Simulizi: Ulimwengu Ndotoni Mwangu

Simulizi: Ulimwengu Ndotoni Mwangu

Sehemu ya 26

Alichokitaka Edmund ni kuishi na Esta tu, hapakuwa na namna nyingine ambayo alitakiwa kufanya zaidi ya hilo, kitu kikubwa alichotaka kukifanya ni kumuacha Angelina taratibu huku akiendelea kuwa karibu na msichana aliyekuwa na mimba yake.
Alitamani kumwambia ukweli wa kile kilichotokea lakini alisita kufanya hivyo, angewezaje na wakati msichana huyo alikuwa akifanya mitihani yake ya mwisho ya kidato cha sita? Kila alipofikiria, hakuona kama huo ulikuwa muda sahihi wa kufanya kile alichotaka kufanya.
Akaacha siku zipite kama kawaida. Aliwasiliana na Angelina na kumwambia maneno mengi ya mapenzi, alifanya hivyo kwa kuwa alimjali, hakutaka kumuharibia ndoto yake ya kufaulu mitihani yake na hatimaye kujiunga na Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.
Baada ya siku kadhaa msichana huyo akaanza mitihani yake, kipindi hicho alikuwa bize sana, alitaka kusoma na kutilia mkazo mitihani yake, alifanya vizuri mpaka alipomaliza na hatimaye kukaa nyumbani na kusubiri matokeo.
Moyo wake ulikuwa na furaha tele, aliamini sasa angekwenda kujiunga na Chuo Kikuu cha Dar es Salaam na kuwa na mpenzi wake. Aliomba Mungu kwa hilo, waliendelea kuwasiliana na kwa Edmund hakutaka kuonyesha tofauti yoyote ile, alijifanya kumpenda Angelina kama alivyokuwa akimpenda kipindi cha nyuma.
Baada ya miezi kukatika, hatimaye matokeo ya kidato cha sita kutangazwa, Angelina alifaulu vizuri na hatimaye kujiunga na chuo hicho. Alifurahi mno, sasa alijua alikuwa akienda kuungana na mpenzi wake, wawe wawili mpaka pale ambapo wangefunga ndoa na kuishi pamoja.
“Hongera sana kwa kufaulu!” alisema Edmund, alikuwa akimpongeza mpenzi wake huyo.
“Nashukuru sana! Sasa nitakuwa huru na wewe,” alisema Angelina bila kujua kilichokuwa moyoni mwa Edmund.
Kwa kipindi hicho alichokuwa akijiunga na chuo hicho tayari mimba ya Esta ilikuwa na miezi saba. Alimpenda mno Edmund, muda mwingi walikuwa pamoja lakini baada ya Angelina kwenda chuoni hapo akaanza kupata shaka kwamba inawezekana wawili hao wakawa wapenzi, akataka kupata uhakika.
Akamuita mpenzi wake na kukaa sehemu, siku hiyo alitaka kuambiwa kila kitu kwani yule mwanafunzi wa mwaka wa kwanza alionekana kuwa karibu naye, hata walivyokuwa wakiongea, walionekana kabisa kuwa wapenzi, kulikuwa na dalili ambazo zilikuwa ngumu sana kufichika.
“Ni kweli alikuwa mpenzi wangu!” alisema Edmund huku akimwangalia Esta.
“Alikuwa?”
“Ndiyo!”
“Na sasa hivi?”
“Ninataka kumuacha!”
“Kwa hiyo bado ni mpenzi wako?” aliuliza Esta.
Edmund akabaki kimya kwa sekunde kadhaa, hakukuwa na uharaka wa kulijibu swali hilo, lilikuwa jepesi sana ila kwenye kutolewa majibu lilitakiwa kuwa na umakini mkubwa. Ili kuzuga, kwanza akapiga funda moja la juisi na kumwangalia tena Esta.
“Ninataka kumuacha kwa sababu yako!” alimwambia Esta.
“Umekuwa naye kwa kipindi gani?”
“Kabla sijakupata wewe. Nimekuwa naye tangu tupo shuleni. Ni mpenzi wangu, anajulikana mpaka nyumbani, ila ninaamua kumuacha kwa sababu yako, ninataka kukaa na familia yangu,” alisema Edmund.
Esta naye akakaa kimya, maneno aliyoongea mpenzi wake yalimshtua na kujiona alikuwa mtu muhimu sana kwake. Aliyaingilia mapenzi ya watu kwa sababu alimpenda, akapata mimba na hatimaye mwanaume huyo alitaka kumuacha mpenzi wake kwa sababu yake kwa kumwambia alitaka kukaa na familia yake.
“Utamwambia lini?”
“Hivi karibuni. Naomba muda, najua wewe ni muelewa na utanielewa kwenye hili!”
“Sawa.”
Alikubaliana na Esta kwamba ni lazima amwambie Angelina ukweli ila kabla ya kufanya hivyo, kwanza alitakiwa kumpangia chumba msichana huyo kwani kwa jinsi ilivyokuwa, hakutaka kabisa kumuona akiendelea kuishi hapo chuoni.
Akamchukulia chumba maeneo ya Changanyikeni ambapo huko ndipo alipoanza maisha mapya huku akiwa amenunuliwa kila kitu cha ndani na kulipiwa kodi ya mwaka mzima. Kwa kuwa Edmund hakutaka kumuona msichana huyo akipata shida, akamuandaa dereva Bajaj ambaye huyo alikuwa na kazi ya kumpeleka popote pale alipotaka.
Siku zilikatika na baada ya miezi miwili huku Esta akiwa amejifungua mtoto wa kike, sasa akajipanga kumwambia Angelina kila kitu, hakutaka kumpotezea muda zaidi, ilikuwa ni lazima amwambie ukweli juu ya kile kilichotokea, kama inawezekana basi waachane.
Alijua Angelina angekuwa kwenye wakati mgumu lakini hakutaka kujali, kwa muda huo kitu alichokitafuta kilikuwa ni amani ya moyo wake na furaha ya mpenzi wake tu. Siku hiyo ya kumwambia ukweli akaamua kumpigia simu na kumwambia alitaka kuzungumza naye.
Walitakiwa kuonana sehemu ambayo wangekaa wawili tu, na sehemu yenyewe ambayo aliitaka ilikuwa ni ndani ya chumba kimoja kwenye hoteli moja iliyokuwa huko Kinondoni. Baada ya Angelina kusikia mpenzi wake alitaka kuongea naye, haraka sana akajiandaa kwa lengo la kwenda huko.
“Au anataka kunivisha pete ya uchumba? Mungu wangu! Nadhani nitazimia kwa hiyo sapraizi,” alijisemea huku akichukua Bajaj na kuelekea Kinondoni.
Njia nzima alikuwa na mawazo juu ya kile ambacho angekwenda kuambiwa huko hotelini. Hakuchukua muda mrefu akafika mpaka kwenye hoteli aliyoambiwa na kuingia ndani. Kwa kuwa aliambiwa mpaka chumba atakachokuwemo, moja kwa moja akaelekea mpaka huko na kuingia ndani.
Alimkuta Edmund akiwa ametulia kwenye kiti kilichokuwa humo, macho yake yalikuwa kwenye simu aliyokuwa akichezea huku na kule, mlango ulipofunguliwa tu, akajigeuza na kumwangalia Angelina aliyeingia humo ambapo sura yake ilikuwa na tabasamu pana.
“Wewe tabasamu tu, ila utaondoka huku ukilia,” alijisemea alipokuwa akimwangalia Angelina.
Msichana huyo akamsogelea na kumkumbatia, alionekana kuwa na furaha tele, moyo wake ulikuwa na shauku ya kusikia kile alichoitiwa ndani ya chumba hicho. Baada ya kumkumbatia, hatimaye akakaa kitako na kumsikiliza.
“Kuna kitu nataka kuzungumza nawe,” alisema Edmund huku akimwangalia msichana huyo.
“Kitu gani mpenzi?”
Alimuuliza! Edmund akakaa kimya kwanza, ni kweli alidhamiria kumwambia Angelina kile kilichotokea lakini ghafla tu akahisi moyo wake ukianza kuwa mzito kumwambia suala hilo. Akaanza kukumbuka jinsi walivyokutana, alivyompenda mpaka kuwa wapenzi.
Angelina alimwacha mpenzi wake kwa ajili yake, moyo wake haukutaka kusahau hilo lakini bado alitakiwa kumwambia kile alichopanga kumwambia na si kukaa kimya na kuendelea kumsaliti.
“Kuna nini kwani?” aliuliza Angelina, tayari ukimya wa mpenzi wake ukaonekana kama kumtia hofu fulani.
“Kwanza naomba unisamehe!” alimwambia.
“Kwa lipi?”
“Kwa jambo baya ambalo nimekufanyia!”
“Jambo gani?”
“Nilikusaliti!” alimwambia.
Angelina akakaa kimya, akamwangalia mpenzi wake, tayari moyo wake ukasikia maumivu makali, wivu mkali ukamshika kwani hakutarajiwa kuambiwa kitu kama hicho na mtu kama Edmund, mwanaume ambaye alijitolea kwa moyo wake wote kumpena.
Leo, alimwambia kwamba alimsaliti! Lilikuwa jambo baya mno kuambiwa na mwanaume, alitamani muda huo angekuwa hata anaota, aamke na kuona kumbe alikuwa kwenye usingizi mzito, ila kile alichoambiwa, hakikuwa ndoto.
“Na msichana wa chuoni?” alimuuliza.
“Ndiyo! Naomba unisamehe sana!” alimwambia.
Angelina akanuna na kuelekea pembeni, akasimama karibu na dirisha na kuanza kuangalia nje. Hapakuwa na mtu aliyemwamini kama Edmund, alimpa kila kitu alichokitaka, alimpenda na kumthamini lakini bila aibu, leo mwanaume huyo alimwambia alimsaliti, yaani alisikia maumivu ambayo hakuwahi kuyasikia.
“Angelina...” aliita Edmund huku akimsogelea, akamshika kwa nyuma.
“Niache!” alisema msichana huyo kwa hasira.
“Najua! Nitakuacha ila naomba unisamehe kwanza,” alimwambia.
Maneno hayo kidogo yalimshtua Angelina, aliposema kuachwa alimaanisha asishikwe lakini yale aliyoyazungumza Edmund yalimaanisha kulikuwa na kitu alichokipanga mahali hapo, ikambidi amgeukie.
“Umesemaje?” aliuliza.
“Usaliti umeleta mimba, mimba ikaleta mtoto,” alimwambia.
“Yaani sijakuelewa. Umesema mimba na mtoto?” aliuliza Angelina.
“Naomba unisamehe sana!”
“Umempa mimba mwanamke mwingine?”
“Ndiyo!”
“Yaani sijakue....” alisema lakini hata kabla ya kumaliza sentensi yake ikambidi anyamaze na kuanza kulia kama mtoto.
Edmund alijitahidi kumbembeleza na kuendelea kumuomba msamaha lakini Angelina hakubembelezeka kabisa. Aliendelea kusikia maumivu moyoni mwake, hakuamini mtu kama Edmund angeweza kumsaliti na mwanamke mwingine, angempa mimba na kujifungua.
Kulikuwa na usaliti mbalimbali kwenye dunia hii lakini ule aliofanyiwa yeye, aliamini ulikuwa mkubwa na haukuweza kusameheka hata kidogo. Mtu kama Edmund, alimsalitije na wakati kila siku alipokuwa akimpigia simu alimwambia ni kwa jinsi gani alimpenda?
“Why?....why?...why?” (Kwa nini?...Kwa nini?...Kwa nini?) aliuliza msichana huyo huku akilia.
“Najua nimekuumiza sana, unanipenda mno, umenionyesha kila aina ya mapenzi, lakini malipo yake yamekuwa maumivu makubwa mno. Naomba unisamehe! Naomba nijihukumu, nikuache na uendelee na maisha yako, sistahili kuwa mpenzi wako,” alisema Edmund huku akimwangalia Angelina aliyekuwa akiendelea kulia.
Alitamani kuongea maneno mengi lakini alishindwa, kila alipokuwa akijaribu kufanya hivyo, alikuwa akiangua kilio tu. Edmund alihuzunika, aliumia kwani aliona kabisa Angelina hakutakiwa kuumizwa hivyo lakini hakuwa na jinsi, ilikuwa ni lazima amwambie ukweli, huo ndiyo ulikuwa uanaume.
“Naomba unisamehe!” alisema Edmund, akaanza kupiga hatua kuufuata mlango, alipoufikia tu, akaufungua na kuondoka zake, hakutaka kuendelea kubaki humo.

Je, nini kitaendelea?
 
Sehemu ya 27

Angelina alibaki peke yake chumbani, hakuamini kumuona Edmund akiondoka zake, alimpenda mwanaume huyo, alikuwa kila kitu kwake. Kipindi cha nyuma aliwasikia tu watu waliokuwa wakimwambia maumivu ya mapenzi yalikuwa makubwa mno, yaliumiza kuliko hata kuchomwa na mkuki moyoni lakini alibisha.
Sasa siku hiyo ndiyo alikuwa akiyasikia maumivu hayo, hakuwahi kuyasikia hapo kabla, alihuzunika na kulia lakini mwisho wa siku alitakiwa kukubaliana na kile kilichotokea kwamba Edmund alimsaliti kwa kutembea na mwanamke mwingine, hiyo akaona haitoshi, akampa mimba kabisa na kumzalia mtoto.
Aliiona dunia ikiwa kichwani mwake, ilimwelemea mno, alitamani kuitua lakini alishindwa, alijiona kama ameacha peke yake jangwani bila msaada wowote ule. Hapo akagundua kwamba kifo kilikuwa kitu muhimu kuliko uhai, hakuona kama angeendelea kuishi bila Edmund, yale maumivu aliyoachiwa aliamini yangekwisha endapo tu angeamua kujimaliza.
“Siwezi kuishi....siwezi kuishi.....” alisema Angelina, hakutaka kubaki ndani ya chumba hicho, akakurupuka na kuanza kukimbia kuelekea nje, lengo lake kubwa lilikuwa ni kujimaliza tu.
Alikimbia kwa kasi, kila mtu aliyekuwa akimuona alimshangaa, alionekana kama mtu fulani aliyechanganyikiwa ama kutupiwa mapepo, alikuwa akilia, alikimbia mpaka alipofika karibu na duka la dawa na kumwangalia dada aliyekuwa akiuza, naye alikuwa akimshangaa.
“Karibu,” alimkaribisha.
“Nahitaji dawa.”
“Dawa gani?”
“Panadol za elfu mbili na Korokwini za elfu tatu,” alijibu Angelina.
Kwa kiasi alichotaja kilikuwa kikubwa mno, kwa wauzaji wa maduka ya madawa hawakutakiwa kumuuzia mteja kiasi hicho cha dawa, na kama aliruhusiwa basi ilikuwa ni lazima mgonjwa aonyeshe kibali cha daktari ambacho kingeonyesha kuruhusiwa kununua dawa za namna hiyo.
“Huwa hatuuzi kwa viwango vikubwa namna hiyo,” alimwambia.
“Nahitaji dada yangu! Naomba unisaidie!” alisema Angelina huku akilia.
“Hapana! Labda uje na kibali cha daktari, vinginevyo haiwezekani!” alisema dada huyo.
Angelina aliona kama anacheleweshwa, akaamua kuchomoka dukani hapo, kitu kilichomjia kichwani ni kwenda kununua dawa ya panya na ikiwezekana anywe na kufariki dunia.
Alianza kutembea kwenye maduka mbalimbali Kinondoni lakini hakufanikiwa kupata dawa ya panya. Kadiri alivyokuwa akitembea kutafuta dawa hizo, kule kutembea kwake, hasira zake zikamfanya kuanza kufikiria mara mbili juu ya kile alichotaka kukifanya, yaani akili yake ikaanza kurudi.
Alitembea kuanzia Kinondoni Manyanya mpaka Mkwajuni, mwisho wa siku akajikuta akikaa kwenye kibanda kimoja kilichokuwa mahali hapo na kuanza kufikiria.
“Nijiue? Yaani nijiue kwa sababu ya mwanaume?” alijiuliza.
Alipojiuliza maswali hayo, majibu yakawa ya aina moja kwamba alikuwa akifanya ujinga mmoja mkubwa sana. Yaani ajiue kwa sababu ya mwanaume ambaye wakati huo angeendelea kutanua maisha yake kama kawaida? Akaona ni ujinga.
Alipoiona Bajaj moja, akaisimamisha na kumwambia ampeleke nyumbani kwao. Macho yake yalikuwa mekundu kutokana na kulia sana, akiwa njiani, akaanza kukumbuka kile kilichotokea mule chumbani.
Moyo wake ukazidi kuuma lakini ghafla tu picha ya Amon siku ile aliyokuwa amemuacha kwa sababu ya Edmund ikaanza kumjia kichwani mwake. Hapo akaanza kujisikia vibaya, akayajua yale maumivu yaliyomfanya Amon kumlilia sana siku ile, yale maumivu aliyoyasikia kijana huyo ndiyo ambayo leo hii alikuwa akijisikia.
Wakati mwingine akahisi ilikuwa ni afadhali kwake, aliambiwa na Edmund kwamba alimsaliti kwa kutembea na mwanamke mwingine na kuzaa naye, hilo halikutakiwa kumuuma sana kwani hakuwa na uhakika kama alifanya hivyo kweli ama la.
Kwa Amon ilikuwa ni maumivu makali kwa sababu alimwacha huku akiwa na mwanaume mwingine, tena aliongea kwa maneno ya dharau, hiyo haikutosha, aliamua kuonana naye tena kwenye mgahawa na kumwambia vilevile kwamba hakuwa akimuhitaji.
Kama yeye alimfanyia hivyo Amon na kijana huyo kuendelea na mambo yake, hakujiua kama alivyotaka kufanya, kwa nini na yeye asiendelee na maisha yake kama kawaida na kuachana na mpango wake wa kujiua?
“Ila yeye ni mwanaume, moyo wake mpana,” alijiambia.
Ni ndani ya dakika kadhaa akafika nyumbani kwao, kwa jinsi mama yake alivyomwangalia usoni tu, alijua kulikuwa na kitu, alionekana kubadilika na macho yake yalikuwa mekundu mno.
Mama yake akashtuka na kumuuliza tatizo lilikuwa nini, akamwambia ukweli kwamba mpenzi wake, Edmund alimwacha baada ya kuzaa na mwanamke mwingine. Mama yake mwenyewe hakuamini alichokisikia. Alimfahamu Edmund, alikuwa kijana mpole na aliyempenda sana binti yake, sasa iweje amsaliti kwa kutembea na mwanamke mwingine na kuzaa naye?
“Edmund amempa mimba mwanamke mwingine na kuzaa naye?” aliuliza mwanamke huyo.
“Ndiyo mama!”
“Pole sana! Yaani ameamua kuzaa na mwanamke mwingine?”
“Ndiyo mama! Mama nitakufa,” alimwambia kwa sauti ndogo, alisikia maumivu kupita kawaida.
“Huwezi kufa binti yangu! Huwezi kufa!” alisema mama yake.
Huyo ndiye alikuwa mfariji wake mkubwa, alimfariji sana na kumwambia kwamba huo haukuwa mwisho wa maisha yake, ilikuwa ni lazima akubaliane na kilichotokea na kuendelea kuishi kama kawaida.
Aliambiwa kulikuwa na watu wengi waliokuwa wakiachwa lakini kamwe hawakuthubutu kujiua, sasa kwa nini yeye ajiue?
“Sahau kila kitu! Anza upya!” alisema mama yake, hata kumpigia simu Edmund hakutaka.
Kuanzia siku hiyo Angelina hakuwahi tena kuongea na Edmund kwenye simu, mwanaume huyo hakuwa akipatikana, alibadilisha namba na kila alipokwenda nyumbani kwao aliambiwa hayupo. Moyo wake ulikuwa kwenye maumivu makali mno.
Hapo ndipo alipoanza kujuta kwa sababu gani alijiingiza kwenye mapenzi. Akahisi kabisa watu ambao hawakuwa kwenye mahusiano ya kimapenzi inawezekana walikuwa na maisha mazuri kuliko yake, akaanza kuwa na msongo wa mawazo.
Mawazo yalimpeleka puta, japokuwa alipanga kuendelea na maisha yake bila Edmund lakini aliona kabisa lilikuwa suala gumu mno. Kwa kipindi cha wiki ya kwanza tu, mawazo yakampelekea kuanza kupungua.
Kila mtu aliyemuona alimshangaa, huyu Angelina alianza kupungua kwa kasi kubwa, watu wakajua kulikuwa na tatizo mwilini mwake, inawezekana alikuwa akiumwa, hapakuwa na mtu aliyejua kama msichana huyo aliachwa, mawazo juu ya mpenzi wake yalimfanya kuwa hivyo alivyokuwa.
Angelina alitamani kuonana na Edmund na kuzungumza naye lakini hata chuoni hakuwa akimuona kitu kilichomchanganya kupita kawaida. Alitakiwa kuzoea kuishi bila Edmund, ni kweli alimpenda lakini mwenzake hakuwa na muda naye, alimwambia alizaa na mwanamke mwingine hivyo walitakiwa kuachana.
Chuoni watu wakaanza minong’ono kwa kusema msichana huyo alikuwa akiugua mmoja wa magonjwa sugu, kama si UKIMWI basi alikuwa na kansa yoyote mwilini mwake kwani alipungua sana. Pamoja na wanafunzi wenzake kuongea mambo mengi lakini hakutaka kuufumbua mdomo wake na kuwaambia kilichotokea.
Kila siku alijiamini, aliamini alikuwa msichana mrembo, wanaume walimbabaikia, walimuona kuwa kama malaika sasa ingekuwaje endapo angewaambia alisalitiwa? Yaani kwake kitu hicho hakikuwa rahisi hata kidogo kwa kuwa angedharaulika.
Wasichana ambao aliwaona kuwa wa kawaida walidumu kwenye mapenzi yao na mwisho wa siku kuolewa, yeye aliyekuwa mrembo aliachwa kwenye mataa, tena baada ya mpenzi wake kutembea na mwanamke mwingine.
Hakika moyo ulichoma mno. Baada ya mwezi mmoja huku akiwa anapelekeshwa na mawazo ndipo hapo akaanza kusikia kuhusu mashindano ambayo Tanzania ilikuwa ikienda kushindana, huko, Amon naye alikuwa mmoja wa wachezaji ambao wangeichezea timu hiyo.
Alijaribu kuwasiliana na kaka yake, Gideon alimwambia asingekuwepo kwa kuwa aliamua kuichezea Ujerumani. Alishangaa, hakutegemea kaka yake kuchukua uamuzi kama huo. Wazazi wake walishangaa, hawakujua kile ambacho wangekwenda kuwaambia Watanzania.
Ni kweli walikuwa na maisha mazuri, pesa za kijana wao ziliwafanya kununua jumba la kifahari, waliishi maisha mazuri, waliendesha magari japokuwa Angelina hakutaka kabisa kumiliki gari kutokana na foleni kubwa za jijini Dar es Salaam.
Leo, huyo Gideon aliwaambia alitaka kuichezea Ujerumani, yaani ilimaanisha hakutaka kuwa Mtanzania tena, waliumia ila hawakuwa na jinsi. Kwa Angelina, hayo yalikuwa maumivu mengine kabisa.
Kwa sababu alikuwa na mawazo tele, akaamua kuanza kujichanganya na watu ili asiwe na mawazo lakini kitu kilichomumiza zaidi ni kuwa muda huyo kila mtu alikuwa bize na mambo ya mpira, yaani alikuwa akizungumziwa Amon tu.
Hakuwaambia watu kama aliwahi kuwa na uhusiano na kijana huyo, alihisi angeonekana mjinga, ilikuwaje uwe na uhusiano na mtu kama Amon halafu umuache, yaani aliamini pale ambapo angewaambia watu kama aliamua kuachana naye, basi wao wangemchukulia Amon huyo na si yule wa nyuma.
Huo ndiyo ulikuwa muda wa kujutia kila kitu kwa alichokifanya kwa Amon, alitamani kumfuata na kumuomba msamaha kwa kilichotokea lakini hakuamini kama angemsamehe kutokana na vile alivyomuumiza.
Akaulizia ratiba ya wachezaji kufika nchini Tanzania, akaambiwa na siku ambayo Amona alishuka ndani ya ndege, akajitahidi kumfuata lakini alishindwa, kulikuwa na watu wengi, mpaka anapanda ndani ya gari, hakufanikiwa.
Ilimuuma sana, hakumuona tena kwa kuwa watu hawakutakiwa kuwasiliana na wachezaji kwani wangeweza kuwaondoa mchezoni, mpaka wanaondoka na kuelekea Morocco, hakuwa amefanikiwa.
Alikaa na kumfuatilia Amon kwenye mechi zote alizokuwa akicheza, hakupenda mpira lakini kwa jinsi alivyokuwa akicheza, akajikuta akipenda kuangalia mpira, hasa Amon anapokuwa uwanjani.
Alifuatilia mpaka mashindano yalipomalizika hivyo timu kurudi nchini Tanzania. Alitamani kumuona, kama kawaida yake akaenda uwanja wa ndege, ili wachezaji watakapotua tu basi amuone, tena alitaka kumuita mpaka jina lake.
Yaani siku hiyo ilikuwa ni afadhali ya siku ile, kulikuwa na watu wengi mno na aliambiwa wengine walikuwa uwanjani, kama kweli alitaka kuonana na mtu kama Amon, basi aende uwanjani.
Hakuwa na jinsi, alikuwa na kiu na hivyo kwenda huko. Hapakuwa na uafadhali, lingekuwa jambo jepesi zaidi kama kaka yake angekuwepo, angetumia mgongo wake kwenda kuonana naye, ila kaka yake hakuwepo, akazidi kuumia zaidi.
Siku hiyo hakufanikiwa kabisa, akaamua kuachana naye na hivyo kupanga kumfuata hotelini ama nyumbani kwake. Kwa kuwa alitaka kumuona mwanaume huyo, basi njia nzuri ambayo alitakiwa kuitumia ni kuonana na wazazi wa Amon na kuwauliza kuhusu yeye.
Akaelekea mpaka nyumbani kwao, akakuta nyumba ikiwa imebomolewa na kujengwa nyingine kubwa na nzuri, alipoulizia, akaambiwa watu hao walihamia Mbezi Beach na mahali hapo kujenga nyumba nyingine na kuhama. Akataka kuelekezwa, akaelekezwa.

Je, nini kitaendelea?
 
Sehemu ya 28

Hakutaka kupoteza muda, akaondoka na kuelekea huko Mbezi Beach, alipofika, akaonana na mzee Stefano na mkewe, akakaribishwa na kuingia ndani. Muda wote alikuwa akijishtukia tu ila hakujua kama wazazi hao walifahamu kilichotokea ama la, alipanga kama asingeulizwa basi naye angewachukulia kama hawakuwa wakijua lolote lile.
Alikaribishwa kwa furaha, akapewa juisi, akanywa na kuanza kupiga nao stori. Akawauliza mahali alipokuwa Amon, akaambiwa hakuwa akiishi hapo, aliondoka na kwenda kuishi sehemu nyingine.
“Wapi?” aliuliza.
“Wewe wa nini?” aliuliza mzee Stefano.
“Gideon aliniambia ana mzigo wangu alikuja nao, ndiyo nimekuja kuuchukua,” alidanganya.
Hapakuwa na mtu aliyepinga, ni kweli inawezekana Amon alikuja na mzigo wake, hivyo wakamuelekeza na kuelekea huko mpaka alipokutana na Amon, wote wakabaki wakiangalia, hata kaka yake, James alimshangaa msichana huyo, ilikuwaje awe mahali hapo na wakati alimuacha mdogo wake?
“Karibu sana,” alisema Amon huku akimwangalia msichana huyo, alifanya kama hapakuwa na baya lolote lile lililowahi kutokea.
Msichana huyo akaanza kuingia ndani, alijishtukia, hakuwa na furaha lakini kwa kipindi hicho alitakiwa kumuomba msamaha Amon kwa kile kilichotokea. Akaingia mpaka sebuleni na kukaa kwenye kochi.
“Za masiku?” alisalimia Amon.
“Salama tu!” alijibu.
Hakuwa na cha kusema, huyo Amon kwa jinsi alivyoongea ni kama hapakuwahi kutokea kitu chochote kile, aliongea kikawaida kabisa kitu kilichomfanya Angelina kuumia zaidi.
“Nimekuja kukuomba msamaha Amon,” alisema Angelina huku akimwangalia Amon, tena machozi yakaanza tena kumtoka kama kujutia kwa kile alichokifanya.
“Kuniomba msamaha?”
“Ndiyo!”
“Kwa kosa gani tena?” alimuuliza.
“Kwa yote niliyoyafanya, nimekuumiza sana!”
“Haukunikosea Angelina!” alimwambia, msichana huyo akainamisha uso wake na kuanza kulia kilio cha kwikwi. Amon akasimama na kumsogelea pale alipokuwa, akakaa pembeni yake na kuupitisha mkono begani kwake kama mtu aliyekuwa akimbembeleza.
“Wakati mwingine tunatakiwa kufanya maamuzi yetu bila kujali ni wangapi wataumia, unapotaka kuchukua uamuzi ambao unaamini kwako ni sahihi, uchukue bila kusitasita Angelina.
“Ni bora uonekane mbaya kwa kitu ambacho unaamini upo sahihi. Inafika wakati hatutakiwi kujali maumivu ya watu, kujali huruma za watu. Unajua ukiwa mtakatifu sana kwenye dunia hii utaongoza kwa kuumia kila siku kwa kuwa utataka watu waishi hivi, wao wataishi vile.
“Wakati wewe unamuonea mtu fulani huruma mpaka hutaki kuchukua uamuzi wako kwa kuwa tu ataumia, yeye akipata nafasi hiyo, atauchukua uamuzi huyo hata akijua kwamba utaumia. Unajua hapa nakufundisha nini?” alisema Amon na kuuliza.
“Hapana.”
“Hujanikosea! Ule ulikuwa uamuzi wako, wakati mwingine unatakiwa kuchukua uamuzi hata kama ningeumia kiasi gani. Sasa ingekuwa na maana gani kuendelea kuishi na mimi huku ukiwa hunipendi? Ungeniumiza zaidi, nadhani ningeumia zaidi ya nilivyoumia siku ile. Uliniokoa sana Angelina, ulinijali na ndiyo maana uliniambia ukweli, yaani kwa kifupi naweza kusema wewe ni Mwanamke wa Chuma,” alimwambia, Angelina alikuwa kimya akimsikiliza.
“Kuwa kwenye mapenzi na mwanaume mwingine huku ukiendelea kuwa nami, hapo ungekuwa umenikosea sana ila kuniacha! Hapana, hujanikosea ila ulifanya kile ulichokuwa ukikiona kuwa sahihi! Shemeji anaendeleaje lakini? Umekwishaanza chuo? Bado una ndoto za kuwa...za kuwaaaa....kuwa nani vile?”
“Daktari wa misuli!”
“Yeah! Ila nalitafuta lile jina lake la kitaalamu!”
“Cardiologist!”
“Yup! Hilo jina ndilo lilinitoka. Bado una ndoto hizo?”
“Yeah! Bado ninazo!”
“Soma sana! Ila nitajaribu kuzungumza na Gideon japo uende ukasomee Ujerumani, nadhani kule ni vizuri kuliko Tanzania,” alisema Amon, yaani aliongea kama mtu ambaye hakuwa na kinyongo chochote kile.
“Nitazungumza naye, ila ukianza kuzungumza naye ni vizuri zaidi!” alisema Angelina.
“Wala usijali! Nitafanya hivyo. Ila hujaniambia kuhusu mtu wako!”
“Tumeachana!”
“Mmeachana! Kwa maridhiano?”
“Hapana! Ameniacha!”
“Pole sana! Naona umepungua sana, punguza mawazo, ishi kwa furaha Angelina. Maisha ni safari ndefu sana, usitake kuona mapenzi yakikatisha ndoto zako. Mtu amekuacha, achana naye fanya mambo mengine,” alimwambia.
“Kila nikijaribu ninashindwa. Wewe uliwezaje?” aliuliza, sasa alimzoea, akawa kama anaongea na rafiki yake.
“Ilikuwa vigumu sana ila baba yangu aliniambia kwanza nikubaliane na kilichotokea, cha pili niusikilize mpango wa Mungu juu ya maisha yangu,” alijibu Amon.
“Mh!”
“Mbona unaguna?”
“Nitaweza kweli?”
“Hakuna kinachoshindika...ila tu ukiamua! Hebu simama kwanza,” alimwambia, naye akasimama.
Akamkumbatia!
“Jitie nguvu! Bado una safari ndefu sana mbele yako, hutakiwi kukata tamaa mapema. Kuna watu wengi wanakuangalia, ukianza kukata tamaa wewe, nao wafanyeje?” alimuuliza.
“Nitajaribu!”
“Nitashukuru!”
Amon hakutaka kumuonyesha utofauti wowote ule, aliamini msichana huyo alipitia mengi ya kujifunza na ndiyo maana siku hiyo alikuwa mahali hapo kumuomba msamaha.
Mtu anapokufanyia kosa, kulalamika ama kumtukana na kukataa kuzungumza naye unamfanya kuwa mshindi, anaamini amekuumiza na kukuwekea kidonda kikubwa moyoni mwako ila unapoamua kuchukulia kila kitu kawaida, yale ambayo ulitakiwa kuyapata wewe basi ilikuwa ni lazima ayapate yeye, maumivu yale ayasikie yeye. Ndivyo ilivyokuwa kwa Angelina.
Kitendo cha Amon kuwa mwema kwake kilimuumiza mno, kilimfanya kujisikia vibaya mno, hakumuonyesha hasira wala hali yoyote ile, hilo likamfanya kwa na deni kubwa moyoni mwake na kumfanya kukosa amani kabisa.
Walizungumza kwa dakika kama arobaini baada ya hapo Angelina akaaga, akaamua kumchukua na kumpeleka nyumbani. Ingekuwa rahisi sana wapitie hata mgahawani kula lakini hakuweza.
Hakuwa Amon wa kipindi cha nyuma, alikuwa maarufu mno, popote pale ambapo angeonekana, watu wangekusanyika na kutaka kumpiga picha, na wengine wangempiga picha, ingekuwaje hilo kutokea na picha kuonekana kwa Jeniffer? Angejitetea nini?
Hakutaka kufanya ujinga huo, aliamua kumsindikiza nyumbani kwao, alipotoka huko, akapitia gym, akafanya mazoezi na kurudi nyumbani, sasa alitakiwa kujiandaa na safari ya kurudi Ujerumani siku inayofuata.

Je, nini kitaendelea?
 
Sehemu ya 29.

“Halo! I want to meet you,” (Halo! Ninataka kukuona!) ilisikika sauti kutoka upande wa pili wa simu.
“Who are you?” (Wewe nani?)
“Dawson Dennis!”
“Dawson?”
“Yup!”
“What do you want?” (Unataka nini?)
“Just to see you! I know I did you wrong, may I see you?” (Kukuona tu! Najua nimekukosea, naweza kukuona?) aliuliza mwanaume aliyekuwa upande wa pili.
“Impossible!” (Haiwezekani)
Yalikuwa ni mazungumzo baina ya Jeniffer na mwanaume aliyejitambulisha kwa jina la Dennis Dawson. Alizungumza naye kidogo tu na kisha kumkatia simu.
Alimkumbuka mwanaume huyo, alikuwa mmoja wa watu ambao aliwahi kuingia nao kwenye uhusiano wa kimapenzi. Kipindi cha nyuma alimpenda sana, alikuwa mwanaume wake wa ndoto ambaye aliamini kuna siku moja tu wangekuja kuoana na kuishi pamoja.
Jeniffer aliweka tumaini lake lote kwa Dawson, alimpenda na alikuwa kila kitu kwake lakini baada ya kupanga mipango ya kufunga ndoa, akaachwa na mwanaume huyo baada ya kurudi nyumbani kwao nchini Marekani kwa ajili ya kumuoa mwanamke mwingine.
Moyo wa Jeniffer uliumia mno, hakuamini kama mwanaume huyo angeweza kumuacha kwa kuwa tu alimkumbuka msichana aliyewahi kuwa mpenzi wake na kurudi Marekani.
Aibu kubwa ikampata, aliwahi kuwaambia marafiki zake kuhusu Dawson, kwamba alikuwa mwanaume wa kipekee na walikuwa wakitarajia kufunga ndoa, ila la ajabu kabisa, ndoa ikafa na mwanaume huyo kutoweka.
Alichanganyikiwa karibu na kuwa chizi, alikuwa na mawazo lukuki, moyo wake uliuma mno, majonzi yakawa sehemu ya maisha yake, aliumia na kulia kila siku. Alidhoofika mwili na kukonda kabisa.
Kila mtu aliyekuwa akimwangalia alijua tu kulikuwa na kitu kilichokuwa kikiendelea, haikuwa kawaida kwa mtu kama yeye kuwa vile, wazazi wake walishangazwa na hali yake na alipoulizwa, aliwaambia kuhusu Dawson.
Nao wakachukia, wakatokea kumchukia mwanaume huyo aliyemfanya binti yao muda wote kuwa na huzuni tele. Walihisi kama walikuwa na uwezo wa kumfundisha adabu lakini waliona kabisa hilo kuwa gumu kwa sababu huyo Dawson alikuwa mtoto wa tajiri mkubwa nchini Marekani.
Hawakujua la kufanya, walipoona wasingeweza kufanya lolote lile, wakaamua kuachana naye, wakawaita watu wa saikolojia kwa lengo la kuzungumza na binti yao na kumrudisha kwenye hali ya kawaida.
Haikuwa rahisi kwani moyo wake ulijeruhiwa sana ila mwisho wa siku, akafanikiwa kuwa kwenye hali ya kawaida, akawa anajichanganya na marafiki zake, hakutaka kumkumbuka tena Dawson, alimchukia na aliamua kuachana naye kwa asilimia mia moja.
Baada ya miaka miwili, leo alipokea simu kutoka kwa mwanaume huyo aliyemwambia alitaka kuonana naye, hakujua alikuwa akihitaji kitu gani kwani kama kuachana, waliachana na kila mmoja kuendelea na maisha yake.
Hilo lilikuwa jambo lisilowezekana hata kidogo, kwa mtu kama Dawson hakuwa wa kuonana naye hata kidogo, hakutakiwa kupata nafasi hiyo kabisa, hivyo akamkatalia na kukata simu.
Kwa upande wa pili baada ya Dawson kukatiwa simu, moyo wake ulimuuma mno. Alijua alifanya makosa kwa kumuacha msichana huyo na kumfuata mwingine ambae baada ya kuishi naye kwa miaka miwili, akagundua hakuwa na sifa kama alizokuwanazo Jeniffer.
Wazazi wake walimlazimisha kuwa na msichana huyo wa nyumbani kwao Marekani kwa kuwa wazazi wake pia walikuwa matajiri lakini baada ya kuwa naye kwa kipindi hicho, aligundua hakuwa mwanamke sahihi, si kwake tu bali hata kwa watoto wake.
Alitaka kuachana naye mapema lakini alishindwa kufanya hivyo, moyo wake ulimwambia kuna siku angebadilika na kuwa mwanamke mwema, mzuri, mnyenyekevu kwani ni ujana tu ndiyo uliokuwa ukimsumbua lakini hilo halikuweza kutokea. Badala ya kuboreka na kuwa mwanamke bora, ndiyo kwanza alizidi kuwa mbaya zaidi ya kipindi cha nyuma.
Kila siku ilikuwa ni lazima Dawson amuite Rachel na kuzungumza naye, alimwambia kuhusu tabia yake lakini msichana huyo hakutaka kabisa kujali, kwake alijona kuwa kawaida tu na hapakuwa na lolote la kumfanya kubadilika.
“Nitamuacha!” hilo ndilo alilolisema kila siku lakini alishindwa kulitekeleza. Alivumilia na kuvumilia na mwisho wa siku kuamua kufanya kweli.
Akamuacha.
Sasa akabaki peke yake, akaanza kuwakumbuka wanawake ambao aliwahi kuwa nao kwenye mahusiano ya kimapenzi, mtu ambaye alikuja kichwani mwake na kuona kulikuwa na umuhimu wa kumrudia alikuwa huyo Jeniffer, akaamua kumpigia simu kwa lengo la kuomba miadi naye.
Alijua alimfanyia mambo mabaya, lakini kama binadamu naye alihitaji kusamehewa, apewe nafasi ya pili na kubadilika, alitaka kuwa naye kama alivyokuwa naye zamani.
Alizungumza naye kidogo na kukatiwa simu, moyo wake ulimchoma mno, hakutaka kuona hilo likitokea, kwake ilikuwa kama dharau lakini hakuwa na jinsi, akaamua kusafiri kutoka Marekani na kuelekea Ujerumani, ilikuwa ni lazima kuonana na msichana huyo na kumuomba msamaha ana kwa ana.
“Naamini atanisamehe” alijisemea huku ndege ya Shirika la Ndege la American Airways lilikata mawingu kuelekea barani Ulaya.
Ndege ilichukua saa zaidi ya ishirini mpaka kufika katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Berlin, akateremka na abiria wengine na kuelekea hotelini kupumzika. Hakujua ni kwa namna gani angempata msichana huyo, alichokijua ni lazima atakuwa amehama na kuishi sehemu nyingine.
Kitu kilichokuja kichwani mwake haraka sana ni kumtafuta Glory! Huyo alikuwa rafiki mkubwa wa Jeniffer, alimpigia simu na kuomba kuonana naye. Glory alishangaa, hakuitegemea simu hiyo hata kidogo, alimjua Dawson, alimuona kuwa mwanaume katili kwa sababu tu alimuacha rafiki yake na kwenda kwa mwanamke mwingine.
“Unataka kuniona?” aliuliza Glory.
“Ndiyo!”
“Haiwezekani!”
“Glory! Najua mimi ni binadamu, si malaika kama mnavyonichukulia, wakati mwingine kufanya makosa ni sehemu ya uumbaji ambao Mungu ametupa,” alimwambia.
Alijua kuongea, kumshawishi mtu, japokuwa Glory hakutaka kuonana naye lakini mwisho wa siku akajikuta akikubali na kuonana naye kwenye mgahawa mmoja uliokuwa hapohapo Berlin.
Huko walikaa na kuzungumza, alichomwambia ni kwamba alitaka sana kuonana na Jeniffer, alijua dhahiri kwamba alimkosea, kwenye maisha yake alifanya makosa makubwa lakini lile kosa kubwa alilolifanya ni kumuacha msichana huyo.
Alimwambia ni kwa namna gani Jeniffer alikuwa mtu muhimu na wa thamani kubwa kwake, bahati mbaya alipewa upofu na kutokuiona thamani aliyopewa na msichana huyo. Sasa alikuwa akijuta, alijua alipojikwaa na alitaka kusimama tena.
“Sidhani kama ataweza kurudiana na wewe,” alimwambia.
“Kwa sababu gani?”
“Ulimuumiza sana!”
“Hilo si sababu! Kwani ana mtu?”
“Sijawahi kumuona na mtu!”
“Nadhani atakubali kuwa nami tena. Moyo unaniuma sana, nilikuwa mpuuzi zaidi ya wapuuzi wote kwenye dunia hii,” alisema Dawson.
Glory hakuwa akijua kitu kuhusu rafiki yake kama alikuwa kwenye uhusiano wa kimapenzi na Amon, ilikuwa siri kwake, hakutaka kumwambia mtu yeyote kwa kuamini labda kwa kufanya hivyo angeolewa na kuwa mke.
Alijitahidi kunyamaza na ndiyo maana hata Glory alipoulizwa kuhusu rafiki yake huyo alisema hajui kuhusu kuwa na uhusiano na mwanaume mwingine.
Baada ya kuzungumza na Dawson, Glory akaondoka kwa lengo la kwenda kuonana na Jeniffer na kumwambia kuhusu Dawson, akampigia simu msichana huyo, alipoipokea, akaanza kuzungumza naye, ila hakumwambia kuhusu Dawson.
Waliongea suala la kawaida na kusema alikuwa na hamu ya kwenda kumsalimia alipokuwa. Hilo halikuwa tatizo, akamruhusu msichana huyo na baada ya dakika kadhaa kwenda kuonana.
Wakaanza kuzungumza. Jeniffer alikuwa mjauzito lakini tumbo lake halikuanza kuonekana, alionekana kuwa kawaida kabisa. Wakaanza kuongea mambo mengi na mwisho kumwambia kuhusu Dawson.
“Ulionana naye?”
“Ndiyo! Nimezungumza naye, yaani ameniambia mambo mengi mno!”
“Yapi hayo?”

Je, nini kitaendelea?
 
Nyemo Chilongani
Ulimwengu Ndotoni Mwangu
0718069269

Sehemu ya 30.

Glory akaanza kumwambia Jeniffer kila kitu alichokuwa amezungumza na mwanaume huyo, kuhusu namna alivyoondoka zake kuelekea Marekani kwa kuwa wazazi walitaka kumuoa msichana mwingine.
Alivyofika huko, akaanza kuishi naye kwenye uhusiano, alimpenda lakini baada ya muda fulani akahisi kabisa hakuwa msichana wake sahihi kwa kuwa hakuwa akiyapata yale yote aliyoyapata kutoka kwake.
Akatafuta njia ya kumuacha, ilikuwa vigumu kwa sababu wazazi wake walikuwa sehemu ya uhusiano huo, aliteseka mno lakini mwisho wa siku akaamua kusimama kama mwanaume na hivyo kuamua kumuacha kinguvu.
Baada ya hapo ndipo akaanza kuwakumbuka watu aliowahi kuwa nao kwenye uhusiano, kwa wote hao, mtu sahihi aliyekuja kwake alikuwa huyo Jeniffer na ndiyo maana leo alikuwa nchini Ujerumani kwa lengo la kuonana naye, azungumze naye na kuwa kama zamani.
“Kwa sasa haiwezekani kabisa,” alisema Jeniffer huku akimwangalia Glory.
“Jeniffer! Nimezungumza na Dawson, yaani anaonyesha kabisa kujutia alichokifanya, yaani ungeonana naye ungeligundua hilo. Naomba umsamehe!” alisema Glory.
“Nimekwishamsamehe!”
“Kwa hiyo upo tayari kurudiana naye?”
“Hapana!”
“Hata kuonana naye?”
“Ndiyo! Sipo tayari!” alimwambia.
Glory aliumia sana, hakujua kilichokuwa kikiendelea nyuma ya pazia, kubwa zaidi alianza kumuona rafiki yake akiwa anazingua, mtu kama Dawson, mwanaume ambaye mwisho wa siku aliamua kurudi na kuomba msamaha, alitakiwa kusamehewa kwa kuwa angebadilika na kuwa mtu mwema.
Msimamo wa Jeniffer haukubadilika, ulikuwa uleule kwamba hakutaka kurudiana naye. Moyoni mwake alikuwa na amani, furaha kwa kuwa alikuwa na mtu aliyempenda kwa mapenzi ya dhati na kubwa zaidi alikuwa na mimba yake.
Glory hakuwa na jinsi, akamtafuta Dawson, wakaonana na kumwambia kile kilichotokea kwamba Jeniffer alikataa katakata kurudiana naye kwani alikuwa na maisha yake mengine kabisa.
“Kwani ana mtu?” alimuuliza.
“Sidhani! Endapo angekuwa na mtu angeniambia tu!”
“Sasa tatizo nini? Au hukumwambia kwamba nimetubu na sitorudia tena kufanya ule upumbavu?”
“Vyote nilimwambia!”
“Sasa kwa nini amekataa?”
“Nadhani ni msimamo wake. Ila si unajua watoto wa kike, jaribu kuonana naye, nadhani atakubali. Ngoja nikuelekeze anapoishi kwa sasa,” alisema Glory, na bila shaka akaanza kumuelekeza mwanaume huyo alipokuwa akiishi Jeniffer.
Dawson hakutaka kushindwa, aliamini huyo Jeniffer ndiye alikuwa msichana wa ndoto zake, hata kama hakuwa akitaka kwa wakati huo aliamini ingetokea siku moja angekubali kuonana naye na kurudiana.
Alitakiwa kupambana kama mwanaume, hakuwa radhi kuona Jeniffer akiolewa na mwanaume mwingine zaidi yake, ilikuwa ni lazima kupambana kiume na mwisho wa siku ampate na kumuweka kwenye himaya yake kama kawaida.
Akaanza kumtafuta kivyakevyake kwa kwenda katika nyumba aliyokuwa akiishi, ilikuwa moja ya nyumba kubwa na ilikuwa kwenye mtaa wa kitajiri. Kwa Dawson hakutaka kuwa na hofu juu ya hilo kwani msichana huyo alitoka kwenye familia ya kitajiri mno.
Baada ya dakika kadhaa kulisimamisha gari mbali kidogo na nyumba hiyo, akaliona gari la Jeniffer likiingia ndani ya himaya la jengo hilo, haraka sana akateremka akiwa na maua mkononi, hata kabla ya geti kujifunga, akaingia na kuanza kulifuata gari la msichana huyo ambalo tayari nalo liliingia nani ya nyumba hiyo huku mkononi mwake akiwa na maua kwa lengo la kumuomba msamaha.
Jeniffer hakutegemea kumuona mwanaume huyo mahali hao, alishtuka, akawa anamwangalia mara mbili mbili kama ni yule aliyekuwa akimfahamu ama alikuwa mtu mwingine. Dawson alimwangalia Jeniffer huku akiwa kwenye hali fulani ya kutaka kuonewa huruma, hapohapo akaanza kumsogelea huku akiwa na maua yake kwa lengo la kumuomba msamaha.
Kitu cha kwanza kabisa kukifanya kilikuwa ni kupiga magoti mbele yake huku akimnyooshea mkono uliokuwa na maua kwa lengo la kuyachukua na kumsamehe kwa kila kitu alichokifanya miaka ya nyuma. Alimsamehe mwanaume huyo kitambo sana lakini kitu ambacho hakutaka kabisa kukiona ni kurudi kwenye uhusiano ambao alijiahidi asingeweza tena.
Kama kuhuzunika, alihuzunika sana, kama kulia alilia sana, hivyo vyote vilitosha na kitu alichokihitaji kwa nguvu zote kilikuwa ni mapenzi, furaha na amani, vyote hivyo alivipata kwa Amon, hakuona kama kulikuwa na uhitaji mwingine wa kutaka vitu hivyo kutoka kwa mtu mwingine.
“Naomba unisamehe Jeniffer, nilikuumiza, nilikuwa mpumbavu sana kuwasikiliza wazazi wangu ambao waliniacha nikiteseka katika mtego mkubwa niliouingia,” alisema Dawson huku akimwangalia msichana huyo, Jeniffer alibaki akiwa amesimama, hakujua kitu cha kusema kwanza, alitaka kumsikiliza.
“Nilipata kila kitu kutoka kwako! Nilipoondolewa niliamini haya huko ambapo nilikwenda basi ningepata kila kitu kama ilivyokuwa kwako, niliteseka sana, niliiona dunia kuwa chungu, naomba unisamehe Jeniffer, dunia imenifundisha,” alisema Dawson huku akimwangalia Jeniffer.
“Dawson! Naomba usimame!” alisema Jeniffer huku akimuinua mwanaume huyo ambaye alisimama, wakaanza kuangalian usoni, wakati huo Dawson alikuwa akilengwa na machozi ambayo baada ya sekunde chache tu yakaanza kutiririka.
“Nilikusamehe zamani sana!” alimwambia huku akimshika mkono.
“Najua ni wazazi wako ndiyo waliamua hivyo, ulikuwa ukinipenda sana, tulikuwa na ndoto pamoja lakini wazazi wako wakaingilia, wakanipokonya wewe kutoka mikononi mwangu, hakika niliumia sana, nililia usiku na mchana,” alisema Jeniffer na kunyamaza kwanza, yale yaliyotokea kipindi cha nyuma yakaanza kujirudia kichwani mwake.
“Naomba unisamehe sana kwa kukuumiza,” alimwambia.
“Nilikusamehe tangu zamani, nisingekuwa nimekusamehe sidhani kama ningeendelea kusimama hapa nilipokuwa,” alimwambia huku akimwangalia.
“Nashukuru sana! Nakuhitaji Jeniffer, ninakuhitaji sana maishani mwangu!”
“Najua unanihitaji! Ila sina tena nafasi ya kukuingiza moyoni mwangu!” alimwambia.
“Kwa sababu gani?”
“Kuna mtu ambaye tayari ameingia kwenye ule moyo uliouacha! Naomba unisamehe kwa hilo. Tubaki tu kuwa marafiki, tushauriane kwenye mambo mengine kama hutojali,” alisema Jeniffer huku akimwangalia.
Kulikuwa na maneno mengi sana aliyowahi kuambiwa maishani mwake ambayo yalimuumiza mno lakini kwa yale aliyokuwa akiambiwa kipindi hicho, hakika yalimuumiza kuliko maneno yote aliyowahi kuambiwa.
Alimwangalia Jeniffer, msichana huyo alikuwa mrembo hasa, alimpenda na alitamani sana kuwa naye lakini alimwambia ilishindikana kwa sababu tayari alikuwa na mwanaume mwingine. Hakutaka kuona hilo likitokea, alitamani kuwa na Jeniffer tu, hakutaka kusikia kitu chochote kuhusu huyo mwanaume mwingine.
Alinyamaza! Aliangalia chini, machozi yakaanza kumtoka, ya sasa hivi hayakuwa ya kutaka kuonewa huruma bali yalikuwa machozi yaliyokuwa na maumivu makali moyoni mwake. Alitamani hata muda urudi nyuma, kipindi kile alichokuwa na msichana huyo na kuwakatalia wazazi wake lakini hakuweza kufanya hivyo.
“Jeniffer!”
“Dawson! Nashukuru sana kwa kipindi chote nilichokuwanacho, hakika ulikuwa mwanaume mwema sana kwangu, ulinifundisha maisha, namna ya kujiamini na pia ukanifundisha kuhusu mapenzi!” alimwambia.
“Jeniffer!”
“Sitoweza kuwa nawe! Naomba unielewe kwa hilo,” alisema Jeniffer, naye sura yake aliiweka kwenye hali ya huzuni kwa kutaka kueleweka kwa kile alichokuwa amekisema.
Dawson akanyamaza kwanza, yaani alihisi kama alikuwa akiota, kile alichoambiwa hakikumuingia kabisa kichwani mwake. Akahisi kabisa Jeniffer alikuwa na mtu mwingine, hakuwa yeye, sasa alikuwa nani?
Alimuuliza maswali ya kutaka kumfahamu mtu huyo lakini Jeniffer hakuwa radhi kumwambia kwa kipindi hicho, hakutaka kwanza dunia ijue kama alikuwa kwenye uhusiano na Amon mpaka pale ambapo aliamini muda ungefika na kumwacha kila mtu afahamu.
Dawson aliomba sana lakini hakukubaliwa hivyo kuondoka zake. Njiani alikuwa na majonzi yake lakini upande mmoja wa moyo ulimkumbusha kwamba Jeniffer alikuwa mwanamke, siku zote wanawake walikuwa watu wa huruma, ulipomuomba kitu, mara ya kwanza alikukazia lakini baada ya kumsumbua zaidi na zaidi, alikubali na hivyo kukipata kwa urahisi kabisa.
Alipokuwa ndani ya gari akaona ni jambo jema kumpigia simu Glory kwa lengo la kuzungumza naye na kumwambia kilichotokea. Haraka sana akafanya hivyo na simu kuanza kuita, iliita kwa sekunde kama kumi, hatimaye ikapokewa na sauti ya msichana huyo kuanza kusikika kutoka upande wa pili.
“Ndiyo nimetoka kwa Jeniffer!” alimwambia.
“Imekuwaje tena?”
“Amenikataa!”
“Amekukataa? Kwa sababu gani?”
“Basi tu, labda kwa yale yaliyotokea, anahisi nitafanya vile tena,” alimwambia.
“Mh!”
“Hivi una uhakika Jeniffer hana mtu?”
“Hana! Kama angekuwa na mtu ningejua tu!”
“Sasa kwa nini anikatae?”
“Ndiyo wanawake tulivyo! Wewe endelea tu kumbembeleza, nina uhakika atakubali tu,” alisema Glory.
“Nashukuru sana kwa msaada wako. Nitafanya hivyo!” alimwambia.
“Sawa.”
Akakata simu na kukubaliana na Glory kwamba angeendelea kumfuatilia msichana huyo, awe anawasiliana naye kwenye simu mara kwa mara kwani alihisi hilo lingemsaidia kwa kiasi kikubwa. Alichukua dakika kadhaa, hatimaye akafika katika nyumba aliyokuwa amechukua kwa muda na kujipumzisha ndani. Sasa mawazo juu ya Jeniffer yakaanza kumsumbua, akaanza kupanga mikakati yake mipya.

Je, nini kitaendelea?

Kumbuka simulizi yangu ya kipelelezi na uchawi ndani yake inaendelea kupatikana kwa sh. 5000 Whatsapp, inaitwa Medusa: Malkia wa Damu.

Inamuhusu msichana Zulfa, aliolewa na tajiri kutoka Kisiwani Mafia. Wakiwa fungate huko Zenji, anamtoroka usiku, anahamisha 100M kwa akaunti yake. Kosa alilolifanya, alichukua kila kitu chake, akasahau chupi.

Yaap! Chupi. Mumewe, mzee Hussein akaichukua na kwenda Mafia, akaloga kupitia chupi hiyo. Kilichotokea, Zulfa akaanza kupata matatizo, anaota ndoto mbaya na za kutisha, akishtuka, ana muhemko wa kufanya mapenzi, akinchukua mwanaume na kwenda naye hotel, jini linatoka ndani yake na kumuua mwanaume huyo.

Ameua watu wengi...sasa kesi inafika mezani kwa mpelelezi Ashrafu Maganza, anaanza kufuatilia hayo mauaji. Ni hadithi nzuri na inasomeka. Njoo Whatsapp kwa namba 0718069269.
 
Nyemo Chilongani
Ulimwengu Ndotoni Mwangu
0718069269

Sehemu ya 30.

Glory akaanza kumwambia Jeniffer kila kitu alichokuwa amezungumza na mwanaume huyo, kuhusu namna alivyoondoka zake kuelekea Marekani kwa kuwa wazazi walitaka kumuoa msichana mwingine.
Alivyofika huko, akaanza kuishi naye kwenye uhusiano, alimpenda lakini baada ya muda fulani akahisi kabisa hakuwa msichana wake sahihi kwa kuwa hakuwa akiyapata yale yote aliyoyapata kutoka kwake.
Akatafuta njia ya kumuacha, ilikuwa vigumu kwa sababu wazazi wake walikuwa sehemu ya uhusiano huo, aliteseka mno lakini mwisho wa siku akaamua kusimama kama mwanaume na hivyo kuamua kumuacha kinguvu.
Baada ya hapo ndipo akaanza kuwakumbuka watu aliowahi kuwa nao kwenye uhusiano, kwa wote hao, mtu sahihi aliyekuja kwake alikuwa huyo Jeniffer na ndiyo maana leo alikuwa nchini Ujerumani kwa lengo la kuonana naye, azungumze naye na kuwa kama zamani.
“Kwa sasa haiwezekani kabisa,” alisema Jeniffer huku akimwangalia Glory.
“Jeniffer! Nimezungumza na Dawson, yaani anaonyesha kabisa kujutia alichokifanya, yaani ungeonana naye ungeligundua hilo. Naomba umsamehe!” alisema Glory.
“Nimekwishamsamehe!”
“Kwa hiyo upo tayari kurudiana naye?”
“Hapana!”
“Hata kuonana naye?”
“Ndiyo! Sipo tayari!” alimwambia.
Glory aliumia sana, hakujua kilichokuwa kikiendelea nyuma ya pazia, kubwa zaidi alianza kumuona rafiki yake akiwa anazingua, mtu kama Dawson, mwanaume ambaye mwisho wa siku aliamua kurudi na kuomba msamaha, alitakiwa kusamehewa kwa kuwa angebadilika na kuwa mtu mwema.
Msimamo wa Jeniffer haukubadilika, ulikuwa uleule kwamba hakutaka kurudiana naye. Moyoni mwake alikuwa na amani, furaha kwa kuwa alikuwa na mtu aliyempenda kwa mapenzi ya dhati na kubwa zaidi alikuwa na mimba yake.
Glory hakuwa na jinsi, akamtafuta Dawson, wakaonana na kumwambia kile kilichotokea kwamba Jeniffer alikataa katakata kurudiana naye kwani alikuwa na maisha yake mengine kabisa.
“Kwani ana mtu?” alimuuliza.
“Sidhani! Endapo angekuwa na mtu angeniambia tu!”
“Sasa tatizo nini? Au hukumwambia kwamba nimetubu na sitorudia tena kufanya ule upumbavu?”
“Vyote nilimwambia!”
“Sasa kwa nini amekataa?”
“Nadhani ni msimamo wake. Ila si unajua watoto wa kike, jaribu kuonana naye, nadhani atakubali. Ngoja nikuelekeze anapoishi kwa sasa,” alisema Glory, na bila shaka akaanza kumuelekeza mwanaume huyo alipokuwa akiishi Jeniffer.
Dawson hakutaka kushindwa, aliamini huyo Jeniffer ndiye alikuwa msichana wa ndoto zake, hata kama hakuwa akitaka kwa wakati huo aliamini ingetokea siku moja angekubali kuonana naye na kurudiana.
Alitakiwa kupambana kama mwanaume, hakuwa radhi kuona Jeniffer akiolewa na mwanaume mwingine zaidi yake, ilikuwa ni lazima kupambana kiume na mwisho wa siku ampate na kumuweka kwenye himaya yake kama kawaida.
Akaanza kumtafuta kivyakevyake kwa kwenda katika nyumba aliyokuwa akiishi, ilikuwa moja ya nyumba kubwa na ilikuwa kwenye mtaa wa kitajiri. Kwa Dawson hakutaka kuwa na hofu juu ya hilo kwani msichana huyo alitoka kwenye familia ya kitajiri mno.
Baada ya dakika kadhaa kulisimamisha gari mbali kidogo na nyumba hiyo, akaliona gari la Jeniffer likiingia ndani ya himaya la jengo hilo, haraka sana akateremka akiwa na maua mkononi, hata kabla ya geti kujifunga, akaingia na kuanza kulifuata gari la msichana huyo ambalo tayari nalo liliingia nani ya nyumba hiyo huku mkononi mwake akiwa na maua kwa lengo la kumuomba msamaha.
Jeniffer hakutegemea kumuona mwanaume huyo mahali hao, alishtuka, akawa anamwangalia mara mbili mbili kama ni yule aliyekuwa akimfahamu ama alikuwa mtu mwingine. Dawson alimwangalia Jeniffer huku akiwa kwenye hali fulani ya kutaka kuonewa huruma, hapohapo akaanza kumsogelea huku akiwa na maua yake kwa lengo la kumuomba msamaha.
Kitu cha kwanza kabisa kukifanya kilikuwa ni kupiga magoti mbele yake huku akimnyooshea mkono uliokuwa na maua kwa lengo la kuyachukua na kumsamehe kwa kila kitu alichokifanya miaka ya nyuma. Alimsamehe mwanaume huyo kitambo sana lakini kitu ambacho hakutaka kabisa kukiona ni kurudi kwenye uhusiano ambao alijiahidi asingeweza tena.
Kama kuhuzunika, alihuzunika sana, kama kulia alilia sana, hivyo vyote vilitosha na kitu alichokihitaji kwa nguvu zote kilikuwa ni mapenzi, furaha na amani, vyote hivyo alivipata kwa Amon, hakuona kama kulikuwa na uhitaji mwingine wa kutaka vitu hivyo kutoka kwa mtu mwingine.
“Naomba unisamehe Jeniffer, nilikuumiza, nilikuwa mpumbavu sana kuwasikiliza wazazi wangu ambao waliniacha nikiteseka katika mtego mkubwa niliouingia,” alisema Dawson huku akimwangalia msichana huyo, Jeniffer alibaki akiwa amesimama, hakujua kitu cha kusema kwanza, alitaka kumsikiliza.
“Nilipata kila kitu kutoka kwako! Nilipoondolewa niliamini haya huko ambapo nilikwenda basi ningepata kila kitu kama ilivyokuwa kwako, niliteseka sana, niliiona dunia kuwa chungu, naomba unisamehe Jeniffer, dunia imenifundisha,” alisema Dawson huku akimwangalia Jeniffer.
“Dawson! Naomba usimame!” alisema Jeniffer huku akimuinua mwanaume huyo ambaye alisimama, wakaanza kuangalian usoni, wakati huo Dawson alikuwa akilengwa na machozi ambayo baada ya sekunde chache tu yakaanza kutiririka.
“Nilikusamehe zamani sana!” alimwambia huku akimshika mkono.
“Najua ni wazazi wako ndiyo waliamua hivyo, ulikuwa ukinipenda sana, tulikuwa na ndoto pamoja lakini wazazi wako wakaingilia, wakanipokonya wewe kutoka mikononi mwangu, hakika niliumia sana, nililia usiku na mchana,” alisema Jeniffer na kunyamaza kwanza, yale yaliyotokea kipindi cha nyuma yakaanza kujirudia kichwani mwake.
“Naomba unisamehe sana kwa kukuumiza,” alimwambia.
“Nilikusamehe tangu zamani, nisingekuwa nimekusamehe sidhani kama ningeendelea kusimama hapa nilipokuwa,” alimwambia huku akimwangalia.
“Nashukuru sana! Nakuhitaji Jeniffer, ninakuhitaji sana maishani mwangu!”
“Najua unanihitaji! Ila sina tena nafasi ya kukuingiza moyoni mwangu!” alimwambia.
“Kwa sababu gani?”
“Kuna mtu ambaye tayari ameingia kwenye ule moyo uliouacha! Naomba unisamehe kwa hilo. Tubaki tu kuwa marafiki, tushauriane kwenye mambo mengine kama hutojali,” alisema Jeniffer huku akimwangalia.
Kulikuwa na maneno mengi sana aliyowahi kuambiwa maishani mwake ambayo yalimuumiza mno lakini kwa yale aliyokuwa akiambiwa kipindi hicho, hakika yalimuumiza kuliko maneno yote aliyowahi kuambiwa.
Alimwangalia Jeniffer, msichana huyo alikuwa mrembo hasa, alimpenda na alitamani sana kuwa naye lakini alimwambia ilishindikana kwa sababu tayari alikuwa na mwanaume mwingine. Hakutaka kuona hilo likitokea, alitamani kuwa na Jeniffer tu, hakutaka kusikia kitu chochote kuhusu huyo mwanaume mwingine.
Alinyamaza! Aliangalia chini, machozi yakaanza kumtoka, ya sasa hivi hayakuwa ya kutaka kuonewa huruma bali yalikuwa machozi yaliyokuwa na maumivu makali moyoni mwake. Alitamani hata muda urudi nyuma, kipindi kile alichokuwa na msichana huyo na kuwakatalia wazazi wake lakini hakuweza kufanya hivyo.
“Jeniffer!”
“Dawson! Nashukuru sana kwa kipindi chote nilichokuwanacho, hakika ulikuwa mwanaume mwema sana kwangu, ulinifundisha maisha, namna ya kujiamini na pia ukanifundisha kuhusu mapenzi!” alimwambia.
“Jeniffer!”
“Sitoweza kuwa nawe! Naomba unielewe kwa hilo,” alisema Jeniffer, naye sura yake aliiweka kwenye hali ya huzuni kwa kutaka kueleweka kwa kile alichokuwa amekisema.
Dawson akanyamaza kwanza, yaani alihisi kama alikuwa akiota, kile alichoambiwa hakikumuingia kabisa kichwani mwake. Akahisi kabisa Jeniffer alikuwa na mtu mwingine, hakuwa yeye, sasa alikuwa nani?
Alimuuliza maswali ya kutaka kumfahamu mtu huyo lakini Jeniffer hakuwa radhi kumwambia kwa kipindi hicho, hakutaka kwanza dunia ijue kama alikuwa kwenye uhusiano na Amon mpaka pale ambapo aliamini muda ungefika na kumwacha kila mtu afahamu.
Dawson aliomba sana lakini hakukubaliwa hivyo kuondoka zake. Njiani alikuwa na majonzi yake lakini upande mmoja wa moyo ulimkumbusha kwamba Jeniffer alikuwa mwanamke, siku zote wanawake walikuwa watu wa huruma, ulipomuomba kitu, mara ya kwanza alikukazia lakini baada ya kumsumbua zaidi na zaidi, alikubali na hivyo kukipata kwa urahisi kabisa.
Alipokuwa ndani ya gari akaona ni jambo jema kumpigia simu Glory kwa lengo la kuzungumza naye na kumwambia kilichotokea. Haraka sana akafanya hivyo na simu kuanza kuita, iliita kwa sekunde kama kumi, hatimaye ikapokewa na sauti ya msichana huyo kuanza kusikika kutoka upande wa pili.
“Ndiyo nimetoka kwa Jeniffer!” alimwambia.
“Imekuwaje tena?”
“Amenikataa!”
“Amekukataa? Kwa sababu gani?”
“Basi tu, labda kwa yale yaliyotokea, anahisi nitafanya vile tena,” alimwambia.
“Mh!”
“Hivi una uhakika Jeniffer hana mtu?”
“Hana! Kama angekuwa na mtu ningejua tu!”
“Sasa kwa nini anikatae?”
“Ndiyo wanawake tulivyo! Wewe endelea tu kumbembeleza, nina uhakika atakubali tu,” alisema Glory.
“Nashukuru sana kwa msaada wako. Nitafanya hivyo!” alimwambia.
“Sawa.”
Akakata simu na kukubaliana na Glory kwamba angeendelea kumfuatilia msichana huyo, awe anawasiliana naye kwenye simu mara kwa mara kwani alihisi hilo lingemsaidia kwa kiasi kikubwa. Alichukua dakika kadhaa, hatimaye akafika katika nyumba aliyokuwa amechukua kwa muda na kujipumzisha ndani. Sasa mawazo juu ya Jeniffer yakaanza kumsumbua, akaanza kupanga mikakati yake mipya.

Je, nini kitaendelea?

Kumbuka simulizi yangu ya kipelelezi na uchawi ndani yake inaendelea kupatikana kwa sh. 5000 Whatsapp, inaitwa Medusa: Malkia wa Damu.

Inamuhusu msichana Zulfa, aliolewa na tajiri kutoka Kisiwani Mafia. Wakiwa fungate huko Zenji, anamtoroka usiku, anahamisha 100M kwa akaunti yake. Kosa alilolifanya, alichukua kila kitu chake, akasahau chupi.

Yaap! Chupi. Mumewe, mzee Hussein akaichukua na kwenda Mafia, akaloga kupitia chupi hiyo. Kilichotokea, Zulfa akaanza kupata matatizo, anaota ndoto mbaya na za kutisha, akishtuka, ana muhemko wa kufanya mapenzi, akinchukua mwanaume na kwenda naye hotel, jini linatoka ndani yake na kumuua mwanaume huyo.

Ameua watu wengi...sasa kesi inafika mezani kwa mpelelezi Ashrafu Maganza, anaanza kufuatilia hayo mauaji. Ni hadithi nzuri na inasomeka. Njoo Whatsapp kwa namba 0718069269.
Jamani leo moja tu🧐
 
Sehemu ya 31.

Baada ya kuondoka nchini Tanzania, Amon akarudi Ujerumani. Watu walipata taarifa juu ya ujio wa mwanaume huyo hivyo walikusanyika uwanjani na kumsubiri. Kipindi alichokuwa ameondoka, mwendo wa Hertha Berlin haukuwa mzuri sana, walikuwa wakishinda lakini kwa ushindi mwembamba mno tofauti na wakati alipokuwepo.
Gideon alionekana kutokuwa na nguvu za kutosha kupambana bila yeye, watu walimsubiri kwa kuwa walitaka kuona akirudi tena ndani ya timu na kuendelea kuipambania timu yake iliyokuwa ikiongoza ligi kuu ya Ujerumani.
Wakati huo, baada ya siku tatu Hertha Berlin ilitakiwa kuingia uwanjani na kucheza dhidi ya Bayern Munich, ilikuwa ni mechi ni mechi kubwa na ngumu kwao, hivyo ilikuwa ni lazima Amon awepo, apambane kuonyesha mabavu yake.
Mashabiki walikuwa wakishangilia tu uwanja wa ndege, kila mmoja alitaka kumuona Amon, wengine walikuwa na vitabu vyao, walitaka kusainiwa vitabu vyao lakini pia walitaka kumpongeza kwa ubingwa aliouchukua huko Afrika alipotoka.
Baada ya ndege kutua, akaanza kutoka na abiria wengine ambao nao humo ndani ya ndege walipokuwa, walikwishaomba kusainiwa vitabu vyao baada ya kugundua walisafiri ndege moja na Amon, mpaka picha wakapiga naye.
Walitembea mpaka walipofika nje, watu wakaanza kumfuata Amon na kutaka kusainiwa vitabu vyao na kupiga naye picha. Ilikuwa kazi ngumu kumridhisha kila mmoja kwa sababu walikuwa wengi, polisi waliingilia na kumtaka Amon kuondoka, kwa kuwa Gideon alifika kumpokea, akamuingiza ndani ya gari lake na kuondoka mahali hapo.
Kila shabiki wa Hertha Berlin ambaye alisikia Amon amerudi alifurahi, sasa wakaona mechi yao dhidi ya Bayern Munich ingekuwa kali na ya kusisimua sana, tena kila mmoja alitaka kuiona mechi hiyo ambayo waliamini ingekuwa mechi bora ya msimu.
“Imekuwaje huko?” aliuliza Gideon huku akiendesha gari.
“Noma sana! Yaani watu wakataka kunimeza mimi, yaani kama ndiye niliyekwambia ubadilishe uraia!” alimjibu.
“Hahaha! Unajua niliichukia sana Afrika!” alimwambia.
“Ni kawaida. Mimi nitakuwa upande wako, nitakusapoti kwa kila kitu!” alimwambia.
“Ulikwenda kuwaona wazazi wangu?”
“Sikuwa na muda! Nyumbani kwetu kwenyewe sikufika, niliwasiliana na mzee mara moja, sikupata muda kabisa. Si unajua nilichelewa kufika, kesho yake tukaondoka, kurudi, nikaambiwa haraka sana nije huku,” alimwambia.
“Duh! Pole sana mzee!”
“Usijali. Ila nilionana na Angelina!”
“Ulionana na Angelina? Yaani kwenu hujaenda, ila ulipata nafasi ya kumtafuta dada yangu!” alisema Gideon.
“Hapana! Sikumtafuta! Alinitafuta yeye, alikuja nyumbani kwangu!”
“Alikuja nyumbani kwako?”
“Yaap!”
“Ikawaje?”
“Kuniomba msamaha kwa yote yaliyotokea. Yule mwanaume amemuacha baada ya kumpa mimba mwanamke mwingine!” alisema.
“Aiseee!”
“Ndiyo hivyo!”
“Kwa hiyo ukamsamehe?”
“Sisi ni binadamu Gideon. Ila kwa kumwangalia tu, bado amechanganyikiwa. Najua hatoweza kusoma huko, mawazo yanamsumbua sana, nimezungumza naye umchukue na kuja kusoma huku Ujerumani!” alimwambia.
“Una uhakika ataweza kusoma?”
“Kwani humuamini mdogo wako?”
“Namwambini sana ila....”
“Muite aje kusoma. Sasa asipokula matunda ya kipaji cha kaka yake unataka akale matunda ya nani?” alisema na kumuuliza.
“Nitawasiliana naye. Kwanza acha nitafute chuo bora,” alimwambia.
Bado walikuwa wakiendelea na safari kama kawaida, baada ya dakika kadhaa, wakafika nyumbani, akateremka na kuelekea ndani. Alimkuta mpenzi wake akiwa kwenye kochi, hakuonekana kuwa kama siku nyingine, alifurahia ujio wake tena lakini akahisi kulikuwa na kitu. Hakutaka kumuuliza kwa sababu Gideon alikuwepo mahali hapo, walikaa na kuzungumza kidogo, mwanaume huyo alipoondoka tu, akaamua kuzungumza naye.
Alimwambia kuhusu Dawson, jinsi alivyofika nyumbani hapo na kumwambia maneno kuhusu kurudiana naye. Alimsimulia kila kitu kwa kuwa hakutaka kuona matatizo baadaye yakitokea, alitakiwa kujua kila kitu.
“Umemwambia kwamba upo na mimi?” alimuuliza.
“Hapana Sikumwambia!”
“Si vibaya pia. Ila nadhani atajua muda si mrefu, naomba usiwe na huzuni tena,” alisema Amon huku akimwangalia mpenzi wake huyo.
Maisha yaliendelea kama kawaida, baada ya siku kadhaa za kufanya mazoezi na timu yake, hatimaye siku ya mechi ikafika. Siku hiyo kila shabiki alikuwa na nguvu ya kutamba, walimwamini sana Amon, alionekana kuwa msumali wa moto.
Bayern Munich ilikuwa timu kubwa na kali, iliyokuwa na mafanikio mengi lakini kwa mara ya kwanza wakaanza kuihofia Hertha Berlin kutokana na uwezo wao mkubwa waliokuwanao kipindi hicho. Mashabiki zao hawakutamba kama kawaida yao, walikuwa wapole na mtu waliyekuwa wakiumizwa naye alikuwa Amon tu.
Kijana huyo alitisha, alikuwa na makali, aliwaliza watu wengi, kila mtu alimuogopa, kila alipokutana na wapinzani, uwezo wake ulikuwa mkubwa na alionekana kupenda sifa kila awapo uwanjani kwani miujiza yake ilikuwa inatisha mno.
Siku hiyo Jeniffer aliamua kwenda na Glory uwanjani, walikuwa wamekwenda kuangalia mechi hiyo ya aina yake. Muda wote msichana huyo alionekana kuwa na furaha isiyo kifani, kwenye kila hatua alimuamini mpenzi kwenye ishu nzima ya kufanya miujiza akiwa uwanjani.
“Ninampenda sana Amon!” alisema Glory huku akishangilia wakati wachezaji wa timu hizo wakiingia.
“Kwa sababu gani?”
“Anajua sana kucheza. Ni mchezaji wangu bora,” alimjibu.
“Na ungejisikiaje kama Amon angekuwa mpenzi wako?” alimuuliza.
“Yaani! Nadhani ningejiona kuwa mtu mwenye bahati kuliko wote katika dunia hii!” alimjibu.
“Kabisa?”
“Ndiyo! Mbona umeniuliza hivyo?”
“Nilitaka kujua tu!”
“Sawa.”
Mechi ya siku hiyo ilikuwa kama za siku nyingine, huyo Amon alionekana kuwa msumali zaidi ya alivyokuwa katika mechi zilizopita. Alicheza kwa nguvu na kuonyesha kila kitu alichokuwanacho.
Uwezo wake wa siku hiyo uliwaonyesha watu kwamba kweli alitakiwa kuwa mchezaji bora wa dunia, kwani alitisha. Kila alipokuwa akipata mpira, aliwasogelea mabeki kama kawaida yake, aliwafanya alivyotaka kama alikuwa akicheza na watoto. Ni ndani ya dakika kumi za kwanza, tayari Hertha Berlin ilikuwa ikiongoza kwa mabao mawili yaliyofungwa na Gideon huku pasi za mwisho zikiwa zimetoka kwa Amon.
Ilikuwa ni furaha tele kwa kila mmoja. Mechi iliendelea, ilipofika dakika ya kumi na sita, Amon alipokea pasi maridhawa kutoka kwa Innocent, aliipokea kwa heshima kubwa, akaanza kuondoka na mpita kwa kasi kubwa.
Alikuja beki wa kwanza wa pembeni akampiga chenga na kuanza kuelekea ndani ya kumi na nane, hakutaka kuingia, hukohuko anaupiga mpira kwa staili ya ndizi, yaani mpira ulikwenda na kujipinda na kutumbukia wavuni kwa pembeni kabisa.
Uwanja mzima ukapiga kelele za shangwe. Amon akaufuata mpira na kuuweka tumboni mwake na kuufunika na jezi kama salamu za mpenzi wake aliyekuwa na mimba. Kila mtu aliyeona hivyo alishangilia, huyo Amon kumbe alikuwa na mwanamke na hapakuwa na mtu yeyote aliyekuwa akijua, kubwa zaidi mtu huyo alikuwa na mimba.
“Amon ana mwanamke mwenye mimba,” alisema Glory huku akirukaruka kwa furaha.
Jeniffer hakusema kitu zaidi ya kutoa tabasamu na kushangilia. Mechi iliendelea, Amon alizidi kuwa msumali wa moto na mpaka mpira unamalizika, Bayern Munich walikubali kipigo cha mabao matano kwa sifuri huku Amon akifunga matatu na kuondoka na mpira kama ilivyokuwa sheria za soka duniani.
Baada ya mpira kumalizika, wakatoka uwanjani, Jeniffer akamchukua rafiki yake, Glory na kuondoka naye mpaka walipopaki gari, wakaingia na kutaka kuondoka mahali hapo. Walikuwa ndani ya gari lakini Jeniffer hakuwasha gari.
“Tunasubiri nini tena?” alimuuliza Jeniffer.
“Kuna mtu tunamsubiri. Hatochelewa!” alimjibu.
Walisubiri kwa dakika kama kumi na tano hivi, wachezaji wakaanza kutoka, mashabiki wakawafuata na kupiga nao picha huku wakisaini vitabu vyao. Si wote waliokuwa wakiingia kwenye basi la timu, kwa wale waliokuwa na usafiri wao, waliingia na kuondoka. Jeniffer alipomuona mpenzi wake anakuja, akafungua mlango na kumfuata, wakakumbatiana huku Glory akiangalia.
Hakuamini alichokiona, mwanaume aliyekuwa amekumbatiwa na Jeniffer alikuwa yuleyule mchezaji aliyekuwa akimuhusudu, alipigwa na mshangao na alibaki ametumbua macho tu. Hakuamini alichokuwa akikiona mahali hapo, aliachama mdomo wazi huku akiwaangalia wawili hao.
“Amon!” aliita baada ya mwanaume huyo kulisogelea gari.
“Hukuwahi kuniambia kuhusu huyu rafiki yako!” alisema Amon huku akimwangalia Jeniffer.
“Anaitwa Glory!”
“Oh! Glory! Mimi naitwa Amon. Nadhani ni mgeni machoni mwako,” alimwambia huku akiachia tabasamu. Glory akashindwa kuvumilia, naye akamkumbatiaAmon.
“Nini kinaendelea? Mnafahamiana?” aliuliza Glory.
“Yeah! Huyu ndiye mpenzi wangu!” alimjibu.
“Mpenzi wako? Tangu lini?”
“Ni muda sasa!”
“Hebu subiri kwanza! Jeniffer! Inamaana wewe ni mjauzito?” alimuuliza, alikumbuka jinsi Amon alivyokuwa ameshangilia bao lake la kwanza.
“Yaap!”
“Unasema kweli?”
“Asimilia mia moja,” alimjibu, msichana huyo akamsogelea na kumkumbatia tena, yaani kwao ilikuwa ni furaha tele. Mapenzi waliyokuwanayo juu yao, hayakuwa ya unafiki, walikuwa wakipendana kama marafiki waliokua pamoja tangu utotoni mpaka muda huo.

Je, nini kitaendelea?
 
Sehemu ya 32.

Moyo wa Glory ulikuwa na furaha tele juu ya mafanikio ya rafiki yake, Jeniffer, hakuamini kama mtu huyo alikuwa kwenye uhusiano wa kimapenzi na mwanasoka aliyekuwa na umaarufu mkubwa, Amon. Kwake, ilikuwa ni kama ndoto, hakuamini kama kuna siku angepata rafiki ambaye angejiingiza kwenye uhusiano wa kimapenzi na mtu maaruu.
Huyo Amon alikuwa akisifiwa na watu wengi kutokana na umahiri wake wa kusakata kabumbu, kulikuwa na wasichana mbalimbali waliokuwa wakimpenda kwa kuwa tu alikuwa maarufu na kubwa zaidi alikuwa na pesa.
Huyo Amon hakuonekana hovyo, alijua kuishi kistaa na muda mwingi alikuwa akitumia kuwa na wachezaji wenzake, hakujua kama rafiki yake kipenzi ndiye aliyeuchukua moyo wa kijana huyo na kuugalagaza vibaya.
Jeniffer alikuwa mjauzito, lilikuwa jambo jema sana hivyo alichokifikiria haraka sana ni kumtafuta Dawson kwa lengo la kumwambia kuachana na mwanamke huyo kwa kuwa asingeweza kumpata hata kidogo. Alipoondoka tu na kuanza kurudi kwake, haraka sana akachukua simu na kumpigia Dawson.
“Niambie jambo zuri la kunitia moyo,” alisema mwanaume huyo hata kabla ya salamu.
“Hakuna zuri kwa upande wako! Ila zuri kwa upande wetu,” alisema Glory kwenye simu.
“Kwa upande wenu, kwa maana gani?”
“Mimi na Jeniffer!”
“Aya niambie kuhusu hilo!”
“Naomba uachane na rafiki yangu,” alimwambia.
Kidogo Dawson akabaki kimya, ni kama alikuwa akiyafikiria maneno hayo aliyoambiwa na msichana huyo, alijua wazi kwamba asingeweza kuachana na Jeniffer kwa kuwa alikuwa akimpenda kwa moyo wa dhati, sasa kumwambia amuache, lilikuwa jambo lisilomuingia hata kidogo.
“Najua unajua siwezi kumuacha,” alimwambia.
“Inabidi iwe hivyo!”
“Kwa nini unaniambia haya yote? Ndivyo alivyokwambia?”
“Hapana! Ni mtazamo wangu tu, achana naye. Jeniffer ana mpenzi wake, tena anampenda sana,” alimwambia.
“Kuwa na mpenzi si tatizo hata kidogo.”
“Na ana mimba!” aliongezea.
Kwa maneno hayo sasa Dawson akanyamaza, hakuamini alichokisikia, maneno yale yalipenya mpaka moyoni mwake na kumchoma vilivyo, hakutegemea kusikia kitu kama hicho, Jeniffer alikuwa na mimba? Alipewa na nani?
Akili yake ilivurugwa mno. Alitamani mno kuona akipendwa na msichana huyo kwa mara nyingine, wawe kwenye uhusiano mzuri na hatimaye kumpa mimba na kujifungua lakini kilichomchanganya ni baada ya kusikia tayari kulikuwa na mwanaume mwingine ambaye alimuwahi na kumtundika ujauzito.
“Haiwezekani!” alimwambia.
“Ndiyo hivyo!”
“Utakuwa unanitania!”
“Nishawahi kukutania kwenye jambo kubwa kama hili?” aliuliza.
“Lakini mbona hakuniambia? Mbona hata mimba sikuiona?”
“Sasa ungeiona vipi mimba ya wiki mbili mpaka tatu?”
“Glory...”
“Naomba uachane na rafiki yangu Dawson. Wanawake wapo wengi, jaribu kumtafuta mwingine,” alimwambia.
Lilikuwa jambo lisilowezekana kabisa, kwake, huyo Jeniffer alikuwa mwanamke aliyempenda kuliko wote, kitendo cha kumuacha kwake lilikuwa jambo lisilowezekana hata kidogo, yaani ilikuwa ni ndoto kwake.
Alichotaka kwanza ni kumfahamu mwanaume aliyempa mimba huyo Jeniffer, alikuwa nani? Kama kungekuwa na uwezekano wa kummaliza, afanye hivyo lakini mwisho wa siku aishi na Jeniffer, kulea mimba ya marehemu halikuwa tatizo kwake.
“Mpenzi wake kwani ni nani?” alimuuliza.
“Anaitwa Amon!”
“Ninamfahamu Amon mmoja tu!”
“Ndiye huyohuyo!”
“Huyu mchezaji mpira?”
“Kwani ulivyosema unamjua Amon mmoja tu ulimaanisha nani?” naye Glory akauliza.
Moyo wake ukanyong’onyea zaidi, alimfahamu Amon, kijana huyo alikuwa maarufu, ana pesa, juzikati tu aliingia mkataba wa euro bilioni kumi na tano kusaini mkataba na Kampuni ya Adidas ya nchini Ujerumani kwa lengo la kuvaa viatu vya kampuni hiyo.
Amon alikuwa na pesa nyingi mno, alikuwa maarufu na alipendwa na kila mtu, pamoja na kupendwa hivyo lakini bado moyo wake ulikuwa na lengo moja tu dhidi yake, amuue na kubaki na Jeniffer wake.
Hakuwa na nguvu ya kufanya mauaji hayo, kama alitaka kulikamilisha hilo ilikuwa ni lazima awakodi watu ambao wataweza kulifanikisha hilo haraka sana. Akaanza kuwatafuta hao.
Akaishi kwa watu wa kundi dogo la watu waliokuwa wakijiita Jumanji Boys ambao walikuwa na makazi yao jijini Munich. Hili lilikuwa kundi la watu waliokuwa na kazi ya kuteka na kuua. Kwenye kila kazi waliyokuwa wakipewa, waliifanya kwa asilimia mia moja.
Dawson akaamua kusafiri mpaka jijini Munich kwa lengo la kuwasiliana na watu hao, alipofika huko, kwa msaada wa marafiki zake, akafanikiwa kuonana na kiongozi wa kundi hilo aliyeitwa Peters Konn na kumwambia kile alichokuwa akikitaka.
“Haina shida. Tunataka euro laki tano,” alimwambia.
“Hilo halina tatizo!”
“Tupe picha yake kabisa,” alisema Konn.
Akapewa picha ya Amon na kumwangalia, alimfahamu mwanaume huyo, alikuwa mmoja wa wanasoka waliokuwa wakisumbua kwa kipindi hicho. Alimwangalia Dawson, hakuamini kama kweli alimpa picha ya mtu kama Amon.
Miongoni mwa wachezaji aliokuwa akiwapenda sana, huyo Amon alikuwa namba moja. Alimpenda kwa kuwa alikuwa na uwezo mkubwa uwanjani, mnyenyekevu, aliyejishusha ila kulikuwa na makubwa mawili ambayo yalimfanya kumpenda zaidi.
La kwanza ni kwa sababu alikuwa akichezea Hertha Berlin, yeye alikuwa mpenzi wa timu ya TSV 1860 Munich ambao walikuwa ni wapinzani wa jadi wa Bayern Munich. Kwenye timu zote ambazo hakuwa akizipenda, Bayern Munich ilikuwa ya kwanza.
Timu yake haikuwa na uwezo wa kushinda kombe la ligi la nchi hiyo lakini kwa kuwa hao Hertha Berlin waliibuka na kuanza kuuvunja ufalme wa Bayern Munich, kwake ilikuwa furaha tele, yaani ulikuwa ni mwendo wa kula bata tu.
La pili lilikuwa ni kamari alizokuwa akicheza. Hertha Berlin ilikuwa ikimpa pesa kila alipokuwa akiibetia. Alikuwa akiweka kiasi kikubwa cha pesa, wakati mwingine alikuwa na hofu lakini kila alipokuwa akimfikiria Amon, alijiamini na kula pesa nyingi.
Kwenye mechi dhidi ya Bayern Munich aliiwekea Hertha Berlin zaidi ya euro elfu ishirini, kiasi kikubwa zaidi, tena aliiwekea kwenye ‘mikeka’ miwili, kilichotokea, yote hiyo Amon alimpa pesa nyingi kitu kilichomfanya kumpenda zaidi.
Leo, huku akiwa anauonja utamu wa Amon, Dawson akatokea na kumwambia aende kummaliza, yaani alitakiwa kufanya hivyo halafu asiwe anapata pesa kwenye kamari zake. Alimwangalia Dawson na kumuona kama mjinga fulani, yaani kwenye kitu alichokuwa akikitaka ni kumuona Amon akicheza soka milele yote ili aweze kuvuna pesa kwenye kamari zake.
“Inakuwaje? Naona umekaa kimya! Itawezekana?” alimuuliza Konn aliyekuwa akiendelea kuiangalia picha ya Amon.
“Ni kazi ndogo sana. Ila kwanza malipo, hawa watu maarufu wanakuwaga na usumbufu sana,” alimwambia.
“Haina shida.”
“Ila si euro laki tano tena, kama inawezekana utoe euro laki nane,” alimwambia.
“Kwa sababu gani?”
“Kwa kuwa jamaa ni maarufu. Watu hawa kuwapata huwa vigumu sana,” alimwambia.
“Haina shida.”
Kwa Dawson pesa haikuwa tatizo hata kidogo, alichotaka ni kuona kazi yake ikifanyika kwa asilimia mia moja. Siku hiyohiyo akahamisha kiasi hicho cha pesa na kulilipa kundi hilo ambalo lilimwambia lingemfanyia kazi haraka sana.
Akafurahi na kuondoka zake. Hakutaka kuwasiliana tena na Jeniffer kwa kuwa alijua alikuwa akienda kumliza sana, tena hakutaka hata kuambiwa kama alikuwa na mpenzi, alihitaji kujifanya kama halijui jambo hilo lakini mwisho wa siku afanikishe kile alichokuwa akikitaka.
Kundi la Jumanji Boyas halikuwahi kushindwa hata kidogo, kila kazi waliyokuwa wakipewa waliifanya kwa mafanikio makubwa, kumteka Amon na kwenda kumuua kwao ilikuwa ni kazi nyepesi sana, kwanza baada ya watu kujua wao ndiyo waliofanya hivyo, ingewaongezea jina mjini.
Wakajigawa, wakapanga mipango yao, walichokubaliana ni kusafiri mpaka jijini Berlin ambapo huko baada ya kufika, wangekaa kwenye hoteli nzuri na siku ya mechi kwenda kwenye uwanja wa Hertha Berlin kujifanya kuangalia mpira, vijana wao wawili wangeingia sehemu wanapopaki magari ya wachezaji na kulifatuta gari la Amon na kuingia humo.
Kabla ya kufanya hivyo kwanza wakataka kufahamu ni aina ya gari gani mwanaume huyo alikuwa akiendesha ili wasipate shida kufanikisha kwenye hilo. Kwenye kupeleleza kwao, wakagundua Amon alikuwa na magari mawili, la kwanza lilikuwa Lambornghin na la pili ilikuwa ni BMW ya milango minne.

Je, nini kitaendelea?
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom