bioto
JF-Expert Member
- Oct 1, 2017
- 1,261
- 2,099
KIDAWA (sijivunii Uchawi)
Kipande cha 1
Na Gaooh
Simu=0654387935
Nawakaribisha wote kwa pamoja kusoma simulizi
hii ya kuvutia.
Katika makuzi yangu sikuwahi kumuona baba wala
mama, sura pekee niliyowahi kuiona pindi tu napata
fahamu za kitoto alikuwa ni bibi, tangu niweze
kuongea na kujielewa sikuona ndugu yoyote
nyumbani kwetu zaidi ya majirani tu ambao nao
walitutenga hakuna alieshirikiana nasi, japo nilifanya
juhudi kadhaa ikiwemo kukataa kula na hata
kutishia kutoroka ili tu bibi anieleze walipo wazazi
wangu lakini haikuwa rahisi wala haikuwezekana
kama nilivyotaka, naweza sema bibi ndio alikuwa
baba, mama, na hata familia nzima, Kidawa ndio
jina langu nina umri wa miaka kumi na tisa sasa
(19) nimeishi nikimtumikia bibi yangu katika kazi
zake, nilijua fika bibi yangu ni mchawi kweli ni
mchawi mara kadhaa alikuwa akiondoka usiku na
kuniacha peke yangu kitandani,na hata sikunyengine
kuondoka na mimi, nilishakula nyama nyingi sana
usiku alikuwa akileta nyama na kunilazimisha nile
zilikuwa mbichi alinilisha kwa lazima kisha nikila
ndio inakuwa furaha yake, vitendo vile vilinifanya
nizoee kiasi kwamba bibi akitoka na asiporudi na
nyama mbichi huwa namlilia,mazoea yalijenga tabia.
Usiku mmoja nikiwa nyumbani,niliandaa chakula
ulikuwa ni ugali na nyama sikujua ni nyama ya nini
bibi alireta na kunitaka niipike huku akisema kuna
wageni wake watakuja usiku huo, nilitii na kuanza
kupika saa kadhaa bibi aliingia, alikuwa peke yake
tofauti na nilivyodhania nitegemea angekuja na
wageni.
“Bibi, umerudi!” niliuliza.
“Ndio vip, chakula tayari?” nae aliuliza, hakuitika.
“ndio tayari bibi wageni wako, wako wapi?”
“Mbona wako hapa, we andaa chakula uweke
mezani ugeni wa leo ni mkubwa si kila binadamu
anaruhuskuwaona we bado mdogo kidawa ukikuwa
utawaona!”
“Hmmmm!” niliguna mana yalikuwa mapya sikutaka
kuingilia mambo ya watu niliandaa chakula kama
bibi alyoagiza na kuweka mezani sambamba na
maji ya kunawa, kisha nikaingia chumbani
kujipumzisha.
Mbali na kuwa na miaka zaidi ya kumi na tano ila
sikuwahi kwenda shule bibi hakutaka niende shule
jibpekee alilonipa ni kuwa “shule nitaenda
kufundishwa ujinga tu” hali ile ilinisumbua kipindi
cha utoto wangu nikiwaona wenzangu wakienda
shule huku wamevalia sale zao, walipendeza
kuwaangalia nilikuwa nikitamani ningekuwa mimi
sikuwa na bahati hiyo ila kwa sasa nishakuwa
mdada sitamani tena shule, nikiwa nimejilaza juu ya
kitanda cha kamba nilisiiki sauti ambayo nilitambua
fika ni ya bibi.
“Kidawa…kidawa..” niliamka kutoka kitandani na
kwenda nilipoitwa.
“Abee, Bibi”
“Ulikuwa umelala… kwani umeshakula!”
“Hapana, Bado ila sihisi njaa!”
“Kipi kimefanya usihisi njaa,”
“Hakuna chochote Bibi!”nilijibu huku nikijinyoosha.
“Leo kuna kazi tunatakiwa tukafanye pamoja ,”
“kazi?””Ndio mbona unashangaa kwani we ni mgeni
na kazi zangu!”
“hapana bibi,”
“sawa tunatakiwa tutoke sasa,” bibi alisema, hapo
yeye alikuwa kashavalia kaniki yake nyeusi,
alinivalisha na mimi kaniki nyengine, kisha alisema
tutoke nje tulitoka hapo nilishangaa kuona nyoka
mkubwa akiwa pale nje tena akiwa na mabawa,
japo tulishawahi kusafiri mara kadhaa kwa kutumia
usafiri wa aina mbali mbali ikiwemo ungo hata
farasi leo nilishangaa nilipandishwa kwenye nyoka
mwenye mabawa, sikulijali sana jambo hilo tulikwea
kisha safari ilianza, ilituchukua muda mchache
nyoka yule alitua kwenye moja ya jengo kubwa
ambalo tulitizamana nalo japo sikwenda shule ila
kusema maneno ya kiswahili niliweza, nilisema
jengo lile na kugundua palikuwa ni muhimbili,
sikuwahi waza ipo siku nitafika hapo, leo imekuwa
kama maajabu, bibi alinielekeza cha kufanya
aliniambia niking’ate kidole changu cha mwisho cha
mkono wa kushoto nami nilitii hapo nilishangaa
kuona umbo langu limebadilika sikuwa binadamu
tena nilikuwa paka bibi nae alibadilika na kuwa
pake mweusi mwenye madoa meupe shingo
aliniambia nimfate nami nilitii tukaingia wodini, mlizi
hakuwa macho wakati huo alikuwa amelala, hivyo
ikawa rahisi kupita muda wote nilikuwa
nikitetemeka juu ya muonekano wangu
ule,tuliongozana mpaka wodi ya wazazi tukaingia.
“Chagua wakike wawili!” bibi aliagiza, na mimi
nilikubali, nilikuwa nikifata maagizo ya bibi bila
kupinga nahisi haikuwa akili yangu kila alichosema
nilifanya nakumbuka siku ile tulibeba vichanga
vitano mimi nilibeba wawili yeye akachukua watatu
ambao wote tuliwachanganya ndani ya ungo kisha
kupakia kwenye nyoka tuliekuja nae na kuondoka
eneo lile, safari yetu ilitufikisha kwenye uwanja
mkubwa ambao ulikuwa kati kati ya msitu, uwanja
huo ulimea viginga vya moto sambamba na kelele
za hapa za hapa na pale wasichana waliimba na
kucheza huku wengine wakipiga ngoma wote
walikuwa wanazunguka.
“BIBi kuna nini hapa,”niliuliza.
“Tupo kwenye ibada ya kuchagua kiongozi mpya,
kiongozi wet wa zamani muda wake umeisha, leo
ndio analiwa nyama kisha nafasi yake anachukua
mtu mwengine,” bibi alinifafanulia tukio lile,
vichanga vile bibi alivipereka pale mbele kati kati ya
mduara ule aliniambia kuwa ni sadaka hivyo ni amri
wanapewa kila mmoja kuleta, wakati bibi
amepereka sadaka yake nilibaki mwenyewe
nimesimama hakuna mtu niliye mjua eneo lile
walikuwa wamama na vijana wengine walitisha jinsi
wanavyoonekana kila mmoja alikuwa yuko makini na
shughuli yake, bibi hakuwahi kurudi alicherewa
jambo hilo lilifanya usingizi uanze kunichukua
nilisinzia pale nilipokuwa nimekaa baada ya
kusimama kwa muda mrefu nilikaa mwishoni
nikaanza kusinzia, sikujua kilichoendelea eneo lile
mwishoe nilistuka nikajikuta nipo nyumbani tena juu
ya kitanda, “Bibi biibiii<” baada ya kuamka niliita
jina la bibi lakini sikuitikiwa nikahisi labda ameenda
kwenye kuni, lakini nilikumbuka kuni tayari nilikuwa
nimeleta za kutosha. “ Atakuwa ameenda wapi
mbona hakuniaga na hapa nyumbani je nimefikaje?”
nilijiuliza sikupata jibu, nilionelea ni bora niamke
kitandani nilipokuwa nimelala, niliamka na kutoka
nje kulikuwa tulivu eneo lote ni miti tu na sauti za
ndege ndio nilizisikia, nyumba yetu haikuwa karibu
na makazi wanayoishi watu wengine tulikuwa
tukikaa mbali kidogo, bibi aliwahi kunieleza kuwa
wanakijiji walimtimua baada ya kutaka kuchoma
nyumba yake ndio akaondoka na kukaa mbali
nao,sikuwa nikijua alipobibi japo nilipata fikra za
kuwa ni mtu mzima kama katoka atarudi nyumbani
mwenyewe, nilisubiri nikasubiri lakini hakurudi siku
hiyo.
Siku zilipita sikumuona bibi tena nikabaki kama
yatima sikuwa na ndugu wala rafiki upweke
uliniandama kuishi mwenyewe porini, niliamua
kuhama kule nilipokuwa naishi na bibi kisha nikarudi
sehemu ambayo wanaishi watu wengine, sikuwa na
mwenyeji pia hakuna aliekuwa akinijua, baada ya
mwendo wa hatua kadhaa nilifika kwenye moja ya
shamba ambalo lipo kando kando ya mto nilifika
pale kwa ajili ya kunywa maji, sikuwa nikijua
niendako nitafikia kwa na nani, baada ya kunywa
maji njaa nayo haikuacha kuonesha uwepo wake
nikajikalia chini ya mparachichi ambao haukuwa na
dalili ya kutoa matunda, nikiwa pale mawazo
yakiniandama kuwa wapi nitapata chakula kuistili
njaa nilikuwa nayo wakati huo ndipo alitokea
mwanamke akiwa amebeba jembe kichwani,
alionekana akitokea shamba, nilimsalimu baada ya
yeye kusimama akinisikiliza alikuwa ni mama wa
makamo nilimweleza kuwa nimepotea sijui nitokapo
wala niendapo, mama wawatu hakuwa na makuu
aliniambia kuwa niongozane nae nami nikatii hapo
nikampokea jembe alilobeba, tulifa mpaka
nyumbani aishimo, hakuwa na mume zaidi ya kuwa
na mtoto mmoja wa miaka tisa anaesoma darasa la
tatu.
“Naishi na mwanangu hapa anaitwa subira anasoma
darasa la tatu!”
Itaendelea.
Baada ya kitambo kirefu kutokana na changamoto
kadhaa sasa tumeamua kurejesha burudani kwenu
uongozi mzima wa Tungo Murua Za Kusisimua
Tungo Murua Za Kusisimua
Tunaomba ushirikiano wenu kama zamani.
like kisha share kwa wingi ili iwafikie watu wengi
pia unaweza kutag marafiki zako wapenzi wa tungo
za kusisimua
pia usisahau kuweka maoni yako tutayasoma.