Watu wa jf hapana jamani ina arosto gani hii story kila siku inawekwa episode 3 muwage mnashukuru basi hata kidogoHii kitu ina Arosto...lakini nimeshindwa kuunganisha dots kutoka episode 51na 52 maana sijaona muendelezo ya nn kilitokea baada yakusoma barua zaidi tunaona jamaa yupo lodge tayari Tabora bila kujua alifikaje na kuhusu ile game vipi alicheza!...nimeshindwa kuelewa kabsa huo muendelezo kutoka hapo 51!
Sehemu ya 45
Nilihisi mwili wote ukinisisimka wakati nipo ndani ya chumba kile, jamaa alichukua ile ngozi ya mnyama na kuitandika, akatutaka tukae juu ngozi hiyo.
Akachukua mkia ule mkia wa Simba na kutupiga nao kidogo kichwani. Akawasha ubani, moshi ulipoanza kufuka, akajivisha kitambaa cheusi kichwani, kile kitambaa kilifunika uso na kichwa chote, halafu akaketi kwenye kinu cha kutwangia.
Mimi na Cholo tuliendelea kuketi juu ya ile ngozi, tukiangalia kile kilichokuwa kinajiri. Dakikla moja badaye jamaa akapandwa na Majini. “Mnataka kupata nafasi ya kucheza kwenye timu yenu?” sauti moja ya mkwaruzu iliuliza. Yalikuwa ni majini ya yule bwana.
“Ndio....ndio,”tulijibu kwa pamoja. “Hao wachezaji mnao shindana nao, wametumia uchawi mkubwa kujikinga, inabidi utumike nguvu kubwa kuua zindiko lao.”
“Sawa....sawa” tuliendelea kuitikia. “Leteni kuku weusi wa kienyeji na sanda za maiti, sawa?”
“Ndio. ”Cholo aliitikia. Mimi nilishindwa kuitikia, niliona kama tulikuwa tunatumwa vitu vigumu.
Baada ya dakika mbili tatu, majini yale yakaondoka, mganga Majeed akarudi kwenye hali yake.
“Wamesemaje?” akatuuliza.
Moyoni nikajiuliza inamaana huyu jamaa anatuuuliza majini yake yanasemaje, yeye alikuwa hayasikii? Lakini nikakumbuka niliwahi kuambiwa kuwa mtu akiwa amepandwa na majini anakuwa hana fahamu. “Wamesema watu tunaotaka kushindana nao, wamejikinga sana, hivyo sharti tutumie nguvu kubwa kuua zindiko lao. Wameagiza kuku na sanda.”
“Sawa, nishajua kinachotakiwa kufanyika,” Mganga Majeed alisema. Akaendelea.
“Mnaweza kupata hao kuku na hizo sanda ama muache pesa nikatafute mimi hivyo vitu?”
“Nadhani heri tukupe pesa ukatafute mwenyewe.”
“Basi acheni pesa.”
“Shilingi ngapi?”
“Kama elfu arobaini itatosha.” Kwa kuwa fedha haikuwa tatizo kwetu, tulimpa hiyo pesa mara moja. Akatutaka turudi kesho yake ili tumalize kazi kabisa.
Tuliondoka na kwenda nyumbani kwao Cholo huko Fuoni Jitimai. Cholo alikuwa anatokea kwenye familia ya maisha ya kati na ya dini sana, alikuwa akiishi na mama yake mzazi na nduguze wa kike, alimdanganya mama yake tulikuja Zenji kwa mambo binafsi na ndani ya siku mbili tungerudi Dar es salam. Mama yake hakuwa na tatizo.