Simulizi ya kijasusi - Nilimdhania kahaba kumbe bikra

NILIMDHANIA KAHABA KUMBE BIKRA

MTUNZI: SINGANOJR

Mono no aware.

SEHEMU YA 652.
Rufi licha ya kwamba alijuwa uwepo wa Xiao Xiao ndani ya jiji la Dar lakini bado hakuamini kama angeweza kukutana nae katika eneo kama hilo la Kawe Beach.
Upande wa Xiao Xiao ukweli ni kwamba haikuwa mara ya kwanza kumuona Rufi, mara ya kwanza alivyomuona hakuamini kama anaweza kuwa Rufi lakini siku hio mara baada ya kumuona kwa mara nyingine hakutaka kudharau hisia zake na aliweza kuthibitisha ni yeye kweli.
Ilimshangaza kumuona Rufi nchini Tanzania mara baada ya miaka mingi ya kutoroka kutoka katika ulimwengu wa kijini.
Rufi licha ya kukamatika hakutaka kabisa kuongea na Xiao na palepale alikimbia kurudi ndani ya mgahawa na Xiao Xiao na yeye alimkimbilia kumfuata.
Roma mara baada ya kumuona msichana huyo wa kichina alikumbuka alivyokutaka nae mara ya mwisho mpaka kuja maeneo hayo hayo na kuachana .
Alikumbuka namna mrembo huyo alivyokuwa akimsumbua kwa kumtumia jumbe za meseji za kumtaka kimapenzi ambazo alidharau na kutomjibu mpaka akajikatia tamaa.
“Nini kinaendelea , kwanini Rufi anakimbiiana na yule mdada?”Aliuliza Amina ambaye alikuwa kwenye mshangao kama Roma .
Muda huo huo kabla Roma hajajibu Rufi alishawafikia na Roma alisimama mbele ya Rufi akimkinga na Xiao Xiao.
Mrembo yule wa kichina mara baada ya kumuona Roma alijikuta akijawa na mshangao kwani ni kama hakutegemea kumuona katika maeneo hayo.
“Hata wewe pia upo hapa , aisee kweli kilichopangwa hakikwepeki nadhani imepangwa tuoanane kwa mara nyingine”Aliongea Xiao Xiao akimwangalia Roma kwa furaha.
“Ndio nipo hapa pia , lakini kwanini unamfukuza Rufi?”
“Rufi!!?Oh.. nafahamiana nae ni shemeji yangu kwa kaka yangu”
“Huyo kaka yako ndio anaefahamika kwa jina la Xiao Hang?”Aliuliza Roma na kumfanya Xiao kutoa macho.
“Umejuaje jina la kaka yangu , au Rufi kakuambia kila kitu?”Aliuliza huku akiwa na mshangao , ingekuwa ngumu kwa Roma kujua jina la kaka yake kwani alikuwa akiishi huko katika jamii ya majini.
Roma hakujibu swali lake na palepale alimshika mkono yule mchina na kisha alianza kumvuta kumtoa nje ya mgahawa huo na ndani ya dakika chache tu walionekana wakiingia upande wa kushoto kwenye vyoo na mabafu ya kubadilishia nguo kwa watu wanaoenda kuogelea.
Amina yeye alikuwa kwenye mshangao kuona Roma amempeleka yule mchina kwenye mabafu .
Upande wa Lanlan hakushangaa kile kilichokuwa kikiendelea na alisimama na kwenda kuchukua kifurushi cha mishikaki na kurudi juu ya meza na kuendelea kula.
Upande wa yule mchina Xiao Xiao hakuelewa Roma anataka kumfanya nini na namna ambavyo alimshika mkono hakuwahi kufanyiwa hivyo na mwanaume na alijikuta mapigo yake ya moyo yakienda spidi spidi.
Pengine alijua labda Roma kadhamiria kwenda kufanya nae bafuni ndio maana anamwingiza huko.
Alikuwa mwekundu kama yai la kisasa kutokana na uzungu wake na aliishia kujiuliza ni kipi ambacho anapaswa kufanya ,ijapokuwa alikuwa akitamani kuonana na Roma kwa mara nyingine na kufanya nae mapenzi ili kuweza kumtumia kupanda levo lakini katika hali kama hio ya kushitukiza alijiona ni kama hakuwa tayari.
Upande wa wanaume ambao walikuwa kwenye mgahawa huo waliishia kumwangalia Roma kwa mshangao na wivu , ukweli ni kama walimdhania Roma na mchina huyo ni wapenzi kwani Xiao Xiao hakuleta ukinzani wakati wa kuvutwa na Roma mpaka kuingiziwa ndani ya mabafu.
Roma hakujali sana macho ya wengi yaliokuwa yakimwangalia , kwani mara baada ya kumfikisha Rufi kwenye bafu ambalo hutumiwa na wanaume aliwapa ishara vijana wadogo waliokuwa wakibadilisha mavazi kuondoka na walifanya hivyo haraka haraka na kisha wakakimbilia nje lakini mmoja wapo ambaye alikuwa mkubwa kidogo aligoma.
“Wewe kama nani mpaka kutuamrisha tuondoke?”Aliongea
Roma alikuwa na hasira na palepale alipiga ngumi ukuta kiasi cha kutengeneza ufa na jambo lile lilimuongopesha yule wmanaume na palepale alikimbia kuelekea nje akiwa kwenye mshangao.
Upande wa Xiao Xiao alikuwa akimwangalia Roma na macho ya aibu , huku akishindwa kuzuia kulegea kutokana na macho yake pamoja na uso ambao ulikuwa umetakata na kumfanya kumuona mtanashati.
Yeah Roma alikuwa amebadilika uso sana tofauti na mwanzo ambapo alikuwa mbeba mizigo , kipindi hicho alionekana kuwa Handsome sana , pengine ni kutokana na kupanda levo, kilichokuwa kikimpunguzia pointi ni aina ya uvaaji wake tu.
Roma alimshika na kumsukumia Xiao kwenye chumba kilichokuwa pembeni kushoto kwake na kisha akafunga mlango na palepale alikwenda kumkandamiza ukutani huku akimwangalia usoni kwa macho yasiokuwa yakielezeka.
Xiao alikwepesha macho kwa aibu huku akiwa na msisimko wa aina yake na alikuwa akisubiria kwa hamu hatua ya pili ambayo Roma anakwenda kufanya.
Ijapokuwa Roma alionekana kuwa siriasi hali ile ya ki uwanaume ilimfanya kuvutiwa zaidi na aliona kitakacho fanyika hapo ni yale mapenzi ya vurugu na hio ndio ilikuwa ‘Fantasy’ yake.
“Kufanyia hapa sio vizuri , kama vipi tufanye haraka haraka tuondoke…”Aliongea huku akionyesha hali ya aibu za kike na kumfanya kuzidi kupendeza..
Wanawake wa rangi nyeupe ni tofauti kidogo na wanawake wa kiafrika hususani katika swala la mahusiano , ni wawazi sana likija swala la mahusiano na anaweza akaruhusu ngono kufanyika hata na mtu ambaye hamjui vizuri.
Upande wa Roma mawazo yake yalikuwa mengine kabisa muda huo alikuwa akijiuliza ni kipi anapaswa kumfanyia , aliogopa kwamba kama ataenda kusema huko kwenye ulimwengu wao kama Rufi yupo Tanzania basi ingekuwa tatizo.
Roma hakutaka matatizo kwa wakati huo kwani nguvu zake za kijini hakuwa na uwezo wa kuzitumia kwa wakati huo na asingeweza kumlinda Rufi kama atakamatwa.
Mbaya zaidi kama itajulikana alikuwa na mahusiano na Rufi ndio ingekuwa tiketi ya majini hayo kuja kumvamia na kutaka kumuua maana alijua tabia yao namna moja ni kutopenda kudharaulika.
“Unataka nifumbe macho kwanza kabla hujaanza kunikiss… najihisi sipo tayari lakini unaonekana una hamu, hivyo sijali kama unataka tufanye , isitoshe nilikuwa nikikufikiria sana”Aliongea Xiao huku akiona pengine Roma alikuwa akiona aibu ndio maana alikuwa akimwangalia tu bila kuchukua hatua yoyote.
Xiao Xiao alikuwa ni mzuri haswa wa sura ijapokuwa alikuwa na rangi ya kichina lakini macho yake yalikuwa tofauti kidogo na wachina wa kawaida , kitu pekee ambacho hakuwa nacho ni umbo tu.
Roma alijiwazia alikuwa ameua watu wengi ambao pengine kati yao hawakuwa na hatia hivyo kujiongezea dhambi kwa kuua na mwanamke mrembo kama Xiao lisingekuwa tatizo.
Alijiambia kama mwanamke huyo ataendelea kuwepo hai basi siri ya uwepo wa Rufi nchini Tanzani itafichuka na ili kuficha siri hio kwa wakati huo hatua ya kwanza ni kumuua.
Baada ya kuwaza kwa muda palepale akili yake ilifanya maamuzi na shetani mtoa roho alimvaa na sura yake iligeuka na kuwa ile ya kikatili na palepale alipeleka mkono kwenye shingo yake.
Xiao alijua Roma alikuwa akitaka kuinua kidevu chake , hio pia ni moja wapo ya staili ambayo alipenda kufanyiwa na mwanaume , kunyanyuliwa kidevu na kuangaliwa usoni na mwanaume mwenye uchu kabla ya kubusiwa.
“Xiao Xiao kama utakuwa na kinyongo na mimi kwa kukuua leo hii basi naomba ukiwa kuzimu roho yako initafute na ulipize kisasi, hili halina uhusiano wowote na Rufi hivyo usije kumchukia”Aliongea Roma.
“Unamaanisha nini?”Xiao Xioa alijikuta akiwa katika mshangao huku akichanua macho yake lakini palepale aliweza kugndua kwamba Roma hakuwa akipanga kufanya nae mapenzi bafuni.
Roma hakutaka kuchelewesha muda na palepale alimshikilia shingo kwa nguvu kumkaba na Xiao Xiao alijihisi kuanza kukosa pumzi.
“No .. usinifanyie hivi..”Aliongea lakini Roma kabla hajakaza mkono mlango palepale mlango ulisukumwa kwa nguvu na aliingia Rufi ambaye alionekana kuhema kwa nguvu.
“Hubby usifanye hivyo , tafadhari naomba umuache ,, huyo sio tishio kwetu”Aliongea Rufi kwa kubembeleza.
Wakari Rufi na Amina wakimuona Roma akimwingiza Xiao kwenye bafu palepale waliangaliana na kisha wakapeana ishara ya kwenda kuchungulia nini kinafanyika.
Baada ya kusikia Roma alikuwa akipanga kumuua Xiao Xiao palepale alisukuma mlango kumuokoa.
Xiao Xiao mara baada ya kujua Roma alikuwa akitaka kumuua na sio kufanya nae mapenzi machozi yalianza kumtoka palepale.
“Uli.. ulikuwa ukitaka kuniua?”Aliuliza huku akionyesha mshangao na uso wake wa kirembo ulibadilika na kuwa mwekundu , pengine angekuwa na nguvu za kijini katika levo ya nafsi basi moja kwa moja angekuwa ashampiga Roma.
“Rufi huyu anatokea katika ulimwengu wa kijini , ukoo uliolazimishwa kuolewa nao , kama ataenda kutoa taarifa ..”
“Najua ...”Rufi alijikuta akimeza mate huku akionyesha huruma.
“Najua ni hatari lakiki sitaki kukuona ukimuua mtu ambaye hana hatia .. pengine hujui hili lakini wakati nilipochumbiwa kwenye ukoo wao walinidharau sana na kuniona kama kiumbe cha ajabu lakini ni Xiao Xiao pekee ambaye hakuoneysha kunidharau, sio mtu mbaya na hawezi kufanya kitu ambacho kitaniathiri”
Roma alimwangalia Rufi na kuona anapaswa kutii kile anachomwambia kwani asingefanya hivyo angeziumiza hisia zake.
“Okey fine”Aliongea Roma na kisha akamwachia Xiao Xio
Xiao Xiao alijikuta akichuchumaa na kuanza kulia kilio cha kwikwi huku akiwaangalia wote na kuangalia mkono wake ambao ushavimba kutokana na kushikiliwa kwa nguvu.
“Umenikatali sana , mimi sio kama baba yangu wala kaka yangu , kama yeye mwenyewe hataki kurudi kwanini aende , kwanini umeshindwa kuongea na mimi vizuri tu”Aliongea na kisha palepale akasimama.
“Kama hunipendi si ungesema tu kwamba hunipendi , kwanini ya kutaka kuniua , nilipatwa na furaha baada ya kukuona kwa mara nyingine kutokana na kukuwazia muda wote tokea mara ya mwisho tuonane kwanini unapenda kucheza na hisia zangu hiv, nakuchukia sana , sitaki kukuona tena kwenye maisha yangu”Aliongea awamu hio kwa Kichina kabisa na kisha alitoka nje kwa kukimbia huku akitoa machozi .
“Hubby asante kwa kunisikiliza”Aliongea Rufi akivuta pumzi ya ahueni.
“Natumaini maamuzi yako ni sahihi na hakuna kibaya ambacho kitatokea”Aliongea Roma.
“Kama mambo yatabadilika nitaondoka kuelekea Mediyerranian kuishi na Sister Rose , nadhani hawawezi kuvuka mpaka kuja mpaka kule”Aliongea
“Rufi unarahisisha mambo , kama watataka wanaweza kwenda mahali popoate hata kama ni kwa kupigana na miungu hawatojali , mwili wako ni hazina kubwa kwao kukupoteza kirahisi , isitoshe majiini ni viumbe ambavyo havipendi kushindwa kirahisi”Aliongea Roma na kumfanya Rufi kutoa machozi.
“Jamani tumekuja hapa kwa ajili ya kumsindikiza Lanlan kucheza hebu tuachane na hayo kwasasa , Nasra ,Dorisi na Lanlan wanatusubiria”Aliongea Amina kwa kingereza huku akitangulia.
“Hubby nimefurahi , tulijua ulitaka kufanya nae kwasababu alikuwa mrembo lakini kumbe ulitaka kumuua kwa ajili yangu , namuoea huruma Xiao Xiao lakini nimefurahi kuona unanijali , Thanks a lot love”Aliongea.
“Nyie warembo siku moja mtaniua”Aliongea Roma huku akimfinya mashavu huku akitoa tabasamu.
Baada ya chakula Lanlan alienelea kucheza michezo akiungana na Nasra na Dorisi na walijikuta wakifurahi sana siku hio.
Ilifikia hatua mpaka Nasra akajiuliza imekuwaje Edna akamuacha mtoto mzuri kama Lanlan kwani uwepo wake tu ulikuwa ukileta furaha.
Roma wakati huo hakuacha kumkumbuka Edna na alijiaribu kupiga simu nyumbani kumuulizia Edna kama amerudi lakini Bi Wema alimwambia bado hajarejea.
“Pengine atarudi jumatatu kwani ndio siku ambayo inatarajiwa kuwa na kikao cha kutangaza mabadiliko ya kampuni ya Vexto”Aliongea Nasra mara baada ya kumuona Roma amekuwa mnyonge.
“Mimi sitaki hata kujisumbua na maswala yake mengine , ninachotaka ni kuongea nae na kuweka mambo sawa tu basi , nimefikiria sana katika hizi siku na nimegundua kuna kitu alikuwa akinificha”Aliongea Roma na Nasra alimshika begani kumtuliza huku akimwangalia kwa kumuonea huruma.
Muda wa jioni wote walirudi nyumbani kwao wakimuacha Amina anapoishi na Roma alichukuana na Lanlan kueleka nyumbani kwa Nasra
Wakati wanaingia getini walishangazwa na uwepo wa magari matatu ambayo hawakuwa wakiyajua, mawili yalikuwa ni Aud rangi nyeusi na moja wapo ilikuwa ni gari aina ya Maserati ya rangi nyekundu.
“Ineonekana tuna ugeni hapa”Aliongea Rom.
“Naona hivyo pia”Alijibu Nasra aliemshika Lanlan mkono.
“Nasra wewe ondoka na Lanlan moja kwa moja kwenda juu akapumzike mimi nitaonana nao”Aliongea Roma na Nasra alitingisha kichwa kumwelewa na kisha alitumia mlango wa nyuma wakati Roma akielekea eneo la seubuleni.
Mtu pekee amaye aliachwa nyumbani alikuwa ni Qiang na mara baada ya kuingia ndani Roma aliweza kumuona mwanadada huyo ambavyo amekosa utulivu kwani alikuwa akizunguka zunguka huko na huko , lakini alijikuta akipatwa na ahueni mara baada ya kumuona Roma.

SEHEMU YA 653.
Roma mara baada ya kuingia ndani aliweza kuona sura anazozifahamu , mmoja wapo alikuwa ni Afande Jamali na mwingine alikuwa ni mwanamke kutoka familia ya Sharif.
Alikuwa amevalia suti nyeusi na viatu rangi nyekundu aina ya skuna, nywele zake alikuwa amezifunga kurudi nyuma na kumfanya kuwana mwoneknao wa kujiamini pamoja na wa kuvutia kwa wakati mmoja.
Alikuwa ni mwanadada mrembo Maimuna Sharif ambaye alionekana kama vile ni ofisa kutoka benki kwa muonekano wake kiasi ambacho kama wewe ni mwanaume wa kawaida ingekufanya kukosa hali ya kujiamini mbele yake.
Afande Jamali mara baada ya kumuona Roma palepale alisimama kwa heshima.
“Mr Roma naomba unipe ruhusa yako kukutambulisha , huyu ni Miss Maimuna Sharif Mkurugenzi mtendaji wa kampuni ya Bale Group na mtoto wa kwanza kutoka kwa mzee Hafidh Sharif”Aliongea Jamali.
“Tunakutana tena Mr Roma”Aliongea Maimuma huku akionyesha tabasamu na kunyoosha mkono wake kumpatia Roma.
Roma aijiuliza mwanamke huyu anafanya nini , alikuwa akikumbuka alimuona siku ya jana yake mkoani Kilimanjaro , lakini licha ya kutoelewa nia ya ujio wake hakuwa akimuogopa hivyo alinyoosha mkono wake kumsalimia.
Roma mara baada ya kugusana na mkono wa mrembo huyo alijikuta akijiambia alikuwa na mkono mlaini mno ijapokuwa haikuwa mlaini kama wa Rufi lakini bado ulikuwa mlaini wa kumpagawisha mwanaume yoyote rijali.
Roma kwa kumwangalia ru Maimuna alijua kabisa sio mwanamke wa kawaida , ilionekana kabisa alikuwa na mafunzo ya kimapigano na alijiambia hakika alikuwa akijua kujijali.
Moja ya mbinu ya kupima kama mtu ana mafunzo ya kimapigano ni kupitia pumzi yake, watu ambao wana mafunzo ya kimapigano hususani ya Kung fu mara nyingi upumuaji wao ni wa tofauti na watu kawaida wanapumua kama vile wanahesamu pumzi inayvoingia na kutoka, kitu kingine pia katika utembeaji wao au pale wanapokuwa wamesimama hii huwatofautisha sana.
Kwa mfano wakati wa kutembea ni kama vile kuna mstari anaofuatisha kwani hatua zake hazipindishiki huku mikono yake yote ikiwa usawa wa mwili , mtu wa kawaida tembea yake inateneza mstari wa Zigzag huku vidole vya miguu yake vinatengeneza angle
Sasa sifa hizo zote alikuwa nazo huyu mwanadada Maimuna ambaye alikuwa mbele ya Roma na kujikuta akimwangalia kwa macho yasiokuwa ya kawaida na kujiambia alikuwa na urembo wa mwili na ngozi yake ni laini mno , pia ni mkurugezi wa kampuni ya Bale lakini pia wakati huo huo alikuwa na mafunzo ya mapigano.
Ilikuwa ngumu sana kumkutana mwanamke mwenye mafunzo ya mapigano kuwa na ngozi laini hususani ya mikono.
Wakati wakiwa wameshikana mkono Roma alijikuta akihisi mtekenyo kwenye kiganja chake na palepale aligundua Maimuna alikuwa amemtekenya kwa kutumia ukucha wa kidole cha mwisho.
Jambo lile lilimshangaza na kumfanya Roma ajulize mwanamke huyo anafanya nini , au yupo hapo kwa ajili ya kumtega.
Baada ya kuachiana wote watatu waliweza kuketi chini huku Qiang akiandaa juisi.
“Afande Jamali nadhani hujamleta hapa kwa ajili ya kunisalimia tu”Aliongea Roma akitaka maongezi yaende moja kwa moja katika topiki ambayo imewalata.
“Ndio Mr Roma , sitozunguka zunguka , nipo hapa kama mwakilishi wa wizara ya ulinzi?”Aliongea.
“Mzee Hashim Tozo ndio kakuagiza?”Aliogea Roma akimaanisha waziri wa ulinzi ambaye alikuwa ni ndugu yake Afande Tozo, Roma alishawahi kukutana nae mara kadhaa nyumbani kwa Afande Kweka na alikuwa amezoeana nae japo sio sana,
“Ndio Mr Roma , nipo hapa kufikisha ujumbe kutoka serikalini , serikali ya Tanzania inaheshimu familia yako pamoja na familia ya Mzee Sharif kwani mchango wenu kwa taifa ni mkubwa , Mstaafu jenerali ametoa taarifa yake kwamba familia yake haihusiki na swala lolote lililotokea siku ya jana na kusema unapaswa kuwajibika kwa kila kitu binafsi, hivyo ndio maana tupo hapa kwa ajili ya maongezi”Aliongea.
“Nenda moja kwa moja kwenye pointi”
“Ngoja niseme mimi… Mr Roma nipo hapa kwa ajili ya kutafuta haki ya familia yangu”Aliongea Maimuna
“Haki ya familia yako?”
“Ndio , nimekuja hapa kwa ajili ya kukutaka urudishe hazina yetu , kisha ujenge upya jengo la ibada na baada ya hapo usujudie roho za miungu wetu mara nne”Aliongea Maimuna huku akiwa na uso wenye urafiki.
“Kwanza nikueleze kwamba hio hazina sijui nini maana mimi sina , pili mmefikiria nini kudhania kwamba ninaweza kwenda kusujudia miungu yenu ilihali mimi ndio niliochoma moto jengo lenu la ibada”
“Mr Roma watu waliokukosea ni Salihi naibu waziri wa elimu pamoja na Asha na kama ni kisasi ulitakiwa kuwalipiza wao , kwanini ukahusisha familia nzima katika kisasi chako kwa kuchoma jengo letu la ibada pamoja na kuiba hazina yetu huku ukiharibu makazi yetu , mpaka kuja kwangu hapa ni kwamba familia yetu imekaa chini na viongozi wa kiserikali na kukubali jambo hili kuisha kwa amani na kusahaulika kama utatii matakwa yetu , urudishe hazina yetu na kisha usujudie miungu yetu kuiomba msamaha”
“Kama hiki ndio ambacho kimewaleta mnaweza kuondoka”aliongea Roma akisimama na kisha kunyoosha kidole kuelekea mlango wa kutokea nje.
Maimuna wala hakuonyesha kuathirika , yaani alikuwa akiongea kirahisi mno na palepale alisimama na kisha akamsogelea Roma karibu zaidi kimadaha na kufanya marashi yake makali ya bei ghali kuathiri pua za Roma.
“Mr Roma , siku ya jumatatu jioni nimeandaa sherehe ndani ya hoteli ya Wache Kigamboni, wageni wangu ni wabia wa kibiashara ambao wanashirikiana kwa ukaribu zaidi na kampuni yetu ya Bale Group , unaonaje ukishiriki na wewe?”Aliongea huku akiwa na tabasamu la kiuchokozi.
“Kwanini nihudhurie?”
“Kwasababu nitakupa sababu ambayo itakufanya ushindwe kukataa kuhudhuria , nina uhakika utaweza kukubaliana na matakwa yetu baada ya hio hafla”
“Vipi kama nisipo hudhuria?”Aliuliza Roma na kumfanya Maimuna kutingisha mabega.
“Nina uhakika mwanaume jasiri kama wewe hutopenda kuonekana Muoga mbele ya familia ya Sharif .. Besides I’ m just a frail woman .. alright that is settled, nitakuja kukuchukua mwenyewe hio siku”Aliongea huku akimkonyeza na kisha alimpita kimadaha na kuelekea nje huku akitingisha makalio yake ya wastani kwa fujo kama zote.
Roma aliishia kushika kiuno na kujiambia hakika ameweza kuamsha shauku yake.
“Vipi mmeshawazuia kutumia njia ya fujo katika kulipiza kisasi?”Aliuliza Roma akimwangalia afande Jamali.
“Hata mimi mwenyewe sijui na nafuata tu maagizo ninayopewa na wakuu wangu , lakini nakushauri Mr Roma hii familia haiwezi kuliacha hili lipite hivi hivi kuna nguvu kubwa ambayo ipo nyuma yao , lakini inaonekana hawataki kufanya fujo kudai haki yao , unapaswa kufikiria mara mbili ili kulimaliza kimya kimya”Aliongea Afande Jamali
“Babu alisema kwasababu mimi ndio msababishaji nitawajibika mwenyewe na hakuna mtu wangu wa karibu ambaye ataguswa “
“Inaonekana kuwa hivyo , isitoshe wanawake wako wote sio raia wa kawaida , serikali haitaki hili swala kuingiliana usalama wa raia … maagizo yashatoka kama famili ya Sharif itafanya jambo lolote la kutaka kudhuru familia yako basi tutaingilia”Aliongea Jamali.
“Nimefarijika kusikia hivyo , isitoshe adui yao ni mimi hivyo nipo tayari kuona nini wananniandalia, ninashauku ya kutaka kujua mchezo wao utazaa nini”Aliongea Roma na kumfanya Afande Jamali kushindwa kumuelewa Roma kabisa kwani alionyesha kutokuwa na hofu kabisa.
Baada ya wageni kuondoka na walinzi wao, Roma alikaa hapo sebuleni kwa muda mpaka Nasra aliposhuka na kukaa pembeni yake.
“Hii familia ya Sharif ina nguvu sana?”Aliuliza Nasra.
“Inaonekana , ila kwa sasa nahitaji kufanya maandalizi”
“Unahitaji msaada wangu?”
“Ndio”
“Nini nikusaidie?”Aliongea Nasra akionyesha shauku.
“Simu yangu imeisha chaji , nichajie na kisha niletee laptop yako hapa , kuna mtu nahitaji kuwasiliana nae kwa njia ya online”Aliongea Roma.
Nasra alijikuta furaha yake ya kutaka kumsaidia Roma ikipotea, na kujiambia alijawa na shauku ya bure.
Ukweli ni kwamba kitendo cha mwanaume huyo kutohitaji msaada wowote kutoka kwao iliwafanya kuwa na shauku kama atataka msaada.
Licha ya kuchukia alichukua simu ya Roma na kwenda nayo juu kuichomokea chaji na kisha alishuka na Mackbook Pro na kumpatia na Roma aliunganisha na internet palepale na aliingia mtandaoni na kulipia VPN na kisha akapakua kivinjari cha Tor na kisha akaingia mtandaoni.
“Naweza kuangalia unachofanya?”Aliuliza Nasra akiwa makini na kumfanya Roma kumwangalia na kutabasam.
“Unaweza ndio kuangalia wewe ni mwanamke wangu”Aliongea
Roma hakuona haja ya kumficha Nasra kile ambacho alikuwa akipanga kufanya , mpango wake ni kutaka kuomba msaada kutoka nje ya nchi kufika Tanzania kwa ajili ya kumsaidia jambo lake.
Roma baada ya kuingia kwenye mtandao wa Deep Web palepale aliandika link ambayo alikuwa ameikariri na dakika hio hio yaliweza kuonekana mawasiliano ya watu mbalimbali na ajabu kila mtu ambaye Roma alikuwa akiwasiliana nae ilimhuhiaji kwanza kuingiza Passcode.
Licha ya kukaa na kuangalia lakini Nasra hakuelewa chochote kwani Roma alikuwa akiwasiliana na watu kwa kutumia lugha tofauti tofauti.
Kitu pekee ambacho aliweza kugundua ni kwamba kila mtu ambaye aliwasiliana nae alionekana kumuheshmu sana Roma
Ilimchukua nusu saa Roma mpaka kumaliza .
“Babe you were so cool”Aliongea Nasra huku akijikumbatisha kwenye kifua cha Roma.
“Umeelewa chochote nilichokuwa nikiongea?”
“Sijaelewa lakini , ulivyokuwa ukiongea inapendeza sana”Aliongea akirembua na kumfanya Roma mzuka kumpanda.
“Lanlan ashalala?”Aliuliza Roma.
“Ndio na anakoroma huyo”Aliongea na kumfanya Roma kutoa tabasamu na kuingiza mkono kwenye kifua cha mrembo Nasra na kuchoropoa embe dodo.
“Kama kashalala unaonaje tukifanyia hapa hapa kwenye sofa na kisha tukaoge wote”Aliongea Roma lakini hakusubiri jibu kwani paleplae alimnyanyua na kisha akamlalia kwa juu na kilichoendelea masofa yatahadithia.
Siku ilofuata ilikuwani jumapili na Roma hakuwa na mpango wa kumpeleka Lanlan kucheza tena.
Siku hio aliona kitu pekee ni kuangalia maendelo yake katika kujifunza mbinu ya Andiko la urejesho, maana aliona Lanlan ni mwendo wa kula bata tu tokea arudi ulimwengu wa majini pepo.
Kutokana na Roma kutokuwa na nguvu za kijini hakuweza kumwangalia Lanlan amefikia levo ya ngapi hivyo kitu pekee ambacho alitaka kujua ni kumchukua na kisha wakaenda hadi msituni na wakati huo akiwa na matofali ya zege.
Baada ya kuyapangilia chini kwa mstali maalumu mawili mwili matatu mtatau na manne nne alimwambia Lanlan aanze kuyapasua kutoka mwanzo mpaka mwisho kwa kutumia ngumi.
Lanlan misuri ya mwili wake ilianza kutuna kama vile ni puto na palepale alianza kuyapasua kwa kasi na ndani ya dakika yote alikuwa ameyapiga na pigo moja moja mpaka kupasuka.
Roma alijikuta akiridhika na alijiambia kutokana na nguvu aliotumia pengine atakuwa katika levo ya Uchoyo au wanaita levo ya kujijali mwenyewe na muda wowote angeingia katika levo ya Takdiri au Hatima kwa lugha nyingine.
Hii ni levo muhimu sana katika mafunzo ya kijini lakini ukiachana katika mafunzo ya kijini lakini pia katika maisha ya binadamu ni moja wapo ya hatua ambayo ni muhimu kwa mafannikio ya binadamu yoyote , ni binadamu wachache sana ambao wanajua Takdiri yao nini katika ulimwengu huu na hao ambao wamebahatika kuijua mafanikio yao ni ya juu sana kuliko wale ambao hawaijui Takdiri yao ni nini.
Kila binadamu huzaliwa na kuwepo katika uso wa dunia kwa kusudi maalumu na ndio maana katika hatua za kujitafuta ili kujua wewe ni nani tofauti na jina lako hutakiwi kuuliza maswali mtu wa nje bali unatakiwa kujiuliza wewe mwenyewe maswali na kutafuta majibu na hapa ndipo utaweza kujua nini Takdiri yako.
Maendeleo ya Lanlan yalimshangaza sana Roma , ijapokuwa yeye wakati wa kujifunza hakutumia vidonge vyvoyote kujibust lakini kwa Lanlan spidi yake ilikuwa ya juu na alikuwa na shauku ya kutaka kujua kitamtokea nini mpaka kupita levo ya kifo na uhai halafu kuzaliwa upya.
Roma alijikuta akimsifia Lanlan kwa kazi nzuri huku akimwahidi mambo mengi lakini Lanlan alitaka kupaishwa juu angani lakini Roma uwezo huo hakuwa nao na alijikuta ile hali ya kutaka kurudisha uwezo wake na kumuondoa mdudu aliekuwa akimtawala kumvaa.
Roma aliona kwamba haijalishi Lanlan uwezo wake unaongezeka kwa spidi namna gani lakini bado tu alikuwa akipaswa kumlinda.
Roma mara baada ya kurudi na kumaucha Lanlan mojakwa moja alielekea katika maabara ya Clark eneo la Makongo juu , maabara ambayo ilikuwa urithi kutoka kwa Profesa Shelukindo.
Roma mara baada ya kufika aliweza kugundua pia Rufi yupo na wote walikuwa bize kupitia baadhi ya vitabu.
“Kuna chochote ambacho mmepata?”Aliuliza Roma akiwaangalia warembo hao namna ambavyo wapo bize.
Clark alikuwa amevalia simple huku nywele zake alikuwa amezifunga na lastick kwa nyuma, muda wote mwanamke huyo alionekana kuwa bize.
“Kulingana na maarifa ya Rufi kuhusu roho mnyama wa maafa , hakuna aina yoyote ya nguvu ya kiroho ambayo inaweza kushindana nayo kwasababu ni mnyama aliewahi kuwepo katika kipindi cha dunia kuwa katika hali ya ukiwa na machafuko , inawezekana alikuwa ni mnyama mwenye nguvu kubwa duniani”
“Dear nipo hapa kwa taarifa nzuri lakini kwanini unaongea kuniogopesha?”
“Mimi ni mwanasayansi na sio motivation speaker , ninachokuambia ni fact , mambo hayapo mazuri sana kwa upande wetu”
“Hubby huna haja ya kujali sana kuhusu alichoongea Clark , ijapokuwa sina wazo namna ya kuishinda lakini tunaweza kushinda kutokana na hasira yake”
“Hasira yake?”
“Ndio”
“Hio ni roho ya mnyama mkali sana ambaye sifa yake kubwa ni kukasirika na kutokuwa na huruma , hivyo tunapaswa kutafuta roho nyingine ambayo ni ya mnyama lakini mpole ili tu kuiamsha ndani yako , ijapokua roho hio inaweza kuwa na nguvu kidogo kushindana na Chaos, hivyo kabla ya jaribio hilo tunapaswa kuanza na nguvu zako za kijini , tunapaswa kuibadili nguvu yako ya kijini na kuiweka katika kitu ambacho kitakandamiza roho yake ya ukali”Yalikuwa ni maelezo mengi ambayo Roma alishindwa kuyaelewa.
“Umeongea vitu vingi , je una mpango wowote?”
“Tuna mawazo tofauti , nilikuwa nikiwaza vipi kama utaombewa kanisani au kusomewa swala msikitini , watu wa dini wana upako wa kutosha, ninachojua nguvu iliopo ndani yako ni ya kipepo hivyo inaweza kusafishwa na nguvu ya kiroho ya nuru ya kidini ambayo ni safi”
“Clark tangu lini wewe kama mwanasayansi ukaanza kuamini katika maombezi”Aliongea Roma kwani siku zote Clark kila mama yake alipokuwa akimlazimisha kwenda kanisani alimwambia hakuna Mungu kwasababu hakuna uthibitisho wa kisayansi.
“Mimi najua mambo mengi kuliko unavyodhania , ijapokuwa sijawahi kuamini katika imani yoyote lakini kuna nguvu ya kiroho ambayo sio ya kawaida katika misikiti pamoja na kanisani ndio maana watu wana imani kali, nimeamini baada ya kujifunza mbinu za kuvuna nishati za mbingu na ardhi”Aliongea na Roma alitingisha kichwa kwani hata yeye alikuwa akikubalaina nae.
“Vipi kuhusu wewe Rufi?”
“Mimi nimeona labda ujaribu kusali kibudha au kihindu, kuna Monk ambao wana uwezo mkubwa wa kufanya ‘Exorcism’ lakini kazi kubwa ni kuwapata na kuwa na utayari kufanya hio kazi, nimeshindwa kujua ni aina gani ya nguvu ya kiroho ambayo inaweza kushindana na nguvu ya Chaos”
“Kwahio mwishowe tuna uelekeo lakini mpango hatuna”
“Sio kabisa , kama tutashindwa kukusaidia kwa njia za maombezi au Exorcisim basi angalau tunapaswa kupata Dhana za kijini za kiwango cha juu kabisa ambazo zina uwezo wa kushindana na roho ya mnyama wa maafa”
Baada ya Rufi kuongea vile mawazo ya Roma yalimkumbusha kitu kimoja ambacho aliiba katika madhabahu ya Mzee Sharif.
“Nimekuja hapa kwa kitu kingine pia , hebu ngoja niwaonyesheni muone..”Aliongea Roma na kisha palepale alitoa ile Kokoto iliokuwa na jina la Hazina na kisha akampatia Rufi.
“Unaijua hii maana yake?”
Write Note:Exorcism ni kama vile wanavyofanya waganga wa kienyejji katika kufukuza mapepo , sasa katika imani ya Kibudha na Kihindu hufanya hicho kitendo pia kwa muumini mwenye mapepo.

SEHEMU YA 654.
Rufi na Clark walikuwa wameshangazwa sana na neno Hazina na palepale walijikuta wakifungua kile kijiboksi kuangalia kilichopo ndani.
Lakini mara baada ya kuona kitu chenyewe walijikuta wakikosa yale matamannio yao, walijiuliza kokoto inaweza vipi kuwa hazina.
“Ndio nini hiki , ndio Hazina uliokuwa ukisemea , mbona inaonekana kama pande la mkaa lakini uzito wake ni mkubwa kuliko wa mkaa , au ni jiwe?”Aliuliza Rufi.
Clark hakuonyesna kukupurukuka na aliishia kuangalia kwa umakini kujaribu kukagua na kulipatia maana yake kwani palepale aliliweka katika Darubini na kuanza kulikagua kisayansi na ndani ya dakika tano tu alionekana kupata majibu kadhaa.
“Linaonekana kama vile ni ‘Carbide’, kuna aina ya madini ndani yake lakini ajabu pia kuna protini , au ni Fossi , asili mara nyingi inakuwaga na vitu ambavyo vinaonekana kama vimekufa lakini bado vipo hai , hata hivyo vitu vya aina hio sio vingi lakini sio adimu pia”(Fossil ni mabaki ya kale)
Roma alijikuta pia na yeye kuchukia na kujiambia hio takataka kwanini iwe ndio Hazina , lakini kwa wakati mmoja alijiambia familia ya Sharif ni matajiri na hata kiboksi kilichotumika kuihifadhia ni cha madini ya Dhahabu, alijiuliza au ni kumbukumbu.
Roma mara baada ya kuona hakuna majibu ya haraka haraka alificha hazina yake alioona kama takataka na kisha akawaambia waondoke pamoja kwa ajili ya chakula cha mchana
Roma wakati akiwa njiani kurejea nyumbani aliweza kupokea simu kutoka kwa Sophia na kumweleza kwamba yupo Afrika ya kusini anashoot matangazo ya Promosheni ya filamu na angerejea Tanzania hivii karibuni kwa ajili ya Show ya siku ya usiku wa Christmas na Roma alimuahidi kwamba atahudhuria show yake.
Roma mara kutoka nje ya gari aliweza kumkuta Lanlan ambaye alikuwa amelalia tumbo kwenye kibaraza huku makaratasi mengi na penseli za kuchotea zikiwa zimezagaa huku pembeni yake akiwa amesimama Qiang Xi.
Muda huo ilikuwa ni jioni na Nasra alikuwa ameenda Supermarket kwa ajili ya kununua vitu vya kupika usiku.
Roma alimsogelea Lanlan na kisha aliinua karatasi ambazo alikuwa amemaliza kuchora na kisha aliona sura ya Superman na chini yake kuna jina la Daddy.
“Lanlan mimi ndio Superman?”Aliuliza Roma huku Lanlan akiwa bize kukoleza rangi ya mti aliochora na alimgeukia Roma na kutingisha kichwa kukubali kwamba ndio yeye.
“Na huyu mwanamke na msichana ni nani ?”
“Huyo msichana mdogo ni Lanlan na msichana mkubwa ni mama yake Lanlan , Mama ana nwele ndefuu mpaka shingoni”
“Umekosea, Lanlan wetu ni kibonge lakini huyu hapa ni mwembamba”
“Lakini Lanlan hapo amekonda kwasababu amemmisi mama yake”Aliongea na kumfanya Roma kutabasamu kwa uchungu.
“Umekonda vipi wakati ulikuwa ukila chakula chote ambacho Aunt Nasra anakuandalia , hujakonda bwana”
“Lakini Lanlan atasikia njaa asipokula , ila anammisi mama yake”Aliongea huku akiwa kama vile anaona aibu kuumbuliwa na kumfanya Roma kutoa cheko.
“Aunt yako Nasra atakasirika , yaani amekupikia chakula kitamu lakini hujamchora?”
“Kwasababu mama simuoni na nammiss ndio maana nimemchora”Aliongea na kumfanya Roma kukaa kimya.
Sio kwa Lanlan ambaye tu alikuwa amemmisi Edna bali hata yeye mwenyewe alikuwa amemkubuka sana .
“Daddy ,Je Mama hatutaki tena?”Aliuliza huku akitia huruma na kumfanya Roma kushangaa.
“Lanlan , unapaswa kukumbuka kwamba mama yako anakupenda na kwasasa hana furaha ndio maana , kila kitu kitakuwa sawa muda si mrefu”
“Nina uhakika Mama ananipenda kwasasabu yeye ndio amenizaa”Aliongea Lanlan akiwa na uhakika na Roma hakuelewa ujasiri wake unatokana na nini.
Ilimfanya kuingiwa na majonzi kwa kuona pengine Lanlan ameshindwa kumtofautisha mama yake mzazi na Edna, Roma alishindwa kujizuia na kumkumbatia.
Qiang ambaye alikuwa akisikiliza maongezi hayo alijikuta akitokwa na machozi tu na kuishia kuyafuta kwa siri.
Hakuna ambaye angeweza kuamini kwamba Lanlan alikuwa ameficha kile anachojisikia na kujitahidi kuonekana ni mwenye furaha muda wote.
Usiku wa jumapili uliweza kuisha vizuri na Roma mara baada ya kuamka alijua ndio siku ambayo Edna atakuwa amerudi na ataenda kazini kama alivyosema Nasra.
Kuhusu hafla ambayo Maimuna aliongea hakutaka sana kuwazia maana ingemfanya tu kuwa na wasiwasi.
Roma alitaka kumsubiri Edna atakaporudi ndio aongee nae lakini alijiambia anapaswa kuchukua hatua yeye kwanza kama mwanaume , alijiambia pengine Edna anasubiria yeye aanze.
Hivyo mara baada ya wazo hilo kumuingia alienda moja kwa moja mpaka nyumbani na aliweza kukutana na Bi Wema ambaye alimwambia Edna alirudi lakini ameelekea kazini.
Roma palepale alifanya maamuzi ya kuelekea huko huko kazini kuonana nae.
Roma mara baada ya kufika ndani ya jengo la makao makuu ya kampui ya Vexto moja kwa moja alienda mpaka Floor ambayo ndio rasmi ofisi ya Mwenyekiti wa kampuni inapatikana , ni ofisini ileile ya Edna lakini ilikuwa imebadilsihwa tu hadhi.
Ijapokuwa Ernest ndio alikuwa CEO lakini hakuwa akitumia ofisi ya Edna ya mwanzo.
Roma mara baada ya kutoka kwenye lift moja kwa moja alitembea mpaka kwenye mlango wa kuingilia ofisni huku akipata burudiko la kiyoyozi na harufu ya kuvutia na kisha aligonga mlango lakini hakuweza kupata mrejesho.
Dakika ileile mlango wa ofisi ya Sekretari ulifunguliwa na aliweza kutoka msichana mrembo kiasi alievalia kinadhifu.
“Wewe ni Mr Roma?”Aliuliza.
“Ndio , wewe ni nani?”
“Mimi ni Sekretari mpya , naitwa Yulia , naamini hunifahamu , upo hapa kwa ajili ya kuonana na Mwenyekiti”Aliongea kwa namna ya heshima.
Ilionekana alikuwa na taarifa zote kuhusu Roma ni nani , ni kama kawaida mfanyakazi mpya lazima ajue Hidden rules za mazingira ya kazi ili kuepuka kufanya makosa na kuwa upande mbaya na watu wakubwa.
Roma aliishia kutabasamu kumuondolea woga , alijua atakuwa ni mbadala wa Recho ambaye alipandishwa cheo na kuwa mkuu wa idara.
“Ndio yupo wapi?”
“Yupo kwenye kikao na Bodi ya wakurugenzi , wapo chumba namba tatu cha mikutano”
Kama ilivyotarajiwa , mwanamke mchapakazi ambaye hana mpango wa kuacha.
Roma hakuwa mgeni hivyo alijua chumba namba tatu cha mikutano kipo upande upi na mara baada ya kufika aliweza kuona viti vyote vilikuwa vimejaa na wafanyakazi wa juu wa makampuni pamoja na wanahisa , wote wakiwa na sura za kitaaluma.
Edna alikuwa amekaa mbele kabisa kawenye kiti cha kibosi akiwa kauzu kama kawaida yake , hakukuwa na ishara zozote kama alikuwa na mawazo na ilikuwa ni kama ukauzu wake uliongezeka zaidi na zaidi.
Kila mfanyakazi aliekuwa ndani ya hilo eneo alikuwa akimhofia Edna huku wengine wakionyesha heshima zao , ilikuwa ni kama mawaziri wanavyomheshimu mheshimiwa Raisi.
Baada ya Roma kufungua mlango na kuingia macho yote yalimgeukia huku baadhi ya Sura zikimwonyeshea tabasamu , akiwemo Ernest Komwe na Monika.
Upande wa Dorisi na Nasra walishangazwa na ujio wake kwani hawakutegemea kama angeweza kuja hapo mapema hivyo.
Roma aliwaonyeshea tu tabasamu na ksiha akageuza uso wake kwa Edna na kumwangalia kwa namna isiokuwa ikielezeka.
Kama sio jasiri usingeweza kuingia ndani ya chumba kama hicho ambacho kilikuwa na zaidi ya watu therathini.
Edna alionekana kukunja sura tu mara baada ya kumuona Roma lakini hakukuwa na mabadiliko makubwa , yaani alimwangalia kwa sekunde tu na kisha akampotezea kama hamjui.
Baadhi ya watu tayari walishagundua mabadiliko hayo na kuishia kuwaangalia kwa namna siokuwa ya kawaida.
Roma baada ya kuona namna Edna alivyomwangalia alijikuta akikosa furaha na aliishia kushika kidevu chake na kufunga mlago na kisha akaegamia ukuta kama bodigadi.
Ijapokuwa alitamani kuongea na Edna lakini hakuona haja ya kumsumbua akiwa katika kazi kama hivyo.
“Recho , please continue with your presentation”Aliongea Edna akimwashilia kwa kunyanyua karamu.
Kampuni hio ilikuwa ikitumia mara nyingi lugha ya kingereza katika vikao vyote na mara nyingi hata wafanyakazi wakifanyiwa usaili wanapimwa uwezo wao wa kuongea kingereza kwa ufasaha na kukielewa pia. Isitoshe lazima iwe hivyo kwani kulikuwa na wafanyakazi na baadhi ya wanahisa ambao ni wazungu wasiokuwa wakijua lugha ya kiswahili , akiwemo Rich pamoja na Ernest mwenyewe.
Recho alionekana kukosa utulivu mara baada ya kumuona Roma lakini alijakaza na kisha aligeukia Projector.
“Kutokana na kuundwa kwa Vexto group kimataifa , itahitajika kugawa majukumu kwa wafanyakazi wakubwa wa kampuni kwenda kufanya kazi katika matawi Tanzu ambayo yapo nje ya nchi ili kurahisisha mwenendo mzuri wa kampuni pamoja na kugundua fursa nyingine za kibiashara, Mwenyekiti wetu wa bodi anaamini sisi wafanyakazi wa ngazi ya juu tunapaswa kuwa mfano katika kutoa mchango wa maendelo katika kampuni hivyo , Mwenyekiti amependekeza Dorisi kupandishwa cheo kuwa sawa na Nasra na watapaswa kuondoka nchini kwenda kufanya kazi katika matawi yafuatayo , Dorisi ataelekea Cape Town Afrika ya kusini na Nasra ataelekea Buenos Aires Argentina, watakuwa ndio Wakurugenzi wa makampuni haya yote mawili ambayo yameanzishwa rasmi na kazi zao ni kujenga msingi wa kibiasara katika masoko hayo mapya.

SEHEMU YA 655.
Dorisi na Nasra ni kama vile hawakuwa wamesikia vizuri , hata Roma ambaye alikuwa amesimama vilevile ni kama hajasikia vizuri.
Afrika ya Kusini , Argentina?!!
Roma hakushangaa sana uwezo wa Edna kuchanja mbuga kimataifa hususani kutokana na mtaji waliokuwa nao , hivyo sio jambo la kushangaza kampuni ya Edna kuanzisha tawi jipya Argentina na Afrika ya kusini lakini alijiuliza kwanini anataka kuwatuma Dorisi na Nasra.
Bila shaka kama wataenda huko ilimaanisha kwamba madaraka yao pamoja na malipo yangekuwa makubwa zaidi lakini kuwaagiza wanawake hao wawili kwenda nje ya nchi ni sawa na kuwafukuza tu ndani ya Tanzania.
Dorisi na Nasra waliweza kuhisi kitu na waliishia kumwangalia Edna kwa macho yasiokuwa ya kawaida lakini Edna hakuwaangalia hata kidogo.
“Mwenyekiti , sote sisi tunajua michango mikubwa na uwezo wao mkubwa katika maendeleo ya kampuni na ni sahihi kuwa wakurugenzi wa kampuni tanzu lakini nadhani wangeweza kufanya kazi nzuri zaidi kama wangebakia hapa makao makuu kutokana na uzoefu wao”Aliongea Ernest Komwe akitoa mchango wake.
“Wanapaswa kuongoza kampuni kama ishara ya kutoa mfano kwa wengine watakaochukua nafasi zao , sitojisikia vizuri kama nikituma mtu ambaye sio mdhoefu na biashara zetu , isitoshe kwenda huko kutawafanya kupata uzoefu wa kimazingira , CEO Ernest vipi unataka kwenda wewe?”Swali hilo lilimfanya Ernest kufunga bakuli lake.
Monika ambaye alishawahi kufanya kazi kama msaidizi wa Edna alikuwa akijua tabia yake hivyo alimwangalia mume wake na kumpa ishara ya kutulia.
Kila mmoja alijua kama Dorisi na Nasra wataenda huko watafanya kazi nzuri sana lakini isingekuwa rahisi kwao kwani walikuwa wakienda kukutana na mazingira mapya.
Roma aliekuwa amesimama kwenye kona ya mlango alijikuta akikunja ngumi na kujiambia je anafanya hayo yote kwa ajili ya kumlipizia.
Alijiambia sio tu kwamba wakati huo alikuwa akimpotezea lakini ameenda mbali na kuanza kuwaondoa wanawake wake karibu na kuwatuma nchi ya mbali.
Bila shaka , kama kiongozi mkuu wa kampuni Edn alisifika kwa kutopenda kupingwa akiamua jambo lake , kwa jinsi ambavyo alimwagiza Recho kusoma mapendekezo yake ilikuwa ikimaanisha kwamba alishafanya maamuzi tayari.
“If there is no objection from the vice presidents , we can proceed with the voting process , raise your hand if you approve of this proposal”Aliongea akimaanisha kama hakuna pingamizi kutoka kwa watendaji wasaidizi wa kampuni basi anaekubaliana na pendekezo lake anyooshe mkono kupiga kura.
Kati ya wakurugenzi ambao walikuwepo ni Mzee Alex mmiliki wa zamani wa kampuni ya Jr ambaye ipo chini ya Edna kama mwanahisa mkuu na wote kwa pamoja waliangaliana na kisha walionekana hakuna ambaye alikuwa akipinga kwani walinyoosha mikono kupiga kura ya ndio.
Yaani kwa jinsi wanahisa hao walivyonyoosha wote pasipo ya yoyote kutopinga ni kama vile walikuwa washajiandaa,
Recho alisimama kwa ajili ya kuhesabu kura hizo lakini Edna alimzuia.
“Hakuna haja ya kuhesabu , tayari tuna asilimia hamsini ya kura zote wanaokubali kabla sijatoa kura yangu , inaonyesha wengi wenu mmekubaliana na pendekezo langu , Miss Dorisi na Miss Nasra matawi yote mawili hayajamaliza hata miezi sita tokea yafunguliwe hivyo tunategemea kazi kubwa yenye mchango chanya kutoka kwenu”
Dorisi aliishia kuwa kimya huku macho yake yakiwa tayari ni makundu , ni kama vile muda wowote angetoa machozi , upande wa Nasra alionyesha hasira na wasiwasi kwa wakati mmoja.
“Edna kuna haja ya kwenda mbali hivi , inaonyesha hapa kabisa ulishaongea na Shareholders kupiga kura ya ndio ili sisi kwenda nje ya nchi mbali na Tanzania , umefurahi sasa?”Alisimama Nasra na kubwata huku akimwangalia Edna kwa macho makavu.
Watu wote kimya , hakuna ambaye alikuwa tayari kuongea lolote , ni kama walikuwa wakitarajia dhoruba kuamka muda wowote.
Ilionekana kwa watu hao ni kama kweli Edna alikuwa akifanya makusudi kabisa na hakujisumbua hata kuficha dhamira yake na ilionekana ni kama kuwadhalilisha mbele ya kila mtu.
Lakini licha ya hivyo hakuna ambaye alikuwa tayari kupinga maamuzi ya Edna , licha ya kwamba maamuzi yake yalionekana kuwa na ukakasi.
Mtu pekee ambaye hakupiga kura ya ndio au hapana alikuwa ni Mzungu Richie peke yake , alikuwa amefumba macho kama vile kuna kitu ambacho alikuwa akiwaza.
“Sijaelewa unachotaka kumaanisha”Aliongea Edna akimwangalia Nasra.
“Edna acha maigizo , unakasirisha ujue”Aliongea Nasra akiwa amepaniki hatari.
“Kama hukubaliani na maamuzi ya bodi , tunakukaribisha muda wowote kuleta barua yako ya kujiuzulu”
“Unadhani nnitashindwa kufanya hivyo?”
“Sidhanii hivyo , najua zipo kampuni nyingi ambazo zinakuhitaji”Aliongea Edna bila ya kuonyesha hisia zozote ni kama vile hakuwa akimjua Nasra,
“Benadetha utadili na hili swala , kama Mkurugenzi Mtendaji Nasra akitaka kujiuzlru nipo tayari kununua hisa zake zote kwa thamani mara mbili iliopo sokoni”Aliongea na Benadetha ambaye alikuwa kimya muda wote aliishia kutingicha kichwa tu.
“Edna unafikiri nimesema haya kwasababu ninajali sana kuhusu hisa zangu , unafikiri nitakuwa na furaha kama utanipa hela?”
“Furaha yako hainihusu , asante kwa mchango wako uliotoa kwa kampuni , sitokutendea vibaya kama utaamua kujiuzulu”Aliongea na kumfanya Nasra kujibwaga kwenye kiti huku akimuona kama Edna sio yule ambaye alikuwa akimjua.
“Nasra huna haja ya kuwa hivi , Mwenyekiti wa bodi ashafanya maamuzi lakini ni kweli hatuwezi kwenda nchi za mbali hivyo kwa ajili tu ya kazi hivyo chaguo lililobaki ni kujiuzulu”Aliongea Dorisi.,
“Dorisi unamaanisha nini kwamba hatuwezi , tatizo hapa sio kwenda mbali hivyo , shida ni kwamba hajaongea na sisi kabla , anatuchukulia sisi kama takataka kututupa kila mahali anapoona panafaa , nimeamua kufanya kazi hapa sio kwasababu sina sehemu nyingine ya kwenda kufanya kazi , sijali sana kuhusu nafasi yangu wala mshahara ninaopata wala hisa ninazomiliki, lakini mimi pia kama mfanyakazi wa hii kampuni nina kanuni zangu na utu wangu ambao unapaswa kuheshimiwa”
Dorisi aliishia kukunja sura , alikuwa akijua Nasra alikuwa sahihi lakini ilionekana haiwezekani kuweka mstari kati ya maswala ya kazi pamoja na mambo binafsi.
Dorisi mara baada ya kuwaza hivyo alijikuta akimgeukia Roma na kumpiga jicho na aliweza kugundua alikuwa kwenye mawazo pia kama vile kuna kitu ambacho alikuwa akiwaza , kwani alikuwa ameinamisha kichwa chake chini.
“Edna tokea siku ambayo nilijiunga na kampuni hii , sijawahi kuwaza kama nitapata chochote , , bibi yako na mama yako ndio watu ambao wamenifanya kuwa Nasra wa leo hii kwa kila kitu nilichokuwa nacho na siku zote nitaendelea kuwa mwenye shukrani , kama shukrani zingeweza kupimwa katika kipimio cha hela basi ningesema faida ambayo nimeingiza kwenye hii kampuni imepita deni ambalo mama yako ananidai , kama sio wewe kuongoza hii kampuni nisingejisumbua kufanya kazi ndani ya kampuni moja kwa miaka yote hio , sikuacha kufuata ndoto zangu na kufanya bidii kwa ajili ya mafanikio ya hii kampni kwa ajili ya mtu yoyote bali nimefanya yote hayo kwa ajili yako , Edna najua ni kweli kabisa nimekukosea wewe binafsi lakini kwanini unataka kunidhalilisha kazini , sijui wengine watanionanje lakini mimi kama mwanamke mwenzio nimekudharau”
Roma alijikuta akiinua uso wake na kumwangalia Nasra ambaye hakutaka kuonekana mnyonge mbele ya Edna , hali yake ya kujiamini na ujasiri wake ilimkumbusha na kumuona kama mwanajeshi.
Edna muonekano wake haukuadilika kabisa , ni kama vile hajamsikia kwa chochote kile alichoongea .
“Kama Miss Nasra na Miss Dorisi watachukua maamuzi ya kujiuzuru , majukumu yao ambayo walikuwa wakiyafanyia kazi kwasasa yatakuwa chini ya Recho , Benadetha pamoja na Rich , nitapenda kuona kila mmoja wenu kuanza kufikiria ni nani ambaye anafaa kurithi kazi zao kabla ya kikao kingine au vinginevyo nitafanya hio kazi mwenyewe”Aliongea kwa kujiamini kabisa.
Ukauzu wake na hali ya kujiamini na kutoathirika iliwaanya wafanyazi kumhofia na kujiuliza inakuwaje akawa haathiriki kwa chochote kutokana na kubweka kwa Nasra.
Nasra alijikuta akimpiga jicho la chuki Edna na palepale alikusanya kila kilichokuwa chake na kisha aliondoka akiwa wa kwanza, ilikuwa ni kama vile alikuwa amepoteza muda mwingi wa kufanya kazi ndani ya kampuni ya Vexto.
Ni Dorisi peke yake ambaye alijitahidi kuzuia hisia zake zisimvae na palepale na yeye alikusanya vitu vyake na kumsogelea Roma na kumpa ishara ya kumfuata.
“Bado tu unataka kubakia hapa?”Aliuliza Dorisi na Roma alijikuta moyo wake ukijinyonga, katika mazingita kama hayo kama angeonyesha kusita sita ingewafanya kujisikia vibaya zaidi hivyo aliuvaa ujasiri na kisha akawashika mkono na kuondoka nao.
“Tutaenda kwenye hoteli yoyote, na nitawaruhusu mywe bia hadi mlewe mpunguze mawazo , mnaonaje?”Aliongea Roma na wote walitingisha kichwa na kuondoka.
Roma alifanya kama alivyowaambia na aliwapeleka katikati ya jiji na kisha akawaagizia chakula pamoja na vilevi na siku hio Dorisi na Nasra walikichafua haswa kiasi kwamba walilewa chakali.
Baada ya kuelwa wote hakuna ambaye alitaka kuondoka na Nasra na Dorisi wote walitaka kulala hotelini na Roma licha ya kwamba ilikuwa mchana bado.
Roma mara baada ya kujifikiria kidogo aliona awape kile walichotaka na palepale alienda kuchukua chumba na kisha aliwabeba wote kwa pamoja na ulevi wao na kuwabwaga kitandani na kupiga Treesome ya nguvu kwa muda mrefu na mpaka anakuja kumaliza wote walionekana kutosheka na bakora za kimkakati na waliishia kukumbatiana na kisha wakapitiwa na usingizi.
Roma alijikuta akitingisha kichwa na palepale aliangalia saa na kuona ni saa kumi na moja kuelekea saa kumi na mbili.
Ijapokuwa Edna alionekana alikuwa amebadilika nje kabisa ya mategemeo yake lakini hakutaka kupitisha hio siku bila ya kuongea nae , hivyo aliingia bafuni na kuoga na kisha akavaa na kuwaacha.
Kwa spidi aliotumia kuendesha ilimchukua dakika chache tu kufika Ununio na ile anaingia katika barabara ya Ununio Road aliweza kuona gari ya Edna kwa mbele akionekana ndio anarudi kazini.
Dakika chache tu gari iliweza kuruhusiwa kuingia ndani ya geti tena kilichomshangaza zaidi Roma ni kwamba ijapokuwa geti lilikuwa likijifungua lenyewe lakini lilifunguliwa ‘Manual’ tena aliefungua ni Lanlan ambaye pembeni yake alikuwa amesimama Bi Wema.
Roma hakujisumbua kuingiza gari ndani kwani alitoka palepale na kukimbilia ndani,.
“Edna subiri”Aliongea Roma mara baada ya Edna kutoka nje ya gari baada ya kuliegesha lakini ni kama hajamsikia Roma.
Lanlan ambaye alikuwa ndio anamalizia kufunga geti alijikuta akitoa tabasamu la furaha na kuanza kumkimbilia mama yake kwa shangwe huku akimwita Mama.. Mamaaa..
Edna mara baada ya kuitwa vile alisimama na ksiha akamgeukia Lanlan na kumwangali kama vile hamjui.
“Umemuita Mama mtu asiesahihi , mimi sio mama yako”Aliongea kwa Kingereza huku akimtoa Lanlan mikono ambayo imemshikilia.
Kitendo cha Edna kumwambia Lanlan vile kilimfanya kumwangalia kwa macho ya kutia huruma na palepale aliishia kuchuchumaa na kuanza kudondosha machozi chini.
Roma alietaka kuongea tena alijikuta mdomo wake ukiishia hewani na hasira zilimpanda mara baada ya kumuona binti yake akilia.
Lanlan alikuwa na furaha ya kumuona mama yake kwa mara nyingine na hata ujio wake hapo ni kutokana na kujua huo ndio muda wa kurudi kazini lakini jibu la Edna lilimnyong’onyesha , alikuwa ni kama vile amemwagiwa ndoo ya maji ya baridi.
Roma alikubali Edna kumchukia yeye lakini alijiuliza kwanini anamfanyia hivyo na Lanlan ambaye anamchukulia kama mama, uvumilivu palepale ulianza kumpotea.
“Edna naona sasa unavuka mpaka”Aliongea Roma kwa namna ya kufoka huku akimpakata Lanlan na kumfanya machozi yake yaloanishe kifua chake
“Mommy doesn’t want Lanlan again …Mommy doesn’t like me anymore..”Aliongea Lanlan akilia akisema kwamba mama hamtaki tena na mama yake hampendi.
Kilio cha Lanlan kiligusa moyo wa Bi Wema na alijikuta akimsogelea Edna na kumwangalia usoni.
“Edna unafanya nini , huwezi kutolea hasira zako kwa mtoto kisa tu mna ugomvi”Aliongea Bi Wema na palepale alimsogelea Lanlan kwa jaili ya kumtuliza lakini ilikuwa ngumu kutulia.
Lanlani alikuwa na kumbbukumbu za kuachwa na mama yake kwa mara ya kwanza hivyo hicho kinachotokea ni kama alikifananisha na kumbukumbu zake mbaya zilizopita ndio maana kilio hakikiwa cha kawaida.
“Bi Wema mimi sitaki kuhusika nao tena , huyo ni mtoto wake na sisi tumeachana, ni kwamba tu hatujasainishiana maswala ya talaka kwani kuna taratibu za kuchukua”Aliongea
Roma alikuwa akitetemeka kwa hasira mno kutokana na kilio cha Lanlan na alijihisi ni kama ule uchizi wake wa siku nyingi unaanza kumvaa.
“Edna ,,, unaweza kunichukia utakavyo na sitolaumu lakini umemuumiza binti yangu kihisia ,, na hii ni sababu ambayo inanifanya nitake kukua sasa hivi..”
Waooo
 
Mkuu bado tupo hapa mashabiki wa kazi zako, tunasubiri muendelezo. Ikikupendeza shusha mzigo wa kutosha arosto ni kali Sana🙏🙏🙏
 
NILIMDHANIA KAHABA KUMBE BIKRA

MTUNZI : SINGANOJR

WATSAPP: 0687151346

Mono no aware

SEHEMU YA 660.

Brewster ni mjukuu wa Sauron , alikuwa amebadilika sana tokea mara ya mwisho alivyokuwa katika visiwa vya wafu wakati Roma alivyoenda kusherehekea harusi yake na Edna.

Wakati huo alikuwa ashapanda cheo na kufikia ngazi ya Kanali wa jeshi na kumfanya kuzidi kuwa kauzu na ule upole wake wote ulikuwa umemwishia.

Tokea mara ya kwanza kupewa misheni ya kulinda usalama katika nchi ya Somalia alikuwa akifurahia sana hio kazi kwani kulikuwa na wanajeshi wengi ambao walikuwa wakisikiliza maelekezo kutoka kwake.

“Madam Tanya kama ulifanikisha kutegesha mabomu kwa msaada wa vijana wako wa Yamata sidhani ni swala la wewe kuwa na wasiwasi , yana uwezo mkubwa sana kimlipuko lakini hayana athari zozote kwa Mfalme Pluto , na isitoshe yeye ndio aliekuambia ufanye hivyo sidhani una haja ya kuwa na wasiwasi”Aliongea Kanali Brewester.

Tanya aliekuwa kwenye wasiwasi alijikuta akiinamisha kichwa chake chini na kisha akageukia wanajeshi waliokuwa nyuma yake.

Ukiachana na hio Manowari ya kijeshi yenye uwezo wa kulipua bomu la nyuklia lakini pia kulikuwa na meli sindikizi mbili(fregates) pamoja na meli ya kivita ya uharibifu moja , zote zikiwa zimejazwa vifaa vya teknolojia kubwa ambayo ilikuwa ni zaidi ya ile ambayo inatumiwa na majeshi ya kawaida.

Wakati wao wanakuja eneo la karibu kwa ajili ya kufanya mashambulizi meli nyingine za kivita zilikuwa zikiwasubiria katika maji ya kimataifa ili kama kutatokea shida yoyote ya kuhitaji msaada basi uweze kutumwa haraka.

Wakati huo manuari hio ya kijeshi haikuwa ikitembea kwa spidi kubwa , ilikuwa ikipiga misele ndani ya maji ya bahari ya Tanzania ili kumsubiria Roma aweze kufika.

Tanya alikuwa kwenye mshangao , mwanzoni baada ya kupewa maelekezo na Roma kuingia Tanzania na kutega mabomu na kisha kwenda Somalia kukutana na kitengo cha The Eagles kwa misheni nyingine alichukulia poa.

Ilikuwa mara yake ya kwanza kufanya kazi katika manowari za kijeshi hivyo alijikuta akishangaa sana na kujiiuliza maswali mengi mara baada ya kuona vifaa hivyo vya kivita vya teknolojia kubwa na alijiuliza imekuwaje Mflame Pluto akafanikisha yote hayo , inawezekana vipi mtu kumiliki meli ya kivita.

Kwa uelewa wake mdogo alikuwa akiamini hata kama uwe na pesa vipi huwezi kumiliki meli ya kivita kirahisi bali ilihitajika nguvu kubwa na ushawishi mkubwa kukamilisha hilo..

Kilichomshangaza zaidi ni kwamba manowari hizo za kijeshi zimekuwa ngumu kushikwa na vyombo vya usalama vya majeshi ya Tanzania ikimaanisha kwamba teknolojia yake sio ya kawaida na kwa haraka haraka alijua teknolojia hio inaweza kuwa tishio kwa taifa kubwa kama la Marekani , hivyo alijiuliza imekuwaje taifa kama la Marekani kuruhusu kitu kama hicho kitokee.

Kama asingepewa ruhusa ya kuhusika katika hio misheni asingejua hayo yote , hivyo alikuwa kwenye mshangao huku wengine wote wakionekana kawaida.

“Kanali , je unaweza kuniambia jina la hii Fleet , sijawahi kusikia kundi la kimasenari kama hili?”

“Madam Hanya ninaweza kukuambia yote kwasababu umeshakuwa mwenzetu , lakini napaswa pia kukurekebisha hii manowari pamoja na meli zile za kivita sio za kwangu bali mmiliki ni Mfalme Pluto , mimi ni Kamanda tu wa hii Ghost Submarine, nimeweza kupatiwa cheo hiki na mfalme Pluto mwenyewe kutokana na kuwa ndugu wa Sauron , sisi sio kundi la kimasenari kwasababu jeshi leti limeundwa kwa taratibu za kimataifa kwani tuna nchi ya kulinda pia na sisi ni sehemu tu ya jeshi lote”Aliongea na kumfanya Tanya kujawa na mshangao akishindwa kuamini kama wanajeshi aliowaona ni sehemu tu ya jeshi.

Tanya pengine hakujua kuhusu visiwa vya wafu vipo chini ya himaya ya mfalme Pluto , ilikuwa sahihi kwani hakuwa amefanya kazi kwa muda mrefu akiwa chini ya Roma.

Ukweli ni kwamba iliwezekana Roma kumiliki vyote hivyo kutokana na kurithi nguvu yote kutoka kwa Pluto wa zamani na Roma aliendeleza tu pale alipoishia , isingekuwa hivyo kwa umri wake asingeweza kumiliki kila kitu alichokuwa nacho.

Historia ya jeshi la The Eagles ni ya muda mrefu pengine kabla ya Roma mwenyewe kuzaliwa.

“Kuna mtu anakuja … ni Mfalme Pluto”Aliongea Tanya huku akiangalia juu ya maji kwani wakati huo manowari hio ilikuwa imejitokeza juu.

Kanali Brewester aliweza kuona pia ujio wa mtu , ilimpa wasiwasi mwanzoni kwani alishindwa kupata mawasiliano na Roma.

Roma alikuwa akiogelea kwa spidi kubwa kama vile ni samaki huku sura ya Maimuna ikiwa imejitokeza kwa juu akiwa amemshika kwa chini na mkono mmoja tu.

Nguo zake zote zilikuwa zimechanika na ilimfanya kujisikia vibya kuogelea mpaka kwenda kuifikia Manowari

Wakari Roma anapambana na wale majini alikuwa na uwezo wa kutoroka katika lile eneo kwa kutumia kanuni za anga lakini aliona isingekuwa njia yenye ufanisi mkubwa , kwani aliamini kulikuwa na uwezekano wa Jini Ghula kumzuia na pia ingemfanya kuonekana mueleko wake.

Roma hakuwa akijua kama anaweza kuokoka kirahisi lakini mara baada ya kutumbukia kwenye lile shimo aligundua kuna bomba kubwa kama handaki ambalo lilikuwa limechimbwa kuelekea baharini na mara baada ya kulifuatisha ndio aliweza kuona njia rahisi ya kujiokoa.

Upande wa Maimuna hakuweza kuathirika saa kutokana na nguvu zake za kijini na hilo ndio ambalo pia lilimrahishia kutoroka.

Wakati Roma anatoroka wale wazee wote wa kijini walikuwa bize kujiokoa katika adha iliowakumba ya mvua yamakombora hivyo hawakuona hata wakati ambo Roma ametoroka.

“Your Majesty Pluto , Chief Commander of the Ghost fleet Submarine , Brewster reports”

“Mfalme Pluto Kamanda wa Ghost fleet , Brewester anaripoti”Aliongea Kanali Brewster huku akipiga saluti mbele ya Roma mara baada ya kukanyaga juu ya Deck ya Submarine huku Maimuna akipokewa na Tanya.

Roma wakati huo alikuwa akiondoa magugu maji ambayo yalikuwa yametapakaa kwenye mwili wake huku akitema pia maji ya chumvi.

“Okey! Brewster habu tuachane na maswala ya saluti kwanza na tuondokeni hapa mpaka maji ya kimataifa”Aliongea Roma

“Yes Sir”Aliongea na kisha Roma akamgeukia Tanya.

“Tanya muangalie huyu mwanamke , ana nguvu za kijini hivyo jaribu kumlisha kitu chochote cha kumfanya apooze , usimuue kwani nina mpango wa kumhoji”Aliognea Roma na Tanya alitingisha kichwa huku akimwangalia Maimuna ambaye alikuwa amemshikilia mkononi.

Tanya alikuwa akishangazwa na urembo wa huyo mwanamke kiasi cha kumuonea wivu.

Baada ya Roma kuingia ndani kabisa ya Submarine palepale ilipiga mbizi na kuanza safari ya kuelekea maji ya kimataifa.

Roma aliekuwa ameloana alitembea mpaka ndani ya eneo la Kamandi huku nyuma akiacha hatua za miguu yake kwani alikuwa peku na Kanali Brewester alikuwa akijiandaa kutoa ripori ya misheni ilivyoenda.

“Mtukufu mfalme Pluto tumeweza kutuma kikosi namba tatu cha Ghost Fleet kama ulivyoamuru , meli nyingine ni manowari ya kinyuklia ya darala la kivirginia , Frigate mbili za daraja la Bazan na meli ya kivita ya daraja la Arleigh Burke , Boti yako ya kifahari , Erebos ipo katika maji ya kimataifa na kwa spidi yetu tutaweza kutoka katika bahari ya Tanzania ndani ya dakika therathini.

“Huwa napendelea sana kikosi chenu cha Ghost Fleet , vipi ni makombora mangapi mmerusha?”

“Jumla ni makobora arobaini ya Tomahawks”Alijibu haraka haraka

“Ni kiasi gani cha pesa kinagharimu kila kombora moja la Tomahawk?”

“Gharama ya udhalishaji ni Dolar laki sita lakini sisi tumefanikisha kununua kwa Dollar laki saba, kwanini unaulzia Mfalme?”

“Nini? Dollar laki saba ..!!”Roma alijikuta akikunja ndita kwa kuchanganyikiwa.

“Kwanini umelipua makombora yote hayo, ulipaswa kupiga na makombora ya wastani lakini wewe umetuma makombora ghali namna hio tena raundi nne , niliamini babu yako yupo vizuri kwenye mahesabu, hapo ni sawa na milioni therathini pesa za kimarekani zimepotea”

Brewster alionekana kama vile amekosewa lakini hata hivyo hakuwa na ujanja wa kupinga , ni Roma yeye mwenyewe ambaye alimwambia alipue eneo lote Mzee Sharif lakini hakuongea chochote kuhusu kuokoa hela.

Roma alijihisi uchungu hela zake zimepotea bure bure , anaweza kuwa tajiri lakini alikuwa na watu wengi wa kulisha na kulipa mishahara , hayo makombora hata hivyo hayakuwa na uwezo wa kuua jini , ni upotevu wa pesa tu ndio alivyoona.

Roma alitaka kufoka kidogo kuonyesha ubabe lakini mara baada ya kukumbuka lile kundi la majini la familia ya Mzee Sharif alijikuta akijawa na shauku kubwa ya kutaka kumhoji Maimuna.

Baada ya dakika therathini kupita sasa kikosi chote cha Ghost Fleet kiliweza kukutana sehemu moja .

Ghost fleet ilikuwa ikimaanisha sehemu ya vikosi vya the Eagles lakini ambacho kinahusika zaidi katika misheni za umbali mrefu za majini na kilijumuisha Manowari ya kijeshi maarufu kama Virginia Class Submarine , Frigate mbil(Meli mbili sindikizi) daraja la Bazan pamoja na meli ya Kivita Alreigh Burke class.

Kulikuwa na giza lakini uwepo wa botiCYatcht) kubwa ya kifahari iliokuwa imewaka yote taa za vyumba vya ndani eneo lilionekana kupendeza sana, ilikuwa ni boti ya urefu wa mita mia mbili ya rangi nyeupe ambayo ilikuwa na chata kubwa la EREBOS.

Ni boti ambayo ilikuwa ikimilikiwa na Roma na aliichukulia kama kifaa cha kuchezea tu.

Baada ya Manowari ile kujitokeza juu karibu na boti hio ya kifahari zile meli mbili sindikizi(Frigates) na mali ya kivita ya uharibifu zote zilijipanga kila upande kutengeneza Escort formation.

Ijapokuwa ilikuwa ni usiku wa giza na baridi kali lakini wanajeshi wote katika kila Deck walikuwa wamesimama wakitangulizwa na makapteni wao kikakamavu kabisa na mara baada ya Roma kutokezea wote walipiga Saluti ya kumkaribisha.

Na Roma aligeuka pande zote na kuwaonyeshea ishara ya Saluti kwa ishara ya kuwasifia kazi wanayofanya ni nzuri.

Tokea siku ambayo Roma alipotea kwenda kusikojulikana jeshi la The Eagles likiongozwa na Sauroni liliweza kupata taarifa hizo na maamuzi ya haraka yalikuwa yamefanyika ni kutuma kikosi cha Ghost Fleet karibu na mipaka ya Tanzania huku kisingizio kikubwa ni kulinda amani katika mipaka ya Somaria.

Hivyo Roma mara baada ya kutoa maelekezo ilikuwa rahisi sana kwa kikosi hicho namba tatu cha majini kusogea karibu kabisa na Tanzania ndani ya siku moja tu na kukamilisha misheni.

Roma mara baada ya kusimama juu kabisa ya ubavu wa Manowari ya kijeshi macho yake yaliangalia boti yake ya kifahari na alijikuta akishikwa na uvivu wa kutumia njia za kawaida kuingia hivyo palepale aliruka na kwenda kutua juu yake.

Ilikuwa imemgharimu Roma zaidi ya Euro milioni miane kujenga hio boti ya kifahari , boti ambayo ujenzi wake ulisimamiwa kwa siri na kampuni ya kijerumani ya BlohmVoss.

Ni kampuni ile ile ambayo ilimjengea boti ya kifahari ya Eclipse tajiri wa kirusi afahamikae kwa jina la Roman Abrahanmovic, boti ambayo iliaminika kuwa boti kubwa binafsi ya kifahari namba moja duniani , lakini ukweli ni kwamba Erebos ndio boti ya kifahari namba moja duniani na Roma hakutaka tu kuitangaza na kupiga mkwala mtu yoyote kutotoa taarifa yake ndio maana mpaka leo hii ilibakia kuwa siri.

Kutengenezwa kwa boti hio madhumuni yake ni kwa ajili misheni za majini ambazo huchukua muda mrefu , yaani ilitumika kama ngome ya majini inayotembea ndani ya jeshi la the Eagles.

Tokea siku ambayo Seventeen aliweza kuondoka akimuacha hakuwahi kuipanda tena kwani ni boti ambayo ilikuwa imejaa kumbukumbu nyingi kumuhusu.

Roma mara baada ya kutia mguu kwa mara nyingine ndani ya boti hio hatimae aliweza kuona hakuna ukinzani aliokuwa nao mwanzo.

Pengine ni kutokana na kuamini sasa Seventeen alikuwa ameenda moja kwa moja au kwasababu amekomaa kiakiri na mangojeo yake yamegeuka kuwa majonzi pekee.

END OF SEASON 22

SEOSON 23.

SEHEMU YA 667.

Tannya alimchukua Maimuna ambaye bado alikuwa hajitambui na kuingia ndae ndani ya boti hio baada ya Roma , kuhusu Brewster alitoka katika manowari na kisha akaingia kwenye meli ya kivita ya Arlreigh Burke na kuongoza njia.

Ndani ya boti watu wote walikuwa wamevaa uniform za rangi ya bluu na kati yao walikuwa ni wazungu na waafrika ambao wapo katika umri wa kati wa ujana wakionyesha sura zenye uzoefu ndani yake.

Licha ya kupendeza sana lakini muonekano wao haukuwa ukivutia, pengine ni kwasababu hawakua na sura nzuri kama ilivyo katika boti nyingine za kifaharai.

Mtu ambaye alikuwa ametangulia kusalimiana na Roma katika kumpokea alikuwa ni mpishi ambaye alikuwa ni mzungu mwenye masharubu yaliojaa mvi kutokana na uzee wake.

“Your Majesty Pluto , I am so happy to be back on the Erebos , We old guys miss you very much”Aliongea yule mpishi akimaanisha kwamba amefurahi kumuona Roma amerudi kwenye Erebos na walikuwa wamemkumbuka sana.

“Mzee Fanny unaonekana kuwa na muda mrefu sana kabla ya kukutana na Mungu , unaonekana vizuri”Aliongea Roma huku akitabasamu na kumshika bega Mzee Fanny.

Huyo Mzee alikuwa pia ni mtu wake wa karibu kama ilivyokuwa kwa Ron na hakuwa mtu wake wa karibu tu pia alikuwa ni rafiki yake Ron .

“Asante sana Mfalme Pluto , maisha ndani ya hii Yatch ni mazuri sana , ni kusafiri kwenda bandarini kununua mahitaji na kisha narudi katikati ya maji nakula maisha”Aliongea na Roma alitingisha kichwa kumwelewa na kisha akageukia wengine .

“Wewe ni Sheryl?”Aliuliza Roma akimwangalia mwanamke ambaye alionekana kuwa katika umri wa miaka kama hamsini hivi , ambaye ni mzungu pia mwenye kiini macho ambacho ni kama kimefifia sana.

“Mfalme Pluto umenisahau?”

“Umebadilika sana , umekuwa wa tofauti sana kiumbo lakini kwa bahati nzuri nimeweza kukufahamu kupitia macho yako yasiokuwa na kiini”Aliongea na kufaya watu wote kucheka na baada ya kusalimiana na baadhi ya aliokuwa akiwajua alianza kumtambulisha Tannya.

“Huyu hapa ni Tannya , kiongozi wa kundi la Yamata na atakaa na sisi ndani ya hii boi kwa siku kadhaa , Sherly mpangie chumba cha kifahari kwa ajili ya kupumzika , mwanamke ambaye ameshikilia ni mateka wangu na nadhani unajua jinsi ya kudili nae”Aliongea na Sherly alitingisha kichwa kukubali , hata hivyo haikuwa mara ya kwanza kwa mateka kuingizwa katika hio meli

Kuhusu Tannya kuwa sehemu ya kundi la Yamata wala haikuwapa mshangao mkubwa sana.

Tannya mara baada ya kuonana na watu hao ni kama alinusa harufu ya hatari kutoka kwao , watu hao aliwaona kama sio wa kawaida licha ya kwamba walionekana kuwa wafanyakazi ndani ya boti hio.

“Mpatie dawa kuhakikisha hatumii nguvu zake za kijini na kisha ndio umpatie Sheryl aendelee nae , umekuwa bize ndani ya siku hizi chache na kazi imemalizika hivyo unapaswa kumpumzika”Aliongea Roma huku akimwangalia Tanya kwa macho makavu.

“Sawa Master , je utahitaji kampani yangu usiku huu?”

Roma alikuwa ndio anajiandaa kuingia ndani kabisa ya boti hio lakini alijikuta akisimama mara baada ya kusikia swali hilo kutoka kwa Tannya.

Alishangazwa na muonekano wake kwani licha ya kuongea kauli hio hakuonyesha aibu ya aina yoyote ile na kumfanya Roma kucheka kivivu.

“Hapana , usifikirie sana kuhusu mimi”

“Sawa Master”Alijibu Tannya kwa utii huku akionyesha kidogo kutopendezwa na jibu la Roma.

Roma mwili wake ulikuwa ukinuka magugu maji tu na harufu ya bahari hivyo hakutaka kujisumbua na mambo mengine zaidi ya kutaka kujisafisha kwa wakati huo.

*****

Wakati huo huo upande wa Iringa ndani ya makazi ya Afande Kweka zilionekana gari tatu , moja ikiwa ni BMW na nyingine zote zikiwa ni Jeep.

Baada ya gari zile kuingia na kusimama mlango ulifunguliwa palepale na alionekana Afande Tozo ambaye alikuwa katika mavazi ya kijeshi , hakuwa peke yake bali alikuwa ametangulizana na wanajeshi wengine pia na alionekana kuwa na haraka sana.

Muonekano wake wakati huo ulikuwa ule wa kikauzu sana , pengine ni kutokana na sura yake , isingekuwa kile ambacho kimetokea usiku huo asingekuja kabisa ndani ya eneo hilo wakati alikuwa likizo.

Baada ya kuingia katika ukumbi wa kukutania wageni taa zilikuwa zikiwaka licha ya kuwa usiku.

Wakati huo Afande Kweka pengine angekuwa ashakwisha kulala lakini alikuwa ameamka akiwasubiri mara baada ya kupokea simu kutoka kwa Raisi Senga na Afande Tozo.

“Marshal ,,, ulikuwa ukijua kuhusu hili ambalo limetokea?”Aliuliza mara baada ya watu wote kuketi.

“Afande nadhani unanifahamu mwenyewe nimekuwa mtu ambaye nimepunguza sana kujihusisha na maswala ya kijeshi , lakini nadhani na wewe mwenyewe unamfahamu yule mtoto anavyopenda kufanya mambo kwa kujiamulia tu bila kujali athari.”

“Hivi anawaza nini mpaka kufanya vile , hii ni ishara ya kuchokoza jeshi letu la Tanzania , inawezekanaje aingie katika eneo letu kama bosi na kuanza kulipua watu na makombora kwa raundi nne , hili swala kama litasambaa jeshi letu litadharaulika sana”

“Nimefikiria sana kuhusu hili , huyu mtoto ana vitu vingi ambavyo hatuvijui , nina mashaka mataifa mengi hawajui jeshi lake la majini lipo upande gani kwa sasa , hawawezi kutambulika nadhani unaelwa mwenyewe ni jeshi ambalo linafanya kazi zake kwa siri , ninachoshauri licha ya kwamba alichofanya sio kizuri nadhani sio vyema pia kumchokoza”Aliongea na Afande Tozo na wengine wote walionekana kumwelewa.

Alitumwa hapo kufanya kikao cha dharula na wakuu wa jeshi kwa niaba ya mheshimiwa raisi Senga na kisha kurudisha tipoti , lakini ukubwa wa Roma ulikuwa ukiogopesha nchi yenyewe , sio kwamba jeshi lilikuwa likimuogopa lakini walichokuwa wakihofia ni ukichaa wa Roma katika kufanya maamuzi.

Afande Kweka licha ya kwamba Roma alikuwa mjukuu wake lakini ukweli ni kwamba alikuwa akimhofia na kujiuliza wazungu wamemfanya nini mjukuu wake mpaka kuwa na akili za kikatili, alihusika katika projekti yake lakini bado alikuwa akiangalia mienendo ya Roma ili kuona matokeo ya kile alichokifanya miaka mingi iliopita.

“Marshal mpaka sasa jeshi lipo kwenye taharuki ya kjiuliza inawezekanaje akaingiza manowari ya kijeshi ndani ya mipaka yetu bila ya kunaswa na jeshi la wanamaji kabisa , kwa kile ninachokijua hata Marekani wenyewe hawana uwezo wa kuingia katika eneo la nchi yoyote ile bila ya kugundulika”

“Nadhani hili swala kama jeshi tunapaswa kuliangalia kwa muelekeo chanya , kama hii teknolojia ambayo anatumia mataifa mengine hawana , unaonaje jeshi letu tukipiga hatua katika mazungumzo na kuweza kuipata , tunaweza kumlazimisha kupitia kosa lake ili kumfanya atupatie siri ya teknolojia yake ya kivita ?”Aliongea Afande Kweka.

Licha ya kwamba Taifa la Tanzania lilionekana kuwa dogo lakini hakuna nchi ambayo haikuwa ikitamani kuwa na jeshi lenye nguvu kuliko jeshi lingine , Afande Tozo alikuwa kwenye maswali mengi ya kujiuliza imewezekanaje Roma kuingia katika eneo lao bila ya kushitukiwa , maneno ya Afande Kweka yanamfanya kuona kabisa kama watapata teknolojia hio basi watakuwa wamepiga hatua kubwa kijeshi.

“Nadhani ni sawa kusema kwamba umeongea kitu ambacho kipo katika akili yangu , tokea juzi tulikuwa tukiangalia Roma atachukua maamuzi gani mara baada ya kuingia katika mgogoro na familia ya Mzee Sharif , nimeongea na mheshimiwa mwenyewe na tulikubaliana ni wakati sahihi wa kupunguza nguvu ya Sharif ndani ya taifa hili ndio maana hakuna hatua yoyote ambacho tuliichukua mara baada ya tukio la kule Kilimanjaro lakini hatukudhania kama angeenda mbali na kutumia makombora, kwa sasa taarifa ambazo zimetufikia familia yote ipo salama , ijapokuwa inashangaza lakini nimesikia kulikuwepo na Master walinzi wa familia yao, kama familia nzima ingeuawa wakati wa shambuliz hilo serikali ingeingia kwenye matatizo ya kidiplomasia”

“Kama wapo salama nadhani hilo ni ahueni , hili swala lazima wananchi watataka kujua nini kimetokea nadhani tunaweza kutoa taarifa kuna mazoezi ya kijeshi yaliokuwa yakifanyika huku hatua nyingine zikifuatia”

“Nadhani tutafanya hivyo , kesho nitarejea makao makuu licha ya likizo yangu haijaisha , nadhani nnitakaa na mheshimiwa na kuongea nae kuhusu hili na kuona ni kwa namna gani Roma anaweza kuadhibiwa”Aliongea , ijapokuwa Roma alikuwa na watu wa kumkingia kifua lakini lazima aadhibiwe kwa kile alichokifanya na namna ya adhabu ndio ilipaswa kujadiliwa na mkuu wa nchi.

******

Ni katika sehemu isioweza kufahamika juu ya maji ya kimataifa , ndani ya boti ya kifahari ya Erebos alionekana Maimuna akiwa ndani ya chumba kidogo ambacho kilikuwa na kitanda kimoja akiwa ameketi , alikuwa akizungusha kichwa chake kulia na kushoto akiangalia kila kitu kwa macho yaliojaa chuki.

Hakuweza kukumbuka nini kilitokea mpaka kuwa hapo kwani alichokuwa akijua ni kwamba baada ya kutokea mlipuko wa mabomu ndio muda ambao aliguswa shingoni na kupoteza fahamu.

Kwa uelewa wake na kitendo cha kuwa hapo alishaelewa kwamba familia yake ishapoteza pambano kwa mara nyingine zidi ya Roma na yeye pengine yupo hapo kama mateka.

Simu yake hakuwa nayo na hakukuwa na namna yoyote kuweza kuwasiliana na familia yake.

Alitamani kutoka nje ya chumba hicho kwa haraka lakini hakutaka kufanya hivyo kwa kukurupuka kwani alishawewza kufahamu alikuwa juu ya bahari na kwa kutumia uwezo wake wa kijini aliweza kugundua alikuwa amezungukwa na meli za kijeshi hivyo kufanya njia ya kutoroka kuwa ngumu.

Wakati akiwa anawaza cha kufanya mlango wa chumba wa chumba ulifunguliwa na mwanamke mweupe mzungu alievalia sare za ukijakazi, ni mwanamke ambaye aliweza kumkadiria umri wake kuwa katika miaka ya hamsini hivi.

“Maimuna umeamka , karibu sana ndani ya Erebos , ninafahamika kwa jina la Sherly , na nahusika na chakula chako”Aliongea yule mwanamke kwa kingereza huku akitoa tabasasamu la kikarimu .

“Hii ni sehemu ya Roma?”Aliuliza.

“Anaitwa Roma kwa jina la huko Tanzania lakini jina lake la heshima ni Mtukufu mfalme Pluto”Aliongea na kumfanya Maimuna kuvuta mdomo.

“Ndio kakuaguzia wewe kunihudumia?”Aliuliza Maimuna akiangalia kifungua kinywa ambacho hakikuwa kama cha mtu ambaye ametekwa , kilikuwa chakula cha kutia hamu ya kula.

“Usiwe na wasiwasi crew yote ndani ya hii boti hatuelewi ni kitu gani kimteokea kati yako na Mfalme Pluto ,kazi yetu ni ni kuhudumia wageni wetu , mfalme hajatupatia utambulisho wa kutosha kuhusu wewe hivyo tunakuchukulia kama mgeni wa kawaida”

Maimuna hakutaka kuamini kirahisi kwamba Roma jambazi mwenye kiburi anaweza kuwa na roho nzuri ya kuagiza vijakazi kumuhudumia , wakati aliposhituka kutoka kwenye usingizi aliweza kujua mwili wake ulikuwa na dawa ambayo ilimfanya misuli ya mwili wake kutoweza kufanya kazi na alisuburia kwa mud mpaka kurudi katika hali ya kawaida.

Ilikuwa bahati kwamba mwili wake haukuwa wa kawaida kama bindamu hivyo ilimchukua zaidi ya nusu saa kuondoa sumu ya dawa kwa mbinu za kijini katika mwili wake.

Kitendo cha kueletewa kifungua kinywa hicho ilimfanya pia kuwa na wasiwasi pengine kulikuwa na dawa ya kumlegeza hivyo hakutaka kumuamini Roma kirahisi na kula.

“Sherly ni chakula gani hicho kinachonukia ambacho umenileta?”

“Naamini utakipenda , kuna Apple pie pamoja na mvinyo uliotongenezwa na Mzee Wetu Fanny” Aliongea huku akimsogezea tray ya chakula karibu lakini kabla hata hajaelewa nini kilichotokea Maimuna alikuwa ashafanya shambulizi la kushitikiza kwa kuchukua uma na kumshika Sherly kwa nguvu shingoni staili ya Roba na kumuwekea ile Uma kwa ishara ya kutaka kumchoma nayo kwenye shingo.

“Usisogee , nitoe hapa ndani au nitatoboa koromeo lako”Aliiongea kibabe huku mapigo ya moyo wake yakidunda kwa nguvu.

Sherly licha ya kushikiliwa kwa staili hio aliishia kutoa pumzi ya masikitiko na macho yake hayakuonyesha kabisa ishara ya kupaniki.

“Miss Maimuna kwanini unafanya hivi , hii ni Erebos na huwezi kutoroka”

“Acha kuongea upuuzi wako nitoe hapa haraka , ninataka kupata simu na kumlazimisha mtu kunirudisha mpaka Tanzania”

“My Child utajutia hiki unachotaka kufanya”Aliongea Sherly na palepale alifanya shambulizi ambalo halikuwa la kawaida kwa kutumia kiwiko cha mkono na kutegua mkono wa Maimuna ulioshikilia uma,lilikuwa shambulizi la kushitukiza penngine ni kwasaabu alimchukulia Sherly ni kijakazi tu.

Maimuna wakati anavumilia maumivu ilikuwa ni kosa kwake kwani alishindwa kushituka kwa muda na palepale alipigwa teke la Shingo kwa namna ya kipekee sana na kurudishwa chini.

Sherly mwili wake wa kibonge ni kama umegeuka bomu au roboti la kivita ndani ya dakika chache tu na mguu wake ulikuwa na nguvu mno kiasi ambacho Maimuna alishindwa kabisa kufurukuta.

“Unapaswa kujua wafanyakazi wote tuliopo ndani ya Erebos ni maveteran wastaafu kutoka kundi la kininja la ZERO , ijapokuwa tunaonekana kama wazee lakini ni rahisi kwetu kudili na mtu kama wewe”

“Wewe ni ninjaa..”Maimuna alijikuta akipoteza sauti yake kwa hofuna mshangao.

“Siku zetu za kuwa maninja zilishaisha , mimi kwasasa ni kijakazi ndani ya hii boti tu”

Dakika ileile aliweza kutokezea mwanamke ambaye amevalia mavazi ya kitamaduni ya kijapani maarufu kama Kimmono na kufanya umbo lake lililotukuka kuzidi kujichoresha na kumfanya kuwa na mvuto wa aina yake.

“Unajiona ni nani kuweza kutoroka kutoka hapa tulipo , kila unaemuona hapa ndani ana mafunzo ya hatari ya uninja na hata kama una nguvu za kijini ni ngumu kwako kutuzidi?”

Tannya siku ya jana yake usiku wakati anafika alishajua watu ndani ya boti hio hawakuwa wa kawaida ndio maana alinusa hatari , yeye ni ninja hivyo aliweza kugundua maninja wenzake licha ya kwamba walionekana kuwa kawaida kabisa.

“Kuna msemo mmoja wa Kijapani ambao unakufaaa unaosema kwamba wakati ukiwa kwenye sintofahamu ukiwa katika njia panda ni kheri kuchagua njia ngumu kuliko rahisi”Baada ya kuongea vile palepale alichuchumaa na kisha alimshika Maimuna kwa nguvu na kumnyanyua na kisha alimtoa ndani ya chumba hicho.

Sherly mara baada ya kuona mrembo huyo anatolewa aliishia kumwangalia kwa majonzi na kutigisha kichwa chake kwa masikitiko.

Nje kabisa juu ya boti alionekana Roma ambaye alikuwa ameshikilia simu kubwa ambayo ni ya Mzee Fanny , na alikuwa akijaribu kuwasiliana na Benadetha ili kutaka kumtoa hofu.

Kwasababu mtandao haukuwa vizuri kwenye hilo eneo aliamua kutuma ujumbe wa meseji.

“Ana tatizo gani huyo?”Aliuliza Roma mara baada ya Maimuna kufikishwa juu akiwa ameshikwa kibabe na Tannya.

“Alitaka kumtumia Sherly kama mateka ili kuroroka”

Roma mara baada ya kusikia kauli hio alikuwa katika hasira lakini hakutaka kuifanya imvae , alikuwa amekimbilia kwenye maji ya kimataifa ili kuepuka familia ya Mzee Sharif kutuma majini kuja kumshambulia.

Hakuwa pia na mpango wa kurudi mapema kutokana na kwamba alikuwa hana uwezo wa kutumia nguvu za kijini kwa wakati huo, sasa alikasirika baada ya kusikia huyo mateka kwake anataka kutoroka ili hali alikuwa amepoteza hela nyingi mpaka kumfikisha hapo.

“Kwanini familia yenu ghafla tu mlibadilika na wote kuungana kutaka mimi nikuoe , unapaswa kunijibu kwa utii kwani sipo katika mudi nzuri ya kukubembeleza”Aliuliza Roma.

“Yaani unajisifia kabisa haupo kwenye mudi nzuri , unadhani mimi nipo kwenye mudi nzuri eh, Roma hivi wewe ni mwanaume wa aina gani kumshambulia mwanamke , hivi unajiona ni mwenye haki kumchukua mwanamke kama mateka , huna lolote wewe ni ukatili tu uliokujaa na nataka nikuambie hivi kama utaniua Mzee Nguluma na mke wake watazikwa na mimi”Aliongea Maimuna kwa kijeuri na kumfanya Roma kuona huyu mwanamke kweli ni jeuri maana licha ya kwamba yupo kwenye hali ya hatari lakini bado tu alikuwa akiongea kiburi.

Roma alipiga hatua na palepale alimshika kwa nguvu Maimuna na kumzungusha kwa spidi na kufanya ageuke kichwa chini miguu juu, Maimuna alijitahidi kumshambulia Roma miguuni lakini ngumi zake ni kama zilikuwa zikimtekenya tu.

Roma hakutaka hata kumchcelewesha kwani palepale alimpiga kigoti cha mbavu na Maimuna alijikuta akitoa kilio kikali cha maumivu baada ya mbavu zake kuvunjwa kikatili.

Tokea alivyokuwa mdogo alikuwa ni kama malkia ambaye muda wote atahudumiwa kwa kila hitajio lake na hakuwahi kuyahisi maumivu makali kama hayo.

“Roma wewe ni shetani…”Aliongea na palepale alijipinda akitaka kung’ata mguu wa Roma .

“Chochote unachosema ,,”Aliogea Roma na palepale alisogea mbele kwenye boti hio akimburuza kama vile ameshikilia kuku na alitoa ishara ya kupatiwa kamba na mara ileile alifunguwa fungwa kiunoni na kutupiwa majini.

Kilichomkuta baba yake Rose mzee Situ ndio alichokuwa akifanyiwa Maimuna kwa wakati huo.

“Roma unafanya nini?”Alipiga ukulele mara baada ya kutua majini , ijapokuwa alikuwa na nguvu za kijini lakini ubaridi aliokuwa akiusikia haukuwa wa kawaida kabisa.

“Nafanya kile unachokiona , wewe ni mateka halafu bado mjeuri hivyo ili twende sawa lazima kwanza nikutoe ujeuri ndio tuendelee na mazungumzo, muda si mrefu utatembelewa na wafalme wa bahari”Aliongea Roma.

Wafalme wa bahari? Maimuna hakuwa mjinga , mguu wake ulikuwa ukivuja damu ambayo ilikuwa ikisambaa ndani ya maji kiasi ambacho kilimfanya kupata hisia zisizokuwa za kawaida.

“Kuna papa ndani ya hili eneo”Alijikuta akipiga ukulele wa mshituko mara baada ya akili yake kuweza kuhisi hatari.

“Muangalieni , kama akitaka kurudi juu lazima akubali kujibu maswali niliomuuliza na aahidi kunisujudia kutokana na makosa yake , vinginevyo kila akipanda mrudisheni chini”Aliongea Roma.

“Yes Master”Alijibu Tannya kwa utii na Roma hakutaka kujali tena kitakachoendelea zaidi ya kurudi ndani kwani alikuwa hajapata kifungua kinywa na njaa ilikuwa ikimuuuma , isitoshe pia alikuwa na hamu ya kula chakula kilichoandaliwa na Mzee Fanny.

Maimuna alikuwa akipanda na na kushikilia kamba iliomfunga ili asiweze kutumbukia majini, licha ya kuhisi kuna hali kubwa ya hatari ambayo ingemtokea lakini alijiambia ni kheri kufa kuliko kumsujudia Roma.

“Wewe na mimi sote ni wanawake , kwanini unataka kufanya kazi chini ya huyo shetani , anakutumia tu ili kumsaidia na mwisho wa siku atakuacha”Aliongea Maimuna akimwangalia Tannya kwa macho ya kumshawishi.

Licha ya maneno yake , Tannya muonekano wake haukuwa umebadilika kabisa, ni kama hajamuelewa Maimuna kile ambacho anataka kuongea na alikuwa na hasira nae pengine wivu pia wa kuwa mrembo zaidi kuliko yeye ilimfanya kutaka kumuua na alijiambia isingekuwa Roma basi muda huo asingekuwa hai.

Maimuna kumwangalia Tannya tu alijua kabisa mwanamke huyo hashawishiki na aliona ni muda muafaka wa kutafuta njia mbadala ya kuweza kujiokoa, lakini kabla hata hajaiona njia yenyewe hatimae aliweza kuona papa wa rangi ya bluu akisogea karibu na alipo.

SEHEMU YA 662.

Papa wanafahamika kwa uwezo wao wa kunusa harufu ya damu hata kwa umbali mrefu na hicho ndio kilichowasogeza hapo kwani Maimuna alikuwa akivuja damu ambayo ilikuwa ikidondokea majini.

Kutokana na uwezo wake wa nguvu za kijini alikuwa na uwezo wa kuhimili kushindana nao lakini ingekuwa ni swala la muda mpaka kukosa nguvu.

Mapigo yake ya moyo yalikuwa yakidunda mno baada ya kuona papa mkubwa akimsogelea kwa spidi , alijikuta kwa haraka sana akishikilia ile kamba na kujaribu kupanda kidogo kuelekea juu.

Yule Papa alionekana kuwa na njaa kali mno kwani mara baada ya kufikia tu alitokezea kichwa chake juu juu huku akipanua mdomo wake na kufanya ulimi wake usiokuwa wa kawaida kuonekana.

Maimuna hakutaka kuruhusu kushambuliwa kizembe kwani mara baada ya Papa yule kumsogelea palepale alimpiga kwa nguvu kwenye eneo la usoni na kumfanya Papa yule kuhisi mauminu na kurudi ndani ya maji.

Nywele zake zilikuwa kitimtimu na alijikuta akianza kutokwa na machozi kutokana na udhalilishaji huo anaofanyiwa.

Haikuchukua muda mrefu Papa wengi zaidi waliongezeka huku kila mmoja akianza kumrukia kutaka kumrarua.,

Kila aliekuwa akimkaribia alijitahidi kukwepa huku akishambulia kwa nguvu lakini kutokana na wingi wao na spidi ya kumshambulia alianza kuchoka kwa haraka mno.

Baada ya kuona hakuwa na namna tena ya kujiokoa kitu pekee ni kujaribu kutumia uwezo wake kupandisha juu lakini Tannya alikuwa akilinda kwani alipomkaribia tu alimrudisha chini kwa teke la tumboni na aliishia kupiga yowe la maumivu lakini hata hivyo hakutaka kudumbikia majini kwani ingekuwa mwisho wake hivyo aliweza kujizuia njiani.

“Uwezo wako ni mzuri lakini kadri unavyopambana ndio unazidi kujichosha”Aliongea Tannya lakini Maimuna alionyesha ujeuri.

Dakika chache tu alijikuta akikosa kabisa pumzi na aliona akileta mchezo angekufa na palepale aliamua kusalimu amri.

“Nipo tayari , nipo tayari , nitaongea?”Aliongea kwa nguvu kwa sauti yake ya kike na kumfanya Tannya kutoa tabasamu la kijeuri huku akimwangalia namna ambavyo mrembo huyo alivyojeruhiwa mkononi na papa na kufanya damu kutoka zaidi na zaidi.

Baada ya dakikka kumi na tano Roma alirudi na kumkuta Maimuna akiwa na adabu amepiga magoti chini huku akilia kilio cha kwikwi.

“Vipi upo tayari sasa kuongea?”Aliuliza na Maimuna bado alikuwa ameiinamisha kichwa chake chini , hakuamini kwenye maisha yake angekuja kupitia maisha ya aina hio , alikuwa akijiamini siku zote kutokana na kuwa na uwezo usiokuwa wa kawaida lakini mara baada ya kukutana na Roma ule ujeuri na hali ya kujiamini yote imepotea.

“Master anauliza , toa majibu?”Aliongea Tannya na palepale alimpiga teke na kumfanya kudondoka chini na kuishia kuugulia maumivu huku aking’ata meno yake kwa hasira.

“Si familia yako ilikuwa ikiniambia nisujudie sijui na kurudisha hazina, sasa leo kwa niaba ya familia yako nataka uonje dawa yake , nitahesabu mpaka tatu kama hutoongea nitakurudisha majjini uliwe na Papa”

“Moja … mbili..”Alihesabu Roma.

“Hapana nitaongea..”Aliongea Maimuna na kwa haraka sana alikwenda kupiga magoti mbele ya Roma.

“Naomba unisamehe ,,, nimekosea, nisemehe”Aliongea akiwa katika hali ya kuomba , ile hali ya kujikomba yote ilikuwa imeisha na sasa kilichokuwa kimebakia ni woga.

“Hivi unajua kosa lako kwanza?”Aliuliza Roma huku akichuchumaa na kushika kidevu chake na kukinyanyua juu na kumwangalia kwa macho makavu.

“Kosa letu hatukupaswa kukudanganya”

“Nadhani bado hujanielewa na unataka kurudi majini, hivi kwanza unajua tofauti ya Papa na samaki wengine?”Aliuliza na kumfanya Maimiuna kitingisha kichwa kwamba hajui,

“Papa hawana Swimming Blader , Papa tokea wanazaliwa maisha yao ni kwenye kupambana ili kuendelea kuishi , lazima wachezeshe mikia yao ili mradi tu wasije wakazama chini kabisa majini , kitendo cha kupigania maisha yao na kuwa wafalme wa bahari ni kama mimi, ili niishi lazima nipambane mwenyewe na sio kama nyie ambao mnategemea nguvu flani iliojificha ili kuendeleza ubabe wenu , uwezo wenu sio binafsi bali ni msaada mnaopata na hilo tu linawakosesha sifa ya kupambana na mtu kama mimi…”

“Niambie kwanini ghafla tu ukataka mimi nikuoe , sababu ni nini?”Aliuliza Roma huku akiwa katika hali ya ukauzu.

“Ni presha kutoka kwa Master namba moja?”Aliongea Maimuna na kumfanya Roma kushangaa.

“Master namba moja unamaanisha nini?”

“Mimi mwenyewe sijui maelekezo yote lakini kwa uchache ninachojua ni kwamba Master namba moja ndio mkuu wa muungano wa majini na ndio muwakilishi wa majini katika ulimwengu wa kawaida , baada ya mgogoro kutokea kati ya familia yetu na wewe , maelekezo ambayo familia yetu ilipokea ili kudumisha amani ni wewe kunioa , maana yake ni kwamba tukifunganisha familia zetu kupitia ndoa basi swala la Hazina itakuwa rahisi kulimaliza bila mikwaruzano”Roma alishawahi kusikia kwa uchache sana kuhusu muunganiko wa majini lakini hakuwa na taarifa za kutosha.

“Huyo Master Namba moja ni nani haswa , je ni jini au ni binadamu mwenye uwezo wa kijini?”Aliuliza Roma akiwa na shauku.

“Sijui ni nani lakini ninachoweza kusema ni kwamba nasikia ni binadamu wa kawaida tu lakini ambaye analindwa na nguvu kubwa ya kijini ambayo hata chanzo chake bado haijawahi kufahamika, nguvu yake ni kubwa kiasi kwamba kila mmoja anamheshimu, nadhani umeuona wale Master wa ukoo wetu , wale ni majini na kuwepo katika ulimwengu wa kawaida ni ruhusa maalumu ilioweza kutoka kwa Master Namba moja”Aliongea.

Roma alishangaa kidogo lakini hata hivyo aliona swala hilo lina mantiki, ilikuwa ni uvunjaji wa sheria kwa majini kuingia kutoka katika ulimwengu wa kawaida na kuanza kumshambulia ile jana.

Roma mara baada ya kumsikiliza Maimuna na kuona hakuwa akidanganya aliona haina haja ya kujua sana kuhusu hizo habari maana aliona ni kama hazimuhusu , lakini hata hivyo alijiamia popopote pale huyo Master namba moja lazima siku moja atakutana nae na atahakikisha anaijua hio nguvu yake na kama ni jini lazima wapigane.

“Kwasasa upo kwenye mikono yangu, hivyo iambie familia yako kumwachia Mzee nguluma na mke wake na nitakurudisha”Aliongea Roma na Maimuna macho yake yalichanua , hata hivyo hakutaka kuendelea kubakia hapo hata kwa sekunde moja.

“Ukinipatia namna ya kuwasiliana nao nitawaambia”Aliongea na Tannya palepale alitoa simu moja yenye mkonga , ilikuwa ni simu ambayo imetengenezwa na Clark maalumu kwa kuwasiliana hata kwenye mazingira ambayo hayana mtandao na haikuwa ikitumia laini ya mtandao wowote teknolojia ambayo inaifanya hata kama mtu ajaribu kutaka kufatilia mwelekeo wake kushindwa kuitrack.

******

Ni katika fuke ya Bagamoyo ndio makazi ya muda ambayo yalikuwa chini ya familia ya Mzee Sharif mara baada ya eneo la kule Kigamboni kuharibiwa.

Mida huo wa asubuhi watu wakubwa wa familia hio walikuwa wamekusanyika, wakiwemo watu wa dini ambao wanasalia miungu ya Sharif.

Jini Iftri , Jini Marid , Jini Ghula na Jini Imrah wote walikuwepo wakiimalisha ulinzi, huku jumba hilo la kifahari likiwa limezingirwa na walinzi ambao walikuwa wameshikilia siraha kali.

Familia hio ilikuwa katika hali ya tahadhari kutokana na ugomvo wao walioibua na Roma.

Watu wa familia hio pamoja na waumini walikuwa wamekusanyika sehemu moja wakiwa katika mazungumzo makali , hofu zidi ya Roma ilikuwa juu , kitendo cha kuweza kuingiza jeshi lake ndani ya mipaka ya Tanzania na kuwashambulia na makombora halikuwa la kawaida kabisa na pnegine kama sio uwepo wa walinzi wa kijini basi familia yote ingeweza kufa palepale.

Kikao hiko kilikuwa kikizungumzia namna ya kumpata Maimuna ambaye ametekwa na Roma na Hazina yao, kilikuwa ni kikao cha dharula kutokana na uzito wake kwani Maimuna alikuwa ni mrirhi ambaye kitamaduni amekubaliwa na miungu wao kuwa mrithi mkuu wa failia yote na kiongozi wa kidini na Hazina yao ndio msingi wa mkuu wa imani yao.

“Roma mpaka sasa hajulikani alipo na hakuna ambaye yupo salama mpaka sasa na muda ambao Master wetu wamepewa kubakia katika dunia unakaribia kuisha, hii ni hatari kwani hatujui anapanga nini?”Aliongea bwana mmoja mwenye masharubu .

“Sidhani atakuwa na ujasiri wa kurudi na kutushambulia tena , Master wetu wanaweza kurudi katika ulimwengu usioonekana lakini anajua fika inachukua muda mchache sana mpaka wao kujitokeza, mpango kwasasa ni kuhakikisha Roma akirudi anaadhibiwa kisheria”

“Uwezekano wa kuadhibitiwa kisheria ni mdogo sana , jeshi la Tanzania ni kama linamuhofia na isitoshe wote tunaelewa Mheshimiwa Senga ni baba yake”

“Kwa matazamo wangu sidhani kama hilo ni swala la kuogopa , Raisi Senga anaweza kuwa na nguvu lakini wote hapa tunajua kwamba ni mwanachama wa Freemason na anapokea maagizo kutoka kwa Namba moja, ijapokuwa Namba moja haridhishwi sana na matendo yetu ya kusalia miungu wetu lakini bado sisi ni washirika hivyo hatuna haja ya kuogopa lazima tutumie ushawishi wetu kuhakikisha anakamatwa na kuwajibishwa”

“Mimi nadhani ili Maimuna kurudi akiwa salama lakini pia kupata hazina yetu tuanze na familia yake kwanza , twende tukakamamate kila mwanafamilia na kisha tutatumia kama udhaifu wa kuhakikisha anarudisha hazina yetu pamoja na Maimuna , Mzee nguluma inaonekana hamchukulii kwa uzito wake, nashauri tuanze na binti yake Lanlan”

“Umekuwa mjinga ,,,”Alifoka bwana mmoja..

“Nadhani mnajua kwamba ni kwa kipindi kirefu serikali imekuwa ikituvumilia na imetuonya kutofanya kitu chochote cha ajabu kutaka kudhuru mwanafamilia , unataka twende mbali na kumteka binti yake , huoni kwamba hili litaleta ukinzani mkubwa”

“Upo sahihi, nadhani ni vizuri kutogusa familia yake , nadhani tutumie nguvu ya ushawishi wetu kwa washirika wetu wa siri ili kuhakikisha serikali inamchukulia hatua kwa kile alichokifanya , hili litasaidia zaidi na kumshika miguu ..”

Kila mmoja alichangia kwa namna alivyokuwa akitaka huku Mzee Sharif ambaye alikuwa akuhudumu kama kiongozi muda wote alikuwa kimya akisikiliza michango ya pande zote.

“Boss kuna simu imefika , Maimuna anataka kuongea na wewe”Aliongea kingozi mkuu wa ulinzi mara baada ya kuingia katika eneo la kikao na kumsogelea Mzee sharif.,

“:Maimuna…!!”Aliongea kwa sauti na kufanya kila mmoja aliekuwa amesikia kauli hio kutaka kujua anataka kuongea nini.

“Fanyeni haraka kuitrack hii simu inapigwa kutoka wapi”Aliongea Bahe na palepale taratibbu za haraka zilifanyika kuweza kunasa eneo ambalo simu hio ilikuwa ikipigwa.

Baada ya taratibu za awali kukamilika palepale Mzee Sharif alipewa ishara ya kupokea.

“Maimuna ni wewe , unaongea na babu yako hapa”

“Babu nipo juu ya boti ya Roma sasa hivi , amesema kama tutamuachia Mzee Nguluma na mke wake kuwa huru basi atanirudisha”

“Oh…”Mzee alikunja ndita huku akiangalia jopo la watu ambalo linamwangalia.

“Mai,, hebu subiri kwasasa nipo nafanya kikao na wajomba zako na tutashauriana ni kipi cha kufanya”Aliongea na upande wa pili mara baada ya Maimuna kusikia kauli hio moyo wake ulisinyaa kutokana na wasiwasi na kukosa msaada.

“Roma ni kijana muhuni sana , jana tulimualika vizuri kwa ajili ya mazungumzo lakini kumbe tayari ashatega mabomu na kuandaa makombora na kutufanya tuingie mtegoni , hatuwezi kumwamini kwa kile anachoongea”Aliongea Imrah na maneno yake yaliungwa mkono na kila mmoj.

“Baba mchango wa Maimuna katika ukoo wetu sio wa kupuuzwa kabisa , amefanya utajiri wetu kuongezeka kwa kiasi kikubwa sana na sio hivyo tu ameweza kupanua biashara zetu”Aliongea baba yake Maimuna akiwa ndio aliekuwa na wasiwasi zaidi kuliko wote.

“Tunajua kwamba unawasiwasi kwasababu ni mtoto wako lakini kwasasa tunaangalia hili swala kwa mapana yake , kwasasa kitu pekee ambacho tunacho zidi ya Roma ni Mzee nguluma na mke wake , lakini vipi kama tukimwachia yule hashindwi kulipiza kiasi kwa siri”Waliongea wote kwa kuchangia na kila mtu alionyesha hakuna ambaye yupo tayari kumruhusu Mzee Nguluma kuwa huru.

“Maimuna ,,, naomba unisamehe mimi babbu yako m sio kwamba sitaki kukuokoa..”Aliongea Mzee Sharif baada kurudisha jibu kwendakwa Maimuna baada ya simu kuunganishwa,

“Nimekuelewa babu ,, huna haja ya kuongea, kwasasa nipo sawa naamini babu utakuja kuniokoa”Aliongea huku sauti yake ikionyesha kabisa alikuwa akilia na palepale simu ilikatwa.

“Vipi umeweza kupata simu inatokea eneo gani?”Aliuliza Mzee Sharif huku akiwaangalia watalamu wa mitando kwakihangaika,

“Boss teknolojia ya simu iliotumika kuwasilina na sisi ni kubwa mno , na tumeshindwa kupata uelekeo mahususi kabisa ,, tulichoweza kugundua ni kwamba simu hii inatokea upande wa mashariki katika bahari ya hindi , mathalani itakuwa ni kwenye maji ya kimataifa”

“Maji ya kimataifa , hapo unamaanisha bahari yote ya hindi ujue, unatania au?”Aliongea baba yake Maimuna kwa hasira.

“Kama ni upande wa mashariki wa bahari kutoka hapa basi inatosha kabisa kumpata , sisi tutaenda kumtufuta huyu mnyama na kumuua huko huko”

“Master Ghula kama mtaenda huko mbali ni kukiuka sheria za kimataifa za gods treaty”

“Nani anajali , si huyo mshenzi wanamuita Mfalme Pluto lakini nini atatufanya , hao miungu unaozungumzia ni kikundi cha watu wanaolazimisha umaarufu tu hawatuwezi kwa lolote sisi majini , kama kuna mwenye nguvu kati yao sisi wote wa tatu tutamshambulia mpaka kumuua na kisha tutakimbia”Waliongea wale majini wakijigamba hawakutaka kuonekana dhaifu mbele ya binadamu wa kawaida.

Muda uleule Jini Ghula aliwapa ishara jini Iftir na Maridi na wote walipoetea kwenye viti vyao kwenda kumfuata Roma.
 
NILIMDHANIA KAHABA KUMBE BIKRA

MTUNZI: SINGANOJR

WATSAPP: 0687151346

Mono no aware

SEHEMU YA 663

Roma masikio yake yalikuwa na uwezo wa kusikia kwa wepesi mno na aliweza kusikia kile ambacho Mzee Sharif aliongea.

Mzee Sharif hakutaka kabisa kumuokoa mjukuu wake ili mradi tu aendelee kuwashikiria Mzee Nguluma na mke wake , ilimkasirisha sana Roma.

“Wewe mwanamke umezaliwa nje ya ndoa nini? , si nimesikia wewe ndio mrithi wa familia kwanini hawataki kukurudisha?”Aliuliza Roma akiwa amekasirika.

Maimuna alikuwa ameinamisha kichwa chake chini akishindwa kujua namna ya kujibu , pengine hata yeye alikuwa kwenye majonzi , muda ule ule damu puani zilianza kumtoka mfululizo.

Hakuwa hata akijua ni kipi anajisikia kwa muda huo , alijihisi kama vile ametelekezwa , mwanzoni alijua babu yake angefanya chochote kile kumuokoa lakini alichosikia kilimnyong’onyesha.

Namna ambavyo familia yake ilivyokuwa ikimdekeza na kumpenda kwake muda huo aliona ni kama udanganyifu tu , nywele zake ambazo zilikuwa zimeloa ziliishia kufunika uso wake huku machozi na damu puani vikimtoka kwa wakati mmoja, kadri alivyokuwa akijihisi uchungu ndio ambavyo alizidi kubadilika na ule urembo wake kupotea na ilichukua sekunde chache tu kucha za mikono yake zilikuwa zimerefuka huku macho yakibadilika kabisa na kuwa nusu jini.

Hasira zilikuwa kubwa mno kiasi kwamba alianza kutetemeka na palepale alimrukia Roma kama paka akitaka kumng’ata na kumrarua na kucha jambo ambalo lilimshangaza Roma.

“Ushageuka kichaa sio?”Aliuliza Roma huku akikunja sura yake , ingekuwa ni binadamu ambaye hajazoea kuona binadamu akibadilika basi angezimia lakini kwa Roma ilikuwa kawaida sana.

Maimuna ile anataka kumkaribia Roma alipokea kichapo kwenye paji la uso na kumfanya kudondoka kurudi nyuma kwenye sakafu ya meli hio ambayo ilikuwa na ubaridi usiokuwa wa kawaida.

Tannya hata yeye hakushangaa sana mabadiliko ya Maimuna ya kuwa nusu jini , pengine ashawahi kuona mabadiliko hayo kwa binadamu na aliishia kuongea kijapani akimaanisha mwanamke muoga.

Ijapokuwa Maimuna hakuwa akikijua kijapani lakini alijua neno lililotoka mdomoni mwa Tannya ni la kumdharau lakini hata hivyo hakuwa na cha kumfanya.

Alikuwa amepoteza utu wake , upendo wa familia yake , uhuru wake na aliona hakuna kitu kingine ambacho kimebakia kwenye ulimwengu huu kwa ajili yake, alijutia kuingia katika mikono ya Roma na alijiambia laiti angejua asingejihusisha kabisa.

Roma hakutaka sana kujali hali ya kutia huruma ya Maimiuna na namna ambavyo alibadilika zaidi ya kuinua simu yake na kuweka sikioni.

“Makedon umemaliza kazi yako?”

“Mfalme Pluto ijapokuwa mimi sio kijana tena lakini haimaanishi kwamba ufanisi wangu umeshuka , kazi imemalizika muda mrefu uliopita”

“Vizuri sana , tuma hivyo vitu ulivyopata kwa familia yao kwa haraka , nadhani unajua ninachomaanisha”

“Hehe , umeeleweka Mfalme … Brewester yuko sawa?”

“Yeah m Brewester anafanya kazi nzuri ya kuaminika”

“Kama ni hivyo Mfalme Pluto nadhani nikuache , naomba umfunze kadri uwezavyo kama atafanya makosa”

Roma alijua nini ambacho Makedon anamaanisha kwani baada ya mzee huyo kustaafu kutoka katika shirika la kijajusi la Mossad alikuwa ndio kamanda wa Ghost Fleets hivyo hofu yake ni kwamba kazi ambayo amerithi Brewester inaweza kuwa kubwa sana kwake.

“Mrudisheni ndani na hakikisheni anaendelea kuishi , sitaki kuendelea kumuona hapa maana ananniharibia mudi tu”Aliongea Roma.

Tannya aliona ilikuwa ni afadhali kumrushia majini ili kuwa chakula cha papa lakini aliishia kumbeba Maimuna na kumrudisha ndani.

Upande wa Roma alijua tu haitochukua muda mrefu mpaka familia ya Sharif kumpigia , hivyo alitafuta kiti na kuita muhudumu kumletea mvinyo juu ya Deck na kukunja nne akifurahia upepo.

Lakiini sasa ile anapiga pafu moja ya mvinyo uliotongenezwa na Mzee Fanny palepale mkandamizo wa hewa ulizidi kuongezeka na kufanya nywele zake kusimama kutokana na kuhisi hatari na ilikuwa ni kufumba na kufumbua vivuli vya watu watatu viliweza kuonekana vikimsogelea.

Roma alijikuta akisimama haraka kwa mshangao na kujiambia alikuwa amewadharau hao majini kwani hakutegemea kama wangeweza kuja mpaka hapo.

Wale majini watatu kutoka familia ya Mzee Sharif walimwangalia Roma kwa kejeli.

“Ulidhani umekimbia umbali mrefu wewe mshenzi mpaka kujiona una amani?”

Roma mikono yake ilianza kuloa jasho baada ya kuangalia macho yao ambayo yalikuwa na ule ukatili wa hali ya juu , ilionekana dhahiri kabisa wapo hapo kwa ajili ya kumuua tu.

“Hamjui kwamba kuja mpaka hapa mmekiuka sheria za miungu?”

“Miungu ndio upuuzi gani , yaani hao wapuuzi wenzako wanaofosi umaarufu sisi tuwaogope, wewe ni kijimnyama mdogo tu ambaye nakwenda kukuchinja na upanga wangu leo hii”Aliongea Jini Ghula na palepale mikono yake ilipiga mwanga wa flash na kufumba na kufumbua alikuwa na upanga mrefu unaowaka waka ukatao kuwili.

“Senior Ghula , Maimuna yupo kwenye mikono yake bado”Aliongea Marid kwa tahadhari.

“Ni binadamu mwenye damu yetu na hana thamani kubwa sana , kama atakuwa anaishi baada ya kuharibu hii meli basi itakuwa ni bahati yake”

Ijapokuwa kauli yake iliwafanya Jinni Iftir na Maridi kuona ni ya kikatili lakini walijua Ghula alikuwa na hasira sana zidi ya Roma hivyo asingeweza kumuacha kisa ya Maimuna kutokana na udhalilishaji aliofanyiwa siku ya jana.

Upande wa Maimuna uwezo wake wa kijini ulikuwa mkubwa mno kiasi cha kufanya wasiwe na wasiwasi juu yake , alikuwa kwenye levo ya mwanzo wa nafsi hivyo anaweza kuwa na asilimia hamsini za kupona kama tu wataweza kuharibu hio meli.

Muda huo huo Tannya na yeye alikuja kutokea kama kivuli juu ya Deck na haikuchukua muda wanawake maninja wawiwili waliokuwa wamevalia mavazi meusi walitokeza

“Mfalme Pluto , je unataka tuwaue kwa kutumia makombora?”Aliuliza Sherly.

“Haitokuwa na maana , waambieni kila mtu kukaa ndani na wasitoke nje”Aliongea Roma kwa tahadhari.

Roma kwa wakati huo aliona kupambana nao itakuwa ni kazi kubwa kwani hawakuwa na mtu wa kumlinda kama kilichotokea siku ya jana yake na hata kama wakitumia makombora hayatokuwa na msaada..

“Unseal”Aliongea akiita nguvu ya kanuni ya anga.

Roma hakutaka kutumia nguvu yake ya kijini hivyo kitu peke ambacho aliona angetumia kwa wakati huo ni uwezo wake wa akili katika kutambua kanuni za anga na kuzitumia kushambulia.

“Naona unataka kuleta ukinzani , sio mbaya ngoja tuone ni muda gani utatumia kushindana na sisi”Aliongea Ghula na palepale aliwapa ishara Iftir na Maridi kusogea mbali.

Alimnyooshea Roma upanga wake ambao ulianza kukusanya maji ya kiroho yenye nguvu ya kumyeyusha Roma .

Ijapokuwa ilikuwa ni juu ya bahari lakini bado kulikuwa na uwezekano wa kutumia elemeti za mbingu na ardhi kutengeneza mashambulizi.

Upepo ulianza kuongezeka kiasi kwamba hata mawimbi na yenyewe yalianza kuwa makubwa na kuanza kuyumbisha boti na meli zile za kivita. Na Roma mara baada ya kuona kuna uwezekano wa kuharibika kwa vifaa vyake vya kivita pamoja na boti yake palepale alitengeneza Paraller Spaces katika mistari minne na kufanya zile boti na zile meli za kivita kusukumwa umbali mrefu kutoka alipokuwa amesimama.

Juu ya bahari hio ambayo ilikuwa ya bluu tupu kilichokuwa kikionekana ni kama filamu ya kufikirika ya SC-FI kwani kufumba na kufumbua Roma alifanya Space Folding na kumfanya kuteleport kutoka alipokuwa amesimama na kwenda mbele zaidi huku wimbi kubwa la maji likiamka lenye ukubwa wa kufunika meli.

Roma sasa baada ya kuridhika aliona kabisa hata kama majini hayo yatatumia uwezo wao wote kushambulia meli zake haziwezi kuathirika kwani amezitengenezea anga maalumu ambayo ilikuwa ikikipunguza kasi ya mawimbi ya maji.

“Unasikitisha sana , watu wako hawazezi kurotoka hapa na utakufa nao tu”Aliongea Jini Ghula maara baada ya kuona Roma ni kama anafanya kazi isiokuwa na maana.

“Chukua hii”Aliongea na palepale alipigisha upanga wake hewani kwa namna ya kufyeka na ulituma wimbi kubwa la nguvu ya kijini ambayo ilienda moja kwa moja sehemu ambayo Roma amesimama.

Roma mara baada ya kuona shambulizi lile kwa haraka sana alitengeneza Paraller Space zaidi ya ishirini na kuzipindisha ili kutengua shambulizi lile lisimfikie , ilikuwa ni kama alikuwa akitengeneza ngao lakini hata hivyo shambulizi la nguvu ya kijini lilikuwa na nguvu kiasi kwamba anga msambo yote aliotengeneza iliharibiwa.

Huyu alikua ni jini ambaye yupo levo ya Kuipita Dhiki katika kutawala elementi za maji hivyo alikuwa na nguvu isiokuwa ya kawaida

Roma alikwepa shambulizi lile na kwa haraka sana alipotea aliposimama na ile anaibuka alikuwa mbele ya Jini Ghula ambalo lishabadilika muoenkano wake na kuwa nusu jinni nusu binadamu.

Roma ijapokuwa alijua ijapokuwa majini wana nguvu kubwa ya kijini lakini miili yao ni dhaifu kuliko yeye hivyo kama atawashambulia kwa kulenga moyo basi ni rahisi kuwashinda.

“Acha kuota”Aliongea jini Ghula akiwa tayari ashajua mpango wa Roma na alitengeneza ngao ya kijini na wakati huo huo ni kama kivuli cha mtu kilikuwa kikimtoka kwenye mwili wake na kumsogelea Roma kwa kasi.

Roma alijihisi kanuni zake za anga zilikuwa hazina nguvu kabisa , ijapokuwa alikuwa ni kama ameingia mtegoni kwani alihihisi ni kama kuna kitu kimemshikilia ambacho kilimfanya kushindwa kusogea nyuma au kwenda mbele.

“Hivi unafikiri kwa kutegemea tu kanuni za anga unaweza kushindana na Spell za kijini , unachopitia hapo ni nguvu ya kijini maarufu kama ‘Msinyao wa ardhi’ ni mbinu maarufu ambayo ina ufanya mwili wako kuwa kama vile unazama kwenye mchanga wa jangwani bila kuona pakushikilia”Aliongea kwa jeuri.

Roma alijikuta akichanganyikiwa , kama angekuwa na uwezo wa kutumia nguvu zake za kijini ingekuwa rahisi kutoka kwenye mtego huo wa kichawi wa kijini, ilitia huzuni kwani alikosa msingi wa kanuni za anga.

Jini Ghula lilianza kutoa kicheko kikali ambacho kama ni binadamu wa kawaida basi ngoma za masikio zingepasuka na palepale aliinua upanga wake wa kijini na kisha akamsogelea Roma kwa ajili ya kumfyeka.

Roma aliamua kutegemea mwili wake na palepale macho yake yalibadilika rangi na kuwa mekundu na baada ya shambulizi la upanga kumfikia alikwepa na kuufanya upanga ule kupita na bega lake la kushoto.

“Bang!!”

Kwa namna ambavyo upanga ule ulivyokata bega ni kama vile umepita kwenye chuma kigumu sana na kusababisha mlipuko mkubwa sana wa nguvu za kijini ambao ulikuw ani kama bomu na kumsambabisha Roma kushindwa kuhimili na kudondoka chini ya maji kama vile ni furushi na kufanya maji kuruka juu kiasi cha kumfunika na kumfanya Roma kuzidi kuhisi maumivu makali kwenye bega lake.

Ijapokuwa nguvu ya andiko la urejesho ilikuwa Dormant lakini mwili wa Roma ulikuwa umetengenezwa kujiponyesha wenyewe na palepale jeraha lilianza kujiziba kwa kasi kubwa na Roma palepale alitumia kanuni za anga kwa mara nyingine na kumsukuma juu kwa kasi kubwa.

Mpaka anakuja kujiimarisha angani ushahidi peke ulionekana katika eneo alilokatwa ni shati lake kuchanika.

“Nakuona sio wa kawaida lakini usione kwamba siwezi kukuua , nitakukata kata vipande mpaka roho ikutoke , tuone kama nikikata hiko kichwa chako utaweza kupona”Aliongea Ghula kwa hasira na palepale alishikilia tena upanga wake vizuri na kumsogelea Roma kwa kasi kwa ajili ya kumshambulia huku nguvu ya kijini ikiwa imemzingira kwa wingi

Roma alitaka kujikinga kwa kutumia kanuni za anga lakini kutokana na kiasi kikubwa cha nguvu ya kijini kilichokuwa kimetolewa kilibomoa kinga yake na ilimfanya kushindwa kujongea kwa spidi.

Ilikuwa afadhali kwa upanga ule wa Jini Ghula nguvu yake haikuwa kwenye makali yake bali ni kwenye uzito wake, ilikuwa ni dhana ya kijini ya daraja la kati hivyo madhara yake hayakuwa ya kutisha sana lakini hata hivyo Roma alijiambia kama akiendelea kupokea mashambulizi kila mara basi hatoweza kudumu kwa muda mrefu.

“Hii ni mra ya mwisho nakwenda kukata kichwa chako”Aliongea jini Ghula kwa jeuri.

Jini Ghula liliona hata uvivu wa kuongezea nguvu ya kijini upanga wake kwani nguvu ya kanuni ya anga ya Roma ilikuwa ni dhaifu mno , kilichomkasirisha ni namna ambavyo Roma alikuwa akikwepa mashambulizi yake.

Kila jeraha ambalo lilikuwa likimpata Roma lilikuwa likipona kwa haraka sana licha ya ukubwa wake na hilo ndio lilimfanya kuzidi kukasirika lakini hata hivyo hakuacha kushambulia kwani aliona kabisa Roma anazidi kupoteza nguvu yake.

Ili mradi tu Roma hakuwa na nguvu za kijini basi aliona kabisa ni binadamu wa kawaida ambaye hawezi kumshinda kwa namna yoyote ile.

Jini Iftir na Marid waliokuwa wakiangalia pambano walikuwa katika mshangao kutokana na namna Roma alivyokuwa akihimili maumivu ya mikato ya panga.

Walijikuta wakikubali mwili wa Roma kama sio wa kawaida kabisa lakini hata hivyo waliamini muda si mrefu lazima ataishiwa nguvu.

Roma mpaka muda huo alishasahau hata maumivu yakoje na aliishia kukwepa pamoja na kupokea mashambulizi huku akijitahidi kumsogelea Ghula lakini ilikuwa ngumu kwani jini huyo alikuwa akijilinda mno na nguvu ya kijini.

Roma alikosa chaguo na kuishia kupigana tu , alijiambia hayupo tayari kutumia nguvu yake ya kijini ili kushindana kwani madhara yake yangekuwa makubwa sana kwake.

Upande wa wa wanajeshi na Tannya waliokuwa mbali waliweza kushuhudia pambano kwa kutumia Telescope .

Tannya alikuwa na hasira mno kutokana na Roma alivyokuwa akishambulia na alitamani kwenda kumsaidia lakini hakuwa na uwezo wa kupaa kwenye anga kwa umbali mrefu bila kugusa ardhi.

“Captain kwanini tusitumie makombora kuwashambulia , ikiendelea hivi Mfalme Pluto atakufa”

“Tukishambbulia ndio tutazidi kumuongezea ugumu wa kushinda”Aliongea Kapteni.

“Lakin…’”

“Tunapaswa kumwamini Mfalme Pluto mwenyewe na machaguo yake”

Upande wa Jini Ghula lilikuwa likitetemeka kwa hasira kubwa mno baada ya kugundua Roma alikuwa akitaka kumsogelea ili kumshambulia kwenye mwili wake sehemu ambayo ndio udhaifu wake ulipo.

“Mwanaharamu wewe tutaona ni kwa muda gani utawez akuhimili ..,Anjunini Mwanga wa mfekyo…!!!”

Baada ya kuogea vile ni kama upanga wake umetawaliwa na shock za umeme , ilikuwa ni kama vile ni radi na kuufanya kubadilika rangi na kuwa mwekundu kama vile umetolewa kwenye moto mkali kwa ajili ya kuyeyushwa na palepale alielekeza kwa nguvu na kumshambulia Roma kifuani.

“Ah..!!!

Roma shambulizi lile alishindwa kulivumilia na kujikuta akitoa ukulele wa maumivu na mwili wake ulidondoka mpaka kwenye bahari kwa mara nyingine.

“Senior huyu mtoto ndio anaonekana yupo mwishoni kufariki ,unaonaje tukishambulia wote watatu kwa wakati mmoja?”Aliongea Maridi.

“Sawa , huyu ametudhalilisha sana siku ya jana hivyo ni muda wa kulipiza kisasi , na nyie toeni hasira zenu kwa kumkata kata angalu mara tatu tatu ndio tummalize kabisa”

Jini Ifti na Marid walijikuta wakijawa na furaha kubwa mno ya kutuliza kiu yao ya kisasi na palepale kila mmoja aliita panga lake la kijini , ijapokuwa ni dhana za kawaida lakini kwa ushirikiano wa pamoja ilitosha kabisa kumuua Roma.

“Tukishamaliza kumuua tutachukua hazina yetu na kuua watu wake na baada ya hapo kazi iliotuleta kwenye ulimwengu wa kawaida itakuwa imeisha”Aliongea kwa kujiamini.

Wakati huo wakati wakiwa wanaongea Roma alikuwa ashapona kwa mara nyingie na kutumia kaununi za anga na kuelea tena angani, ilikuwa ngumu kutoroka katika hilo eneo na hata kama angetaka kufanya hivyo hakuwa tayari kuwakimbia wenzake.

Kwa muda huo aliona hawezi kuwashinda bila ya kutumia uwezo wake wa kijini hivyo aliona ni kheri tu kuhatarisha maisha yake.

Roma alikuwa katika hali ya wasiwasi kwa muda huo na alijiambia alikuwa amekurupuka na alikuwa mbali sana na miungu wenzake , pengine kwa wakati huo wanaweza kuweza kugundua anatumia kanuni za anga lakini hawajaona haja ya kujitokeza kumsaidia kwa kudhania Roma anao uwezo mkubwa kuliko wa kwao katika kushambulia.

Roma alikuwa yupo sahihi kabisa kutumia kanuni za anga kungewaamsha wenzake lakini walikuwa wakimjua kabisa alikuwa ni mwenye uwezo usio kuwa wa kawaida hivyo hata kama wasingeenda angekuwa salama , lakini wasichokijua Roma uwezo wake ulikuwa ukimuweka katika hatari ya kupoteza akili.

Wakati Roma akifikiria ni kipi afanye kwa wakati huo , huku akiona hana chaguo zaidi ya kutumia uwezo wake palepale wale majini walianza kumshambulia kwa kila upande na kumfanya kuwa katika hali tete ya kukwepa mashambulizi yao.

Spidi yao ilikuwa kubwa kuliko yeye na Roma aliishia kuangalia yale mapanga yakimsogela kwa kasi huku moja wapo likiwa limelenga sehemu ya moyo wake lakini kabla ya kumfikia tu mapanga yale yalipigishwa na kurukia upande mwingine lakini haikuishia hapo zile panga baada ya kuwaponyoka mikononi zilijigeuza kwa nguvu na kuwasogelea wote kwa pamoja kuwalenga kuwachoma kwa spidi.

SEHEMU YA 664.

Mabadiiliko hayo ya Ghafla yaliwafanya majini wote kupigwa na mshangao pamoja na kuchanganyikiwa lakini hata hivyo waliweza kuchukua hatua za tahadhari mapema.,

Roma mwenyewe aliweza kugundua mabadiliko hayo na baada ya kufikiara kwa dakika chache aliweza kugundua nini kimetokea.

“The Space of mirrors!!?”Aliongea kwa mshangao.

Ni mbinu moja bobevu sana ya kutumia kanuni za anga ambayo mara nyingi huakishi mashambulizi ya adui na inawezekana tu kwa kutengeneza nusu mkato na muunganisho(Splicing).

Roma alikuwa akijua mtu pekee ambaye alikuwa na uwezo wa kutumia kanuni hizo za anga kati ya miungu wote ni Athena peke yake.

Roma uwezo wake wa kiuungu ulikuwa umeshuka mno kiasi cha kushindwa kuweza kunasa uwepo wa ongezeko la mtu mwingine na haikuchukua muda mrefu mpaka kuja kuona mwanamke mrembo akiwa juu yake katika vazi la rangi nyeusi akiwa anaelea juu angani kama vile ni malaika.

Ilikuwa mchana wa jua kali na sura yake ni kama ilikuwa ikiakisi mwanga na kuifanya kushindwa kuonekana vizuri na kitu pekee kilichoweza kuonekana kwa uwazi ni nyayo za miguu yake tu ambazo hazikuvalishwa chochote.

Muonekano wa mrembo huyo kwenye shingo ndefu na umbo lake ni kama mara ya mwisho alivyomuona.

Athena macho yake kama kawaida yalikuwa katika hali ya maringo pamoja na kujitukuza na aliwaangalia wale majini chini yake kwa macho ya dharau kubwa mno.

Wale majini waliweza kuhisi kabisa adui huyo ni mwenye uwezo mkubwa , mkandamizo ambao alikuwa akisambaza ulikuwa na nguvu isiokuwa ya kawaida kabisa na walijiuliza imekuwaje hawakuweza kuhisia uwepo wake tokea mwanzo.

Roma alijikuta sasa akivuta hewa ya ahueni mara baada ya mwokozi wake kujitokeza , ijapokuwa alijisikia vibaya kumtegemea mwanamke ili kuendelea kuishi lakini hakutaka kujisumbua zaidi katika hautua hio.

Isitoshe sio mara ya kwanza kwa Athena kumsaidia mara ya kwanza ni nchini Australia baada ya kushambuliwa na mtu mwenye Mask na kuwekewa uchawi wa vipepeo wa kufikirika.

Roma hakutaka kujihatarisha kutumia uwezo wake kwani kuna hatihati ya akili yake kumezwa na mnyama wa maafa lakini alijiuliza imekuwaje huyu mwanamke ndio akajitokeza yeye tofauti na miungu wengine

Roma alijiuliza au ni kutokana na yale alioyasikia kwamba mwanamke huyo alikuwa akimfuatilia kila hatua zake ndio maana alikuwa akijua yupo katika hatari.

“Wewe ni nani?”Aliuliza jini Ghula na wezake wote wakimwangalia Athena kwa mbali.

Hawakuweza kujua imekuwaje Athena akawapokonya mapanga yao na kuyafyatua kuwalenga wao.

“Mababu zenu hawajawafunisha madhara ya kuvunja kanuni za Gods treaty?”Aliuliza Athena huku maneno yake yakiashiria kabisa hakuwa na huruma kabisa na muda wowote anakwenfda kuua.

“Are you also one of the gods?”Aliuliza kama je na yeye ni sehemu ya miungu.

“You are not worth enough for me to kill you , since you have violated the treaty , just end yourself”Aliongea akimaanisha kwamba hawana thamani yeye kuwaua na kwasababu wamevuja kanuni basi wajimalize wenyewe.

Baada ya kusikia maelezo hayo jini Ghula alijikuta akipandwa na jazba licha ya kwamba alikuwa katika hali ya tahadhari.

“Haha ,, unanitania nini , wewe ni mwanamke tu ambaye unampenda huyo mwanaharamu ndio maana umekuja kumuokoa , unadhani tunakuogopa kwasasabbu unajona una nguvu , unajua ni wapi tunatokea , kama una ujeuri wa kupigana na sisi sogea karibu”Aliongea kwa hasira na palepale panga lake lilimrudia mkononi na kuzidi kuwa na nguvu ya kijini na wote kwa pamoja waliyarusha kuelekea aliposimama Athena.

Athena wala hakujihangaisha nao ni kama shambulizi lao lilikuwa la kitoto na alimgeukia Roma.

“Hades wewe ni kilaza ., hata kama umerithi uungu wa H/ades wa zamani lakini uelewa wako wa kanuni za anga ni mdogo”

Roma alijikuta akikunja ndita kwa uchungu hakutegemea Athena angemwita Kilaza wakati alikuwa akijiamini sana likija swala la kuvuna nishati za mbingu na ardhi.

“Ngoja nikuambie sasa , kanuni za anga ni sawa tu na unavyojifuza namna ya kuvuna nishati za mbingu na ardhi lakini inashangaza mpaka sasa umeshindwa kugundua siri ya Space Laws”Aliongea Athena na kumfanya Roma kutoa tabasamu la kifedhuli.

“Sister nadhani huna muda wa kutosha kuanza kunifundisha, ndio wanajiandaa kukushambulia hivyo”Aliongea Roma na kumfanya Athena kutoa tabasamu la dharau.

“Hawa washakufa mbona , hakuna lingine”Aliognea kijeuri .

“Huwa sipendi kabisa kupigana na mwanamke , Dah huku ni kujidhalilisha”Aliongea jini Ghula kwa jeuri

“Wewe mwanamke hebu chukua hii kwanza”Alifoka Jini Ghula na palepale aliongeza nguvu ya upanga wake ukatao kuwili spidi kubwa ukimsogelea Athena kwa nguvu tofauti na alivyokuwa akimshambulia Roma.

Roma alijua kabisa shambulizi hilo halikuwa la kawaida , anaweza kuliepuka lakini kama likimgusa basi pengine uhai wake ungeondoka.

Wakati upanga ule ukimkaribia Athena palepale ulipotea wenyewe isijulikane umeelekea wapi ni kama vile ulikuwa umeyeyuka au umemezwa na anga.

Wakati huo huo majini wote walijikuta wakihisi nguvu isiokuwa ya kawaida chini yao ikiwavuta kwa kasi na kuwafanya kuanza kushindana nayo.

Roma aliekuwa amesimama mbali alikuwa akiona kabisa kilichokuwa kikiendelea na aliweza kuona sehemu ya eneo lao walipokuwa wamesimama anga lake lilikuwa likiporomoka kwenda chini.

Kitendo cha anga kuporomoka ndio kiliwafanya kuanza kukosa balansi na kufanya waanze kujihisi ni kama wanavutwa kwenda chini.

Roma alishangaa kwani hakuwahi kuona kanuni ya anga kama hio na ilikuwa ni kama kinyume chake na vile alivyokuwa akifahamu , kwani ni kama anga limetengeneza shimo.

Ilikuwa ni kama vile uwe umesimama kwenye lift na ghafla tu Lift inafeli na wewe kuanza kuporomoka kwenda chini , kanuni hio ya anga ilikuwa ikifahamika kama Space hole au shimo la anga ni tofauti na Black hole lakini uvutano wake husababishwa na anga kuporomoka(Law of space Collapse)

Wale majini walijikuta wakianza kupaniki baada ya kugundua hali yao haikuwa nzuri kabisa na mbaya zaidi walikuwa ni kama wapo ndani ya mtego kwani walikuwa wamezungukwa na Parallel Space ambayo ilikuwa kama ngao ya kuwafanya wasiweze kukimbia.

Walijikuta wakikosa balansi na kudondoka mpaka kwenye bahari na ile wanafika ile sehemu ilitengeneza shimo ambalo lilizidi kwenda chini na kufanya maji kuzunguka kwa kasi mno lakini mara baada ya sekunde kumi kumalizika kila kitu kilipotea na kurudi katika hali yake ya kawaida na wale majini hawakuonekana tena.

“Majini wajinga sana hawa” Aliongea Athena kwani alichokifanya ni kuwatengenezea mtego ambao ungewahamisha kutoka katika ulimwengu wa kawaida na kumezwa katika anga msambo.

Roma hata yeye mwenyewe aliona kabisa wale watu walikuwa kwenye taharuki kwa namna ambavyo wamezama kwenye kile kitu kilichotokea , mbinu hio ilikuwa imeweza kuua majini wa levo ya kupita dhiki kwa shambulizi moja tu , hakika iliogofya sana.

“Usishangae , nguvu zao ni ndogo sana kulinganisha na Master wa Hongmeng , hii ni mbinu ambayo ilikuwa ikiwafaa sana lakini kama nguvu yao ya kijini ingekuwa kubwa zaidi isingekuwa rahisi kuwamaliza kirahisi”

“Hujatumia nguvu ya aina yoyote , hata kama uwezo wao ungekuwa mkubwa nina mshaka kwamba wasingeweza hata kujaribu kukushambulia”Aliongea Roma akiishia kumkubali Athena.

“Hii ni nguvu inayotokana na nguvu ya kanuni za anga ambayo ulidharau na kukimbilia kujifunza kanuni za kuvuna nishati za mbingu na ardhi”Aliongea Athena kwa majigammbo.

“Hades your situation is in my expectation , do you still think your path is correct”Aliuliza kwamba hali yake ipo ndani ya matarajio yake na anamuuliza je njia aliochagua ni sahihi.

“Ni kama ambavyo wengi wenu mlivyokuwa mkilazimisha mimi kujifunza kanuni za anga ili kuendana na nyie , naamini mlipambana mpaka kufikia mlipo hivyo ni kama mimi tu”

Athena hakutaka kuongea nae zaidi baada ya kusikia maelezo yake alimwangalia kwa ukauzu huku akijiandaa kuondoka lakini Roma alimzuia.

“Nina shauku moja , kwanini kanuni zako za anga zina kani mvutano mkubwa namna hio kiasi cha kutengeneza shimo kwenye anga , ni nguvu ya aina gani ambayo iliwarudisha chini?”Aliuliza Roma.

“As I said before , you don’t understand what space is at all … do you really think that there is a so called force in this universe?”Aliongea akimaanisha kwamba ni kama alivyosema mwanzo kwamba Roma haelewi kanuni za anga ni nini , na anamuliiza je ni kweli anaamini kuna kitu kinaitwa force kwenye ulimwengu huu.

Swali lile lilimshangaza sana Roma kwani hakuelewa anachomaanisha lakini Athena alionekana hakuwa na mpango wa kuongea na kufumba na kufumbua tu alikuwa ashapotea.

Roma alijikuta akianza kujiuliza maswali kuhusu kanuni za Force katika anga ni nini na kujiuliza hicho sio ndio kitu ambacho Fizikia inafundisha .

Roma alijiuliza pengine anapswa kumuuliza Clark kuhusu hilo swali , huenda akawa na majibu au mawazo mbadala.

Licha ya kuchanganyikiwa kwake kitu muhimu ni kwamba alikuwa ameshaokoka na familia ya Sharif ishapoteza majini wao wanaowapa ulinzi hivyo alijua pengine hakuna uwezekano wa kutuma wengine kuja kumshambulia na angalau sasa alijisikia ahueni.

Roma mara baada ya kurudi juu ya boti wahudumu wote pamoja na Tannya walikuwa katika furaha lakini ilimfanya Roma kuona aibu kwani ukweli ni kwamba ni Athena ambaye amemfanya kuishi.

“Mfalme Pluto kuna simu yako hapa kutoka Tanzania”Aliongea Sherly ambaye alitoka ndani ya boti na kuja juu kwenye Deck.

Roma mara baada ya kusikia kuna simu yake moja kwa moja alijua pengine ni kutokea katika familia ya Mzee Sharif lakini mara baada ya kugundua mpigaji aliishia kutoa tabasamu la kutoridhika.

“Mheshimiwa waziri mteule hakika umeniingiza kwenye matatizo awamu hii”Aliongea Roma.

Alikuwa ni Afande Maeda ambaye alitteuliwa kuwa Waziri wa ulinzi mara baada tu ya Roma kurudi kutoka ulimwengu wa majini pepo.

“Mr Roma naona hujashangazwa na simu yangu”

“Najua ni Mzee Kweka ndio amekupa njia za kuwasiliana na mimi sina haja ya kushangaa hebu nenda moja kwa moja kwenye topiki ,najua mnanitumia tu ili kutimiza malengo yenu ya kupunguza nguvu ya Sharif ndani ya Tanzania”

“Upo sahihi tulikuwa tukikutumia lakini hatukutarajia ungeenda mbali namna hii” Aliongea waziri.

“Kwahio unamaanisha kwamba nipo kwenye hali mbaya kwa sasa?”

“Wewe unaonaje , nilikuwa sijui sana kuhusu familia ya Sharif lakini napaswa kukuambia nguvu yake ni kubwa sana kuliko unavyofikiria , mpaka sasa taarifa ambayo tupo nayo ni kwamba wametuma majinni watatu kwa ajili ya kuja kukushambulia , hivi unadhani unaweza kurudi nchini kirahisi”Aliongea na kumfanya Roma kutoa cheko.

“Nilikuwa nikipanga kuomba mtu kunisaidia kufikisha ujumbe kwa familia ya Sharif , majini wao watatu waliokuja kunishambulia wamepotea milele na milele”

“Unamaanisha nini?, unasema umewaua?”

“Sio mimi , wamekuja kwenye maji ya kimataifa wenyewe kwa ajili ya kunishambilia huku wakijua kabisa wanavunja sheria ya Gods treaty , hivyo kilichowatokea ni kwamba Athena amewapoteza kwenye anga na shambulizi moja tu , natamani ningekuwa na uwezo kama wake ingekuwa rahisi kumaliza familia yote ya Mzee Sharif”Aliongea Roma na sauti upande wa pili ilikaa kimya.

“Hili ni tatizo kubwa , familia ya Sharif haitoliacha hili lipite , Roma hebu sikiliza ushauri wangu kama unataka kurudi Tanzania usilikuze sana hili swala , sukumia lawama zote kwa miungu wenzako na sema haujahusika kuwaua”

“Huo ni ujinga , naweza nikawa sijahusika ndio lakini nilipokea uungu kutoka kwa Hades wa zamani , siwezi kupotezea maswala ya miungu wenzangu kirahisi hivyo ili kujiepusha na lawama”

“Hebu acha kuwa mbishi , nimepewa jukumu na babu yako kulimaliza hili swala kimya kimya”Aliongea

“Ninachomaanisha mimi ni mwaminifu na siwezi kukimbia wajibu wangu kutokana na changamoto:”Aliongea Roma huku akijiambia ni kheri kufungamana na Christen na kina Stern kuliko wazee hao waabudu shetani.

“Ukweli ni kwamba shauku yangu ni kutaka kujua nguvu ambayo ipo nyumba ya familia ya Sharif na ni miungu ya aina gani wanayosalia”

“Naogopa kusema kwamba hakuna ambaye anajua , kashabrasha lao mwenye ‘Clearence’ ni mheshimiwa raisi peke yake , ila ninachoweza kukuambia ni kwamba kuna nguvu kubwa mno ambayo inaweza hata kushindana na majini ya koo zote”Aliongea mzee huyo na Roma alijikuta akikunja ndita na kujiambia kwanini mzee huyo anaongea kama anamtisha.

“Kama nilivyokuambia Mr Roma simu hii ni kwa ajili ya kuzungumza ili kukusaidia”

“Kunisaidia, naamini lazima kutakuwa na masharti”

“Kama ulivyo msemo wa no free lunch , tumetoka kwenye kikao na mheshimiwa raisi na amesema kama upo tayari kutoa mchango kwa taifa pamoja na kurudisha hazina yao atahakikisha anasaidia familia ya Mzee Nguluma kuwa huru , kuhusu taarifa za vifo vya majini wao tunaweza kukusaidia namna ya kulimaliza bila ya kuamsha hasira yao”

“Mara ya mwisho uliniomba kufundisha kikosi mbinu za kivita , awamu hii unataka nini kutoka kwangu?”

“Huna haja ya kufundisha kikosi chochote , tunachotaka kujua ni vipi manowari yako ya kijeshi imeweza kuingia katika mipaka ya maji yetu bila kujulikana na kufanya mashambulizi na kisha ukatoweka na mpaka sasa hakuna rada yoyote ilioinasa”Aliongea Waziri Maeda

“Haiwezekani , teknolojia iliotumika katika meli zangu za kivita ni kubwa mno na inaweza kugeuza mpangilio wote wa kijeshi wa dunia , kama nitatoa siri yake nitakuwa nimevunja pia kanuni ya The Gods treaty”Aliongea Roma.

“Tunachotaka ni kuwa na hio teknolojia kwa ajili ya kujilinda siku za mbeleni , na sisi hatuwezi kuvamia taifa lingine , Tanzania ni nchi ya Amani”

“Binadamu kuonea mnyonge ni asili yake , mnaweza mkawa hamshambulii wengine lakini vipi kuhusu watu ndani ya jeshi , nina uhakika wanaweza kuiuza kwa mataifa mengine hapo ndio shida itakapoanzia”

“Kama unagoma basi sitokuwa na msaada kwako na inabidi udili na hali hii mwenyewe”

“Hakuna tatizo”Aliongea Roma na simu palepale ilikatwa.

“Mfalme Pluto Tanzania ni nchi yako kwanini usiimarishe kijeshi, unaweza ukafanya jambo hili kwa siri na hakuna taifa lolote ambalo linaweza kukupinga”Aliongea Tannya.

“Hivi kwanza aunajua kwanini meli zangu zote zinaanziwa na neno Ghost?”Aliuliza Roma na Tannya alitingisha kichwa kwamba hajui.

“Kipindi cha nyuma wakati nilipompa madaraka Sauron ya kusimamia ujenzi wa meli hii ili kuepusha kufatiliwa na majeshi ya majini ya mataifa makubwa alimuomba Clark kutengeneza mfumo wa Stealth unaojitegemea kwa ajili ya meli , hizo meli hazikujumuisha mfumo wa Aegis kutoka Marekani ikiwemo makombora ya kivita pamoja na mfumo kujilinda na makombora lakini pia teknolojia yake imejengwa kwa ajili ya kuweza kutonaswa na mifumo ya kiuliuzi ya kidunia , ilimchukua Clark mwaka mzima kutengenza huo mfumo , ilikuwa ni gunduzi ngumu sana kwake na shukrani alikuwa na data za kisayansi za siri ambazo ziliachwa na Hades wa Zamani na mfumo huu mpaka sasa unajulikana kwa jina la Cunei”Aliongea Roma na kumfanya Tannya kuwa katika mshangao,

“Mfalme Pluto kwahio unamaanisha kwamba teknolojjia iliotumika ni ile ile iliotumia katike ujenzi wa dhana ya invisible Helmet?”

“Upo sahihi , teknolojia ambayo ipo ndani ya hizi meli imetokana na data zilizoachwa na Hades wa zamani , baada ya Clark kusoma taarifa hizo na kufanya uchakachuzi kuunda kitu kipya ndio aliupa mfumo huu jina la Cunei, Dhana ya Helmet ilishapotea miaka mingi iliopita lakini teknolojia yake haikupotea kwani alieoiunda ni Hades wa zamani , hivyo unaweza kusema kwamba ile manowari ya kivita inaweza kuingia ndani ya mipaka ya taifa lolote bila kugundulika na ikafanya shambulizi na kutoroka kimya kimya”Aliongea Roma huku akicheka.

“Clark anajua nguvu ya huo mfumo na tulikubaliana kabisa kwamba siri ya teknolojia hii isije ikatolewa kwa taifa lolote na mimi niliahidi hivyo siwezi kwenda kinyume”

“Clark atakuwa na furaha unakumbuka ahadi yake vizuri”Aliongea na Roma alitingisha mabega, Clark alikuwa mwanamke ambaye amemsaidia katika vitu vingi , ni sawa na kusema maisha yake yote aliishi kumsaidia Roma.

“Lakini master kwa kile tulichoifanyia ile familia sidhani kama itakuwa rahisi kurudi Tanzania”Aliongea Tannya akionyesha wasiwasi wake na kumfanya Roma kutabasamu.

“Mpaka sasa muda umeenda sana , nina uhakika familia hio itakuwa imepokea zawadi yangu niliowatumia , hebu mleteni hapa Maimuna ili aipigie familia yake simu”Aliongea Roma na muda uleule Maimuna aliletwa.

SEHEMU YA 665.

Mremho huyo hakuwa katika hali nzuri kabisa , alikuwa ni kama ameshaanza kuchanganyikiwa na hakujua hata ni kipi kinaendelea na Tannya alimlamba vibao viwili vya nguvu kumshitua na kisha alianza kuelewa kile ambacho anaambiwa na kisha alichukua simu na kuandika namba na kisha kupiga.

“Mnyama sana wewe Roma , unafanana na nguruwe wewe , hivi unafikiri familia yangu inaweza kukuogopa kwa njia hii?”Sauti ya Mzee Sharif akiwa katika jazba ilisikika.

“Babu ni mim….”Aliongea Maimuna huku aking’ata lipsi zake akionekana kama mtu anaetaka kulia.

“Maimuna mpe Roma Simu”aliongea na kumfanya Maiuna kidogo tu aidondoshe , moyo wake ni kama umevunjwa vipande vipande , yaani babu yake alionyesha kabisa kutomjali na jambo hilo lilimuumiza.

Upande wa Mzee Sharif alikuwa kwenye kiwango cha juu cha hasira na hakutaka kabisa kujua Maimuna anamfikiria nini kwa wakati huo , usalama wa mjukuu wake ilikuwa ni kipaumbele cha pili na taswira ya familia yake ilikuwa ni kipaumbele cha kwanza .

Roma alichukua simu kutoka kwenye mikono ya Maimuna na kisha akaweka sikioni huku macho yake yakimwangalia mrembo huyo na alijikuta akimuonea huruma kidogo.

Ukizaliwa kwenye familia kubwa kama ya Mzee Sharif cheo chako kinaendana na uwezo wako na alipaswa kujua hilo , kosa kubwa ni kwamba alikuwa amezoea kubembelezwa sana na wanafamilia wote

“Kuna shida gani mzee , mbona umekasirika hivyo?”Aliongea Roma huku akitoa kicheko.,

Upande mwingine katia makazi yao huko Bagamoyo familia hio ilikuwa imejikusanya sehemu moja wakiendelea kusubiria taarifa kutoka kwa majini waliotumwa kwenda kumsbambulia Roma.

Kabla ya habari hio kuwafikia kilikuja kiboksi ambacho kilikuwa kimebeba CD ndani pamoja na barua sasa waliweza kugundua nini kipo ndani ya CD hio na Mzee Sharif wakati akiongea na Roma alikuwa ameishikilia mkononi huku akitetemeka kwa hasira.

“Unanitishia , hivi unadhani mimi Sharif ni mwepesi kuchokozwa hivyo?”

“Sitaki kuongea pumba na wewe mzee, kitu ambacho umefikishiwa ni kopi yake tu na file original lipo kwenye mikono yangu , kama unataka kulinda taswira ya familia yako ni kheri ukamuachia huru Mzee Nguluma na mke wake, nakuambia usijaribu kunichokoza tena”Aliongea Roma kibabe na palepale alikata simu.

Mzee Sharif alikuwa kwenye kiwnago cha juu cha hasira , ukweli ni kwamba hakutegemea kama swala hilo lingefikia hapo.

Kitu ambacho Roma amemleta kama zawadi kilikuwa ni kitu kichafu sana kwa familia hio.

Ijapokuwa Mzee Sharif alikuwa akisalia miungu yake lakini katika ulimwengu wa kawaida alikuwa akiaminika kama muumini mzuri wa dini na sehemu nyingi kama Dubai na maneo kadhaa walikuwa wakimheshimu lakini ukweli ni kwamba Mzee huyo alikuwa ni mnafiki wa dini.

Roma siku kadhaa mara baada ya kuwasiliana na Makedon alimwambia achimbe udhaifu wowote wa familia ya Sharif, udhaifu ambao kama mzee huyo atauona basi hawezi kufurukuta na swala hilo lilikuwa jepesi sana kwa Makedon.

Ukweli ni kwamba hata Makedon mwenyewe hakujua kama swala hilo llikuwa ni rahisi lakini mara baada ya kuanza kufatilia familia hio aliweza kupokea taarifa kutoka kwa mtu ambaye hakuwa amejitambulisha jina , katika baadhi ya taarifa hizo moja wapo ni Vidio ambayo ilikuwa ikiwaonyesha Naibu waziri Salihi na mama yake wa kambo wakifanya mapenzi hotelini tena katika vidio hio walikuwa wakisikika sauti kabisa namna ambavyo Asha alikuwa akimkejeli mume wake kama hakuwa akiujua mchezo vizuri huku Salihi akimuunga mkono.

Ilikuwa ni Vidio chafu sana na kama ingesambaa ingeathiri sana familia ya Sharif.

Sasa hayo hayakuwa yakijulikana na mara baada ya vidio hio kufikishwa kwa mzee Sharif na kuiangalia alijikuta akipandwa na ghadhabu mno na hakuwa hata akijua ni kipi afanye.

Baada ya simu kukatwa palepale alitoa maagizo ya Waziri Nguzo na mke wake waletwe ukumbini pamoja na mtoto wao Salihi na swala hilo lilifanyika haraka sana kwani ndani ya nusu saa waliweza kufika.

Mzee Sharif alikuwa amekasirika sana na mara baada ya wote kufika alimpa ishara mtu wa mitambo kuchezesha vidio ile mbele yao na mara baada ya Waziri Nguzo kuona kile ambacho kilikuwa kikionekana alijikuta akishika moyo wake huku machozi ya kiume yakimtoka , upande wa Salihi na Asha walijikuta wakiziba midomo yao kwa mshituko.

Ukweli ni kwamba ni kweli wakikuwa wapenzi wa muda mrefu sana , kabla hata ya Asha hajaolewa na Waziri tayari alikuwa na mahusiano na Salihi na mara nyingi kila alipokuwa akisafiri kwenda nje ya nchi kilikuwa ni kisingizio tu cha kwenda kikazi lakini alikuwa akienda kukutana na Salihi na kisha kunyanduana.

Asha alikuwa akimpenda sana Salihi kuliko alivyokuwa akimpenda mume wake na ndio maana alihakikisha kila mwanamke ambaye alikuwa akimsogelea Salihi alikuwa akimkomesha kwa aidha kumtumia majambazi kumpa onyo au kumuua kabisa akileta ukiburi.

Waziri Nguzo alijikuta akimkaba Asha akitamani kumuua huku machozi yakimtoka lakini hakuweza kuubadilisha ukweli, kilio chake kilizidi kumkasirisha Mzee Sharif na palepale alitoa bastora kwenye kiuno chake na kuikoki na kufumba na kufumbua tu alikuwa ameruhusu risasi na kumchangua kichwa Waziri nguzo na kudondoka palepale.

Kitendo kile kilishangaza watu wengi kwani hawakutegemea kama mzee huyo angeweza kuua mtoto wake wa damu lakini ilikuwa imewezekana.

Mzee Sharif hakuishia kumuua Waziri nguzo tu bali alimchapa risasi Asha pamoja na Salihi na wote wakawa wafu na katika familia hio akabakia mtoto mmoja tu ambaye ni Ayubu.

Taarifa ya kuuwawa kwa Waziri na naibu waziri ilisafiri na kufika Ikulu ambapo kulikuwa na kikao kizito kikiendelea kilichokuwa kikihusisha wanausalama wa nchi.

Ajenda kubwa iliokuwa ikiendelea katika kikao hicho ni namna ya kumaliza swala ambalo linaendelea kati ya familia ya Mzee Sharif na Roma.

Baada ya Afande Maeda kuweka wazi kile ambacho kimesababisha Waziri na naibu Waziri kupigwa risasi Mheshimiwa Raisi alimpa kazi Waziri Maeda kuwasiliana na Roma tena ili kupata kujua mpango wake.

Ukweli ni kwamba mheshimiwa Raisi Senga alikuwa na mpango mwingine kichwani ambao alikuwa akiendeleza akishirikiana na Nadia pamoja na Suzzane.

*****

Upande wa pili katika boti ya kifahari Roma alikuwa amekaa kabisa katika eneo la mapumziko juu kabisa huku akiwa amevaa kijibukta tu akiwa amelala kifudi fudi akifanyiwa masaji na Tannya ambaye muda huo alikuwa amevalia Bikini tu.

Ijapokuwa umbo lake lilikuwa likivutia sana kiasi cha kumpagawisha mwanaume yoyote lakini Roma hakutaka kumuingia , alijua kama atafanya mapenzi na huyo mrembo basi moja kwa moja ingekuwa ndio kuhalalisha mahusiano yake jambo ambalo hakutaka kuliruhusu litokee.

Hakutaka kutengeneza deni na Tannya kabisa , ijapokuwa alikuwa mtiifu lakini bado hakutaka kuchukua hatua zozote zidi yake.

Wakati Roma akiendelea kufanyiwa huduma hio iliotukuka palepale simu iliokuwa pembeni ilianza kuita na Tannya aliichukua haraka haraka na kuangalia anaepiga na kisha akamkabidhi Roma.

Roma alishajua anaepiga ni Afande Maeda hivyo moja kwa moja aliweka sikioni kumsikiliza.

“Niambie waziri”

“Roma sijategemea kama ulikuwa umekusanya uchafu wote pamoja na ufisadi wa familia ya Mzee Sharif”Aliongea Waziri wa ulinzi na kumfanya Roma kutoa kicheko.

“Waziri unaonekana una mfumo wa intelijensia mpaka ndani ya familia ya Sharif , heko kwako”Aliongea Roma huku akitoa kicheko.

“Unaweza ukaona umelimaliza hili swala kwa kutumia udhaifu wao lakini siamini kama linaweza kuisha kirahisi hivyo”

“Unamaanisha nini , najua ile familia inachojali ni taswira yao , wakinichokoza tena wataisoma namba nitahakkiisha natumia ushawishi wangu kuwadhalilisha”

“Ninachomaanisha ni kwamba unaweza ukawa umelimaliza kwa upande wa familia hio lakini kitaifa hili swala halijaisha , umejeruhi usalama wa taifa na kila kiongozi analazimisha uwajibishwe la sivyo usiruhusiwe kurudi Tanzania”Aliongea Waziri Maeda na kumfanya Roma kukunja sura.

“Kwahio Waziri nadhani hujanipigia simu kuniambia kuhusu msimamo wa serikali hebu nenda moja kwa moja kwenye topiki”

“Upo sahihi , nimekupigia simu nikiwakilisha serikali kukuambia msimamo wetu , kama hutokubali kutii masharti tuliokuwekea basi huruhusiwi kukanyaga ndani ya Tanzania”

“Waziri nadhani hujanielewa nikisema hapana ni hapana , teknoljia ya kijeshi ya mfumo wa Cunei haiwezekani kutolewa, ila ninaweza kutoa ofa ya kitu kingine ili kumalizna na hili swala”

“Nakusikiliza Mr Roma”

“Najua Tanzania kwasasa inapitia wakati mgumu sana katika maswala ya mafuta ya petroli na kusababisha bei kupanda kwa kiasi kikubwa, nipo tayari kusaidia taifa la Tanzania kwa kuiwezesha kuingiza mafuta barrels milioni nne kwa nusu bei kwa kipindi cha mwaka mzima”Aliongea Roma na kufanya upande wa pili kuwa kimya.

“Upo siriasi juu ya hili , hiko ni kiasi nusu ya mafuta ambayo tunaagiza kwa mwaka mzima?”

“Nipo siriasi katika hilo lakini nina sharti ninalohitaji kutoka kwenu ili kuweza kutumiza ahadi”Aliongea

“Weka wazi sharti lako”

“Nahitaji Najma kupewa cheo cha unaibu waziri wa Elimu baada ya kuteuliwa mbunge wa viti maalumu”Aliongea Roma

“Nitaongea na mheshimiwa kuhusu hili , ni ofa nzrui”Aliongea Waziri.

Siku ambayo Roma alienda kumuokoa Najma kituoni alimuuliza ndoto yake ni nini na Najma alisema anataka kuingia katika siasa, Roma aliona kuingia kwenye siasa ni swala ambalo lingemchukua muda mrefu mpaka kufikia ngazi za juu hivyo alimuahidi ataangalia namna ya kumsaidia.

Kwa mwaka Tanzania huagiza kiasi cha Barrels(mapipa) milioni nane za mafuta ya petrol ambazo zina thamani ya Dollar bilioni mbili nukta nne , hivyo kama Roma atawezesha Taizania kupanta nusu ya kiasi cha mafuta yanayoagizwa kwa nusu bei inamaanisha kwamba ni hela nyingi sana ambazo taifa ingeokoa na kuzielekeza katika mambo mengine lakini pia bei ya mafuta ingeshuka kwa kiasi kikubwa.

Dakika kumi na tano tu mara baada ya Roma kumaliza mazungumzo na Afande Maeda ambaye ni waziri wa ulinzi palepale alirudisihwa jibu na kuambiwa kwamba serikali ipo tayari kupokea ofa yake na kutimiza masharti , Roma alitoa tabasamu la ushindi na sasa aliona yupo huru kurudi Bongo.

Baada ya kumaliza swala hilo aliwasiliana na Ron kwa ajili ya kuandaa mchakato kuiwezesha Tanzania kupata mafuta nusu bei na baada ya hapo alitoa maagizo kwa Tannya safari kuanza kurudi Tanzania.

Muda huo huo wakati Roma akijiandaa kurudi Tanzania alifika Sherly na kumwambia kwamba Maimuna anataka kuongea na yeye na Roma alishangazwa na taarifa hio na kuishia kutoa ruhusa aletwe kwake.

Maimuna mara baada ya kuletwa mbele ya Roma palepale alimpigia magoti huku akitetemeka jambo ambalo lilimshangaza kila mmoja.

“Ongea kwanini unataka kuonana na mimi”

“Naomba unifanye kuwa mwenye nguvu kubwa”Aliongea Maimuna huku akisujudu mbele ya mtukufu mfalme Pluto lakini ombi lake liliwashangaza wote.
 
Hatariii
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom