Chilojnr
JF-Expert Member
- Jul 5, 2012
- 308
- 1,354
- Thread starter
- #41
Sehemu ya 19.
Kila mmoja alitaka kuona hayo maajabu ambayo Amon aliyazungumzia, walitaka kuona kama walikuwa na jipya jingine ama yalikuwa ni mahojiano tu.
Ni dakika ya tano tu, Amon alipewa pasi na namba nane yao aliyeitwa Innocent, aliipokea pasi ile, akageuka na kukutana na mabeki wawili mbele yake, akaanza kuwasogelea kwa kasi, alikuja beki wa kwanza, alichokifanya ni kumchezea mwili tu kwamba kama anakwenda kushoto, beki akalala kushoto na yeye kupita kulia.
Alipomuona beki mwingine anakuja, haraka akampigia pasi Gideon ambaye alisimama na kumtingisha beki mwingine, alipomuona ametingishika kama alivyotaka, akaubetua mpira kwa juu, ukaenda kwa Amon, akautuliza kifuani, beki wa kwanza alipomrudia, akampiga kanzu na kubaki yeye na golikipa tu.
Mashabiki wote walisimama kushudia kilichokuwa kinafiata. Alichokifanya ni kama Ronaldinho, alimpiga mkasi mmoja tu golikipa, akaelekea kulia na yeye kupita kushoto, akabaki yeye na goli, akafunga bao safi kabisa.
Mashabiki wakalipuka kwa shangwe, hawakuamini kumuona mtu akicheza namna ile, wale waliokuwa kwenye baa, hawakutaka kusubiri, kwa burudani ile moja tu hukutakiwa kuitazama mechi kwenye televisheni tu ulitakiwa kwenda uwanjani, wakachukua simu zao na kuanza kukata tiketi harakaharaka.
Kitu alichokifanya Amon ni kumkimbilia Gideon, akamkumbatia, akamuita Innocent na wachezaji wengine na kuanza kushangilia. Ilikuwa ni dakika ya tano tu lakini tayari watu waliona kulikuwa na balaa lililokuwa linafuata.
Kupitia bao hilo la kwanza, timu ya Schalke 04 ni kama walichanganyikiwa, huyo Amon alionekana kuwa msumali wa moto, alikuwa na kasi alipokuwa akienda kushambulia, alikuwa akipiga chenga za maudhi na alijua zaidi kuuficha mpira.
Yeye na Gideon walikuwa wakionana sana, walipigiana pasi na kuwasogelea maadui kwa kasi kubwa. Wala hazikuchukua dakika nyingi, ni dakika ya kumi tu, Amon akapewa pasi, alikuwa katikati ya uwanja, akaanza kuondoka na mpira ule, alichokuwa akikifanya ni kumpiga chenga kila mchezaji aliyekuwa akija.
Alipowapiga chenga wawili, akayainua macho yake, akamuona Gideon akikimbia mbele, akamwangalia beki mwingine, akamuona akiwa sawa na Gideon, haraka sana akaipiga pasi ndefu, ilipofika kwa Gideon, alipomuona beki anakuja wanguwangu, akaugusa kidogo tu, ukampiga tobo beki, akabaki yeye na kipa, hakutaka kumsogelea, akauinua mpira, lilikuwa moja ya tukio ambalo hata kipa hakulitegemea, akashtukia mpira ukipita juu yake na kwenda wavuni.
Lilikuwa bao maridadi la pili lililofungwa na kijana mwingine wa Kitanzania. Ilikuwa ni furaha kwa kila mmoja, kocha wao alibaki akishika kichwa, hakuamini kile alichokuwa akikiona, kilimshangaza na kilikuwa kitu ambacho hakukitarajia kabisa.
Wachezaji wale wawili walionekana kuwa nuksi, hawakuwa na masihara hata kidogo, mpaka mapumziko, tayari Schalke 04 walipigwa mabao matano huku matatu yakifungwa na Amon na mengine mawili yakifungwa na Gideon.
Ndani ya chumba cha kubadilishia nguo kila mmoja alikuwa akiwaangalia kwa mshangao. Wengi walikuwa na ndoto za kucheza na Messi, Ronaldo lakini watu hao wawili walionekana kuwa sawa na wachezaji hao, Gideon alikuwa na uwezo wa Ronaldo, Amon alikuwa na uwezo wa Messi, yaani walikuwa na maajabu makubwa.
“Kila mtu atavutiwa na timu hii, ni muda wa kuonyesha maajabu,” alisema Amon huku akimwangalia kocha wake.
Hatimaye baada ya dakika kadhaa wakarudi uwanjani, uwanja ulikaribia kujaa, mashabiki waliongezeka baada ya kuona kile kilichotokea, kila mmoja alionekana kuwa na furaha isiyo kifani.
Wakasahau kwamba wao ndiyo waliokuwa wakiwachukia wachezaji hao, walisahau kila maneno mabaya waliyokuwa wametamka kwao, kila mmoja muda huo alikuwa akiwapenda, na wengi wakaanza kuimba majina yao.
Kipindi cha pili kilianza, kilikuwa ni kipindi cha maajabu mengine, walipiga mpira ambao hapakuwa na mtu aliyeamini, walionekana kuwa mwiba mkali, kwenye kila pasi waliyokuwa wakipokea walionyesha maajabu makubwa, yaani mpaka mpira unamalizika, walishinda kwa mabao nane kwa sifuri, ushindi mkubwa sana kwao. Mabao manne yakifungwa na Amon, matatu na Gideon na moja na kiungo wao mshambuliaji, Merlin.
Mechi ilimalizika, wakatakiwa kuhojiwa lakini kocha alikataa, yeye aliwachagua wachezaji wengine wa kuzungumza na waandishi lakini si hao wawili. Kwa kile kilichotokea, hata mashabiki ambao hawakuiona hiyo mechi kutokana na ubize wa kazi, wakataka kuiona kwani waliyoyasikia yalikuwa mengi na makubwa mno.
Kila aliyeiona mechi ile, aliamini kulikuwa na mengi sana yaliyokuwa yakija mbele yao, hao walikuwa wachezaji wenye hatari sana, walikuwa msumali wa moto kwa timu nyingine.
Wakati hayo yakiwa yametokea, Anita hakuwa na habari, alikuwa na kazi zake nyingine, hakutaka kuangalia mechi hiyo kwa kuwa aliamini kabisa wachezaji hao wasingefanya kile alichokitarajia. Hakutaka kuwasiliana na mtu yeyote yule kuhusu mechi hiyo.
Alipoona mechi imekwisha, haraka sana akaingia kwenye mtandao wa Livescore kuangalia matokeo. Alichokiona hakuamini, timu yake ilishinda kwa mabao nane, akafungua kuona wafungaji, moyo wake ulikuwa na furaha tele. Huku akiwa hajui ni kwa namna gani alitakiwa kufurahia, ghafla akaona simu yake ikianza kuita, haraka sana akaangalia kioo, alikuwa baba yake, akaipokea.
“Hawa watu uliwatoa wapi?” lilikuwa swali la kwanza la baba yake baada ya kupokea simu.
“Najua unajua kila kitu baba!”
“Ni wachezaji ambao sikutarajia kuwaona! Uliiona hiyo mechi?”
“Hapana! Nilikuwa naogopa!”
“Hebu itazame inarudiwa baadaye! Hii ni pesa ndefu sana, hawa wachezaji ni hatari mno!” alisema baba yake, kama mfanyabiashara, alifikiria pesa tu.
Siku hiyo habari kubwa ikawa ni Amon na Gideon, walipewa sifa ya kila aina, hawakuvimba kichwa, walichowaambia wachezaji wenzao ni kwamba kulikuwa na mengi yajayo, waendelee kuvumiliana kwani bado hawakuwa kwenye ile fomu waliyoizoea kuwa nayo.
“Yaani hamkuwa kwenye fomu?” aliuliza mchezaji mmoja.
“Ndiyo! Ila tunavyoendelea kucheza, naona tutarudi kwenye fomu yetu,” alijibu Gideon, kila mmoja aliyesikia maneno hayo alishangaa, yaani hawakuwa kwenye fomu yao walicheza vile, je, wangekuwa kwenye fomu yao wangechezaje? Kila walilojiuliza, walikosa jibu.
Je, nini kitaendelea?

noma sana