Simulizi: Soka Lilivyonikutanisha Na Shetani

Sehemu ya 52

MAPIGO yangu ya moyo yalinienda kasi sana. Mauzauza ya usiku huo yalinitisha kuliko kawaida. Labda unaweza kudhani mambo haya ninayo yasimulia ni hadithi tu ya kubuni. Laa!. Hakuna hata moja katika yote niliyoeleza ambalo ni la uongo ama nimetia chumvi.

Kila kitu nilicho simulia ni ukweli tupu, kilitokea nikiwa kijana wa miaka 24 tu. Nakumbuka nilibaki nimesisimama katikati ya chumba hicho nikiwa mwenye wasiwasi na mashaka makubwa. Kwa mujibu wa saa yangu ya mkononi, ilikuwa yapata saa tisa kasoro, usiku.

Hapakuwa na chakara chakara wala sauti yoyote. Ukimya wa ghafla ulitamalaki ndani ya chumba hicho cha pili, ilikuwa ni kana kwamba hakukuwa na lolote lilitokea muda mfupi uliopita.

Nilikuwa naogopa mno. Usiku ulikuwa mrefu. Katika maisha yangu yote, sikuwa kukutana na mauzauza yoyote ya kichawi. Mambo ninayo yasimulia nilizoea kuyasoma katika vitabu mbalimbali hasa vya riwaya.

Nilisogea kitandani na kuketi kitako. Bulb ya umeme iliendelea kuwaka. Kwa kuwa ndani kulikuwa na ukimya wa kuogofya, niliona kheri niweshe runinga angalau iniondelee ule ukimya wa ajabu.

Nilisimama na kuisogelea runinga. Ilikuwa imepachikwa kwenye kikasha cha chuma katika ukuta. Niliwasha na kuweka stesheni moja ya muziki. Wakati naketi kitandani, mara runinga ile ikazimika!.
Toba!

Kwa nini imezima? Nani kaizima? Nilijiuliza kimoyomoyo. Nikasogea na kuiwasha tena. Ile nasogelea kitandani tu, runinga ikajizima tena. Nikatambua bado kulikuwa na wachawi waliokuwa wakinichezea mule ndani.

Siku moja katika maisha, niliwahi kusikia kwamba wachawi ama mchawi, ukimwonesha woga wako, ni rahisi kukudhuru kuliko ukimwonesha ujasiri. Katika hali hiyo, ndani ya chumba cha hoteli hiyo, nikajikuta najivika ujasiri bandia.
 
Sehemu ya 53

Nikabweka kwa sauti nikisema:
“Nyie mbwa wachawi, hamna lolote la kunitisha wapumbavu ninyi. Mimi nimeaga kwetu. Kama hamjipendi nifanyeni lolote niwaonesha mimi ni nani. Shenzi taipu”
Sikujibiwa na sauti wala chakara chakara yoyote. Ndani ya chumba kulibakia kimya ule ule. Nikaendelea kuketi kitandani nikitegemea kuona kioja chochote. Hata hivyo hali iliendelea kuwa shwari.

Sijui kama ni ule mkwara niliotoa ama ni wachawi tu wenyewe waliona inatosha kunisumbua, kwani niliketi kitandani nikiwa macho hadi inatimu saa kumi alfajiri, utulivu uliendelea kushika hatamu.

Mara nyingi unaambiwa muda wa wachawi kuwanga mwisho huwa ni saa kumi alfajiri, ukizidisha hata sekunde moja baada ya muda huo, ni rahisi mchawi kufumaniwa ama kuonekana na watu.

Kwa kuwa elimu hiyo nilikuwa naitambua vizuri kupitia masimulizi ya vitabu ambavyo niliwahi kusoma, hivyo nikaona angalau sasa naweza kuwa huru dhidi ya mauzauza yaliyonitesa usiku kucha ndani ya chumba cha hoteli.

Nilikwenda bafuni na kuoga kwa ajili ya kujitayarisha na safari ya Dar es salam asubuhi ya siku hiyo. Nilijiandaa nikafungasha kila kilicho changu nikaondoka katika hoteli ya Ristalemi mjini Tabora nikibaki na kumbukumbu isiyoweza kufutika akilini mwangu.

Niliwasili mjini Dar es salam Usiku wa saa tatu. Baada tu ya kuteremka Ubungo, niliwasiliana na kocha wangu mzungu na kumweleza kwamba nimekwisha fika Dar. Akanipa pole ya safari, halafu akanitaka kesho asubuhi niwahi program yake ya mazoezi.

Kutoka pale stendi ya mabasi Ubungo nilichukua usafiri wa tax hadi nyumbani kwangu Sinza, kama utakuwa unakumbuka niliwahi kueleza nyumba niliyokuwa naishi, tulikuwa watu wawili.

Mimi na Cholo, rafiki yangu mwenyeji wa huko Unguja, aliyeniingiza kwenye dunia ya mpira na uchawi. Baada ya kufika, tukasalimiana kisha, nikamsimulia kila kitu juu ya mauzauza niliyokutana nayo huko hotelini Tabora.

“Wacha weee!!! Unataka kunimbia hayo ndio yaliyokukuta? ” Cholo alimaka. “ Huwezi kuamini Cholo. Usiku wote ulikuwa ni vituko tu.” “Felex Kisu naye kumbe mwanga yule jamaa! Si nilikwambia Ajibu.”
 
Sehemu ya 55

“We acha tu ndugu yangu Cholo. Yanii jamaa anajifanya mlokole kumbe mwanga mkubwa.”
“Lazima tufanye kitu.”

“Kipi?”
“Lazima tupambane Ajibu, usitegemee jamaa atakupotezea tu hivi hivi kibwege.”
“Sasa tufanyeje Cholo?”nilimuliza kwa wahaka.

“Tukaonane na yule dokta wa Unguja.”
“Ewaa! Hata mimi nilikuwa na mawazo kama hayo.” Nilishadadia. Nikamuuliza tena.

“Sasa tutaonana naye lini? Kumbuka wiki hii yote tuna michezo ya ligi.” Nilisema. Nikaendelea.

“Tunacheza Jumatano dhidi ya timu ya mkaoni Tanga pia Jumamosi tutakuwa na mchezo na timu ya mkoani Morogoro.”
Cholo alifikiria, uso wake ukaonesha kukubaliana ugumu wa ratiba. Ratiba yetu ilikuwa imebana sana. Nafasi ya kwenda Zanzibar kwa mganga wa kienyeji ilikuwa ngumu.

Akaniuliza:
“Uliwasiliana na kiongozi yeyote juu ya kuwasili kwako leo Dar?” “Niliongea na kocha baada tu ya kuwasili Ubungo.”
“Hilo ni kosa.” “Kivipi?”

“Kama ungekuja kimya kimya ungepitilizia kesho asubuhi Unguja kwa dokta. Jioni ungerejea Dar.”
“Kweli nimepuyanga,” nilikubaliana na mawazo ya Cholo. Nikamuliza.
“Sasa nitafanyaje? Tumtafute mganga mwingine ama?”

“Hapana. Sio jambo zuri kuchanganya waganga kwenye mambo ya shiriki, unajua mambo ya kichawi kila mtaalamu anajua dawa yake ameiandaaje kuchanganya waganga ni kujitengenezea matatizo mapya yatokanayo na dawa hizo hizo.” Cholo alisema.

Jamaa alionekana kuyajua sana mambo ya watalamu. Alionekana ni mtu aliyekuwa mzoefu sana wa kuzunguka kwa waganga. Kama ungepata bahati ya kumwona rafiki yangu huyo, ungeona bangili baya la shaba kwenye mkono wake wa kushoto.

Kwenye vidole vya mkono huo pia, alikuwa amejaza pete karibu kila kidole. Pete ambazo kwa kuzitizama tu hazikuwa na mvuto wowote.

Aliwahi kuniambia vimto vile kila kimoja kilikuwa na kazi yake maishani mwake.
Ukimya ulipita baina yetu. Kila mmoja alikuwa anawaza namna lake.

“Mimi nadhani ulale, hadi kesho asubuhi tutajua cha kufanya. ” Cholo alishauri.
Nilikwenda kuoga ili kuondoa uchofu wa safari, nikala achakula, kabla ya kulala Cholo akanipa mafuta fulani hivi ya maji mfano wa griselini.

“Haya yanaitwa mafuta ya Mzaituni, wanasema yanaondoa nuksi pia hukuwenga mbali na wachawi na majini.
 
Hii kitu ina Arosto...lakini nimeshindwa kuunganisha dots kutoka episode 51na 52 maana sijaona muendelezo ya nn kilitokea baada yakusoma barua zaidi tunaona jamaa yupo lodge tayari Tabora bila kujua alifikaje na kuhusu ile game vipi alicheza!...nimeshindwa kuelewa kabsa huo muendelezo kutoka hapo 51!
 
Hii kitu ina Arosto...lakini nimeshindwa kuunganisha dots kutoka episode 51na 52 maana sijaona muendelezo ya nn kilitokea baada yakusoma barua zaidi tunaona jamaa yupo lodge tayari Tabora bila kujua alifikaje na kuhusu ile game vipi alicheza!...nimeshindwa kuelewa kabsa huo muendelezo kutoka hapo 51!
Watu wa jf hapana jamani ina arosto gani hii story kila siku inawekwa episode 3 muwage mnashukuru basi hata kidogo
 
Story iko poa sana
Sehemu ya 45

Nilihisi mwili wote ukinisisimka wakati nipo ndani ya chumba kile, jamaa alichukua ile ngozi ya mnyama na kuitandika, akatutaka tukae juu ngozi hiyo.

Akachukua mkia ule mkia wa Simba na kutupiga nao kidogo kichwani. Akawasha ubani, moshi ulipoanza kufuka, akajivisha kitambaa cheusi kichwani, kile kitambaa kilifunika uso na kichwa chote, halafu akaketi kwenye kinu cha kutwangia.

Mimi na Cholo tuliendelea kuketi juu ya ile ngozi, tukiangalia kile kilichokuwa kinajiri. Dakikla moja badaye jamaa akapandwa na Majini. “Mnataka kupata nafasi ya kucheza kwenye timu yenu?” sauti moja ya mkwaruzu iliuliza. Yalikuwa ni majini ya yule bwana.

“Ndio....ndio,”tulijibu kwa pamoja. “Hao wachezaji mnao shindana nao, wametumia uchawi mkubwa kujikinga, inabidi utumike nguvu kubwa kuua zindiko lao.”

“Sawa....sawa” tuliendelea kuitikia. “Leteni kuku weusi wa kienyeji na sanda za maiti, sawa?”
“Ndio. ”Cholo aliitikia. Mimi nilishindwa kuitikia, niliona kama tulikuwa tunatumwa vitu vigumu.
Baada ya dakika mbili tatu, majini yale yakaondoka, mganga Majeed akarudi kwenye hali yake.

“Wamesemaje?” akatuuliza.
Moyoni nikajiuliza inamaana huyu jamaa anatuuuliza majini yake yanasemaje, yeye alikuwa hayasikii? Lakini nikakumbuka niliwahi kuambiwa kuwa mtu akiwa amepandwa na majini anakuwa hana fahamu. “Wamesema watu tunaotaka kushindana nao, wamejikinga sana, hivyo sharti tutumie nguvu kubwa kuua zindiko lao. Wameagiza kuku na sanda.”

“Sawa, nishajua kinachotakiwa kufanyika,” Mganga Majeed alisema. Akaendelea.
“Mnaweza kupata hao kuku na hizo sanda ama muache pesa nikatafute mimi hivyo vitu?”

“Nadhani heri tukupe pesa ukatafute mwenyewe.”
“Basi acheni pesa.”
“Shilingi ngapi?”
“Kama elfu arobaini itatosha.” Kwa kuwa fedha haikuwa tatizo kwetu, tulimpa hiyo pesa mara moja. Akatutaka turudi kesho yake ili tumalize kazi kabisa.

Tuliondoka na kwenda nyumbani kwao Cholo huko Fuoni Jitimai. Cholo alikuwa anatokea kwenye familia ya maisha ya kati na ya dini sana, alikuwa akiishi na mama yake mzazi na nduguze wa kike, alimdanganya mama yake tulikuja Zenji kwa mambo binafsi na ndani ya siku mbili tungerudi Dar es salam. Mama yake hakuwa na tatizo.
 
Sehemu ya 56

Asubuhi hiyo, baada ya kupata stafutahi ya asubuhi, wachezaji tuliruhusiwa kuchangamsha akili, kwa mambo mbalimbali, mfano, kuangalia runinga, kusikiliza muziki, kutizama filamu na kadhalika.

Mimi nilikuwa nasikiliza muziki kwenye walkman yangu ya CD, nikiwa kwenye utulivu mkubwa. Mara, nikaikumbuka barua ya mpenzi wangu Lawalawa. Mwanamke mrembo Chotara.
Haraka nikalindeea begi langu la nguo na kutoa bahasha iliyokuwa na barua. Nikairarua bahasha hiyo, nikaichomoa.

Ilikuwa ni barua yenye maneno machache, Niliketi na kuanza sofani na kuanza kuisoma barua ile. Kadiri nilivyokuwa nikisoma mstari mmoja baada ya mwingine ndivyo mapigo yangu ya moyo yakawa yananienda kasi hadi nikaogopa.

Barua Iliandikwa hivi:
Mpenzi Ajibu
Bila shaka u mzima na unaendelea na vema na shughuli zako.
Lengo la ujumbe huu ni kukwambia kwamba, nimepitisha maamuzi magumu kwangu lakini mabaya kwako.

Kuanzia sasa, unavyosoma barua hii, mimi sio wako tena. Muda wowote nitafunga ndoa takatifu na mwanaume mwingine kutoka nchini Yemen.

Ajibu, nasikitika kukukwambia kwamba, nina mimba ya miezi minne ya mume wangu huyo mtarajiwa, huna budi kunisahau maishani mwako. Endelea na maisha yako ya soka, mimi na wewe hadithi yetu imeishia hapa.
Wako wa zamani.
Lawalawa.

Nilipomaliza kusoma barua hiyo, mwili ulikuwa unanitetemeka kama mgonjwa wa homa kali. Jasho jekejeke lilikuwa linanichuruzika maungoni.

Mate yalikuwa yamenikauka kinywani, donge kavu lilikuwa limenikaba kooni, barua kutoka kwa mwanamke ninaye mpenda ilikuwa inanikaanga vibaya sana. “Lawalawa!!!” nilinong’ona. Nilihisi dunia inazunguka kwa kasi mno. Akili yangu ilikuwa imechanganyikiwa.

Nilitamani muda huo huo, niondoke nikaonane na mpenzi wangu yule, anieleze maneno yale kwa mdomo wake. “Ajibu umesikia hiyo?” Cholo, rafiki yangu wa wakati wote alinisemesha, uso wake ulionekana kuwa na furaha. Nikaishia kumwangalia tu bila kumjibu swali lake.
 
Sehemu ya 57

“Umesikia kilichompata kipa namba mbili?” aliniuliza tena. swali lake likanitoa kidogo kwenye tafakuri juu ya barua ya mpenzi wangu Lawalawa.

“Kuna nini Cholo?”
“Jamaa emeshikwa na maralia, unaambiwa yuko tight vibaya. Nimeambiwa nijiandae kwa mchezo wa leo, kweli yule mganga kiboko. ” Cholo alisema kwa furaha.

Akili yangu ilikuwa imevurugika, alichonieleza Cholo nililiona ni jambo la kawaida tu. Jamaa yangu huyo alifurahi na mua ule ule akaanza maandalizi ya kucheza mchezo wa siku hiyo.

Bado mimi nilizidi kusumbuliwa na barua ya Lawalawa, hadi muda wa mchezo ulipowadia akili yangu ilikuwa haiko sawa. *** WATU walikuwa wamefurika kwenye uwanja wa taifa. Wachezaji tulikuwa na presha kubwa, wakati tunaingia uwanjani mimi sikuwa kwenye utimamu wa akili.
Kila nukta, maneno ya kwenye barua niliyoandikiwa na mpenzi wangu Lawalawa yalikuwa yakijirudia akilini.

ILIKUWA ni mechi kubwa katika maisha yangu ya soka. Timu pinzani ilikuwa na utitiri wa mashabiki. Kama nilivyosema mwanzo, muda wote nilikuwa siko sawa kifikra. Nilikuwa najilazimisha kujisahaulisha barua ya Lawalawa, lakini wapi.

Nilipoikanyaga ‘pitch’ ya uwanja wa taifa, kitu fulani kama mzuka kikanivaa mwilini. Ghafla, nikajiona nina morali kubwa. Zile fikra za barua ya mpenzi wangu Lawalawa sijui hata ziliyeyukia wapi.

Dakika chache badaye, mpira ulianza kwa kasi. Tulicheza kwa nidhamu tukiwaheshimu wapinziani wetu. Muda ulivyozidi kwenda ndivyo tulivyozidi kuizoea ile timu kongwe hapa nchini.
Tukawa tunafunguka.

Tunatengeneza nafasi, hatari zikawa nyingi langoni mwao. Dakika ya thelathini nilipata nafasi nzuri, niliuchop’ mpira kiufundi nikimwona mlinda mlango ametoka kidogo langoni.. Kwa bahati tu, mpira ule uligonga nguzo na kurudi dimbani.

Kama samaki, niliruka na kubabatiza mpira kwa kichwa. ukajaa wavuni. Nikaandika bao la kwanza. Uwanja uliokuwa umejaza mashabiki wa timu hiyo kongwe kutoka Kariakoo ukatulia tuli.

Nilishangilia kama mwehu bao hilo.
Ilikuwa ni dakika ya arobaini kipindi cha kwanza, mpira uliwekwa kati, tukacheza kwa tahadhari kubwa.
 
Sehemu ya 58

Timu nzima ilibaki ikilinda bao lile, mbele waliniacha peke yangu na tukawa tunatumia mbinu za ‘counter attack’
Ilitokea hatari nyingine, wakati nakimbilia mpira nikiwa na beki wa timu pinzani, mara nilishikwa na tatizo la msuli, nikajikuta nakwenda chini.

Maumivu makali mapajani yakanitambaa.
Hata nilipopewa huduma ya kwanza, bado sikuweza kupata nafuu. Daktari wa timu aliniuliza kama naweza kuendelea na mchezo. Kwa hali niliyokuwa nayo, nilimkatalia.

Nikatolewa nje na nafasi yangu ikachukuliwa na mtu mwingine. Mchezo huo hadi unamalizika tulitoka kifua mbele kwa ushindi wa bao moja kwa bila.

Bao ambalo nililifunga mwenyewe, lilituacha na point tatu. **** Siku ya pili, jina langu lilikuwa gumzo mtaani, kitendo cha kuichakaza timu kongwe, yenye mashabiki wengi hapa nchini ilikuwa ni tukio lililo bakiza alama fulani kwa wadau wa soka hapa nchini.

Kwa siku mbili zile, niliandikwa kwenye magazeti na kupata interview nyingi, nilichukiwa na mashabiki wa timu ile lakini nilipendwa na mashabiki wa mahasimu wao.

Thamani yangu hata kwa timu yangu ikawa kubwa, kila kiongozi akawa ananiangalia kwa jicho la thamani.

Hakuna aliyemkumbuka tena Felix Kisu.
Siri ya kwenda unguja kwa mganga na kuwaroga wachezaji wenzetu iliendelea kubakia kuwa siri yangu na Cholo. Hakuna aliyekuwa anatambua chochote kuhusu jambo hilo.

Kuhusu Mpenzi wangu Lawalawa, donda la kuachwa na mwanamke huyo liliendelea kuniuma moyoni. Kwa mara kadhaa nilijaribu kuwasiliana naye ili kujua undani wa barua yake, hata hivyo sikuweza kabisa kumpata mrembo huyo.

Maazimio niliyokuwa nimefikia ni kwenda mjini Tabora na kumwona. Nakumbuka baada ya kama wiki moja, kwenye mchezo wetu mmoja wa ligi huko mjini Dodoma, niliomba ruhusa ya kwenda Tabora.

Kwa kuwa tayari nyakati hizo nilikuwa nafanya vizuri kwenye timu, nilikuwa nasikilizwa sana matakwa yangu, waliniruhusu kwenda Tabora huku wakinitaka ndani ya siku tatu niwe nimekwisha rejea Dar kujianda na michezo mingine ya ligi.

Nilipanda basi hadi Tabora mjini, kwa kuwa nilikuwa nimefika mapema.
 
Back
Top Bottom