Simulizi ya kusisimua

Simulizi ya kusisimua

SEHEMU YA 21
NA Gaooh TheAuthor
SIMU=0654387935
TULIPOISHIAA SEHEMU ILIYOPITA
Nilihisi kuchoka ila ilinibidi niendelee na safari
yangu, nikiwa safarini kelele za watu pamoja na
sauti za wanyama zilinipokea nilianza kusikia, hapo
kidogo nilipata tumaini, tumaini jipya la kuwa
nakaribia makazi ya watu nilizidi kukazana tena
wakati huu nilikimbia ili nifike kwa wakati looh! cha
ajabu sauti zile hazikuwa zikifikika yani kila
ninapojitahidi nifike ndio nazo zinazidi kusogea
mbali nami NILICHOKA nikasimama..
SASA ENDELEAAAA
“MUNGU NISAIDIE,” nilisema maneno hayo ambayo
mimi tu ndio nilielewa ila kama ungebahatika kuwa
pembeni yangu katika umbo langu hili la paka
usingeelewa nilichosema zaidi ya kusikia sauti ya
nyau tu,Mungu wetu ni mwepesi kusamehe na siku
zote anaweka njia sehemu ambayo ulidhani
hutaweza kupita ukimuomba anatimiza haijalishi
umefanya mabaya kiasi gani, hata sisi wachawi
huwa tunaomba mungu atusaidie hata waganga pia
humuomba Mungu ili wakamilishe kazi zao,
nilipoomba kwa kusema Mungu anisaidie hapo
nikaamka nikiamini nitasaidika kisha nikaanza
kuondoka tena, wakati huu sikuangalia nyuma tena
nilikuwa nikitembea kisha muda mwengine
nikikimbia ili niwahi japo jua halikuacha kunichoma
ila nilijikaza ili nitimize nilichokianza baada ya
kutembea umbali mrefu MUNGU si athumani’
nilianza kuhisi upepo ukipuliza huku mawimbi nayo
nikiyasikia, Kwa akili zangu nilijua hapo ni baharini
na kweli kulikuwa baharini wakati huu nilipotokea
kweli niliyaona maji, hapo nilimshukuru Mungu, na
kuyasogelea maji yale.
Nilitembea pembeni yake nikitafuta chochote cha
kula lkama si Samaki basi nipate hata wale wadudu
wa ndani ya Maji, baada ya kutembea kidogo
nilifanikiwa kupata hapo nilianza kula samaki yule
ambaye alikuwa ametolewa pembeni na mawimbi,
nilipommaliza nilijihisi kutosheka, sikuwa
nimekatisha adhima yangu, sikutaka kuendelea
kuishi kwa mateso tena hivi niliamua nitafute
makazi ya watu ambako nitaishi nao,
Niliondoka baharini pale sikuwa nikipajua ni bahari
gari japo inajulikana ni bahari ya hindi ila sehemu
ile sikuijua ni wapi, sauti za watoto nilizisikia,
wakikuwa wakicheza mpira juu ya mchanga huku
wengine wakiwa wamekaa ufuoni hapo wakitizama
maji na wengine wakiogelea nilipita pembeni yao,
mana nilihofia wanaweza kunidhuru nilipita mbali
kabisa kwenye njia, ufuo huo ulijawa na minazi
pamoja na makoche, eneo kubwa ilijaa miti hiyo
pamoja na miti midogo ya miba, nilifatisha njia
nikidhamiria kufika eneo wanalo ishi binadamu, hasa
nikijua wazi sehemu amabyo nitafika itakuwa ni
makazi ya familia za kivuvi yani wanaotegemea
samaki kama kitoweo na hata chanzo cha mapato
yao, KIDAWA mimi nilifika kwenye kijiji hicho
ambacho kilikuwa sio kikubwa sana kwa
kinavyoonekana POPOTE KAMBI’ ndivyo akili yangu
ilivyonituma, hata miguu na nyayo zangu zilijaa sugu
na kuwa nyeusi tii na zile kucha za mikono na
miguu zilikuwa ndefu japo sio sana, siku hii niliingia
kwenye moja ya nyumba na kujifanya mwema
sikutaka wanione nilikimbilia juu ya dari, nilitaka
nijipendekeze kwao kwa kutoa msaada wa
kukamata panya kisha nipite nazo mbele yao ili
waniamini na kunifanya kama paka wao, ndivyo akili
zangu zilinituma na mimi nilifanya hivyo.
Kule dalini japo kulikuwa na giza ila nilijitahidi
kukaa huko, nyumba hii ilionekana kusumbuliwa na
panya sana kwani hata kule dalini hawakuacha
kukimbizana kwenye miti iliyopotengeneza dali lile,
hapo ndipo nikajipa ujiko nilikamata mmoja wa
panya ambaye alikuwa mkubwa kiasi chake baada
ya kumkata nilimtuliza sikumla limng’ata hadi pale
alipokufa ndio nikamueka chini, jioni familia ile
ilijumuika alikuwa ni baba, mama na watoto wao
watatu, nilipowaona wamekaa ndipo nikashuka na
panya wangu akiwa mdomoni, nilipotokeza tu
mmoja wa wale watoto alitaka kunirushia ndala
anipige hapo nikasita hata kutembea.
“Fai muache si unaona amekamata panya
wanaotusumbua usimpige,”mama yake alisema,
hapo yule mtoto ambaye anaitwa fai ndipo akaweka
ile ndala chini na mimi nikapita kwa maringo na
panya wangu mdomoni, kutokana na kujitolea
kuwasaidi kumaliza panya walinza kuniamini wiki
moja tu ilitosha kujenga imani na familia ile
wakanifanya kama paka wao sasa shombo za
samaki pamoja na utumbo walikuwa wakinipa hata
ugali pia walinirushia na mimi nilikuwa nikila kama
paka wengine, watoto wa mama yule walipenda
kucheza nami mara nyingi walikuwa wakinifukuza
nami nikiwafukuza kama mchezo walinipa mpaka
jina tasii, tasii nililizoea jina lile kila waniitapo
niliwatiii.
Nilipata falaja kuishi maisha haya mapya japo ya
kinyama ila yalikuwa na ahueni tofauti na polini,
familia hiii ilinijari vilivyo, Siku moja fai alikuwa
akielekea sokoni ikabidi nimfate nae alipenda
nifatane nae na mimi nikamfata alifurahia eti
kwavile nilimtii kwa kila kitu hakujua kuwa mimi ni
binadamu, tulifika sokoni akanunua alichoagizwa
alininunulia embe la kuiva lilimenywa kish
akanitupia hapo nilianza kula sikuwa nimekula muda
mrefu embe, hivyo nilijiona wa thamani sana kwao
hatukuchukua muda mrefu tukarudi nyumbani nilirudi
dalini kukamata panya kila siku ilikuwa ni lazima
nikamate panya alafu kwa sifa napita na panya
mbele yao ili wajue nawasaidia.
Niliamini haya yanamwisho, kwavile hakuna lenye
mwanzo likakosa mwisho, sikuzaliwa paka siwezi
kufa nikiwa paka, Najua ni jambo gumu sana hata
wewe ukiambiwa uishi kwenye mwili wa mnyama
sidhani kama utakubali japo hata mimi sio kwa
kupenda kwangu, Nilitokomea ufuoni nikatafuta
sehemu nzuri yenye jiwe kisha nikakaa hapo
nilienda kwa lengo moja tu la kutaka msaada
nilitaka wanisaidie kunirudishia umbo langu la
kawaida nilijaribu kutumia njia kadhaa kuwaita
hazikusaidia.
“Hahahahahahahahahahahahahahaha hahahaha
hahaha,” zilikuwa ni sauti za vicheko ambazo
zilikuwa zikinicheka nilipotazama hapo kidogo
nikataka kukimbia ila nilikuwa kati kati walikuwa ni
watu ambao niliwaua kichawi kuanzia Hajji wa
kijijini mpka wale wezi, hata zile kafara tulizofanya
na bibi pamoja na vitoto ambavyo wakati huo
vilikuwa vidogo sasa eti wote wamekuwa wakubwa
nao wananichekea kisha alitokea mzee ambaye
kavalia mavazi meupe.
“Hatuna msaada na wewe, ulijisahau na kuvuka
mipaka,” “muda wa kukurudisha utakuja lakini sio
sasa, utafika muda tutakurudish aufanye kazi zetu
inavyotakiwa” mzee yule alisema huku sauti yake
ikiwa kama ya mwango yani inajirudia rudia.
Nilimuomba anisaidie niwe binadamu wa kawaida
nilijua ananisikia kila ninavyomuomba wale watu
walicheka huku yeye akinipinga na kusema siwezi
saidika kwa sasa, “hatuwezi kukusaidia mpaka
muda ufike” “ muda gani huo mnaniacha nataabika
hivi inamana nilivyowatumikia vyote ndio mnilipe
hivi’ “sina msaada nawe” alisema na kupotea na
watu wale Machozi yalinitoka, uchungu uliniandama
nikifikili kuishi hivyi mpaka huo muda wao ufike,
nilikuwa nimechanganyikiwa zaidi siku hii nilirudi
kimya kimya na kukaa dalini bila kutoka.
“Fai mbona leo sijamuona atakuwa wapi?” mama
fai alikuwa kiuliza baada ya kutokuniona siku nzima,
kila alimuuliza hapo ndani walisema hawakuniona,
mimi nilikuwa nimetulia dalini mawazo
yakiniandama, nilikuwa nikitoka usiku tu kwenda
kutafuta chakula hata panya niliokuwa nikiwapata
nilikuwa dalini bila kushuka nao walinitafuta sehemu
kadhaa bila kuniona.
Usiku mmoja nilishuka, siku hii nilipanga niondoke
nyumbani pale kabisa japo niliishi nao vizuri ila
nilihitaji kwenda mbali zaidi kupata usaidizi
mkubwa, niliondoka kimya na kufata njia ya sokoni
nikiamini nitapata bara bara ya magari, ambayo
itanipereke sehemu tofauti na hapo nilizunguka
sehemu kadhaa sikufanikiwa kuona njia ilionekana
huku nilipo ndio mwisho yani nilipotoka kule
msituni ndio kuna njia ya kwenda mji mwengine ila
huku nilipokuja ni mwisho yani kumezungukwa na
maji mbele pamoja na kushoto na kulia, nilifikilia
kurudi nilipotoka kulikuwa mbali zaidi.
 
SEHEMU YA 22
NA Gaooh TheAuthor
SIMU = 0654387935
LIKE ILI NIPOST SEHEMU INAYOFUTA
ILIPOISHIAA SEHEMU ILIYOPITA.
ambayo itanipereke sehemu tofauti na hapo
nilizunguka sehemu kadhaa sikufanikiwa kuona njia
ilionekana huku nilipo ndio mwisho yani nilipotoka
kule msituni ndio kuna njia ya kwenda mji
mwengine ila huku nilipokuja ni mwisho yani
kumezungukwa na maji mbele pamoja na kushoto
na kulia, nilifikilia kurudi nilipotoka kulikuwa mbali
zaidi.
SASA ENDELEAAAA
Hakika niliteseka, kuna muda niliwaza hata nijitoe
uhai ili niepukane na tabu hizi, kule nbani sikutaka
kurudi tena, hivyo nilianza kujichanganya maisha ya
mwituni kwa kutegemea samaki, siku zilisogea
Nilikata tamaa, niliishia kujibatiza tu kuwa nitaishi
hivyo hivyo kama paka tu.
Siku moja nikiwa ufuoni katika kuzunguka zunguka
niliona moja ya ngalawa ya kubebea samaki ikiwa
imepakiwa pembeni kwa ajili ya safari, siku jiuliza
mara mbili hapo nilisogelea japo kulikuwa na maji
karibu yake ila nilijitahidi kuruka ikiwa ni baada ya
kuingia maji kidogo, nilifanikiwa kuingia kwenye
mashua ile ndani yake kulikuwa na samak ambayo
wapo kwenye nyavu pamoja na viroba nilijificha
kwenye kiroba ili wavuvi wale wanaomiliki usafiri
huo najua wakiniona wanaweza nirudia nchi kavu,
nilianza kumuomba mungu nikiomba wasinishushe
wala kuniona kweli hata waliporudi hakuna alieshuku
uwepo wangu, niliwasikia tu wakiongea huku
wakicheka pamoja, safari iliendelea mpaka pale
ilipofika mwisho hapo sasa nilianza kusikia sauti za
watu wakinadi samaki zao kidogo nilifurahia
kasheshe ilikuja wakati wananitoa, wavuvi wale
walitoa viroba ambavyo vina samaki japo nilifanya
adabu sikula samaki zao hata kidogo wakati
wanashusha samaki hapo nikatoka mimi
waliponiona tu mmoja wao alirusha teke ambalo
lilinipiga sawia nyuma karibu na mkia nilitoa sauti.
“huu ndio uchawi wenyewe yani tumebeba paka
humu tumuue huyu,
” walijisemea hapo nikaanza kupiga kelele
walikosea eti wanataka kunikamata ndipo nilipata
upenyo wa kukimbia, nilikimbia eneo lile huku
nikiugulia maumivu,maumivu ya kupigwa teke,
potelea mbali bora nimeondoka pale nilifurahia
baada ya kugundua nimerudi dar, akili yangu haraka
haraka ilinituma cha kufanya, ndio nilipaswa nifanye
hivi nitafanyaje? Nilijiuliza hapo akili ikanambia
nisubiri usiku ndio nifanye? Sikujua nifanye nini ila
akili ndio ilikuwa kama ikiniongoza cha kufanya
kweli usiku ulifika hapo ndio nikajua cha kufanya
nilijipereka kwenye moja ya makanisa usiku huo
nikajiweka sehemu huku nikisubiri kukuche ili niingie
kanisani kwa maombezi niliamini nitafanikiwa.
Nilikaa moja ya sehemu baridi ikinipiga nilivumulia
yote ilimladi nitimize lengo langu, niliamini nijia
pekee ya kurudi kama kawaida ni njia ya mungu tu,
ambayo ndio njia sahihi kuliko zote, Asubuhi ilifika
jambo la kushukuru siku hii ilikuwa jumapili, ni
kama imepangwa vile kweli Mungu akitaka
kukuinua hakuandikii barua, yani siku ya jumapili
ndio na mimi nimefika kanisani hapo.
Nilisubiri waumu waingie kwanza kisha na mimi
ndio niingie, kweli waliingia cha ajabu nje kulikuwa
na mlinzi nilianza kuhofia jinsi ya kuingia mana
asingeruhusu niingie akiniona, nilikuwa nikimtazama
nikisubiri ageuke upande ili niingie.
Nilianza kuhisi kama Juhudi zangu bure, mlinzi yule
nilihisi kama nimewekewa mimi, kuna mdada
alikuja pale akiwa na mtoto wake yule mtoto
alikuwa akitembea wakati mwenyewe, mtoto yule
alipofika pale alikuwa akilia huku akimsogelea yule
mlinzi kuanza kuvuta suruali yake aliyovalia, hapo
mlinzi yule alianza kumtoa ndipo na mimi nikapata
nafasi ya kupita nikajificha chini ya kiti, nilimshukuru
mtoto yule na kujihisi mwenye amani baada ya
kupita.
Mchungaji alianza ibada Misa zilifanyika zote
zilizisikia mpaka ukafika muda wa maombezi hapo
ndio na mimi nikajipereka mbele watu waliponiona
walishikwa na taharuki ambayo kila mmoja
hakutegemea kuona paka sehemu ile, mchungaji
alianza kufanya maombezi akikemea mapepo hapo
na mimi nilijisogeza zaidi madhabauni.
“Bwana yesu asifiweee,”
“Ameeeeeeenii,” waumini waliitikia kwa pamoja.
“Naona leo tumepata mgeni, sauti ya bwana
ilinionesha maono tangu usiku kuwa leo nitapata
mgeni wa tofauti,” mchungaji alisema hali ya kuwa
kama alikuwa na miadi ya kuonana na mimi kabla.
“Huyu sio paka kama mnavyomuona, nilipata
maono usiku wa kuamkia leo kuwa kitakuja kiumbe
kinachohitaji usaidizi..” aliendelea kuongea
mchungaji yule hapo waumini wote waliambiwa
wanyooshe mikono juu ili kufanya maombi pamoja.
Maombi yaliianza kila mmoja akikemea kivyake,
walikemea vya kutosha ila sikubadilika kila
walipokemea ulitoka moto tu kichwani kwangu
ilikuwa kazi ngumu mchungaji alikuwa akijifuta
jasho tu mara kwa mara kuonesha ugumu wa kazi
hii.
Baada ya maombezi karibia saa moja nzima ndipo
mchungaji alipohitimisha akiwataka waumu warudi
nyumbani kisha watanifanyia maombi wakati
mwengine.
“Nadhani kila mmoja ameona ugumu wa kazi hii,
japo Mungu ashindwi na chochote ila inaonesha
amefunga kwenye sehemu ambayo, hatuwezi
kumsaidia kwa maombi ya muda mchache
inapaswa tukemee zaidi, najua kwa sasa waumini
kila mmoja anatakiwa awepo nyumbani kwake kwa
ajili ya kufanya shughuli nyingine mimi nitabaki na
mnyama huyu jioni tutaanza maombi saa kumi
kama kunaatakae weza kufika basi aje tusaidizane
kumuombea mnyama huyu..” mchungaji
alitanabaisha mambo mengi sana, nilijiona kama
mkosefu nisie stahili kuishi mana kama hata kwa
mungu imeshindikana basi sipaswi kuishi tena
kwenye dunia hii nilioitendea dhambi.
Walihitimisha ibada baada ya sadaka kisha
waliimba nyimbo za kusifu alafu wakanza kuondoka
mchungaji alimwagiza mfanya kazi wake anipereke
kwenye gari yake, ili badae turudi wote kwa ajili ya
maombezi zaidi, waliamini Mungu hashindwi hivyo
hata mimi nitarudi kama kawaida.
Nilijikatia tamaa hata pale nilipowekwa kwenye gari
la mchungaji nilihisi kuna sauti zilikuwa zikinicheka
na kunizomea, huku nyengine zikisema
haitawezekana siwezi kurudi kuwa binadamu kama
mwanzo, nilijawa na majonzi hata machozi yalitoka
machoni kwangu na kutiririka kwenye mashavu
yangu, nilikuwa nikichungulia dilishani mchungaji
akipeana mikono na waumini wake, kwa kuagana
baada ya kuagana walikuja ndani ya gari pamoja na
familia yake yeye mkewe na mtoto wao wa kike wa
makamu kumtazama ni kama ana miaka kati ya sita
au saba kulingana na muonekano wake.
Waliingia ndani ya gari na kunikuta nimekaa kwenye
siti za nyuma mtoto wa mchungaji aliniogopa hivyo
yeye alikaa siti ya mbele mama yake ndio akakaa
nyuma, mfanyakazi wa mchungaji nae alipanda
akanipakata bila ya wasi wasi wowote safari
ikaanza.
Safari ile ilitawaliwa na ukimya hakuna alieongea
safari nzima kila mmoja alikuwa kimya kivyaje hata
mchungaji hakuongea.
“Unajua kazi zetu zina majaribu sana, shetani
anatumia mamlaka aliyopewa na mungu kuwatesa
wengine,tizama binadamu huyu aliepewa umbo la
mnyama inatia huruma sana,” mchungaji alivunja
ukimya hapo maneno yakamtoka.
“Ni kweli ila mume wangu, Shetani hungojea mpaka
pale anayejaribiwa na amevunjika moyo, na kuisha
nguvu. Yeye hungoja mpaka pale p maombi yana
kaa kana kwamba hayajibiwi _ pale matumaini
yamekwisha kabisa, pale ambapo mbinu zetu
zimekwisha hilo ndilo lilimtendekea petero,
alipomuomba Bwana wake akiteswa mbele ya kikao
cha mafarisayo. Lilimtendekea ayubu, aliye lazimika
kuwaza alipo poteza kila kitu cha muhimu kwake.
Pia angalia maswali yanayochipukia akili kwa
anaepitia majaribuni kama huyu aliegeuzwa
mnywama pengine atumsikii ila yeye hapo anajiuliza
“Mungu uko wapi? Kwanini maombi yangu
hayajibiwi?” hapo ndio shetani huchagua kupanda
uongo wake akilini mwa mtu huyo akimwambia
“Mungu amekuacha, amejitenga nawe hakusikii,’
huo ni uovu wa shetani Kumbe mungu wetu
hajakuacha na hatawahi kukuacha, nakuambua
mume wangu “MUNgu anakuambia , ‘
nimekuhakikishia sitakuacha kamwe. Sasa simama
enenda ukalishe kondoo wangu chunga mbinu za
shetani kinyume nawe, tazama niko nawe hata
mpaka mwisho wa dunia.”
Mke wa mchungaji alisema maneno hayo ya kumtia
moyo mumewe hapo nikisikiliza tu mimi sikuwa na
chakusema waliendelea kuongea maongezi yao
ambayo yalisindikiza safari yetu mpaka nyumbani
kwa mchungaji.
 
SEHEMU YA 23
NA Gaooh TheAuthor
Simu = 0654387935
LIKE SHARE NIPOST TENA
TULIPOISHIA SEHEMU ILIYOPITA.
Mke wa mchungaji alisema maneno hayo ya kumtia
moyo mumewe hapo nikisikiliza tu mimi sikuwa na
chakusema waliendelea kuongea maongezi yao
ambayo yalisindikiza safari yetu mpaka nyumbani
kwa mchungaji.
SASA ENDELEAA…
Tulifika nyumbani kwa mchungaji yule, ilikuwaa
nyumba nzuri kuanzia nje ikipambwa na uzio
mkubwa wenye geti jeusi, huku ndani bustani nzuri
zilizojaa kijani cha majani mabichi zilipendeza
kuangalia, kwavile tuliposhuka kwenye gari yule
mlinzi alinibeba kama mtoto tukaingia ndani looh!
Ndani kulikuwa kuzuri zaidi ya nje kulijaa thamani
nyingi kuanzia sofa za kisasa tv kubwa taa za
kupendeza na rangi nzuri ukutani.
Japo sikuwa binadamu ila walinikaribisha hata
wakati wa kula vile vyakula ambavyo wanakula wao
ndivyo nami walivyoniwekea,hata muda wa
kukiombea chakula n walinijumuisha , nilifarijika
sana nikaanza kula waliniwekea mpaka maji ili
chakula kipite vizuri baada ya muda wa saa kadhaa
tukiwa tumekaa pale tukitizama runinga waliniweka
kwenye kochi na mimi nikiangalia yalikuwa ni
mahubiri ya mchungaji Tb joshua walikuwa
wakiyafatilia kwa uzuri zaidi.
“sasa mke wangu nadhani muda tayari umefika”
Mchungaji alisema hapo akiwa anatoka kuoga.
“Ndio mume wangu usisahau na yale mafuta yako,”
“Nimekwisha yachukua ngoja sisi tuwaache,
tukakamilishe hili,”
“Sawa mume wangu, na sisi tutakuja sio muda
mrefu najua hilo ni a letu letu kumsaidia binadamu
huyu,” waliongea hapo mfanyakazi wa mchungaji
akanichukua na kunibeba kuelekea kwenye gari
baada ya kuingia mchungaji nae akaingia kisha
safari kuanza kurudi kanisani.
Hatukuchukua dakika nyingi tulifika hakukuwa na
foleni njia ile hivyo tulifika kanisani, waumini walijaa
siku hiyo unaweza kusema wtu hawajaenda makwao
kumbe laa walienda pia wamerudi kushuhudia
muujiza, tukaingia kanisani muda wote nilikuwa
nimebebwa mpaka tunafika mbele,pale madhabauni
ndio nikaweka chini kwenye sakafu.
Mchungaji akaanza maombi baada ya nyimbo za
kusifu kuimbwa, waumini waliimba na kumtukuza
bwana yesu aliehai, ziliendelea shughuli nyengine
ikiwemo neno la bwana muda ukafika, muda ambao
watu wengi ndio walikuwa wakiusubiri, muda wote
nilikaa kimya tu hata kichwa changu niliinamisha
chini, kutokana na kila pale niangaliapo mbele
nyuso za huruma zilikuwa zikiniangalia mimi tu
pamoja na wengine kutokwa na machozi ya huzuni
dhidi yangu.
Mchungaji aliingia kwenye kile chumba cha pale
mbele, ndani ya dakika chache akarudi, na kuanza
kukemea.
“Nguvu ya bwana, naituma kuondoa mamlaka ya
shetani kuvunja maagano yote na visa visasi vyote
nateketeza kwa jina la yesu aliye hai, jehooova’
“naondoa kila kilichopandikizwa ndani ya mwili huu
wa mnyama asie na hatia naya teketeza maovu yote
na makao ya shetani, kwa jina la yesu” mchungaji
alikuwa akikemea huku ameshika kichwa changu
cha paka, haikuwa kazi rahimchungaji aliepewa
uwezo na Mungu wakutenda yale wengine
wasiyoweza kutenda, alizidi kukemea uchafu wote
ulipandikizwa kwangu alitaja kitu na kuvikemea
kuanzia majini vinyamkela, ulozi. Vyote alitaja
akivikemea , mama mchungaji nae alifika pale
mbele kuongeza maombi walijitahidi kadri
wanavyoweza hatimae mwili wangu ule wa paka
ulianza kuteketea kwa moto, sikuwa nikihisi
maumivu yoyote mwili ule wakati unatekea mimi
nilikuwa nikiona kama picha mwili ule ulipoisha ki
ndio kilichoonekana kwenye macho yangu hakuna
nilichoona tena.
“Asante yesu, asante yesu asante yesu, kwakutenda
tukakushukuru baba,” sauti hizo zilinipokea nikiwa
kwenye giza nilihisi nikishikwa mkono hapo
nikapiga kelele ‘msinichukue msinichukue’ nilisema
hapo nikafumbua macho nikiwa nimelala chali
nikaamshwa.
Machozi hayakuacha kunitoka nililia zaidi sikuwa
nimeamini kabisa kama nimerudi kuwa binadamu
wa kawaida, waumini wote hata mchungaji hakujua
kama mimi ni mwanamke, watu walimsifu yesu
kristo kwa kutenda miujiza hakika ulikuwa muujiza
mkubwa sana.
Baada ya maombi na nyimbo za kusifu hapo ilibidi
waniambie nitoe ushuhuda, kiza tayari kiliingia taa
zikawashwa, ili kuleta mwangaza eneo lile watu
walifulika sana.
Nilianza kutoa ushuhuda wangu nikianzia maisha ya
kijijini mapak nilivyoingizwa kwenye uchawi pamoja
na yote niliyofanya watu wengi walihamaki kutokana
na mambo makubwa nililiyoongea, nilihitimisha
mpaka kilichoperekea niwe paka, baada ya kuongea
yote nilihitimisha ibada iliendelea hakuna
aliyeondoka mpaka pale mchungaji alipotaka watu
warudi majumbani kwao.
Ibada ilifika mwisho ilikuwa saa tatu usiku, niliona
kupitia saa kubwa iliyopo kanisani pale, nilikuwa
nimevaa kanga sikujua nimevalishwa muda gani
kanga hiyo, watu walitawanyika huku mimi na
familia ya mchungaji tulibaki kanisani kusubiri watu
watoke , siku hii sadaka zilikuwa nyingi sana
zilizotolewa tuliondoka kanisani tukimuacha
mhasibu akizihesabu sadaka zile tulitoka nje ya
kanisa watu pia walikuwepo wengi walinipa pole
wengine wakinipa sadaka zao kisha tukaaga na
kuingia ndani ya gari ya mchungaji na familia yake,
tuliondoka kuelekea nyumbani kisha tulifika
nyumbani kwa mchungaji, walinikaribisha ndani kwa
wakati mwingine wakati huu nikiwa binadamu sasa,
tulipoingia mama mchungaji alinielekeza bafu
ambalo ningeweza kwenda kuoga na mimi nilienda.
Lilikuwa bafu zuri ambalo nilikumbuka niliwahi
kuliona hotelini tu bafu lenye kioo kizuri na maji
yatiririkayo kwa juu, nilipoingia sikuoga kwanza
nilivua nguo nilizokuwa nimevaa na kubaki mtupu,
nikaanza kujiangalia kwenye kioo, bado nilikuwa
siamini kama mimi ndio nilikuwa mnyama yani
mpaka mwili wangu tayari niliuhasi, nilidhani
pengine sitaweza kurudi kwenye mwili wangu
HAKIKA MUNGU NI MWEMA hakuna linaloshindikan
a kwake, wote mliolemewa na mizigo nendeni kwa
bwana atawapumzisha, sikuwa nikiamini kabla
kuhusu miujiza ukuaji wangu na kuishi kwangu mjini
nilikuwa nikiamini wale vilema, vipofu, vichaa na
wale wenye mapepo yawasumbuayo, nilikuwa
nikijua kuwa, wale ni watu tena wazima wa kila kitu
ni wachungaji wanawachukua na kupanga nao njama
za kujilemesha ili kuwaaminisha waumini wake
kuwa yeye anauwezo wa kuponya, wamuamini kwa
minajili ya kupata sadaka nyingi, ndivyo nilivyokuwa
nikijua siku zote, leo hii miujiza imenitokea mimi
mwenyewe kweli BWANA YESU ASIFIWE, niliendelea
kujitafakari bafuni kule.
“Kidawa,” nilisikia sti ya mama mchungaji akiniita
nilijua wazi alikuwa na wasi wasi kutokana na
ukimya wangu, nilimwitika na kumwambia natoka
sio muda mrefu,aliniambia pia nisicherewe chakula
tayari, nilipo mwitika nikarudi kwenye kioo, huku
mikono, nikipitisha kwenye nywele zangu ambazo
wakati huo zilionekana kuchakaa pia zilikuwa timu
timu, sikujiangalia sana nikaoga na kuhakikisha
nimetakata ndio nikatoka, nilipotoka tu mama
alinipokea na kunikabidhi nguo kisha kunielekeza
chumba cha kwenda kubadilisha nguo, alinielekeza
kisha nikaenda huko wakati huo watu wapo mezani
wakinisubiri, na mimi niliingia kwenye chumba kile
nikabadilisha nguo kisha nikatoka nikakaribishwa
mezani.
Nilichogundua familia hii ilikuwa na upendo zaidi,
walikuwa na upendo pia ukalimu, nguvu ya bwana
ilikuwa ndani yao nilipofika mimi, walifanya maombi
kwa ajili ya chakula tena mtoto wa mchungaji ndio
aliongoza maombi hayo mpaka pele alipohitimisha.
Nilikuwa na njaa sana wakati huo, hata tumbo langu
halikuacha kunipigia kelele ni sauti tu zilisikika
ndani ya tumbo zikiniisihi ‘tunataka chakula tunataka
chakula’ nilikuwa nikifananisha mngurumo watumbo
kama sauti zenye uhitaji wa chakula hapo nikaanza
kula baada ya kujichotea kwenye sahani.
ITAENDELEAA
 
SEHEMU YA 24
NA Gaooh TheAuthor
Simu 0654387935
LIKE ILI NIPOST SEHEMU INAYOFUATA
ILIPOISHIA SEHEMU ILIYOPITA
Nilikuwa na njaa sana wakati huo, hata tumbo langu
halikuacha kunipigia kelele ni sauti tu zilisikika
ndani ya tumbo zikiniisihi ‘tunataka chakula tunataka
chakula’ nilikuwa nikifananisha mngurumo watumbo
kama sauti zenye uhitaji wa chakula hapo nikaanza
kula baada ya kujichotea kwenye sahani.
SASA ENDELEAAA..
Nilikula chakula kile huku nikifurahia, hakuna aliona
furaha yangu ila mimi nilifurahia ni kitambo kirefu
kilipita bila kula chakula hiki wala kukaa sehemu
kama hii, nyama za kuku, na nyama ya ngombe
iliyokaangwa na biliani pamoja na rosti la nyama na
viubwagizi bwagizi ambavyo vilijaa pale mezani,
nilitafuna nyama kama sitakula tena, hata pale
nilipomaliza niliongeza tena.
Tulipomaliza kula chumba changu cha kulala
nilioneshwa tuliagana kila mmoja akaingia
chumbani kwake, chumba changu kilikuwa kizuri
tofauti na kile nilichopanga kule kagera, hakikuwa
na uzuri kama hiki. Ngoja nikwambie chumba hiki
kilikuwa simple rangi ya dhambalau ndio iliyopakwa
ukutani ndani kulikuwa na kitanda kikubwa cha
kisasa, kulikuwa na wardrobe kubwa iliyopo ukutani
kulikuwa na dressing table nzuri ya mbao yenye
kioo kizuri pia juu kulikuwa na ua zuri lililopachikwa
juu kwenye gypsum board, hata chini marumaru
zake zilikuwa zimewekwa kwa urembo yani
pembeni ziliwekwa za rangi nyeusi na kati kati
zikawekwa za kawaida nisikuelezee sana ukitaka
kujua njoo uone mwenyewe.
Usiku wangu ulikuwa mzuri sana tena cha ajabu
niliota ndoto eti nimekuwa tajiri namiliki gari zuri
aina ya BMW X7 hahaha ndoto hizi, nilipostuka
kutoka usingizini asubuhi hii nilijinyoosha huku
nikijikagua kama kweli ni mimi hakika nilikuwa
mimi pia nilikuwa si haba mtoto wawatu ni uchawi
tu ndio umenifuja ila nilikuwa mzuri bana
asikwambie mtu.
Niliamka na kutoka nje nikamkuta mama mchungaji
amekaa kwenye kochi akitazama habari asubuhi
hiyo huku mezani kwake kukiwa na kikombe sijui
kilikuwa na chai sijui kilikuwa na nini.
“Shikamoo mama,” nilimsalimu hapo akaacha
kuangalia tv akaniangalia mimi.
“Marahaba mwanangu,bwana yesu asifiwe”
“Milele amina” nilijibu
“Za tangu jana mwanangu, nilisema nisikusumbue
upunguze uchovu,”
“Ndio ushaisha mama,najiona mpya mama hakika
bwana Mungu ni mwema, najiona nimezaliwa upya,”
nilisema
“Ndio mwanangu ila kidogo leo tutakuwa na
mazungumzo na wewe mchungaji akirudi, ametoka
kidogo ila kwa sasa jiandae unywe chai kuna
sehemu twende,” mama mchungaji alisema
nilimuelewa vyema nikaelekea bafuni huko nilikuta
kuna boksi la miswaki pamoja na dawa nilichukua
msakwi na kuweka dawa kisha kuanza kupiga,
nilipomaliza nilioga kisha nikatoka baada ya
kumaliza niliingia chumbani kwangu sikuwa na nguo
hivyo nilivaa zile zile nilizopewa usiku wa jana,
baada ya kuvaa nikatoka na kukaa na mamapale.
“Chukua chai iko pale,” alisema. Hapo nikaelekea
mezani na kukuta mkate upo juu ya meza pamoja
na blueband nilichukua na kuanza kupakaa kisha
ilipoenea kote ndio nikamimina chai kwenye
kikombe na kuanza kunywa nilitumia muda
mchache nikamaliza, nilipomaliza nilitoa vyombo
kisha nikaenda mpaka pale alipo mama.
“Upo tayari mwanangu twende,” alisema.
“Ndio mama,”nilipomwambia akaamka na kuingia
chumbani kwake alitoka na mkoba wake huku
mkononi akishikilia funguo na kuniambia twende
tukatoka nje, hapo akaelekea kwenye gari yake
ndogo akanitaka niingie na mimi nikaingia kisha
mfanya kazi wa getini akafungua geti hapo gari
ikatoka na kuianza safari tulianza kuondoka na
kuikata barabara, sikuwa na muda wa kuangalia nje
nilitulia tu nikiangalia barabara hata mitaa
tuliyokuwa tukipita sikuwa nikiijua hata, tulienda
mpaka pale gari iliposimama. “tushuke tumefika”
mama alisema hapo tukashuka, tuliposhuka
nilishuhudia duka kubwa la nguo ambalo lilikuwa
limependezeshwa na bango kubwa liliopo nje kwa
juu ya frem hizi tukaingia, mama alinipa uhuru wa
kuchagua nguo nitakazo, nilichagua nipendazo japo
sikuchagua vinguo vifupi nilichagua nguo zenye
stara baada ya manunuzi wakati huo nilibadili nguo
na kuvaa mpya ambayo tulinunua dukani hapo
mama mchungaji alinisifia sana kwa muonekano
wangu, Mama mchungaji alifanya malipo tukatoka
na mizigo yetu ambayo tuliingiza kwenye gari kisha
safari ikaanza amabyo ilikomea kwenye mojan ya
saloon kubwa za kike huko nilienda kusukwa vizuri
nilipendeza zaidi hakika nilikuwa mpya, Kidawa si
ndio mimi bwana utanitaka!, tulipotoka saloon
hatukurudi nyumbani, tulipitia kwenye moja ya hotel
kwakuwa muda ulishasogea, hivyo tulienda hapo
ilikupata chakula cha mchana.
Tulifikla sehemu kisha tukakaa, hapo mama
alimwita mhudumu akaniambia niagize chakula
niliagiza naye akaagiza cha kwake.
“Mwanangu kuna jambo nilitaka nikueleze,”
“jambo gani hilo mama?,” niliuliza.
“Tumekuja kukaa hapa ili tuongee mwanangu sisi
kama wasichana japo najua hapo badae tutakaa na
kuongea na mchungaji,”alisema
“Ni sawa tu mama tuongee,” nilimbia nilimwambia
huku chakula tayari kilifika kabla hatujakula simu
yake iliita.
“Triiiiiiiii triiiiiiiiiiii,” ilitoa mlio hapo aliitizama simu
yake kuangalia mpigaji.
“endelea kula nakuja ngoja nikaongee na hii simu,”
mama mchungaji alisema na kuamka na mimi
sikusubiri arudi nilianza kula kama vile alivyosema
nisimsubiri niendelee kula, sikujua alichoenda
kuongea huko ni nini?, ila nilichojua ni kuwa
alichoenda kuongea ni cha muhimu zaidi ndio mana
hakutaka kuongea mbele yangu kwa vile haikuwa
ikinihusu basi niliacha umbea wa kutaka kujua
alichoenda kuongea, niliendelea na kula huku macho
yangu yakipepesa pepesa pembeni kuangalia huko
na huko.
Dakika kadhaa mama mchungaji alirudi, alikuwa na
haraka zaidi alipofika alishika mkoba wake.
“Mwanangu twende, mimi sitakula tena tuondoke
nimepigiwa simu hapa ya dharurla hivyo twende,
ngoja nikafanye malipo pale,” alisema, nilishangaa
ila sikutaka kujua mana nilijua hayanihusu alikuja
tukaondoka, safari haikuwa ndefu sanan tulifika
nyumbani tukaingia ndani mfanya kazi wa getini
alishangaa kuniona hakuacha kunisifia
nilivyopendeza nilimshukuru, kisha tukaingia ndani
nikiwa na mizigo yangu, tulipofika ndani mama
aliniambia kuwa yeye anatoka amenifikisha mimi
yeye anaenda sehemu, sikutaka kumuuliza chochote
mana nilijua hayanihusu, alipotoka nilibaki peke
yangu nyumba nzima nilingia chumbani kwangu
huku nikijaribu zile nguo nilizokuwa nimenunuliwa,
sikuwa na njaa kabisa hivyo nilishinda chumbani
ikanibidi nipumzike nililala mana sikuwahi pata
amani na furaha kwa muda, nililala kwa saa kadhaa
hadi pale mlango wangu ulipoanza kugongwa
nilistuka usingizini kisha nikashuka kitandani baada
ya kusikia sauti ya mama mchungaji, nijiweka sawa
kisha nikatoka nje ya chumba changu tulisalimiana
akanipa pole ya upweke alioniacha nao.
Hapo aliniambia kuwa twende jikoni tukasaidiane
kupika hata mwanae alisharudi kutoka shule alirudi
nae, ndipo tukaelekea jikoni kuandaa chakula
nilitaka kumuuliza mama alichotaka tuongee kule
hotelini, sijui nini kilinizuia nikashindwa kuongea
ikanibidi ninyamaze, tuliendelea kupika mpaka
tukaivisha chakula kile baada ya kuivisha wote
tulijumuika mezani kwa ajili ya chakula.
Chakula kilikuwa kitamu baada ya kula na kusaza
wote tulifrahia hapo sasa mtoto wa mchungaji
alikuwa akianza kusinzia hivyo aliperekwa kulala
tukabaki watatu yani mimi mama mchungaji na
Mchungaji wafanyakazi wake hakuwa akiishi nao
sikujua ni kwanini ila hayakunihusu hayo.
“Umekuwa na siku nzuri sana leo, mke wangu
aliniambia mmeenda kufanya manunuzi,”
“Ndio baba nimefurahi sana leo, nimepata amani
amabyo sikuwahi kuipata kabla,muda wote
najiwazia pengine saahizi ningekuwa nikitanga tanga
mtaani nikitafuta chakula, ila bwana ameniita na
kunionyesha kwenu,” nilisema
“Ni kweli mwanangu kwa Mungu hakuna gumu
asiloweka kulitenda japo anaweza kucherewa ila ni
lazima atende, najua ni nguvu ya Mungu ndio
imekuvuta mpaka ukaja kanisani kwangu,”
“Ni kweli baba nikikumbuka njia nilizopita mpaka
kufika kanisani hazikuwa rahisi nilipitia changamoto
nyingi baba..” nilielezea kwa sauti ya simanzi hapo
kikao kiliendelea lengo la kikao lilikuwa ni kutaka
kujua undani wa maisha yangu .
Nami sikusita nilielezea kinaga ubaga kila kitu
kuanzia nilipokuwa nikiishi na niliyofanya,tuliongea
mengi sikuhiyo, nao walielezea ukuu wa MUNGU na
maajabu yake na weka anaotenda kwa binadamu,
hakika tulijua zaidi tukapanga kesho ya siku hiyo
twende kwenye nyumba ambayo nilikuwa
nimepenga, baada ya kuhitimisha maongezi kila
mmoja aliingia kwenye chumba chake baada ya
kuagana.
Kulikucha asubuhi na mapema baada ya kimya cha
usiku mzima, siku hii niliwahi kuamka nikifanya kazi
za ndani nilisafisha nyumba kila sehemu kisha
nikaandaa na chai nikaweka mezani, mama
mchungaji alitoka alishangaa kuniona nimefanya
kazi peke yangu za nyumba nzima, alifurahi sana.
 
SEHEMU YA 25
NA Gaooh TheAuthor
SIMU=0654387935
TULIPOISHIA SEHEMU ILIYOPITA
Kulikucha asubuhi na mapema baada ya kimya cha
usiku mzima, siku hii niliwahi kuamka nikifanya kazi
za ndani nilisafisha nyumba kila sehemu kisha
nikaandaa na chai nikaweka mezani, mama
mchungaji alitoka alishangaa kuniona nimefanya
kazi peke yangu za nyumba nzima, alifurahi sana.
SASA ENDELEAAAAA..
Tayari mtoto alimwandaa hivyo alitoka na baba yake
ambaye ni mchungaji tulisalimiana,akiniuliza
usikuwangu ulivyokuwa pia akiniuliza kama
nimeamka salama, hapo wakapata kifungua kinywa
pamoja.
“Kidawa kwa vile mimi bado wiki hii ninavikao basi
wewe utaenda na mama yako mkaangalie, sehemu
uliyokuwa ukikaa mwanzoni, naomba mimi niwaage
bado nina vikao nadhani vikiisha tutapata wasaa
mzuri wakuwa pamoja tufundishane neno,” alisema
aliposema hivyo mama aliniangalia, aliponiangalia
haikunifikilisha sana nilijua ni kawaida tu.
Baada ya kumaliza kupata kifungua kinywa walitoka
nikabaki na mama,hakuniuliza chochote na mimi
nikajua hakuna tatizo lolote, hapo nilimaliza
shughuli zote za siku hiyo kisha mama aliniambia
nikajiandae ili twende mapema, nilienda kujiandaa
nikavaa nguo zangu nzuri za kupendeza, baada ya
wote kuwa tayari tuliondoka na kuingia ndani ya gari
kuianza safari kwenda magomeni kagera nilipokuwa
nakaa mwanzo.
Tulitoka nyumbani hapo, baada ya foleni kadhaa
tulifika magomeni kagera nilimwelekeza mama
mchungaji mpaka kwenye njia ambayo
angesimamisha gari kisha tungeingia kwenye
vichochoro ambayo ingetufikisha huko, baada ya
kufika pale alisimamisha gari hapo nilimwambia
kuwa anisubiri niende kisha nitarudi baada ya muda,
kweli alinielewa nikamuacha kwenye gari, hapo
nikatoka na kuingia kwenye kichochoro ambacho
ndio njia ya kwenda nyumba niliyopanga mwanzo,
nilitumia dakika chache mpaka kufika kwenye
nyumba ile nilipofika ilikuwa ya tofauti sana yani
haikuwa kama mwanzo nilishangaa kuiona ilifanyiwa
marekebisho ikiwemo kupakwa rangi mpya,
nilibisha hodi na kuingia ndani baada ya
kukaribishwa, nilipoingia kulikuwa kwa tofauti sana
cha kushangaza kile chumba ambacho nilikuwa
nikikaa mimi kilikuwa na panzia jipya tena alitoka
mtu ndani yake, nilishangaa alikuwa ni mdada
tukasalimiana, hapo niliulizia mwenye nyumba, hapo
niliambiwa kuwa nyumba imeuzwa na alieinunu kwa
sasa alikuwa akikaa nje ya nchi KENYA nilishangaa
kusikia hivyo niliulizia baadhi ya wapangaji
nikaambiwa hawapo walishahama bada ya
kushindwa na bei mpya ya kodi, hivyo baada ya
kushindwa kulipa ikabidi wahawame niliwauliza
kuhusu chumba kile kama walikuta vitu vyangu
nilijibiwa kuwa hakukuwa na kitu zaidi yab sofa
ambalo limewekwa pale nje, hapo ikabidi nitazame
nilitizama kushoto ndipo nikashuhudia kochi langu
likiwa limechoka hata sponji yake ilikuwa
imenyambuka nyambuka, mvua na chua ndio
vilikuwa vyakula vyake, NILICHOKA sikuwa na jinsi
ikanibidi niage, niliwaaga na kuwaambia kuwa
nitarudi tena.
Niliondoka nyumbani pale huku nikiwa hata nguvu
za kuendelea kutembea zimekata nilijilazimisha tu
mpaka kulifikia gari la Mama Mchungaji hapo
niliingia.
“Vipi mwanangu mbona kama huko sawa
kunaendelea nini huko,”aliuliza akiwa na wasi wasi.
“Mama yani nimefika kule vitu vyangu hakuna hata
nyumba pia iliuzwa kwa mtu mwengine vitu vyangu
wakavitelekeza,”
“Pole mwanangu usijali ni hali ya kawaida,” “utapata
vyengine,” aliendelea kusema.
“Asante mama najua ni mapito tu haya
yatapita,”nilimwambia hapo aliwasha gari kisha
kugeuza, kurudi tulipotoka tukiwa njiani sasa hapo
ndio mjadala ulianza.
“Kidawa,” aliniita,
“Abeeh mama,”niliitika.
“kuna kitu nataka kukwambia ila kila nikijaribu
kuanz a, nakosa nguvu za kuendelea.”
“Kitu gani mama, kwani kunatatizo gani mama,”
nilimtaja mara mbili mbili.
“Mwanangu, ila ngoja tukifika nyumbani tukikaa,
nitakuambia mana hapa naendesha nikianza kukbia
na tupo barabarani ni hatari,” alisema, alianza katika
sintofahamu mana nilipata shauku ya kutaka kujua,
ila kwa vile alisema atanambia tukirudi nyumbani
basi sikumuuliza tena nilikaa kimya akabadirisha
mada.
“Hivi unaweza kuendesha gari?” aliuliza.
“Gari ndio najaribu jaribu ila bado sijakuwa dereva
mzuri,”
“Hahaha” tlicheka pamoja.
“Kwahiyo umekuwa dereva wa maneno,” alisema
mama hapo nikacheka tena.
“Mbona naendesha mama,”
“Nishuke uje uendeshe wewe nikuone,”
“Hapana mama sijaendesha muda mrefu nishaanza
kusahau baadhi ya vitu,” nikjitetea, hapo alibadilisha
story akaleta nyingine kabisa story hii ndio
ilihitimisha safari yetu kwani alipiacha ilitusogeza
mpaka nyumbani ilikuwa ni story kuhusu miujizo
aliyofanya baba mchungaji alipda kwenye tamasha
la ufunuo huko sumbawanga alinielezea ulifanya
ufunuo kwa watu ambao walikuwa na matatizo pia
kuna watu waligeuzwa mawe arudisha pia wachawi
wengi alijisalimisha mbale ya Mungu, story hii ndio
ilihitimisha safari tulifika nyumbani, kila mmoja
alitanga kuchoka si mimi wala mama mchungaji
wote tulikuwa tumechoka hivyo tuliagana akasema
anaen chumbani kuoga.
“Ngoja nikaoge mwanangu nawe pia unaweza
kwenda kupumzika nikitoka tutapika” alisema.
“Sawa mama,” nilimwitika akaingia ndani, nilitamani
sana kwenda ndani kupumzika ila niliona hakuna
sababu ya mimi kwenda ndani, eti na mimi none
boss haha, eti kama ile ndoto haha hapana,
niliweka uster duuh pembeni alijisemea yule kibaka
wa salenda alietaka kuniibia na wenzake eti
akisema mimi sister duh the the, wote huo niliuacha
nikaingia jikoni kwa vile kila kitu kilikuwa ndani
niliosha mchele hapo nikaeka ndani ya rice cooker
kisha nikachukua nyama ambayo ilikuwa kwenye
friji, nilichukua na viunge vyake nikakata kata vizuri
kwa ajili ya kupika baada ya muda tayari nyama
ilikuwa ikichemka huku nikisubiri wali uive
nikachukua soseji na kuzipasha, nilisubiri dakika
kadhaa kabla mama hajatoka tayari chakula kilikuwa
tayari niliweka kwenye hotpot na kupereka mezani
ilikuwa mchana japo jioni ilikuwa nayo ikikaribia ni
kwenye saa nane fulani hivi na nusu, nilipomaliza
kuweka mezani nikaingia bafuni kuoga, yani muda
wote nimeingia bafuni mpaka natoka bafuni mama
alikuwa bado ndani, ikabidi nimwite.
“Mamaa mamaaa,” nimwita hapo aliitika kwa sauti
ya chini, kisha mlango ulifunguliwa alionekana
mchovu sana.
“Ooh, pole mwanangu, nilipotoka kuoga nimepitiwa
na usingizi nimechoka kweli yani kama usingenistua
ilikuwa nilale mpaka usiku.”
“Pole mama chakula tayari,”
“Umepika?”aliuliza.
“Ndio mama nimepika, niliona muda ule ule niingie
ndani nipike tu.”
“Asante sana mwanangu, japo nilikwambia unisubiri
tuje kupika wote siunajua we bado mgeni, nilijua
majiko yatakusumbua kwenye kupika,” alisema
hapo nikacheka kimoyo moyo eti majiko siwezi
kutumia chefu mama mchungaji ananiona mie
mshamba haha’ nilijisemea akaniambia nitangulie
yeye anavaa atoke, nilimwacha na mimi nikarudi
mezani hazikupita dakika nyingi alikuja kisha
tukakaa pamoja muda huo tulikuwa wenyewe baba
mchungaji na mtoto wao hawakuwepo, hivyo tulikula
huku mama mchungaji akikisifia chakula
nilichopika.”Kumbe nawe fundi hivi mwanangu,’
“Kawaida mama sijawa fundi mzuri bado,” nilisema
hapo tukacheka pamoja.
“Inamana hata chakuaa hujakuwa fundi mzuri bado,
gari pia hivyo hivyo lini utakuwa fundi mzuri sasa,”
alisema sikuwa na jibu, nikaamka kisha nikamimina
juisi ya embe kwenye glasi yake na mimi
nikajimiminia, tulikunywa ikiteremsha chakula chetu
taratiibu, baada ya kumaliza ndipo tulipata wasaaa
wa kukaa wakati huu nilivunja ukimya ule woga wa
kumuuliza sasa niliutoa, nikauvaa sasa uhalisia
wangu ikabidi nimuulize mama, hapo ilinijie na ile
kumbu kumbu ya mama MCHUNGAJI kuniangalia
wakati Baba MCHUNGAJI akiniambia maneno yale
ya kuwa akimaliza vikao tutapata wasaa mzuri wa
kufundishana neno, japo mwanzo nilitaka kusahau
ila kumbu kumbu hii ndio ilinisukuma kuuliza.
“Mama nakukumbusha ulisema utanambia tukifika
nyumbani, ndio tumefika sijui unaweza kuniambia
mana nimekuwa na wasi wasi muda wjambo hilo,”
nilisema kwa sauti ya chini iliyojaa unyenyekevu,
niliamini siku zote ili upate unachohitaji kwa mtu
jitahidi kujishusha kabisa uwe chini ndio utapata
unachohitaji.
“Ni kweli mwanangu ila sio mambo makubwa sana,
kwanza nilitaka tu kujua unampango gani wa
maisha utakaa kwetu mpaka lini?,”
 
SEHEMU YA 26
NA Gaooh TheAuthor
SIMU 0654387935
ILIPOISHIAA SEHEMU ILIYOPITA
“Mama nakukumbusha ulisema utanambia tukifika
nyumbani, ndio tumefika sijui unaweza kuniambia
mana nimekuwa na wasi wasi muda wjambo hilo,”
nilisema kwa sauti ya chini iliyojaa unyenyekevu,
niliamini siku zote ili upate unachohitaji kwa mtu
jitahidi kujishusha kabisa uwe chini ndio utapata
unachohitaji.
ENDELEEAAAA SASA
“Ni kweli mwanangu ila sio mambo makubwa sana,
kwanza nilitaka tu kujua unampango gani wa
maisha utakaa kwetu mpaka lini?,” alisema huku
akiendelea hapo kidogo nilikaa makini kusikiliza
maneno yake mana sikujua dhamila yake. “kama
huna muelekeo wa maisha naweza kuongea na
mume wangu au hata mimi mwenyewe nikakupa
pesa ukapange chumba ili uanze maisha yako,”
aliposema hivi kidogo nikatabasamu, ila aliendelea.
“Usinielewe vibaya hivi ushawahi jiuliza kwanini
nyumbani kwetu hatuna dada wakazi wala
watumishi wale wa kanisani?, mwanzoni tuliishi na
wafanya kazi wawili pia tuliishi na masister pia ila
Ndoa yangu iliingia matatani sitakwambia kwanini
ila najua unajua udhaifu wa wanaume, mimi sipendi
tufikie mwisho wa ndoa yangu na mume wangu,
najua udhaifu wake” mama aliendelea kuongea
mengi zaidi akinipa historia ya yaliotokea nyumbani
kwako japo mwanzo alikataa kusema ila wakati huu
alisema sijui ndio kuweka msisitizo, alisema zaidi.
“ Hivyo nakuomba mwanangu unielewe, usiendelee
kuishi na sisi hapa mi nitakupa mtaji ili ukaanzishe
biashara yako.”
“Mama ni kweli, nami sikupenda kuendelea kuishi
nanyi hapa miaka yote nilitamani nikaanze maisha
yangu ila kam unavyojua hali yangu, mi naomba
unipe muda nikae kae hapa nyumbani kisha
nitafanya unavyotaka.
“Hapana kidawa mi nilitamani uondoke hata ….”
Aliposema hivyo alistushwa na simu yake ilipotoa
mlio, ikabidi anyamaze kuongea kisha akaishika
simu yake na kuanza kuongea, alikuwa akiongea
huku akitaja “bwana yesu asifiwe” sikujue
anayeongea nawe wala taarifa aliyopewa sikufatilia
mana nilijua haikuwa ikinihusu, umbea niliaachaga.
Baada ya maongezi yale ambayo yalikatishwa na
simu japo alishaniambia kila kitu, nilibaki
nikitafakari, kitu pekee nilichotafakari usiku wa siku
hiyo baada ya kumaliza kazi za kutwa sambamba
na kula pamoja mezani na mchungaji na mtoto wao,
hivyo nikiwa kitandani ndio nilianza kuwaza mambo
yale. ‘NINI HATMA YA MAISHA YANGU’ Nilisema
kwa sauti kubwa ambayo haikuhitaji kuongezwa
niliamini inatosha, nilisema nikiwa nimeshika kichwa
changu kwa nyuma na mikono miwili huku nikiwa
nimelala chali uso ukitazama juu, hata taa haikuwa
ikiwaka hizo nilitazama juu nilichokuwa nikiona ni
giza tu, ndio niliweka urafiki nalo giza kunisaidia
kutatua na kung’amua yale yote niwazayo
yalioninyima usingizi na kuondoka nae huko pasipo
julikana, haha alafu nimekumbuka hivi wale watu
wasiojulikana washaanza kujulikana mana watu
wasiojulikana bado hawajulikani, tuyaache hayo.
‘hivi mama mchungaji ni kwamba hana imani na
mimi kuishi hapa kwake, inamana matukio yangu
yaliopita ndio, chanzo cha yeye kutokuniamini, ila
mbona anaonekana na roho nzuri tu. Mbona
nikimtazama anaonekana amejaa hofu ya Mungu,si
ndio yeye alimpa maeno ya matumaini mchungaji
kipindi nina taswira ya paka, kisha akanikaribisha
ndani kwake leo imekuache au ni baada ya kujua
mimi ni msichana ndio imani yake imeshuka,
nilijisemea mwenyewe, huku lindi la mawazo
likinijaa kichani, potelea pote nilichukua shuka langu
na kujifunika gubi gubi, mpaka kuna kucha, nilistuka
mapema baada ya kusikia jogoo likiwika niliamka
na kufanya kazi za nyumbani hapo nilijiaminisha
kuwa nikijipendekeza kufanya kazi zote kwa moyo
basi mama Mchungaji ataondoa imani yake potofu
na kuniamini kisha kunifanya kama mtoto.
Kweli kazi zilikuwa nyingi ila nilijitahidi kama
mwanamke washoka nikapambana nazo nikiwa ndio
naosha vyombo baada ya kumaliza kudeki sebuleni
na kufuta vioo, hapo nikiwa jikoni ndio mama
mchungaji alikuja.
“we kidawa mbona unatusumbua inamana hujui
kama muda huu tumelala,?” alisema.
“Hapana mama sijapanga kuwasumbua, nimeona
nifanye kazi mapema ili mkiamka mkute kila kitu
tayari hata baba akitoka akute chai tayari
nimeiandaa anywe na mtoto,” nilisema huku
nikitetemeka hata vyombo niliacha kuosha
nikimuangalia.
“Wewe ndio mama mwenye nyumba?, je
nimekutuma uoshe hivi vyombo?,wewe ndio mfanya
kazi bora sana ambae unafanya kazi hata ambazo
hujaambiwa ufanye?” alisema mama mchungaji
hapo nilimwangalia kama nisie amini pengine labda
sio yeye, lakini macho na masikio yangu
viliniaminisha kuwa ni yeye kuanzia sura mpaka
sauti vilikuwa vya kwake looh! Kidawa mimi.
“Nisamehe mama yangu, sijapenda iwe hivi,”
“Msyuuuuuuuuuuuuu,” alisonya kisha kuondoka pale,
sonyo lake liliamsha kule machozi yangu
yalipokuwa yamelala, yalianza kuserereka kwenye
mashamvu yangu, sikuwa na leso nilitumia tu
mkono kufuta macho yangu, SIKUKOMA.
Niliendelea kuosha vyombo vile, huku chai
ikiendelea kuchemka ambayo nayo nilibandika,nil
iosha hima hima nisije kutwa kisha ikanibidi niende
kuoga wakati nikielekea bafuni nilisikia kelele, sio
kelele za kupiga au kelele zile za nanilii mlizo zoea
kuzisikia hapana, zilikuwa kelele za majibishano
tena sauti ya kike ndio ilikuwa ikiongea, japo
niliacha umbea ila hili sikutaka linipite ikabidi
nisogee pale mlangoni nikaskie.
“SITAKI SIMTAKI KIDAWA AENDELEE KUKAA
HAPA,UTATAFUTA KWA KUMPEREKA.”
“Mke wangu, ebu jitahidi huyo pepo mchafu kumtoa
ebu kemea kwa jina la yesu Kidawa mbona binti
wawatu ni mzuri tu hana, mambo mengi anafanya
kazi vizuri,”
“Hizo sifa unampmba wewe hata kama anafanya
kazi ila kama ningekuwa na shida ya binti wa kazi
kule kwetu marangu wamejaa tele, wakiina manka”
nilisikia ila niliona wakati huuu nitasikiwa hivyo
ilinibidi niondoke mlangoni pale, niliingia bafuni
hata hamu ya kuoga sikuwa nayo, hata pale
nilipojitahidi kujimwagia maji, nilijihisi hata maji
hayaniloweshi mana akili haikuwepo sehemu hiyo
muda huo, nilionelea ni bora nitoke tu hapo
nilipotoka niliingia chumbani kwangu na kufunga
mlango kabisa.
Ngoja niwaambie kitu.. unajua familia nyingi
uzionavyo nje ni tofauti na ndani, unaweza kuta
familia kwa nje inaupendo wanaishi vizuri mpaka
ukayatamani maisha yao uishi wewe,kumbe hujui
nyuma ya pazia changamoto wazipitiazo, hata mimi
japo sijakaa siku nyingi hapa ila nimeshaanza kuona
ndoa hii ya baba mchungaji na mama mchungaji
isivyo na baraka, ule upendo niliouona siku ya
kwanza sikuamini kumbe wanakorofishana hivi
looh! Ndoa zinamambo mengi asikudanganye mtu,
japo kuficha ya ndani ni vizuri zaidi japo haisaidii ni
sawa na kuficha moto na gunia hapo lazima moshi
utakuumbua tu au gunia litaungua kabisa.
Nilikaa kitandani akili yangu ikiwa haipo kabisa,
muda wote niliokuwa ndani sikusikia nikiitwa si
mama wala baba, sikujali nilitoka ndani kwangu
kulikuwa kimya hata milango ilifungwa kwa nje yani
kana kwamba hakuna mtu ndani, NILICHOKA.
Hapo nikaenda mezani nikitegemea nitakuta chai
ambayo niliipika, looh sikuamini hakukua na chai,
na friji pia lilifungwa na funguo hata umeme
haukuwepo ulizimwa looh kidawa mimi.
Hata njaa nayo ilijenga makazi tumboni kwangu,
vyakula hakuna. Niliona isiwe kesi hata maji
yatosha ndipo nikawa naelekea store ambako
kunakuwaga na ndoo za maji looh, kitasa
kilisimama kikinilaki mlangoni na mimi nikaamini
kinanikaribisha kwa tabasamu looh! Nikifinye sasa
niingie ndani chafunguka sasa!, hakikufunguka
kikimaanisha kimefungwa, sikuwa na chengine cha
kufanya kama ni simu ambayo ningeweza kufanya
mawasiliano ili nipate msaada sikuwa nayo, kitu
pekee ambacho kilikuja akilini kama wazo eti
nikanywe maji yale ya kuoga chooni kwa vile
hayakuwa mabaya yalitoka juu ya tenki, kidogo
wazo hili nililipa maksi na kulitii nilijipereka mzima
mzima kuufata mlango wa chooni huku nikichekelea
kimya kimya eti nafurahia amenifungia kote kasahau
chooni ambako hata maji naweza kuyapata.
FUNGUA SASA si nikashika mlango wa chooni
nifungue nao wafunguka sasa, looh! Kweli
nimepatikana kidawa mimi.
 
SEHEMU YA 27
NA GAOOH
SIMU =0654387935
ILIPOISHIAAA SEHEMU ILIYOPITA
kidogo wazo hili nililipa maksi na kulitii nilijipereka
mzima mzima kuufata mlango wa chooni huku
nikichekelea kimya kimya eti nafurahia amenifungia
kote kasahau chooni ambako hata maji naweza
kuyapata. FUNGUA SASA si nikashika mlango wa
chooni nifungue nao wafunguka sasa, looh! Kweli
nimepatikana kidawa mimi.
SA ENDELEAAAA.
Mlango pekee niliachiwa ni wa chumbani kwangu,
naamini hata jikoni kungekuwa na mlango pengine
ungefungwa, nilijipa ujasiri na kurudi ndani kwangu,
nilichoka hata kuwaza kitu pekee nilichoamua ni
kulala.
Mungu hamtupi mja wake baada ya kujilazimisha
kulala kisha kupata usingizi, Mungu alivyowaajabu
usingizi wangu ulinipa chakula,ndio ulinipa chakula
usishangae basi kulala kwangu kulifanya niote ndoto
za vyakula ambavyo nilifakamia ndotoni kisha
nikashiba hahahahahahaha’,Mama mchungaji
hajanikomoa Mungu wangu ananipenda bado, baada
ya muda kadhaa niliamka nikitoka usingizini, hapo
nilijidhoosha huku nikipiga miayo haikuwa njaa bana
msijesema sijashiba nilishiba chakula nilichokula
ndotoni, niliamka huku nikijawa na uchovu hapo
nikatoka nje tayari kiza kilikuwa kimekaribia
nilipotoka nilimkuta mama MCHUNGAJI akiwa jikoni
anapika nilimuona kwa mbali ikanibidi nimfate.
“Shikamoo mama,”
“Kua nawe upate yako, chefuuu,”
“Mama kwani kuna kibaya chochote
amabchonimefanya,”
“Utajua mwenyewe, tulikusaidia ulitakiwa baada ya
kupona upaka wako uondoke urudi ulipokuwa
ukiishi sio kukaa kwangu,”
“Mama sijakataa najua hapa sio kwetu wala
sikuzaliwa hapa mama, nimekaa tu kwa hifadhi
mama yangu ya muda.”
“Umeshinda nini kwenda kutafuta hifadhi huko nje
ukajileta hapa kwetu, nimekuvumilia jana wanipereka
pereka na kama sio mume wangu nisingeenda
kukununulia hata hizo nguo ulizovaa Mbwa
wewe,”Mama mchungaji ndio tumefikishana huku,
nilijiwazia hata nguvu za kuongea tena tayari
nilishazikosa, niliamua kuondoka mpaka kwenye
sofa nikalaia pale nikitizama runinga muda wote
nilikosa amani ,hata pale kwenye kochi nilipokaa
nilishikilia tama tena wakati huu hata kile chakula
nilichoshiba ndotoni tayari kilishaisha tumboni,
Mtoto wa maam mchungaji na baba mchungaji nae
alikuwa amekaa mezani hakuwahi kuniongelesha,
alionekana kutokuwa na heshima mbali na miaka
yake saba.
Sikumjali kwa vile nilijua ni mtoto bado hajajua
maana ya maisha,wakati nikiwa pale kwenye
makochi hata machozi yalikuwa yakinitiririka
MTIHANI huu niliona mkubwa sana.
“Ooh, kidawa mzima mwanangu,” nilisikia sauti
hapo ikabidi niamshe kichwa kuangalia ndipo
nikakutana uso wa baba mchungaji uliojawa na
tabasamu,.
“Mzima baba, shikamoo,” nilimsalimia naye aliitika
huku akinitajia maswala la yesu akimtukuza na
kusema mazuri yake ya kutia moyo, nilifurahi kiasi
hapo alipereka mkoba wake chumbani kisha kurudi
na kukaa mezani wote tukajumuika kupata chakula
baada ya maombezi mara kwa mara mama alikuwa
akiniangalia, muda huo mchungaji akielekezea
changamoto anazokumbana nazo katika kazi yake
ya kumtumikia bwana akitupa kama story,kutokana
na mama kuniangalia mara kwa mara niliamua kula
nikiangalia chini, baada ya muda kadhaa mama na
mwanae waliondoka huku wakiwa wamefura.
“Vipi mke wangu umeshida,”baba mchungaji aliuliza
huku akimtazama mkewe.
“Ndio tumeshiba pia tumechoka,” alihitimisha na
kuondoka baada ya kunawa.
Walipoondoka tulibaki wawili mimi na baba, baba
MCHUNGAJI alionekana mwenye simanzi sana,
hakuwa na furaha japo nje alionekana mwenye
furaha ila ndani hakuwa na furaha kabisa na hata
kama anayo basi ni kidogo.
Tulikaaa kimya wote kila mmoja akiwabusy na
sahani yake ni vijiko tu ndio vilisikika kuongea.
“Mwanangu,” baba mchungaji alivunja ukimya,
niliogopa hata kumuongeresha.
“Abee baba,”
“Najua siku ya leo imekuwa ndefu sana
kwako,hakuna nisichokijua mwanangu najua
umefungiwa ndani na ninajua mke wangu
hakupendi.” Mchungaji alisema hapo akaendelea
mimi nikiuvaa ukimya..
“Mke wangu ni mbinafsi pia mchoyo na hata roho
mbaya pia anayo kuna muda nawaza labda wivu
lakini kama ni wivu mbona amefukuza mpaka
wanaume,wamewahi kuiishi watu wengi hapa kwetu
wavulana wasichana lakini aliwafukuza,sikuwahi
kujua sababu, ni mengi sana mke wangu amefanya,
visilani visa vya hapa na pale. Hakika ndoa yangu
haina furaha Mwanangu, najua wengi wanafurahia
kuwa pamoja kwetu wanatuona tunafuraha, na kweli
mke wangu kanisani tukiwa pamoja hata nje kwa
macho ya watu anakuwa mwema sana ila ndanio
tatizo mara nyingi natamani hata nisafiri nikakae
hata muda mrefu ndio nirudi lakini inashindikana
kanisa linanihitaji,” mchungaji aliongea huku akitoa
kitambaa chake kisha kujifuta usoni.
“mwanangu kama tutapata siku ambayo tutaongea
vizuri nitakuelezea mengi mwanangu hapa si
sehemu sahihi ya kuongea. Nakuomba kesho
asubuhi uondoke mwanangu nitakuachia kiasi
kidogo cha pesa za kujikimu na kuanzia maisha
sitopenda wala kufurahishwa nikikuona unateseka
hapa, nakuomba usijihisi vibaya mimi niko upande
wako sijakutenga pia siwezi kukutenga, shika hii
weka pia namba yangu hii kama itatokea
hatutaonana basi ukiondoka ujitahidi kunitafuta”
baba alisema kisha akaondoka kuelekea
chumbani,hapo nilizichukua pesa zile bila hata
kuhesabu nikazichomeka kwenye sidilia yangu,
kisha sikufanya ajizi mbali na masimango ila
chakula chake wakati huu nilikula huku nikilamba
lips zangu kwa utamu wa chakula kile cha Mama
Mwenye roho mbaya.
Kwavile mimi ni msichana tena ambaye bado
nategemea kuolewa, hivyo niliamua nitoe vile
vyombo mezani mwaya chakula cha watu nimekula
basi nikaoshe vyombo, nilivichukua na kwenda
navyojikoni ambako kuna sinki la kuoshea vyombo,
niliviosha kwa umakini huku nikihofia kuvunja ila cha
kushukuru nilimaliza vizuri hapo nikapanga vyombo
kwenyekabati “oohghoohh’nilibehua kweli saa hii
nilishiba tofauti na ndotoni, baada ya kumaliza
nikaingia chumbani kisha nikachukua kanga baada
ya kuvua nguo zangu ili nikaoge, leo ilikuwa kama
jana tofauti zilikuwa ni siku tu ila ni vile vile yani
wakati naenda bafuni nilisikia sauti kama jana hapo
nikaenda tena kusikiliza.
“Unajifanya unmjali sana KIDAWA yani sisi
tumeingia ndani wewe ndio kwanza umebaki nae
mtongozane sio?”
“Mke wangu kwani unashida gani na msichana
wawatu ebu nambie leo unanini kinachokusumbua,
nataka nikusikilize,”nilimsikia baba mchungaji.
“Kinachonisumbua ni kumuona huyu malaya wako
hapa nyumbani, simtaki, na pia nataka kesho
asubuhi nisimuone,” maneno ya mama niliyasikia
hapo sikutaka kusikiliza tena niliingia bafuni
nikaoga haraka haraka na kutoka hapo nilikimbilia
chumbani kwangu nilianza kupanga nguo zangu
kwenye begi, eeh begi langu lilikuwa ni mfuko ule
ambao nilinunuliwa nguo, kule dukani baada ya
kupanga vizuri, hapo nikajitupa kitandani hata mwili
wangu ulinitangazia kuwa umechoka, mimi ni nani
nisiutii niliutii nikajilaza, ila kabla sijalala
nilikumbuka ile hela ikabidi nitoe nguo zote mana
nakumbuka baada ya kuvua nguo sijaiangalia ooh
nilitoa nguo zote ambazo nilikwisha zipanga mpaka
nikaifikia ile ambao ilikuwa na hela nikazitoa kisha
nikaanza kuhesabu zilikuwa nyekundu nyekundu
sidhani hata baba alihesabu wakati ananipa, ndipo
nikahesabu zilifika laki nne japo hazikunitosha kwa
matumizi makubwa ila nilishukuru hapo sasa
nikaanza kupanga upya nguo zangu nilipomaliza
nikajilaza kitandani pesa zile nikiziweka kifuani
kwangu kisha nikalala bila kujali, hakika nililala kwa
amani zaidi.
Nilistushwa na sauti za honi nje za magari, hapo
niliamka baada ya kuamka cha kwanza kilikuwa
kuangalia zile pesa ooohhh Mungu wangu hazikuwa
kifuani kwangu tena pesa zile, sikuamini nilishuka
kitandani nikatimua nguo kuangalia kama zipo looh,
hazikuwepo hapo ndio nikajaribu kufungua mlango
ulikuwa wazi kabisa, ndipo kumbu kumbu zangu
zikanikumbusha kuwa sikufunga mlango usiku
wakati nalala “Mungu wangu’ nilisema kwa sauti ya
chini “Inamana pesa zangu zimechukuliwa”
 
SEHEMU YA 28
NA Gaooh TheAuthor
SIMU =0654387935
LIKE ILINIPOST SEHEMU INAYOFUATA
ILIPOISHIAAA SEHEMU ILIYOPITA
Nilistushwa na sauti za honi nje za magari, hapo
niliamka baada ya kuamka cha kwanza kilikuwa
kuangalia zile pesa ooohhh Mungu wangu hazikuwa
kifuani kwangu tena pesa zile, sikuamini nilishuka
kitandani nikatimua nguo kuangalia kama zipo looh,
hazikuwepo hapo ndio nikajaribu kufungua mlango
ulikuwa wazi kabisa, ndipo kumbu kumbu zangu
zikanikumbusha kuwa sikufunga mlango usiku
wakati nalala “Mungu wangu’ nilisema kwa sauti ya
chini “Inamana pesa zangu zimechukuliwa”
SASA ENDELEAAAAAAA
Nilishikwa na butwaa sikuamini kilichonitokea,
ikanibidi nifungue mlango nilifungua mlango na
kuchungulia nje kulikuwa kimya nikarudi ndani
kwangu kwa huzuni nikaanza kuingiza nguo zangu
ndani ya mfuko ule niliziingiza tena baada ya
kuzitoa, kisha nilivaa nguo na kukaa
“sasa niende ama ni bakie hapa” nilijiwazia huku
nikiwa nimekaa juu ya kitanda, nilifikilia nikibaki
mwisho niwekewe sumu hapo tena nikafikiria
kuondoka bila pesa nitaenda wapi? Nilijiwazia kabla
sijafanya chochote.
“We kidawa nataka uondoke ushapewa pesa ondoka
sitaki kukuona kwangu ondoka,” sauti ilisikika nje
ya malango wangu haikukoma iliendelea tena.
“Naingia ndani nikitoka uwe ushaondoka kama
nitakukuta hutaamini kitu ambacho nitakufanyia,”
alisema hapo sasa akili ikanikaa sawa huyu mama
amejuaje kama nimepewa pesa wakati napewa
hakuwepo na hata angekuwepo asingekubali nipewe,
sasa amejuaje itakuwa ndio aliezichukua pesa
zangu huyu huyu, wakati nikiendelea kuwaza
nilijisahau kabisa baada ya niondoke ndio nilikaa eti
sipati jibu,ndipo hapo sasa kilipotokea kizaazaa
mama mchungaji aliingia chumbani kwangu akiwa
amefura uso kisha kukwapua kale kamfuko kangu
kenye nguo na kunishika mkono kama mtu
anaevushwa bara bara alinivuta kama mwizi, sikujua
roho mbaya ametoa wapi ya namna hii kweli
sikuamini kama alivyosema alinivuta mpaka nje ya
geti kisha kunirushia mfuko wangu wenye nguo
hapo akafunga geti lake baada ya kusonya.
Pesa sina kwa kufikia sina ndugu sina, niliokota
mfuko ule ndio wangu sio wa mtu mwengine
niliuokota kisha kuanza kutembea hata nilipokuwa
nikienda sikuwa nikipajua, wakati natembea niliona
nisitembee mpweke niliona nijifariji,nijifariji na
wimbo ndio nilianza kuimba huku nikitembea,
sikumbuki wimbo huu aliimba nani ila ulipendeza
kinywani mwangu kuuimba, ulikuwa ukiimba shida
shida mpaka siku ya kifo oohh shida,’ safari yangu
ilikuwa nzuri isiyochosha ikichagizwa na wimbo huu.
Baada ya mwendo kadhaa tayari nilihisi kuchoka
hata jasho jepesi lilitiririka mgongoni kwangu, hapo
ikabidi nikae pembezoni ambako kulikuwa na jengo
kubwa la gorofa nilikaa pembeni kwenye ukuta wa
fensi ya gorofa hiyo.
Nilitathimini kidogo niendapo sikupata jibu sehemu
nyingi nilishazisahau tayari niliamka na kuanza
kutembea nilipita kwenye makaburi baada ya kupita
sehemu ambako wanauza matunda,wauza matunda
wengi walikuwa wakinishangaa,japo sikujua
wanachoshangaa kutoka kwangu mana nilikuwa
sawa au kwa sababu nikopeku hapana mbona hata
yule msanii mrisho mpoto anatembea peku na watu
hawamshangai hapo ndio nikajua kuwa ni hulka za
wanaume tu kupenda kungalia angalia
wanawake,sikujua ni makaburi ya wapi hapo nikawa
nafata barabara nikitizama makaburi yale nilihisi
uchungu nikiyakumbuka yale niliyofanya kipindi cha
nyuma kufukua makaburi na kula nyama za watu
MUNGU NISAMEHE haikuwa akili yangu najutia yote
niliyofanya pengine nduio yametengeneza mwisho
wangu mwisho huu unaonitesa na kufanya
ninanyanyasika.
Nilipita pale machozi yakitiririka mashavuni kwangu
hakika iliniuma sana,niliwaza pia wakati nikifanya
vile nilikuwa kwenye hali gani yani kula nyama za
binadamu wenzangu oooh MUNGU NISAMEHE
hakika majuto ni mjukuu baada ya kutembea umbali
mrefu nilitokea barabara kubwa hapo kulikuwa na
kituo cha mwendo kasi ambacho kiliandikwa
Kinondoni B,inamana yale makaburi nilipopita ni
makaburi ya kinondoni.
Nilikuwa kama mkimbizi na mfuko wangu wenye
nguo mana sikuwa hata na viatu mguuni kwa haraka
haraka waweza kusema kuwa mimi chizi fresh,
sikujali ndio maisha yangu, siku hii nayo pia ilikuwa
moja ya siku ndefu zaidi kwangu, sikuwa na usaidizi
wowote niliona dunia yote imenilemea hata namba
ya mchungaji sikuwa nayo tena, hapa niliwaza hata
zile pesa nilizopewa pengine nisingelala nazo
zingenisaidia kuanzia maisha aaaaahhhh, haikuwa
fungu langu.
Nilianza kutembea nikitokea hapa biafra kushuka
chini mpaka kufika studio ambako kwa pembeni
kulikuwa na duka la vunja bei, hapo niliangalia mara
mbili hii njia ya kupitia hapa studio inapoingia
nilitamani kuipita japo sikujua ntatokea wapi, ila
tena nikafikiria bora nifate njia ya mwendo kasi
hapo nikaachana na hii ya studio na kuanza
kunyoosha tu, ilikuwa ndefu kidogo hata jua lilianza
kuichoma miguu yangu hasa nyayo sikujali pia
niliendelea kutembea, mpka nikafikia kanisa kubwa
hapo kibao cha kituo cha mwendo kasi ndio
kinanionesha kuwa hapo ni kanisani yani magomeni
kanisani.
“Samahani kaka,Naomba kipande cha muwa nina
njaa pia nina matatizo naomba msaada wako,”
nilisema nikimuomba muuza miwa ambaye alikuwa
amesimamisha mkokoteni wake pembeni akimenya
miwa, uzuri kaka wawatu alikuwa na huruma
alinisikiliza kweli nilionekana ninashida akanipa
mfuko wa miwa hapo nikaondoka nikimshukuru,
aliniambia pia kuwa angekuwa na pesa asingesita
kunisaidia.
Safari yangu iliishia hapo sikutaka kutembea zaidi
nilihisi kuchoka ikanibidi nitafute sehemu nikaka
hapo kanisani nilitamani sana niende kanisani
pengine nitasaidika ila sijui ni nini kilinisitisha
pengine ni baada ya kujua siku hiyo haikuwa ya
ibada hivyo hata ningeenda nisingesaidika.
Niliafuta sehemu hapo nikachukua ule mfuko wangu
nikavaa nguo mbili mbili yani nikimaanisha
nilipandishia nguo juu alafu nikachukua kanga
nikazifunga bundu ambalo nililiweka mgongoni
hazikuwa nyingi hivyo ilikuwa rahisi kuzifunga baada
ya kuzifunga, niliendelea kuzunguka huku jua
likizama kumaanisha jioni inakaribia kuingia hapo
niliingia mtaani nikijifanya omba omba, nilianza
kuomba kwenye foleni za magari kuna ambao
walinipa wengine wakinifukuza haikuwa rahisi
kuomba omba kulinifikisha mpaka usiku kufika giza
likimeya angani, nilihesabu pesa nilizopata wakati
nikuomba omba hazikufika hata elf mbili zilikuwa
ndogo sana, ila nilishukuru kwa vile nimepata japo
ni ndogo pesa niliyopata nikatumia kwenda kununua
chakula kisha nilikula siku hii ikapita.
Niliona sina uelekeo wa maisha hata msaada sina
pia niliamua nisijichanganye na watu sikutaka kuishi
kwenye manyanyaso tena, sio kwamba sikuweza
kwenda kuomba kazi za ndani ila sikutaka kazi
pekee ambayo niliona bora niifanye ilikuwa ni
kuokota chupa za maji, ndio chupa za maji ndio
niliona kama kazi ya kufanya huku nikibaki vile vile
mchafu chafu kuoga mara moja moja ni wiki sasa
naokota machupa ya maji nazunguka mitaani kula
yangu ilikuwa ni mpaka nifanye kazi ya kuokota
makopo kwa bidii zipatikane kilo nyingi ndio nipate
pesa ya kula, kulala ndio ilikuwa mtihani, usalama
wangu ulikuwa mdogo sana ndio mana nilikuwa
nikilala kwa makini pia wakati mwengine silali au
nilale mchana kufidia usingizi wa usiku, hakika
maisha haya yalikuwa magumu zaidi japo sio kama
yale ya kuwa paka, niliendelea na kazi hii kama ya
kujipatia kipato mara nyingi nilikutana na adha ya
wanaume waliokuwa wakinizinga zinga kunitaka ila
sikuwahi kukubali, siku moja sijui niliwaza nini hapo
nikaenda dukani, sikuwa na kitu cha kununua ila
nilienda huku nimeshika shilingi miambili, hapo
fuko langu la makopo nikalitua pembeni.
“Sasa nimekuja kununua nini,?” nilijiuliza hapo
nikatabasamu kisha nikajisemea “ahaaaa” kuonesha
nimekumbuka.
“Naomba sumu ya panya,
ITAENDELEEEE
 
SEHEMU YA 29
NA GAOOH
SIMU +0654387935
ILIPOISHIAAA SEHEMU ILIYOPITA..
“Sasa nimekuja kununua nini,?” nilijiuliza hapo
nikatabasamu kisha nikajisemea “ahaaaa” kuonesha
nimekumbuka.
“Naomba sumu ya panya,
SASA ENDELEAAA….
Nilijikuta nikitamka neno hilo mwenye duka nae kwa
vile ni kazi yake ya kuuza na kuwahudumia wateja
basi hakusita alipokea pesa yangu kisha nilimuona
akichukua kipakti kidogo na kukifunga kwenye
gazeti.
“Kuwa makini unaposhika,pia ukiifungua hakikisha
unanawa mikono yako na sabuni hiyo kiboko
haicherewi,” alisema muuza duka huku akinipa.
“Ndio hii hii niitakayo asante,” nilisema na
kuondoka hata muuza duka nahisi alishangaa, ila
hakujali kwa vile hayakumuhusu, sumu ile niliifunga
vizuri kwenye kanga fundo kisha nikachukua fuko
langu la makopo na kuondoka dukani pale.
Japo nilinunua sumu ile ila sikujua nilitaka kufanya
nini, japo kazi ya sumu inajulikana nilizunguka mitaa
kadhaa nikiokota makopo jua nalo halikuacha
kunichoma bila huruma, mara zote niliamini jua hili
linanichoma na kunisurubu kama malipo ya
matendo niliyofanya huko nyuma, baada ya
kutembea umbali kadhaa ndipo nilikumbuka kile
nilichobeba kwenye khanga ambacho nimefunga
fundo,niliweka tena fuko langu chini, wakati huu
nilipoweka nikajitafuta tena hapa kifuani sehemu
ambayo huwa nawekaga pesa zangu ndipo niliona
ipo shilingi elfu moja peke yake, nilitabasamu kama
mtu asie na akili nzuri kisha nikajongea kwa muuza
vinywaji ambaye aliponiona alikaa kwa makini huku
akiniangalia alionekana kuwa na hofu na ujaji wangu
pale alitegemea nitakachofanya ni fujo tu kwake,
alinikazia macho nami nilijongea nikitazamana nae.
“Naomba maji ya mia tano tafadhali,” ndio neno la
kwanza nililo anza nalo, kidogo hapo muuzaji yule
alishusha pumzi akinitazama pengine hakutegea
kama nitakuja vile.
“Unaitaji masafi, afya au kilimanjaro au hill water,”
aliuliza kwa kubabaika mana alishindwa kumakinika
na kufungua jokofu lake analouzia vinywaji vyake
alikuwa akinitazama mimi niliekuwa nimesimama
tu.
“Nipe ya mia tano,” nilisema.
“masafi,afya hill water,” aliuliza tena, hapo
nikamsogelea.
“Nataka maji,” nikaongea kwa mkazo nilimuogofya.
“Chukua haya,” alisema akanipa na pesa yangu
iliyobaki niliondoka nikimuacha akitetemeka,
“Hahahahahaha,kumbe nafaa kuwa mbabe KIDAWA
Mbabe” nilijisemea huku nikicheka na kuokota fuko
langu la machupa hapo nikaanza kutembea memo
yakishindana na mfuniko wa chupa ambao
nilidhamilia kuufungua kwa meno.
“msyuu shenzi.” Sonyo lilinitoka baada ya kuona
mfuniko ule ukicherea kufunguka.
Ikanibidi niweke fuko langu jichi hapo nikashika na
mikono miwili kisha nikang’ata na meno chupa
ikafunguka ilipofunguka tu yakaruka usoni kwangu
kwa vile nilikuwa nimekandamiza chuka na mikono
miwili.
Nilipoifungua hapo nikatafuta sehemu ambayo
ilikuwa pembezoni mwa barabara , kulikuwa mti
wenye vitunda vya sukari nikakaa chini yake kisha
nilikunywa maji yangu, baada ya kupiga funda
kadhaa nilikohoa “khooo khooo khooo,” maji
yalinipalia hapo nikayaweka pembeni na kufungua
kanga yangu kuchukua ile sumu niliyokuwa
nimefunga kwenye nguo baada ya kuinunua dukani.
Ilikuwepo nikaitoa kisha nikaiweka mkononi
mwangu ‘Kuwa makini unaposhika,pia ukiifungua
hakikisha unanawa mikono yako na sabuni hiyo
kiboko haicherewi,’ maneno ya muuza duka
yarijirudia akilini kwangu alafu nikacheka tena
kicheko kikubwa “hahahahahahahaha’’ kicheko hiki
nilicheka baada ya kufikiri sasa hii sumu nimenunua
nataka kuitumia je mikono nitanawa muda gani
wakati itakuwa ishafanya kazi mwilini mwangu, KAZI
YA SUMU NI KUUA acha na mimi nife nitangulia
niende kule ninakopaswa kwenda nilipowapereka
wenzangu wasio na hatia, hakika nilikata tamaa ya
maisha tabu na shida zote pamoja na suruba
zilinichosha jambo pekee niliona napaswa kufanya
ni KUFA ndio niliona ni stahili yangu natakiwa kufa
japo nimeomba msamaha ila Mungu bado
hajanisamehe, pengine angenisamehe nisingepata
tabu zote hizi tizama mwili wangu ulivyo chakaa,
tizama lile umbo langu zuri la kike lilivyo chakaza
na mlo hafifu, tizama hata ngozi yangu ilivyofubaa
Oooh Mungu wangu najileta mbele yako unipokee
baba, najileta uniadhibu kwa dhambi nilivyofanya
kupitia mikono yangu, najileta najua kwako ndio
sehemu ya hukumu, ngoja nije baba unipe stahili
yangu eeh Mola nipokee’ nilisema huku macho
yangu nikiwa nimefunga sumu ile nikiwa nimeiweka
mikononi hapo nikafungua macho sasa nikidhamilia
kuifungua niirambe nitimize azma yangu.
“Mungu wangu,” nilistuka baada ya sumu ile
kutokuwepo mikononi mwangu, hapo nilipigwa na
butwaa nikatupa macho pembeni ya pale nilipo kaa
ndipo niliona kipande cha gazeti ambacho kilikuwa
kinapepea pepea nilikitizama kwa makini kilibeba
kichwa kikubwa ambacho kiliandikwa NEVER GIVE
UP sikuamini ikabidi niamke pale nikiitafuta sumu
ile kwenye kikaratasi ambayo ilikuwa imefungwa
haikuwa pale tena, niligazabika nikachukua machi
yangu ambayo niliacha kunywa hapo nikapiga funda
kadhaa na kuamka nilipokuwa nimekaa nilijihisi
mnyonge hata yale mawazo ya kunywa sumu tena
yalishanitoka, Njaa ndio ilishamiri tumboni kwangu
nilihisi ikinifukuta, hapo niliamka pesa pekee
niliyobakiwa nayo ilikuwa shilingi mia tano tu ya
kitanzania na chakula cha mia tano hakikuwa
kikipatikana niliweka fuko langu pembeni na
kujipereka kwenye foleni kama kawaida usoni
kwangu kulijaa weusi sikuwa nikioga kwa wakati
siku mbili hadi tatu ndio nilioga, kule kuokota
makopo na kujishika usoni muda mwengine kuokota
mifuko ya mkaa kuitumia kama kibebeo ndio
kulifanya uso wangu uwe na rangi nyeusi hii ni
baada ya kujitizama kwenye moja ya gari liliokuwa
kwenye foleni, nilijitazama usoni na kugundua hayo,
sikujali kwa vile ndio maisha yangu haya siwezi
pingana na ukweli wala kuigiza gari la kwanza
niliomba kwa kupereka mkono wangu baada ya
kioo kufungulia hapo niliwekewa maganda ya
machungwa kisha viooo vikafungwa sikufadhaika
nilishukuru tu kwa vile ni pesa zake siwezi
mlazimisha anipatie huku nikiwa sijazifanyia kazi
yoyote.
Nilipita karibia magari kumi hakuna nilichopata
hapo nikajikatia tamaa na kuamua nirudi nilipoacha
mfuko wangu wa machupa, wakati narudi nilihisi
sauti ya mtu ikiniita nyuma.
“Kidawa……kidawa….kidawa,” sauti hii sikuitilia
manani kwa vile nilijua hakuna mtu anaenifahamu
hapo nikijiona nipo tofauti pia nilijua aneitwa sio
mimi, kila nikizidi kujongea kufata fuko langu ndipo
sauti ile ilizidi kuniita hapo ikabidi nigeuke na
kutizama nyuma alionekana kijana wa makamu
ambaye huwezi kumueka kwenye ukijana wala
kwenye uzee alikuwa saizi ya kati alionekana kuvalia
suti yake safi, nilimshangaa kwa vile sikuwa
nikimjua hata nilipojitahidi kumuangalia mara nyingi
akilini kwangu hakuwepo kabisa.
“huyu nani?” nilijiuliza naye akinikaribia.
“Kidawa,” aliita tena huku akinipokea mfuko wangu
wa makopo na kuuweka kandon akionekana kutaka
kuongea nami.
“We nani?” nilimuuliza hapo akanitazama.
“hapana ndio wewe bana, ndio wewe,” alisema huku
akiniangalia kuanzia chini mpaka juu.
“Ndio mimi nani?” nikauliza tena.
“Kidawa,”
“Kwani we nani?”
 
ILIPOISHIAAA SEHEMU ILIYOPITA
“hapana ndio wewe bana, ndio wewe,” alisema huku
akiniangalia kuanzia chini mpaka juu.
“Ndio mimi nani?” nikauliza tena.
“Kidawa,”
“Kwani we nani?”
SASA ENDELEAAA
sikuwa nikimuelewa kaka huyu alionekana kama
mtu aliestushwa na kuniona tena asieamini kama
ameniona, ilibidi nimsikilize.
“Kidawa siamini kama wewe ndio umekuwa hivi,
kidawa umekutwa na nini?” hakika alizidi
kunichanganya mana sikuwa nikimjua kabisa kaka
huyu alionekana kuning’ang’ania zaidi.
“Tafadhali mbona mimi sikufahamu ni nani kwanza
ebu wacha kubabaika niambie wewe nani pia
unanijuaje mimi.”
“mimi naitwa John tulikutana bar kipindi fulani
ukanidanganya unaitwa janet, siku ile tulifurahi
pamoja nikakurudisha kwako lakini ulikataa
nisipajue japo ulikaataa ila nilikufuata pia
nikakutumia mtu akufuatilie baada ya kujua
unapokaa haikuwa rahisi kiasi hicho kwa vile hata
yule niliemtuma ulimfokea hata alipotaka namba
yako,ilikuwa taarifa mbaya kwangu kwa vile
nilitegemea kukupata ila haikuwezekana kama
unakumbuka kuna siku nilikupigia simu kabla
sijaongea kitu nilikata simu hiyo ilikuwa ni baada ya
yule mtu niliemtuma kukufata alipokuona basi
nilikata simu kama unakumbuka ulikuwa ukiongea
na muuza duka.” Kaka huyu alielezea hapo kidogo
nilikumbuka hapo kidogo kumbu kumbu za huyu
kaka na yale matukio aliyonielezea yalinilejea
kichwani kwangu.
“Kwahiyo ulikuwa unatakaje sasa,” nilimuuliza.
“Nakuomba tuongozane nina mengi ya kuongea
nawe ni kama bahati kukuona hapa sikutegemea
kama ningekuona tena japo niliweka imani ya kuwa
nitakuona naomba kama hutojali tuongozane,”
alisema nilimkatalia na kumtaka aniache lakini
aliniomba sana huku akiniambia atanilipa pesa ya
makopo yangu.
“Najua upo kazini makopo hayo nitayanunua mimi
shika hizi kama ununuzi wa makopo hayo,” alisema
hapo akitoa noti mbili za elfu kumi kumi
nikazipokea haraka haraka kisha nikamkubalia hata
lile fuko niliachana nalo sikuliangalia tena
tuliondoka pale akiniambia nimfate mpka tukalifikia
gari,gari ambalo lilikua la kwake tukaingia.
Mbali na kuwa mchafu chafu kaka huyu hakujali,k
aliniruhusu nikae kwenye gari yake, kwenye siti zake
zilizokuwa safi zikivalishwa kava zuri lililozipendeze
sha zaidi.
Nilikaa hapo akageuza nyuma kisha kuingia kwenye
barabara kubwa, huku safari ikiendelea nilikaa kimya
nikisubiria atasema nini ila roho na anafsi yangu
havikutaka kabisa kuwa ndani ya gari lile, nilijitahidi
tu kumheshimu kwa vile aliniomba pia alinilipa
pesa ya makopo yangu ya siku hiyo ambayo
nilikuwa nikiendelea kuokota.
“Samahani Kidawa naomba tupitie hapa hotelini
kisha utaenda kuoga ili uwe safi na mimi
nikakuchukulie nguo kisha tutaongea,” alisema.
“Hapana hunipereki hotelini, wataka ukanibake,”
nilisema nikimuangalia.
“Hapana kidawa siwezi kufanya hivyo nakuomba
uniamini naitaji kukusaidia,”
“Utanisaidia na kipi maisha yamenipiga na haya
ndio malipo yangu,”
“Hapana usiseme hivyo, kila jambo hutokea kwa
sababu, najua hali unayopitia ni kipimo,Mungu
huwapa kipimo waja wake ili kujua imani
waliyonayo ndani mwao, unaweza kupitia magumu
mengi ila hayo yote ni kipimo unapimwa Kidawa
naamini Wakati wako waja sasa, nahitaji uwe na
mwisho mwema matatizo hayakuzaliwa kwa ajili
yako” John alisema.
“Nishakata tamaa hakuna ninacho amini John,”
nilimwambia hapo aliendelea kunihadaaa na kunitia
moyo, kutokana na maneno yake nilimwamini hapo
nilifanya alivyonitaka nifanye kweli tulienda hotelini
akaniacha akaniambia nikaoge kisha yeye alienda
kunitafutia nguo, nilienda kuoga nikiwa siamini
kama ndio mimi mwili wangu ulifubaa sana mafuta
yote yaliisha, ilionekana mifupa tu yani, Nilisikitika
nikijiangalia kwenye kioo hapo machozi yalianza
kunitiririka niliumia, ikanibidi nitoke kwenye kioo
nilipo toka nilisikia mlango wa chumba nilichopo
ukigongwa hapo ikabidi nifute machozi niliyokuwa
nayo kisha nikaamka na kufungua mlango,
nilipofungua nilikutana na mhudumu ambaye
alitabasamu pale alipo niona.
“Habari madam, nguo zako hizi,” alisema hapo
nikazipokea yeye akaondoka, hapo nilielekea
kwenye kioo kwa ajili ya kuvaa, nilivaa huku nikiwa
sijiangalii sikutaka kujiangalia mana nilijua
sijapendeza urembo wangu wote uliisha,
nilichoshukuru nguo zilinitoshea hapo nikapata
amani, amani ambayo ilinifanya nitabasamu.
Nilipovaa kisha nikatoka nje ya hoteli hii, nilipoteza
John alininyooshea mkono kuonesha kuniita hapo
nikamtizama kisha nikaenda kule alipo,”
“Wooow, umependeza sana Kidawa,” alinihadaa
namimi niliitika tu “asante’ huku nikijua sijapendeza
wala sina uzuri huo wa kupendeza kwa sasa, nilikaa
alipokaa yeye ambako vilikuwa viti viwili tu yani
upande huu na huu hivyo nilivyokaa ikawa kama
tunaangaliana vile, hapo aliitisha chakula kaniambia
na mimi niitishe, hakika nilikua na njaa hivyo
sikuremba wala kuleta urembo wa zamani niliitisha
chakula hapo vikaleta changu na chake, wala
sikwambii nimeitisha nini mana wakati nina njaa
hata hujanikaribishaa we kula kusikia tu hahahahaha
tuendelee bana ntawakaribisha siku nyengine.
“Hotel hii ni nzuri sana huwa napendelea kupata
chakula cha mchana hapa, wanahuduma nzuri na
wanachakula kizuri,” alisema.
“hata mimi naona huduma zao ni nzuri kweli,”
“naweza kukulisha,”
“hapana mbona mikono ninayo.”
“Basi nisamehe, Kidawa….. samahani kama
ntakukosea ila nakuomba unielezee historia yako
mpaka kufika hapa, kipi kimeharibu maisha yako
nataka kujua nieleze hata kidogo nakuomba,” John
aliniomba akitaka nimulezee maisha yangu,yangu
ambayo ndio yananihaghalimu alitaka kujua mapito
yangu ambayo sitamani hata kuyakumbuka, nilisita
kumwambia ila alizidi kuniomba huku akinishawishi
kunisaidia.
“John mapito yangu sitamani kukumbuka
yananitesa sana sitaraji kukumbuka chochote
kilichopita, unaweza kunielewa tukaacha hayo
yakapita,”
“Kidawa ni kweli tunaweza kuacha yapite, ila
huruma na huzuni vimenijaa baada ya kukuona
ukiwa ai ile najua umebebavingi sana tafdhali
nakuomba nielezee japo kwa uchache,” alizidi
kuniomba hapo niliingiwa na imani ikabidi
nimuelezee.
“John nilidaanywa na mwanaume nikamkabidhi kila
kitu changu, mwisho wa siku alinishauri niuze vitu
vyangu nikaishi naye kisha pesa ile nimpe aweke
kwenye biashara zake, mwisho wa siku alinifukuza
kama mbwa nyumbani kwake akaleta mwanamke
mwengine sikuwa na kwa kusemea hata nilipoenda
kumshitaki sikuwa na ushahidi kesi ilpuuzwa pia
nikaambiwa nilipe hela ya usumbufu nilikuwa na
kahela kangu ikabidi nikatoe mana walisema
watanilaza ndani..”niliamua nimdganye sikutaka
ajue ukweli wangu niliona anaweza kuniogopa
kabisa.
“Pole sana kidawa kwanini ulimwamini mtu ambaye
lengo lake lilikuwa kuharibu maisha yako,” alisema
eti nae alikubali uongo wangu.
“Baada ya tabu zote nilibahatika kupata kazi kwa
Mchungaji,” nilimuelezea yale yote yaliotokea kwa
mchungaji alisikitika na kunionea huruma, tukiwa
uendelea na maongezi jioni ilitukuta pale ndipo
aliponiomba twende wote kwake sikuwa na sababu
ya kumkatalia, nilikubali tukaingia ndani ya gari
yake.
Njia nzima tuliongea tukicheka pamoja huku
nikijiona mwenye furaha na amani, alinieleza maisha
yake kwa ufupi akaniambia amejenga madale
anaishi peke yake pia ni mfanya kazi kwenye
kampuni ya logistics ambayo inahusika na
usafirishaji a upokeaji wa mizigo bandarini, tulienda
mpaka kwake akanikaribisha nikaingia muda huo
usiku ulishaingia hivyo aliingia jikoni akaandaa
chakula tukala pamoja kilikuwa kitamu kumbe john
anajua kupika sikusita kumpa sifa zake nae
alizipokea kisha tukacheka pamoja.
 
SEHEMU YA 31
NA Gaooh TheAuthor
SIMU 0654387935
ILIPOISHIAA SEHEMU ILIYOPITA.
Njia nzima tuliongea tukicheka pamoja huku
nikijiona mwenye furaha na amani, alinieleza maisha
yake kwa ufupi akaniambia amejenga madale
anaishi peke yake pia ni mfanya kazi kwenye
kampuni ya logistics ambayo inahusika na
usafirishaji a upokeaji wa mizigo bandarini, tulienda
mpaka kwake akanikaribisha nikaingia muda huo
usiku ulishaingia hivyo aliingia jikoni akaandaa
chakula tukala pamoja kilikuwa kitamu kumbe john
anajua kupika sikusita kumpa sifa zake nae
alizipokea kisha tukacheka pamoja.
TUENDELEEE SASA
Nilianza maisha mapya nikiwa kwa john hakuwahi
nitaka kimahusiano tuliishi kila mtu chumba chake,
huku tukiogopana siku zilianza kupita kisha zafatia
wiki mpaka mwezi nilianza kunawili mwili wangu wa
kirembo ulirejea utanitaka Kidawa mie.
Nilianza kuona raha ya maisha john alinijali kwa kila
kitu tulienda kila nilipotamani kwenda nae hakika
alijua thamani yangu, nitake nini john asinipe.
“Kidawa leo natamani twende mbuga ya wanyama
tukafurahie wikiend,”
“Woow kweli John,”
“Ndio natamani tukaone wanyama si unajua kesho
ni jumamosi hivyo hivyo nitakuwa siendi kazini
mpaka jumatatu,” john alisema hapo tukiwa
tunatizama runinga sebuleni japo yeye alikuwa
makini na laptop yake.
‘Ni kweli sio jambo baya” nilisema.
“Unaonaje ukachagua wewe mbuga ya kwenda,”
aliniuliza akitaka nimtajie, aliponiuliza haikunifikilish
a sana.
“Mikumi,” nilichagua mikumi, ndio mbuga ambayo
ilikuja haraka kichwani, nilipomtajia alionekana
kufurahia mbuga hii niliyomtajia, baada ya maongezi
machache nilienda kutenga chakula nilikuwa nishaka
hivyo nilikitenga mezani nikamwita kwa ajili ya kula
pamoja, tulionekana wenye furaha zaidi unaweza
kusema ni mke na mume kumbe wala tuliishi kama
kakan na dada, chakula kilikuwa kitamu sina
mashaka na upishi wangu, hakuacha kunisifia.
“Chakula kitamu sana Kidawa inaonekana
mwanamke atakae kuoa atafaidi sana,” alisema
hapo sikuwa na jibu niliishia kucheka nae akacheka
tukacheka pamoja, nilijua tu ananichokora hivyo
mada ile tulipotezea baada ya kucheka.
Chakula kile hakikushushwa na maji nilitengeneza
sharubati tamu ya embe nayo aliisifia, nilizoea sifa
zake za kunipamba.
Baada ya kumaliza tuliagana kisha akaniambia
kuwa nijiandae kwa ajili ya safari ya kesho.
Kila mmoja aliingia ndani kwake, nikiwa kitandani
nilianza kumuwaza John,John aliteka akili yangu
niliwaza yote anayonifanyia, nilijikuta nikitabasamu,
kila ninapotaja jina lake kisha nikingata papy za lips
zangu “John” ndio jina liliotawala usingizi wangu
mpaka kunakucha nilimka nikiwa na jina la John,
nilipoamka asubuhi hiyo nilipanga nikaandae chai
hivyo nilitoka haraka haraka nikiwa na khanga
nikijua John amelala, muda huo nilipotoka tu
nilishtushwa na kumkuta John amekaa kwenye
makochi na laptop yake.
“Heeeeh, John umeamka saa ngapi?”nilimuuliza
huku nikijisogeza ukutani kuegemea.
“Ooh kidawa sio muda nimeamka, nilikuja kunywa
maji chumbani kwangu yaliisha, nilitaka nirudi ndani
ila nikaona bora nimalizie kazi yangu hapa,”alisema.
“Na laptop je?” nikamuuliza.
“Oohh hii niliisahau hapa jana, vipi na wewe wapi
sahizi,”
“Nilikuwa nataka niandae chai,”alinikatisha na
kuanza kuniuliza kuhusu mimi.
“Hapana usijichoshe we jiandae si unajua leo
tunatakiwa kusafiri hivyo jiandae tuwahi foleni chai
tutakunywa hotelini,” alisema kisha nikarudi ndani
kwangu nikihema sikutegemea kumuona pale alafu
na vile nilivyokuwa nimevaa khanga tena moja tu
ambayo iliyaacha wazi nusu ya mapaja yangu,
nilijiandaa vizuri kisha nikavaa nguo zangu ambazo
alininunulia John mliman city, nilipozivaa kisha
nikajitizama kwenye kioo hakika nilipendeza Kidawa
mimi hips za haja umbo namba tisa kama si nane
na kinguo nilichovaa kikilichora umbo langu
vizuri,hapo tuliingia ndani ya gari kuianza safari,
John alikuwa dereva mzuri aliendesha gari kwa
ustadi tukaiacha dar na kuingia kibaha hapo sasa
ndipo aliniambia tuingia mgahawani kwa ajili ya
kupata chai, tuliingia kwenye moja ya mgahawa
maarufu hapa kibaha kisha tukaagiza chai, chai
ambayo ilikuwa nzito hakika nilishiba japo ni
asubuhi ila nilitosheka tulipomaliza tukaendelea na
safari.
“Kidawa mfano ikatokea dereva wako nikachoka
kuendesha je utaendesha wewe,?” aliuliza, hapo
nikacheka kidogo.
“Hahaha ndio, anaekaaga pembeni ya dereva nae
lazima ajue kuendesha,”
“Real, inamana nawe unaendesha.” Aliponiambia
hivi kidogo kumbu kumbu zangu zilihama hapo
nikamkumbuka mama mchungaji nae alipojifanya
mwema kwangu kipindi fulani kisha kuonesha
makucha yake na kuanza kuninyanyasa.
“Heyy kidawa vipi mbona unaonekana hupo hapa
nini tatizo?” aliuliza hapo ndio nikastuka mana
mawazo yalishahama kabisa nikaanza kujitetea.
‘Hapana john niko sawa nambie,”
“Najua haupo sawa hutaki tu kusema ila si mbaya,
sipendi nikukwaze,”alisema hapo aliendelea
kuniuliza maswali kadhaa nikawa namjibu mara
nyingi alipenda kuona nikifurahi na mimi nilijitahidi
kuonesha ushirikiano, zile story za hapa na pale
ndio zilitufikisha mpaka msamvu stand hapo
hatukuingia stand tulijongea mpaka kingsway hotel
kupata chakula cha mchana, tulikula kwa pamoja
kisha baada aosheka safari iliendelea saa moja
ilitosha kutufikisha mikuni yani kutoka msamvu
mpka mikumi tulitumia saa nzima hapo tukafika
mapokezi ilikuwa mchana kwenye saa sita hivi,
sikuhii tulifanya utalii wa kutembea yani unawaona
wanyama kwa ukaribu unaona nyayo zao unaona
vitu wanavyokula ulikuwa unaitwa WALKING SAFARI
nilienjoy sana siku hii, tulifurahi na kujifunza mengi,
naweza sema siku hii ilikuwa moja ya siku ambazo
nilifurahi sana na kujiona kama nimezaliwa upya,
baada ya matembezi na mihangaiko basi tuliondoka
mbugani hapo.
“Nadhani umefurahi Kidawa,” John alisema.
“Bila shaka nimefurahi john,umenifanya nifurahie
kukujua ulikuwa wapi john siku zote,”
“Kila kitu hutokea kwa sababu pengine
ulizungushwa, kisha kuletwa kwangu,” john alisema
huku akiniangalia, tulipiga story za hapa na pale
kisha gari iliendelea na safari.
“Na huku wapi?” nilimuuliza kwa vile hatukurudi na
ile njia ya dar tulienda ile ya iringa ikabidi
nimuulize,.
“Oohhh nimesahau kukwambia Kidawa, hatuwezi
kurudi leo dar nimeonelea bora tukalale hapo mbele
kuna hotel nzuri ya veta mikumi.”
“Nka tunarudi leo s, ila sio vibaya mana tukirudi
utachoka zaidi jumatatu unatakiwa kazini bora leo
tupumzike kisha kesho ndio turudi dar.” Nilisema,
hapo tukaendelea kilomita chache tukaifikia mizani
wa mikumi jioni hii kulikuwa na foleni kidogo japo
ni magari makubwa ndio yanapimwa ila yalituweka
kwenye foleni njia ilikuwa ndogo sana o magari
yalipita kwa kupokezana, baada ya muda kidogo
tulipita hapo mita chache tukaifikia hiyo hotel
ilikuwa hotel nzuri ya kitalii, iliitwa VETA TOURIST
HOTEL, tulipofika hapa John akachagua sehemu
nzuri ambapo ilikuwa kama kibanda ambacho juu
kimeezekwa na nyasi pamoja na nguzo za miti
ambazo zimeshikilia paa hilo ilikuwa sehemu nzuri
iliyojaa miti , baada ya kuniacha pale John alienda
reception kufanya booking ya nyumba, kisha akarudi
hakunambia chochote kuhusu nyumba ila
alinikaribisha kisha kuniambia niagize chakula.
“Sehemu hii huwa naipendaga sana nishawahi lala
mara nyingi hapa, nikiwaga safarini hasa safari za
kampuni huwa tunafikia hapa mara nyingi,”alisema.
“Kwahiyo wewe ni mwenyeji hapa,?” nikaamuliza.
“Ndio hata baadhi ya wahudumu wananijua,”
alisema huku akiniangalia.
“Basi vizuri kumbe nipo na mwenyeji, ehee
mwenyeji vyoo viko wapi,” nikamuuliza akacheka.
“Hahahaha, nishakuwa mhudumu ila anyway kwavile
ni kwa ajili yako acha iwe hivyo,”
“Jamani John kwani vibaya ukiwa mhudumu kwa
ajili yangu,” nilideka.
“Sasa ni hivi nyoosha hii njia kisha kabla hujafika
pale reception ya vinywaji kunja kushoto
kishanyoosha moja kwa moja utaona kibao
kimeandikwa wash room choo cha kwanza
wanaume cha pili ndio wanawake wewe utaenda cha
mwisho ambacho ndio cha pili,”alitoa maelekezo
marefu ambayo nilihisi kutokuelewa.
“Mmmmm,” niliguna.
“Mbona waguna au hujaelewa nikupereke, we
nitumie uwezavyo kidawa nipo kwa ajili yako,”
alisema hapo nikatabasamu na kujiona mwenye
bahati.
“Hapana nimependa maelekezo yako, nimeelewa
vizuri kuliko hata ningefundishwa na mwalimu wa
hisabati nisingeelewa unaonekana mwalimu mzuri
sana.” Nilimwambia akafurahi ghafla aliitwa “john”
hapo akaniambia kuwa ameitwa na rafiki yake
ambaye ni meneja wa hotel hii anaitwa mr juma,
ndipo nikmuaga kuwa naenda uwani nimezidiwa
nilimwacha akiongea na rafiki yake kama
alivyosema, nilienda uwani nilifatisha vile
alivyosema kisha nikafika mpaka kilipo choo
nikaingia sikutumia muda mrefu nilirudi wakati huu
kiza kiliingia tayari.
“Umeelewa eeh, nikajua hujaelewa kidogo nipate
wasi wasi nikufate nikajua umeingia jikoni mana
mkono wa kulia kuna jiko pale na huu wa kushoto
kuna jiko la kuoka mikate.”
“nashindwaje kuelewa wakati mwalimu wangu
umenielekeza vizuri,” tuliongea machache ukafika
muda wa kulala, muda ambao nilikuwa nikiusubiri.
“Twende kidawa nadhani tunatakiwa tupumzike
sasa, ili kesho tuanze safari mapema” alisema.
“sawa john, ila we ndio mwenyeji uongoze njia mimi
sipajui huku,” nilisema nikideka, hapo akaniambia
nimfate nilitamani kumshika mkono ila nikasita
kisha nikamfata aliagana na yule kaka ambaye
aliniambia anaitwa Mr Juma, tulifika kwenye
nyumba akafungua kilikuwa chumba namba 101
alipofungua tukaingia, kuna kitu nikakiwaza hahaha
sikwambii ni kipi hahaha, tulipoingia kilikuwa
chumba kizuri chenye tv ya ukutani pia kilikuwa na
ac alinielekeza jinsi ya kuwasha na kuzima pia
kuwasha tv alinieleza.
“Kidawa nadhani hiki chumba ni kizuri, kila kitu kipo
ukiwa na tatizo utapiga simu iko pale mhudumu
atakuja kukusaidia,” nilikuwa nikimsikiliza kwa
makini kisha akaendeleaa, “ngoja mimi niende
chumbani kwangu nadhani asubuhi nitakuja
kukuamsha mapema, ooh nimesahau bafu hili hapa
pia maji yake ni ya moto ngoja mimi niende
kwenye chumba changu jirani.”
“Inamana hatulali wote..
 
SEHEMU YA 32
NA Gaooh TheAuthor
SIMU 0654387935
ILIPOISHIAAA SEHEMU ILIYOPITAAA…
“ngoja mimi niende chumbani kwangu nadhani
asubuhi nitakuja kukuamsha mapema, ooh
nimesahau bafu hili hapa pia maji yake ni ya moto
ngoja mimi niende kwenye chumba changu jirani.”
“Inamana hatulali wote..
SASA ENDELEAAAA…
Nilijiwazia baada ya kuona anaaga mwanzoni nilijua
tutalala wote chumba kimoja kumbe john alichukua
viyumba viwili,nilitamani usiku huu tungelala wote
ila niliona hata aibu kumwambia, niliogopa
kujirahisisha kwake japo nilimpenda vilivyo,
aliondoka hapo nikabaki mwenyewe, niliingia bafuni
kuoga maji yake yalikuwa na moto niliyapenda sana
mbali na baridi iliyopo morogoro ila hotel hii ya
kitalii walikuwa wakichemsha maji ya kuoga.
Nilipohakikisha nimetakata hapo nilichukua taulo
ambalo lilikuwepo chumbani hapo nililichukua kisha
nikajifuta maji na kujilaza kitandani, sikuona hata
sababu ya kuwasha tv usiku huo nililala nikiangalia
juu macho yangu yakitizama miti ambayo
imeshikilia chandarua hakika hotel hii ilipendeza
kwa usuri wake ilikuwa ya kitalii haswaa.
Usiku haukuwa mrefu kivile, nililala nikimuwaza
John John John hakika aliteka akili yangu, nilisikia
mlango ukigongwa hapo nikaamka kwenda
kuangalia ni nani nilitoka hadi mlangoni nikiwa na
taulo tu, nikafungua mlango uso na macho kwa
John.
“Oohh, Kidawa bado umelala kumbe” alishangaa
kuniona vile.
“Si bado ni usiku sahizi John,” nilimwambia nisijue
ni saa ngapi, hapo akatoa simu yake na
kunionyesha looh! Ilikuwa saa kumi na mbili kasoro
nilishangaa. Kumbe sikuwa nimelala kabisa nikajua
bado ni usiku,john alitaka kuniacha nilale kisha
muda ambao nitakuwa nimeamka ndio tuondoke.
“Hapana john, yuondoke tu sahizi sina usingizi
ngoja nijiandae,” nilimwambia akakubali na
kuniambia yupo ananisubiri hotelini, hapo nikaingia
bafuni kutoa wenge la usingizi nilioga chapu chapu
nikavaa nguo zangu dakika kadhaa nikatoka hapo
nikaelekea mpaka alipo, alikaa kwenye moja ya
vibanda nilipofika aliagiza supu pamoja na chapati
kila mtu zake.
“Asubuhi unatakiwa kunywa supu sio chai ya rangi
sio nzuri kiafya, yani ukikosa supu basi kunywa
maji ya uvugu vugu yatakusaidia sana.” Alisema
hapo nikamwitika.
“Sawa dokta,” niliposema hivyo akachekaa kisha
tukacheka wote.
“Umenikumbusha mbalii hahaha,”
“Wapi tena huko wakati tupo hapa,”
“Umenikumbusha rafiki yangu mmoja kila
nitakachomuelekeza ananitungia majina hapo hapo
yani ilikuwa tangu utoto mpaka tunakua ni hivyo
hivyo yani unakuta mfano tunaangalia magari
nikimwambia kuwa gari ile inambio inaweza
kuyapita yote ya mbele utaskia anakwambia ‘sawa
dereva’ nikimwambia tena kuhusu mazoezi utasikia
‘sawa dokata’ nikimwambia kuhusu mpira utamsikia
‘sawa kocha’ hata nikimwambia kuhusu mambo ya
elimu utamsikia ‘sawa mwalimu, haha yani
nimekumbuka mbali kweli japo asaiv hayupo rafiki
yangu,” alisema kisha baada ya furaha niliona
hudhuni machoni mwake.
“John una nini mbona umebadirika ghafla,” ikabidi
nimuulize baada ya kuona amebadirika, hata
machozi yalianza kumrenga renga.
“Hapana kidawa rafiki yangu walimuuwa,”
“Oohhh pole John, pole sana,” Nilimpa pole pia
sikutaka kumuuliza kuhusu rafiki yake alikufa na nini
mana nilijua nitazidi kumuongezea majonzi,
nilimbembeleza kwa kumtia moyo.
“Kidawa rafiki yangu ni yule ambaye ndio alikuwa
anakufata kule ulipokuwa ukiishi, kifo chake
kimeniuma sana, najitahidi kutokukumbuka ila
nashindwa kusahau,” aliongea kwa uchungu ikabidi
nibadiri mada japo nilikuwa nikimjua yule kaka
aliekuwa akinifata fata kule dukani kwa mangi nami
ilinigusa ila sikujali sana nilichojali ni furaha ya john,
alitulia hapo tukamaliza kunywa supu kisha akaenda
kuaga ndio tukaondoka na kuingia ndani ya gari kwa
ajili ya kurudi dar,tuliondoka safari ikaanza, safari
ambayo ilichagizwa na story za hapa na pale ile
simanzi yote iliisha story tulizopiga zilimbadilisha
hali yake, nilifurahia akumuona hivyo sikupendezwa
pia sikutaka kumuona John akiwa katika hali hiyo,
niliona furaha pekee ndio kitu anachotakiwa kulipwa
kutokana na mazuri anayonionyesha. Baada ya saa
kadhaa tulingia dar tena tukipita njia ya bagamoyo
ilikuepukana na foleni, tulichepuka bunju kisha
tukatokea tegeta hapo tukachepukia njia ya wazo
kwenye kiwanda cha cement tulipia moja kwa moja
tukiacha vituo mara kontena mara polisi kisha
flamingo mbele kidogo tukafika madale alipojenga,
hapo gari ikaingia mpaka ndani baada ya kufungua
geti lilikuwa geti la kutumia remote hivyo mchana
huu tuliingia ndani tukashuka aliniambia nitangulie
ndani yeye akafungua pale mbele kwa gari sijui
panaitwaje akafungua kisha nikamuona akienda sijui
kuchukua maji sikumwangalia tena nikaingia zangu
ndani, usingizi ulianza kuniandama mana kwenye
gari sikulalan kutoka na story za John sasa wakati
huu ndio uliniandama zaidi ule ambayo nilikesha
nikimuwaza john, nilitoka nje kumfata john alipo.
“John mimi naingia kulala kidogo,” nilimuaga nae
akaniambia kuwa atatoka kidogo kupereka gari yake
gereji kidogo, nilimhoji kama limeharibika,
akanijibu.
“Hapana huwa nafanyaga service gari yangu
inapotembea umbali mrefu mana ukiliacha hivi hivi
linakufa mapema,” alinijibu ila mi hakuna
ninachoelewa kuhusu magari nikamuaga na kuingia
ndani moja kwa moja chumbani kwangu,
nikajiwashia ac kisha nikalala, usingizi ulikuwa
mtamu wa aina yake ulinichukua na kunisafirisha
mbalii zaidi kisha kunirudisha nilistuka hapo
nikakomoa kuweka koo langu sawa nilihisi kiu na
njaa kwa wakati mmoja ikabidi niamke huyo moja
kwa moja mlango paaah, nikaungua ukajibamiza
wakati wa kujifunga, hapo nikajongea hima hima.
“Oohhh umeamka Kidawa,” nilipokewa na john
aliekuwa mezani akitenga chakula.
“John umepika,?” niliuliza kwa hamaki.
“Ndio nimepika nilionelea umechoka sipaswi
kukusumbua, kwavile najua kupika basi nipike tu
KUIMBA KUPOKEZANA” john alisema hapo
nilifarijika sana, hakika sijawahi fikilia kama dunia
ya sasa kulikuwa na wanaume kama John, nilikuwa
nikiwasikiliza tu marafiki na watu mbali mbali
wakitoa ushuhuda na wengine kupost mitandaoni
ubaya wa wanaume kumbe wanaume wazuri wapo
na wamejaa tele ona mimi sikuwa kuamini kama
wapo ila leo nimekutaja na john mwenye kila sifa za
kuwa mume wa mtu, nakushauri nawe ulievunjika
moyo, ulioumizwa uliodhalilisha ulie tengwa,
wanaume ndio baba zetu, ndio wajomba zetu, ndio
kaka zetu na hata babu zetu, hupaswi kuwaona
kuwa wote ni wanyanyasaji na wasio na huruma,
kumbuka mungu hakupi kile unachokitafuta eti
useme tu nataka mwanaume wa hivi na vile umpate
hapana sio rahisi Mungu hukupa kile unachostahili,
hivyo pengine hao waliokutesa na kuumiza
hawakuwa kusudio la mungu, hivyo usichoke weka
imani wako atakaekupenda na kukuheshimu lazima
atakuja tu kama sio leo hata kesho endelea
kuamini, Wanaume wabaya wapo na wazuri pia
wapo tena wazuri ndio wengi kuliko wabaya CHEMA
CHAJIUZA KIBAYA CHAJITEMBEZA.
Muda wote nilikuwa nikila chakula huku nikimtizama
john sidhani kama alikuwa akiniona ila niliamini
hakuniona, mana nilifanya hivi kwa muda mrefu
nakula alafu namtizama nakula alafu namtizama
tonge john tonge sahani hahaha, nilikuwa nikitizama
nyusi zake zilizojaa, macho yake yalioingia ndani
pua yake iliyochongoka na kukaa vizuri mdomo
wake uliojichora huku ukipabwa na papi kubwa za
lips tizama na zile ndevu zake woooiiiii, john
amenibamba.
“Inaonekana leo usoni mwangu kuna tivi,” john
alisema, hapo nikastuka kumbe alikuwa akiniona
wakati namwangalia.
“Hapana bana john mi natizama pale ukutane ebu
angalie kuna mjusi alipita nikawa namtizama,”
niliongea kwa kudeka muda huu ilikuwa ni usiku
sasa, baaada ya kumaliza kula tuliongea machache
kisha tukaagana kila mmoja kwenda kulala kwake,
si nikajisahau nikamshika john mkono alistuka
akaniangalia kisha akaniaga, sikuwa na namna
niliingia chumbani kwangu nikajilalie miye kidawa
john wangu tu atanasa.
Kiukweli siwadanganyi nilimpenda john, kikwazo
kilikuwa tunaogopana na kuoneana aibu nilihisi john
nae alikuwa akinipenda ila tatizo ni aibu.
Kuna muda nafeel kabisa kumkiss ila wooii
naogopa, nisaidieni basi kunitongozea john jamani
Nampenda mwenzenu nikinywa maji namuona
kwenye glass, nikila wali namuona juu ya kijiko,
nikitizama tivi namuona yeye tu hahahaha john huyu
 
Sehemu ya 33
Na Gaooh TheAuthor
Simu = 0654387935
ILIPOISHIAA SEHEMU ILIYOPITA.
Kuna muda nafeel kabisa kumkiss ila wooii
naogopa, nisaidieni basi kunitongozea john jamani
Nampenda mwenzenu nikinywa maji namuona
kwenye glass, nikila wali namuona juu ya kijiko,
nikitizama tivi namuona yeye tu hahahaha john huyu.
SASA ENDELEEAAAAA.
Tuliendelea na maisha haya kwa muda karibia
mwezi,bila ya kila mmoja kujihusisha na mwanzake
japo tulitamaniana, sikuwahi kujua john ni
mwanaume wa aina gani kwa upande wa pili yani
tunapika na kupakuwa pamoja muda wote tupo
ndani wenyewe lakini anashindwa nitamkia neno
nakupenda woiiii hivi yupo mwanaume kama john
anyooshe kidole juu, hakika hakuna labda john tu
john wangu.
Siku moja nikiwa nafuta vioo, siku hii john
hakuwepo nyumbani aliniaga kuwa anaenda kazini
basi niliona vioo vimejaa vumbi hivyo ikanibidi
nifanye kazi hiyo nikiwa naendelea na kazi hii
nilisikia honii kisha geti lilifunguka nikajua ni john
tu, hivyo sikutilia manani nikaendelea na kazi nikijua
akitoka ndani ya gari atanistua niliendelea na kazi
vioo nilivyokuwa nasafisha hapo milango ya gari
ilifunguliwa wakatoka watu,watu ambao mmoja
nilimfahamu ni john wangu ila mwengine sikumjua
kabisa alikuwa msichana alievalia sketi iliyovuka
makoti yake na shati jeupe la mikono mirefu huku
kichwani nywele zake akiwa amezibana nyuma, “Ni
nani tena huyu?” nilijiuliza bila majibu wakashuka
ndani ya gari ikabidi niache kufuta madirisha macho
na uso wangu vilikuwa kwa John na yule msichana,
sijui john hakuniona waliingia ndani wivu ulinikaba
koo nilihisi kumeza mtu, walioingia ndani nilitamani
kuwafata huko huko ila nikajikuta ninasita
nilichofanya nikaenda dilishani dilisha pale sebuleni
nilikodoa macho nikiangalia japo hawakuingia
chumbani ila walikaa pale wakionekana kuongea na
kucheka sikuwa nikisikia wakiongeacho nilitizama
vitendo mara john akaamka kisha akarudi sijajua
anachotafuta sikuhii niliumia zaidi nikahisi kuwa
kumbe john anamwanamke ndio mana hataki
kuniongelesha kuhusu mahusiano, nilikasirika kiasi
chake kisha sikukaa tena pale nilienda nyuma huko
kisha nikakaa nilikaa chini ya kibanda cha tenki la
maji hapo nikakaa asubuhi hiyo nilikaa muda mrefu
nikiwa nimefura.
Nikiwa pale nilisikia sauti za viatu vikijongea karibu
yangu hapo ikabidi niamke hapo kuamka nikakutana
na john.
“Kidawa vipi ulikuwa huku muda mrefu au nimekuwa
nikikutafuta sijakuona,?”
“Nilikuwa nikifuta vioo,”
“Sawa naenda kazini nimekutafuta nikutambulishe
kwa mgeni sijakuona ngoja nawahi kazini tutakutana
badae, aliniaga kisha akaondoka.
Siku hii sikuwa na raha kabisa niliona wazi
napokonywa john mikononi mwangu, hasira zangu
zilinifanya kutwa nzima nishinde kualala tu hata
kupika sikupika niliamua siku hii nile hasira tu,
ilipofika jioni John akarudi nyumbani, sikuwa na
furaha wivu ulinikaba kooni kabisa unataka kutokam
kumpenda john nampenda ila kumwambia ndio
mtihani, tulikula pamoja kama kawaidan kisha
tukaagana sikuwa mchangamfu kwake nilitamani
kumuuliza kuwa yule msichana aliekuja ni nani
wako? Ila nitamuuliza nikiwa mimi kama nani?
Mpenzi, Dada, rafiki au? Hivyo sikuwa na sababu ya
kuuliza nilibaki tu na jambo langu moyoni ndio
niliona njia lahisi ya kulimaliza ni kubaki nalo
moyoni.
Usiku mzima nilikuwa nikimuwaza john huku
matuanmaini ya kuwa mke wake yakianza kupotea,
nilijiona mfamaji asieisha kutapa tapa john wangu
ndio huyo anaondoka, hapo nikajiapiza lazima
nimwambie john nitamwambia tu, nilijisemea klisha
kujifunika shuka gubi gubi ikawa kama tiketi ya
kuianza safari ya usingizi iliyoandalia na usafiri wa
kitanda ,
Kulipokucha niliamka na kuandaa chai, chai ambayo
ndio kifungua kinywa cha john kila siku anapotaka
kwenda kazini lazima nimuandalie kifungua kinywa.
“Mbona kama chai ya leo haiko sawa,?” aliuliza john
hapo nikamwangalia.
“haiko sawa kivipi john,” nami nikamtupia swali
baada ya yeye kuuliza swali.
“Naona haina radha kama ya sikuzote yani imepoa
hata haijachangamka, ila anyway ngoja mimi niende
kazini nitakunywa huko huko na Loveness,” woiii
John alimtaja jina hapo akili ikaruka hasira zikapnda
mpka kichwani kumbe huyu msichana anaitwa
Loveness nilijisemea kabla sijamjibu john.
“Kama haiko sawa si ni bora bnikuandalie nyengine
john, hiyo mkono umenitereza ngoja nipike nyengine
mara moja,” nilisema ila john hakutaka tena.
“No, kidawa nacherewa, ngoja niwahi kazini
nitakunywa huko huko we kuwa na amani tu.”
Alisema hapo sikuwa na neno la kuongeza ilinibidi
ninyamaze mithili ya mtu aliefungwa mdomo na
kufuli tena kufuri kubwa lililoubana wote akashindwa
kutoa sauti,muda mchache john aliondoka na
kuniacha mwenyewe ndani akienda kazini, kiasi
fulani nilianza kuona john kama amebadilika, ule
upendo wote ulipungua hata kunijali hakukua kama
zamani, niliishia kuwa shuhuda tu wa yote yanayo
endelea, zilianza kubadilika siku zilianza mbili tatu
nne tano mpaka wiki hatukuwa kama zamo hapo
ikanibidi sasa nitafute hatima ya mambo hayo
nilijua wazi nikicheza nitamkosa john kabisa na
mimi kumkosa ni jambo ambalo sikutamani wala
sikuwa nikitaka linitokee niliamini john ndio
mwanaume wa ndoto zangu.
Siku moja john akiwa ndani baada ya kusema siku
hii anapumzika basi alikaa ndani, huku akifanya kazi
zake. Mimi nilikuwa nje nikifanya usafi kwenye
maua, nikiwa naendelea na kazi yangu nilisikia honi
ikipiga nje ya geti la nyumba ya john.
“Ni nani huyu,mbna john hakutoka leo?” nilijiuliza
hapo nikajongea nikilifata geti kujua honi inatoka
wapi nilifika hadi kwenye malango mdogo nilifika
kisha nikafungua na kutoka nje hapo ndio
nikaishuhudia gari ndogo aina ya ist ikiwa
imesimama nje ya geti ikabidi nilisogelee, woiiii
loveness alikuwa ndani ya gari hiyo nilingata meno
hasira zikinipanda.
“Umefata nini hapa,?” ndio swali nililomuuliza kabla
ya salamu.
“we nani unaeniuliza hivyo, pia unaniuliza kama
nani,” loveness alinijibu kwa nyodo kisha akashuka
ndani ya gari, nilimtizama kwa ghadabu zaidi, huku
nikimmezea mate nikitaka ajirete tu nimalizane nae.
“We dada wa kazi unaniuliza nimefata nini? hivi
unajielewa kweli,” alisema akiwa ameshuka ndani ya
gari aliyokuwa amepanda.
“Ndivyo john alivyokwambia sio,” nilimwambia hapo
nikashika nywele zake niliposhika nikajikuta
naondoka nazo alikuwa kavaa wigi, nilipomshikilia
akabaki na kipili pili hapo ndio tukashikana na
kuanza kuvutananikamlaza chini na kukaa juu yake,
nilitumia siku hii kumaliza hasira zangu, Loveness
niliona ndie alieleta shida kwangu mimi na john na
kufanya mpaka john apunguze upendo kwangu
wakati mwanzo hakuwa hivi,alitumia nguvu
akaniangusha kisha akasimama na mimi
nikasimama kisha tukaanza kurushiana maneno
huku tukivutana nilimtandika makonde kadhaa
yaliomuweka alama usoni kwake, kelele hizi za
mpambano usio na refa ndizo zilizomtoa john ndani,
alitoka nje haraka haraka na kutufata pale tulipo,
nilikuwa nimemshikam loveness sehemu ambayo
hakuweza kufurukuza yani nilimtia roba, John
alikimbilia kunishika mimi na kunitoa kwa loveness
ambaye alikuwa kama amechanganyikiwa .
“John john wewe wa kumtuma house girl wako
anipige john asante sana, nashukuru kwa
kunidhalilisha,” aliongea kwa hasira Loveness huku
akihema juu juu kama mtu alitoka kukimbizana,ali
toa matusi mengi kisha akaingia ndani ya gari na
kuondoka, john alikuwa amenishikilia mimi,
nilishangaa amenishika mimi huku asiongee
chochote kisha kunishika mkono na kuniambia
twende ndani, nami nilikuwa nikihema hasira
zilinipanda vilivyo.
“Ndio umefanya nini kidawa. vile,?”
 
SEHEMU YA 34
NA Gaooh
SIMU +0654387935
TULIPOISHIAAA SEHEMU ILIYOPITA.
"Ndio umefanya nini vile kidawa"
SASA ENDELEAAA..
John aliongea huku amefura hapo ni baada ya
kuongia ndani, nilijitetea nikimwambia kuwa
ameniita mimi house girl.
"John amenifanyia dharau ambayo imeniuma ndio
ikawa sababu ya kufanya vile nakuomba unielewe
john sijafanya makusudi,"milijitetea ila john
hakusema kitu zaidi ya kuongia ndani kwake hapo
akiniacha, nipo pale pale sitting room, halika john
alikasirika vilivyo sikujua anauhusiano gani na
loveness mpka akasirike vile.
Alipoondoka nilibaki peke yangu mawazo nayo
yakiniandama huku machozi yakinilenga lenga hofu
ya kumpoteza john ilinikaa vyema, Naweza sema hii
pia ilikuwa moja ya siku zangu za huzuni zaidi,
kwani hata ilipofika mchana nilijitahidi kupika
tenannikopika chakula kizuri nimfurahishe john
wangu ila pale nilipogonga mlango wake kumuita
aje tule hakuniitika wala kutoka, niliita mara kadhaa
ila hakukuwa na uitikie kulikaa mithili ya kuwa
hakuna mtu ndani, iliniuma zaidi hata hamu ya kula
sikuwa nayo tena, nilionelea bora ni sile chochote
kama john nimemkasirisha mpka akatae kula basi
hakuna sababu ya mimi kula chakula hicho, hivyo
nilichofanya niliielekea chumbani kwangu kitanda
ndicho kilikuwa mfariji wangu na mshauri wangu
mara nyingi nakitumia kulala nankuwaza mambo
yanayonitatiza kisha kunipa majibu kwavile nakuwa
nimetulia nikitafakari yanayonisibu.
Nilipoingia ndani kitanda kilinilaki huku kikinitazama
kwa bashaha, kilinitazama huku lugha ya vitendo
ikitumika ambayo niliona wazi kitanda kiliniita sijui
ni wenge langu ila nilijionea kikiniita kabisa "kidawa
njoo, kidawa njoo" hapo sikuwa na shaka nami
nikakipandia kitanda changu sponji laini ikanipokea
kichwa nikakiegemeza juu ya mto laini wa sufi
hewalaaaa, nikalala mawazo na hasira zangu zote
nilizizika hapa sikumbuki hata kama sikuwa
nimekula kwani hata njaa sikuwa nayo tena hakika
usingizi ulikuwa mtamu vilivyo, nililala mchana hadi
nafikia kuamka tayari kiza kiliingia hapo nikaamka
hima hima na kuanza kujinyoosha moja mbili moja
mbili mikono juu nikakaa sawa, na kufungua mlango
wa chumba changu nilisahau kuwa nilimkasirisha
john, nilipotoka chumbani kwangu nilipokelewa na
ukimya hata taa hazikuwashwa hiyo kumaanisha
hakuna mtu ndani, niliwasha taa kisha nikafungua
mlango wa nje na kutoka kulikuwa kimya pia,
ikabidi nirudi ndani kuangalia chakula ambacho
nakumbuka nilipika alafu sikukila, nilipofika kilipo
nachokilikuwa vile vile.
"Kwani john kaenda wapi inamana hasira zake bado
hazijaisha tu jamani," nilijiuliza mwenyewe,
nikajongea mpaka mlangoni kwake kugonga tena.
'john,john,john" niliita mara kadhaaa hola si john wa
sauti yoyote sikusikia.
Nilihisi kuchoka nikakaa chini ya malango wa john
kichwa changu nikikiegemeza kwenye migono
yangu ambayo ilikuwa juu ya magoti.
Nilikaa pale kwa muda kadhaa nilistushwa na sauti
za ndege walizokuwa wakiilia kwa kupokezana
pamoja na honi za magari zilizosikika kwa mbali
looh! Hapo nikaamka 'mama yangu' nilipatwa na
hamaki baada ya kugundua kumekucha, yani
nimelala mlangoni kwa john mpka asubuhi.
"Inamana john ametoka na hakurudi pia kalala huko
huko"nilijiuliza kisha nikang'ata meno kwa hasira
iliyoletwa na wivu "inamana yule msichana
nivyompiga hajatosheka ameona bora amchukue
john wakalale wote kabisa sio?" Nilikuwa tayari
nimeamka njaa iliniandamana vilivyo tumbo lilipiga
kelele mithili ya baba mwenye nyumba anaetaka
kodi yake kelele zilikuwa nyingi kutoka tumboni
hapo nikaliendea jokofu kisha nikatoka na boksi
lililosomeka Tanga fresh, nilifika nalo mpka kwenye
jiko la umeme nikachukua sufuria na kuyatia
maziwa yale ndani yake, dakika kadhaa yalianza
kuchemka hapo nikayatoa na kuweka kwenye
kikombe kisha kurudi kwenye jokofu (friji)
nikachukua mkate wa slesi tatu zilinitosha, nikaanza
kunywa maziwa nilipo maliza tumbo halikuwa na
shukurani kabisa mbali na kulipatia lilichotaka ila
nalo lilionesha hasira eti likaanza kuuma wooiii,
maumivu yalinikaaa tena likiuma chini ya kitomvu,
nilishikilia tumbo langu huku kelele a maumivu
zikinitoka, hata vyombo niliacha pale pale nikaingia
chumbani kwangu, nilijilaza kitandani kama mzigo
nikiita jina la john, wito ambao hakuna aliesikia
sikujua john ameenda wapi hivyo nikiumia peke
yangu, nilihisi kama mkojo unanitoka ila
nikashangaa mkojo gani huu unashuka kwenye
mapaja mzito ndipo nikajichungulia woiii, zilikuwa
nidamu.
Kutokana na mawazo nilishasahau kuwa siku yangu
ya hedhi imekaribia, hivyo nilipogundua ndio
yenyewe nilichukua boksi langu la HQ ambalo
nilikuwa nalo ndani kisha nikatoa pedi moja na
kujikokota mpka chooni huku maumivu nikifanya
kama siyasikii, nilipofika chooni nilijimwagia maji
kuondoa ile michulizi ya damu kisha nilipotakata
nikavaa pedi yangu na kujizungushia kagha, sikuona
sababu ya kuacha kufua nguo yangu ya ndani
iliyochafuka niliifua kisha kuianika huko huko
nikarudi chumbani kuvaa.
Nilivaa nguo zangu wakati huu yale maumivu ya
chini ya kitomvu yalipungua sikuwa nikiyasikia tena,
nilianza kufanya kazi zangu za ndani nikazimaliza
zote kisha nikapumzika, nikiwa nimepumzika
nikitamani ningekuwa na simu nimpigie john nijue
hali yake nilijihisi kummis zaidi john wangu, ooh
john wewe uko wapi.
Upweke uliniandama kukaa ndani nikahisi joto hivyo
nilitoka nje hapo nikatazamana na bembea ya
chuma nikajongea mpka ilipo nikaikalia juu yake
huku nikijibembeza, ilidumu pale kwa saa kadhaa
nilipojiona kuchoka ikanibidi niamke, niliamka na
kuingia ndani sikuwa na kwa kwenda moja haikai
mbili haikai nilingia ndani na kutoka kisha nikaanza
kuzunguka nyumba kushoto kulia kushoto kulia,
nilikosa kazi ya kufanya hivyo niliona bira nizunguke
tu nyumba.
Nilifika sehemu kwenye mnazi nikasimama hapo
nikawa naangalia nazi, nilifipoka hapa ndio
nikakumbuka kitu. "mbona gari yake ipo" nikajiuliza
hapo nibaada ya kuona gari ya john ipo,. "inamana
amekndoka na gari ya loveness amekuja kumchukua
usiku wakalale wote" niliongea kwa hasira huku
nikuma meno, "huyu dada ananitafuta nini jamani
kwani huu uchawi haurudi tu nifanye kazi
yangu,"nilijisema hapo nilipo sema hivyo
nikistushwa na upepo uliovuma kisha sauti za
vicheko zikasikika ambazo watu walicheka kwa
nguvu sauti zao zikiendana na kuvuma kwa upepo,
hapo nilikimbia kwa woga pale chini ya mnazi
hakika niliogopa hata nywele zilinisisimka vilivyo
ikabidi niingie ndani huku nikiogopa, nilipoingia
nilikimbilia chumbani nikiogopa cha ajabu vicheko
vile ni kama vilikuwa vikinifata "Mungu
wangu"niliogopa chumbani nikatoka na nilihisi si
salama nikiwa peke yangu hivyo nikatoka sebuleni,
nikiwa hapo nilisikia geti likifunguliwa, akili za
haraka haraka nikanijia nilichofanya ni kujificha
pembezoni mwa kochi kuu kuu, haikuishia getini
ndipo wa ndani nao nilisikia ukifungulia hapo
nikakunbuka sikuwa nimeufunga na funguo
nilijilaumu, mwishowe ulifunguliwa akaingia
mwanaume jilimtizama alipogeuka woow alikuwa
john, hapo nilitoka nilipokuwepo kisha nikajipereka
mpaka alipo nikamkumbatia john....
ITAENDELEAAAA
 
SEHEMU YA 35
NA GAOOH
SIMU 0654387935
ILIPOISHIAAA SEHEMU ILIYOPITA
Nilimkumbatia john baada ya kuingia ndani.
"We kidawa vipi?" Aliniuliza.
"John usiniache, nimekukumbuka john tangu
unikasirikie mwenzio sina raha nisamehe john
tafadhali,"niliongea kwa kudeka huku nikinisahaulish
a vile vicheko vilivyokuwa vikinifata, niliongea
nikimbembeleza john bila kumwachia, hapo
akanitoa.
"Kidawa."aliita jina langu, japo alikuwa akinitoa ila
nilimshikilia ipasavyo mikono yangu ikipita kiunoni
kwake.
"John najua nimekukosea naomba nikiri miguuni
mwako nisamehe john maumivu niliyopata kutokana
nakukasirika kwako ni makubwa john nauomba
msamaha wako tafadhali"nilishuka chini na kupiga
magoti mbele yake.
"inuka kidawa,"aliniambia hapo akanishika mkono
na kuniinua kisha akanikumbatia kifuani kwake,
"Wewe ni msichana mzuri kidawa,"John alinitamkia
huku akiendelea hapo mimi nilikuwa kifuani kwake
tu, "wewe ni msichana ambaye mwanaume yoyote
anatamani kuwa nawe, nakuona huna kasoro hata
moja"maneno aliyokuwa akiongea john yalinifanya
nianze kusinzia kifuani kwake, aliongea mengi ya
kunisifia ila katika maneno yote sijasikia akisema
nakupenda,
"Naomba niende chumbani, nikajimwagie maji mimi
nimekusamehe na yale yashapita, loveness
kanielewa" alipotaja jina la loveness ndio mzuka
ukanipanda, wivu nao ukaongozeka sikutaka
kumwachia nikijua loveness atakuwa ndani ndio
anamfata.
"john NAKUPENDA, nimeshindwa kuzuia hisia zangu
hakika nakupenda mwenzio sijawahi kumpenda
mwanaume hivi kiasi cha kumtamkia ila wewe ndio
wa kwanza John nakuomba usinifikilie vibaya"
nilitamka maneno hayo ambayo sijui hata ujasiri wa
kuyasem niliutoa wapi, aibu sijui nikiliziweka wapi,
kule kuona aibu na kuogopa kusema hisia zangu
kwa John leo kumeisha nilijikuta nikimtamkia wazi
wazi LIWALO NA LIWE.
"KIDAWA Mbona umecherewa sana.." kabla
hajamaliza kuongea nilimkatisha asiendeleee hapo
nikaanza kulia na kukimbilia chumbani, akili yote
ikijua john si wangu nilifunga mpk mlango wa
chumbani kwangu.
"KIDAWA KIDAWA" John aliishia kuita bila kumuitika
nilibaki nikilia chumbani kwangu, john nimpendae
tayari anamwanamke mwengine, jambo hili
liliniumiza zaidi sikutoka ndani humo mpaka kuna
kucha siku ya pili kilio ndio ulikuwa wimbo wangu
hata kulala sikuwa nimelala, ilipofika asubuhi john
aligonga kisha kuniaga huku akiniomba nifungue
tuongee ila niligoma nikimwambia aondoke zake,
nilisubiri muda kadhaa mpka nilipoona kimya
nikatoka ili kupata chai, niliandaa chai ambayo
nilikunywa na mkate niliishia kujifungia tu chunbani
kwangu, sikutaka kuongea na john kila alipokuwa
akirudi basi najifungia ndani zilipita siku tatu hali
ikiwa hivi hivi hata hedhi yangu ilikuwa imekata
tayari.
Siku hii ya nne ambayo ilikuwa ni ijumaa john
alinidanganya kuniaga kuwa anaenda kazini kumbe
sio kweli nilisubiri dakika kadhaa nikatoka loohh
kutoka nilimkuta john tena mlangoni amesimama
huku kashika maua na kiboksi kidogo chekundu
ambacho sikujua kina nini ndani yake.
"Niache john umeniumiza vya kutosha kwann,
hukwenda kazini kwa mkeo loveness unangoja nini
john,"nilisema kwa hasira hapo nikataka kurudi
ndani ndipo john akanishikilia kisha kunileta kifuani
kwake na kunibusu, busu la john lilifanya nisisimke
kila kiungo cha mwili wangu, nilijiona wa tofauti
sana sikuwa nimekutana na jambo hili muda mrefu
john aliponibusu na kunikumbatia nikajikuta
namng'ang'ania na kumganda kama ruba.
"Naomba unisamehe Kidawa ulinielewa vibaya
sikuwa nimemaanisha vile, maana yangu ni kuwa
umecherewa kusema yani, mimi pia nilikuwa
nakupenda ila umecherewa kunambia mwenzio
nilikuwa nasubiri mpka wewe unipende kwa hiyari
yako kuliko nikutamkie nakupenda kumbe moyo
wako haupo kwangu,"John aliongea mambo mengi
sana ambayo yalinifariji vilivyo, hapo john akapiga
magoti na kunivisha pete ya uchumba nilifurahi sana
siku hii ama kweli BAADA YA DHIKI FARAJA, niliona
nami faraja yangu imewadia sasa Good bye tabu na
shida.
Baada ya kunivisha pete John hapo jikajisalimisha
mwili wangu kwake, pale pale kwenye makochi
tulifurahishana, baada ya kumaliza kila mmoja
alimsifia mwenzake hakika siku hii nilienjoy sana
sikuwa kujua kama mapenzi ni matamu kiasi hiki,
tulielekea bafuni pamoja mimi na john wangu,
Mume wangu mtarajiwa.
Tuliingia na kuoga wote, hapo ndipo tukalianza
penzi letu jipya,penzi langu mimi na John wangu
upendo ulizidi kiasi kwamba sikutaka hata aende
kazini nikitamani tushinde ndani tu niwe namuona
kila mara.
"Sasa mpenzi wangu nisipoenda kazini unazani
tutakula nini"
"Kukuona nashibe tosha kwangu"nilimwambia
nikideka hapo nikiwa kifuani kwake, aliona ndio
nikamkibalia akaenda kazini.
Japo nimepitia changamoto nyingi za maisha ila
niliziona kama zinafaida kwangu kwavile ndio
zimenikutanisha na John wangu mwanaume
nimpendae kwa dhati.
Mapenzi yetu mimi na john yalikuwa ya kweli, ni
kwamba tulipendana mizani yetu ya upendo ili
elemea sawa sawa uzito ulikinzana.
Siku nazo zilisogea leo ikizaa kesho na kesho ikizaa
kesho kutwa,zilibadilika badirika tukiwa pamoja.
Siku moja ya mapumziko nilikaa na john niitaka
kujua jambo hivyo nilikaa karibu yake kisha
kuongea nilichopanga kumwambia.
"Mpenzi wangu" niliita kwa sauti ya chini huku
nikichezea ndevu zake.
"Naaam"aliitika kwa sauti yake ya bass iliyopenya
mpka ndani ya moyo wangu.
"Lini utanipereka kwa wazazi wako ili wanijue"
nilimuuliza huku mkono wangu ukiendelea kuvuta
vuta ndevu zake zilizojaa kidevuni kwake,
nilishangaa alibadilika nilipomuuliza swali hili huzuni
ilimkaa, alionekana mwenye majonzi muda huo huo.
"Mpenzi wangu kwani kunashida gani mbona hivi ?"
"Kidawa umenitonesha kidonda mpenzi wangu!"
"Kwani unaumwa, kipo wapi hiko kidonda jamani
mbona hukusema kama unakidonda ulifanyaje
kwani?"niliuliza maswali mawii mawili.
Nisijue anakidonda gani, hao ndio akaongea tena.
"Kidawa mimi wazazi wangu hawapo,"
"Hawapo kwani wameeenda wapi?"
"Kidawa wazazi wangu tayari wamekwisha fariki
miaka mingi iliyopita walikufa maji kwenye ajali ya
meli ya mv bukoba, ni majonzi na simanzi ndio
vilitutawala familia nzima kwani mama baba na
wadogo zangu wawili walikuwepo kwenye ajali
hiyo"john alisema huku akitokwa na machozi ndipo
nikapata kazi ya ziada na kuachana na ndevu zake
kisha nikaanza kumfuta machozi yaliokuwa
yakiserereka mashavuni kwake.
"Polee sana mpenzi wangu, nisamehe kwa
kukukumbusha yaliopita, umenifanya hadi na mimi
nijihisi uchungu jamani, pole sana"
"Asante mpenzi wangu"alisema hapo nikaamka na
kuliendea jokofu nikatoka na maji ya chupa ya
kilimanjaro nikajongea hadi pale alipo John
nikampatia maji tena nilimnywesha, alipotosheka
nikabadiri mada ili nimrudishe kawaida nilianza
kuongelea vitu vyengine hapo akacheka nikaona
tabasamu lake tena.
Mada ya ndoa niliiacha kwa wakati huo ila baada ya
kimya kifupi john alianza kuongea
"Upo tayari kuolewa na mimi..
 
SEHEMU YA 36
NA GAOOH
SIMU 0654387935
ILIPOISHIA SEHEMU ILIYOPITA
"Upo tayari kuolewa na mimi,
SASA ENDELEAAA.
"Upo tayari kuolewa na mimi,kidawa" john aliniuliza
swali ambalo jibu lake lilikiwa ndio sikuwa na
kipingamizi chochote john ndio alikuwa mwanaume
wa ndoto zangu hivyo nilimkubali.
"Ndio John nipo tayari kwa moyo wangu wote,
Nakupenda sana" nilisema hapo nikahamisha mkono
kifuani kwake.
"Basi tufanye maandalizi mwezi ujao tufunge
ndoa,nitaalika wajonba zangu pamoja na ndugj
zangu na marafiki, je vipi kuhusu familia
yako?"aliniuliza hapo nikakosa neno, hata ule
mkono kifuani kwake niliutoa.
"Vipi?" Aliuliza.
"John historia yangu haijatofautiana na wewe, mimi
pia wazazi wangu walishafariki miaka hiyo iliyopita
ninavyokwambia hapa sina ndugu yoyote, yani hata
nikifa kesho kwa kuzikwa sina"
"So sad..."john alisema"Pole sana kidawa kumbe
nawe ni yatima, inauma sana, naomba
nikuhakikishie nitakuwa kila kitu kwako kuanzia
rafiki, mpenzi na hata ndugu"aliongea mambo
mengi kiasi cha kunifariji, nikajikuta napata furaha
ya ajabu nikamkumbatia john kwa nguvu, nae
akanikumbatia nilijihisi kuzaliwa upya kwa wakati
huu furaha yangu ilikuwa kupendwa na john pekee,
tulianza taratiibu za kuoana, kiukweli sikuwahi kujua
dini yangu mana nimejijua tu mimi kidawa alafu
nikaingia kwenye uchawi nikiwa mdogo kisha
kuutumikia, mwishowe nikaingia kanisani sasa
nataka kufunga ndoa na john, ilinibidi nifate dini
yake john, aliwaalika marafiki ndugu pamoja na
watu wake wa karibu harusi yetu ilifungwa katika
kanisa la EFADHA MINISTRY liliopo mwenye,
ilikuwa furaha kwetu wote kwa pamoja tukayaanza
maisha mapya,maisha ya ndoa kati yangu na Mume
wangu kipenzi john sasa mimi nimekuwa mrs john,
niliamini huu ndio mwisho wa matatizo yangu ya
maisha nilijiona nimefukia shida zote na tabu zote
za nyuma nilizopitia msemo wa BAADA YA DHIKI
FARAJA niliuona ndio unaanza kutendeka kwangu
kumbe la haukuwa mwisho naweza sema ndio
ulikiwa mwanzo mpya mwanzo wenye hatim ya
mwisho wangu.
Tulipendana mimi na John wangu, alinishirikisha
kila siri zake na hata mipango yake ya bdae alikuwa
akinishirikisha.
Siku moja tukiwa mezani tunalisha kwa mahaba
kilizuka kizaa zaa, kizaa zaa ambacho nilianza
kutapika pale pale bila hata kutalajia.
"Vipi mke wangu una nini? "
"Sielewi mume wangu hali hii imekuja tu ghafla"
"Au kuna kitu umekula hakija kupenda,"alisema john
hapo akiniwekewa maji kwenye glasi kabla
sijaipokea nilitapika tena, ikabidi aniambie twende
hospitali, niliamka kwa kujikongoja huku nikiwa sina
nguvu kabisa mpka tukafika nje lilipo gari yake
alinikalisha vizuri nankunifunga mkanda alafu
tukatoka kuelekea hospital kama alivyonambia,
ilikuwa usiku hivyo aliona bkra atafute hospital nzuri
ambayo nitalazwa moja kwa moja kuliko kupimwa
tu nankuondoka hivyo aliendesha gari kwa kasj nnia
nzima akinibembeleza mana nilikuwa nikilalamika
kuuma kwa tumbo hasa chini ya kitomvu japo
kulikuwa na foleni lakini haikuwa kubwa sana ya
kusababisha msongamano wa magari hivyo
alipofika pale bondeni akachepukia njia ya kawe
huko alienda moja kwa moja mpka mikocheni
kwenye hospital ya private alinifikisha na kuwaita
manesi ambao walikuja nankitanda kunichukua,
nikalazwa kisha kuingizwa wodini., nikiwa ndani ya
chumba kile kulikuwa na dokta ananishughulikia
hapo john tukimwacha nje, walikuwa wakinifanyia
vipimo dakika kadhaa akaondoka baada ya
kuandika kwenye daftali lake alilolishikilia mkononi.
Nikabaki peke yangu nisijue kinachoendelea, nikiwa
pale john alikuja.
"Mke wangu, unajisikiaje" aliniuliza john huku
akishika nywele zangu.
"salama naendelea vizuri dawa walizoniwekea
zimenisaidia kiasi fulani"nilimwambia.
"Mke wangu nimepewa taarifa njema, sijui upi tayari
nawe nikupe"john alisema.
"Taarifa gani hiyo, njema"
"Upo tayari au?"
"Ndio mume wangu,"
"Nimeambiwa kuwa wewe tayari ni mjamzito,"taarifa
hii ilikuwa njema kwetu tulifurahia kwa pamoja
dokta nae alikuja, aliongea vile vile alivyonambia
john.
"Tunaweza kuondoka Dokta,"John aliuliza.
"Hapana kuna vipimo bado hatujamaliza nadhani
kesho ndio mtaondoka" Dokta alisema, hapo john
akaniaga kuwa anatoka na kwenda kuniletea chakula
kwavile sikuwa nimekula tena baada ya kile
nilichokula chote kukitoa,akatoka na kuniacha.
Nilipobaki peke yangu nilimshukuru Mungu,
nikijiona sasa nimepata ndugu yangu, ndugu
ambaye ndio atakuwa kila kitu kwangu, Mungu
mkubwa dakika kadhaa John akarudi.
"Pole kwa kukuacha mwenyewe mke wangu,
nimerudi sasa"
"Usijal mume wangu, hata usingerudi mimi niko
sawa tu," nilimwambia, akatoa kile alichoniletea
alileta ndizi za rosti zilizochanganywa na nyama
akaleta na juisi ya matunda kisha akaanza kunilisha.
"Na wewe?" Ilibidi nimuulize mana alinilisha mimi tu
alafu yeye akawa hali.
"Ukishiba wewe malkia wangu ni sawa tu kama
tumeshiba wote,"john alisema.
"Hapana John wangu hiyo ni misemo ya zamani
unapswa kula na wewe,"
"Kula kwanza wewe ukishiba nami nitakula,"
"Basi na mie sili kama we hutaki kula,"nilimwambia
alafu kwa kudeka nikageuza shingo pembeni, ndipo
akaanza kula na yeye tukawa tunakula wote,
aliruhusiwa kulala na mimi japo kulikuwa na kitanda
cha mgonjwa tu ila hakutolewa nje hivyo tulibaki
wote mpka napitiwa na usingizi aliniaga kwa
kunibusu, sijujua kilichoendelea muda wote, hadi
pale sauti za watoto na mchaka mchaka wa miguu
ziliponiamsha niliamka na kuona John hayupo
sikujua alipokwenda hivyo nilijinyanyua kitandani
alafu nikakaa miguu yangu nikiiweka chini ya
sakafu, ila kabla sijasimama nitembee john alikuja.
"Umeamka mpenzi,?" Ndio swali aliloniuliza.
"Nimeamka John wangu, ulikuwa wapi?" Nilimtupia
swali.
"Nilienda kukuanalizia supu, ila wameniambia
wataleta," alisema tukaongea machache muda huo
huo supu ilikuja wakati huu niliweza kuamka
mwenyewe hivyo supu ilivyokuja nilimwambia John.
"Mume wangu sasa ni zamu yangu kukulisha we
umenilisha usiku sasa ni zamu yangu na
mimi,"nilimwambia japo alikataa akitaka kuendelea
kunilisha ila niliweka msimamo wangu ambao aliutii
kabisa nikanywesha, dakika kadhaa tulimaliza hapo
tukaongozana mpka kwa daktarj na kupewa
maagizo kadhaa, wakimfundisha john jinsi ya
kunitunza kama mjamzito, baada ya John kufanya
malipo tuliongozana nje mpka kwenye gari yake,
akanifungulia mlango nikaingia,
Mbali na kunipenda John aliniweza kunijali kama
malkia, alinijali vilivyo naweza kusema Joh ni
mwanaume wa mfano natamani ningekuwa na
uwezo ningezihamisha tabia za john kwa kila
mwanaume Hakika Duniani tungeishi kwa amani
kabisa.
Siwasemi vibaya wanaume wengine ila nawaweka
sawa wanaume wengi wamekuwa wakiubeba
udhaifu kwa mwanamke kama fimbo ya kunchapia
na kumuweka alama zisizofutika, Unakuta
mwanamke bado unampenda unamjali unamvulia
kwa kuwa hana kipato ila bado anakunyanyasa, au u
akuta mwanamke anahangaika na mumewe kipindi
mwanaume hana chochote ila akija kupata basi
thamani yake haipo tena, atamdhihaki na
kumdhalilisha Ohhh Mungu tusaidie wanawake wote.
Baada ha kutoka hospital gari ilitembea umbali
kadhaa kisha tulifika nyumbani Madale, akalifungua
geti tukaingia ndani kisha akalifunga geti, alikuja
akanifubgulia mlango nikashuka akinishika kisha
akafunga mlango tukaongozana ndani.
Nikienda moja kwa moja kukaa kwenye sofa.
"Mke wangu,"aliita.
"Abeeh Mume wangu"nikimwitika.
"Utaoga kwanza au nikuandalie chakula ule kwanza,"
"John" nilimwita.
"Naam"
"Unafanya yote haya kwa ajili yangu,?" Nikimuuliza.
"Wewe ndio kila kitu kwangu sasa, wewe ni kama
ndugu, wewe ni kama familia yangu sasa, sinabudi
kukufanyia kila kitu Mke wangu" alisema hapo
maneno yake yalitua vyema masikioni mwangu,
huku sauti yake ikindirima kwenye ngoza za masikio
yabgu taratiibu nikahisi usingizi kunipitia.
"Nakupenda john" nilimwambia Huku nikishikilia
mkono wake.
"Nakupenda pia Mke wangu"alisema kisha
kunianbia anaenda kuniandalia chakula, ila kabla ya
kuondoka aliniwashia tv na kuniacha nikiangalia....
 
SEHEMU YA 37
NA GAOOH
SIMU 0654387935
TUNAENDELEA PALE TULIPOISHIAA
"Nakupenda pia Mke wangu"alisema kisha
kunianbia anaenda kuniandalia chakula, ila kabla ya
kuondoka aliniwashia tv na kuniacha nikiangalia....
Sasa endeleaaa.
Alienda jikoni kuniandalia chakula nami nikabaki
pale nikitizama tivi, nilikaa dakika kadhaa huku
nikisikia tu sauti za vikaangizo jikoni niiliona sio
vizuri nikimwacha john apike peke yake hivyo
nikajitahidi kuamka sio kama nilizidia sana hapana
nilikuwa na nguvu hata za kutembea ni vile john
alinidekeza tu, hivyo niliamka pale nilipokuwa
nmekaa nikaelekea jikoni kwa kunyata bila ya John
kuniona nilipofika, nilimsogelea mpka alipo akiwa
kashika flampeni nyeusi, hapo nilijisogeza zaidi
nikamshika huku ubavuni kwenye mbavu looh
aliruka nusura atupe flampeni.
"Haah mume wangu hazijaisha tu"
"Zinaanzaje kuisha wakati kila nikikuona zinarudi
upya, alfu mbona umekuja huku si nimekwambia
upumzike nikupikie"alisema.
"Nimeona kule nipo mpweke sana ndo mana nikaja
huku mume wangu"
"Hapana unapaswa kukaa kule mke wangu"
"Hapana john napenda kukuona kila mara"
nilikwambia hapo nikiwa nimemlalia mgongoni huku
mikono yangu nikipitisha kiunoni kwake tukiwa
tumesimama.
Alinilisha kipande cha karoti kisha akanibeba na
kuniweka juu ya meza ya pale jikoni ambayo
ilijengwa kwa zege sio mbao, nilikaa nikimwangalia
john wangu anavyopika.
"Ebu onja na wewe mboga kama imeiva" alisema
huku akinyooshe mwiko ambao ulikuwa na kipande
cha nyama juu yake, nilitaka kukiokota ila akaniwahi
alikichukua yeye kisha kunilisha, nilipokitia
mdomoni nilimsifia kwa kumwambia jinsi kilivyo
kitamu, alifurahia tukacheka pamoja hapo alipika
hima hima kisha akamaliza tukarudi mpka dining,
haoo akaniambia nikae akanza kutenga chakula siku
hizi tulikuwa tunakaa karibu sio kama zamani, yani
viti vyetu vinakaa karibu karibu hapo tukaanza kula
kwa kulishana dakika kadhaa tulimaliza hapo ndio
tukaelekea bafuni kuoga tuliogeshana huku
tukitaniana na kurushiana maji, nilifurahia sana
michezo hii ilinirudisha utotoni kabisa, kwa vile ni
michezo ambayo watoto huicheza ilikuwa furaha
kwetu sote tukamaliza na kurudi ndani tukijifuta
maji.
Siku zilianza kusogea ikianza wiki kupita nilitamani
kuwa na biashara yangu kukaa nyumbani tu
kulinichosha hivyo usiku mmoja nikiwa kitandani na
john nilimdokezea mada hiyo.
"Mume wangu, hivi unafurahia mimi kukaa
nyumbani tu hivi?"
"Unamaana gani mke wangu,?"
"Yani mimi kuwa wa kukaa tu bila kufanya kitu
chochote"nilimwambia huku nikiwa juu ya kifua
chake kipana.
"Oohh, naelewa mke wangu, ila si unajua wewe ni
mjamzito"
"Najua ndio ila sio sababu!"
"Hapana hiyo ni sababu tena kubwa unapaswa
kutulia yani usifanye kazi yoyote ngumu,"
"Sasa wewe ukitoka nabaki mwenyewe kutwa nzima"
"Najua mke wangu ndio mana najitahidi mara nyingi
kurudi nyumbani mapema,ondoa hofu mke wangu"
"Hapana John nina hamu na mimk kuwa n sehemu
ambayo itaniweka busy"
"Nakumba usijal, ukijifungua fu nakufungulia ofisi na
wewe uwe kama wanawake wengine wa mjini."
"Ofisi ya nini?"
"Yani nitakufungulia duka ambalo utakuw ukikaa
ukiuza nguo z kike madera mabaibui na hata blauzi
za kike na viatu."alisema hapo nilifurahi
nikamkunbatia na kumbusu.
Asubuhi john aliamka akanda chai kisha kwenda
kuoga alipotoka akaniamsha na kuniaga nilibaki
peke yangu, sikuona sababu ya kuamka mapema
nilichoamua ni kulala tena hadi pale nilipohisi
kuumwa na njaa ndio nikaamka na kuiendelea meza
ambayo ilikuwa na themosi kubwa ya chai pia ndani
ya jokofu kukikuwa na pakti kubwa na maziwa fresh
nilichukua na mikate nikapaka blue band kisha
nikaanza kula wakati nikila mawazo yote yalikuwa
kwa john nikimuwaza na upendo wake, nilikuwa
nikiwaza huku nikitabasamu peke yangu, nikajikuta
mpka naangusha kipande cha mkate nilichokuwa
nimeshikilia.
Baada ya kuhisi nimetosheka hapo niliamka mezani
na kutoa vyombo ambavyo hata sikutaka kuviosha
nilivitelekeza jikoni kisha nikatoka nje na kwenda
kukaa ju ya bembea kisha niiaanza kujibebembeza,
niliamka baada kuhisi nimechoka hapo nikarudi
ndani yani sikuwa na sehemu ya kwenda ilikuwa ni
kama kuku ndani ya banda yani atazunguka kote ila
atarudi pale pale, hapo nikawasha tivi na kuanza
kuangalia nikiwa naangalia tivi nilihisi gari kuingia
ndani sikuwa na shaka kwa vile nilijua ni john
wangu na kweli aliingia hapo akaja mpaka nilipo na
kuniziba macho na mikono yake.
"John" nikaita hapo akakaa kimya.
"Mume wangu" bado kimya nikaanza kuogopa sasa,
nikawa nahangaika kutoa mikono yake alivyoona
nahangaika sana ndipo akacheka na kuniita
muoga"John bana mi sitaki kutishana si wajua mimi
muoga."akacheka tena kwa sauti.
"acha woga mke wangu, vipi lakini za kutwa"
"Salama alafu vipi mbona leo umerudi mapem
hivi?"nilimuuliza.
"We saa kumi na moja hii kasoro ndio mapema."
"Haijafika bana, si saa hizi hizi tu"
"Ebu tizama palee"alisema hukubakinyoosha kidole
ilipo saa kubwa ya ukutani, nami nikatizama kweli
ilikuw saa kumi na moja kasoro.
"Vipi umekula nini?"aliniuliza.
"Hapana sikula kitu"
"Kama nikivyoju tu utakuwa hujala basi si tatizi
utabiri wangu umeenda sawa"alisema hapo akatoka
nyuma ya kochi alipokuwa amekaa kisha akasogea
huku mbele yangu akiwa n mfuko ambao ulionekana
unavitu ndani yake.
"Umebeba nini?" Ndio swali nililo anza nalo kwake.
"Hahaha unaharaka mama kama kama unaoga nje
vile" aliongea huku akicheka hapo tukacheka wote,
ndipo akatoa boksj refu refu lenye umbo kama
duara.
"Guess what" alisema kisha akafunua, waooooh
ilikuwa piza nilifurahi kuiona.
"Nakula bila kunawa sasa"nilimwambia huku
nikiikata.
"We kula tu ukiugua mimi si nipo nitakupereka
hospital" alisema kisha nikaendelea kula nae
akasema anakula bila kunawa tukawa tunakula wote
kama kawaida hatukuacha kulishana, tulishaambulia
pizza ile mpka ikaisha kila mmoja akitangaza
kushiba. John akaamka na kuelekea jikoni dakika
kadhaa alirejea akiwa kashik maji ya chupa na
bakuri ambalo lilionekana lina maji,alipofka nilipo
akaninawisha kisha kunipa maji ya kunywa ulikuwa
ni upendo wa aina yake.
"Umeshiba sasa?"
"Yeah hapa niko vizuri nimeshiba baba"
"Sasa kwa vile umeshiba basi kuna mchezo
tuucheze."
"Mchezo gani?, John si unajua nimeshiba
kukimbizana siwezi."Niliongea kwa kudeka.
"Haha wapenda kukimbizwaa, sio mchezo huo hata'
alisema huku akicheka, akaushika mfuko wake na
kutoka na boksi mbili ambazo zote zilifanana
sikujua zina nini ndani yake wakati huu nikakaa kwa
kutulia nikimsikiliza john.
"sasa ni hizi ndani ya hizi boksi kuna vitu hivyo
utachagua boksi moja utakachokikuta ndio
chako,"alinipa maelekezo nikawa nimemuelewa
ilivyo akayaweka mezani na kuniambia nichague,
maboksi yote yalifanana hata gift paper
yaliyofungwa zilifanana, sikuchukuza sana
nikachagua la pili tofauti na la kwanza lililokuwa
mkono wa kushoto nikichagua la upande wa kulia,
hapo john akaja kulichukua na kunionyesha
nilichochagua.
"Woooh uko makini umechagua kitu ambacho
huna"alisema kisha akanionyesha simu hapo
nilifurahia ilikuwa simu kubwa aina ya samsung
alitoa na line pale pale anbayo amekwisha isajili
akaiweka ndani ya simu kisha akatoka nje na
kuniambia nipokee tuangalie kama iko sawa, ilikuwa
kama mchezo vile alipotoka nje alipiga kisha
kuongea na mimi huku akinitania.
Baada dakika kadhaa akarudi ndani na kufungua
boksi la pili lilikuwa na cheni ya gold sikuitamani
sana kwa vile nilikuwa nayo tayari, saa zilisogea
mpka usiku ukaingia nikiwa na john alipika tukala
kisha tukaoga pamoja na kupanda kitandani kulala,.
"Nikijikuta niko mbioni nikikimbia huku mwanangu
nimembeba kwa mbele, sauti na upepo vikivuma na
kunifata kule niendako, mwanangu nae hakuacha
kulia sauti yake kali ya mwisho ilimtoka tena tukiwa
kati kati ya msitu uliojaa kiza mara kadhaa
nilianguka chini viganya vyangu viliishia kushika
mufupa na mafuvu ya vichwa ambayo yalijaa eneo
hilo, nikiwa kwenye harakati za kuokoa uhai wangu
ghafla mbele yangu alitokea binti wa makamu
ambaye alipotokea eneo lile lilipata mwangaza binti
mdogo wa miaka karibia 17 alisimama mbele
yangu tukitizamana......
 
SEHEMU YA 38
NA GAOOH
SIMU 0654387935
ILIPOISHIA SEHEMU ILIYOPITA..
mifupa na mafuvu ya vichwa ambayo yalijaa eneo
hilo, nikiwa kwenye harakati za kuokoa uhai wangu
ghafla mbele yangu alitokea binti wa makamu
ambaye alipotokea eneo lile lilipata mwangaza binti
mdogo wa miaka karibia 17 alisimama mbele
yangu tukizamana......
Sasa endeleaaaa...
Nilitizama binti yule aliekuwa akiniangalia na macho
amenikazia vilivyo, niliogopa huku kilio cha
mwanangu kikiendelea, ghafla binti yuke alinyoosha
mkono akininyokshea baada kuwa kimya sasa ndio
alikipa uhai kinywa chake nilimtizama.
"Nipe huyo mtoto,"alisema huku akileta mikono
yake.
"Nikupe huyu ni mwanao unamtaka wa nini,?"nilimuli
za huku nikimkodolea macho pima.
"Huyu sio mwanao, tupe mwanetu," alisema tena,
tulianza majibizano ya maneno kila mmoja akiongea
la kwake yeye akitaka mtoto na mimi nikimkatalia
kitendo hiki ndicho kilimfanya binti yule afanye
maamuzi ya kikubwa, alinitizama kisha kuhema kwa
nguvu hapo ulitoka upepo wenye ambao upepo ule
ulinirusha pembeni ya pale nikamwachia mwanangu
niliekuwa nimekumbatia baada ya kumwachia ndipo
yule binti alimchukua nikiona kabisa hapo hata
nguvu za kuamka siku nazoniliishiaa kupiga kelele
tu.
"Mwananguuuuu" ukelele ulinitosh hapo nikastuka
kutoka usingizini kitendo ambacho nilimstua mpka
John aliekuwa amelala, wakati huo.
"Mume wangu wamemchukua mtoto wetu
wamemchukuaaa wamemchukuaaa"nilipiga kelele
nikiwa kama mtu alichanganyikiwa au kutokwa na
fahamu.
"Mke wangu wamechukua wakina nani nambona sisi
hatuna mtoto nini kinaendelea?"John aliniuliza swali
ambalo sijaona kama nilipaswa kulijibu wakati huo.
"John mtoto wetu wamemchukua hayupooo
wamenikimbiza wakamchukua" nilizidi kubabaika
hapo john ikabidi aamke na kuwasha taa, uzuri taa
ilikuw ni zike za mezani hivyo aliwasha hapo hapo
mana sikutaka aondoke kabisa woga ulinikaa mimi
nikamkumbatia.
"Unatatizo gani Kidawa Mke wangu mbona hatuna
mtoto,"alisema hapo mimi wakati huo nilikuwa na
woga.
Nilimueleza kilichotokea mpka kukimbizwa kisha
mtoto kuchukuliwa.
"Ni ndoto usijal mke wangu zitapita,"ndicho
alichonijibu yeye aliona ni ndoto ya kawaida ila
mwenzake haikuwa ya kawaida kabisa
ilinikumbusha kipindi cha nyuma ilivyonijia ndoto ya
namna hii, ila niliamua nipuuzie nikiamini yale ya
zamani yashapita.
"Hiyo ndoto mke wangu, itakuwa ni mawazo yako
unawaza sana kuhusu mtoto ndio mana zinakuja
ndoto za namna hii."alisema kisha kunipiga piga
mgongoni.
"Sasa ni saa kumi usiku hivyo lala mke
wangu,"alisema John baada ya kuangalia saa iliyoko
mezani chumbani kwetu, nilionelea bora nilale
kifuani kwa mume wangu japo woga bado nilikuwa
nao alinibembeleza mpka usingizi ukanipitia hapo
nikalala.
Nilistuka baada ya John kunistua kwa kunitingisha
na kuniita.
"Amka mke wangu, nimekuandalia chai" alisema
kisha akaniamsha alinichukua kwa kunibeba yani
mkono mmoja umeshikilia miguu yangu na
mwengine ukitulia juu ya mgongo wangu hapo na
mimi nikapereka mikono yangu kwenye shingo yake
tukatoka mpka dining alinishusha na kuniweka juu
ya kiti nikakaa, baada ya kukaa aliniwekea maziwa
kwenye kikombe kisha sukari kidogo akaikoroga
ndani yake, alinisogezea na sahani ambayo
alikaanga mayai ambayo tayari aliyakata kata na
uma akaanza kunirisha, kitendo kile kilinifanya
nisahau yake yote ya jana usiku maziwa.
"Leo nataka tutoke,"
"Twende wapi John"
"Nataka twende sehemu, tukafurahie, upo tayari?"
"Wapi huko john sasa hupataji mpka nikubali je
nisipokupenda huko"
"Nataka twende mbudya,"
"Ndio wapi huko, mbona sipajui,?" nilimuuliza,
"Oohh, pole mke wangu inamana hupajui mbudya
hujawahi fika ama hujawahi kupasikia?" alisema.
"Kuna vyakula vizuri na je huko ni hotel kubwa au?"
Nilimuuliza tena swali ambaloilimfanya acheke kwa
nguvu.
"Hahahahaha,"
"Unanicheka john basi sitaki sitaki" nilisema kisha
nikajifanya nimesusa.
"Mke wangu sijakucheka nimefurahi tu, ngoja sasa
nikwambie mbudya ni wapi."
"Sitaki ushanicheka kwanza siendk tena huko"
niliongea nikideka John akapata kazi ya ziada
alianza kunibembeleza, alinibembeleza akiniomba
nimuelewe, hapo nikamkubalia kishingo upande.
"Mke wangu mbudya ni kisiwani, yani huko unaenda
na boti unafika huko ni sehemu nzuri ya kufurahia
kuna hali ya hewa nzuri kuna vivutio mbali mbali
hata misitu pia ipo"
"Mi naogopa maji nitaendaje huko" nilimtania John.
"Najua waniongopea nakuomba twende nataka hizi
ndoto zako uzisahau kabisa sifurahishwi wala
sipendi nikikuona ukiwa na huzuni" alisema kisha
nilimkubalia alifurahi kusikia nimekubali hivyo
aliniambia nijiandae tuondoke mapema kisha
tukalale huko alafu turudi kesho yake nilimkubalia,
baada kumaliza chai niliingia bafuni kujiandaa yeye
alikwisha oga tayari, baada kutoka bafuni alikuja na
kunipaka mafuta kisha akanichagulia nguo ya kuvaa
na kunivalisha tulitoka na gari yetu njia nzima
alinisifia uzuri wa kisiwa hiko.
"Yani mke wangu ni kuzuri tofauti kabisa na Coco
beach yani kule ni fukwe ya watu wenye pesa
zao,"aliendelea kunitambia uzuri wa huko.
"Na wewe uliendaga na nani huko, mpaka unapasifia
hivyo?"
"Kazini kwetu huwa tunatoka mara nyingi tunaenda
sehemu nyingi, tushaendada magoroto na hata
mbudya huwa tunatembea vivutio mbali mbali hata,"
"Magoroto ni wapi?"Nilimuliza, john alinisikiliza yani
alinifundisha kila isichojua yani kila ninachomuuliza
alinijibu tena vizuri.
"Magoroto napo ni kivutio cha utalii yani ni sehemu
ambao ipo kati kati ya msitu alafu maji yamejitenga
na ku hukue eneo kubwa ni pazuri sana na
panavutia kupaona hata kwenda yani
kunamaporomoko ya maji ya mawe makubwa,
wanafanya utalii wa ndani ya maji nakumbuk mimi
nilivu samaki mmoja tukamchoma na wenzangu
tukamla"John alinisimulia ilivyokuwa kwenye safari
yao hiyo, baada muda sasa tulifika bandari ambayo
ndio zipo boti za kwenda huko mbudya, John
alikodisha boti ambayo tulikuwa wawili tu mimi na
yeye kisha safari kuanza ilituchukua dakika kadhaa
mpaka tukafika mbudya nilishangaa mazingira yale
yalikuwa mazuri ya kupendeza alafu kulijaa watu
wahindi na wazungu walieneo eneo like huku
waswahili wachache pia walikuwepo.
Tulireport kisha kutafuta eneo ambalo tulikaa na
john akaagiza madafu.
"Si wanasemaga maji ya madafu ni mabaya kwa
wanaume,?"
"Maji ya nazi au maji ya madafu,"
"Maji ya nazi si ndio hayo hayo ya madafu"
nilimwambia.
"Hata kama ila tofauti"
"Shauri zako utatokwa na busha"
"Hahahaha" tukacheka pamoja.
"Si utanipenda na busha langu au?"
"Yataka moyo" nilisema hapo tukacheka tena huku
tukifyoza maji ya madafu ambayo tuliagiza, yalikuwa
matamu kiasi chake.
John aliniambia nimsubiri yeye akaelekea kwenye
hotel, alichukua chumba kisha kurudi hapo
akaniambia twende nilimfata tukaenda ndani
aliagiza chakula na vinywaji tukala na kunywa kisha
tukienda kuogelea nilipotosheka nikarudi na john
ndani hapo nikisikia baridi nilivaa nguo zangu jioni
hiyo nikamuomba John tukatembee kwenye minazi
na mibuyu mikubwa inayopatikana huko.
Na mimi nilijitoa ushamba nikaanza kupig picha na
simu yangu nikiyonunuliwa na John nilifika sehmeu
ambayo inambuyu john alisema anaenda kunikotoa
buyu akaniambia nisiondoke hapo nilipo nilimwitika
ila sikufanya Kile alichokitaka, hapo nilianza
kuzunguka zunguka kwenye mibuyu nikitizama na
kupiga picha wakati nikitembea bila kujua, nilijikuta
nikitokomea nisipokujua miti mikubwa ikiyoweka
kimvuli ndio iliyokuwepo sehemu hiyo nikiwa
naendelea na safari nilishangaa mbele yangu chini
ya mbuyu kuona mtu ameinama, niliogopa sana kwa
vile sikuwa nikimjua pia alionekana wa kike, nikiwa
nimesimama miguu imesita kusogea mbele mtu
yule alianza kuinua uso wake hapo ndipo niliona
kitu ambacho kilinifanya nipige kelele....
 
SEHEMU YA 39
NA GAOO
SIMU 0654387935
TULIPOISHIA SEHEMU ILIYOPITA
nikiwa nimesimama miguu imesita kusogea mbele
mtu yule alianza kuinua uso wake hapo ndipo
niliona kitu ambacho kilinifanya nipige kelele....
SASA ENDELEAAAA
Nilipiga kelele baada yakuona sura ya mtu yule,
ilikuwa sura ya kutisha tena wakati huu ikiwa na
matobo tobo macho hayakuwepo yalikuwa matobo,
tena alifanana vyema na yule alienikimbiza ndotoni
na kumtaka mwanangu.
Kelele nilizopiga ndizo zilifanya mtu yule
anisogelee, hapo kwa woga nikaaita kwa
nguvu"Johniiiiii" "Johniiiiiii"
Nilistustwa na mtu alienishika nyuma.
"Mke wangu unanini?" ilikuwa ni sauti ya john
nilimkimbilia na kumkumbatia john wangu huku
nikitetemka nilishangaa eti kunbe nilikuwa pale pale
sikwenda popote kama nilivyokuwa nikiona.
"Tuondoke john tuondoke siwezi kukaa hapa
nipereke ndani nataka nikalale,"
"Kwani kuna nini mpenzi wangu si nimekambia
unisubiri hapa nikuletee mabuyu, sasa kimetokea
nini?"
"Tuondoke hapa John"nilikwambia kweli alinisikia
tukaondoka eneo lile nankurudi ndani moja kwa
moja kwenye hotel.
"Kwani umeona nini kidawa woga gani huo inamana
bado unaota ndoto za ajabu ajabu,?"
"Hapana john kule kunatisha mi nilikuwa naogopa,
na vile ulivyoniacha peke yangu ndio nikaogopa
zaidi," nilimdanganya john sikutaka ajue.
"Pole punguza woga, John wako nipo,"alisema
kisha kunikumbatia na mimi niiazidisha kudeka"
baada kukaa kwa saa kadhaa ndani pale usiku
ulipoishia john alisema tutoke tukale hivyo nilitoka
nae, akaagiza vyakula vya ufukweni yani samaki
samaki walioungwa, tulilishana huku akinitolea
miba.
Tulikula mpka pale nikiposikia shibe ndipo
nikipomwambia john tukanywa vinywaji kisha tulikaa
pale ufukweni tukipiga stori muda wote sikuwa na
amani woga ulinikaa vilivyo niliogopa, hatma ya
maisha yangu sikuwa nikijua kabisa nilijiaminisha
kuwa nimeipata furaha ambayo itanisahaulisha
mapito yote niliyopitia ila nahisi ndio mauza uza
yananianzia, tuliongea mengi nabJohn akijitahidi
kunipa faraja,tulikaa kwa muda mrefu woga bado
ulijuwa ukiniandama
"John nasinzia naomba tukalale mpenzi,"nilimwa
mbia nae hakunigomea alipenda kunisikiliza
nankunipa kipaumbele tukarudi mpka ndani, kiukweli
sikuwa hata na usingizi ila niliogopa tu kukaa pale
nje yanaweza kunitokea tena tulipoingia ndani na
kufunga mlango kidogo amani ilinirejea kiasi.
Tukavaliwa nguo za kulalia kisha wote tukapanda
kitandani baridi iliyokuwa kisiwani pale ndio ilafanya
tujifunike shuka tukiwa tumekumbatiana huku
vichwa vyetu vikiwa nje.
"Mume wangu we unapendekeza jina gani kwa
mtoto wetu?" Nilimuuliza akatulia kidogo kisha
akajibu.
"Si bado mpenzi wangu, ila akiwa wa kiume
nitafurahi akiitwa David na wakike akiitwa anna"
"Jamani hilo la David hapana kwa kweli,
wanakuwaga na tabia mbaya sana hao, ukimpa jina
hilo huoni kama tutamwaribu mtoto"
"Hapana sio kama Davidi wote wapo hivyo, ni
wachache tu,"
"Ni wengi tizama hata yule davidi wa kwenye kitabu
cha Naomi, david ambaye alibadilisha maisha ya
Naomi kisha kumfanyia ukatili,"
"Heeeh kumbe nawe ulisoma hiko kitabu haya
ulikisomea wapi kitabu hiko?"
"Ndio nilikisoma mtandaoni ila sikukimaliza"ni
limjibu baada yakuniuliza kuhusu kitabu cha
NAOMI.
"Lini na wakati simu nimekununulia juzi tu?"
"Hapana kipindi cha nyuma ndio nilikisoma kipindi
kile tunakutana kwa mara ya kwanza"
"Ahaa mi pia nikilikisoma kwenye simu,"
"Sasa umeona tabia za David alafu ndio tumpe
mtoto wetu."nilimwambia Tabia za davidi wa
kwenye kutabu cha Naomi nilichosoma kwenye
mtandao wa facebook zilikuwa sio nzuri sikuhadithii
sana ila jitahidi ukisome.
"Basi tumwite gao,"
"Weeeeeh si bora asiwe na jina kuliko tukimwita
hivyo,"nilishangaa eti mwanangu tumwite gao na
tabia zile hapana nisije lea wajukuu wasio na
mama.
"Bora aitwe christopher"nilipendekeza jina hilo
akalikubali hapo tukalala, usingizi wa usiku huu
ulikuwa mtamu sikuota chochote mpka kunakucha,
siku mpya ambayo asubuhi hiyo tulipata supu ya
pweza,kisha john kunipa taarifa kuwa tunarudi
nyumbani aliniambia nikajiandae.
Taarifa hiyo ilikuwa njema kwangu nikiifurahia
vilivyo mana nilishachoka kuishi kwa mashaka na
mawazo hapo kisiwani, baada ya kujiandaa
tukaianza safari tulibanda boti la watu karibia kumi
tulichanganyikana na wachina na waswahili wawili
pamoja na mzungu mmoja sisi wengine tulikuwa
kimya huku sauti za wachina ndio zilivyochukua
nafasi pale hatukuwaelewa wanachoongea wengine
tulikaa kimya mpka safari yetu ilipofika yard
bongoyo ndio tukashuka kisha John akikiendelea
pale alipoacha gari yake tukaianza safari ya kurudi
nyumbani njiani nilipasifia kinafki mbudya, niliamua
tu nipasifie huku nikijinadi kuwa nimefurahia kumbe
sio kweli, kwa mbudya ni pazuri ila mimi
sikufurahia sana kwa vile sikuwa na raha muda
wote.
Tulifika nyumbani baada ya kutoka yard bongoyo.
Tuliingia ndani nikiwa nimechoka zaidi mwili wangu
niliuona mzito sana.
"Naomba nikalale mume wangu, nimechoka sana,"
"Sawa mke wangu kalale upumzike ngoja na mimi
niweke sawa kazi zangu za ofisini," alisema hapo
nikaingia chumbani nilipoingia nae akanifata na
kuchukua laptop yake kisha akatoka hapo nikajilaza
kitandani usingizi ukanijaa.
Maisha yangu na John yali tawaliwa na furaha john
akinijali na kunipenda, minba yangu iliendelea kukua
hapo tayari nilianza clinic yale mauza uza
hayakunitokea tena hata ndoto za ajabu hazikunijia
tena.
Siku moja nikiwa nimekaa na john wangu
tunaangalia tivi ndipo maongezi yalipoanza baada ya
kimya cha muda mchache ndipo akavunja ukimya
hapo alikohoa kidogo kuweka koo lake sawa kisha
akaongea.
"Nadhani mke wangu unatakiwa upate msaidizi wa
kukusaidia kazi"
"Hapana mimi sitaki dada wa kazi kwangu,"
"Mke wangu anakusaidia kipindi hiki tu
ukishajifungua ataondoka,"john aliniradhimisha eti
aniletee dada wa kazi nilimkatalia ila alizidi
kunibembeleza ikanibidi nikubali kumridhisha john.
"Sawa asante kwa kunielewa nitaongea na rafiki
yangu mtu wa tabora anitafutie binti wa kazi kwao"
"Sawa asiwe mkubwa nataka msichana mdogo sio
uniletee mwanamke mkubwa," nilimpa masharti.
"Sawa mke wangu napenda kukufanyia vile
unavyopenda wewe" alisema wakati huo tukiwa
tumekaa tukiangalia taarifa ya habari baada ya kula,
muda ulisogea mpka kufika saa tatu na nusu baada
ya kumaliza kuangalia huba kwenye dstv ndio
tukaingia ndani kwa ajili ya kulala mpka kunakucha
john akaniamsha nikamuandalia chai akaoga kisha
nikamfunga vifungo vya shati lake pamoja na
kumfunga, nilipomaliza tukaelekea mezani huko
alikunywa chai haraka haraka ili awahi kazini.
Zilipita siku mbili kisha siku ya tatu mchana ndipo
John alinipigia simu akiniambia dada wa kazi
amepatikana hivyo atakuja nae baadae.
Nilimwitika kisha nikaendelea na kazi zangu mpka
pale ilipofika jioni ndipo John alipokuja na
msichana msichana ambaye nikihisi namjua ila
kumbu kumbu zangu zilikuwa haziji kama
ninavyotaka.
Alitambulishwa kwangu na John akisema anaitwa
somoe, ameacha shule baada ya kumaliza darasa la
saba hivyo wazazi wake hawakuwa na uwezo wa
kumuendeleza, Japo sikuwa nikijua sana ila majina
ya somoe sidhani kama ni watu tabora kama john
alivyonambia kuwa msichana atatokea tabora, aah
sikujali sana nikaamua nifunike tu kombe
mwanaharanu apite, tulimuonesha chunba chake
cha kulala..
Somoe ndani ya nyumba je somoe ni nani? Unamjua
somoe?
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom