa ndipo
likazuka jambo la ajabu, mlango wa chumba cha
Somoe ndio nilipokomea Sauti za ajabu zikisikika
ndani humo nikiogopa kupiga hatua, kwani kelele na
milio isioeleweka ilisikika ndani mwa Somoe.
ENDELEAAA SASA
Masikio na macho yote yalikuwa malangoni kwa
Somoe, nilipata mshtuko nisijue yeye ni mtu wa
aina gani.
Sijui nilichokuwa nafata mlangoni kwake, ilikuwa ni
sawa na kusikia gari la mafuta limeanguka alafu
nikachote mafuta, ooh Mungu warehemu ndugu zetu
waliotangulia katika ajali ya moto morogoro"
Nilienda hivyo hivyo bila kuogopa.
"Somoeee somoee" Nikipata ujasiri nikaanza kuita
mlangoni kwake, ila nilipoitaa tu sauti zile zilikata
taa ikazima na kuwaka hali ya kuwa sijaizima,
niliogopa ila sikujali "haka ni katoto tu hawezi
kunitisha mimi mtu mzima"nilijisemea maneno ya
kijasiri kisha nikakifata kitasa cha mlango wa
Somoe japo kulikuwa na giza ila nilijua kilipo
nikakishika nikiamini mlango utakuwa wazi looh,
nilifinya kitasa mlango ufunguke wapi
"hahahahahaaha" vilisikika vicheko tu amabvyo
sikujua vinatokea wapi hasira zilinikaa vyema huku
sura nikiikunja na kuhema kwa nguvu.
"Kidawa una nini mbona upo mlangoni kwa
Somoe,"nilistushwa na sauti iliyotoka nyuma
ambayo ilikuwa ya John,niliondoka pale na kumfata
mana tayari nikisimikwa na woga ulionivaa mwili
mzima.
"Nilikuja kuzima taa mana Somoe hakuamka nikajua
mlango wake uko wazi ndo mana nikaja
kuuangalia,"
"Kuwa makini saizi ni usiku usipende kutoka nje
peke yako, tena wewe ni mjamzito mke wangu,"
"Nimekuelewa mume wangu sitatoka tena peke
yangu,"
"Sawa twende chumbani, ila umeniogopesha sana"
John alisema.
"Nisamehee Mume wangu,"nilimjibu kisha tukaingia
ndani, hatukuongea sana tulilala hapo
nikamkumbatia john wangu japo nikizoea nikiwa
kifuani kwa John basi usingizi unanikuta haraka ila
muda huu ulikuwa tofauti zaidi kwani kila nilipojaribu
kuutafuta macho yalinisaliti hata kufumba
hayakutaka kabisa yalibaki vile vile hapo ndio
nikapata nafasi ya kumjadiri Somoe kichwani
Kwangu.
"Somoe ni nani na amefata nini hapa kwangu,"nilijiu
liza tena swali hili lilikuwa kama wimbo usioleweka
kichwani kwangu kwani nikijiuliza kila saa ninapo
mfikiria Somoe, nitamtoaje hapa nyumbani huyu
nikiwaza tena, siku hii sikupata hata lepe la usingizi
mpka inafika asubuhi nilikuwa sijalala hata kidogo,
asubuhi hii John wangu nae alilala zaidi kwa vile
ilikuwa ni mwisho wa juma hakuwa na ratiba ya
kwenda kazini siku hii, hivyo alilala akijua hana kazi,
na mimi nilishuka tu kitandani ili niiaandae chai
nilipotoka nje ya chumba chetu na Mume wangu,
nilimkuta Somoe akifanya usafi wa kudeki.
"Shikamoo dada umeamkaje?" Ndio neno la kwanza
alilonianza nalo pale aliponiona tu, niking'ata meno
kisha nikaachia na kubana meno yangu ya juu
kwenye lips za chini huku ya juu nikiisimamisha
hapo sonyo likanitoka nikipoelekea mezani baada
ya kumoita Somoe, nilikuta kila kitu kipo mezani
yani chai kashapika na ametenga tayari, "we Somoe,
njoo hapa"nilimwita kwajazba.
"Abee, dada," aliitika na kunifata nilipomwita japo
aliitika na kujua ila sikujua hata nimwambie nini
mana kama ni chai ni wajibu wake kupika yeye ni
mdada wa kazi, ikabidi nimtafutie sababu,
"Mbona hii meza chafu umetenga chai bila
hujaifanyia usafi, ndivyo kwenu walivyokufunza
kuwalisha watu sehemu chafu,"Nilimwambia, meza
ilikuwa safi ila nilitafuta cha kuongea tu.
"Samahani dada niliifuta labda sijafuta vuzuri
nisamehe bure,"alisema kisha akachukua kitambaa
na kuanza kufuta tena, niliigia chumbani bado john
amelala, ikabidi nimwamshe nilimtingisha tingisha
mpka akaamka.
"Unalala mpka saa ngapi Mume wangu,"nilionea
kwa mideko.
"Niache nioumzike Kidawa si unajua nimechoka
sana,"aliongea kwa kujinyoosha staili ya uchovu.
"Nataka tuongee John,"Nilisema kwa mkazo ili ajue
namaanisha.
"Tutaongea badae acha nipumzike kidogo Mke
wangu," alionekana kuchoka ikabidi nimwache tu,
nikajiweka zangu kando kwenye kochi la chumbani
kwetu hapo nikawa nimeduwaa nisijue nafanyaje
usingizi ukanipitia pale pale, kitendo cha kulala tu
nilijionaa nikiserereka kwenye shimo refu ambalo
chini linafuka moto mwekundu unaowaka bila
kukoma, sikujua nimetokea wapi ila nikijikuta
nikiteremka kwenye maporomoko hayo nikiufata
moto wa chini nilipiga kelele ila sauti yanyu ilikata
haikuwa ikitoka hata ilikoma na kukwama isitoke
tena, nikiwa nazidi kushuka chini ndipo nikakwama
kwenye moja ya mti ambayo ulikuwa njianii
nikaushikiria kwa mtindo wa kuu kunbatia na miko
yote miwilii, kitendo cha kuushika vile nao
ukanisaliti ulijiachia mti ule kisha kuanza kushuka
moja kwa moja, hapa sasa nikaiona hatma yangu
ikabidi nijaribu kupiga kelele, wakati huu sauti
ilitoka, " haaaaaaaaaaaaaah" sauti ambayo ilikuwa
kali zaidi .
"Wee kidawaaaa kuna nini?"John akimka usingizi
hapo na mimi tayari nilistuka, nikakaa kimya kidogo
kutunga uongo wa kundanganya.
"Nisamehe, nikikuwa nataka nikuamshe we si
umekataa kuamka,"niliongea huku nikipiga koda
vidole vyangu na uso nikiangalia kando mithili ya
mtu mwenye aibu.
"Umenistua sana, nilijua kuna jambo limetokea una
nini Kidawa,?"
"Naomba tuongee john tafadhali,"Nilisema nae
akajileta na kuketi kwenye lile kochi.
"Sawa nakusikiliza mke wangu, Nambie,"alisema na
kunipa usikivu hapo nikamwangalia na kushika
mkono wake na kuubebesha juu ya wangu.
"Mume wangu mi nadhani, Somoe hafai kukaa na
sisi hapa?"
"Kwanini hafai na wakati Anafanya kazi zake vizuri,
sijana sijui juzi nimemsifia kwa utendaji wake kazi
mzuri nawe ukalizika,"
"Mi naona kazi anazofanya zote nazimudu, sasa si
itakuwa anafanya kazi na kulipwa wakati hakuna
kazi nisiyoimudu,"
"Ni wivu au ndio ubahiri, hiyo elf 80 tunayompa
kama mshahara wake wa mwezi ndio ikutoe imani
kwake na kuona anakula pesa zetu nyingi,mbona
pesa tunazo Kidawa ya nini unitese Mke wangu"
"Hapana so hivyo ila..?"
"Ila nini ni wivu au, mimi nakosa kazi nitembee na
msichana wa kazi ambae muda wote ananitumikia
kama kijakazi alafu nitembee nae!"Aliongea John
kidogo akionekana kama amekasilishwa na jambo
lile.
"Hapana John nisamehe, hakuna lolote ninalowaza
baya,"
"Kama hakuna baya, Somoe atakaa hapa mpka
ujifungue na mtoto akue akienda shule ndio hapo
sasa tunaweza mruhusu somoe aondoke, rafiki
yangu alienipa huyu msichana alinipa kwa masharti
pia alinieleza shida nyingi za huko kwao mimi ni
binadamu kama yeye, siwezi kumfanyia ubaya
wakati matatizo yake nayajua, wewe nimke wangu
na nina kusikiliza pia nakupenda ila naomba huyu
msichana abaki hapa, sijaona sababu yako ya
msingi ya kutaka aondoke."john aliongea kwa hasira
japo hakufoka sana, hapo ikabidi nijishushe na
kuanza kuomba msamaha, alinipa sharti kuwa
jambo hili lisijirudie tena, hakulipenda.
"Siku zote tupo karibu mpka tumefunga ndoa bado
unanionea wivu kwa katoto hako kana kipi cha
kunipa kiasi chakukusaliti wewe,"aliongea john kisha
kuamka na kulekea bafuni. Aliniacha peke yangu
pale kwenye kochi huku nikitafakari
NITAMUONDOJE SOMOE KWANGU??
 
SEHEMU YA 42
NA GAOOH
SIMU 0654387935
ILIPOISHIAAA SEHEMU ILIYOPITA
"Siku zote tupo karibu mpka tumefunga ndoa bado
unanionea wivu kwa katoto hako kana kipi cha
kunipa kiasi chakukusaliti wewe,"aliongea john kisha
kuamka na kulekea bafuni. Aliniacha peke yangu
pale kwenye kochi huku nikitafakari
NITAMUONDOAJE SOMOE KWANGU??
ENDELEEEEAA SASA
Niliumia huku nikifikiria kuhusu Somoe, nilitegemea
pengine mume wangu atakiwa upande wangu nae
kumbe si hivyo, alimtetea Somoe nilikosa hata
nguvu za kuamka nilipokuwa nimekaa kitu pekee
nilichoweza ni kupanda juu ya kitanda na kujifunika
shuka sikutaka kuongea tena, hata pale John
alipotoka bafuni hakunizingatia alivaa nguo zake
mwenyewe kisha kutoka chumbani nikabaki peke
yangu nikichezea tumbo langu, nilikumbuka
jumatatu ni siku ya kwenda clinic na leo ni
jumamosi, nilijifunua tu shuka kisha nikachukua
simu yangu iliyokuwa chini ya mto hapo nikaanza
kuichezea Game pekee ndio lilikuwa kifariji changu
Zuma chalenge ndio nililolicheza, kule lenga lenga
kete za kufanana na kuzimaliza kwenye mduara
wake ndio kunipa furaha game hili lilinifariji hapo
nikajikuta nasahau hata yaliotokea kwa wakati huo,
baada ya kucheza niliamka kwenda kuoga kisha
nilipohakikisha nimeoga na kutakata ndipo nikavaa
nguo na kutoka nje, woiiii John.
Nikishangaa kumkuta John amekaa kwenye meza ya
chakula na Somoe wakinywa chai, roho iliniuma
sana.
"John wangu kapewa nini mpaka kumpa kipaumbele
huyu mwanga na kumtetea"Nilijiuliza kisha kukohoa
kidogo kwa sauti kisha nikaelekea meza.
"Si ulikuwa umelala,?"John aliuliza.
"Ndio nililala ila nimekuja siwezi kuacha unakunywa
chai peke yako,"
"Kwani chai si kapika Somoe!"
"Ndio amepika yeye,"John inaonesha bado alikuwa
na hasira anbazo hata sikuamini kama itakuwa
hivyo.
"John mbona unanijibu hivyo inamana hayajaisha tu
Mume wangu, alafu huyu aliekaa hapa inamana kazi
zimeisha mpaka akae juu juu akinywa chai na
wewe,?"
"Mwache mtoto wa wawatu nae binadamu,"Sikue
lewa kipi kinaendelea kwa john wangu yani nahisi
alianza kubadirika kitendo kile ndicho kilifanya hata
hamu ya kula iniishie, chai haikupita kinywani
kwangu nilichoamua ni kwenda sitting room,
kuangalia runinga pengine itanipa faraja.
Nikiwa pale john alikuja baada ya kumaliza kunywa
chai
"Unajua kidawa mke wangu umeanza tabia ya
ubinafsi mpka nakushangaa, hivi umeitoa wapi,"
"John mimi mbinafsi,?"
"Ndio umekuwa mbinafsi kwanini unakuwa na roho
mbaya na huyu binti wawatu asie na hatia,"
"John mimi sijawahi kuwa na hiyo tabia, kuna
mengi huyajui John ila utakuja kujua wakati ambao
tayari utakuwa umecherewa,"
"Hakuna nisichojua ni roho mbaya yako tu kwa huyu
binti wawatu, umesahau nilipokutoa Kidawa," Johj
aliongea kwa ukali nilimwona Somoe akiwa
kaangalia upande huu tulipo akionekana kutusikiliza
hapo ikabidi ninyanyue uso kuntazama, wooiii
nilishangazwa na macho yake kuwa mekundu alafu
nikipokuwa nikigonganisha yake na yangu hapo
nilihisi nguvu kuniisha nikajitoa haraka na kuangalia
kando.
"Inamana huyu ni mchawi na amefata nini?"
Nikijiuliza pekenyangu hapo hata john sikuwa
nikimsikiza.
"Umeona sasa dharau zako naongea na wewe hapa
hunijibu ushapata wa kukudanganya si ndio"
aliposema hivyo nikastuka na kutoka mawazoni.
"John maneno gani unaongea hayo, mimi wa kuwa
na mwanaume mwengine kweli ndio tumefikishana
huko,"
"Niache tena usinishike,"alisma kwa hasira na
kuamka pale tulipokaa akaeleke chumbani
tunakolala.
Somoe umemfanya nini john wangu, niliendelea
kujiuliza peke yangu nikikosa jibu la kujijibu,
Uzalendo ulinishinda kukaa pale nikimwangalia
Somoe kwa wizi kukinishinda nilichoamua ni
kuelekea nje kwenye bembea na kukaa juu yake,
hapo nikaanza kujibembeza mwenyewe japo
nilizoea kubembezwa na john ila leo niko
mwenyewe, hivyo nilitumia miguu nikijivuta nyuma
kwa kutembea kinyume nyume kisha kujiachia hapo
nikaanza kurushwa rushwa, nilifarijika kiasi japo
haikusaidia.
"Penzi nililolihangaikia anakuja kidudu mtu
kuliharibu kirahisi hivi"nikijiwazia. Nilikaa kwa mud
kisha nikashuka kuingia ndani nikikuta wakila
mezani hata sijaitwa, ila afadhali mana sikuwa na
haja ya chakula chao nilichofanya ni kuelekea jikoni
nikajipikia chakula changu ambacho ni ugali nilipiga
ugali na dagaa pamoja na bamia na ngogwe
nilivyovichanganya ndani ya dagaa nilipoivisha
nikaanama ili nile kule kule jikoni kwa kusimama
hakukuwa na kiti niliona bora nile wima, nilikata
tonge la kwanza kisha kuchovya baada ya kuchovya
nilihisi kitu cha tofauti mdomoni ila sikujali kivile
nikajua ni shombo la samaki la kawaida, ikabidi
nikate tonge la pili looh hili ndio lilikuwa baya zaidi
nikipoliweka mdomoni nikahisi vitu vikitembea
mdomoni kwangu looh, nikatema nikichoona
sikuamini funza walikuwa wakitembea, kitendo kile
ndio kilinitapisha nilitapika na kuanguka chini
nikipiga magoti mana tumbo lilikuwa likivuta, Japo
nilikula tonge moja ila nilishangaa kutapika vitu
nyengine ambavyo hata sikuwa nimekula,
nilitegemea kitendo kile kitamstua Mume wangu
John na kuja nilipo lakini haikuwa hivyo, ndio
kwanza walicheka na somoe mezani.
"Johniiii johniii,"ilibidi nimuite nikitegemea atakuja
looh, john huyu sio yule John wangu aliekuwa
akinidekeza kama mtoto huyu ni John wa Somoe
niliumia ikabidi niamke nilipokuwa nimepiga magoti
nikitapika, sikuwa na msaidi nilipata ujasiri na
kuchukua kitaa kilichokuwa juu ya meza ambacho
nilitumia kushikia sufuria ya ugari hicho ndio
nikatumia kukusanya sehemu moja matapishi yale,
kilikuwa ni kitaulo.
Nilipomaliza nilinawa vizuri kisha nilielekea
chumbani kwangu kulala,tumbo lilinivuta zaidi hasa
chini ya kitovu ndio kulichachamaa kuuma,
nilishikilia tumbo langu nikiugulia maumivu yale.
Ndipo nikakumbuka ninazo dawa ndani ilibidi
nizichukue kusitili maumivu ya tumbo langu
nilipomeza vidonge hivi nikajilaza kitandani, japo
inashauliwa mjamzito kutokutumia dawa zozote ila
mimi niliamua kuvunja masharti na kunywa dawa
bila kujali.
Nilianza maisha ya tabu hiyo ni baada ya wiki
kupita, sikumfatilia
Somoe ila John wangu alianza kubadirika taratiibu
hata ule upendo niliouzoea haukuwepo tena, ilifika
wakati hata nikimuomba anipereke clinic kuangalia
maendeleo ya mtoto alikuwa akikataa nabkuniambia
yuko busy ooh john.
"We Kidawa hiyo mimba yako huzai tu, kila siku
unapita pita la litumbo lako."Somoe alisema,
nilitamani kumpiga ila nguvu natoa wapi mimba
ilizidi kukua ikifikisha miezi nane niliumia zaidi
nilihisi mateso mno.
John hakuisha kunisakama huku Somoe nae
akinisakama ni kama vile nilitengwa nyumbani
hapo, mara kadhaa nilikuwa nikipapasa usiku
kitandani kumuangalia John hakuwepo, ilionesha
wazi ameenda kwa Somoe hali hii nilijitahidi
kuinyamazia ila niliona inazidikukua hivyo siku hii
sikutaka kuiacha ndipo na mimi nilipoamka kutaka
kujua kuna nini na wanaenda kufanya nini huko japo
nilijua kiwa wanaenda kulala ila akili himaikunipa
hivyo nilifungua mlango nikatoka chumbani kwangu
Nilipotoka ndipo nikaona jambo la ajabu ambalo
sikulitegemea kabisa, macho hayana panzia hata
kope pia haziwezi yaziba yasione.
Kitendo cha kutoka nilimkuta Somoe Na John
mume wangu wakiwa hawana nguo wote huku john
akiwekwa kati kati amekaa na Somoe amesimama
akimzunguka...
 
SEHEMU YA 43
NA Gaooh
Simu 0654387935
Ilipoishiaaa sehemu iliyopita
Kitendo cha kutoka nilimkuta Somoe Na John
mume wangu wakiwa hawana nguo wote huku john
akiwekwa kati kati amekaa na Somoe amesimama
akimzunguka...
Sasa Endeleaaa..
Niliwatizama kwa tahadhali, ila nilichogundua john
hakuwa na fshamu zozote alionekana kama mtu
anaebuluzwa yani kufanyiwa vitu bila matwa yake,
nilita.ani niende pale nikamuumbue somoe ila
nitawezaje sina nguvu ninazotegemea, huku hali
yangu ni mjamzito tena ujauzito wangu ukiwa
mkubwa zaidi, kitu pekee nikichoona ni sahihi
wakati ule ni kurudi ndani na kumuacha Somoe
akifanya uchawi wake kwa mume wangu, machozi
hayakuacha kuonesha uwepo wake machoni
mwangu yalianza kuserereka kwenye mashavu
yangu, niliporudi ndani usingizi haukunitaka kila
nilipojaribu kufumba macho nilale haikuwa rahisi, ni
mwili tu ndio ulikuwa juu ya kitanda akili na
mawazo vyote havikuwepo hapo, nilijilazimksha
mpaka asubuhi john hakuwa amerudi usiku bali
alikuja asubuhi kwa ajili ya kuoga.
"John umelala wapi mume wangu?"nilimuuliza
nikitegemea atajibu kama nikivyoomuuliza au hata
atanidanganya kama wafanyavyo wanaume wengine
yani ni bora akudanganye kuliko kukwambia ukweli
UTAUMIA.
"Mbona unanichunga hivi kwanj wewe ulitaka nilale
wapi?"
"Hilo sio jibu la swali, nikilokuuliza John umekuwaje
Mume wangu,?"
"Inamana nimebadirika Rangi tuseme nimekuwa
mweusi sana au mwemundu kabisa"
"Ndio majibu ya aina gani haya, na yametoka wapi
John,"
"Ebu niache Kidawa, usinisumbue nyumba yangu na
kila kitu changu hivyo wewe kaa kimya na sitaki
unisumbue,"Jkhn alisema bila haya wala soni, ni
kweli John karogwa na akili yote ametekwa ilibidi
nikae kimya huku nikijifaridhi John wangu
mwanaume wa mfano ameenda likizo hivyo atarudi
siku yoyote, nikipokaa kimya John akaingia kuoga
dakika kadhaa alitoka kisha akajifuta maji na kuvaa
nguo zake , na mimi sikoni eti nikajitega nikisubiri
kubusiwa aniagenloooh! Anibusu wapi john
hakunisemesha alivaa akaondoka.
Baada ya John kuondoka nilikaa muda mchache
kisha nikatoka kwa ajili ya kula nilihisi njaa
ikiniuma.
"Somoe somoe"niliita baada ya kuona kimya, ndani
yani kumepoa baada ya kuita mara kadhaa ni kimya
tu ndio kilinipokea, Niliingia jikoni nikajiandalia
chakula, nilipika uji wa mchele ndio nilikunywa,
kisha nikatoka nje, nikipofika nje nilitazamana na
Somoe alikuwa juu ya bembea nilimtazama kisha
kugeuza na kubadili uwelekeo sikwenda tena kule
kwenye bembea ikabidi izunguke kwenye maua
nikiyatizama, nilifika mpka pale nikaanza kuyashika
shka mauwa yale huku nikijenga tabasamu bandia
usoni mwangu.
"Kidawa kidawa,"Nilisikia sauti ikita jina langu,sauti
ambayo haikuwa ngeni masikioni mwangu alikuwa
ni Somoe.
"Unasemaje?"nilimuuliza.
"Nikajua muda wote unamwagilia hayo mauwa hivi
huoni kama yananyauka kwa kukosa maji
unashindwa kuyamwagia,"alisema.
"Hivi Somoe unajielewa kweli?.... Hivi hii kazi ya
kumwagilia mauwa maji si ni kazi yako,"
"Unaniambia hivyo kama nani,?"alinijibu kwa dharau.
"Mimi ndio mama mwenye nyumba usijisahau we
mtoto hapa ni kwangu,"
"Nyoo kwako ni makaburini mchawi mkubwa wewe,
na kwa taarifa yako John si wako tena andaa
mazingira ukijifungua hiko kibudu chako urudi kule
kijijini kwa wachawi wenzio,"Somoe aliongea
maneno ambayo yalinitia hasira nilijikuta napata
ujasiri ambayo sikujua unapotokea nikimtandika
kibao,kibao cha shavu kitendo kile ndicho
kilimfanya Somoe anioneshe sura yake halisi
alinishika shingo ule ujasiri wote uliondoka nilikuwa
kama niliepigwa ganzi alishikilia shingo yangu kisha
kunivuta juu, na koo langu amelikamata kitendo hiki
kiliniumiza zaidi, mbali na kunikama pia hakuacha
kunitamkia maneno ambayo yalinitisha Zaidi.
"Mimi ndie Somoe, huwezi nipanda kichwani hata
siku moja hakuna nisichokijua kuhusu wewe na
kama utaendelea kunifatilia fatilia nitamwambia
John kila kitu akufukuze na limimba lako
hilo,"alisema kisha akaniachia nikaanguka chini japo
niliangukia makalio ila niliumia zaidi baada kunitupa
chini hapo nilihisi maumivu kwenye tumbo langu
tumbo lilinivuta nikalishikilia huku nikiita msaada,
Somoe hakujali aliondoka pale nilipokuwepo na
kuniacha nikitapa tapa peke yangu.
"Somoe nakuomba unisaidiee nipereke hospital
Somoe nisaidie,"Nilpiga kelele nikiita jina lake
haikusaidia ilikuwa ni sawa na kupiga gitaa sikioni
kwa Mbuzi, Hakunisikia akaingia ndani. Nilibaki
peke yangu pale ikabidi nijisaidie kwavile hata
maandiko yanandikwa "JISAIDIENI NAMI
NITAWASAIDIA" andiko hili ndio lilinipa ujasiri
nilijivuta nikitambaa na makalio huku niking'ata
meno nikiamini ndio nitapunguza maumivu ooooh
ndio yalizidi maumivu niliamua kupambana KIKIKE
hapo nikajivuta mpka mlango wa kuingia ndani,
kutokana nankutembea kwa kukaa kutokana na
maumivu pale mlangoni ilikuwa changamoto
kufungua kitasa kwani vitasa vyote ukitaka kufungua
ni mpaka ukizungushe kutoa lock ndio ufungue sasa
mimi kutokana na kukaa kwangu sikuweza
kujisaidia kwa kufungua kitasa kile nilibaki
mlangoni pale maumivu yakiendelea kuniandama,
Mungu si Athumani mlango ulifunguliawa Somoe
akatoka.
"Unakaa kaa vipi mlango mwanga wewe au ndio
unataka umuue john kabisa ili umiliki mali
zake,"alisema na kunipita hapo nikivumilia maneno
yame huku mguu wangu mmoja wa Kushoto
nilitumia kuzuia mlango usijifunge hapo Somoe
akapita huju akiniachia masonyo ambayo niliona si
kitu kabisa alipopita ndipo nikaingia ndani wakati
nikijiburuza kuingia ndani ndipo nikahisi kitu cha
tofauti kwenye mapaja yangu, nikihisi kuchuruzikiwa
na maji kwenye mapaja yangu siku jali nikajisukuma
mpka ulipo mlango wa chumba nilalacho na John
kufika kule napo haki ilikuwa ni vile vile mlango
umebanwa, sasa huku nikavaa ujasiri nikajitahidi
kusimama bahati nzuri kitasa cha chumbani
hakikuwa kikibwa kama cha pale nje hivyo
nikisimama kidogo tu kukifikia kika funguka
nikaingia chumbani kwa mtindo ule ule sasa wakati
huu niliziona damu na sio kama maji nikiyohisi ndio
yananichuruzika mwanzoni, nilijivuta mpaka
kitandani na kuichukua simu yangu kisha nikaanza
kutafuta jina la john, nilipata na kuipiga kweli iliita
lakini hakuchukua simu yake, nilipiga mara kadhaa
iliishia kuita tu.
Baada ya kupiga zaidi ya mara tano na simu kuita
bila kupokelewa nilijikuta nikiumia zaidi huku
nikijiona nisie na thamani mtu pekee niliemtegemea
kunisaidia Kuja kunichukua alikuwa ni John na yeye
ndio nampigia hapokei simu yangu,nilijikatia tamaa
nikamkabidhi Mungu kilichopo tumboni kwangu
nikiwa nimechanganyikiwa simu ilipata uhai tena na
mlio ukatoka wimbo wa VUMILIA UTANIKUMBUKA
ndio ukaipa uhai simu yangu Jina la MUME WANGU
ndio likasomka kama nilivyo lihifadhi nilitabasamu
kisha nikaipokea.
"We mpunbavu unanisumbua inamana hujui kama
sahizi ni mida ya kazi unapiga piga simu, alaaaahh
kwanini?"Sauti ya John ya kufoka ilitoka ndani ya
simu, sauti ambayo ilinivunja nguvu zaidi ila
nikajipa ujasiri nimwambie.
"Mume wangu.."kabla sijamaliza akinikata kauli
akafoka.
"Nani Mume wako wewe mpunbavu,"Sikukoma
nikiongea hivyo hivyo mbali na maneno aliyokuwa
akinijibu.
"Naomba msaada wako John kaka yangu, tumbo
linaniuma nakiomba uje unipereke hospital
nakufa,"Nilisema haraka haraka kwa sauti ya
huruma, mbali na kusema hivyo lakini haikunzuia
John kuongea tena.
"Unasema nini Mjinga usieelimika wewe usiesoma
kabisa kwahiyo niache kazi zangu nikufate wewe
kukupereka hospital,"Sikukoma niliendelea
kumuomba tena nikimsumbua zaidi.
"Sawa nakuja."alijibu kisha akakata simu sikuelewa
kama hiyo nakuja yake ni ya heri au shari ila nilijipa
imani John atakuja, niliendelea kuugulia maumivu
dakika chache kama nusu saa nilisikia mlio wa honi
ya piki piki nje sikujali kwa vile ndani hatuna
mwenye piki piki sauti ile zilipopita dakika
zisizopungua tano mlango wa chunbani
ukafunguliwa John akaingia nilitabasamu kumuona
nikiamini amenisikiliza Looh, john hakujali
nilivyokuwa nikiumwa pale pale alivua mkanda wake
wa ngozi.
"Nikikuambia sitaki unisumbue nikiwa kazini si
hutaki kunisikiliza, ngoja leo nikufundishe heshima
ya kazi kidogo,"alitamka kwa ghazabu kisha
mkanda ula alianza kunitandika nao hakuchagua
kwa kupiga, mbali na kelele za maumivu nilizokuwa
nikitoa ila hazikuwa kitu masikioni mwa John.
"Mpige mpige mpenzi wangu, hanielewi huyo"sauti
ya Somoe ilisikia nje ya mlango wetu, wakati
akiendelea kunipiga na Mkanda ule hapo ndio
nilihisi kitu kinatoka kati kati ya mapaja yangu
nilijitaniua kikatoka looh sikuamini kilichotoka hata
John aliacha kunipiga wote tukiangalia kitu kile
paka mkubwa mweusi ndio niliemzaa..
 
SEHEMU YA 44
NA GAOOH
SIMU 0654387935
ILIPOISHIA SEHEMU ILIYOPITA.
Mkanda ule hapo ndio nilihisi kitu kinatoka kati kati
ya mapaja yangu nilijitanua kikatoka looh sikuamini
kilichotoka hata John aliacha kunipiga wote
tukiangalia kitu kile paka mkubwa mweusi ndio
niliemzaa..
ENDELEE AA NAYOOO
"Kumbe we nimwanga umenidanganya unamimha
kumbe ndio umebeba huu ushenzi," John alisema
kisha akanipiga tena na mkanda ule mbali na
kunipiga sikuyahisi maumivu yoyote nilipigwa na
butwa nisiamini kilichotoka tumboni kwangu nilihisi
kama ndoto tu, huju nikitamani niamke nikimwona
mwanangu, sikutarajia kama itakuwa vile.
"Unatuzalia wadudu wenzio wanazaa binadamu
wewe unazaa wadudu ndani ya nyumba
hahahaha,"Somoe aliongea huku akicheka nilijiuliza
amejuaje ikiwa yeye alikuwa nje ya chumba chetu
hapo ndipo nikapata jawabu kuwa Somoe ndio
sababu ya haya alijua kabla kilichopo tumboni
kwangu,John aliniacha kisha akatoka chumbani
alipotoka paka yule akapotea pale alipokuwa
hakukuwa na paka tena.
Nilijivuta vuta kama kawaida na kuingia bafuni,
nilijivuta na kuingia kwenye jakuzi hapo nikafungulia
maji kujisafisha damu zilizonitapakaa mwilini.
Sikuwa na usaidizi wowote hivyo nilifanya kila kitu
mwenyewe nikajisafisha baada ya kujisafisha
nilipata nguvu za kusimamajapo bado mfuko wa
uzazi ulikuwa upo nilivaa tu kanga yangu.
Siku zikianza kusogea john akiwa vile vile kipindi
hiki hakulala na mimi kabisa tena alinichukia zaidi
yani hakula chakula changu hata kuongea na mimi
hakutaka mfuko wa uzazi niliukata kwa kutumia
mkasi mkubwa uliokuwa kwenye droo.
"Kwavile umeshindwa kufanya vilivyokuleta hapa
kwangu basj Nakutangaza kuanzia kesho wewe ndio
utakuwa house girl na kazi zote ni juu yako kama
hutaki ondoka urudi nilipokutoa"John aliongea huku
akizungusha Fungo ya gari lake.
"John lakini mimi ni mke wako wa ndoa, kama
mtoto yule ameharibika mbona tunaweza kujaribu
tena tukapata mtoto wewe"
"Sitaki kusikia ujinga huo tena usije niambia nirudie
huo upuuzi,"
"John mume wangu Somoe ndio mchawi
amesababisha haya yote Nakuomba usimwamini..,"
"Weeee weee mwanga nikome, uchawi ufanye wewe
alafu unisingizie mimi John ndio ulivyomfunza huyu
kigagula wako,"alitokea Somoe hapo akanifokea
huku akiongea.
"Nisamehe baby, Nisamehe mimi sijamfunza ni
kukosa kwake heshima tu"John alisema huku
akiamka na kumkumbatia kitendo ambacho Somoe
alimsukuma "Sitaki niache, huwezi kaa na kuona
nadharilishwa huku ukimwacha,"somoe alisema.
"Nisamehe Somoe wangu" ukweli kuhusu somoe
kipindi anakuja alionekana mdogo mdogo pengine
hata ukitajiwa anamiaka 15 huwezi, kataa ila muda
mchache alipokaa kwetu amenenepa na kunawili na
kupendeza kiasi kwamba amekuwa mama sasa
anasauti ya kufoka na kunifokea ooohhh.
John aliposema vile alinifata pale nilipokaa kochini
akanivuta masikio na kuanza kunipiga makofi huku
akiniambia nikome, niliumia sana nilitamani
ningekuwa na uwezo wangu nipambane na somoe
ila ndio sina, sikuwa na kitu cha kufanya kulia na
kuumia ndio malipo yangu, NANI WA KUNIONEA
HURUMA najua sikustahili haya, nilistahili kuishi
kwa furaha ili nisahau yale yote niliyopitia nyuma ila
laah bado nipo kifungoni nahisi nimezaliwa ili nipate
mateso, baada ya kunipiga alimuaga Somoe na
kuondoka nikiwa pale pale Somoe aliingia ndani
kisha kutoka akiwa na lundo la nguo
alizozikumbata.
"Nguo hizi hapa uzifue na zitakate zote, na
zisipotakata uzirudie zote nitakagua,"alisema na
kunirushia kichwani.
"Ole wako usizifue nitamwambia john akufukuze
mbna wafanya kazi wapo wengi kijijini wanatafuta
kazi,"alisema hapo niliposikia John ikanibidi
nikubali kwa vile nilijua nikikataa na John
akaambiwa basi anaweza nifukuza kabisa nyumbani
hapa.
Nilizibeba kinyonge kisha nikatoka nazo nje kwa
ajili ya kufua nikizifua kivivu vivu ila nilijihakikisha
zimetakata, nikazianika nguo zote, juu ya kamba
nilibeba mapovu niliyoanikia nguo ili nikayamwage
nje ya geti ndio alipotokea Somoe.
"Njoo hapa Kidawa." Aliposema nikasimama hapo
nilikuwa nikiukaribia mlango wa nje yani geti.
"Hivi ndo umefua hivi, inamana ndio nguo zako
unavyofua haraka haraka , sasa nataka uzirudie tena
na usipotakasha utarudia,"alisema kisha bila aibu
akazivuta nguo zote huku akizitupa chini kuzitoa
kwenye kamba, iliniumiza sana hali ile ikabidi hata
yale maji nirudi nayo ili nizifue tena alikuwa
anaondoka niliporud mpka pale kwenye nguo na
kuanza kuziokota kabla sijatia kwenye maji yale
alinijia juu kisha akachukua beseni lenye maji yale
Hapo bila woga akanimwagie.
"Ndio unavyofua hivi maji machafu ndio unataka
ufulie nguo zangu na za Mume wangu koma mbwa
wewe!"
Alisema kisha akaondoka niliinama nikipiga makoti.
"Mungu wangu, kama nimekukosea nisamehe
maumivu ninayo yapitia yananitosha Mungu wangu,
Najua hakuna binadamu wako uliemuumba ili
ateseke, umetuumba tukuabudu, pia najua kila
anaekosea akikiri mbona husamehewa kwanini
kwangu ni tofauti au sikupaswa kuzaliwa
kuzaliwa."niliongea kwa uchungu na huzuni kubwa
kisha nikizifua tena zile nguo wakati huu nikichukua
maji mengine kabisa nilipomaliza nikazianika
nilipoingia ndani nilimkuta anakula mezani vilikuwa
ni viazi vya rosti nilitegemea na mimi atakuwa
ameniwekea looh, nilipofika hakunisemea alikaa
kimya yeye na sahani yake nikajua ameniwekea
jikoni nilielekea jikoni hima hima looh sufuria
niliiona viazi sasa looh, vilibaki ila alivitia maji
pamoja na maganda ya nyanya na vitungu, nilichoka
hata kupika sikuweza nikaingia ndani kwenda kulala.
Vinalalika sasa, ilibidi nitoke nje kwenye bembea
kisha nikajikarisha juj yake huku nikisikiliza miziki
kwenye simu yangu na kuifatisha.
"Unakaa hapo unaukubwa gani mpka ujikalishe hapo
mwanga mkubwa toka," Ilikuwa kama hila
aliponikuta juu ya bembea alinifukuza niliishindwa
hata kuongea nitasema nini, kwa upole nikaondoka
pale akakaa yeye.
"NITAMTOAJE SOMOE HAPA NYUMBANI"Niliwaza
kisha nikatabasamu, Nikipata wazo, wazo ambalo
nikipanga kulitekeleza "NIMUUUWE"Niliwaza kwa
sauti kubwa zaidi kisha nikatabasamu tena, kitu
pekee ambacho ningefanya ni kumuuwa Somoe
ndio nitamuondosha nyumbani hapa, bila ya hivyo
atanitumikisha na kunitesa wakati nyumba ni yangu
na Mume wangu John, Nilikuwa chini ya mnazi
nikiyawaza haya mpka jioni ilipoingia na mimi
nikaingia ndani moja kwa moja chumbani kwangu
njaa ilinisumbua ila niliacha iwe hivyo, sikuwa na
jinsi kupika sikutaka.
Baada ya saa kadhaa John alirejea nikiwa ndani
nikimsikia akiongea na Somoe, sikuelewa
walichokuwa wakiongea ila dakika chache John
aliingia chumbani kwangu.
"We mshenzi kwanini hujafanya kazi, inamana kazi
yako ni kujaza choo tu hapa ndani"alifoka kisha
akanivuta na kunitoa nje kwa vile nilikuwa na njaa
basi nikipepesuka huku na huko.
"Umepika chakula umekula mwenyewe mpnzi wangu
hukumpa na umekitia maji,unajua pesa nazipata
wapi mpka uchezee chakula,"Somoe alinisingizia
kesi ambayo hata sijaifanya john kwavile alikuwa
akimsikiliza hivyo aliamua kuniadhibu na kunipiga,
alinipiga na kuniambia nikapike tena akimtuma
Somoe anisimamie nisije weka kitu kibaya kwenye
chakula, kusimamiwa na Somoe ilikuwa ni kama
kufundishwa alinifundisha kila kitu huku akinikosoa
mara kwa mara nilipika kikaiva bado aliniachia
nibebe nipereke mezani, Njaa na Maumivu viliniuma
kwa wakati mmoja.
walikaa mezani kisha Somoe akaamuru mimi
nikakae mbali nao, eti nikalie jikoni nilitii
nikaondoka, walipomaliza kula wakaniita
niwanawishe looh, nilikubali sikuwa na jinsi nilifanya
kwa matakwa yao, Hakuna alieshukuru walipomaliza
wakumbatiana kisha kuingia chumbani John akiwa
nyuma kwa Somoe amemkumbatia, Iliniuma sana,
Hapo nikawaza kutimiza mpango wangu siku inayo.
Nikiwa juu ya kitanda sikuwa nimelala, nilienda
jikoni kimya kimya na kuchukua kisu,Nilikiandaa
kisu kile ambacho ndio nilipanga kumchoma
Somoe, Nilichagua kile chenye Ncha kali.
 
SEHEMU YA 44
NA GAOOH
SIMU 0654387935
ILIPOISHIA SEHEMU ILIYOPITA.
Mkanda ule hapo ndio nilihisi kitu kinatoka kati kati
ya mapaja yangu nilijitanua kikatoka looh sikuamini
kilichotoka hata John aliacha kunipiga wote
tukiangalia kitu kile paka mkubwa mweusi ndio
niliemzaa..
ENDELEE AA NAYOOO
"Kumbe we nimwanga umenidanganya unamimha
kumbe ndio umebeba huu ushenzi," John alisema
kisha akanipiga tena na mkanda ule mbali na
kunipiga sikuyahisi maumivu yoyote nilipigwa na
butwa nisiamini kilichotoka tumboni kwangu nilihisi
kama ndoto tu, huju nikitamani niamke nikimwona
mwanangu, sikutarajia kama itakuwa vile.
"Unatuzalia wadudu wenzio wanazaa binadamu
wewe unazaa wadudu ndani ya nyumba
hahahaha,"Somoe aliongea huku akicheka nilijiuliza
amejuaje ikiwa yeye alikuwa nje ya chumba chetu
hapo ndipo nikapata jawabu kuwa Somoe ndio
sababu ya haya alijua kabla kilichopo tumboni
kwangu,John aliniacha kisha akatoka chumbani
alipotoka paka yule akapotea pale alipokuwa
hakukuwa na paka tena.
Nilijivuta vuta kama kawaida na kuingia bafuni,
nilijivuta na kuingia kwenye jakuzi hapo nikafungulia
maji kujisafisha damu zilizonitapakaa mwilini.
Sikuwa na usaidizi wowote hivyo nilifanya kila kitu
mwenyewe nikajisafisha baada ya kujisafisha
nilipata nguvu za kusimamajapo bado mfuko wa
uzazi ulikuwa upo nilivaa tu kanga yangu.
Siku zikianza kusogea john akiwa vile vile kipindi
hiki hakulala na mimi kabisa tena alinichukia zaidi
yani hakula chakula changu hata kuongea na mimi
hakutaka mfuko wa uzazi niliukata kwa kutumia
mkasi mkubwa uliokuwa kwenye droo.
"Kwavile umeshindwa kufanya vilivyokuleta hapa
kwangu basj Nakutangaza kuanzia kesho wewe ndio
utakuwa house girl na kazi zote ni juu yako kama
hutaki ondoka urudi nilipokutoa"John aliongea huku
akizungusha Fungo ya gari lake.
"John lakini mimi ni mke wako wa ndoa, kama
mtoto yule ameharibika mbona tunaweza kujaribu
tena tukapata mtoto wewe"
"Sitaki kusikia ujinga huo tena usije niambia nirudie
huo upuuzi,"
"John mume wangu Somoe ndio mchawi
amesababisha haya yote Nakuomba usimwamini..,"
"Weeee weee mwanga nikome, uchawi ufanye wewe
alafu unisingizie mimi John ndio ulivyomfunza huyu
kigagula wako,"alitokea Somoe hapo akanifokea
huku akiongea.
"Nisamehe baby, Nisamehe mimi sijamfunza ni
kukosa kwake heshima tu"John alisema huku
akiamka na kumkumbatia kitendo ambacho Somoe
alimsukuma "Sitaki niache, huwezi kaa na kuona
nadharilishwa huku ukimwacha,"somoe alisema.
"Nisamehe Somoe wangu" ukweli kuhusu somoe
kipindi anakuja alionekana mdogo mdogo pengine
hata ukitajiwa anamiaka 15 huwezi, kataa ila muda
mchache alipokaa kwetu amenenepa na kunawili na
kupendeza kiasi kwamba amekuwa mama sasa
anasauti ya kufoka na kunifokea ooohhh.
John aliposema vile alinifata pale nilipokaa kochini
akanivuta masikio na kuanza kunipiga makofi huku
akiniambia nikome, niliumia sana nilitamani
ningekuwa na uwezo wangu nipambane na somoe
ila ndio sina, sikuwa na kitu cha kufanya kulia na
kuumia ndio malipo yangu, NANI WA KUNIONEA
HURUMA najua sikustahili haya, nilistahili kuishi
kwa furaha ili nisahau yale yote niliyopitia nyuma ila
laah bado nipo kifungoni nahisi nimezaliwa ili nipate
mateso, baada ya kunipiga alimuaga Somoe na
kuondoka nikiwa pale pale Somoe aliingia ndani
kisha kutoka akiwa na lundo la nguo
alizozikumbata.
"Nguo hizi hapa uzifue na zitakate zote, na
zisipotakata uzirudie zote nitakagua,"alisema na
kunirushia kichwani.
"Ole wako usizifue nitamwambia john akufukuze
mbna wafanya kazi wapo wengi kijijini wanatafuta
kazi,"alisema hapo niliposikia John ikanibidi
nikubali kwa vile nilijua nikikataa na John
akaambiwa basi anaweza nifukuza kabisa nyumbani
hapa.
Nilizibeba kinyonge kisha nikatoka nazo nje kwa
ajili ya kufua nikizifua kivivu vivu ila nilijihakikisha
zimetakata, nikazianika nguo zote, juu ya kamba
nilibeba mapovu niliyoanikia nguo ili nikayamwage
nje ya geti ndio alipotokea Somoe.
"Njoo hapa Kidawa." Aliposema nikasimama hapo
nilikuwa nikiukaribia mlango wa nje yani geti.
"Hivi ndo umefua hivi, inamana ndio nguo zako
unavyofua haraka haraka , sasa nataka uzirudie tena
na usipotakasha utarudia,"alisema kisha bila aibu
akazivuta nguo zote huku akizitupa chini kuzitoa
kwenye kamba, iliniumiza sana hali ile ikabidi hata
yale maji nirudi nayo ili nizifue tena alikuwa
anaondoka niliporud mpka pale kwenye nguo na
kuanza kuziokota kabla sijatia kwenye maji yale
alinijia juu kisha akachukua beseni lenye maji yale
Hapo bila woga akanimwagie.
"Ndio unavyofua hivi maji machafu ndio unataka
ufulie nguo zangu na za Mume wangu koma mbwa
wewe!"
Alisema kisha akaondoka niliinama nikipiga makoti.
"Mungu wangu, kama nimekukosea nisamehe
maumivu ninayo yapitia yananitosha Mungu wangu,
Najua hakuna binadamu wako uliemuumba ili
ateseke, umetuumba tukuabudu, pia najua kila
anaekosea akikiri mbona husamehewa kwanini
kwangu ni tofauti au sikupaswa kuzaliwa
kuzaliwa."niliongea kwa uchungu na huzuni kubwa
kisha nikizifua tena zile nguo wakati huu nikichukua
maji mengine kabisa nilipomaliza nikazianika
nilipoingia ndani nilimkuta anakula mezani vilikuwa
ni viazi vya rosti nilitegemea na mimi atakuwa
ameniwekea looh, nilipofika hakunisemea alikaa
kimya yeye na sahani yake nikajua ameniwekea
jikoni nilielekea jikoni hima hima looh sufuria
niliiona viazi sasa looh, vilibaki ila alivitia maji
pamoja na maganda ya nyanya na vitungu, nilichoka
hata kupika sikuweza nikaingia ndani kwenda kulala.
Vinalalika sasa, ilibidi nitoke nje kwenye bembea
kisha nikajikarisha juj yake huku nikisikiliza miziki
kwenye simu yangu na kuifatisha.
"Unakaa hapo unaukubwa gani mpka ujikalishe hapo
mwanga mkubwa toka," Ilikuwa kama hila
aliponikuta juu ya bembea alinifukuza niliishindwa
hata kuongea nitasema nini, kwa upole nikaondoka
pale akakaa yeye.
"NITAMTOAJE SOMOE HAPA NYUMBANI"Niliwaza
kisha nikatabasamu, Nikipata wazo, wazo ambalo
nikipanga kulitekeleza "NIMUUUWE"Niliwaza kwa
sauti kubwa zaidi kisha nikatabasamu tena, kitu
pekee ambacho ningefanya ni kumuuwa Somoe
ndio nitamuondosha nyumbani hapa, bila ya hivyo
atanitumikisha na kunitesa wakati nyumba ni yangu
na Mume wangu John, Nilikuwa chini ya mnazi
nikiyawaza haya mpka jioni ilipoingia na mimi
nikaingia ndani moja kwa moja chumbani kwangu
njaa ilinisumbua ila niliacha iwe hivyo, sikuwa na
jinsi kupika sikutaka.
Baada ya saa kadhaa John alirejea nikiwa ndani
nikimsikia akiongea na Somoe, sikuelewa
walichokuwa wakiongea ila dakika chache John
aliingia chumbani kwangu.
"We mshenzi kwanini hujafanya kazi, inamana kazi
yako ni kujaza choo tu hapa ndani"alifoka kisha
akanivuta na kunitoa nje kwa vile nilikuwa na njaa
basi nikipepesuka huku na huko.
"Umepika chakula umekula mwenyewe mpnzi wangu
hukumpa na umekitia maji,unajua pesa nazipata
wapi mpka uchezee chakula,"Somoe alinisingizia
kesi ambayo hata sijaifanya john kwavile alikuwa
akimsikiliza hivyo aliamua kuniadhibu na kunipiga,
alinipiga na kuniambia nikapike tena akimtuma
Somoe anisimamie nisije weka kitu kibaya kwenye
chakula, kusimamiwa na Somoe ilikuwa ni kama
kufundishwa alinifundisha kila kitu huku akinikosoa
mara kwa mara nilipika kikaiva bado aliniachia
nibebe nipereke mezani, Njaa na Maumivu viliniuma
kwa wakati mmoja.
walikaa mezani kisha Somoe akaamuru mimi
nikakae mbali nao, eti nikalie jikoni nilitii
nikaondoka, walipomaliza kula wakaniita
niwanawishe looh, nilikubali sikuwa na jinsi nilifanya
kwa matakwa yao, Hakuna alieshukuru walipomaliza
wakumbatiana kisha kuingia chumbani John akiwa
nyuma kwa Somoe amemkumbatia, Iliniuma sana,
Hapo nikawaza kutimiza mpango wangu siku inayo.
Nikiwa juu ya kitanda sikuwa nimelala, nilienda
jikoni kimya kimya na kuchukua kisu,Nilikiandaa
kisu kile ambacho ndio nilipanga kumchoma
Somoe, Nilichagua kile chenye Ncha kali.
 
SEHEMU YA 45
NA GAOOH
SIMU 0654387935
TULIPOISHIA SEHEMU ILIYOPITA
Nikiwa juu ya kitanda sikuwa nimelala, nilienda
jikoni kimya kimya na kuchukua kisu,Nilikiandaa
kisu kile ambacho ndio nilipanga kumchoma
Somoe, Nilichagua kile chenye Ncha kali..
SASA ENDELEAAA
Nilikitazama kisu hiki mara mbili mbili nikiwa
kitandani ndicho nilichopanga kumchoma nacho
Somoe ikiwa kama njia nyepesi niliyofikilia kuwa
ndio nitamuondoa nyumbani hapo na kutuachia
uhuru mimi na Mume wangu Turejee kama zamani,
Mbali na kuwa usiku wa deni haukawi kucha ila
nilishangaa usiku huu ulikuwa mrefu zaidi hata
nilipotamani kulala nikifumba macho ilikuwa kazi
bure nilifumba na kufumbua muda huo huo, Ni
kwamba macho yalinisaliti hayakutaka pumziko
hivyo ikanibidi nikae macho wakati niko macho
nilikumbuka kitu, kitu ambacho wachawi tulifunzwa
jinsi ya kujilinda iwapo atatokea mchawi ambaye ni
adui yako ukitaka kupambana nae kwa kutumia
siraha yoyote tofauti na upanga wa kichawi,
nilikumbuka kitu ambacho alinifundisha bibi, bibi
nilieishi nae tangu utotoni mpka nakuwa na kufika
muda akachukuliwa na wachawi kama sadaka.
"Kidawa kuna vitu wachawi wengi hawakijui, ndio
hawakijui kama binadamu anaweza mpa jeraha japo
hata muua kwa mara moja ila atampa jeraha
ambalo litahatarisha maisha yake,"
"Bibi si huwa wachawi wanakuwa na uwezo na
nguvu tofauti na binadamu sasa iweje tena
binadamu aweze kumdhuru mchawi kiasi hiko,"
"Usemayo ni kweli ila nikujuze mjukuu wangu,sisi
wachawi tunamtegemea Mungu tunamuomba hata
tukifanya kazi zetu tunanuwia kwa jina la Mungu,
hivyo hata binadamu anaweza kumuomba mungu na
akatuangamiza hivyo hivyo, hasa mchawi akilala
kisha akatoa mtu mwenye nia mbaya nae akatumia
kisu kumchoma kwenye mbavu zake basi hilo ni
jeraha ambalo linaweza kuchukua muda kupona pia
akifanya mchezo anaweza kufa kabisa, tizama hata
sisi tunapojibadirisha na kuwa paka kisha binadamu
wakitujeruhi huoni tunavyoumia hivyo kuwa makini
Kidawa"Niliyakumbuka vyema maneno ya bibi, hasa
nikikumbuka alisema mchawi akiwa amelala ndio
unaweza kumuangamiza kwa urahisi nilitoka
chumbani na kisu changu huku nikiwa nimevaa nguo
ya kulalia tu, nilifika mpaka nje ya chumba cha
Somoe, sauti za mahaba na kelele zilinipokea
ilionesha wazi John na Somoe wakifanya mapnzi
Muda huo, nikieikia kelele za kinafki za Somoe
Nilipata hasira zaidi nikatamani kuingia nikawauwe
wote ila nilifikilia uchawi wa Somoe anaweza
niangamiza kabla sijatimiza lengo langu, hali hiyo
ilinirudisha chumbani kwangu miko yangu nikiweka
nyuma na kisu nikikishika huko huko, nilipoingia na
kufunga mlango nikajitupa kitandani wakati huu
usingizi ulinichukua na kunisafirisha mbali zaidi.
Sauti za ndege na mwangaza ulipenya ndani
kwangu, huku sauti ya kugongwa malango nje
ilisikika hapo niliamka, "ooohh kumbe sikuwa
nimefunga madirisha"nilijishangaa ila sikujali sana
nikawasha simu yangu kuipa uhai tena haikuwa na
ujumbe wala simu zisizo fanikiwa (Missed Call)
niliposhuka kitandani nilikiokota kisu changu
kilichokokuwa chini ya kitanda karibu na sehemu ya
kushukia nipokiokota nikakificha chini ya mto kisha
nikafungua mlango.
"Umekuwa boss sio, we ndo Boss Lady unalala
mpaka sahizi mwanga mkubwa wewe,"Yalikuwa
maneno ya Somoe alishindwa hata kunisalimu ila
alikurupukia kunitamkia hivyo.
"Somoe, waungwana hatuishi hivyo tusalimiane
kwanza hata kama unanitendea mabaya ila hupaswi
kunifanya hivyo,"Niliongea kiupole nikitaka amani
kwake.
"Sitaki kusikia ngonjera zako, nakusalimia kwa lipi
toka ufanye kazi zako wewe ni mtumwa tu na
utabaki hivyo wewe ndio mfanya kazi wa hapa
ndani," Aliongea kisha kuniamuru nideki ndani
sikuwa mbishi nilifanya vile atakavyo nilichujua maji
na kutia sabuni kisha nikaanza kudeki ndani
hapo,Nilikuwa nikifanya kazi huku nikimsomea
ramani Somoe, Siku hii nilijifanya mwema kiasi
chake nilifanya kazi zangu kwa moyo wote na
kupika kabisa, "leo imekuwa siku nzuri hatuja
kwazana kabisa kumbe unaweza kuwa mtu mzuri
wakati mwengine,"alisema Somoe, nilitabasamu
asijue kipi namuwazia kumfanyia.
"Wakati mwengine binadamu tunatakiwa tuishi kwa
upendo na amani haijalishi ni ubaya kiasi gani
unefanyiwa ila unapaswa kuyashinda yote na
kujaribu kuwa mwema,"
"Kumbe unabusara hivi Kidawa,basi kuanzia leo
kama utakuwa mwema hivi sitarumbana na wewe"
"Ndio ninavyotaka tuishi kwa furaha"nilimwambia.
"Unajua Kidawa mdogo wangu.."nilimkatisha kabla
hajamaliza sentensi yake.
"Umesemaje?, mbona kama unaanza kunichokoza"
nilishangaa aliponiita mdogo wake hapo nikapata na
neno la kusema.
"Oooh, pole ila Kidawa unajua kuwa mimi ni
mkubwa kwako yani usinione hivi nina miaka mingi
ni kamwili kangu tu kalivyo huoni Neema ya hapa
imefanya nivutike na kuwa hivi mpka john kunitaka,
Mimi mwenzio ni Mzaliwa wa huko
sumbawanga,"alikuwa akinielezea Somoe.
"Ila tuishie hapo usinijue zaidi,"
"Ni sawa ni vizuri pia kujua uhalisia wako mwanzoni
nilikuchukulia kama mtoto tena mdogo kumbe ni
tofauti kabisa,"sikutaka kuongea mengi niliongea
machache tu nae hakunieleza undani wake.
"Unatakiwa uniamkie sasa mimi ni dada yako,pia
nataka kuishi vizuri na wewe najua kila kitu kuhusu
na hata uhalisia wa maisha yako."
"Aloooh, kumbe unanifahamu ni vizuri
dada,"nilimwambia hapo tukaanza sasa kuelewani
Nikijua ninachotaka, ndio mana nikajitumikisha
kwake nikifanya kila kazi ili mradi kumpumbaza.
Somoe hakunijua aliona nimesahau mabaya yote
aliyonifanyia, hata pale jioni John aliporudi hakuacha
kunisifia.
"John Kidawa amekuwa sasa,naona ameanza
kuelewa majukumu yake, hatusumbuani
tena,"Somoe alisema wakati huo nikiwa jikoni.
"Ndio vizuri hivyo, japo tumemkatili ila anatakiwa
kujua Mapenzi huisha,Upendo hupungua, mwanzoni
nilimpenda tena sana ila nashangaa tangu umekuja
hapa na kuanza kukujua,nimekupenda zaidi
wewe,"John nae alisema roho iliniuma sana,
Nikijiapiza kulimaliza hizi Siwezi fanyiwa dharau
huku naona.
"Kumbe nawe wajua Mume wangu, mimi pia
nakupenda sana sana, nipo tayari kufanya lolote kwa
ajili yako."
"Nafurahi kusikia hivyo, Nitakuoa"John alisema hapo
moyo ulinipasuka zaidi nilichungulia ili niwaone
nilikuwa kwa nyuma Somoe alikuwa akichezea
kidevu cha John kilichojaa ndevu ambazo ndio
zilikuwa furaha yangu hapo mwanzoni, maneno ya
John kutamka kuwa atamuoa Somoe ndio
yalipandisha hasira zangu zilizokuwa zimelala
nilijikuta nikichukua flampeni nia na dhumuni
nikampige nayo Somoe ya kichwa looh,! Vinaendeka
sasa nilijikuta nikiuhisi uzito wa miguu yangu, Woga
na hofu viliniingia kwa pamoja nikashindwa
kunyanyua mguu nikajikuta flampeni ikiniteleza
mikononi nikiwa mlangoni.
"We Kidawa vipi, kuna nini?" Waliongea kwa pamoja
baada ya kelele za flampeni niliyoiangusha huku
wakiniangalia, nilijitetea nijuavyo.
"Kuwa makini umetushtua sana,Endelea na kazi
zako,"John alisema ndipo hasira zikikomoa hapo
nikarudi jikoni hata kula sikuwa na hamu tena
niliweka chakula pembeni, kisha nilikaa juu ya meza
ya jiko huku nikishikilia shavu langu. Nilipitiwa na
usingizi nikiwa pale pale mpka nikastuka ndipo
ndipo nikashuka pale juu na kutoka jikoni, nilipotoka
hawakuwepo pale hivyo nilitoa vyombo na kusafisha
meza kisha nikaingia chumbani kwangu, ndipo
nikakikumbuka kisu changu nilikitoa jini ya mto
nikakishika kwa hasira nilijikata kidole na
kusababisha damu kunitoka halikuwa jeraha kubwa
hivyo damu zile niliishia kuzinyonya pale kidoleni
kwangu.
Siku hii ndipo nikakumbuka Umuhimu wa kujali
muda nikiamua kutegesha Alam nikiweka saa 11.40
ndio muda nikiotega kwa ajili ya kuamka, kisha
nikalala kimya kirefu kilipita.
Hatimae Alam haikunisaliti iliniamsha Muda ule ule
niliouweka haoo nilipoamka tu nikakishika kisu
changu na kushuka kitandani hapo nikauendea
mlango wangu taratiibu nikaufungua. Kishanikapiga
macho sebuleni pale, hakukua na mtu wala dalili ya
kuwa na mtu nilienda mpka nje ya chumba alalacho
Somoe na John nilipofika mlangoni Kulikuwa kimya
ndani huko Nikajitoa fahamu kufua kitasa
nikitegemea mlango ufunguke loh haikuwa hivyo
mlango ulifungwa kwa ndani, hapo nikikosa cha
kufanya nilirudi ndani kwangu huku nikitega sikio
kusikiliza kinachoendelea nje, zilipita saa kadhaa
nilisikia John akiagana kwa mabusu na Somoe
kisha john akatoka ndipo na mimi nilikaa makini
dakika 15 zikitosha kusubiri john alipotoka kisha
nikaafungua mlango wangu taratiibu nikafanya kama
mwanzo kuchungulia nje pale sebureni kama Somoe
yupo hakuwepo ndipo nikanyata na kufikia mlango
wa chumba chake, nilishika kitasa wakati huu
kilinitii nikakizungusha taratibu ndipo mlango bila
ajizi ukafunguza na kunipa fursa ya kuingiza kichwa
nikichungulia kama mwizi anaetegemea kuiba
sehemu Mungu Mkubwa Somoe alikuwa amelala
Nilijipa Ushindi hapo hapo nikiamini nitamaliza
shida inayosumbua ngumbani kwangu, Niliurudishia
mlango taratiibu nisimtoe usingizi hapo nikakikaza
kisu mkononi kwangu sawa sawa na kumsogelea
somoe kitandani hapo nikavuta mkono huku
niking'ata Meno na kukishusha mwilini kwa Somoe
tena kwenye mbavu.
"Aiiiiiiiiihhhh" Ukelele wa maumivu ulimtoka....
 
SEHEMU YA 46
NA GAOOH
SIMU 0654387935
ILIPOISHIA SEHEMU ILIYOPITA
kumsogelea somoe kitandani hapo nikavuta mkono
huku niking'ata Meno na kukishusha mwilini kwa
Somoe tena kwenye mbavu.
"Aiiiiiiiiihhhh" Ukelele wa maumivu ulimtoka....
SHUKA NAYO SASA
Kelele iliyomtoka ndio ikanipa Nguvu na ari ya
kumchoma tena nilikivuta kisu mara ya pili
nikakichoma tena pale, wanasema ili kumuangamiza
adui yako hakikisha ukitaka kumdhuru fanya ule
wakati ambao hajajiandaa ndivyo nilivyomfanyia
Somoe visu viwili nilivyomchoma alimka alipokuwa
kalala hapo akipushia na upepo ambao haukuwa na
nguvu sana.
"Kidawa ndio umeamua kunifanyia hivi,
aaahhhh.......aaaahhhh Utajuta,"alisema huku
akiugulia maumivu nilikuwa nimekishika kisu huku
nimepumbazika nisielewe cha kujibu japo nilikuwa
muuaji mzuri ila wakati huu ni woga ndio umeniihia
na hofu, nilikitupa kisu chini cha kushangaza
hakikuwa na damu wala pale kitandani hapakuwa na
damu zozote.
"Utajuta Kidawa huu sio mwisho, Nilitumwa
nikuangamize ila niliamua nikutese na si kukuua ila
wewe ndio umeamua kunifanyia hivi Utajuta."alisem
a hapo akavuta mkono wake kama mtu
anaekusanya maji ila alipojaribu kutaka kufanya
kama ananirushia alishindwa maumivu yalimzidi.
Kitendo hiko ndio kilifanya Somoe apotee mbele ya
macho yangu alipotea kama moshi huku akiniacha
na maneno ya vitisho eti Nitajuta, sikuyatilia manani
nikiyaona kama maneno ya mkosaji yasio na faidia,
ni kama dua la kuku kamwe haliwezi kumpata
mwewe.
Niliokota kisu changu kilichokuwa kikavu
kisichokuwa hata na tone la damu, hata yale
mashuka yaliokuwa yamelaliwa na Somoe akitumia
kujifunika hayakuwa na damu zaidi ya tundu la kisu.
Niliamua kuyakusanya yote kisha nikatoka nayo nje
huko sikuyakawiza niliyafua kisha kuanika,
nilipokamilisha nilirudi ndani nikachukua kila
kilichomilikiwa na Somoe kuanzia nguo mpaka
vipodozi vyake nikakusanya sehemu moja kwa
kuvifunga bundu kwenye kanga ambayo pia alikuwa
akiivaa, nikatoka nje nikilikumbata kifuani kisha
nililitupa chini na kuingia ndani huko nikaelekea
jikoni na kukitwaa kidumu cha mafuta ya taa
nikachukua na kibiriti juu ya kabati nikatoka nje
hapo nikazimwagia mafuta nguo zile na kuziwasha
moto zikawaka.
Sikutaka kuondoka nilikaa nikishuhudia hatima ya
Somoe, sikujali milipuko ya Chupa za pafyumu
niliivumilia hata zilipopasuka na kutoa sauti sikujal
nilipohakikisha yamebaki majivu ndipo nikalifata
jembe lililokuwa pembeni ya pale chini ya tanki la
maji, nilipolitwaa nikasogelea mpka pale kwenye
yale majivu, niliyafukia kwa kuchimba pale pale
kisha nikakanyaga udongo uliokuwa juu yake alafu
nikamwagia maji kwa juu SOMOE kwisha.
Niliingia ndani kwa furaha nikafungulia mziki kwa
sauti kubwa hapo nikaamua nifanye usafi nyumba
nzima, nilianza kudeki kuanzia chumbani kisha
kutoka mpaka sebuleni, nilipomaliza sikupumzika
sauti ya mziki ilinipa furaha, wimbo wa baba lao
ndio ulicheza kwenye sabufa zile kuu kuu "Mzuka
ukipanda na hili shati navuaa...... Acha uongooo,...
Jamanii navuaaa ...... Acha uongoooo.... Ooohh
kuna basataa.."kipande hiko nilinikuta nikikifatisha
hapo nikaliendelea Friji na kutoa samaki aina ya
sato ambao jihn mara nyingi huwa analeta akitoka
nao bandarini anakofanyia kazi, nikalifata jiko kisha
nikaanda mapishi kila kitu kilikuwa ndani kuanzia
vutunguu,nyanya, karoti hoho na kila kitu kihusicho
mapishi, nilianza kuandaa kisha kupika nilimuunga
samaki vizuri na nazi ya maji kisha nikapika na wali
niliofunikia hapo nikatoka nje nikijipa kazi ya kuanza
kuosha gari lilikuwa pale tofauti na lile aliloondoka
nalo john.
Niliosha na kulifuta likawa safi zaidi kisha nikaanua
mashuka yaliokuwa yamekauka nikaingia nayo ndani
na kutandika.
Muda nao ulisogea sikutaka kula niliamua kutunza
njaa ili nije kula pamoja na John wangu,
nilijizungusha zungusha huku kumbu kunbu za
mateso ya Somoe zikilejea kichwani mwangu
niliyakumbuka yale mabaya yote aliyonitendea
Somoe, kila nililokumbuka niliishia kucheka tu,
nilikaa pale sebuleni nikitizamana runinga kwa
wakati huo nilifurahi peke yangu kutoka na kipindi
nilichokuwa nikikiangalia saa zilizogea mpka kufika
Jioni hapo nikapasa mboga kwenye jiko la umeme
pia nikaweka chakula kwenye hotpot na kutenga
kabisa mezani, sikuwa na haja ya kutengeneza juisi
tayari ilikuwemo ndani hivyo nilijiweka tayari
kumpokea John, nikakaa karibu na mlango
kumsubiri John arudi.
Dakika kadhaa zilipita lakini hakukuwa na dalili za
kurejea kwa John Sikuchoka kusubiri niliamini
subira inavuta heri nilikaa kitako nikiendelea kusubiri
arudi looh! Anarudi wapi saa zilizidi kusogea, Hapo
sasa ikabidi nisimame na kuanza kuzunguka huku
na huko nikizipiga hatua kama mtu aliekosea njia
nilienda na kurudi, nikatoka nje bado nasubiri,
niliwasha taa nza nje na ndani ikabidi nikachungulie
getini juhudi zote nikizofanya hazikuzaa matunda
ndipo nilipokumbuka simu yangu, ikabidi nirejee
ndani, niliifikia simu yangu na kuanza kutafuta jina
la John nililosave kama Mume wangu, haikiwa kazi
ngumu kwa vile sikuwa na namba nyingi kwenye
simu yangu hivyo nililiona kwa wakatj nikaipiga,
mara ya kwanza nilipoipiga ilijikata hapo nikajaribu
mara ya pili nikapokea na madada wa mtandao
akinifahamisha kuwa ninaye mpigia hapatikani kwa
muda huu,Nilipata fadhaiko la.moyo hapo nikrudi
sofani nikakaa nikijifariji kuwa john atarudi, nilisalia
pale pale kwenye sofa nilikuja kustuka asubuhi
ikiwa tayari imeingia kila kitu kipo vile vile si taa
wala milango, niliamka nikijinyoosha.
"Inamana John hakurudi atakuwa wapi,huyu
mwanaume.?"Nilijiuliza huku nikipiga miayo njaa na
uchovu vilinikaa kwa pamoja, sikuwa nimekula
sikuwa nimeoga nilimsubiri John,John ambaye
hakurejea nyumbani.
Nilifungua mlangu ulikuwa wazi sikuwa nimeufunga
na funguo sikujal sana kitu peke nilichoona nastahili
kufanya ni kwenda kuoga nijiweke safi, uchovu
unitoke kisha ndio nijue jinsi ya kufanya kweli
niliingia bafuni nikajimwagia japo maji yalishuka
mwilini mwangu ila nilihisi kama siogi vile akili
haikuwa pale, akili yote ilimuwaza john wangu
nisiejua alipo, nilitoka bafuni kisha nikavaa nguo
zangu hata njaa wakati huu sikuihisi tena nilichukua
simu yangu na kuiweka kwenye pochi yangu kisha
nikatoka nje sikujua niendako ila niliradhimika
kwenda kuntafuta John, kwavile kutoka tunapokaa
na barabara zipitapo daladala ni mbali hivyo nilianza
kutembea nikiifata njia hiyo ndefu mpaka pale
nilipotokea kwenye barabara kuu hapo ndipo
nikasimamisha daladala nayo ikanitii iliposimama
nikaigia ndani yake na safari kuanza, nikikaa kwenye
gari nikiwa mwingi wa mawazo hata mkono wangu
mmoja ulishika shavu langu, hapo nikajisahau kama
nipo ndani ya gari.
Sauti ya konda akinadi vituo nikiisikia kwambali
konda akitaja kituo kwa kituo.
"Flamingo....contener.. Bwawani."ikisikika kwa
mbali hali ya kuwa konda hakuwa mbali nami,
nilijisahau kabisa.
"Sister tumefika mwisho nauli yako"sauti na mguso
wa konda ndio ulinistua kwenye lindi la mawazo,
hapo nikatoka mawazoni.
"Sh ngapi?"nilimuuliza.
"We sister vipi inamana hujui nauli ya huku, au ndio
malingo,"
"Samahani kaka yangu, basi ngoja nikupe niliyokuwa
nayo,"Baada ya kuona hanitajii bei hapo ndio
nikamwambia nitampa nikiyokuwa nayo nikafungua
pochi yangu kutoa hela, nilianza kutafuta looh! Simu
pekee ndio ilionekana ndani ya pochi hakukuwa na
hela.
 
SEHEMU YA 47
NA GAOOH
SIMU 0654387935
ILIPOISHIA SEHEMU ILIYOPITA.
Baada ya kuona hanitajii bei hapo ndio
nikamwambia nitampa niliyokuwa nayo nikafungua
pochi yangu kutoa hela, nilianza kutafuta looh! Simu
pekee ndio ilionekana ndani ya pochi hakukuwa na
hela.
SONGA NAYO SASA.
Nilipoangalia kwenye pochi yangu na kukuta
sinapesa nilikosa cha kusema konda alinikazia
macho akisubiri pesa yake.
"Samahani kaka yangu, Niliweka pesa humu ila
sizioni,"
"Unasemaje,?"
"Niliweka pesa huku ila sizioni,"Nilirudi hapo konda
yule hakuwa na uvumilivu alianza kuniwakia
aliniwakia akitaka hela yake hapo tayari tulifika
nyuki.
"Samahani shida si hela tu basi kaa na hii simu
yangu nikikuretea pesa yako unanirejeshea,"
Nilimwambia huku nikitoa nilifanya hivi kuepusha
kelele tu kwani konda huyu hakuwa na staha hata
kidogo hakujali nipoje hata huruma yangu na upole
hakuuona kabisa.
Nilipotoa simu yangu nikamnyooshe hapo akitaka
kuipokea ndipo alishtukizwa na mtu aliemshika
mkono, hata mimi sikumjua ndipo nikanyanyua
kichwa kumuangalia sikuwa nikimjua,alikuwa kijana
mtanashati aliejazia misuri tena akivalia kofia nyeusi
chini akivaa sarawili nyeupe ya jeans sambamba na
tisheti nyeusi.
"Brother vipi, tunashikana mikono kama wahalifu."
Alimwambia.
"Mpe huyo dada simu yake tuongee,"alimwambia
ndio lilikuwa neno lake la kwanza kama salamu.
"Nampaje wakati ninamdai nauli yangu,?"
"Kwahiyo nauli ndio inathamani ya simu yake au
unataka kumfanyia wizi,"
"Si tumeelewana lakini,"
"Mpe simu yake, chukua jero yako hii hapa,"kaka
yule alisema huku akimpa konda hela yake, hela
ambayo alisita kuipokea mwanzoni ila yule kaka
alimkazia macho hapo akaipokea na kunipa simu
yangu, wakati wote nilikuwa mtazamaji
tu,nikiwatizama.
"Asante kaka nashukuru sana, kwa wema
wako."Nilimwambia aliitika na kuniambia nisijali
kaka wawatu hakuwa na makuu hakuniomba kitu
tukashuka kwa pamoja wakati tunashuka nilisikia
sauti ya konda akiongea kwa manung'uniko. "watu
wengine bana, yani wanabeba vyuma ili waje kuleta
ubabe mtaani tu si angeniacha nipate simu anareta
ubabe aaah, watoto wa nje ya ndoa utawajua tu
wakorofi sana," konda aliongea bila kujua kama
bado hatujashuka tena yule kaka alinitanguliza mimi
akinisubiri kwa kushika mlango wa gari hilo.
"Unasemaje wewe, umeniambiajee mimi
nani?,"aliongea na kumfata konda aliekuwa akihaha
wakati huo, sikuangalia ila nilisikia mdundo tu japo
niliona mkono ukivutwa ila sikujua umeshukia wapi
nilichosikia ni mdundo tu hapo nikashuka na
kuondoka pale nikiacha zogo sikutaka kufatilia sana
kwa vile nilikuwa na yangu yalionijaa kichwani,
Niliondoka na kuelekea kwenye gari za kariakoo na
makumbusho hapo nikasimama nisijue la kufanya
huku nikikumbuka pochi yangu haina kitu.
Hata nilipokuwa nikitaka kwenda sikuwa nikipajua
japo nilidhamiria kumtafuta John ila nitamtafutia
wapi, ikiwa sijui chochote kuanzia sehemu ya kazi
wala popote, japo marafiki zake nawakunbuka ila
sikuwa na mawasiliano nao wala kujua makazi yao.
"Nirudi tu nyumbani huku naenda wapi hata nauli tu
sina,"nilijisemea kisha nikaanza kutoka stand hapo
nikifatia njia ya stand ili nitokee Bagamoyo road,
nilichepuka haraka haraka nikiwahi magari kabla
hayajapita nikavuka na kutokea hapa sheri ndio
nikaanza safari ya kurudi kwangu, kutokana na
mawazo ya John sikuona umbali wa sehemu
niendayo hivyo nilizidi kutembea tu hata magari
nisiangalie mara kadhaa nilistuliwa na honi.
Baada ya magari kadhaa kunipita baada ya
kunipigia honi za tahadhari nitoke barabarani sasa
gari hili lenyewe lilisimama baada ya kunipigia honi
likasimama mpka nilipo.
"Shemeji vipi,?"ndipo mtu yule akanena, sikuwa
nikimkumbuka kabisa hata nilipomwanamgalia.
"Shemeji yako kwa nani unanijua wewe,?"nilimwam
bia hapo nikiwa nimevulugwa tayari.
"Wewe si Kidawa mke wa John inamana
umenisahau,?"alisema nilimwitika japo sikuwa na
kumbu kumbu naye.
"Ooohh, ndio Na John yuko wapi,?" John wapo
mbele wametangukia na rafiki yetu mwngine mimi
ndio nilipereka gari yak sheri ikawekwe mafuta.
"Inamana hii ni gari yake"
"Ndio inamana hujaijua tu gari ya mume wako, ebu
anaglia namba kisha ingia ndani turudi
nyunbani,"Aliposema hivyo nilienda mpka mbele na
kuangalia kweli looh,! Lilikuwa gari la John ila
sikuweza kulitambua haraka, baada ya kuona ndipo
akanifungulia mlango nikaingia na safari kuanza.
"Imekuwaje mpaka John hakurudi jana usiku, na leo
sahizi ndio unasema unarudi nae."
"Kidawa kwanza utusamehe, John hatujui amepatwa
na nini alituambia ule muda tunatoka kazini alisema
hatarudi nyumbani hivyo anatualika twende club tule
na kunywa, japo tulimuuliza kwanini huku tukijua
ameoa ila alikataa kusema akatuambia anamawazo
sana, hatukumuelewa ndipo tulienda nae club kama
alivyotuomba tulipofika kule tulipiga story huku
tukitafuna nyama na kushushia na bia japo wote
tulikunywa ila mwenzetu alikunywa kwa kasi sana,
ndipo baada ya kulea alianza kukutaja wewe Kidawa
huku akisema amekukosea sana kwa kukufanyia
unyama, alienda mbali na kusema anajuta huku
akitaja Somoe ni katili, aliongea mengi sana sisi
tulijua ni pombe tu mana siku zote tulijua kwenu
mpo wawili wewe na yeye na mnaishi kwa furaha,
tulichojua ni kuwa John amezidiwa na pombe
alizokunywa. Muda ulisogea ila yeye alizidi kunywa
hata tulipomuomba kurudi nyumbani alikataa kata
kata ikabidi tumuache aendelee na starehe yake
usiku ulikuwa mkubwa tuliona tusimsumbue wote
tukapitiwa na usingizi pale mezani tulipokuwa
tukinywa ila tulipostuka John alikuwa macho
akiendelea kunywa pombe ndipo tulimpokonya, jinsi
alivyokuwa na manenoalioongea tukiogopa kumleta
nyumbani John alikuwa akitukana matusi pia
alisema asiperekwe nyumbani kwake atamuua
Somoe, maneno yale ndio ikabidi tumpereke
hospital asubuhi ile na
kumtundikia dripu na kuwekwa sawa ili akili yake
itulie, baada ya kumuona yuko sawa ndio tukaamua
tumlete nyumbani tujue kuna nini."alihitimisha rafiki
wa john ambaye sikujua hata alikuwa anaitwa nani.
Maneno yake yalinifikilisha hapo na mimi nilianza
kumuelezea yaliyotokea japo nilimdanganya kidogo
kwa kumwambia kuwa yule msichana ameondoka
mwenyewe hali ya kuwa nilimjeruhi ndio akaondoka,
alisikitishwa sana na habari niliyompa akanisifu kwa
ujasiri niliokuwa nao, baada ya mwendo wa nusu
saa na kupita vituo kadhaa tulifika nje ya nyumba
yetu hapo geti likafunguka tukaingia ndani.
Tulipoingia nikashuka ndani ya gari nikakimbilia
ndani ya nyumba hata salamu sikuitoa kwa yule
niliemkuta nilikimbilia kuuliza.
"John yuko wapi?"Nikiuliza huku nikipepesa macho
kuntafuta huku na huko.
"Ooh shemeji pole kwanza ulikuwa wapi John
nilipofika nae hapa alikutafuta sana, nae alizunguka
kila sehemu akikutafuta, ila sasa anaoga yuko
bafuni.,"aliposema hivyo sikuamini nikataka kuingia
chumbani ndipo akanizuia na kuniambia nitulie kisha
kunitaka nikae kwenye kochi kumsubiri john,
nilimsikiza sikumpinga yule nilikuja nae kwenye la
john akaingia ndani tukawa watatu tukimsubiri John
nae alitoka japo ilitamani kumkumbatia ila nikisita
kumfata taswira ya mateso ilikaa kichwani pale
nilipomuona tu alinisogelea na kupiga magoti mbele
yangu.
"Nisamehe Mke wangu, furaha yangu,malkia wangu,
najua nimekukosea sana hata kukutizama naona
aibu siamini yale yote niliyokufanyia nashndwa
kuelewa ilikuwaje, sielewi akili zangu zikikuwa wapi
wakati nikikutesa vile natamani siku zirudi nyuma
yale yote niliyotenda kwako niyasawazishe..
,"aliongea mambo mengi john huku machozi
yakimtoka japo aliniumiza ila kiukweli John
nilimpenda mno na alikuwa chaguo la moyo wangu
machozi yake ndio yaliyatoa na yangu hapo
tukaanza kulia kwa pamoja, nilimuomba asimame
nae akasimama huku machozi yakimtoka.
"Nimekusamehe John wangu wewe ndio mwanaume
wangu wa maisha yangu nikupende kwa dhati kuliko
ninavyojipenda, Nimeumia sana siwezi kuelezea
maumivu yangu ila nilijua hazikuwa akili zako John
ulifanya vile kwa ajili ya msukumo wa yule shetani
alieharibu mimba yangu na kuigeuza ktu cha
ajabu,tungekuwa na mwanetu John.."Niliongea huku
nikilia kwa kufika fika, kisha tukaachiana na kukaa
kwenye makochi rafiki zake John walimuombea
john msamaha kwa mara nyingine kisha kutuasa
tuishi kwa upendo na amani kila mmoja aijue
thamani ya mwenzake, maneno mengi yaliongelewa
John akakiri kila kitu yakaisha hapo ndio nikaingia
jikoni kuandaa chakula cha mchana nilipika pilau
ambayo wote tulikula na kunywa kwa furaha kwa
kila mmoja wetu mpka ilipofika jioni wakatuacha na
kutuaga wanaenda kwao watarejea siku nyingine.
Walipoondoka tulifunga milango hapo tukaenda
kuoga pamoja kisha tukala chakula cha usiku
tuliposhiba wote tuliingia chumbani mimi nikiwa wa
kwanza kupanda kitandani nilimhitaji zaidi ya yeye
alivyonihitaji sikuwa nimekutana nae ni muda sasa
hata mwili wangu ulijaa ganzi ya kuhasi tendo
nikahisi john anacherewa ndipo nilimfata alipokuwa
kisha nikamtupia kitandani.....
 
SEHEMU YA 48
NA GAOOH
SIMU 0654387935
TULIPOISHIA SEHEMU ILIYOPITA
sikuwa nimekutana nae ni muda sasa hata mwili
wangu ulijaa ganzi ya kuhasi tendo nikahisi john
anacherewa ndipo nilimfata alipokuwa kisha
nikamtupia kitandani.....
ENDELEAA SASA
Nilipomrushia kitandani hapo na mimi nikamjia juu,
lilikuwa tendo la furaha sana kwangu.
Nilifanya nikiwa na furaha ambayo sikuwahi ipata
kabla baada ya mishindo kadhaa tulilala pamoja
nikimkumbatia John wangu.
Asubuhi na mapema niliwahi kuamka nikimuacha
John akiwa amelala hapo niliingia jikoni na kuandaa
chai, chai ambayo nilijaza viungo kumfurahisha john
wangu.
Baada ya kuandaa nilingia chumbani kwa mahaba
nilimuamsha John akajiandae ili aende kazini
aliamka na kunibusu hapo tukaingia pamoja bafuni,
huko nilicheza nafasi yangu kama mke tulianza
kistaarabu kisha uchokozi ulianza nilimchokora john
kule bafuni tukaingia tena mapenzini hakika nilikuwa
nimezidiwa sana kipindi nilichokaa bila kukutana na
mume wangu kiliudhoofisha mwili wangu hivyo
kusababisha niwe na ganzi kiasi tulivyokutaka ganzi
yote imeisha sasa.
Tulipomaliza kuogeshana tukatoka kisha tukaanza
kupakana mafuta na kuvalishana mimi nikavaa nguo
za kawaida ila john alivaa suti yake safi ya kuendea
kazini,alipo vaa kidogo nilimsifia wakati huo
akijitizama kwenye kioo tukakumbatiana hapo
tukatoka mpka mezani, tulikunywa chai kisha
tulipomaliza ndio john akaniaga na kuelekea kazini
kwake nilibaki peke yangu.
Siku hii nilikuwa na furaha sana yani nilitabasamu
muda wote nisiamini kama nimeondokana na shida
pamoja na tabu zote nilisimama nikitizama nje
dirishani kuna kitu nilikiona hapo ikabidi nitoke nje
nilipotoka nikaitizama bembea, nilipoiangalia
nikaanza kuvuta hisia nipo na mwanangu
nambembeza kwenye ile bembea kila nilipokuwa
nikiingalia machozi hayakuacha kunishuka
yaliteremka kwenye mashavu yangu japo sikutoa
sauti ila niliumia moyoni, "Kazi ya Mungu haina
makosa" nilijisemea huku nikijua haikuwa kazi ya
Mungu mikono ya shetani ilitumika kitendo cha
kuiangalia bembea ile ndipo niliifata na kukaa juu
yake huku nikiyafuta machozi yangu kwa viganja vya
mkono.
Niliamini ipo siku nitapata mwengine "Bora uhai"
nilijisemea kisha nikaingia ndani nilianza kufanya
kazi zangu nikianza kuzishungulikia kazi zote,
kuanzia ndani kisha nikafata za nje baada ya muda
nilizimaliza kazi zile.
Siku haikuwa ndefu hivyo jioni ilifika haraka haraka
John wangu akarudi nilimkumbatia nikimpa pole na
kazi, tayari nikishaandaa chakula hivyo alivyokuja
nilimvua kote lake nikalishika pamoja na mkoba
wake.
"Pole kwa kukuacha na upweke, Mke wangu"
"Asante ila niko sawa mume wangu,sijakumis hata."
"Hujanimis basi ngoja niondoke."
"Hapana Mume wangu sijakumis sana sababu
nilijua utarudi nitakuona hivyo sikuwa na shaka sana
japo ndio nimekumis,"
"Nimekumis pia yani hata nilipokuwa nikifanya kazi
ni jina lako tu ndio likikuwa akilini mwangu,"
"Usijal Mume wangu, umerudi nyumbani na
umenikuta mimi nipo,"nilimwambia wakati huo
tulikuwa tumesimama karibu na mlango, hapo
tukaingia chumbani kuoga pamoja tulioga wakati
huu tulioga bila kuchokozana, tulipomaliza tulijifuta
maji akavaa nguo za kulalia pensi yake ha blue na
tishet nyeusi alipo na mimi nikavaa night dress
yangu hapo tukatoka kula pamoja mezani, tulikula
kisha tuliposhiba tukaingia ndani kulala.
Tukiwa kitandani ndipo John alipo nikumbusha kitu
ambacho sijategemea.
"Mke wangu hivi yule shetani kaenda wapi,?"
"Nani?"Niliuliza hali ya kuwa nilijua mtu
aliemuulizia.
"Somoe"Nae akajiu moja kwa moja.
"Ameondoka Mume wangu, nilimpiga yeye
mwenyewe akaniomba msamaha na kuondoka"
"Kumbe nawe bondia siku hizi umekuwa
ebitoke,"john aliongea huju akicheka.
"Napigania Penzi langu we hujui jinsi gani
ninavyokupenda."
"Yameisha yule shetani hawezi kurudi tena hapa
sijui hata alinilisha nini kiasi cha kumsikiliza yeye na
kukuumiza mke wangu."John alisema kwa majozi
"Nakuomba unisamehe sana" aliomba msamaha
tena nilimwambia yameisha tukakumbatiana na
kujifunika shuka gubi gubi na kulala.
Maisha yaliendelea furaha ikitawala miongoni
mwetu, nilimhitaji zaidi john wangu hakuniisha hamu
kila siku nimuonapo nilitamani niwe namuona yeye
saa zote, nikitamani hata macho yangu nifumbe
kisha muda aliopo john ndio niyafumbue
nikimtizama, 'ooh John wangu' siku zikisogea
mambo ya kumhusu somoe tulimsahau kabisa hata
kukumbuka kama kulikuwa na mtu anaeitwa somoe
hatukukumbuka.
Siku moja baada ya John kuondoka, nilikuwa peke
yangu nikikosa cha kufanya,Siku hii nilitamani
kutoka nje ya nyumba, niliona bora niende
nikajichanganye hata niende ufukweni nikabadili
mazingira, hapo ndio nilivaa nguo za kutokea baada
ya kuoga na kunywa chai, wakati huu nikakumbuka
kuchukua hela nilichukua kiasi kinachonitosha
nikaweka kwenye pochi yangu ambayo ndani yake
ilikuwa na simu nilijiandaa nikafunga milango,
nilifanya kama vya mwanzo nilitembea mpaka
kufika barabarani yapitapo magari hapo nilipanda
piki piki ambayo tulielewana bei na
dereva,nikimwambia naenda beach.
"Beach ya Wapi unaenda,?"
"Nipereke kawe beach"
"Sawa poa bei ni hiyo hiyo niliyokutajia"alisema,
hapo safari ilianza kuitafuta kawe tulipita vituo
kadhaa dereva hakuwa na haja ya kuvitaja kwavile
nilipokuwa nikienda alipajua, alitembea kwa
mwendo baada ya saa moja tulishafika kawe
ukwamani hapo nilimwambia anipereke ufukweni,
alinipereka nikamlipa pesa yake kisha akaniacha na
kuondoka aliponiacha nikisogea hadi kule mbele
nikatafuta sehemu na kukaa nilikaa nikitazama maji,
nilihisi kufarijika japo nilitamani ningekuwa na john
wakati huo tukichezea maji kama watoto,nikiwa
pale nilitizama mbele zaidi sehemu ambayo haina
watu wengi, nikijikuta nikitamani kwenda kule ila
kabla sijaenda kuna kaka alionekana akifanya
mazoezi eneo lile nilihisi kumjua ila sikutilia
manani,pia sikuamini macho yangu haraka haraka
ikinibidi nijongee mpaka kule nilipofika nilimfata
nikamsalimia alipoinua uso wake ndipo
nikamkumbuka vyema.
"Kaka habari yako,"nilimsalimu.
"Salama za siku,"
"Salama sijui za kwako, naona ndio tumepotezana
tangu siku ile" Nilimwambia.
"We ndio huonekani kwanza hata jina lako
hujanitajia mimi naitwa James, pia sio vizuri
kusimama tukiongea unaonaje tukakae pale ili
tuongee vizuri"alisema nikimkubalia tukaondoka
pale,hapo tulielekea kwenye uzio wa uliokuwa
pembeni pale uzio wa hotel.
"Kwanza unisamehe siku ile nilikuwa siko sawa
nilishindwa hata kukuuliza chochote, jina langu
Janet."
"Usijal japo niliposhuka nilikutafuta, nilitaka nikupe
hela kidogo nilijua huna ya kurudia"
"Aah, nilitembea kurudi nyumbani."
"Ooh pole za maisha lakini."
"Maisha safi tu yanaendelea."
"Vipi mbona uko huku umemfata nani,au umekuja na
mzee?"aliuliza.
"Aah, hapana leo nimejisikia tu kuja huku kupunga
upepo, ndio imekuwa kama bahati kukutana
nawe,"Tulipiga story za hapa na pale
tukifahamishana zaidi ila sikumtamkia kama
nimeolewa pia sikumuelezea undani wa maisha
yangu, Siku zote nilipenda kuweka siri mambo
yangu yanayonihusu hivyo kuyatoa kwa watu sikuwa
nikiweza kilichonihusu mimi ilikuwa ni siri yangu tu.
Kuna muda Unatakiwa kujaribu kuwa msiri kwavile
kama siri zako wewe mwenyewe umeshindwa
kuzificha je huyo unayemwambia ataweza
kukufichia, story zilinoga James aliita madafu
ambayo tulipewa na mrija, nilihisi amani zaidi japo
hakuna nikichofikiria kuhusu james, wakati
maongezi yanaendelea tukicheka na kufuraha ndipo
simu yangu ikaita Namba iliyopiga ilikuwa ya John
nikiipokea nimsikilize hofu ilinitanda nikijiona
ntakuwa na maswali ya kujibu ikiwa John amerudi
nyunbani na hakunikuta, niliipokea hivyo hivyo na
kuweka sikioni.
"Hallo hallo"ikisikika sauti upande wa pili haikuwa
ya john.
"Hallo"Nilimwitika.
"John ameangu...."alisema hivyo kabla hajamaliza
nilimkatisha na kudakia maneno juu juu.
"John amefanyaje Nilisema hapo simu ikakata.."
 
SEHEMU YA 49
NA GAOOH
SIMU 0654387935
TULIPOISHIA WIKI ILIYOPITA.
"Hallo hallo"ikisikika sauti upande wa pili haikuwa
ya john.
"Hallo"Nilimwitika.
"John ameangu...."alisema hivyo kabla hajamaliza
nilimkatisha na kudakia maneno juu juu.
"John amefanyaje Nilisema hapo simu ikakatwa.."
SHUKA NAYO SASA
Nilihisi kurukwa na akili, japo sikujua kilichompata
John ila roho ilinienda mbali zaidi, maumivu
nisiotarajia yalinijaa vilivyo.
"Janet kipi kinaendelea mbna kama hauko
sawa,?"James aliteta akiniuliza.
"Kwaheri James tutatafutana siku nyingine, ngoja
niwahi nyumbani,"Nilimwambia James nikimwacha
akiwa na butwaa hapo nikaondoka, Nilinunua vocha
kwa wale watu wenye vibanda beach hapo, niliingiza
kisha ilipoingia hapo nikanza kuipiga namba ya
John nilijaribu mara kadhaa ila niliambiwa namba
ilikiwa ikitumika, nilipanda dala dala, kuelekea
nyumbani nikitegemea labda john atakuwa
nyumbani, nilihisi kucherewesha Konda alipokuwa
akinadi watu wajae kwenye gari yake nilihisi kama
kunicherewesha hivi nilitamani nishuke nikapande
piki piki ola pesa sikuwa nayo ya kitosha hivyo
nilisubiri mpaka gari ikaondoka, njia nzima
nilimuwaza john wangu huku nikiomba mungu
sikutwe na baya lolote, japo Mungu hajaniambia
kama amesikiliza maombi yangu ila niliamini
Mungu wetu ni mwaminifu hivyo atatenda vile
vimpendezavyo.
Gari ilifika nyuki napo nikachukua dala dala ambayo
inaenda madale haikucherewa ilipojaza ikaondoka
kituoni hapo tukaianza safari, gari ilitembea kwa
kasi ya kawada ila ilinifikisha hadi kwenye njia ya
nyumbani kwangu, nilifungua geti na funguo ambazo
nilikuwa nazo kitendo cha mlango kufunguka
nilipayuka kwa sauti kubwa "John john johnii mume
wangu,"Niliita kama sina akili nzuri, mbali na kuita
kulikuwa kimya kuonesha kuwa hakukuwa na john
hapo nilizunguka Sehemu kadhaa ila hakuna wakati
nikiangaika kumtafuta john ndipo simu yangu
ikapata uhai na kutoa mlio ikiwa kwenye kochi
niliifata mpka ilipokuwa hapo nikaichukua na
kuishikilia kiganjani namba ilisomeka john.
"Njoo Muhimbili,hapa emergency"sauti ile ile ya
mwanzo ilisikika hapo ndipo nikatoka ndani
nilichokumbuka kubeba ni mkoba wangu hata simu
kama nisingekuwa nimeishika pengine nayo
ningeiacha, Sikumbuki kama nilifunga geti na
mlango wa ndani, nilichomoka tena kwa kukimbia
moyo ukinienda mbio hadi kufika kituoni hapo
nusura nigongwe na piki piki ambayo ilisimama
baada ya kunikosa.
"We dada vipi umechanganyikiwa au,?"alisema huku
akiniangalia mimi sikujali nilimfata, bila kusema
chochote nikapanda juu ya piki piki yake.
"Samahani naomba nipereke muhinbili tafadhali
nakuomba tuwahi,!"nilimwambia.
"Muhimbili kufanya nini na tunaendaje hatujaongea
au unataka ukanikabe huko,"
"Samahani nakuomba twende kuna mtu
nimeambiwa yuko huko na sijui kipi kimemtokea
naomba twende haraka pleaseee pleasee."nilimu
omba, hapo kishingo upande akaanza kuiondosha
piki piki yake.
"Kimbizaaa kimbiza tuwahi"Nilifoka.
"Dada taratibu, tusije vunja kila kiungo hapa,"alisema
huku akikanyaga mafuta kuniridhisha, mbali na
upepo kunitoa machozi lakini bado niliona hakimbii
kiasi kwamba ndio nikamwambia aongeze mwendo,
nilikuwa kama mtu niliechanganyikiwa akili haikuwa
pale kabisa, baada ya mwendo kadha tulifika n
ubungo naye akaniambia nikapande mwendokasi
huku akinisisitizia kuwa Muhimbili hawaruhusu piki
piki wala bajaji, nilisonya kwa hasira yule kaka
aliondoka na kuniambia kanisaidia tu hakutaka
malipo yoyote, nilienda mpka sehemu ambayo ndio
watu hukata ticket za mwendokasi mwanza ile foleni
tu nilichoka nilitamani kukimbia nikapite na kusubiri
gari ila haikuwa hivyo ilibidi niwe mpole mpka
nilipofikiwa hapo nikapata ticket ambayo ndio
nilipoipokea nikaenda kusubiri gari. Nilikaa karibia
nusu saa hakukuwa na gari nikikasirika sana ndipo
ikaja ikabidi nipande bila kujua looh,! Hata ile jina
lililoandikwa pale kwenye sehemu linapopita
sikukumbuka kuangalia, nilibanana mpka kupata
nafasi ya kuingia ndani, nikashikilia chuma kijasho
chembamba kikiteremka mgongoni kwangu, yote
sikujali nilikaa kwa kutulia urefu wa gari hili kwenye
kona ndio ulinipashida sikuwa nimeshika popote
hivyo gari likikata kona mara nyingi nikikuwa
nikianguka japo sikuanguka chini niliangukia watu.
"Kuwa makini usituangukie angukie hovyo,"alisema
mmoja ya wazee aliechonga ndevu zake huku
akiegesha miwani yake kichwani ambako hakukuwa
na kofia pia alinyoa kipara, mbali na kusema
sikumjali wala kumjibu gari lilisimama vituo
vuchache ambavyo hata sikushuka nikisubiri
mwisho wa gari nikiamini ndio muhimbili looh,
baada ya mwendo ule tulifika mwisho hapo gari
likaingia kituoni, nilitegemea itakuwa muhimbili
looh, hapakuwa muhimbili nilimuuliza mmoja wa
abiria wenzangu.
"Samahani hivi hapa ni wapi?"
"Kivukoni"alinijibu kisha hakutaka maongezi mengi
akaondoka.
Nikisonya huku nikiangalia gari lile pale juu nyuma
likiandikwa EXPLESS 0001 nilikasirika sikuwa na
jinsi ikabidi niulizie gari ya muhimbili walinionyesha
nikawahi na kupanda muda huo nilichoka kuanzia
mwili mpka akili yani huku nisijue kipi kinaendelea,
hakika nilikuwa na hali mbaya zaidi.
Gari haikuchukua muda ikianza kuondoka wakati huu
nilipata kiti ndio niliketi nikitizama mbele haikuwa
safari ndefu baada ya kupita vituo kadhaa gari
iliingia Fire nilikaa tu sikutaka kuangaika hatimae
tulifika muhimbili gari ikasimama, nilikuwa wa
kwanza, nikateremka hima hima nilitembea mpaka
mbele kulikokuwa na watu wengi japo niliona
msafara watu wakiingia ila sikuelewa ikabidi niulize,
nikajibiwa ndipo na mimi nikafata foleni muda wote
nilitamani hata niruke ila sikuweza zamu yangu ya
kupita ikafika.
"Kadi iko wapi,?"aliuliza yule mlinzi pale, kitendo
ambacho nilitamani kumtukana, mdomo koma,
nilimwangalia.
"Kadi iko wapi unainhmgiaje bila kadi huku."aliuliza
tena.
"Mwache apite huoni anaonekana mama
huruma"mwenzake alisema ndipo akafungua
nikapita, nilipopita nilianza kujikunbusha
nilipoelekezwa kila nikikumbuka kumbu kumbu haiji,
ikabidi niipige ile namba haikuwa ikipatikana ikabidi
nianze ku kutembea nisijue uelekeo wangu,.
"Nipo hapa Emergency, nyie mtakuja saa
ngapi,"nilisikia mtu akiongea hapo akili yangu
ikajipambanua kwa haraka masikio yakasikia na
kupereka taarifa kwenye ubongo ambao nao
ulichakata data haraka haraka jina Emergency
likanasa nilipokumbuka tu nikaingia mzima mzima
mpka mapokezi.
Niliulizia john, yule aliekuwa pale akaanza
kunitafutia jina hilo, na kunijibu halipo nilimwambia
muda alioleta yote nilisema kwa kudhani kwa vile
sikujua kilichotokea ndipo akaniambia kuna john
alieandikishwa hapo ila amekosa nafasi
wamemwamisha.
"Wapi alipoamishwa?" Nikiuliza nilijibiwa kuwa
nikaingie wodi fulani akanitajia namba nikaangalie
kama ndiye yeye au sie nilienda haraka haraka
mpka pale, nje ya chumba kile nilimkuta mtu
ambaye nilimkumbuka alikuwa rafiki yake John
ambaye ndio walimreta john nyumbani ile siku.
"Shemeji vipi,?"aliuliza ila mimi sikujibu zaidi ya
mimi kuuliza tena.
"Kunaendelea nini hapa john amepatwa na nini?"
"Punguza jaziba shemeji,"alinituliza tena sikutaka
kumuelewa hata kidogo.
"John ameumia,"
"Ameumia na nini ebu nyoosha maelezo mbna
sikuelewi,"
"John ni nusu mfu anapambania maisha yake sasa,"
"Unasemaje naomba uniambie vizuri, mbona
sikuelewi?"Rafiki yake john aliekuwa akiniambia na
yeye alionekana kuchanganyikiwa hata ongea yake
haikuwa ya kueleweka naye alionekana
kuchanganyikiwa.
"Kidawa mumeo ameumia vibaya...."Alianza
kuniambia lakini hakumaliza akaacha kuongea huku
machozi Yakimtoka..
 
SEHEMU YA 50
NA GAOOH
SIMU 0654387935
Ilipoishiaaa sehemu iliyopitaa
"Unasemaje naomba uniambie vizuri, mbona
sikuelewi?"Rafiki yake john aliekuwa akiniambia na
yeye alionekana kuchanganyikiwa hata ongea yake
haikuwa ya kueleweka naye alionekana
kuchanganyikiwa.
"Kidawa mumeo ameumia vibaya...."Alianza
kuniambia lakini hakumaliza akaacha kuongea huku
machozi Yakimtoka..
ENDELEAAAA SASAAA
Nilitaka kuingia ila nilizuiwa nikaishia pale nje,
nilijaribu kumhoji kilichotokea ila alishindwa
kuongea zaidi ya kulia tu, nilikosa cha kufanya na
mimi nilikaa sehemu nilihisi kuchoka zaidi, dakika
kadhaa chumba kile ambacho ndio shemeji
alichosema kinamo john ndani yake kilifunguliwa
kisha kitanda kilichotundikwa drip la damu pamoja
juu kilipitisha, nilitaka niangalie ila nilizuiwa manesi
na madaktari walikizunguka kisha wakatoka nje na
kuingiza kwenye gari, walikuwa wakimwamisha,
shemeji nae aliamka akiwa amechanganyikiwa, gari
iliondoka pale kuelekea upande wa kushoto ambako
kuna jengo kubwa la jakaya kikwete, sikujua
kilichoendelea daktari alituita mimi na shemeji,
akatuuliza maswali kadhaa nabkutupa maelezo
anapoperekwa john alisema wanampereka moi kle
ndio atapata huduma stahiki nilikuwa sijui
kilichotokea.
Kwa kufuta machozi na kulia kwa kufina fina alianza
kunisimulia kilichotokea hapo nikikuwa makini
nikimsikiliza.
"Shemeji leo wakati tuko kazini kule bandarini john
aliomba kumsaidia derava anaetoa mizigo kwenye
kontena na kile kigari maaulum alikubaliwa kwa vile
alipenda kuwasaidia wengine, siku hii yule dereva
hakuwepo hivyo john aliamua akatoka mizigo, ni
kweli aliweza na alijitahidi kutoa kwa usahihi.."alipo
fika hapa alinyamaza na kuanza kulia.
"Samahani tunaomba mrudi nyumbani mgonjwa
wenu yupo ICU hamwezi kumuona madaktari
wanapambania uhai wake bado,"alisema nesi
mmoja akimkatisha asiendelee kunisimulia hapo
tuliondoka na kwenda mpka kwenye mabanda
ambayo watu wanapumzika nikiyafuta machozi yake
yaliokuwa yakisarauka mashavuni kwake, tulifika
mpka pale na kukaa ila akili haikutulia ikabidi
tuelekee moi huku tukiikumbuka namba ya ward
tuliyoelekezwa, hatukutumia muda mrefu tulifika
pale hapo tukaa nje tukisubiri, madaktari waliingia
na kutoka.
"Hamruhusiwi kumuona bado hali yake sio nzuri
haweze kutoka ICU leo wala kesho,"alitupa taarifa
nesi na kuondoka na kweli tukishinda hapo
sikunzima bila kula hatukuruhusiwa kumuona John,
shemeji alinieleza kuwa john amepata jeraha
kichwani pia baadhi ya viungo vyake pia vimekutwa
na mkandamizo wa ajali aliyoipata akiwa katika kazi
ya kumsaidia dereva, alisema kuwa lilikuwa kama
jambo la kushangaza kwavile john hakuwahi tamani
kuendesha vigari vile pia aliladhimisha sana
kuendesha hivyo wakamkubaria. Niliumia sana
kusikia hivyo nilijiona mtenda zambi mkubwa
kwavile nimemkosea Mungu pakubwa kiasi kwamba
maisha yangu yamejawa na huzuni na machozi
nahisi sistahili kupata fulaha hata chembe.
Bila kujua hali ya John tulikuwa tukienda hospital
kila siku jibu tunalopewa kuwa john bado hatuwezi
kumuona ni siku tatu sasa ndipo dokta alituita
ofisini kwake.
Baada ya salamu ndipo alitupa maelezo mafupi
huku akitutia moyo.
"Mke wa john si ndio wewe kwanza poleni sana
kwa tatizo lililomkuta ndugu yenu, au mume wako
najua ni mipango ya Mungu huwezi kujua kusudi la
Mungu, ila naomba niwape pole kwa mara nyingine,
sehemu ambayo john ameumia kuna mambo karibia
matatu au mawili anaweza kutana nayo la kwanza,
John anaweza kupona ila akapoteza kumbu kumbu
yani akasahau kila kitu ambacho aliwahi kufanya au
alichowahi kukutana nacho kutokana na
mahalialipoumia yani ubongo umepata hitirafu
kubwa kitaalamu tunaita... Nimesahau kidogo jina
lake ila sana sana ni kupoteza kumbu kumbu zote,
cha pili anaweza pona ila mwili mzima ukapooza
viungo vyote, cha tatu anaweza kupoteza uhai
kabisa, najua ni hakuna cha afadhali kati ya hivyo ila
timu yetu ya madaktari bingwa wanaendelea
kupambana na uhai wa John tumuombee dua kwa
uwezo wa mungu atapona, usilie Mrs John"dokta
alitoa maelezo nilishindwa stahmili maneno yake
hapo machozi yalinitoka bila kutarajia nikayafuta
dokta akaendelea kunipa matumaini kisha alituomba
turudi nyunbani kwa vile john yupo katika chumba
cha wagonjwa mahututi anatumia mipira kula
pamoja na kupumua.
Tulimsikiza dokta, hapo ndio na sisi tulianza safari
kuja kila siku na kuondoka marafiki zake mbali
mbali nao walikuja kuangalia mandeleo yake zilipita
wiki mbili ndipo tukaruhusiwa kumuona john
nilifurahi taarifa ya kumuona john wangu tuliingia na
kumkuta kitandani akiwa amelala tu huku kichwani
akivalishwa kifaa kama helmet sijui kinaitwaje
sijasoma mimi sijui jina lake, john alikuwa kimya
mipira tu ndio ilionekana mdomoni kwake, macho
akiwa amefumba ilikuwa nafasi ya upendeleo
hatukuruhusiwa kumuona dokta alitufanyia
upendeleo kwa vile tumekuwa tukizunguka muda
mrefu bila kujua anaendelea, sikuacha kulia mbele
ya john kilio cha uchungu kilinitoka vilivyo.
Dokta alitutoa ndani hapo siku hii nilirudi nyumbani,
mapema nilijaribu kumshukuru mungu pamoja na
kumuomba amrejeshe john kama zamani, nilifanya
maombi., hata hamu ya kula sikuwa nayo kila
nikijitahi nipike hamu ya kula haiji nilishazoea kula
na john mara zote niliishia kumwaga chakula tu na
kunywa chai tupu, chakula kilikuwa hakimezeki.
Nilianza kwenda kanisani nikiamini ndio sehemu
sahihi ambayo nitasaidika, kwenda kwangu kanisani
kdogo upekwe ulianza kupungua hata muda wa kula
nilipakua sahani mbili yangu na ya john kisha
nakula yangu huku nikifanya kama john yupo karibu
yangu hata kulala nikifanya hivyo hivyo nilipanga
mito sehemu moja kisha kuifanya kama john.
Siku moja nilienda hospital hapo ilikuwa ni baada
ya kupita siku moja sijaenda hivyo siku hii niliamua
niende, nikifika hadi kwenye chumba alicholazwa
john pale nje nilikuwa sielewi kwa vile walionekana
watu tofauti wakiingia ndipo nikaenda kwa dokta
nawe sikumkuta ikibidi nikaulize mapokezi jibu
nikilopewa sikuamini pia likinishangaza zaidi.
"Mgonjwa wako amehamishiwa mloganzila"alinijibu
hivyo.
"Mloganzila ndio chumba gani mbona mi najua
alikuwaga chumba kile pale"nikimwambia nikiwa na
wasi wasi nisipajue mloganzila ni wapi.
"We dada, mgonjwa wako ameperekwa hospital ya
mloganzila hapa hayupo,"alizidi kunichanganya.
"Amehamishwa vipi sasa mbna sijapewa taarifa, na
huko alikohamishwa ni wapi,?"nikiuliza maswali
mfurulizo lakini hakunijibu nikahisi ananioima imani
nikaenda kukaa pale pale nikiwa nimepanga jambo
la kufanya dakika kadhaa nikiw pale ndipo
nikamuona muuguzi akiingia looh, sikusubiri
niliingia nae humo humo yeye akiwa kabeba kibaketi
kilichoonekana na mikasi nilipoingia nikakimbilia
kuangalia pale looh john hakuwepo, nusura nipige
kelele bahati nzuri dokta aliniona akaniwahi kunitoa
huku akifoka na kuniambia watu hawaingii huku,
nilihisi kurukwa na akili ila nikiwa pale nje ndipo
simu yangu ilipata uhai na kuanza kuita niliitizama
namba ilikuwa ngeni sikujishughulisha nayo nilibofya
kitufe cha kuzimia simu japo sikuizima nilifanya
hivyo kutoa sauti iliyokuwa ikitoka ikabidi nirudi
tena mapokezi ila kabla sijafika simu iliita tena
hapo ikabidi niipokee wakati huu nilipopokea
nikaisikia sauti ambayo haikuwa ngeni masikioni
mwangu.
"Samahani shem John tumemhamishia huku
mloganzila hivyo chukua bajaji hapo utamwambia
akulete huku."alisema kisha simu ilikatwa hakutaka
kuniruhusu niongee, nilichukizwa na jambo hilo yani
amemhamisha john bila kuniambia Nilitoka hima
hima mpka kufika nje hapo niliona bajaji
zilizojiweka kwa ajili ya safari nilipanda moja.
"Samahani kaka naomba unipereke hospital ya
mlugunzela,"
"Mlugunzela ndio wapi,?"
"Si hospitali,"
"Ni mloganzila ndio panaitwa hivyo,"
"Aah mimi sipajui ila si bora umeelewa basi
nipereke huko,"nilimwambia akanitajia nauli ya mpka
kufika huko nilimwambia pesa sio tatizo bora nifike
tu.
Safari ilikuwa ndefu tukivipita vituo kadhaa mpka
kufika huko, ilikuwa hospital kubwa kwa kiasi chake
nikampigia simu rafiki yake John akanielekeza
sehemu alipo deleva bajaji alinifikisha mpka pale
hapo akalipwa pesa yake na kuondoka alinipa
maelekezo kadhaa huku akinianbia john anapata
nafuu pia huku tunaruhusiwa kumuona maneno yake
kidogo yalipunguza hasira nikizokuwa nazo,
tukaingia hapo moja kwa moja alinipereka
alipolazwa john, huku pia alikuwa akipumua kwa
kutumia mashine pia kichwani alikuwa na mabendeji
mengi yaliozunguka kichwa chake, nilikaa pembeni
yake nikimuangalia tu huku nilijaribu kumuongelesha
ila hakuna kikichoonesha uwepo wake hakika
alikuwa nusu binadamu nusu mfu, furaha yangu
ilikuwa kumuona john nilijitahidi kufanya maombi
nikimuombea kwa mungu apone haraka hatimae
tulimaliza mwezi mluganzila, siku moja nikiwa
nimekaa nimeshika mkono wa John uliokuwa
umebanwa na kibanio kidoleni, nilimshikilia huku
nikigusa kifua chake na mkono wangu mwengine
john alikuwa kimya, nikiwa nimemshika alianza
kuchezesha kidole chake ndipo nilipopiga kelele
nikimuita daktari niliamka kabisa na kutoka nje
nikimuita daktali nae alikuja akiwa na vifaa vyake
alianza kumpima john dakika kadhaa mapigo ya
moyo ya john yalianza kupungua kabisa, nilitizama
kwenye mashine amabyo ilikuwa pembeni yake
ikionesha mapigo yake ya moyo, daktari alinitoa
ndani pale nisijue kinachoendelea rafiki john nae
akikuwa pale hapo ndio dokta aliniita baada ya
kutoka ndani, akiniambia nimfate ofisini kwake.
"Nimekuita hapa peke yako nakuomba uwe na
ujasiri,"dokta alisema hapo nilikaa kimya
nikmsikiliza.
"Kidawa,"
"Abee,"
"Pole sana kidawa,"
"Pole ya nini dokta,"
"John hatupo nae tena, pole sana Kidawa."dokta
alisema, sikumwelewa nikimuomba arudie tena.
"John amefariki Kidawa"dokta alirudia hapo ikawa
ndio kama amenipandisha kichaa changu, nikipiga
kelele, nikatoka nje nikikimbia sikujua ninachofanya
nilijikuta nikiongea vitu visivyoelewka hapo nikaanza
kuvua nguo looh, kabla sijamaliza iliyopo ndani
nikishikiliwa na watu walionifunga kamba ilionkana
wazi nimechizika sikuwa nikielewa ninachofanya.
Nilizidi kupiga kelele nikitaka waniachie nikaingizwa
kwenye gari, nilirusha rusha miguu lakini haikusaidia
kamba ilinikamata vyema.
MWISHO
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom