Simulizi: Sister Murcia

bioto

JF-Expert Member
Oct 1, 2017
1,261
2,095
SISTER MURCIA.
NA HEMED MAYUGU.
NO. (01).
Ni sister ambaye alikuwa na upako mkubwa na
inasadikika alikuwa na uwezo wa kuomba chochote
na mungu akamtekelezea. hata kama alikuwa na
njaa yeye alishushiwa chakuala mahara popote.
Licha ya kuwa na upeo mkubwa. syster murcia
alikwenda kuongeza elimu yake italia.
Baada ya mwaka mmoja alirudi Tanzania kutoka
masomoni.
Alipofika akapewa taarifa kuwa kuna kijiji kimoja
kinaogopwa hasa. watu wageni na watumishi wa
mungu wakienda huko wanauliwa.
Kwa kukatwa katwa mapanga na sehemu zao za siri
kuchukuliwa kwa wanaume na wanawake hubakwa
na kutupwa misituni kama chakula cha mizimu.
Mbali na hilo pia watu hao wanaamini sana imani za
kishirikina.
Baada ya maelezo hayo sister murcia aliombwa
yeye aende huko kwenye hicho kijiji cha kutisha kwa
ajili ya kuiokoa jamii hio na imani potofu imani ya
kishetani na uchawi.
Sister Murcia akakubali kuwa yeye anaweza
kulifanya hilo. kwa imani kubwa ya mungu wake.
Safari yake alikuwa ameambatana na mabint wawili.
Mercia na Alicia mabint hao walikuwa ni wanafunzi
wake. Pia alikuwepo kijana mmoja wa kiume yeye
alijulikana kwa jina la Lukas na deleva wa gari. huyu
aliitwa kwa jina la Moris. Moris ndiye pekee alikuwa
anakijua kijiji hicho. Safari ilianza ya kuelekea katika
kijiji hicho cha kutisha.
Wakiwa njiani walikutana na vitu vingi vya kutisha
kama vyungu vilivyokuwa vimetanda kila mahara
zenye njia panda, mizoga ya wanyama hasa kuku
wekundu na njiwa zilikuwa zimefungwa kwenye miti
imening'inia. Ilikuwa ni safari ya kutisha kweli muda
wote walikuwa wameshikilia Rozari zao wakiomba
mungu awafikishe salama katika kijiji hicho. Masaa
yalikwenda lakini kufikia tamati ya safari yao
ulikuwa ni mtihani mkubwa hatimaye ilitimu mida ya
saa moja za usiku hali iliamza kubadilika kabisa
sauti na miungurumo za ajabu zikaanza kusikika.
Watu wengine walianza kuogopa lakini sister murcia
aliwambia wasiogope wamtumainie mungu na
bwana aliye hai.
Wakiwa wanaendele kukisogelea kijiji hicho gari
ilizima. kupiga sitata ikagoma. Dereva akashuka na
Lucas kuangalia nini kinasumbua gari. lakini hakuon
tatizo. akaomba mercia, Alicia na sister Murcia
washuke wasaidie kuisukuma gari. Ilikuwa ni ngumu
sana kwa Alicia na Mercia kushuka kwenye gari,
mazingira yaliwatisha sana. Kwa ujasiri wa sister
murcia aliwambia vijana wake mericia na Alicia
washuke kwenye gari wasaidie kusukuma.
Kwa pamoja walishuka na kuanza kulisukuma gari,
lakini ilikuwa aisaidii gari iligoma kabisa kutoka.
Waliangaika kama Robo saa lakini hawakufanikiwa
gari liligoma liligoma.
Moris aliangalia tena kama kweli kuna tatizo lakini
tatizo halikuonekana. Wakiwa wanaangaika, kilitokea
kiumbe cha ajabu mbele yao kiumbe hicho kilikuwa
kama mtu lakini chenye mapembe. Uso wake
umetapakaa Damu. Alicia mercia na Lucas. Wote
wakakimbilia kuingia ndani ya Gari. Inje akabaki
Sister Murcia pekee.
Kiumbe kile kililisogerea gari lakini kabla akijalifikia
ulitokea moto ukakizoa na kutupilia pembezoni mwa
barabara na kukiteketeza. Hayo yote yakiwa ni
maombi ya Sister murcia. Baada ya tukio hilo
Pale pale na gari likawaka. Soster murcia akaingia
kwenye Gari na kuwambia vijana wake. "Hakuna njia
njema kama kumwamini mungu na kukaa na imani
thabiti msiyumbe shetani atawaingia kirahisi"
Baada ya kuambia hivyo wote waliitikia sawa na
gari kuondoka. waliivumilia sana safari yao ya
kutisha Usiku mida ya saa mbili na dakika 48
walifanikiwa kukifikia kijiji hicho cha kutisha.
Walilifikia kanisa la kijini hapo. Kanisa lililokuwa
njiani tu. Mazingira ya kanisa hilo yalitisha sana
kulikuwa pachafu sana mapopo ndio lilikuwa ni
makazi yao. Wanyama kama mbwa ndio yalikuwa
makazi yao. Kiujumla ilikuwa ni harufu mbaya kila
mahara ndani ya kanisa hilo. Kwa uzuri walikuwa na
taa zao wakaingia na kuangalia hali ya kanisa
ikawashinda. Wakarudi wakamuomba Dereva wa
gari(Moris), awapeleke kwa uongozi wa kijiji hicho.
Moris aliwambia hapajui na katika kijiji hicho watu
wote huwa wanalala saa moja kuanzia saa 12:30
huwa wanajifungia ndani ya nyumba zao.
Walipoangalia saa zao tayari ilikuwa imetimu mida
ya saa tatu na nusu. Baada ya kuona hivyo syster
murcia aliomba walale ndani ya gari wangoje kesho
ndio waende kuuona uongozi.
"Sister kwanini tusiende kuwaamsha"
Alicia alisema. Bint huyo aliyekuwa mdogo kuliko
wote yeye alikuwa ni muoga hasa mazingira yale
aliyaogopa kabisa. Mambo na Vitu alivyokutana
navyo njiani pindi wanaelekea ndani ya kijiji hicho
yalimtisha. Kijiji hicho kwa jina kilijulikana kwa jina
la Shimo la moto kiliogopeka sana hakuna mgeni
aliyeweza kufika huko na kudumu. Ila wenyeji tu
hata vijana waliokulia huko wakafanikiwa kutokako,
waliogopa kabisa kurudiko.
"Alicia we ni mtoto mwema wa mungu ingieni ndani
ya Gari hakika ulinzi wa mungu u juu yetu tumekuja
kuzipigania Roho za watu wapate uongofu wa
mungu"
Sister Murcia alisema.
"Sawa sister Murcia. Lakini hawa inaonekana
washagongwa mihuri ya shetani hawawezi kutoka
huko"
Alicia alisema.
"Alicia hii ni jamii ya kiafrika hata wewe, babu wa
babu yako alikuwa kama hawa je usingekuja
ukombozi juu yao kutoka kwa watu kama wewe
unazani wewe ungekuwa wapi?"
Sister murcia alimwambia Alicia
Kwa usikivu na utiifu wa mwalimu wao Alicia Lucas
na Mercia waliingia kwenye gari.
Wakala chakula chao walichokuwa ameambatana
nacho. Walipomaliza kula.
Wote kwa pamoja wakaanza kuisoma sala ya
salamu maria kisha Baba yetu uliyembinguni.
Walipomaliza kuzisoma izo sister murcia akaingoza
sala ya kulala. Vijana wake walilala lakini murcia
alitoka ndani ya gari na akatandika kitambaa chake
akakiweka kitabu chake kitakatifu cha biblia kisha
akapiga magoti na kuanza Maombi.
Hakiwa anaendelea nyuma kilitokea kikundi cha
watu.
 
SISTER MURCIA.
NA HEMED MAYUGU.
NO. (01).
Ni sister ambaye alikuwa na upako mkubwa na
inasadikika alikuwa na uwezo wa kuomba chochote
na mungu akamtekelezea. hata kama alikuwa na
njaa yeye alishushiwa chakuala mahara popote.
Licha ya kuwa na upeo mkubwa. syster murcia
alikwenda kuongeza elimu yake italia.
Baada ya mwaka mmoja alirudi Tanzania kutoka
masomoni.
Alipofika akapewa taarifa kuwa kuna kijiji kimoja
kinaogopwa hasa. watu wageni na watumishi wa
mungu wakienda huko wanauliwa.
Kwa kukatwa katwa mapanga na sehemu zao za siri
kuchukuliwa kwa wanaume na wanawake hubakwa
na kutupwa misituni kama chakula cha mizimu.
Mbali na hilo pia watu hao wanaamini sana imani za
kishirikina.
Baada ya maelezo hayo sister murcia aliombwa
yeye aende huko kwenye hicho kijiji cha kutisha kwa
ajili ya kuiokoa jamii hio na imani potofu imani ya
kishetani na uchawi.
Sister Murcia akakubali kuwa yeye anaweza
kulifanya hilo. kwa imani kubwa ya mungu wake.
Safari yake alikuwa ameambatana na mabint wawili.
Mercia na Alicia mabint hao walikuwa ni wanafunzi
wake. Pia alikuwepo kijana mmoja wa kiume yeye
alijulikana kwa jina la Lukas na deleva wa gari. huyu
aliitwa kwa jina la Moris. Moris ndiye pekee alikuwa
anakijua kijiji hicho. Safari ilianza ya kuelekea katika
kijiji hicho cha kutisha.
Wakiwa njiani walikutana na vitu vingi vya kutisha
kama vyungu vilivyokuwa vimetanda kila mahara
zenye njia panda, mizoga ya wanyama hasa kuku
wekundu na njiwa zilikuwa zimefungwa kwenye miti
imening'inia. Ilikuwa ni safari ya kutisha kweli muda
wote walikuwa wameshikilia Rozari zao wakiomba
mungu awafikishe salama katika kijiji hicho. Masaa
yalikwenda lakini kufikia tamati ya safari yao
ulikuwa ni mtihani mkubwa hatimaye ilitimu mida ya
saa moja za usiku hali iliamza kubadilika kabisa
sauti na miungurumo za ajabu zikaanza kusikika.
Watu wengine walianza kuogopa lakini sister murcia
aliwambia wasiogope wamtumainie mungu na
bwana aliye hai.
Wakiwa wanaendele kukisogelea kijiji hicho gari
ilizima. kupiga sitata ikagoma. Dereva akashuka na
Lucas kuangalia nini kinasumbua gari. lakini hakuon
tatizo. akaomba mercia, Alicia na sister Murcia
washuke wasaidie kuisukuma gari. Ilikuwa ni ngumu
sana kwa Alicia na Mercia kushuka kwenye gari,
mazingira yaliwatisha sana. Kwa ujasiri wa sister
murcia aliwambia vijana wake mericia na Alicia
washuke kwenye gari wasaidie kusukuma.
Kwa pamoja walishuka na kuanza kulisukuma gari,
lakini ilikuwa aisaidii gari iligoma kabisa kutoka.
Waliangaika kama Robo saa lakini hawakufanikiwa
gari liligoma liligoma.
Moris aliangalia tena kama kweli kuna tatizo lakini
tatizo halikuonekana. Wakiwa wanaangaika, kilitokea
kiumbe cha ajabu mbele yao kiumbe hicho kilikuwa
kama mtu lakini chenye mapembe. Uso wake
umetapakaa Damu. Alicia mercia na Lucas. Wote
wakakimbilia kuingia ndani ya Gari. Inje akabaki
Sister Murcia pekee.
Kiumbe kile kililisogerea gari lakini kabla akijalifikia
ulitokea moto ukakizoa na kutupilia pembezoni mwa
barabara na kukiteketeza. Hayo yote yakiwa ni
maombi ya Sister murcia. Baada ya tukio hilo
Pale pale na gari likawaka. Soster murcia akaingia
kwenye Gari na kuwambia vijana wake. "Hakuna njia
njema kama kumwamini mungu na kukaa na imani
thabiti msiyumbe shetani atawaingia kirahisi"
Baada ya kuambia hivyo wote waliitikia sawa na
gari kuondoka. waliivumilia sana safari yao ya
kutisha Usiku mida ya saa mbili na dakika 48
walifanikiwa kukifikia kijiji hicho cha kutisha.
Walilifikia kanisa la kijini hapo. Kanisa lililokuwa
njiani tu. Mazingira ya kanisa hilo yalitisha sana
kulikuwa pachafu sana mapopo ndio lilikuwa ni
makazi yao. Wanyama kama mbwa ndio yalikuwa
makazi yao. Kiujumla ilikuwa ni harufu mbaya kila
mahara ndani ya kanisa hilo. Kwa uzuri walikuwa na
taa zao wakaingia na kuangalia hali ya kanisa
ikawashinda. Wakarudi wakamuomba Dereva wa
gari(Moris), awapeleke kwa uongozi wa kijiji hicho.
Moris aliwambia hapajui na katika kijiji hicho watu
wote huwa wanalala saa moja kuanzia saa 12:30
huwa wanajifungia ndani ya nyumba zao.
Walipoangalia saa zao tayari ilikuwa imetimu mida
ya saa tatu na nusu. Baada ya kuona hivyo syster
murcia aliomba walale ndani ya gari wangoje kesho
ndio waende kuuona uongozi.
"Sister kwanini tusiende kuwaamsha"
Alicia alisema. Bint huyo aliyekuwa mdogo kuliko
wote yeye alikuwa ni muoga hasa mazingira yale
aliyaogopa kabisa. Mambo na Vitu alivyokutana
navyo njiani pindi wanaelekea ndani ya kijiji hicho
yalimtisha. Kijiji hicho kwa jina kilijulikana kwa jina
la Shimo la moto kiliogopeka sana hakuna mgeni
aliyeweza kufika huko na kudumu. Ila wenyeji tu
hata vijana waliokulia huko wakafanikiwa kutokako,
waliogopa kabisa kurudiko.
"Alicia we ni mtoto mwema wa mungu ingieni ndani
ya Gari hakika ulinzi wa mungu u juu yetu tumekuja
kuzipigania Roho za watu wapate uongofu wa
mungu"
Sister Murcia alisema.
"Sawa sister Murcia. Lakini hawa inaonekana
washagongwa mihuri ya shetani hawawezi kutoka
huko"
Alicia alisema.
"Alicia hii ni jamii ya kiafrika hata wewe, babu wa
babu yako alikuwa kama hawa je usingekuja
ukombozi juu yao kutoka kwa watu kama wewe
unazani wewe ungekuwa wapi?"
Sister murcia alimwambia Alicia
Kwa usikivu na utiifu wa mwalimu wao Alicia Lucas
na Mercia waliingia kwenye gari.
Wakala chakula chao walichokuwa ameambatana
nacho. Walipomaliza kula.
Wote kwa pamoja wakaanza kuisoma sala ya
salamu maria kisha Baba yetu uliyembinguni.
Walipomaliza kuzisoma izo sister murcia akaingoza
sala ya kulala. Vijana wake walilala lakini murcia
alitoka ndani ya gari na akatandika kitambaa chake
akakiweka kitabu chake kitakatifu cha biblia kisha
akapiga magoti na kuanza Maombi.
Hakiwa anaendelea nyuma kilitokea kikundi cha
watu.
Copied from one of Nigerian movies
That is too bad

Sent from my TECNO K9 using JamiiForums mobile app
 
NO. (02).
ILIPOOSHIA.
Walipomaliza kuzisoma sala izo sister murcia
akaingoza sala ya kulala. Vijana wake walilala lakini
murcia alitoka ndani ya gari na akatandika kitambaa
chake akakiweka kitabu chake kitakatifu cha biblia
kisha akapiga magoti na kuanza Maombi.
Hakiwa anaendelea nyuma kilitokea kikundi cha
watu.
FUATILIA.
Kikundi hicho cha watu, kilikuwa ni kikundi cha
ajabu watu wale walikuwa wamejipaka marangi
usoni, nyuso zao zilionekana kutisha.
Sister Murcia yeye aliendelea na maombi bila hata
kujua kama kuna kundi la watu Saba nyuma yake
wenye kutisha tena wote wanaume wameshikilia
mapanga mikononi wamevaa mairizi shingoni mwao
na mikononi mwao.
Murcia aliiweka Roho yake kwa mungu.
"Eeee! Mungu wewe ndiye tegemeo la moyo wangu,
wewe ndiye msaada na msimamizi wa kila jambo
na mwongozo wa kila nafisi.
Nakushukuru kwa kuweza kutufikisha salama katika
kijiji hiki cha shimo la moto.
Eee bwana mungu, nimejiweka mbele zako
kwakuwa wewe ndiye kimbilio la kila nafisi, nami
nakukimbilia wewe kwa kuhitaji msaada. Ombi
langu kubwa kwako usiku huu nahitaji usambaze
jeshi lako la mbinguni kwa ajili ya ulinzi kwetu kwa
siku zote tutakazo kuwa hapa......."
Bado Sister Murcia akiwa anaendelea watu wa
nyuma walizidi kumsogelea lakini kutembea kwao
kulikuwa kwa hatua moja wanasimama halafu
wanacheza kwa kutikisa vichwa vyao kwa utulivu
huku wameng'ata irizi zao zilizokuwa zimening'inia
mashingoni mwao.
Bado wakiwa wanaendelea kucheza walipomkaribia
wakasimama mmoja kati yao alisogea mbele
kabisa karibu na sister akainua mkono wake wa
kushoto kumkamata kichwa sister Murcia. mkono
wake ulipo kikaribia kichwa cha sister Murcia
alirushwa mbali kama kapigwa na shoti ya umeme.
Wenzake wote wakapotea kimiujiza lakini cha ajabu
mtu yule alishindwa kutoka pale akawa analia moto
moto. Lakini kelele zake zote sister murcia alikuwa
azisikii kabisa bali yeye aliendelea na maombi
mwisho yule mtu akazima kabisa lakini bado
alienedelea kupumua.
"Eee, Bwana ubarikiwe na ushukuliwe, uhidimiwe
siku zote milele amina"
Sister Murcia alimaliza maombi yake kisha
akaichukua biblia yake hakaishika na kitambaa
chake alichokuwa katandika chini na kugeuka kwa
ajili ya kuingia kwenye gari.
Lakini alipogeuka tu akakutana na Mwili wa mtu
yule aliyerushwa na shoti ya hajabu. Sister Murcia
alishituka kwanza kisha akamsogelea mtu yule
alipofikia akamwangalia akagundua kuwa ni mzima.
Sister Murcia alimshika kichwan mtu yule kisha
akasema.
"Eee! Bwana hakika wewe ndiye mwenye kayafanya
haya yote basi mfanye huyu apate kuamka"
Baada ya maombi hayo mafupi tu. Mtu yule aliamka
na kukaa. Macho yake yalipokutana na sister
Murcia alishituka akataka kukimbia lakini sister
murcia akamshika mkono na kumwambia.
"Usiogope kwani tayari upo katika mikono salama
iliyojaa ulinzi wa Bwana"
Mtu yule hakiwa na wasiwasi naye pia akamuuliza
Sister Murcia.
"Kwani wewe ni nani?"
"Mimi ni naitwa Sister Murcia, nimekuja kwa ajili ya
kukiweka kijiji hiki katika mikono salama ya mungu"
"Kwani mungu ni nani?"
"Mungu ndiye mwenye mamlaka yote ya duniani na
mbinguni. Yeye ndiye muumbaji wa kila kiumbe na
anamamlaka ya kuuwa na kufufua"
Sister murcia alisema.
"Lakini mbona niliona moto umekuzunguka
nilipokukaribia lakini mbona uko mzima tu
hujaungua?"
Sister Murcia aliulizwa na mtu yule.
"Uliona moto umenizunguka?"
Sister Murcia aliuliza kwa mshangao
"Ndio niliuona moto
Pindi tu nilipotaka kukishika kichwa chako
nikarushwa kwa nguvu halafu nikauona huo moto
umekuzunguka"
Mtu yule alisema.
"Sasa ulitaka kufanya nini kichwani kwangu?"
Sister mulcia aliuliza.
Akiwa anatetemeka mtu yule alisema.
"Sisi ni walinzi wa eneo hili, ni kundi la kutisha
ambalo liko chini ya kiongozi wa kijiji hiki. Sisi
huwa tuanatumwa kuuwa kila mtu amayekuja hapa"
Mtu yule alisema.
"Kwanini sasa munaua kila mgeni anayekuja hapa?"
"Kwasababu, mala nyingi watu wanaokuja hapa
wanafika na kuaribu mila zetu za kuiomba mizimu
yetu na kuweka utamaduni unao ichukiza mizimu
yetu"
Mtu yule alisema.
"Kwahio wewe bado unataka kuua na kuendelea
kuabudu hio mizimu yako?"
Swali hilo kutoka kwa sister murcia lilikuwa zito
sana kujibiwa na mtu yule.
"Hapana nataka kujua kwanini wewe moto ulikuwa
umekuzunguka halafu ukuungua na kwanini
nilipokukaribia nilirushwa kwa nguvu na wakati
sijawahi kushindwa kabisa mimi?"
Badala ya kujibu mtu yule naye aliuliza tena.
"Moto uliokuwa umenizunguka ni ulinzi wa Bwana
mungu wetu aliye hai. Na kurushwa huko ni mungu
alitaka kukuonesha kuwa yeye hashindwi na
chocbote. Kwani unajua kwanini hujafa?"
Sister Murcia aliuliza.
"Sijui?"
"Basi mungu anakupenda na amekuokoa kutoka
katika imani potofu ya kishirikina. imani mbaya ya
kumwabudu shetani na jeshi lake"
Baada ya kusema maneno hayo mazito yaliyokuwa
yamejaa wokovu mkubwa. Mtu yule alisimama
kisha akasema basi nami nifanye kama wewe, watu
wabaya wakinikaribia basi nami moto unizunguke
nao warushwe kama yeye.
Sister murcia aliinua macho yake juu akamshukuru
mungu kwa muujiza wake, hapo hapo akahesabu
tayari anaye mmoja usiku huo.
*****
Wakiwa kabisa wanahofu kundi lile la vijana saba
walitokezea kwenye mji mkubwa kabisa na mji huo
ndio ulionekana mkubwa kuliko zote kwenye hicho
kijiji. Ndani ya mji huo kulikuwa na kikao kikubwa
cha watu waliokuwa wamekaa mbele yao kulikuwa
na kitambaa kikubwa kilichokuwa kinaonesha kila
kitu ambacho kilikuwa kinafanywa na Sister murcia.
 
NO. (03).
ILIPOISHIA.
watu waliokuwa wamekaa mbele yao kulikuwa na
kitambaa kikubwa kilichokuwa kinaonesha kila kitu
ambacho kilikuwa kinafanywa na Sister murcia.
SONGA NAYO.
Watu wa kikao hicho walikuwa wanaongozwa na
mwanaume mmoja mtu mzima.
Walikuwepo watu zaidi ya kumi, watu hao wote
walikuwa watu wazima tena umri wao ulikuwa si
chini ya miaka 45. mavazi yao wote yalikuwa meusi
isipokuwa mmoja tu, mwenye vazi jekundu na
weupe uliokuwa umepita kiunoni kama mkanda.
huyo ndiye alikuwa mkuu wao. Mavazia yao
yalikuwa ni magauni mapana. Walikuwa
mchanganyiko. Wanaume kwa wanawake. Nyuso
zao zilikuwa zinatisha kabisa kiasi kwamba
ukikutana naye hata mchana lazima ukimbie. Vidore
vilikuwa na kucha ndefu kwa wanawake.
Kikundi cha vijana sita waliosalia kilipita mpaka
mbele wakaanguka mbele ya mkuu. wakamsujudia
na kumuomba msamaha kwa kusema.
"Hakika tulicho kiona kwa mtu yule ni cha ajabu
sana kwetu kututokea hapo kabla ndio mala ya
kwanza ewe mkuu"
Alisema kijana mmoja.
"Ewe mkuu katika Ardhi hii ya shimo la moto basi
tusamehe sisi, na hutupe nafasi nyingine tupate
kujipanga upya kwa ajili ya mtu huyo na hakika
tutamleta kwako mkuu"
Kijana mwingine alisema.
Ingawa kulikuwa na mwanga wa mbalamwezi katika
hanga hilo lakini walipokuwa wamekaa kulikuwa si
chini ya mti wala ndani lakini kwao kulikuwa hakuna
mwanga wa mbalamwenzi lilikuwa giza na walitumia
mwanga wa moto waliokuwa wameukoka.
Kabla hajasema chochote yule mkuu alisiamama,
kisha akasema.
"Nyangubha, nyamumwi, Nyamwesi, Muhoja,
Maengela, na Tulimanywa.
Yalikuwa ni majina ya watu na kila alipokuwa
analitaja jina hilo muhusika alisiamama.
"Enenda mche kumpima Omuno yo amanaka kaye"
Mkuu yule alisema maneno hayo kwa Rugha yao ya
kichawi akimaanisha.
"Nataka mkampime mtu huyo nguvu zake.
Nyangubha, nyamumwi na Nyamwesi. Hawa
walikuwa wanawake, na ndio walikuwa wanaaminika
kuliko wengine wote isipokuwa mkuu wao.
Muhoja na Maengela. Hawa walikuwa wanaume
ndio waliokuwa wanaaminiwa na mkuu wao kuliko
wengine wote.
Baada ya kuambiwa tu waondoke kumpima Sister
Murcia nguvu zake. Wote palepale walipotea mpaka
eneo la kanisa, mbele ya Gari walilokuja nalo watu
wa mungu ndipo walipotokea, sisiter murcia
hakiwa hana Habari kabisa yeye aliendelea
kumuuliza kijana yule maswali ili apate kukijua kijiji
hicho vizuri.
"Ujanambia unaitwa nani?"
Murcia aliuliza.
"Mimi ninaitwa Chaka.
"Chaka!?"
Murcia aliuliza kwa mshangao.
"Ndio"
"Hapana, nitakubadilishia jina. Majina mazuri yamo
ndani ya Biblia. Unajua kusoma?"
"Kusoma?"
"Eee!kusoma?"
"Hapana sijui"
Baada ya kusema hapana sijui, Chaka aliinua uso
wake. Macho yake yalikutana na kikundi cha watu
watano waliokuwa wametumwa kumpima Sister
Murcia, kitendo cha kuwaona wachawi wale tena
wakiwa wanacheka, chaka alimgusa Sister Murcia
begani kumwashilia ageuke nyuma kuwa kuna
jambo la kumshangaza. Sister Murcia aligeuka
nyuma kutazama lakini hakuona kitu.
"Kuna nini we chaka?"
Murcia aliuliza.
Hata kabla hajasema chochote Pale pale waliisi
kama Ardhi inayumba yumba, kile kikundi cha
nyangubha, Nyamwesi, Nyamumwi, Muhoja na
maengela kilianza kuonesha nguvu zao.
Bado wakiwa wanaona kama Ardhi anayumba
yumba kipindi hicho hicho upepo mkari ulivuma
kwa nguvu, mpaka walio kuwa ndani ya gari Alicia,
mercia Lucas na Moris wote wakashituka ilikuwa ni
kazi nzito sana kwa Murcia kuikabili.
Vyote hivyo vikiwa vinafanyika watu wale walikuwa
wamesimama karibu yao kabisa. Huku wameitanua
mikono yao kama mabawa ya ndege na
wakiyumbisha yumbisha vichwa vyao pande zote,
kila walivyozidi kutikisa vichwa ndivyo Sisiter
Murcia alizidi naye kuyumba lakini alikuwa akiisoma
sara ya Baba yetu moyoni, kipindi hicho chote
Chaka yeye alikuwa kaisha anguka chini umepoteza
fahamu.
Kwenye gari, kelele ndizo zilizidi kusikika na
kutwala. Gari nayo ilionekana kuyumba
"Najua mungu uko pamoja nasi, basi kiangamize
kizazi hiki chenye kumwabudu na kumtumikia
shetani"
Murcia aliomba ombi hilo baada ya kuimaliza Baba
yetu uliyembinguni. Kundi lile la wachawi lilipotea
pale pale na hali ikabadilika pale pale na kurudi
katika hali ya hawali.
Murcia alishuka chini na kupiga magoti
akamshukuru mungu kwa ukombozi mwingine
kutoka kwake.
Hali ya pale ilitulia kabisa kabisa.
Ndio muda huo huo, Chaka naye alishituka kutoka
kwenye kupoteza fahamu. Moris na Pamoja na
wenzake wote waliokuwa kwenye gari walitoka inje
kuona nini kimetokea. Sisiter Murcia yeye aliendelea
kumshukuru mungu kwa uokovu aliomuonesheakwa
mala nyingine.
Alicia na wenzake nao walipoona hivyo wakapiga
magoti na kuungana naye kuomba mungu awalinde
zaidi ili kulifanikisha zoezi lao la kukikomboa kijiji
hicho cha Shimo la moto.
*****.
Ndani ya kambi ya wachawi. Mambo yalikuwa
tofauti kabisa na matarajio waliyoyatarajia hali ya
nyangubha ilikuwa ni mbaya, alikuwa analia macho
tu, macho yake yalipata upofu wa ghafra.
Ingawa wengine hawakujeruhiwa lakini walikuwa
wanalia mbele ya mkuu wao na kusema kuwa
waliisi vitu kama sindano zimewashukia na
kuwachoma mwili mzima.
"Mkuu mimi hapana siwezi tena siwezi tena"
Nyangubha alisema.
Japo kuwa tayari wenzake walijieleza kabisa kuwa
walichokutana nacho kilikuwa sio cha kawaida lakini
mkuu wao, akutaka kuamini na kusema bado
watapambana naye.
Baada ya tukio hilo kuwa gumu, mkuu yule wa
wachawi aliamuru wampeleke Nyangubha katika
kifungo asubili adhabu yake ya kukataa kuendelea
kuwa mchawi.
 
NO.{04}
ILIPOISHIA.
Baada ya tukio hilo kuwa gumu, mkuu yule wa
wachawi aliamuru wampeleke Nyangubha katika
kifungo asubili adhabu yake ya kukataa kuendelea
kuwa mchawi.
SONGA NAYO.
Murcia na timu yake waliendelea kuomba.
Usingizi kwao ulikata kabisa. Maombi ya Murcia
yalikuwa ni mungu aweze kuwapa wepesi watu wa
kijiji hicho cha kutisha wokovu wa uzima wa milele.
Alicia na mercia kwa uwoga wao walipenda hata
kulimaliza zoezi hilo kesho asubuhi. Waweze kurudi.
Alicia na Mercia walikosa ujasiri kabisa
wakuendelea kuomba pamoja na sister Murcia.
Mawazo yao yaliwarejesha tena nyuma.
Wakavikumbuka vyote walivyo kutana navyo njiani,
Hasa mapigo ya moyo yalizidi kwenda kasi.
walipokuwa wanamuona chaka jinsi alivyokuwa
akionekana.
Vazi lake lililokuwa ni kitambaa cheusi kajifunga
kiononi, marangi aliyokuwa amepaka usoni.
Muonekano wa chaka uliwatisha na kuwaogopesha
sana. wakatamani warudi kwenye gari lakini waliona
aibu, wakavumilia na kukaa wasubiri mpaka sister
murcia amalize.
Toka tukuio la wachawi kutokea sister murcia na
vijana wake hawakulala walikuwa wanafanya
maombi tu usiku kucha. Toka kipindi hicho
hakukutokea kitu kingine cha kuwasumbua usiku
ulikuwa umetulia ulibadilika ukawa angavu usiku
mpaka kucha.
Asububi mida ya saa kumi na moja ndio muda
ambao Sister Murcia alimaliza maombi.
Watu wengine wote walikuwa wanamwangalia tu,
wao tayari walikuwa washachoka.
Baada ya kumaliza maombi yake sister murcia.
Alikaa akawambia vijana wake.
"Hakika kweli hili ni shimo la moto hakika ni shimo
la moto.
Huku tunahitaji tuiokoe jamii ya watu wa huku
wapate wongofu wala si kuangamiza, ingekuwa ivyo
basi ningemuomba mungu akakiangamiza kijiji hiki
chote kwa moto basi naye angefanya. Lakini
kwanini hajafanya hata kukiangamiza kijini cha watu
hawa. Kwasababu mungu alijua toka hawali kuwa
ninyi ndio mtakiokoa kijiji hiki"
Sister murcia aliwambiw vijana wake.
"Lakini Sister Murcia huyu katoka wapi?"
Mercia aliuliza hakiwa anamuoneshea chaka.
"Ndio maana nikasema kwenu kuwa mungu
kawaleta ninyi akijua kabisa ndio mtamletea
ukombozi katika kijiji hiki cha shimo la moto. huyu
anaitwa chaka. Tangu sasa ni pamoja nasi kwakuwa
tayari yumo ndani ya mikono ya damu ya bwana.
"kwani katoka wapi?"
Alicia aliuliza.
"Huyu kaletwa kwetu na mungu, mungu kamleta
kwetu yeye awe njia yetu na mwongozo kwetu kwa
kijiji hiki"
Sister Murcia alisema.
Baada ya kusema hivyo wote walinyamaza kusikiliza
maagizo mengine kutoka kwa kongozi wao.
Murcia aliwaomba wampe maji Chaka ajisafishe
uso na lucas ampatie nguo zake avae.
Baada ya kumaliza zoezi hilo sister murcia
aliwaomba vijana wake waanze kazi ya usafi
kanisani pamoja na vyumba viwili vilivyokuwa
vimejengwa nyuma ya kanisa. Kwa ajili ya kulala
watumishi wa mu gu.
Maji kwao hayakuwa yashida kwani pale pale
kanisani kwao kulikuwa na Kisima. Chaka alikuwa
anafanya kazi kwa juudi sana kuliko wengine wote.
Kitendo hicho kilipelekea sister murcia kuvutiwa
naye sana na akamfanya mfano kwa wenzake. Siku
nzima kwao ilikuwa ya usafi tu. Kiujumla mazingira
ya kanisa yalionekana vizuri kabisa.
Kila kitu kinachousu chakula walikuwa nacho kutoka
mjini. Kwakuwa mazingira ya kijiji hicho yalikuwa
hayana umeme pia walikuwa na Solar waliyoifunga
kuwasaidia katika mwanga nyakati za usiku.
Toka asubuhi, mchana, jioni hakukutokea kitu cha
kuwatisha.
Siku hio kwao ilikuwa safi kabisa hata usiku wake
walila vizuri tu. Kwelj ulinzi wa mungu ulikuwa juu
yao.
Ikiwa ni siku nyingine mpya. Ilikuwa siku ya Ijumaa.
Sister murcia aliomba afunguliwe chumba cha
kuifadhiwa vitu vya kanisa. (SAKARASTIA) Chumba
hicho kilikuwa kimefungwa na ijulikani mala ya
mwisho kufunguliwa ilikuwa ni lini ingawa walikuwa
wanajua kabisa kuwa ni miaka miwili huko nyuma
ndio alikuja padri akiyejulikana kwa jina la Joseph.
Lakini naye pia haijulikani aliishia wapi. Kwani toka
aingie kijijini hapo hakuwahi kuonekana kabisa na
wala taarifa zake hawakuwahi kuzipata.
Moris wakishilikiana na chaka, pamoja na Lucas
waliweza kulibomoa kufuri la chumba hicho
kilichokuwa kimefungwa miaka kazaa nyuma.
Walipoifungua sakarastia kila mmoja alistaajabu
walizani watakutana na harufu mbaya, vumbi kibao
na takataka zingine.
Lakini kulikuwa angavu mwanga wa ajabu na pakiwa
safi kabisa hata makabati yake yalionekana kung'aa.
Murcia aliinua mikono juu kumshukuru mungu kwa
ulinzi wake kwa vitu vyake kuviweka salama muda
wote.
Akiwa na wanafunzi wake. Walitaka kuimgia mdani
ya chumba hicho lakini walishindwa kabisa, kila
walipokuwa wanajaribu bado walishindwa. Ikawa
kama vile kuna nguvu iliyokuwa i awasukuma
kuwarudisha nyuma.
"Sister nini hiki?"
Alicia aliuliza.
"Sijui lakini huwenda hatujawa wenye imani thabiti
na Bwana mungu wetu"
Kweli baada ya kusema hivyo tu, Murcia aliisi kama
kuna sauti inamuita.
"Murcia, Murcia, Murcia"
Sauti iliyokuwa inaita kwa kunong'oneza. Sister
Murcia aliiskiliza sauti hio akawa anashindwa
kuitambua inatoka wapi. Alibaki kujiuliza na
kugeuka geuka.
"Sister Murcia nini mbona unakuwa hivyo?"
Moris au dereva wao, aliuliza?"
Bila hata kujibu Morcia aliitoka inje ya kanisa
akikimbia kurudi chumbani kwake na kujifungia.
Kitendo hicho kilichanganya Alicia, mercia, moris,
lucas na Chaka wote wakabaki tu, wamesimama
wasitambue nini kimemkuta sister Murcia.
Wakiwa bado kila mmoja wao amesimama kwa
sitahili yake. Mala mlango wa sakarastia ukajifunga
wenyewe hata bila kuguswa. Walipoona mlango
umejifunga wakazani ni upepo tu, Moris akajaribu
kuushika mlango huo ili afungue lakini hakuweza
hata kuufungua. Hakawambia wenzake kuwa
mlango ni mgumu kufunguka nao pia wakajaribu
lakini wilishimdwa hapo kila mmoja akajawa na
uwoga na kutoka inje ya kanisa.
 
NO. (05)
SISTER MURCIA ARUDI TENA NDANI YA
SAKARASTIA SAUTI YA AJABU YAJA. APEWA
KITABU CHA UKWELI KUUSU KIJIJI CHA SHIMO LA
MOTO. ALICHOKIKUTA KIMEANDIKWA NDANI
CHAMSHANGZA.
ILIPOISHIA.
Moris akajaribu kuushika mlango huo ili afungue
lakini hakuweza hata kuufungua. Hakawambia
wenzake kuwa ni mgumu kufunguka nao pia
wakajaribu lakini wilishindwa hapo kila mmoja
akajawa na uwoga na kutoka inje ya kanisa.
SONGA NAYO.
Vijana wote wanne kila mmoja alibaki akijuiliza
kwanini Sakarastia imejifunga pekee kunanini. mbali
na hilo Kazi waliyoifanya ya kulisafisha kanisa
ilikuwa si ya mchezo ilikuwa ni kazi kubwa
kutokana na uchafu lakini ndani ya Sakarastia
kulikuwa safi. ingawa ilikuwa imefungwa lakini hata
vumbi wala utando wa buibui hukuwemo.
Kila mtu alikuwa na lake.
Wakiwa kwenye wimbi la mawazo hivyo hivyo Alicia
na Mercia walienda kwenye chumba chao.
Kumwangalia Sister Murcia lakini walikuta kaufunga
mlango, wakajaribu kuita hakuweza kuitika.
Walipoona hivyo wakaenda kuchungulia dirishani
wakamkuta sister murcia anasali.
Walikaa wakamsubili amalize ndio wafanye
shughuri, zingine.
Alikaa muda sana ndani ya chumba murcia akisali.
Alitumia kama saa moja na nusu ndio akatoka Inje
na kwend moja kwa moja mpaka kanisani. Murcia
aliusogelea mlango wa Sakarastia, alipoukaribia tu,
ukafunguka wenyewe. Sister Murcia akaingia. Pindi
yote hayo yanafanyika Mercia, Alicia, moris, Lucas
na chaka walikuwa wanaona. Sister Murcia alipongia
tu ndani mlango wa sakarastia ukajifunga kama
ulivyokuwa. Murcia akasalia ndani peke yake.
Hakiwa huko huko ndani ya Sakarastia sauti ya
Hajabu tena ikaanza kuliita jina lake, sauti hio
Murcia alishindwa kutambua ni yanani. Aliendelea
kuisikiliza sauti hio ambayo yeye mwenyewe
alikuwa haitambui kabisa kabisa inatoka wapi na
ninani anayeitamka.
"Murcia, Murcia, murcia. Sogea upande wa kulia
mwa kabati hio yenye vitabu kuna box ndogo ya
mbao uifungue utakacho kikuta ukichukue"
Sauti hio ambayo Murcia alikuwa hajailewa inatoka
wapi na ninani anayeizungumza ilianza kumuongoza.
Bila kusita Murcia naye alifuata maelekezo ya sauti
hio ya ajabu. Alipoichukua box alioambiwa
kuichukua akaifungua akakuta kitabu kidogo kabisa
akakichukua kama alivyo ambiwa.
Baada ya kukichukua kitabu hicho Murcia alisema.
"Bila shaka we utakuwa ni malaika wa bwana,
uliyetumwa kwangu ili kuniongoza na kunilinda. Basi
niongoze katika ukweli na unilinde kama Bwana
mungu wetu alivyokuagiza"
Sister Murcia alisema.
Baada ya kusema hivyo ile sauti ilimjibu.
"Hapana Murcia, hapana mimi siye maraika wa
bwana bali binadamu kama wewe"
Sasa kama ni binadamu mbona sikuoni?"
Sister murcia aliuliza.
"Soma kitabu hicho kwanza basi nami utanijua ni
nani, ukimaliza utarudi"
Sauti ile ilisema kisha ikanyamaza.
Akiwa anataka kuzungumza kitu mlango wa
Sakarastia ukafunguka. Sister murcia kwa hofu,
akijiuliza mwaswali mengi kuusu sauti hio, alitoka
inje ya sakarastia. Alipotoka tu na mlango
ukajifunga.
Vijana wake walikuwa wakimsubiri sister ndani ya
kanisa wakingoja wamuulize ni kwanini hayo
yanatokea. Wengine mpaka wakaanza kuogopa.
Lakini hata kabla hawajauliza wao sister murcia
yeye ndiye aliwauliza.
"Nazani hata sasa, mmejawa na hofu na maswali
mengi vichwani mwenu yamerundikana. Kwani si
mwataka kuuliza?"
Kila mmoja alishangazwa na alichokisema sister
Murcia.
"Sasa kajuaje kama sisi tunamaswali?"
Wote waligeukiana wakaulizana, isipokuwa chaka
kwasababu yeye alikuwa bado hajui chochote kuusu
habari za kanisa zaidi yeye alikuwa akijua hasa
maswala ya uchawi.
"Amin nawambieni ninyi. hakika imani zenu ni
ndogo. Imani zenu kwangu ni sawa na kutembea na
mwamvuri, wakati wa mvua iliyochanganyika na
kimbunga. Je unazani utakusaidia?"
Baada ya Murcia kusema maneno hayo wanafunzi
wake wote walipiga magoti na kumuomba
msamaha. Chaka naye bila kujua akapiga magoti
naye kuomba msamaha.
"Tazama nawambieni mimi. Ninyi mmefanya mpaka
kizazi chema kitakachotoke katika tumbo la mtu
mtakatifu na mwema ndicho kije kukikomboa kizazi
hiki kwani ninyi si wenye kuweza"
Kauli hio ilimshitua kila mtu pale.
Mercia, Alicia, Moris na Lucas walikuwa wakijua
kuwa ni maneno kutoka kinywani mwa Sister murcia
kumbe hata yeye alikuwa kanyamaza tu
akiwaangalia wanafunzi wake hao. Sauti hio ilikuwa
ni ya Malaika wa bwana iliyekuwa juu ya kichwa cha
Murcia.
"Kizazi cha mtu huyo mwema ni miongoni mwenu"
Malaika wa bwana alisema tena.
Baada ya kusema tena hivyo na wanafunzi wote
wakiwa wamepigwa na bumbuwazi kwa maneno
waliyoamini kuwa yanatoka kwenye kinywa cha
murcia kumbe hapana bali kutoka kwa malaika
mwema wa bwana.
Alipotea na kumwacha Murcia peke yake.
"Unajua mimi nawashangaa. Badala muandae
chakula cha mchana tule ninyi bado mmekaa.
mnajiuliza nini mbona mmezubaa sana?"
Hio ndio ilikuwa kauli ya Sister murcia.
Bila hata kuzungumza chochote wanafunzi wake.
Yaani, Mercia, Alicia, Moris na Lucas pamoja na
chaka wakatoka inje na kutekeleza alichokisema
mwalimu wao.
Sister murcia yeye alibaki kanisani kukisoma kitabu
alicho pewa ndani ya Sakarastia.
Murcia alikigeuza kitabu chake kwa upande wa
mbele akakuta kimeandikwa. Ukweli kuusu kijiji cha
shimo la moto na ukombozi wake.
Maneno hayo yalimshangaza sana sister murcia,
ikambidi akifungue kitabu na kuanza kukisoma.
Jina langu ni Murcia na hiki ndicho kijiji cha shimo
la moto. Nilifika katika ukanda huu mnamo mwaka
1991 mpaka sasa yapata miaka 23, nipo katika kijiji
hiki cha shimo la moto. Nilifika huku na padre John
Joseph.
Mimi nilizaliwa katika mji wa BUKOBA TANZANIA.
nilianza kulitumikia kanisa tangu nikiwa na umri wa
miaka mitano tu, muda wote nilimtumainia Bwana
mungu wangu nilifanya kila jambo kwa kumtegemea
mumgu. Nikiwa na Umri wa Miaka kumi nilikuwa
tegemezi kubwa katika maombi kwa mungu.
Nikawa nauwezo wa kuwaponya wagonjwa, kupitia
imani kubwa ya bwana. Baada ya wazazi wangu
kuliona hilo waliona si vema kukaa Tanzania,
Tukasafiri nao kunipeleka Vatican katika kanisa kuu
Takatifu la Roma duniani. Ndani ya kanisa
nilifundishwa taratibu za utawa, jina langu la
kuzaliwa niliitwa Joyce, ilipofika kule nikaitwa jina la
MURCIA, jina hilo linasiri kubwa na huwa ni kwa
watu maalumu.
Ndani ya kanisa takatifu la Vaticani moyo wangu
ulikuwa umefungamana na mungu. Muda mingine
sikutaka hata kula nilijifungia ndani ya chumba
changu nikifanya ibada ya kumtukuza na kumuomba
mungu wangu
moyo wangu ukafungamana na mungu mungu
kuliko watawa wote. Na hata nilipo hisi njaa peke
yangu ndani ya chumba. chakula kiliweza kusushwa
na Malaika wa Bwana nikala nikashiba. Nilipofikisha
umri wa miaka kumi na tano. Uongozi wa kanisa
takatifu ulipendekeza niwe kiongozi wa watawa wote
ndani ya kanisa.
Sikutegemea kama ningeweza kuwa na cheo
kikubwa vile.
Nilikubali nami nikawaongoza watawa wote. sielewi
akili na Busara zangu zilitoka wapi, lakini kila
Mtawa mwenzangu alipokuwa ananitazama lazima
ainame na kuniitii. wangine wakawa wanapiga
magoti mbele yangu.
Muda wote huo bado nilikuwa sielewi kwanini
wananifanya hivyo. Kumbe kichwa changu kilikuwa
na nuru. niliweza hata kuomba chochote kutoka kwa
bwana basi nami nilipewa.
Mnamo mwaka 1989. Ndio siku ambayo nilikutana
na Padre John joseph, alipokuja Kuongeza elimu
yake ndani ya vatican.
Padre Joseph alizipata taarifa zangu akanifuata na
kuongea nami kuusu kurudi nyumbani. Tanzania,
nikiwa mwenye furaha hasa, nilikubari kurudi
Tanzani hata kwa wiki basi. Nikiwa nimeongzana na
padre Joseph tuliianza safari ya kuja Tanzani.
Tulifikia ndani ya kanisa kuu la Mtakatifu joseph
jijini Dar es salaam. Tulikaa siku mbili lakini katika
hizo siku mbili padre john joseph hakunitambulisha
hata kwa watawa wala hawakunijua. Kwakuwa hata
kipindi hicho kiswahili nilikuwa sikujui nilishindwa
kuzungumza nao. Lugha yangu ilikiwa ni kiitaliano
basi, hio ni kwasababu nimekulia Italia toka nikiwa
mdogo. Baada ya siku hizo mbili kukaa pale.
Tuliondoka tukaja hapa morogoro, mpaka kwenywe
hiki kijiji cha shimo la moto. Pindi tunakuja katika
kijiji hiki kulikuwa tulivu sana.
Tulifika hapa wawili tu na Padre Joseph. Kanisa hili
lilikuwepo na inasadikika lilijengwa miaka 80
iliyopita na wakorono wa kijerumani.
Baada ya kufika hapa siku mbili Padre John joseph
aliniomba tukitembelee kijiji hiki cha Shimo la moto
tena ilikuwa ni majira ya saa moja za usiku, kipindi
hicho kijiji hiki, kilikuwa hakina sifa za kutisha.
Nilikubali nikaongozana naye mpaka kwa kiongozi
wa kijiji hiki. Ambaye ndio kiongozi wa kundi la
upande wa mashariki wa wamtumikiao shetani.
Tulipofika hapo yule kiongozi alisema neno moja
kwa padre john kuwa TAYARI.
Sitolisahau neno hili. Kamwe sitolisahau.
Baada ya kusema neno hili niliombwa kuingia ndani
nyumba ya kiongozi huyo. Sikuelewa mabadiliko
yalitokea wapi niliisi kizunguzungu na kuanguka
kisha nikapoteza fahamu. Baada ya hapo nilijikuta
tu, niko inje ya kanisa, bahati nzuri sikuwa na jeraha
lolote namshukuru sana mungu. Sababu iliyonifanya
niweze kunguka kumbe ulinzi wa mungu hukuwa
kwangu, basi uchawi uliweza kuniingia na kupoteza
fahamu. Mapenzi makubwa ya Bwana mungu wetu
ndio yaliyonitoa ndani ya nyumba ya kiongozi huyo
mpaka hapa kanisani. Baada ya kufika kanisani
niliingia ndani ya Sakarastia. mpaka leo makazi
yangu ndio haya.
Inasemekana kijiji hiki uchawi ulikuwa ni wakwao na
lakini ulikuwa si wa nguvu kiasi kama cha leo.
Japokuwa katika kijiji hiki kila mtu ni mchawi.
Uchawi wa vita ulianza tu, pale waliposhindwa
kunitoa mimi Kafara lao, hapo ndipo mgawanyiko
wa uchawi ulipoanzia. Ukawa ni vita ambayo ilizuka
baina ya kundi la Padre joseph na kiongozi wa kijiji
hiki.
Vita hio ilikandamiza watu wote wa ngazi ya chini
wengi walikufa kwa kukosa nguvu kubwa ya
kichawi. Hapo ndipo ulipotokea mgawanyiko wa
makundi mawili makubwa ya kichawi upande wa
Mashariki na Magharibi.
Kijiji hiki si wapumbavu wote bali kuna maprofessa
wanaokiongoza na wasomi wakubwa wanaokitumia
kwa ajili ya manufaa yao.
Ukombozi wa kijiji hiki si kwa mwanamke na
haitawezeakana labda kwa Kizazi cha kiume kutoka
katika tumbo la mtu mwema na mume mwema.
Mtoto atakaye zaliwa kutoka katika kizazi cha watu
wema wawili, huo ndiye atakuwa chaguo halisi la
kukikomboa kizazi hiki. Mtoto huyo atalindwa
kutoka katika kizazi chema atakuwa chini ya
mamlaka ya mungu na ulinzj mkubwa kamwe
mkono wa shetani hutomfikia. Kwa Mwanamke
itakuwa ngumu kwa sababu ikifika wakati wa siku
mbaya ni vigumu sana mungu kuyapokea maombi
yake katika uzito wake. Bali nikatika ulinzi tena
usiomkubwa.
Hizo ni siri ambazo washirikina wa hapa wanazo na
wanazitumia. hutojua siku watakayojua wewe huko
katika wakati mbaya bali utashangaa tu unaingia
katika mtego mbaya. vita ni vichache ulivyo viona.
Bado vita kubwa kutoka pande mbili ikiwemo
upande wa padre joseph, ambaye yeye ndiye
kiongozi wa upande wa magharibi.
Murcia wewe ndiye unafaa kwa ajili ya kizazi chema
kukikomboa kijiji hiki.
Baada ya kukisoma kitabu hicho kidogo alichokitoa
ndani ya sakarastia Murcia alichoka.
"Murcia jina lenye siri kubwa. Mimi ndiye nasitahili
kujitoa kwa ajili ya kizazi chema"
Sister murcia alisema kisha akasimama na kurudi
ndani ya Sakarastia.
 
NO.(06).
YAWA NGUMU KWA SISTER MURCIA KUKUBARI
MANENO ALIYOAMBIWA KUUSU KUZAA.
BAADA YA KUENDELA KUBISHANA SANA MWENYE
SAUTI YA AJABU AJITOKEZA.
ILIPOISHIA.
"Murcia jina lenye siri kubwa. Mimi ndiye nasitahili
kujitoa kwa ajili ya kizazi chema"
Sister murcia alisema kisha akasimama na kurudi
ndani ya Sakarastia.
SONGA NAYO.
Sister Murcia aliisogelea mlango wa Sakarastia
lakini ukufunguka akajaribu kuusukuma bado kwake
ilikuwa ngumu, akawaita wanafunzi wake wote na
kuwambia wajaribu kuusukuma wote kwa pamoja.
Badala ya kumsaidia nao pia wakabaki
wanamwangalia tu.
"Ninyi badala mje mnisaidie. Mmesimama tu,
mananiangalia!"
"Hapana sister hata sisi tunashangaa kwanini
umekushinda na wakati unatoka ndani kuja kuingia
ulifunguka wenyewe tu?"
"Sasa mnamaanisha nini?"
"Inaonekana mlango huo ukijifunga mpaka utake
wenyewe kujifungua"
Alicia alisema.
Baada ya kushindwa kuufungua mlango wa
Sakarastia Sister Murcia aliwambia wanafunzi wake
waendelee na shughuri zao wamwache mwenyewe
kanisani.
"Lakini sister kuna jambo umelisema sisi bado
linatupa mashaka!"
Mercia alimwambia sister murcia.
"Jambo gani hilo Mercia?"
Sister murcia aliuliza.
"Umesema kuwa, kwasababu ya udhaifu wetu wa
Imani tutasababisha kizazi cha kijiji hiki kishindwe
kukombolewa mpaka Azaliwe mtoto kutoka katika
kizazi chema. Na huyo mtoto ndiye atakaye
kikomboa kijiji hiki!"
Maneno hayo ya kweli kabisa kutoka katika kinywani
mwa Mercia. Yalimshangaza Murcia, akabaki
kuwaangalia wanafunzi wake asijue azungumze nini.
"Sister Murcia mbona usemi?"
Alicia aliuliza baada ya kuona sister wao kanyamaza
kama anatafakari jambo.
"Hapana! Nimesema saa ngapi maneno hayo?"
Murcia aliuliza.
Ulisema kipindi tu, unatoka ndani ya Sakarastia
ukiwa umebeba kitabu hicho hivyo hivyo".
"Kweli?"
"Ndiyo!"
Sister Murcia aliuliza kwa mshangao, kwasababu
kilichozunguzwa kuwa yeye ndiye kakisema sio
kweli, japo ni cha kweli lakini yeye hajasema bali
kakisoma kwenye kitabu alichopewa ndani ya
sakarastia. Alichokisema Mercia kimetamkwa na
malaika mwema wa bwana.
Baada ya kuona kuwa kilichozungumzwa na
wanafunzi wake kimemuingia Murcia aliwaomba
wanafunzi wake wakendelee na shughuri zao yeye
atawapatia majibu baadaye.
Wanafunzi wake walimwacha na kwenda kuendelea
na Shughuri zao.
Akiwa mwenye mawazo mengi, akitafakari
alichokisoma na alichoambiwa vyote vinafanana,
lakini ni nani kakisema ambacho Ameambiwa na
Mercia kuwa yeye ndiye kakitamka. Hilo lilikuwa ni
swali alilokuwa akilitafakari sana Sister Murcia.
Baada ya kufikiri kama dakika tano bila majibu
aliamua arudi kwa Bwana mungu wake. Huko alijua
majibu lazima hayapate.
Murcia aliisogelea Bikira maria na kuanzia kusali
sala ya salamu Maria. Baada ya kumaliza aliyainua
macho yake akaanza kuomba alichokuwa anakihitaji
kwa Mwenyezi mungu, akiwa anaendelea kusali,
Mlango wa Sakarastia ulifunguka, sauti ya Ajabu
ikaanza kumuita kutoka ndani ya Sakarastia. Kwa
utulivu kabisa aliisikia sauti hio, ikimuita. Baada ya
kuisikia sauti hio, sister murcia alijinyanyua na
kuelekea kwenye Sakarastia. Alipoingia tu mlango
ukajifunga.
"Murcia umesoma kitabu hicho?"
Sauti iliuliza.
"Ndio nimesoma!"
Sister murcia alijibu.
"Kipi ambacho ujakielewa?"
Sauti iliuliza.
"Mengi tu sijayaelewa na sijui kwanini!"
Murcia alisema.
"Najua hujaelewa lakini mimi nimekaa miaka yote
hio 23, tena ndani ya Sakarastia humu, humu.
Huwenda wewe kipindi hicho ndio ulikuwa na miaka
12, uwezo wangu wa kuongea na mungu ni mkubwa
kuliko wewe, vigezo mimi nalala humu humu,
nakula humu, na macho yangu yamejizuia na kuona
mambo ya Dunia. Wakati wote yanasoma na
kutazama mamlisho ya mungu. Kinywa changu
Akifanyi kingine zaidi ya kulitaja jina la Bwana
mungu wetu aliye hai mbinguni"
Sauti ilisema.
"Murcia sasa wewe, kwanini aliamua kukaa humu na
kushindwa kukiokoa kijiji hiki cha wachawi?"
Sister Murcia aliuliza sauti Ambayo pia mwenye
nayo anadai ni Murcia.
"Nilibaki mwenyewe tu, sikuweza hata kufanya
chochote, hapo niliamua nimuombe mungu aniifadhi
humu mpaka nitakapokufa!"
Baada ya kuambiwa Hivyo sister Murcia hakutaka
kuuliza chochote kuusu maisha ya Murcia
kwasababu alikuwa anajua kabisa sifa zao, Murcia
wote ndio kawaida yao. Walikuwa ni watu wa
kufungamana na mungu muda wote. Alibakiwa na
maswali mawili tu ambayo yalimuusu yeye.
"Nimesoma katika kitabu umesema jina la Murcia ni
la siri kubwa. Napenda kujua?"
Sister Murcia aliuliza.
"Soma historia yako. Wewe uliitwa Judith. Jina hili
lilikufa tu, baada ya kukulia katika chuo cha utawa,
kilichopo katika kanisa la Mtakatifu Joseph. Dalili
za kwanini wewe Uliitwa Murcia ni kwamba wewe,
ulikuwa na Upeo mkubwa wa kuongea na mungu.
Namaanisha ulikuwa unaomba chochote lazima
kitimilizwe, watu wa aina hio tu ndio wanaitwa
Murcia. MURCIA ni neno la kirumi lenye maana.
UKARIBU KWA MUNGU"
Maneno hayo kutoka kwa Murcia ambaye Sauti tu
ndio inasikika yalimuingia sister Murcia na
kuayaelewa.
"Nimesoma kwenye kitabu, kuwa Kijiji hiki hakiwezi
kukombolewa na Mwanamke mpaka azaliwe mtoto
mwema wa kiume kutoka katika kizazi chema. Na
ukanipendekeza mimi ndio nastahili kumzaa mtoto
huo?"
Sister Murcia aliiuliza Sauti.
"Dalili zote ushaziona. Na nazani mungu hakupitisha
kwangu tu taarifa hizo. bali kazipitisha kwako
kupitia mwanafunzi wako.
Murcia si lazima we kufanya hivyo lakini tayari
utabili kutoka kwa mungu siku zote huwa wa kweli
na wala huwa haupingiki wala kukimbiwa.
Kumbuka wewe nikiumbe chema murcia hata
ikienda wapi, mikono ya mungu itakuwa juu yako tu,
ndio maana wewe unastahili kubeba mimba kutoka
kwa mwanaume mwema ili umuzae mtoto
aliyemwema kwa ajili ya kijiji hiki. Hakika sisi
wanawake tuna udhaifu mkubwa ingawa tayari
historia yetu sisi wanawake mabikira tunaomuenzi
Bikira maria ni strong kutoka ulipoanzishwa"
Sauti ilisema, kwa msistizo maneno hayo
yalimuingia sisiter Murcia lakini bado ilikuwa ngumu
kukubaliana nayo.
"Ebu angalia hata katika kitabu sisi wanawake
mabikira tulivyo na sifa ya kipekee. Kufuatana na
mifano ya Yesu Kristo na Bikira Maria, Agano Jipya
linatoa habari za wanaume na wanawake
waliojinyima ndoa kwa ajili ya ufalme wa Mungu,
kama vile mabinti wanne wa Filipo mwinjilisti
waliokuwa mabikira na manabii (Mdo 21:9). Hasa
mtume Paulo aliwahimiza Wakristo wowote
wanaoweza wafanye hivyo kama alivyofanya
mwenyewe kwa kufuata shauri la Bwana (taz. 1Kor
7:25-34). Nitaanzia wapi kuzaa wakati tayari
nishakula kiyapo kikubwa, Murcia bora nipambane
mimi mwenywe"
Sister murcia alisema tena mpaka kwa kuutoa
mfano mwema wa wanawake Bikira kutoka ndani ya
biblia.
Baada ya kusema hivyo, ghafra mwanga mkubwa
ulitokea mbele yake. Kilichotokea pale alikuwa
mwanamke mzuuri mwenye mng'aro wa pekee.
"Mimi ndiye Murcia wa kwanza kwako. Hata mimi
nasikikitika lakini lengo ni kukikomboa kijiji hiki.
Kumbuka Lengo la Ubikira kwa wanawake ni
kumuenzi na kumtukuza Mtakatifu aliyebarikiwa
kuliko wanawake wote. Pia ni sifa ya kipekee
kuonesha ukristo ulivyo na nguvu kuliko kikingine
chochote.
Na hata kwa wanaume pia ni kama ulivyotoa mfano
wa mtume paulo alivyo fanya kwa kufuata shauri la
Bwana. Lakini hakuna namna inabidi ujitoe kwa ajili
ya kizazi hiki"
Murcia wa kwanza alisema.
 
NO.(07).
SISTER MURCIA AJIFUNGIA NDANI YA SAKARASTIA
SiKU MBILI AKISALI. AOTA NDOTO MBAYA YA
KUTISHA. AIKOLEWA NA MTOTO.
MTOTO AMWITA SISTER MURCIA MAMA.
ILIPOISHIA.
Na hata kwa wanaume pia ni kama ulivyotoa mfano
wa mtume paulo alivyo fanya kwa kufuata shauri la
Bwana. Lakini hakuna namna inabidi ujitoe kwa ajili
ya kizazi hiki"
Murcia wa kwanza alisema.
SONGA NAYO.
Macho ya sister Murcia yalibaki kumtazam Murcia
mwenzake. Kichani mwake alikuwa.Akitafakari ni
jinsi gani ataweza kubeba mimba na kuzaa na
wakati tayari yeye kaisha kula kiyapo kuwa yeye
atabaki kumtumikia bwana tu wala si kwa swala
lingine.
"Murcia nimeenda kuongeza Elimu yangu kwa ajili
ya kuendelea kuwa karibu na mungu. Mi naamini
kabisa mungu yu pamoja nami, mungu awezi
kuniacha niteseke na kukiacha kizazi hiki kiangamie
lazima nitapambana na mungu atanipa nguvu tu na
kunilinda"
Sister Murcia alisema kwa upole.
"Murcia hata Bikira maria alitegemewa kuwa nabii
wa bwana lakini akazaliwa mwanamke. Hakuweza
kufanya mapenzi mpaka anachumbiwa, kwasababu
alikuwa mwnamke mwema mungu akampa mtoto
kupitia Roho matakatifu, ambaye huyo mtoto ndiye
mkombozi wa ulimwengu huu. Mungu aliona kuwa
ulimwengu umejaa dhambi ndio maana akamtoa
mtoto wake kipenzi na wa pekee kwa ajili ya
ulimwengu. Tazama mungu akakubari kumdhalilisha
mwana kwa kutundikwa msalabani lakini kwa ajili
ya ukombozi. Ingekuwa ni nguvu za mungu kwa
mwanamke si angemwacha Mariam ndiye
akaukomboa ulimwengu kutoka Katika dhambi.
Tafadhali hili niagizo la Bwana. Limepitia kwangu.
Hata usipo amini bado mimi ni mkubwa kwako"
Murcia mkubwa alisema.
Baada ya kusema hayo Murcia huyo alisimama na
kusema.
"Nilikuwepo hapa tangu miaka 23 iliyopita na leo
naondoka kwakuwa mwisho wangu umepita.
Tafadhali wewe ndiye mwenye mamlaka na chumba
hiki, tangu sasa. Mtoto utakaye mzaa njoo mkabizi
kwenye chumba hiki ili awe karibu na bwana"
Baada ya kusema maneno hayo, Murcia alitoweka
kama alivyo tokea.
Akiwa Mwenywe mawazo ajui nini cha kufanya
Sister murcia alijinyanyua pale alipokuwa na kutoka
ndani ya Sakarastia. Japo alikabiziwa yeye chumba
hicho lakini alipotoka tu hata akuugusa mlango
wenyewe tu ulijifunga. Alikaa chini ndani ya kanisa
akiyatafakari maneno aliyoambiwa ndani ya
Sakarastia. Akawa aamini kabisa kama ni kweli
machozi yakaaza kumtoka. akiwa bado yuko
kwenye mawazo mengi, Alicia alikuja kumuita kwa
ajili ya chakula.
Alicia alishindwa hata kumwambia Murcia swala la
chakula, naye pia alikaa ili kujua nini kinamsibu
mwalimu wao.
"Sister Murcia, nini kinakusumbua mbona unalia?"
Swali hilo Murcia akulijibu, alishindwa aanzeje
kuongea na vijana wake kuusu kubeba mimba na
kuzaa mtoto ambaye ndiye atakikomboa kijiji hicho
cha shimo la moto.
"Naomba unambie kweli mimi nilisema kuwa
anapaswa azaliwe mtoto mwema kutoka katika
kizazi chema, ili awe mkombozi wa kizazi hiki cha
Kichawi?"
Sister Murcia aliuliza kwa kujing'ang'aniza.
"Ndio umesema, tena umeanza kwa kutolea mfano
kuwa sisi si wenye imani thabiti. Kuwa nasi ni sawa
na mwamvuri wakati wa mvua iliyoambatana na
kimbunga"
Maneno hayo sister Murcia aliyasikia lakini
akashindwa kuamini kabisa. Ilimbidi amrudishe
murcia na kumwambia kuwa waendelee kula yeye
ajisikii njaa. Akiwa na masikitiko makubwa sana
moyoni. Murcia aliamua arudi ndani ya sakarastia
kumuomba mungu amuoneshee ukweli juu ya jambo
hilo.
*******
Murcia alikaa ndani ya Sakarastia siku mbili. siku
mbili bila kunywa wala kula. alikuwa kama ni mtu
aliyefunga akiomba. Ikiwa ni Majira ya saa sita
mchana, Kutokana na njaa Murcia alianguka chini
ndani ya Sakarastia. Alipoanguka pale pale, usingizi
ulimpitia kabisa. Akiwa usingizini aliota ndoto akiwa
polini karibu na mto akionekena mwenye Damu
kwenye nguo zake. Alisikitika sana, akazivua nguo
zake na kuzifua. baada ya kuzifua akazianika, akiwa
bado anasubili zikauke avae, alisikia makelele kama
kimbunga na sauti za ajabu kama za watu
zikimfuata. Ghafra aliona kundi la watu nane wa
ajabu likimsogelea, watu hao walionesha dalili zote
za kuwa ni wachawi, walikuwa ni watu wazima
kabisa. Wanne wakiwa ni wanawake na wannne
wakiwa ni wanaume. Murcia alishindwa afanye nini
na kipindi hicho alikuwa hana nguo. Baada ya kuona
kundi linazidi kumsogelea alisogea kinyume nyume
mpaka zilipokua nguo zake na kuzichukua hivyo
hivyo na kujifunga kusitili sehemu za wazi. Akiwa
anafanya haraka haraka, sister murcia alipiga magoti
na kusema. Eee mungu, nilinde na hili kundi baya la
Shetani. Kitendo cha kusema hivyo tu, alitokea
mtoto mmoja wa kiume umri kama miaka mitano,
mtoto huyo alikuwa kavalia mavazi meupe kama
padre mbele yake. Mtoto huyo alilinyoshea tu
mkono kundi lile la watu likaanguka chini na kufa
pale pale.
Baada ya kitendo hicho, yule Mtoto alimsogelea
sister murcia na kumwambia
"Mama nenda kwa Amani kwani ufalme wa bwana
uko juu yako nami pia niko mbele yako"
Bado akiwa usingizini aliisikia sauti ikimwiita
Mama, amka amka tayari amka. Sister murcia
akiwa na njaa kubwa alishituka. Kutoka usingizini
huku akiwa anahema, ndoto aliyoita ndio ilisabisha
kushituka. Lakini alivyoshituka usingizini macho
yake yalikutana na Mtoto kama huyo aliyekuwa naye
ndotoni kaweka chakula mbele yake na kumwambia
"Mama kula uwasadie wanafunzi wako kwani hata
sasa wanateseka hawana msaada"
Baada ya kusema hivyo yule mtoto alitoweka mbele
ya macho yake. Sister Murcia alishindwa kuamini
kabisa kile alichokiona, bado alishindwa kayaamini
macho yake. Akayapikicha akiamini kuwa yupo
usingizini lakini ilikuwa ndio ukweli. Kusimama
alishindwa kwasababu ya njaa ikabidi aombe sala
ya chakuka.
Akaweka njia ya msalaba.
"Kwajina la Baba na la mwana na la roho mtakatifu
amina.
Eee baba yetu uliyembinguni, nashukuru kwa
kuniwezesha chakula nile ili nipate nguvu ya
kukutumikia vema amina"
Baada ya kumaliza kusali sala hio fupi sister murcia
alikila chakula hicho ambacho ilikuwa mikate
mitamu iliyoshushwa toka mbinguni. Alipomaliza
kula. Akamshukuru Bwana kwa chakula kisha
akaomba kutoka.
Mlango wa Sakarastia ulifunguka sister murcia
akatoka. Alikuta tayari ni giza kumbe toka alale saa
sita za mchana alikuja kuashwa saa moja za jioni.
Kanisani aliwakuta wanafunzi wake kila mmoja
kajikunja kwenye kona yake kwa uwoga.
Alipotazama inje aliona kundi la watu kama nane
wakiwa wameshikila mapanga. Watu wale walikuwa
wamekaa tu na walikuwa wanaume tupu. Pembeni
yake alimuona chaka kafungwa kamba na akiwa na
majeraha usoni, na miguuni sistet Murcia aliumia
sana kumuona chaka yupo katika hali ile. Bila
kuogopa sister murcia alitoka inje ya kanisa
kuwafuata watu hao . Alipotoka tu inje ya kanisa
kichwa chake kikaanza kutoa mwangaza wa mkali,
watu wale walipomuona tu hivyo wote walikimbia
kila mmoja njia yake hakuna aliyebaki kuendelea na
kilichokuwa kimemleta. Sister murcia mwenywe
alibaki anajishangaa lakini tayari alijua kuwa ni
ufalme wa Bwana u juu yake. Alimsogekea Chaka
na kumwangalia akagundua kuwa amepoteza
fahamu, bila machozi yalianza kumtoka sister
Murcia, pale pale jina la kumuita chaka la kikiristo
likamuhijia.
"Paulo amka, Amka paulo!"
Maneo hayo mawili mala mbili, majeraha yote
yaliyokuwa katika mwili wa chaka/paulo yalififia
yote, akarudi katika hali yake na kusimama. Baada
ya tukio hilo sister Murcia aliongozana naye mpaka
kanisani akawakuta wanafunzi wake Moris, Lucas,
Mercia na Alicia. Wote wamejikunja pande zao.
Murcia aliwakusanya ili awaulize nini kimefanywa
kwao na watu wale walikuwepo na mapanga.
Wanafunzi wote kwanza walikuwa awaamini
kumuona chaka/paulo yupo katika hali ya uzima
kabisa.
 
NO.(08)
ILIPOISHIA.
Murcia aliwakusanya ili awaulize nini kimefanywa
kwao na watu wale walikuwepo na mapanga.
Wanafunzi wote kwanza walikuwa awaamini
kumuona chaka/paulo yupo katika hali ya uzima
kabisa.
SONGA NAYO.
Hapo kila mmoja moyoni akaanza kujua kuwa imani
yake kweli ni ndogo.
"Tangu sasa huyu mtamuita paulo"
Murcia alisema.
"Sawa"
Hio ndio ilikuwa kauli ya kwanza kutoka kinywani
mwa sister Murcia katika kikao chake,
akimtambulisha chaka kwa jina jipya la paulo.
"Hebu naombeni mnambie ni nini watu wale
walifanya kwenu?"
Murcia aliwauliza wanafunzi wake.
"Walikuja kwa ajili yako walivyo dai!"
Mercia alimjibu.
"Kwanini ninyi msinge wazuia mkapambana nao?"
"Sisi hatukua wenye huwezo wa kupambana nao,
hata chaka aliyewazoea yeye alijaribu kupigana nao
lakini wakamwangusha mala moja tu na kumjeruhi.
Tulivyo ona hivyo hatukuwa tena wakukaa ikabidi
tukajifiche humu, tukiwa humu wakasema hawakuja
hata kwetu bali kwako!"
Alicia alisem.
Kipindi hicho chote Moris na Lucas wao walikuwa
wamenyamaza wakiona aibu hata kuongea.
"Tazameni ninyi watu. Mbona nwamuuzi bwana,
tazama ninyi mmechaguliwa kwa ajili ya
kukipambania kijiji hiki ili kukibadilisha. lakini ninyi
mnafanya vyenye kumuuzi bwana mnakosa imani
kabisa mnazidiwa na Paulo/chaka, ambaye hata
kusoma na kuandika hajui. Je amna imani na
bwana mungu wenu?"
Murcia alizungumza kwa kufoka mbele ya wanafunzi
wake.
"Eeee! Murcia hakika wewe ndiye kiongozi wetu.
Tusamehe na utufundishe yaliyomema, hakika imani
yetu ni haba!"
Mercia kwa kuwawakilisha wenzake alisema.
Sister murcia alisikitika sana, akuamini kabisa
kilichokuwa kinatoka vinywani mwa watu wale.
"Hata wiki mbili hatujamaliza, bado hata kuanza
kuwatembelea watu kwa ajili ya kuwapa fundisho la
bwana sijui itakuwa vipi"
Murcia alisema.
Lilikuwa ni jambo la kumsikitisha sana Murcia.
hakuweza kuamini, akaanza kujutia kwanini
alichukua maamuzi ya kuongozana na watu
wasiyokuwa na faida kwake. Usiku mzima
hakuweza hata kusema nao tena mpaka kunakucha.
Siku iliyofuata Murcia alimchukua chaka na kuingia
naye kwenye sakarastia na kuanza kumfundisha
kusoma na mafunzo mengine ya dini ya ukristo.
Zoezi lilikuwa endelevu wanafunzi wengine aliwapa
zoezi la kuisoma biblia na kuomba mungu ili
wapate kuzikuza imani zao.
Zoezi la kumfundisha chaka lilimchukua wiki tu,
mwanaume yule akaweza kusoma. Jambo hilo
lilimshangaza sana Sister nurcia, hakuweza hata
kuamini, imekuwaje mtu yule aliyekua na imani
haba apate wepesi wa kujua kusoma mapema.
Ikiwa ndio wamemaliza wiki ya Tatu pale kijijini,
Murcia aliwakusanya wanafunzi wake wote ili
kuzungumza nao na kupeana darasa juu ya uwepo
wa Bwana.
Wanafunzi wote walikusanyika wakakaa pamoja ili
kumsikiliza mwalimu wao.
Murcia aliwaomba kwanza chaka awambie ni nini
siri yake ya kuweza kukisoma kitabu kitakatifu ndani
ya wiki. Wakiwa makini kabisa wote kumsikiliza,
chaka alisema.
"Hakika haya sio mamlaka yangu kuja kwenu bali tu
yeye yule aliyembingini!"
Maneno hayo tu, yaliwafanya wote mpaka sister
Murcia kumgeukia na kumtazama.
"Ebu ninyi ndugu zangu tazameni. Kwani hata lile
neno alilolisema bwana amkuliona?"
Paulo/chaka aliuliza. Kila mmoja alibaki
kumshangaa, wote hata sister murcia wakauliza
"Neno gani hilo paulo?"
"Hakuna mtu awezaye kuja kwangu, asipovutwa na
Baba aliyenipeleka; nami nitamfufua siku ya
mwisho."
Chaka alisema.
Neno hilo liliwashangaza wote, hakuna aliyeweza
kuamini kama chaka anauwezo wa kuisoma biblia
na kuyatambua yaliyomo kwa siku chache.
"Ninyi; mimi nawambieni pia nawakumbusheni.
Kwani siku ile ya kwanza kuja kwangu, Sister murcia
aliwambieni nini kuusu mimi?"
Hapo kila mmoja alinyamaza hakuna ambaye
aliweza kulijibu swali la chaka.
"Basi alisema. Huyu ni mwenzetu, bwana kamleta
kwetu ili awe njia kwetu!
Je hakusema neno hilo?"
Wote kwa pamoja wakaitikia alisema.
"Mimi nayajua mengi hata msiyoyajua ninyi. Na
ninyi amjui kwasababu imani zetu ni haba. Tizama
maneno ya Bwana juu ya watu wenye imani na
wasiyo na imani.
Twajua ya kuwa Mungu hawasikii wenye dhambi;
bali mtu akiwa ni mcha Mungu, na kuyafanya
mapenzi yake, humsikia huyo"
Chaka/paulo alisema.
Alicia, Mercia, Lucas na Moris walibaki kumshangaa
chaka/paulo.
Kila mmoja alitamani kujua chaka kawezaje
kuisoma na kuyasema yaliyomo kwenye biblia bila
hata kusoma.
Uwezo wa chaka ukuwashangaza wenzake tu hata
Murcia naye ulimshangaza.
"Chaka unaweza kusema, umewezaje kuyajua hayo?"
Murcia aliuliza.
"Hakika imani ni ukombozi wa kila moyo katika
ardhi ya bwana.
Ndio maana Bwana akasema.
" Mngekuwa na imani kama chembe ya Haradali
basi mngeweza kuuwamuru huu mti wa Mkorosai
ung'oke na ukajitose baharini, basi nao ungetii"
Chaka alisema maneno ambayo kila mmoja
yalimuingia.
Chaka/paulo anasema kuwa walipokuwa anamaliza
kufundishwa na Sister Murcia jioni. Muda wa kulala
usiku yeye alikua akiomba ikifika muda wa saa
saba za usiku bwana mungu haweze kumwamsha ili
asome.
Anasema kuwa
"Mida hio nilikuwa natoka chumbani kwetu naenda
ndani ya Sakarastia. muda huo nilikuwa naamini
kuwa sister Murcia alikuwa kaisha toka ndani ya
Sakarastia. Nilikuwa nikifika pale mlango
unafunguka wenyewe, nami niliingia na kusoma,
nilifanya hivyo katika siku tano nikawa nimeweza
kuisoma biblia"
Huyo ndio ukweli kuusu kijua biblia.
Mazungumzo yao yalichukua muda kama saa zima
yakamalizika. Baada ya kumaliza kikao hicho
chaka/paulo alimuomba sister Murcia wazungumze
kwa usiri. Wote kwa pamoja wakaongozana
kuelekea kwenye Sakarastia.
Walipofika ndani ya Sakarastia Paulo alimwambia
Sister Murcia.
"Je waonaje juu ya hili jambo la mtoto mwema
atokaye kwa bwana kwa ajili ya kukiokoa kijiji hiki?"
Maneno hayo kutoka kwa chaka yalimshangaza
sana, Murcia hakuamini kama paulo/chaka naye
analijua swala hilo.
"We umejua vipi?"
Sister murcia aliuluza.
"Nikiwa nimelala usiku humu ndani ya Sakarastia
nimepatwa na ndoto, kutoka kwa mtu aliyekuwa
kashikilia kitabu akanambia. Yupo mtoto mwema
mwenye kuzaliwa kwa ajili ya kijiji hiki kutoka katika
kizazi cha watu wema. Huyo ndiye mwenye
mamlaka ya kukikomboa kijiji hiki. Nilipoambiwa
hivyo nilishituka kutoka usingizini na kurudi
chumbani kwangu"
Paulo/chaka alimwambia sister murcia.
"Mala ya tatu nalisikia neno hili, tena nimeoneshwa
mtoto akiniita mama huku akinikomboa kutoka
katika kundi la shetani"
Sister murcia alijisemea kimoyo moyo. Kisha
akamuomba chaka atoke inje yeye angelifanyia
kazi.
********
Basi masaa yalienda sister murcia akaona tayari
kuwa kipimo cha imani kwa wanafunzi kimekuwa
Imara. Usiku huo wa siku hio aliwambia wanafunzi
wake kuwa kesho wataanza kutembea ndani ya kijiji
ili kulitangaza neno la bwana kwa watu wa kijiji cha
shimo la moto.
Kwakuwa kipindi hicho walikuwa salama kabisa
awasumbuliwi na kundi la Shetani kesho kulikucha
salama na safari ya maandalizi yao ya kutembelea
miji ya wakazi wa kijiji hicho cha shimo la moto
ikaanza.
Walikitembelea, walijitahidi kupita kila nyumba
waliyokuwa wanakutana nayo, muongozo wa
msafara alikuwa ni chaka/paulo. Ilikuwa ni safari ya
kusumbuka kwao, nyumba zingine walijaribiwa kwa
uchawi lakini waliweza kupambana nao na
kuushinda. walijitahidi kuubili sana kwa watu wa
kijiji hicho. lakini kwao ilikuwa ni ngumu kueleweka.
Siku ilipita lakini hawakupata hata mtu wa
kuongozana nao. Kesho yake tena walikwenda hivyo
hivyo, lakini bado hawakupata mtu aliyeweza
kuyafuata mafundisho yao.
Walifanya hivyo wiki, bado hawakuweza kupata hata
mtu mmoja katika watu wa kijiji hicho. Zaid walizidi
kukimbiwa na hata watoto.
Kazi hayo haikuweza kuleta matumaini. Ikiwa ndio
siku ya tatu katika siku ya tatu ya juma chakula
kiliwaishia, sister murcia akamuomba Moris na
Chaka/paulo waongozane kwenda mjini kufuata
chakula.
Kijijini Murcia alibaki na vijana wake watatu. Alicia,
Mercia na Lucas.
Wakiwa inje ya kanisa wakifanya shughuri ya usafi
mida ya saa 4 za asubuhi. Ghafra upepo mkari
ulitokea giza nene likatanda kila mahara katika kijiji
hicho, upepo ulikuwa mkari, vumbi likatibuka
sehemu hio ya kanisa, hakuna aliyeweza kumuona
mwenzake. Ilikuwa ni jambo la kushitukiza kwao.
 
NO.(09).
ALICIA APOTEA NA KUCHUKULIWA NA KIKOSI CHA
SHETANI, SISTER MURCIA ASHINDWA KULA,
AOGOPA KUINGIA NDANI YA SAKARASTIA. PAULO
NA MORIS WATEKWA NA KUNDI LA WACHAWI.
ILIPOISHIA
Wakiwa inje ya kanisa wakifanya shughuri ya usafi
mida ya saa 4 za asubuhi. Ghafra upepo mkari
ulitokea giza nene likatanda kila mahara katika kijiji
hicho, upepo ulikuwa mkari, vumbi likatibuka
sehemu hio ya kanisa, hakuna aliyeweza kumuona
mwenzake. Ilikuwa ni jambo la kushitukiza kwao.
SONGA NAYO.
Upepo huo ulichukua muda kama robo saa ndio
ukatulia, ulikuwa ni upepo ambao kila mmoja
akuutegemea kabisa. Baada ya upepo huo kutulia
Sister Murcia alikuwa kabaki peke yake eneo hilo la
kanisa, hapo aliisi kuchanganyikiwa akaanza kuita
majina ya Wanafunzi wake watatu, Lucas, Mercia na
Alicia. Lakini hakuna aliyeitika. Sister Murcia
alichoka na kuchoka.
"He baba najua hata manabii wako walipata
misukosuko kama hii basi nilinde juu ya ili janga
zito!"
Murcia alisema akiwa ameunua macho yake juu.
Baada ya kusema hivyo akili zake zilimtuma
azunguke nyuma ya kanisa, bila kuchelewa naye
alifanya hivyo. Baada ya kufika nyuma ya kanisa
Sister Murcia alisitaajabu baada ya kuwakuta Mercia
na Lucas kila mmoja ameanguka upande wake.
Bado Murcia aliizidi kuangaza kama angemuona
Alicia lakini hakuweza kumuona. Ndipo sister
Murcia alipo waamsha wanafunzi wake wawili yaani
mercia na Lucas ambao aliwakuta nyuma ya kanisa,
Wote wawaili hakutumia nguvu kubwa kuwaamsha ,
aliwagusa tu mala moja nao wakaamka. Baada ya
kuwaamsha wanafunzi hao wawili, Murcia
aliwaomba wasaidizane kumtafuta Alicia wote kwa
pamoja. Walitafuta maeneo hayo ya kanisa nyuma
na mbele hawakuweza kumuona, waliamua wasogee
mbele tena ya hapo, napo pia hawakuweza
kumuona. Walitafuta sana bila mafanikio, walisogea
mpaka katika nyumba za wanakijiji hicho, ambazo
zilikuwa umbali kama umbali wa viwanja vitatu vya
michezo kutoka lilipokanisa. Huko ndiko kulikuwa
kama wanajisumbua, hakuna mtu hata mmoja
aliyekuwa anazungumza nao wengine walikuwa
wanawakimbia, wengine walikuwa wanawasotea
vidore na kuwaponda wasijaribu kuzisogelea
nyumba zao Karibu.
Wakiwa wametafuta bila mafanikio kabisa, Murcia
alichoka akashindwa afanye nini, kuomba allijaribu
mala nyingi eiza mwenyezi mungu amsaidie
kumuona mwanafunzi wake, maombi yake yalikuwa
kama hayapokelewi.
Siku hio mchana ilipita tu, hata kula walishindwa
kwasababu ya kumkosa mwenzao.
*******.
Ni mida ya saa moja za jioni tu, katika nyumba
kubwa ndani ya kijiji hicho cha Shimo la moto,
jumba hilo lilionekana linaukumbi mkubwa na lipo
katikati ya pori, kulikuwa na kundi kubwa la watu
wamekusanyika, mmoja akiwa amekaa kwenye kiti
kikubwa kama mfalme, mtu huyo alionekana ndiye
mkubwa na kongozi wa wengine wote. Watu
wengine walikuwa wakiinama na kuinuka. Kwa
maana walikuwa wanasujudu na kuinuka mbele ya
Mtu huyo. Ndani ya jumba la mtu huyo kulikuwa na
misalaba kama ya kanisani.
"Ha ha ha ha. Tumefanikiwa Ha ha ha ha!"
Mtu aliyekaa kwenye kiti alicheka kwanguvu na
kutamka neno hilo moja tu.
"Sasa namuomba mtu mmoja mwnamke mwenye
ujasiri ajitokeze hapa tumpe kazi!"
Mkuu yule wa kundi hilo la wachawi alisema. Baada
ya kusema hivyo tu, alijitokeza Bibi mmoja.
"Mkuu ni mimi Nyamumwi, nimetumwa na mkuu
wangu nije nikusaidie kazi hii"
Baada ya bibi yule kusama hivyo, Yule mkuu wa
wachawi alicheka sana akasema. Hii ndio faida yetu
sisi wachawi tukishindwa jambo huwa
tunashirikiana, tukimaliza ndio tunarudi pale pale"
"Kweli mkuu!
Bibi yule alisema. Hawa wachawi wa upande huu
walikuwa wamevaa nguo nyeusi tupu ispokuwa
mkubwa wao alikuwa amevalia nguo jekundu likiwa
na misaraba.
Baada ya Bibi yule kujitokeza, yule mkubwa wa
wachawi alinyoosha fimbo aliyokuwa kaishikilia
mkononi mwake kwenye kitambaa cheupe
kilichokuwa mbele yao. Mala moja ikatokea video
kwenye kitambaa hicho; video hio ilimuonesha
Sister Murcia akiwa anafanya maombi, mkuu yule
wa wachawi alicheke sana, kisha akasema.
"We ni mwanamke tu, uwezi kuwa na mamlaka
makubwa ya kutushinda sisi, kwani uliona wapi
mungu akamleta nabii mwanamke katika Dunia hii,
Hata mariam Mwanamke aliyekuwa Mwema kuliko
wote yeye hakupewa upeo wa kuwaongoza na
kuwafundisha watu habari za mungu wangeanzia
wapi kumwelewa, zaidi wangemponda mawe na
kumuua. Mimi ndio Joseph padre mkubwa
makanisani huko wananijua Ha ha ha ha ha!"
Mkuu yule alisema na kumalizia kwa kucheka.
"Je mkuu wataka tumfanye nini mtu huyu?"
Mmoja wa watu katika wachawi wale alisema.
"Muda wake wa kuishi umefikia tamati.
" mkuu yule si ndiye miongoni mwa watu
wakuogopwa na wanamamlaka makubwa mbele za
bwana mungu?"
Mtu yule tena aliuliza, mtu huyo alionekana ni
msomi kabisa kimawazo.
"Ha ha ha ha ha ha! Huyo hana mamlaka makubwa
na msaada mbele za mungu kwa sasa, kwani yupo
katika wakati mmbaya, malaika wadumisha ulinzi
wa bwana hawawezi kumsogelea kwani wao si
wakumsogelea aliye mchafu, na ndio maana
mwanamke ajapewa mamlaka ya kuwaongoza watu
katika maswala ya kiimani labda kwa dharula sana"
Baada ya kusema vile mtu yule aliyejiita Joseph
ambaye ni padre aliita "Nyambi!"
"Nipo mbele zako wewe upaswaye kuwabudiwa!"
Nyambi, kijana mmoja wa kiume alijitokeza.
"Niletee kafara ya Rusifa"
Bila kuchelewa nyamba alitoka na kuingia chumba
cha pembeni akamtoa Alicia akiwa hoi kabisa
ajitambui, Nyambi alikuwa amembeba mikononi
mwake.
"Mlaze mbele ya mazabahu ya kuitoleya kafara kuu
ya mkuu katika wakuu wa Ulemwengu"
Mkuu wao alisema.
Baada ya mkuu yule kumaliza vile akasema. Huwa
tunatoa kafara moja ya mwanamke Bikra kwa
mwaka, mwaka huu tayari kafara tumeisha ipata"
Kila mtu alipiga makelele kushangilia alichokisema
mkuu wao.
"Sasa mkuu mimi nitafanya nini?"
Yule Bibi Nyamumwi aliuliza.
"Wewe nataka ujigeuze uwe kama huyu bint, kesho
asubuhi na mapema kabla hawajaamka ufike pale
kanisani wakukute umelala ndani ya kanisa. Taarifa
ya jinsi gani tutafanya kuusu kumkamata na
kummaliza huyo Murcia tutakuwa tunawasilina"
Kama vile ilikuwa umeme baada ya padre joseph
kusema vile, yule Bibi Nyamumwi Bibi aliyekuwa
emtoka upande wa magharibi kuongeza nguvu
katika upande wa Mashariki, alijigeuza na kufanana
kama Alicia.
Kitendo hicho kila mmoja alikipongeza na
kumshangilia.
Wakiwa wanamshangilia mala aliingia kijana mmoja
wa kiume.
"Mkuu wale watu, wawili waliokuwa wameenda
mjini tayari washakaribia kufika katika makutano ya
njia mbili"
Baada ya kijana yule kusema. Padre joseph
alimwambia watoke vijana kumi wenye nguvu
waende wakawakamate.
Baada ya Agizo hilo hakukuwa na kuchelewa vijana
wale walijikusanya kisha wakachukua Misumari
mikubwa kabisa kama nondo iliyokuwa
imechongwa vizuri na kuondoka nayo.
********
Ikiwa ndio inatimu mida ya saa mbili kama na robo
Paulo na Moris wakiwa ndani ya Gari la kanisa
kutoka mjini, ndani ya gari kukiwa kumesheheni
vyakula na mafuta ya kupikia pamoja na mitungi
mitatu ya Gas walifika eneo la njia panda sehemu
ambayo ilikuwa na kona na sehemu hiyo ndio
ilikuwa inapendwa na wachawi kufanyia madawa na
wengine kutolea kafara yao, na ndio sehemu
ambayo kikundi kilichoagizwa na joseph kilikuwa
kwa ajili ya kufanya yao.
Wakiwa hawana hili wala lile vijana wale wawili
kwenye gari walishsitukia tu tairi ya mbele imelia
Pa! Hicho kilikuwa kiashilia tosha kuwa tyre ya
mbele ya Gari imepasuka. Kila mmoja ndani ya Gari
alishituka, tayari walianza kujitayarisha kwa
mapambano, eneo hilo hakuna ambaye alikuwa
halijui kati ya wale wawili. Chaka au paulo yeye
alikuwa anajua kabisa hapo ilikuwa ni sehemu ya
wachawi kuchezea na kufanyia madawa yao, kwani
hap kabla hata yeye alikuwa ni miongoni mwao.
Moris anapakimbuka kwasababu siku ya kwanza
kuja kwenye kijiji hicho cha zima moto ni hapo
hapo Gari ilikwama akatokea kiumbe wa ajabu.
Wakiwa bado vijana wale wanajiuliza mala kikosi
kilichokuwa kimeagizwa na kikundi cha padre
joseph kilijitokeza kutoka mafichoni. Chaka kwa
ujasiri tena kwa kumtumainia Bwana na imani
Thabiti alitoka ndani ya Gari na panga aina ya
jambia alikuwa kalichukua mjini kwa ajili ya ulinzi
kwa wenzake pale kanisani, alishuka ndani ya Gari
kupambana nao. Hata Moris naye alipoona hivyo
naye akachukua lake kama kijana wa kiume kwa
ujasiri akaungana na mwenzake kupambana na jeshi
la Shetani. Ilikuwa ni vita ya kifo timu ya vijana
wawili wamtumikiawo bwana na timu ya watu kumi
imtumikiayo shetani. Kabla awajalianzisha
chaka/,paulo alisema.
"Eee! Bwana Nipe nguvu na ujasili wa kuliangusha
ili kundi la watu waovu, wamtumikiawo shetani bila
kujua?" Usiku huo huo na mwanga wa mbala mwezi
mapanga yalianza kulia, kweli Paulo alikuwa ni
jasiri. aliweza kupigana na vijana wale na
kuwajeruhi vibaya pale pale wote, kundi zima la
shetani likakimbia na kutoweka. Ingawa Paulo naye
alipatwa na majeraha kidogo lakini yeye Alilishinda
kundi la shetani. kipindi hicho Moris yeye alikuwa
kajificha chini ya uvungu wa Gari baada ya kuona
vita ile sio ya mchezo.
Kazi ilibaki ni kutoka hapo, uwezekano haukuwepo
tena, ingawa tairi walikuwa nayo lakini Moris
aliogopa kutoka inje ya Gari kwa hofu ya watu wale
kurudi, Paulo alimng'ang'aniza na kumuomba ili
aweze kutoa na kubadili tairi ya gari kwa kusadizana
wawili, Moris aliogopa kabisa na kugoma. Ni muda
huo huo Kilitokea kikosi kingine hicho kikiongozwa
na Mwenywe padre Joseph pamoja na kiongozi wa
upande wa Nagharibi pale pale kwenye gari.
Hawakuweza kujua jinsi padri Joseph alivyoingia
ndani ya Gari na kuwatoa kisha kufungwa kamba na
kuondokana nao wakaliacha gari hapo hapo.
Waliongozana nao huku wakipigwa mijeredi mpaka
katika jumba au kanisa la Shetani alikokuwa kaweka
kambi yake Padre joseph.
Huko walifika, wakaoneshwa kila ambacho tayari
washakifanyakwa Waliokuwa wamebaki katika
kanisa la bwana, waliwaonesha Sister Murcia akiwa
hoi kabisa kalala kanisani usiku huo hakiwa hana
matumaini. Wachawi hawo hawakuishia hapo
walimuonesha Alicia jins alivyokuwa anataka
kutolewa kafara.
"Bado siku tatu tatamtoa kafara"
Padre joseph aliwambia Paulo na Moris.
"Baada ya yeye nyinyi Mtakaa hapa mteseke na njaa
halafu siku ya Tano tutawafanya kama ambavyo
wanaume huwa tunawafanya"
Padre joseph alisema tena. Paulo na Moris wakiwa
wamepigishwa magoti mbele ya Wachawi wote.
Kipindi hicho wachawi wale walikuwa wakicheka
sana.
"Mkuu mimi huyu ungenipa tu, nimtafune mzima
mzima yeye kajifanya kumfuata huyo sijui bwana;
mbona hatuuoni msaada wake huyo bwana!"
Nyamumwi alisema akiwa anamshika shika chaka
mabegani.
Baada ya hapo walitolewa na kuwekwa katika
chumba kilichokuwa na harufu kali kama za uvundo
wa vitu vilivyokufa. Huwezi kuamini kumbe wachawi
huwa hawatumii uchawi tu, hata njia za kawaida za
kumdhoofisha mtu huwa wanatumia wakiona
wameshindwa kwa uchawi. Kama alivyo ongea
Murcia wa kwanza kumwambia sister Murcia kuwa,
ndani ya kijiji hicho kuna wasomi wakubwa
wanaokitumia kijiji hicho kwa manufaa yao, ndivyo
hivyo hivyo. Wachawi wale waliwachoma Paulo na
Moris Sindano za kupunguza nguvu na kuwafanya
walegee kabisa na kukosa nguvu.
 
NO. (10).
ALICIA WA KICHAWI AFIKA AONEKANA MWENYE
KUFUNGAMANA NA BWANA. AJA TENA BINT
MWINGINE WA KICHAWI KWA AJILI YA
KUMMALIZA SISTER MURCIA. NAYE AMPOKEA
BILA KUJUA.
ILIPOISHIA.
ndani ya kijiji hicho kuna wasomi wakubwa
wanaokitumia kijiji hicho kwa manufaa yao, ndivyo
hivyo hivyo. Wachawi wale waliwachoma Paulo na
Moris Sindano za kupunguza nguvu na kuwafanya
walegee kabisa na kukosa nguvu.
SONGA NAYO.
Muda huo huo walilala usingizi mzito kabisa na
kusahau kila kitu kilichoendelea duniani. Usiku huo
ulikuwa ni shangwe na vigerere kwa wachawi
wakisheherekea sikukuu ya kuipata kafara kuu kwa
ajili ya Rusifa.
********
Siku iliyofuata asubuhi na mapema kabisa sister
murcia akiwa na mawazo ya kupotelewa na
Mwanafunzi wake, tena bado hana taarifa kuusu
akina Moris na Paulo ambao walienda mjini toka
asubuhi na mapema ya siku iliyopita na aliwatarajia
wafike siku hio hio ya jana lakini hawakufika. hivyo
vyote vilimpa mawazo sana Sister murcia, Sister
ambaye alikuwa na upako mkubwa kutoka kwa
bwana, lakini kipindi hicho alikuwa kwenye wakati
mgumu sana. Hata maombi yake kwa bwana
yalikuwa kama hayapokelewi katika uzito wake.
Hivyo hivyo na mawazo yake, alitoka ndani
akachukua maji kwenda kuoga kuondoa uchafu
mwilini mwake. Baada ya kumaliza kuoga alijifunga
na kuvaa nguo zake, kisha akaelekea kanisani
kufanya maombi.
Ilikuwa ni mapema sana, kama mida ya saa kumi
na moja za asubuhi. Sister murcia aliushika mlango
wa kanisa ambao ulikuwa hujafungwa bali
Umeegeshwa na kuufungua, cha kwanza kuingia
ndani ya kanisa ulikuwa ni mguu wake wa kulia kwa
maombi maalum aliyo yatanguliza, kisha uso wake
ukafuata. Sister murcia akuamini kabisa alipomuona
Alicia fake kapiga magoti mbele ya sanamu ya
Bikra maria akiomba. Sister Murcia akiamini kabisa
kuwa aliyeko mbele yake ni Alicia aliyemzoea
aliinua mikono yake juu kwanza akamshukuru
Bwana mungu kwa shukurani kubwa. Baada ya
kumshukuru bwana mungu aliye hai, Murcia aliita
Alicia, Bila hata uwoga Alicia fake, alicia wa kichawi
au Nyamumwi aliyejigeuza na kuwa Alicia aliitika na
kusema.
"Bwana mungu awe nasi Daima milele, hakika
nimeokoka kutoka katika jeshi la Shetani kwa
msaada wa bwana. Mungu anapaswa ashukuliwe
kwa ukubwa milele amina"
Alicia fake akionekana kabisa kuwa ni mwenye
imani kubwa na Mungu aliye hai, mungu wa kweli,
mungu mwenye mamlaka na kila kilichomo ardhini,
alisema maneno mazuuri yaliyopokelewa kwa
"EMEE" kubwa kutoka kwa Sister Murcia.
"Alicia ni wewe kweli?"
"Sister mulcia aliuliza kwa shauku ya kujua.
"Ndiyo mimi sister Murcia, kwani uamini kuwa
bwana mungu ameniokoa kutoka katika mikono
mibaya ya Shetani?"
Alicia fake isema huku akitabasamu.
"Hapana! Nikwasababu jana....!Tukio la jana
liliniweka kwenye wakati mgumu sana. Sijalala
usiku kucha nikikuwaza!"
Sister Murcia alisema.
"Kwani sister? we hukufanya maombi kwa ajili
yangu?"
Alicia aliuliza.
"Nilifanya lakini maombi yangu asaiv yana...........!"
Sister murcia akutaka kuimalizia Kauli yake.
"Yana nini sister?"
Alicia fake, Alicia wa kichawi au nyamumwi aliuliza
kwa lengo la kuthibitisha kuwa alichokuwa
anakisem padre joseph kuusu sister Murcia ni cha
kweli.
"Hapana! Naomba unambie ni nini ambacho
kilikukuta huko?"
Badala ya kujibu Murcia naye aliuliza na kubadili
mada pale pale.
"Baada ya kupotea katika kile kimbunga cha jana,
nilijikuta niko kwenye pori kubwa, huko palikuwa
panatisha sana, nilianza kuogopa nilipofika huko,
nilikuwa peke yangu tu. Baada ya muda kama
dakika tano niliisi kama sauti ya Shetani ikiniita.
Pale pale namimi nikapiga magoti na kuanza
kuomba halafu nikiliita jina la yesu, yesu! yesu!
huku nimefumba macho, sikujua nilipotea vipi
maeneo yale nikajikuta niko humu kanisani"
Alicia wa kichawi alisema kwa kujiamini kabisa.
"Mh! Pole sana. Mimi huwa nawambia mnapaswa
muwe na imani kama hio. mungu ni wa ajabu
anamuokoa na kumlinda kila mwenye kumtumainia"
Sister Murcia alisema. Mbele ya shetani mkubwa,
mchawi aliyebobea katika fani ya kuwanga na
kuwaloga watu, Aliyejulikana kwa jina la Nyamumwi.
Moyoni mchawi yule alikuwa akimcheka na
kumzomea Murcia huku akijisemea.
"Subiri uje uone na ujue ni nini maana ya kijiji cha
shimo la moto, lazima ufe iwe isiwe lazima ufe"
Akiwa kaisha gundua kabisa kuwa alichokisema
padre joseph kuusu sister murcia ni cha kweli, ya
kwamba kuwa Maombi yake hayapokelewi
ipaswavyo mbele ya Bwana kutokana na kuwa
katika hali mbaya, hali chafu, hali ambayo kila
mwanamke huwa inamkuta. Nyamumwi kwa ulimi
wake alimwambia sister Murcia.
"Sister naomba tuwafanyie maombi Akina Paulo na
Moris ili mungu awape wepesi wa kurudi haraka, au
kama kuna tatizo limewakuta, basi wapate
kuokolewa"
Sister Murcia akuamini kabisa alichokisiakia kutoka
kwa mwanafunzi wake ambaye alikuwa na imani
haba kuweza kusema maneno ya kuwaombea watu
walioko mjini.
"Alicia naona umebadilika unapenda kusali na
kumuomba mungu ipasavyo sasa. Basi naomba
wewe ndiye uwe muombaji mkuu wa maombi haya
kwakuwa wewe u msafi"
Sister murcia alizidi kujiweka wazi kwa mchawi yule
nyamumwi. Bibi mchawi kabisa aliyekuwa kajigeuza
na kuichukua sura ya Alicia na wakati kipindi hicho
Alicia alikuwa mikononi mwa jeshi la shetani akiwa
ajitambui kabisa.
Maombi yasiyokuwa na faida kutoka kwa watu
wawili sister Murcia na mchawi yalianza ndani ya
kanisa. Ndicho kipindi hicho hicho Mercia naye
alifika na kuendelea na maombi hakutaka
kuwasumbuwa wenzake ijapo kuwa alishikwa na
butwaa alipomkuta Alicia yumo kanisani akiomba
na Sister Murcia. Bado wakiwa wanaendelea
kuomba Lucas naye alifika na kuunganisha nao
katika kuomba.
Maombi yaliwachukua kama lisaa limoja kisha
wakamaliza. Baada ya kumaliza Mercia na Lucas
nao walimuuliza Alicia kuusu alipokuwa. Alicia huyo
mchawi kabisa bila hata aibu naye aliwasimulia
habari za uongo wake nao pia wakawa wenye
kuamini.
Kweli wasemavyo waswahili kuwa kumjua mchawi
huwa ni vigumu wakati wa mchana hata usiku labda
akutokee akiwa katika hali yake ya kishirikina, na
hata wale wasemao kuwa hata mchawi umtegemea
mungu ili afanikishe maswala yake basi huwenda ni
kweli. Mchawi yule aliyekuwa kajibadilisha kafanana
kabisa kila kitu na Alicia alifanya kazi kwa bidii
sana, tena yeye ndiye aliyebadilika na kuwa
muamasishaji wa wenzake kusali kuisoma Biblia
takatifu. Mpenzi msomaji zingatia kabisa kuwa
yaliyomo ndani ya Biblia au kwenye Kitabu chochote
cha Mungu hayana msaada kwako usipokuwa na
imani nayo, hata ufanyaje hayawezi kukusaidia.
Shetani anayatumia akiwa na Tahadhari kubwa
akijua kabisa akienda nayo ovyo yatamwangamiza
na kumuua lakini Sisi binadamu wenye imani haba
ndio tunayachukulia kawida.
Mchawi yule Nyamumwi aliweza kuwaingia akilini
wote ndani ya siku moja tu, kila mmoja pale
akaamini kabisa kweli Alicia kabadilika kawa mtu
wa kumtumikia bwana na mwenye imani kubwa.
Kumbe walikuwa wanamuwazia kiumbe ambaye
amekuja kuwangamiza na akuwa Alicia waliyekuwa
wakimzani.
********
Masaa yalizidi kwenda, hatimaye ikatimu mida ya
saa kumi jioni, hazikuonekana hata dalili za kufika
kwa Moris na Paulo kurudi kutoka mjini sister
murcia na wanafunzi wake hapo ndipo walizidi
kuchanganikiwa kabisa.
"Oooh! Mungu wangu hawa wanekamatwa na
kikundi cha wachawi, mbona hawarudi?"
Sister Murcia alijisemea huku wasiwasi ukiwa
umemtanda, alishindwa kuvumilia machozi
yakamdondoka kabisa. kuingia ndani ya Sakarasitia
kuomba kwake ilikuwa ngumu.
"Jamani msiwe na hofu, mungu atawalinda na
kuwaokoa, si tunamtegemea mungu kwa kila jambo
kwanini tusimwamini mungu wetu"
Alicia mchawi alisema.
Bibi huyo wa kichawi aliyekuwa kajigeuza kwa sura
ya Alicia alizungumza upuuzi tena kwa kuweka
kejeli za ajabu kabisa. Maneno hayo yalimkasirisha
kila mmoja pale na kumkemea.
"Sister naomba mnisamehe sitarudia kusema hivyo
tena"
Baada ya kusena hivyo mchawi yule alijifanya kuzira
na kukaa pembeni kuona wenzake watasema nini.
Lakini napo pia hawakumjali mawazo ya Sister
Murcia yaliishia kwa Paulo na Moris.
"Chakula kimetuishia hata usiku hakitoshi, sijui
tutaishi vipi hapa, mungu wangu Eee! kipokee kilio
chetu tunateseka waja wako"
Sister Murcia alisema.
Maneno yake yakisikika moja kwa moja masikioni
mwa mchawi Alicia. Kumbe kipindi hicho naye
alikuwa anapokea taarifa kutoka kwa mkuu wake
taarifa ambazo zilikuwa zinasikika moja kwa moja
masikioni mwake kupitia cheni aliyokuwa ameivaa
shingoni.
Alipomaliza kuzisikiliza taarifa kutoka kwa mkuu
wake, mchawi yule ambaye pia maneno ya murcia
aliyasikia vizuri alisema.
"Naomba mwalimu wangu, naomba leo tukajaribu
kwenda kukitembelea kijiji hiki, mi ninaamini kabisa
watu watatusaidia hata chakula cha kula usiku huu
Halafu kesho tuaweza kutafuta namna nyingine au
huwenda kesho paulo na Moris watarudi"
Mchawi yule aliutoa ushauri mzuuri ambao tayari
yeye alikuwa anajua ni nini madhara yake.
"Hapana Alicia aiwezekani kabisa hiki kijiji mimi
nakijua watu wa hapa si binadamu ni watoto wa
shetani kabisa hawaoni wala awaelewi"
Sister murcia alisema.
"Murcia mimi nipo nitajitoa sadaka kwa hawa
ndugu zangu, naomba wao wabaki tuongozane na
wewe, au kama hata wewe hutaki ngoja mimi
niende pekee, nina hakika ninaweza kuja na chakula
kutoka kwa watu hao"
Wakiwa bado wanazungumza alikuja bint mmoja
mzuri kavalia nguo nzuri kabisa. Bint yule kila
mmoja pale alimshangaa, alikuwa ni bint wa aina
yake. kwa mazingira ya kijiji kile akuna ambaye
alikuwa anauwezo wa kumfikia hata kimvuto kwa
jinsi alivyokuwa akionekana.
Bint yule kumbe naye alikuwa shetani, kambi moja
na Alicia fake aliyetumwa na padre joseph aje
kusaidizana na Nyamumwi kummaliza sister
murcia.
Baada ya kufika bint yule alijitambulisha kwa jina la
Josephina, alisema kuwa yeye ni mwenyeji wa kijiji
hicho cha zima moto lakini siku ni nyingi toka
aondoke karibu miaka mitatu, alikua kaja kumuona
mama yake, lakini alipofika akaambiwa kuwa siku
nyingi mama yake kaisha fariki na alipokuwa
anaishi kiwanja washauza na hakuna tena ndugu wa
kwenda kumfikia kwahio aliomba alale hapo
kanisani kwa siku moja tu ili kesho yake aamke
akawatafute ndugu zake.
Maelezo ya bint huyo yalimuingia kila mmoja, lakini
bado wote walikuwa na wasiwasi huwenda jeshi la
shetani limewavaa.
"Wewe! watu wa hapa wote, huwa hawaji katika
kanisa hili, wote wanalichukia kanisa la bwana, Au
umetumwa?"
Aliyekuwa wa kwanza kuuliza alikuwa Alicia mchawi,
yote hayo kutaka kuyatengeneza mazingira ya
kumkaribisha mchawi mwenzake.
"Jamani kweli ndio hivyo basi ngoja nikalale
kichakani tu!"
"Sisi hatujakataa kukusaidia lakini kwanini
usiwambie hao wanakijiji wakakusaidia?"
Mercia aliuliza.
"Mimi ni mtoto wa kike, mazingira ya watu wa hapa
kijijini sijayazoea kwanza nilikuwa nimemuijia mama
yangu kesho tu nianze safari ya kurudi naye mjini"
Bint yule alisema kwa unyenyekevu kabisa, kipindi
hicho sister murcia yeye alikuwa akiwaza mbali,
mawazo yakawa yanajirudia kichwani mwake kuusu
alivyoambiwa na Murcia wa kwanza kuusu
kikombolewa kwa kijiji hicho cha shimo la moto.
"Sister murcia ebu sema kuusu mtu huyu?"
Lucas alisema.
Maneno ya Lucas ndio yalimrudisha sister Murcia
katika hali ya kawaida.
Apite akaye bwana katufungulia njia"
Maneno ya sister murcia ndiyo yalikuwa kama
ruhusa wa kuingia ndani ya kanisa kwa bint yule.
Bint yule mchawi aliingia ndani ya kanisa huku
kashikili begi yake ya kisasa yaliyoshonwa mfumo
wa kigunia halafu begani kauvaa mkoba wa kung'aa
kabisa aliyafurahia mapokezi ya kuingia ndani ya
kanisa.
 
NO. (11).
ILIPOISHIA.
Bint yule mchawi aliingia ndani ya kanisa huku
kashikili begi yake ya kisasa yaliyoshonwa mfumo
wa kigunia halafu begani kauvaa mkoba wa kung'aa
kabisa, aliyafurahia mapokezi ya kuingia ndani ya
kanisa.
SONGA NAYO.
Ilikuwa ni furaha moyoni mwa Bint yule mchawi na
Alicia wa kichawi. Walikaa wakaongea kwa pamoja,
wakisimuliana matukio ya kijiji hicho na
kufundishana mafundisho ya Mungu, jioni hio kwao
ilikuwa yenye furaha kwa watu wawili Alicia na bint
Josephina. Kwa sister Murcia ilikuwa ni majonzi
moyoni, mawazo yake yaliishia kwa Moris na paulo.
Mazingira ya mawasiliano kwa kijiji hicho
hayakuwepo kabisa labda angefanya utaratibu wa
mawasiliano. Muda wote alikuwa anawaza.
*********
Usiku mida ya saa moja walitaka kuandaa chakula
lakini hawakuwa nacho cha kutosha, walifikiri
watafanya nini, hata basi wangemuomba bwana
labda angefanya muujiza wake hawasaidie lakini
haikuwezekena au hata wavumilie mpaka kesho
waone kitatokea nini, hilo tu ndilo lilikuwa wazo lao.
"Sister Murcia mimi nina mikate mitatu hii tunaweza
kula kwa pamoja tukashiba usiku huu"
Bint yule wa kichawi alisema baada ya kuona kuwa
watu wale wanauliza kuusu chakula. Baada ya
Murcia kusikia yule bint anamikate akawambia
waitenge wale wao wote lakini yeye hakuwa na
hamu ya chakula. Kukataa kwa sister Murcia
kulikuwa ni pigo kwa wachawi wale, wao walitaka
Sister Murcia ale chakula chao kilichokuwa na sumu
ya kuwafanya wote wapatwe na gonjwa la kuzimia
halafu wajue namna ya kuwabeba kutoka eneo lile la
Kanisa mpaka kwao uchawini.
Baada ya sister murcia kugoma wachawi wale
walijitahidi kumshawishi aweze hata kula kidogo.
"Sister Tafadhali jua kesho ni mbali na uwezekano
wa watu wale kufika haupo kwasababu hatuna
taarifa nao!"
Alicia wa kichawi au Nyamumwi kama alivyokuwa
anaitwa uchawini kwao alisema.
"Hapana Alicia hata ningalifanya nini! Hamu na kula
kwangu haipo kabisa kabisa haipo!"
Sister murcia alisema.
Baada ya kuona kuwa Sister Murcia kagoma kula
wachawi wale waliamua kuwapa mkate uliokuwa na
madawa yao ya kichawi Mercia na Lucas wao
wakabaki na mkate mmoja ambao ulikuwa hauna
kitu ndani yake na mmoja wakasema wautunze
wakidai kesho Sister Murcia anaweza kuamka akiwa
na njaa akala, lakini moyoni walikuwa na jipya
badala ya kutumia mkate waliamua waplani njia
nyingine ya kumukamata sister Murcia.
Sister Murcia aliwaacha watu wale wanakula
chakula/mikate yao yeye akaenda kuoga kwa ajili ya
maombi ya usiku.
Hio ndio ilionekana nafasi nzuri na muwafaka kwa
wachawi kumfanyia kile walichotaka kukifanya kwa
sister murcia. Lucas na Mercia walikula mkate kwa
dakika Tano tu wote wakaanza kulewa kisha
wakasisinzia hoi kabisa usingizi mzito hawakujua
nini tena kilipaswa kuendelea Duniani. Baada ya
kuona kuwa huku kanisani wamewaacha Mercia na
Lucas wamezimia, wao moja kwa moja wakaelekea
chumbani kwa Sister Murcia wakimngoja atoke
bafuni wamfanyie kile walichokuwa wamepanga
kumfanyia.
Haikuchukua muda dakika mbili tu toka waingie
Sister murcia aliingia ndani kutoka bafuni kuoga.
Kitandani alimkuta Alicia wa kichawi au Nyamumwi
amekaa, kipindi hicho Josephina alikuwa kajificha
nyuma ya mlango. Sister murcia alimwangalia Alicia
na kumuomba ampishe avae, Alicia yule wa kichawi
alisiamama, kumbe mkononi alikuwa kakumbatia
madawa ya kichawi yakiwa ya unga. Sister Murcia
hakiwa hana hili wala lile alishitukia anapuliziwa
unga ule usoni, ukamtapakaa uso mzima, mwingine
ukamwingia machoni akashindwa kuona, mwingine
ukamwingia puani na hata mdomoni, haikupita hata
dakika mbili sister Murcia alianza kulewa akaanza
kuona kizunguzungu, akawa aoni vizuri kabisa.
Mambo yalimuwia magumu Sister nguvu zikawa
zinamuishia mwilini huku anayakumbuka maneno ya
Murcia wa kwanza jinsi yeye alivyotaka kuuliwa
bahati mbaya akaponea chupu chupu kwa nguvu za
Mungu. Muda huo huo Murcia alianguka chini
puuuu! wachawi wale wawili walicheka na kufurahi
kwa mafanikio yao ya kuweza kumkamata Sister
murcia na kumuweka katika Imaya yao. Baada ya
kumaliza zoezi lao wachawi wale Nyamumwi
aliyekuwa kajigeuza umbo la Alicia na Josephina
Bint ambaye alikuwa kaja kumsaidia Nyamumwi
waliwasiliana na Kikosi chao kikuu kuwapa taarifa
kuwa wamekamilisha kazi yao. Haikuchukua muda
kikatokea kikundi cha vijana watatu wa kiume
pamoja na Padre joseph mwenywe, walipofika wote
kwa pamoja walipotea na mwili wa sisiter Murcia
pekee na kuwaacha Lucas na Mercia ndani ya
kanisa hawajielewi kabisa.
*******
Ikiwa ndio siku ya kwanza toka kupigwa dawa ya
kupoteza fahamu na kundi la wachawi, Usiku huo
mida ya saa nne na nusu uwezi amini kwa uwezo
wa mungu paulo alijikuta anapata nguvu na kuamka
kutoka katika kupoteza fahamu na kuamka, baada
ya yeye kuamka katika janga hilo huku hakiwa na
njaa kabisa alijaribu kumwamsha Moris ili naye
aamke wapate kuondoka eneo hilo hata kwa
kutoroka tu, lakini kila alivyokuwa anaangaika
kumwamsha Moris hakuweza kuamka, ilikuwa kama
kusujisumbua tu, baada ya kuona mwenzake aamki
Paulo akajua moja kwa moja kuwa kaisha kufa.
Kilichofuata yeye mwenyewe alianza kutafuta namna
ya kutoka ndani ya jumba lile la kichawi. Bahati
nzuri chumba hicho kilikuwa hakina mlango lakini
kila alipokuwa akijaribu kutoka ikawa kama vile
anazunguka mule mule ndani ya chumba hicho.
"Eee mungu, niondoe na unilinde katika jumba hili
la shetani"
Maneno hayo tu yalitosha kumfungulia Paulo mlango
wa shetani na kutoka mdani ya chumba cha Shetani,
aliweza kutoka kirahisi sana ndani ya jumba lile
kama vile alikuwa aonekani, aliweza kutoka pale
kwenye jumba lile la wachawi na kutembea,
hakukua na dalili kabisa za kufukuzwa wala
kufuatiliwa na Wachawi. Paulo alikuwa akitembea
kwa kulitaja jina la Bwana ndani moyoni mwake,
njia nzima alikuwa akimuomba mungu amuongoze
afike haraka sana kanisani. Muujiza wa mungu
ulifanyika kwake, akalifikia kanisa. Alipofika kanisani
cha kwanza alikisogelea chumba alichokuwa analala
sister murcia na wanafunzi wa kike na kukigonga
chumba hicho. Paulo alijitahidi sana kuugonga huku
akiita majina ya watu wote lakini haikusikika hata
sauti ya mtu kuitika, baada ya kuona kimya
aligundua kuwa hakuna mtu ndani ya chumba hicho
japo kuwa taa ilikuwa inawaka, Paulo aliamua aende
kanisani. Alipofika kanisani alisitushwa na
alichokikuta ndani ya Kanisa, aliwakuta Mercia na
Lucas wamelala fo fo fo hawajitambui kabisa.
Alichokifanya nikuwamsha huku akiwafanyia
maombi lakini ilishindikana kuamka, sumu
waliyokuwa wameila kwenye mikate ilikuwa ni sumu
kali sana, sumu ya Mchawi. Baada ya kuona Lucas
na Mercia hawaamki Paulo aliamua kwenda ndani
ya Sakarastia kutazama labda angemkuta sister
murcia, alipo ukaribia mlango ukajifungua na
kuingia, alipoingia tu mlango ukajifunga naye
akaanguka chini na kupoteza fahamu.
Sisiter murcia atapatikana?
 
NO. 012.
ILIPOISHIA.
Kundi la wachawi linafanikiwa kumchukua sister
Murcia kutoka kanisani na kutoweka naye ikiwa ni
baada tu ya kumpulizia dawa yao ya kichawi kazi
iliyofanywa na Nyamumwi au Alicia wa kichawi
pamoja na Josephina Bint ambaye pia alitumwa na
hao hao wachawi kwa ajili ya kumsaidia nyamumwi
kumteka Murcia; kweli kama zoezi lao lilivyo kuwa
limepangwa wamefanikiwa kutoweka naye. Kipindi
hicho hicho Paulo naye anafanikiwa kufika kanisani
baada ya kutoroka katika mikono ya wachawi,
Baada ya kufika kanisani Paulo anamkosa Sister
Murcia anawakuta Mercia pamoja na Lucas lakini
wote wakiwa hawajitambui ikiwa tu ni baada ya kula
sumu ya kichawi iliyokuwa kwenye mikate. Akiwa
kashindwa kuwaamsha Paulo anaingia ndani ya
Sakarastia. Baada ya Paulo kuingia ndani ya
Sakarastia anaanguka na kupoteza fahamu na
mlango wa Sakarastia unajifunga.
SONGA NAYO.
hatimaye usiku ulikucha. kanisani Mercia na Lucas
wote kwa pamoja wanaamka lakini wakiwa na njaa
pamoja na kiu isiyo na kifani. wote kwa pamoja
waliangaliana kwa muda kama wa dakika tano bila
kusemeshana, hapo walikuwa wakijiuliza maswali
yasiyokuwa na majibu. baada ya dakika hizo kupita,
Mercia alimuuliza mwenzake.
"Lucas kwanini tuko humu kanisani, kwanini
hatukulala Vyumbani?"
"Hata Mimi sijui labda tukamuulize Sister Murcia
anaweza kutueleza!"
"Halafu naisi njaa, na kiu utafikiri nilikuwa shambani
sijui kwanini, hivi Jana tulikula kweli?"
Mercia aliuliza tena.
"Hapana, hata Mimi ni kama wewe na sikumbuki
kama tulikula"
Majawabu ya Lucas yalimtosha kabisa Mercia
kuendelea kuuliza. Kumbe wote kwa pamoja
walisahau kuwa jana usiku walikula. Hivyo hivyo
Wote kwa pamoja wakiwa na njaa zao walitoka inje
ya kanisa kwa ajili ya kwenda kumuona Sister
Murcia, mungu wangu, vichwani mwao hakukuwa
hata na wazo lolote wala hawakuju kama kipindi
hicho kanisani hapo walikuwa wamebaki peke yao
tu, na wala hakukuwa na mwingine zaidi ya Paulo
ambaye naye alikuwa yumo ndani ya Sakarastia
akiwa hajitambui kabisa. Vijana wale wote wawili
walikisogelea chumba ambacho alichokuwa
anakitumia Sister Murcia pamoja na Mabint wakike
kulala ili wamuulize kwanini wao wamelala kanisani.
Waliufikia mlango na kuugonga wakisubili
wafunguliwe mlango huo, waligonga mlango mala
nyingi bila kufunguliwa wala kuitikiwa karibu. baada
ya kuona kimya Mercia aliamua ausukume, mlango
na kuufungua mwenyewe, Mercia bila kuogopa
aliingia ndani ya chumba hicho kangalia kama kuna
mtu lakini hawakumkuta Sister Murcia, wala Alicia
wala Mgeni wao(josephina) lakini taa ya chumba
hicho bado ilikuwa inawaka. Hali hio iliwafanya
kujipa matumaini kuwa huwenda sister Murcia
atakuwa kanisani ndani ya Sakarastia akisali.
baada ya kuona hivyo wote kwa pamoja
wakasemeshana kuwa bila Shaka Sister na Alicia
watakuwa kanisani kwenye Sakarastia. Basi wote
wawili waliamua waongozane kurudi kanisani kwa
ajili ya kumwangalia Sister Murcia wakizani kabisa
kuwa yumo ndani ya Sakarastia, waliongozana
mpaka ulipokuwa mlango wa Sakarastia, lakini
walipofika mlangoni walijaribu kuufungua mlango
ule, lakini mlango haukufunguka uligoma kabisa
kufunguka. Hali hio iliwanyima Furaha Lucas na
Mercia. Baada ya kuwakosa wenzao kanisani
waliamua wote watoke inje, wazunguke nyuma ya
kanisa wakiamini labda huwenda wakawaona, Nako
huko waliwakosa hawakuwaona.
"Sasa hawa wameenda wapi?"
"Hata Mimi sijui"
"Labda watakuwa, wametoka na yule mgeni wa
Jana"
"Mgeni!?"
Alicia aliuliza kwa mshangao. Kwani alikuwa
amesahau kama Jana walikuwa na mgeni.
"Ndiyo! Umesahau kama Jana kuna mgeni wa kike
alikuja hapa?"
Lucas alisema.
"Sawa lakini Sister Murcia hawezi kuondoka hapa
bila kutushilikisha sisi"
Mercia alisema.
"Sawa Mercia wewe unaamini si unakumbuka
kabisa hapa kuna uhaba wa chakula, huwenda
wameongozana kwenda kutafuta chakula"
Lucas alisema.
Baada ya kuzungumza hivyo, wote kwa pamoja
bado wakiwa wamesimama, nyuma ya Kanisa
walianza kuulizana usiku ilikuwa vipi mpaka
wakalala ndani ya Kanisa. Baada ya kuulizana
maswali machache wakakumbuka kuwa Jana usiku
wao walikula mkate kutoka kwa Josephina. Mkate
huo ndio huwenda umewafanya kulala ndani ya
kanisa.
hapo ndipo Akili ziliwaingia wakajikuta wanaamini
kuwa Wenzao huwenda, wametekwa. Mawazo yao
yakawapeleka kwa Josephina, fikira zao zikawambia
kuwa Josephina hakuwa mtu mzuri huwenda alikuwa
ni miongoni mwa watu wabaya aliyekuwa
ametumwa kuja kuwaangamiza. Kitendo cha
kukumbuka machozi yalianza kuwatoka wote kwa
pamoja wakajua kabisa wamempoteza sister
Murcia. Bado wakiwa wanaendelea kulia nyuma ya
Kanisa, mala Josephina alitokea mbele yao akiwa
katika sura ya kutisha Sura ya kishetani, Sura ya
kichawi. Lucas na Mercia baada ya kuona hivyo kila
mmoja alikimbia kujificha mgongoni kwa
mwenzake, walikuwa kama wanapigana ili kila
mmoja kuutafuta mgongo wa mwenzake kwa ajili ya
kujificha. Kitendo hicho kilimfurahisha sana
Josephina, Akacheka kwa nguvu kisha akasema.
"Yeyote akija huku huwa arudi alikotoka, wala
hakuna taarifa ambazo huwa zinarudi mliko toka, ni
wakati wenu wa kufaaaaaa Ha ha ha ha haaa!"
Josephina alisema
Maneno yaliyokuwa yanatisha huku akimalizia kwa
kicheko cha nguvu, maneno hayo yaliwaingia Lucas
na Mercia yakawa yanazikwangua nyoyo zao.
huwezi amini wote kwa pamoja wakavikumbuka
vitendo na mafunzo ya Sister Murcia, alivyokuwa
anawaambia kuwa wanapaswa wawe na imani
kubwa miyoni mwao ili kulishinda jeshi la shetani.
Hata hawakuwa na namna na njaa zao walianza
kulia kuomba msamaha kwa Josephina asiwauwe,
walishindwa hata kumuomba na kuziweka imani zao
kwa Bwana mungu wao labda wangeokolewa, wao
walikuwa wakupiga makelele ya kuomba msamaha
kwa shetani hawasamehe.
"Hivi unaweza kumuomba shetani msamaha halafu
baadaye umshinde. Basi jueni kuwa Shetani kazi
yake ni kuwangamiza, haijarishi ni kwa njia gani ila
yeye huwa anaangamiza tu, hata nikikusameeni
nitakuwa sijawasaidia. kawaida nikipata chasi ya
kuuwa na kunywa Damu huwa siiachi hata kama ni
mtoto mchanga"
Josephina alisema.
Maneno hayo yaliwashitua sana, hapo ndipo Lucas
na Mercia wakajua kuwa wasipomtumainia bwana
watakufa kweli, hapo wakajikakamua kuanza
kumuomba mungu huwenda akawasaidia kutoka
katika janga hilo. Ilikuwa kama ni kujisumbua, Imani
zao zilikuwa bado kabisa. Ilikuwa ni rahisi kwa
Josephina kuwasogelea karibu yao. Ndicho kipindi
hicho hicho Nyamumwi naye alitokea akiwa bado
katika sura ya Alicia. bila kujua wala kutambua
Mercia na Lucas wakamsogelea kumuomba msaada
wakizani kuwa ni Alicia. Kabla hawajamfikia
walishitushwa baada ya kuiona ni Sura ya Bibi
mwingine kabisa Ambaye hawajawahi kumuona
toka wanafika kijijini hapo. Kitendo cha kuona Alicia
kugeuka kuwa bibi tena mwenye kutisha, mdomono
amejaa mapengo na makucha ya kutisha, waliogopa
na kurudi nyuma kwa kasi kumuepuka yule Bibi
mchawi, Bibi Ambaye alikuwa kajigeuza katika Sura
ya Alicia.
"Ha ha ha ha! Mwanzo mlikuwa vichwa mpaka
mkapelekea wenzetu kujeruhiwa na kupoteza
sehemu katika mihili yao, Leo mmepatikana.
Lazima tuwale, ha ha ha ha ha"
Yule Bibi alisema na kucheka.
Tayari muda huo Mercia alikuwa kaisha zima. Lucas
alijitahidi kukimbia kurudi ndani ya kanisa akizani
labda kuna kupona lakini napo haikusaidia kikundi
kile cha wachawi wawili, kilimtokea huko huko. Bila
Kupoteza muda, Josephina alimpiga pigo moja
Lucas naye akazimika kisha wakatoweka naye
pomoja na Mercia.
 
NO (013).
ILIPOISHIA.
Lucas alijitahidi kukimbia kurudi ndani ya kanisa
akizani labda kuna kupona lakini napo haikusaidia
kikundi kile cha wachawi wawili, kilimtokea huko
huko. Bila Kupoteza muda, Josephina alimpiga pigo
moja Lucas naye akazimika kisha wakatoweka naye
pomoja na Mercia.
SONGA NAYO.
Bado ilikuwa ni mapema sana za asubuhi. Baada ya
Mercia na Lucas kuchukuliwa na kikundi kile cha
wachawi yaani Nyamumwi na Josephina. Sister
Murcia alikuwa ndani ya msitu mkubwa uliokuwemo
ndani yake pango kubwa. muda huo alikuwa
ajitambui kabisa, alikuwa amelala kama maiti. Ni
muda huo huo sister Murcia akiwa amelala hapo
hapo, kilitokea kikundi cha vijana wengine saba
wakiwa na mwanamke mmoja mzee, Bibi kabisa,
Ambaye alikuwa akiwaongoza vijana wale. Lakini
vijana wale hawakuwa peke yao Bali walikuwa
wamebeba mwili wa mtu uliokuwa umefunikwa kwa
likitambaa jeusi, nao pia wakiusogeza Mahara
alipokuwa amelala sister Murcia. Vijana wale
walisimama pale pale alipokuwa amelala Sister
Murcia, kisha yule Bibi akawaambia wauweke mwili
waliokuwa wameubeba pale pale chini mkabala na
alipokuwa amelala sister Murcia, baada ya kuuweka
mwili huo, Bibi yule alikiondoa kitambaa kile cheusi
walichokuwa wameufunikia mwili ule. La hasha!
Kumbe mwili ule haukuwa wa mwingine, bali
ulikuwa wa Alicia, mwili wa Alicia ulikuwa ujastiliwa
hata chembe ya nguo, ulikuwa mtupu kama alivyo
zaliwa, mwli mzima ulitapakaa Damu; mwili huo
ulikuwa ukionekana kama umechanjwa na visu.
baada ya kufanya Yale yote, Bibi yule aliwaamrisha
vijana wake wauvue mwili wa sister Murcia nguo
alizokuwa kazivaa. Bila kuchelewa walimvua nguo
zake. Walipomvua nguo zake bibi yule mchawi
alichukua fimbo yake kisha akauchapa mwili wa
Sister Murcia mala tatu, yote hayo yalikuwa
yakifanyika Sister Murcia alikuwa ajitambui kabisa.
Alikuwa kama maiti aliyekuwa anangoja kuoshwa
akafanyiwe maziko. Bibi yule akuishia kuupiga mwili
wa Sister Murcia Bakora, aliendelea na jambo
lingine la ajabu. Alichukua Dawa nyeusi kabisa
iliyokuwa kwenye ungo ulio kuwa eneo hilo na
kuanza kuimimina kuuzunguka mwili wa Sister
Murcia. Bibi aliiuzunguka mwili pia mala tatu.
Baada ya kulimaliza zoezi lake, Sister Murcia
aliamka mwenyewe mzima mzima. Alikuwa ajielewi
bado alikuwa Zezeta tena zezeta. Baada ya kuamka
bibi yule alikuwa akimfanya alivyojisikia kumfanya.
"Sasa Mimi Naondoka naombeni mkamfanye kama
ambavyo huwa tunafanya, kisha mkamtupe kwenye
kiota cha joka"
Bibi yule alisema. Destuli ya kijiji hicho wanawake
walikuwa wakibakwa na wanaume walikuwa
wakikatwa sehemu zao za siri kisha nao
wanatupwa. Zoezi lililokuwa linaenda kufanyika kwa
Sister Murcia lilikuwa ni zoezi la kubwakwa. Bibi
yule mchawi aliondoka na kuwaacha vijana wale
pamoja na Sister Murcia, akiwa mtupu vile vile hata
atambui kama yupo mtupu. Kwani mpaka muda huo
alikuwa ni zezeta. Baada ya yule Bibi kutoweka tu,
wale vijana wakaanza kumuongoza sister Murcia
kutoka karibu na pango lile na kuelekea mahara
walipokuwa wanapataka wao. Yote hayo alikuwa
yanafanyika ndani ya msistu huo huo. Vijana pamoja
na Sister Murcia waliondoka na kuuwacha mwili wa
Alicia uko pale chini ujitambui.
*****
Ni muda huo huo, ndani ya Sakarastia, Paulo
alikuwa akiota ndoto kama maono ya kwamba kijiji
cha Shimo la moto kinapata ukombozi Mkubwa na
ukombozi huo mkubwa unafanywa na mtoto mdogo
yapata miaka kumi mpaka kumi na miwili. Ndoto
au maono hayo hayakuishia hapo, bali yalimpeleka
mpaka akaona watu wa kijiji hicho wakiruka ruka
kwa Shangwe huku wakicheza ngoma zao za Asiri,
ngoma za kichawi, ngoma ambazo zikichezwa ujue
ndani ya kijiji hicho kuna jambo zito, jambo la
kumtolea mungu wao zawadi tena zawaidi yenyewe
ni mwanamke Bikra kabisa. Baada ya maono hayo
Paulo alishituka akashindwa kutambua ndoto zile
mbili zilimaanisha nini. Akaanza kuitafakari ndoto ya
kwanza akalipata jibu ya kuwa Sister Murcia
yapaswa hapate mtoto na mtoto huyo ndiye tu
mwenye kukikomboa kijiji hicho cha Shimo la moto,
na mtoto atakaye zaliwa lazima atoke katika tumbo
la mama mwema na Baba mwema. Hakukuwa na
Baba mwema katika kijiji hicho kama si Paulo.
Ndoto ya pili hiyo bado alishindwa kuielewa, si
kwamba alishindwa kuelewa kwakuwa alikuwa ajui
hapana alikuwa anajua ilimaanisha nini. alichokuwa
akijiuliza ni vipi kijiji kikombolewe kisha kirudi kuwa
katika hali ya kishetani. Bado akiwa katika wimbi
zito la mawazo, wazo lilimuhijia akajikuta anajiuliza;
Sister Murcia yuko wapi? Kitendo cha kuwaza vile
alishituka Sana, akanyanyuka haraka na kusisamama
kutoka inje ya Sakarastia. Lakini kabla hajatoka
halishangaa sana baada ya kuona panga pamoja na
Ngao, vyote ni vifaa vya kivita. Vitu hivyo kwa
pamoja vilikuwa vimesimamishwa, vikiwa
vimeugemea Malango. bila kujiuliza, Paulo alilishika
panga lile pamoja na ngao yake, pale pale nguvu za
ajabu zikamuingia mwilini akajikuta ni mtu
anayewaza kupambana na jeshi la Shetani. Bila
kuchelewa mlango wa Sakarastia ulijifungua
wenyewe naye akatoka. Alivyo toka ndani ya
Sakarastia alipitiliza moja kwa moja kutoka inje ya
kanisa, hakukumbuka tena kama siku aliyoingia
ndani ya kanisa kutoka katika mikono ya mateka,
yakishetani aliwakuta Mercia na Lucas wamelala
huku hawajitambui. akiwa Bado yupo mlangoni mwa
kanisa Paulo alitamka maneno haya.
"Kwako wewe baba, jina lako litukuzwe, ufalme
wako utukuzwe, hapa duniani na mbinguni. Nifanye
mshindi katika vita hii ya kupambana na jeshi la
watu waovu, nifungulie njia nyepesi kila nitakapo
pita ili kuifanikisha dhamila yangu ya ukombozi
katika kijiji hiki. Amina"
Baada ya kuyasema maneno hayo mazito kabisa,
Paulo alizunguka nyuma ya kanisa, akakitazama kijiji
cha Shimo la moto jinsi kinavyo onekana.
Alichokiona kwenye maono ya ndoto kilikuwa cha
kweli. watu wa kijiji kile walikuwa wakishangilia na
kupiga vigelele. Bado Paulo hakuamini akaamua
akisogelee kijiji kile vizuri aone. kila hatua
aliyokuwa akiipiga tena akikimbia kwa kasi ndipo
nguvu ziliongezeka kwake. Hata njaa ya siku mbili
yeye alikuwa aisikii kabisa.
 
NO. 014.
ILIPOISHIA.
Alichokiona kwenye maono ya ndoto kilikuwa cha
kweli. watu wa kijiji kile walikuwa wakishangilia na
kupiga vigelele. Bado Paulo hakuamini akaamua
akisogelee kijiji kile vizuri aone. kila hatua
aliyokuwa akiipiga tena akikimbia kwa kasi ndipo
nguvu ziliongezeka kwake. Hata njaa ya siku mbili
yeye alikuwa aisikii kabisa.
Songa nayo.
Paulo alikimbia mpaka karibu na nyumba za
wanakijiji, akaona vizuri walivyokuwa wanacheza,
kwa hasira alitoka mbio kuelekea msituni
wanakotelea watu kafara zao, alijua tu tayari Sister
Murcia kaisha kamatwa kama si yeye basi ni Alicia
kwani toka mwanzo walikuwa wamemuahidi kuwa
Alicia atatolewa kafara siku zikifika. Alikuwa mbio
zisizo za kawaida. Upanga wake pamoja na ngao
yake akiwa navyo mikononi alikimbia mpaka karibu
na msitu ambao huwa wanatolea kafara wachawi wa
kijiji hicho cha kichawi. Kabla ajaingia ndani
alisimama, kisha akapiga magoti, kisha akasema.
"Eee mungu, hakika wewe ndiye tumaini la kila
mwanadamu, wewe ndiye ngao ya kweli ndani ya
nyoyo zetu, wewe ndiye ulinzi na ukombozi wa
milele wa maisha yetu. Nilinde Mimi, nioneshe wapi
panafaa kuanzia na wapi panafaa kimalizia, nipe
nguvu za kukishinda kikosi hiki cha shetani. Amina"
baada ya kumaliza kuyasema maneno hayo, ambayo
yalikuwa ni maombi kwa bwana mungu wake,
alisimama. Akavishika tena vifaa vyake vya kazi. Ni
muda huo huo alikuwa kama anasubuliwa amalize
kusali, kilitokea kikosi cha kutisha maeneo hayo,
kikosi hicho kilikuwa cha vijana wa kichawi, vijana
waliokuwa wamevalia mailizi mazito mashingoni
mwao, nao pia wakiwa na mapanga yao. Paulo
hakuogopa wala kutetereka yeye alivishika vifaa
vyake kwa nguvu na kuwasogelea vijana wale
ambao walikuwa wamesimama mbele yake.
Alichokifanya aliinua panga lake juu. panga lile
alilokuwa la ajabu lilitoa miale ya mwanga kama ya
jua, kisha likabadilika likawa la moto. Kilichofuata
pale hata wale vijana wa kichawi walianza kuogopa
kumsogelea. Paulo akulijali hilo aliona kama
wanamchelewesha, alitoka mbio huku akipiga kelele
za hasira huku kaliweka panga lake la moto tayari
kwa ajili ya kukata kichwa cha mtu Ambaye
angejitanguliza kimbelembele. Bado vijana wale wa
kichawi wakijiuliza wafanye nini, walishangaa vichwa
vya wenzao watatu vipo chini, tena Paulo akijiandaa
kumkata mwingine wa nne, wote kwa pamoja
walikuwa waoga Ghafra na kutoweka maeneo hayo.
Baada ya tukio hilo Paulo mwenyewe alijishangaa
nguvu zote zile zimetoka wapi? Hata matukio
aliyokuwa akiyafanya alishindwa kutambua kuwa
yeye ndiye aliyekuwa akiyafanya.
"Bila shaka nguvu ya bwana iko nami" Paulo
alisema pale pale akainza safari ya kuingia msituni.
Msitu wa ajabu msitu ambao umemlea,
ukamfundisha taratibu zote za kishirikina. Kwa
ushujaa aliokuwa nao ndani ya kikosi cha wachawi
hapo kabla, ukasababisha apewe uongozi wa kikosi
cha kudumisha ulinzi wa kijiji kwa wageni
wanaoingia ndani ya kijiji hicho. Akiwa ndani ya
msitu Paulo alikuwa anatembea huku akilitaja jina la
bwana, kimoyo moyo alikuwa akimuomba mungu
amsaidie haweze kutoka salama ndani ya msitu huo
wa kutisha. Yeye mwenyewe alikuwa anaujua
maajabu yake. Akiwa anatembea huku akigeuka
geuka kuangalia kila upande ndani ya msitu huo wa
kichawi mala lilitanda Giza nene, Giza ambalo
alikuwa haoni mbele wala nyuma. Akiwa bado
anastaajabu hicho alishituswa na Sauti ya Mtu
ikimsemesha.
"Nashukuru kwa kurudi nyumbani ingawa si kwenu
tena" sauti hio haikuwa ya mwingine Bali ilikuwa ya
kiongozi wa wachawi wa kijiji cha Shimo la moto,
kiongozi wa upande wa Mashariki akina nyamumwi,
Ambaye pia ndiye alikuwa mwenyekiti wa kijiji
hicho.
Kitendo cha kuisikia sauti hio Paulo alijiweka tayari
kwa mapambano ingawa alikuwa amuoni Adui yake.
Akiwa bado anageuka gauka kuangalia alishangaa tu
anapigwa na kitu kizito ambacho hata yeye
alishindwa kukitambua ni nini, kipigo hicho kizito
kabisa kilimpeleka Paulo chini moja kwa moja.
Richa ya kuanguka chini mwanaume alijikusanya
tena na panga lake mkononi akasimama tena.
Kama vile kulikuwa na maneno yanamuongoza,
alizungusha panga lake kwa nguvu upande wa
nyuma, kilicho sikika ni sauti ya kilio cha mtu.
Hakuishia hapo alilinyoosha panga lake juu kisha
likatoa mwanga mkali; mwanga ambao ulisababisha
ndani ya msitu huo kuwe kweupe nakusababisha
kila kitu kionekane. Kumbe ndani ya msitu
hakukuwa na mtu mmoja kilikuwa ni kikosi cha
vijana wale wale waliopotea baada ya kushindwa
vita ya mala ya kwanza. Kipindi hichi hata wale
vijana walionesha okomavu, wakayashika mapanga
yao kwa ajili ya kupambana na Paulo. Wote kwa
pamoja walimsogelea kwa kasi ili kumvaa. Paulo
aliliona akainama chini huku kainua ngao yake juu,
kilichofuata ni vijana wale kuanguka chini huku
wakipiga makelele ya maumivu, huku miguu yao
ikiwa vibutu tayari ishakatwa. Zoezi hilo lilimchukua
kama dakika tatu tu kwa uwezo wa bwana akawa
amelimaliza. Alipolimaliza zoezi hilo Paulo
alimtafuta mkuu wa wachawi wa kijiji hicho
hakumuona, kumbe tayari hakuwepo. Kwa mwendo
wa tahadhali Paulo aliendelea kusogelea upande
liliko panga la siri la kutolea kafara ya kijiji kwa
mungu wao ili kuwaokoa watu wake.
*****
Ulikuwa ni umbali kama mita amsini kutoka liliko
pango la kutolea kafara, Paulo kwa tahadhali na
umakini wa hali ya juu huku matumaini yake yakiwa
kwa bwana, mapigo ya moyo yalimlipuka baada ya
kumkuta Mercia yupo amefungwa kamba kwenye
mikono na miguu yuku chini akiwa kama alivyo
zaliwa. Kamba zile zilikuwa zimekaa kila moja
upande wake, ikiwa kama vile anataka kuvutwa kila
kipande cha mguu na mkono upande wake. Kitendo
hicho Paulo ilikijua kabisa kuwa ni kawaida ya watu
wa kijiji hicho. Kwa hasira akijua kabisa Mercia
bado mzima alikimbia kuziwai kamba kabla
azijavutwa kumgawanyisha Mercia vipande vinne.
Ilikuwa kama anangojewa yeye ili wamchane
vipande vipande yeye akiona. Kabla hata hajazifikia
kamba zile zote kwa pamoja zilivutika ili kumchana
Mercia vipande vinne. Kwa bahati nzuri aliwahi
akafanikiwa kuzikata kamba zote nne hata kabla
azijaleta madhara kwenye mwili wa Mercia. Richa
ya kumuokoa Bint yule mwanafunzi mwenzake lakini
tayari alikuwa kaisha fariki, hakuwa tena Mercia
Ambaye alikuwa amemzoea ulikuwa mwili wa
Mercia. Ilimuuma sana paulo kumpoteza
mwanafunzi mwenzake Ambaye alikuwa
akifundishwa naye mafundisho mema ya kumjua na
kumtumikia bwana. Hata matumaini ya kumpata
sister Murcia akiwa mzima yalififia, akachoka na
kuchoka. Akiwa pale pale chini huku kapiga magoti,
kichwa cha Mercia kikiwa viganjani mwake juu ya
malaja yake, machozi yamkitoka, kilitokea kipepeo
kikatua kwenye mkono wake wa kulia, kitendo cha
kukiona kipepeo kile kilichokuwa na langi nyeupe,
Paulo akayakumbuka maono ya ndoto kuwa kijiji
cha Shimo la moto kitakombolewa na Mtoto
mwema kutoka katika kizazi cha watu wema. Yaani
Baba mwema na mama mwema, kitendo hicho
kilimrudisha Paulo katika hamasa na nguvu za
ajabu, akasimama kisha akapiga kelele zisizo za
kawaida; kelele ambazo hata msitu nao uliitikia wito
kwa nguvu, kisha ukatulia tulii tayari kwa kuzipokea
taarifa za kilichokuwa kinafuata. Akiwa hapo hapo
kikosi kingine kilitokea, kikosi hicho alikuwa
anakijua vizuri, kilikuwa ni kikosi maalumu kwa ajili
ya kubaka na kukata sehemu za siri kwa wanaume
na ndicho hicho hicho kilicho kuwa kinataka
kuuchana mwili wa Mercia. Kwa kipindi hicho watu
wale wangejua basi wasingejisumbua hata
kumsogelea Paulo. Mwanaume alikuwa kaisha
vimba kwa uchungu wa hasira, hasira ambazo hata
mate yake tu ya kinywa yalikuwa yashakuwa sumu
hatari sana. Kwa hesabu ya haraka haraka kikosi
hicho kilikuwa cha vijana au vidume kama kumi na
sita. Kwani unajua hata kikosi kizima kilivyo kwisha,
vichwa tu ndivyo vilivyokuwa vinadundadunda chini
kama mpila umekoswa wa kuupiga.
"Nguvu ya Bwana ipo nami" Paulo alisema tena.
Mwanaume kila alipokuwa analisema neno hilo
alijiisi kama ndiye mwanaume mwenye nguvu na
uwezo wa kupigana kuliko wote Duniani. Na
haikuwa uongo kweli nguvu ya Bwana ilikuwa naye.
Baada ya kumaliza kazi hio alikata majani ya miti
ndani ya msitu huo akausitiri mwili wa Mercia.
Sasa swali likabaki.
"Wengine wako wapi? au nao washauliwa?" Paulo
alijiuliza. Hapana lazima wapo, nitawapata wapo.
Pale pale mwanaume alipiga tena kelele nyingine
kwa hasira.
"Nitawapataaaaaaa!" Kisha akaiyazisha safari
kuelekea sehemu ya pango la kafara.
 
No: 015.
ILIPOISHIA.
Baada ya kumaliza kazi hio alikata majani ya miti
ndani ya msitu huo akausitiri mwili wa Mercia.
Sasa swali likabaki.
"Wengine wako wapi? au nao washauliwa?" Paulo
alijiuliza. Hapana lazima wapo, nitawapata wapo.
Pale pale mwanaume alipiga tena kelele nyingine
kwa hasira.
"Nitawapataaaaaaa!" Kisha akaiyazisha safari
kuelekea sehemu ya pango la kafara.
SONGA NAYO.
Paulo mwanaume wa shoka alitoka mbio kuelekea
pango la kafara, kwakuwa haikuwa mbali kweli
alipafikia. Baada ya kufika alishituka kuuona mwili
wa Alicia uko mtupu halafu umejaa Majeraha kila
mahara.
"Hapana!..Hapana!...nasema hapanaaaaa! Ilimuuma
Paulo ilimuuma sana tena sana. Kwa kujiamini
aliusogelea mwili wa Alicia ili auone kama bado yu
hai. Akiwa bado anausogelea alipigwa tena na kitu
kizito kichwani akaanguka chini. Kipigo hicho
kilikuwa kama kimempuliza tu akaanguka hata
maumivu Hakuyasikia. Mwanaume akanyanyuka
kutoka chini hata bila kutazama ni nani aliye mpiga
kisha akasema.
" Bwana yu nami, hakika yeye ndiye mwenye
mamlaka juu yangu, na kila kitu hutoka kwake yeye
aliyemkuu kwetu na ndiye tegemezi langu" baada ya
kusema maneno hayo tu aligeuka nyuma. Paulo
alistaajabu sana baada ya kugeuka alimkuta
Nyamumwi pamoja na Josephina wako kama
wameganda huku mikono yao imeunuka juu kama
walitaka kumpiga, kwake aliona ni tukio la Ajabu
sana. Baada ya kuona hivyo akasema.
"Hakika wewe ndiye tumaini langu, wewe ni njia ya
uongofu. Nashukuru kwa ulinzi wako juu yangu kwa
mashetani hawa, Amina"
Alipomaliza kuyasema akainama chini na kuushika
mwili wa Alicia, kwakweli hali aliyokuwa nayo Alicia,
ulimuumiza sana Paulo. Tayari Alicia naye alikuwa
kaisha fariki. Pale pale aliinua mikono yake juu
akasema.
"Hili ni janga lingine la jeraha kwangu, Eee mungu
niepushie hili tena niweze kuwapata hata waliosalia.
Usinipe maumivu makubwa mengine moyoni
mwangu wewe uliyetegemezi la moyo wangu,
amiina" paulo alisema. Kisha akalichukua likitambaa
jeusi lilikuwa limepambwa maeneo hayo ya kichawi
na kuufunika mwili wa Alicia kisha akaubeba na
kuondoka maeneo hayo na kuwaacha wachawi
wawili Josephina na Nyamumwi wakiwa
wameganda kama wamepigwa Shoti. Hakiwa
anatembea huku kaubebea mwili wa Alicia hasira
zilimpanda akajikuta anapiga kelele kubwa za kuita
jina la Sister Murcia.
"Murciaaaaaaaaa! Murciaaaaaaaaa! Murciaaaaaaaaa!
" Sauti yake ilijirudia mala tatu. Msitu mzima
ukaitika kama alivyo kuwa anasema. Kilichokuwa
kinasubiliwa ni majibu ya Msitu huo tu basi, baada
ya kulitaja jina hilo Paulo aliisi maumivu makubwa
sana moyoni, akaushusha mwili wa Alicia chini
kisha akasimama ili kwenda kumtafuta Sister
Murcia. Hakiwa anageuka nyuma hakuamini macho
yake, baada ya kukutana na Uso wa Sister Murcia
akimwangalia kwa hofu huku akihema kwa nguvu,
Paulo alishindwa kuvumilia akageuka tena nyuma
kuficha macho yake ili asimwangalie Sister Murcia.
Aliona haibu kubwa kwani kipindi hicho Sister
Murcia alikuwa kama Alivyo zaliwa wala hakuwa
hata na nguo yoyote mwilini mwake na
haikujulikana amefika vipi alipokuwa amesimama.
Kila mmoja Aliona haibu kwa mwenzake hata Sister
Murcia naye aligeuka nyuma baada ya kujigundua
kuwa yuko mtupu ndani ya msitu tena mbele yake
hakiwepo Mwanafunzi wake. Kila mtu akiwa
kamtegea mwenzake mgongo Paulo alijiangalia
mwilini mwake, amevaa nguo ngapi kwa bahati
mbaya alikuwa na Suruali moja, kifuani nguo tayari
ulikuwa ishatatuliwa imebaki madaso. Alitamani
alitoe likitambaa alilokuwa kaufunikia mwili wa
Alicia ampe sister Murcia ajifunge ilimradi astiri
mwili wake ili wasiendelee kuangaliana katika hali
ya kuogopana. Kulikuwa hakuna namna Paulo
alilishika panga lake na kuyakata jamani mengi
kisha kwa ushujaa tu akamsogelea Sister Murcia na
kumfunga nayo. Hata sister Murcia alishindwa
kukataa kwasababu kulikuwa hamna jinsi.
Walipolimaliza zoezi hilo, Paulo aliubeba tena mwili
wa Alicia hivyo hivyo wote wakiwa na maumivu
mpaka sehemu alikokuwa ameuwacha mwili wa
Mercia. Sister Murcia hakuamini baada ya kuwaona
wanafunzi wake wakike wote wameisha kufa. Alilia
sana ndani ya Msitu huo akashindwa kabisa kuamini
kama ni kweli. Alilia mpaka akawa anauliza mala
mbili mbili kama ni kweli. Paulo yeye machozi tu
ndio yalikuwa yakimtoka. Ilimchukua kama nusu
Saa sister Murcia kuwalilia wanafunzi wake, Paulo
alimuinua na kummtoa eneo hilo. Kilichofuata
kilikuwa ni kutoka ndani ya Msitu huo. Walitembea
kwa majonzi hivyo hivyo huku wote kwa pamoja
wamechoka, kabisa mpaka inje ya msitu. Matumaini
ya kuwatafuta Lucas na Morise yalififia Ghafra.
Wakiwa inje ya msitu huo wa kutisha sister Murcia
alianguka chini na kupoteza fahamu. Paulo
alimbeba na kuanza kutembea naye kurudi kanisani.
Njiani kote kulikuwa kimya kabisa wala hapakuwa
na mtu wala mchawi aliyejitokeza mbele yao.
Ilimchukua kama dakika arobaini na tano Paulo
akawa amefika ndani ya kanisa.
*****
Kanisani Paulo alipakuta kimya kabisa hata
hapakuwa na mtu Ambaye alijitokeza hata
kuwabuguzi wala wakuongea naye. Kwakuwa
alikuwa kamfunga Sister Murcia kwa majani ambayo
nayo yalikuwa yashaanza kunyauka aliingia kwenye
chumba walichokuwa wanalala wanawake akafikia
kitandani akachukua shuka na kurudi kanisani
alipokuwa kamuweka sister Murcia na kumfunika
shuka. Tayari muda ulikuwa ushaenda sana, ilikuwa
kama ni saa tano na nusu za asubuhi. Akiwa
anawaza afanye nini kumsaidia Sister Murcia, wazo
lilimuijia kuwa lazima itakuwa ni njaa
inayomsumbua sister Murcia. Pale pale alijinyanyua
akaelekea kwenye chumba walichokuwa wanalala
wao, akachukua maji mengi kwenye jagi kisha
akarudi kanisani kwa Sister Murcia. Baada ya kufika
alimwagia maji kichwani kuona kama ataamka au
kushituka. Kweli kama alivyokuwa anawaza, Sister
Murcia alitikisa kichwa chake na kuyafumbua
macho yake. ingawaje bado alionekana kuwa ni
mchovu Paulo alijiskia kidogo nafuu kumuona sister
akifumbua macho. Paulo alimnywesha Murcia maji
kidogo hili kumuongeza nguvu. Baada ya kinywa
maji Yale Sister Murcia aliweza kijinyanyua na
kukaa.
"Sister unajisikiaje?" Paulo aliuliza.
Sister Murcia alikuwa akimwangalia tu Paulo usoni
hakuweza hata kulijibu swali aliloulizwa.
"Sister Murcia unajisikiaje sasa hivi?" Paulo aliuliza
tena. Lakini bado sister Murcia alimwangalia tu bila
kumjibu. Bado sister Murcia akiwa anamwangalia
mwanafunzi wake aliyekuwa anampenda kuliko
wote, machozi yalianza kumtoka. Akajiangalia
akakuta kafunikwa shuka halafu ndani kavaa majani
ya miti. Sister Murcia aliomba tu Paulo amsaidie
kumshika ili asiamame. Paulo naye hakuweza kusita
alifanya kama alivyo agizwa. Baada ya kusimama
sister Murcia alimwambia Paulo kuwa anaisi uchovu
sana anaomba amsaidie maji akaoge. Paulo alitoka
mbio ndani ya kanisa akachukua chombo cha
kutekea maji ya kuoga, mbio mpaka kisimani na
kuteka maji kisha akayapeleka Bafuni akaweka na
Sabuni kisha akarudi na kumwambia sister Murcia
kuwa tayari kila kitu. Sister Murcia alijikaza kwa
kujivuta vuta mpaka bafuni akajimwagia maji.
Haikuchukua muda hakawa ametoka huku kajifunga
Shuka lake akaelekea chumbani kwake, akavaa nguo
nzuri kisha akarudi kanisani. Paulo naye alikuwa
mule mule kanisani hakiwa hana habari mawazo
yake yakiwa mbali, alishituka kusikia sauti ya Sister
murcia akimsemesha.
"Paulo wewe husikii njaa?"
"Aaaah! Hivi kweli kuna kula, kweli nahisi njaa sana"
Paulo alisema huku akishika shika tumbo lake.
Majonzi waliyokuwa nayo tayari kwa muda mfupi
yalikuwa yashaanza kufutika miyoni mwao. Mpaka
kipindi hicho hakuna Ambaye alikumbuka kama
Moris na Lucas bado hawajapatikana. Muda wote
huo Paulo alikuwa na nguo zile zile, shati lililokuwa
limechanika chanika na Suruali yake ambayo pia
tayari ilikuwa na Majeraha madogo. Baada ya
kujibiwa hivyo sister Murcia alicheka.
"Kwani wewe husikii njaa?" Paulo naye aliuliza.
"Natamani sana chakula hicho kwasababu lazima
kiwe cha kwangu nami pia niwe cha kwake" Murcia
alisema. Maneno hayo Paulo hakuyaelewa, alibaki
kumwangalia mwalimu wake Ambaye kipindi hicho
alikuwa akitabasamu huku akimwangalia yeye usoni.
"Najua njaa ipo basi ngoja nikatafute chakula?"
"Wapi Paulo utakipata chakula?"
"Usijali nitakipata tu" Paulo alisema. Kisha
akachukua panga na ngao yake vyote vya ajabu na
kutoka mbio kuelekea alikokuwa anaamini angepata
chakula.
 
ILIPOISHIA.
Najua njaa ipo basi ngoja nikatafute chakula?"
"Wapi Paulo utakipata chakula?"
"Usijali nitakipata tu" Paulo alisema. Kisha
akachukua panga na ngao yake vyote vya ajabu na
kutoka mbio kuelekea alikokuwa anaamini angepata
chakula.
SONGA NAYO.
Alikimbia mbio kweli kweli, alipofika umbali kama
wa mita amsini kutoka kanisani. Akasogea sehemu
iliyokuwa na mti mzuri wenye kivuri kisha akapiga
magoti na kusema.
"Eee bwana sina hakika na niendako kama
nitakipata chakula bali tumaini langu nikipate
chakula. Wewe uliyemlezi wa viumbe vyote nifanyie
wepesi nikipate, niongoze njia ya kweli ya kukipata
chakula hicho" baada ya kusema maneno hayo
alimalizia na neno Ameen kuashilia maombi yake
yapokelewe. Baada ya kumaliza kusema hivyo paulo
alitoka pale kwenye mti akiwa haelewi anaenda
wapi. Kilichokuwa kinamuongoza ni njia tu basi.
Kwa bahati mbaya alikuwa akiongoza njia ya
kuelekea mjini. Njia ambayo wanapita watu
waliokuwa wanatoka mjini kuingia katika kijiji hicho
cha shimo la moto. Hakiwa mbio hivyo alijikuta
akisimama ghafra baada ya kuona kichwa cha
Lucas njiani. Paulo alichanganyikiwa kabisa
akashindwa kuamini ikambidi akisogelee kichwa
hicho. Kabla hajakifikia alitokea mwenyekiti wa kijiji
hicho. Ambaye pia alikuwa ndie mchawi mkuu wa
kambi ya magharibi. Mzee yule alikuwa ameshikiria
kamba iliyokuwa kama bakora.
"Najua unajiamini sana na huyo mungu wako, lakini
nazani inaweza kuwa ndiyo mwisho wako wa kuishi"
paulo alimwangalia mzee yule kwa hasira
akamtamani vilivyo. Lakini moyo wake ukamuonya
asimsogelee mzee yule mchawi. Moyoni maneno
yakamuhijia kuwa sema.
"Kwa bahati yako mungu wangu kanikataza
kukumaliza lakini utaonywa kwa madhambi yako"
haikupita hata sekunde nzee yule mchawi alianguka
chini na kujipigiza utafikiri kabwebwa juu kisha
akatupwa. Kipindi hicho pauli alikuwa kaisha
iendeleza safari yake kuelekea alipokuwa
anaongozwa, hata habari za kichwa cha Lucas
alizisahau muda huo. Sijui lakini huwenda yote
yaliyokuwa yanafanyika kwake yalikuwa
yakiongozwa na bwana mungu wake. Alikimbia
mpaka mahara pa njia panda, kama ni mwenye
kumbu kumbu mahara hapo ndiko kuna kona.
Mahara hapo ndipo kuna vibwanga vya hatari na
ndipo walikwama na kutekwa wakiwa na Moris
kisha wakatekwa na kupelekwa makao makuu ya
kichawi iliko kambi ya Mashariki ambayo
inaongozwa na padre Joseph. Cha ajabu alipofika
hapo alilikuta gari lao liko hapo, kila kitu kikiwemo.
Alistaajabu sana kukuta kila kitu kimo kwenye gari,
alipo angalia upande mwingine kungalia kama kuna
chochote cha kumletea madhara hakuona chochote,
swali likabaki ni vipi ataweza kukitoa chakula kile
kwenye gari.
Alijikuta akijisemea moyoni.
"Nitakibeba!"
Atakibeba vipi wakati ni kingi? kitu hicho alikisahau,
tasimini yake ilikuwa haina maana, labda aliplani
kubeba kile ambacho angekiweza. Basi paulo
alipiga magoti kisha akasema.
"Eee mungu hakika wewe unastahili kushukuliwa
sifa njema zikwendee. Hakika wewe ni tegemezi la
moyo wangu, milele amina"
Ilikuwa kama vile ni maombi ya miujiza maombi
yake yalipitiliza moja kwa moja na kupokelewa.
Bado hakiwa amepiga magoti huku machozi
yakimtoka aliishitukia tu gari inatikisika. Akageuka
nyuma kwa mshituko kuangalia nini kimesababisha.
Hakuona chochote, bado akiwa anashangaa mala
mlango wa gari ulifunguka akawa kama anavutwa
kuingia ndani ya gari. Paulo akiwa aelewi ni nini
kinafanyika alijikuta akiingia ndani ya gari kisha
akakaa sehemu ya Dereva. Akili zake zikamtuma
aliendeshe gari, naye akafanya vile, hakika lilikuwa
ni tukio la kushangaza sana kwake alijikuta
akiliendesha gari lile kutoka pale lilipokuwa
kuelekea kanisani. Njia nzima paulo alikuwa
akiendesha gari huku aamini kama ni yeye kweli,
gari liliongoza njia mpaka kanisani. Halipo fika
akapiga honi kuashilia kuwa amefika. Sister Murcia
alitoka ndani ya kanisa mbio kuja inje kuangalia.
Sister akuamini macho yake baada ya kumkuta
paulo akishuka kwenye gari huku akiangalia mikono
yake, kwa muda mfupi paulo alijiona chizi,
alishindwa kuamini kama ni yeye baada ya kufika
pale kanisani.
"Paulo ni wewe au hapana?" Sister Murcia aliuliza.
"Hata mimi sijui kama ni mimi" paulo alijibu. Wote
kwa pamoja walisaidizana kuingiza vitu ndani zoezi
liliwachukua kama nusu saa. Tayari mpaka muda
huo ilikuwa ishafika mida ya saa nane kasoro. Sister
Murcia bado alishindwa kuamini akamwangalia
paulo kisha machozi yakamtoka, kumbe katika vitu
vile kulikuwemo na matunda. Kama ndizi
maparachichi na mapapai lakini kwa uwezo wa roho
mtakatifu na nguvu ya bwana hakuna hata kimoja
kilichonesha arama ya kubadilika.
"Paulo, Naomba unisamehe" Sister murcia alisema.
"Nikusamehe kwa lipi sister mbona hakuna
chochote ulichonikosea" paulo alisema.
Hakiwa na uzuni mkubwa moyoni sister murcia
alijisema.
"Hakika yapaswa iwe kweli, hakika yapaswa aje
mkombozi wa kijiji hiki kutoka katika wewe"
Paulo bado alishindwa kuayaelewa tena maneno ya
mwalimu wake. Kipindi hicho chote sister murcia
alikuwa akitokwa na machozi.
"Hakika sitokuwa na mamlaka juu yako, bali wewe
ndiwe mwenye mamlaka kwangu toka sasa" sister
murcia alisema kisha akajinyanyua alipokuwa
amekaa akaingia ndani ya Sakarastia akaja na
kitabu alichokabiziwa na Murcia wa kwanza
alipofika akayasogelea mazabahu, akapiga magoti
kisha akasema.
"Mapenzi yako yawe juu yake, mpe ujasiri na
umsamehe mazambi yake. Uweke moyo wangu
akaye nao moyoni mwake mpaka pale utakapo
mchukua. Amiina" baada ya kusema maneno hayo
Sister murcia alimsogelea Paulo pale alipokuwa
amekaa na kumbusu katika paji lake la uso kisha
akamkabizi kitabu kile akisome.
Paulo alipokifunua tu kitabu kile cha ajabu kitu cha
kwanza alichokutana nacho, alijikuta anakifunika
kitabu kile kisha akasema.
"Je yapaswa iwe kama maandiko haya yanavyo
sema?" Paulo aliuliza.
"Bila shaka yapaswa iwe hivyo" sister murcia
alisema.
Baada ya kusema maneno hayo paulo ambaye
alikuwa na njaa aliingia ndani akachukua matunda
na kuanza kula. Yote hayo yakiwa yanaendelea
sister murcia alikuwa akimtazama tu.
"Sister wewe si ndiye uliyekuwa wa kwanza kusema
kuwa una njaa?" Paulo aliuliza baada ya kumuona
Sister Murcia akimwangalia. Maneno yake yalikuwa
kama sumu noyoni mwake, badala ya kujibu sister
alianza kutokwa na machozi tena. Tena wakati huu
alikuwa akisema.
"Tafadhali eee bwana mungu wangu, usiniache
nikawa mwenye mateso, mfanye hawepo nami
milele"
 
No.............(017).
ILIPOISHIA.
Maneno yake yalikuwa kama sumu moyoni mwake,
badala ya kujibu sister alianza kutokwa na machozi
tena. Tena wakati huu alikuwa akisema.
"Tafadhali eee bwana mungu wangu, usiniache
nikawa mwenye mateso, mfanye hawepo nami
milele"
Songa nayo.
Sister murcia alipo maliza kuisoma sala yake
akamgeukia Paulo kisha akasema.
"Niamuru basi nami nitatii kwakuwa una mamlaka
makuu kwangu Toka sasa"
Paulo alimwangalia sister murcia kwa aibu,
alishindwa afanye nini kwasababu tu agizo la mungu
lilipaswa litimizwe. Bado akiwa anaendelea
kumwangalia Sister Murcia alitokwa tena machozi.
Paulo alishindwa kuelewa kwanini mwalimu wake
kila alipokuwa anamwangalia alikuwa akilia.
ingawaje alidai ananjaa lakini tayari chakula cha
kutosha kipo. Baada ya kushindwa kuelewa ilimbidi
aulize.
"Sister mbona unalia kila ukinitazama?"
Swali hilo sister murcia bado akulijibu zaidi alizidi
kulia. Baada ya kuona hivyo paulo alimsogelea
akamshika kichwa akakilaza kifuani kwake kisha
akamuuliza tena.
"Je kuna mauzi ambayo nimekufanyia?"
"Hapana, naogopa kusema" sister murcia alisema.
"Je ni kuusu swala la mtoto mwema, mwenye
kukikomboa kijiji hiki?"
"Hapana hilo hata si lenye kiniumiza"
Kwa sauti ya upole iliyokuwa imejaa unyenyekevu
sister murcia alikuwa akiongea. Paulo alishindwa
kuelewa mwalimu wake alimaanisha nini ilimbidi
amuulize tena kwa mala nyingine.
"Je kama si hicho ni nini? Au kupotea kwa
wanafunzi wenzangu?"
"Hapana paulo wewe ni moyo wa faraja kwa moyo
wangu, wale hawakuwa na imani na mungu wao,
labda ndio maana imekuwa hivyo" sister murcia
alisema.
"Kama si hivyo nambie ni nini kilichomo moyoni
mwako?"
"Naogopa kubaki peke yangu" sister murcia
alisema.
"Unaogopa kubaki peke yako! Mbona mi nipo nawe
wakati wote?" Paulo aliuliza kwa mshangao baada
ya kauli ya sister murcia kumshangaza.
"Paulo.....lazima......lazima mtoto apatikane baina
yangu na wewe kwani wewe ndiye uliye mwema
katika kijiji hiki, lakini nilikuwa ndani ya Sakarastia
nikaona kuwa wewe lazima ufe pale tu mimi
nitakapokuwa na mjamzito"
Sister murcia alisema, machozi yakimtoka huku
kichwa chake kimeegeshwa kifuani kwa paulo.
Maneno hayo yalimshitua paulo na ndio ulikuwa
ukweli kuwa sister murcia akipata mimba ya mtoto
atakaye kikomboa kijiji cha shimo la moto yeye
yapaswa afe. Hayo yalikuwa ni maono ya kweli
aliyooneshwa sister murcia.
Kwa upole na kwa unyonge paulo alimshika sister
murcia kichwani akasema.
"Hakika ni katika wema, na kitokacho kwa bwana
mungu wetu hakipaswi kukataliwa au kukimbiwa ni
dhambi kubwa kwetu kupingana na agizo la bwana
mungu wetu. Yapaswa litimizwe ili ufalme wake
utimie na ukamilike. Hakika bwana mungu wetu
yeye aujua ukweli wa nyoyo zetu na maisha yetu,
yeye ndiye mwanzo na mwisho wetu yapaswa tutii
na kutekeleza maamrisho yake, ili ufalme wake
utimie"
Paulo alitamka maneno yaliyomjaza imani sister
murcia akakiinua kichwa chake kutoka katika kifua
cha paulo na kumtazama tena usoni. Akilia kwa
kwikwi sister alimkumbatia paulo na kusema.
"Naomba unisanehe kwa maneno hayo"
"Ujanikosea hakika moyo wangu unakwamini na
kukusikiliza, basi yanipaswa niyatii na kuyapokea
yatokayo kwako" paulo alisema.
Baada ya kusema hivyo paulo alimshika murcia
begani na kumpa ndizi ale kwani toka watoke
msituni alikuwa ajala chochote. Sister murcia
aliipokea na kuila, lakini bado alikuwa akimwangalia
paulo machozi yakimtoka. Paulo alijinyanyua kutoka
kanisani akaingia jikoni akaliwasha jiko lao la gesi
akachemsha chai haraka kisha akachukua mkate
akarejea navyo kanisa na kumtengea sister murcia
ale ili apate nguvu maswala mengine yaendelee.
*****
Siku zilipita mwezi ukakatika wote wakiwa wanaishi
wawili katika eneo hilo la kanisa, hakukuwa na
usumbufu wowote. Walidumisha maombi na kusari
kwa nguvu hata kukumbuka kuwa kuna kuzaliwa
mtoto walisahau mbali na hilo walisahau pia kuwa
siku za kufa paulo zinasogea.
Ilikuwa ni siku mpya ndani ya mwezi huo huo. Sister
murcia aliisi mabadiliko ambayo ni ya lazima kwa
mwanamke yoyote kumkuta katika maisha yake.
Kiujumla zilikuwa ni siku katika siku za hesabu.
Siku hizo ndizo huwa siku za kupata mtoto. siku hio
Toka mchana mpaka jioni wote walikuwa
wakiangalina kwa kuogopana, hakuna aliweza
kumwangalia mwenzake kwa muda kwani hali ya
kufanya tendo la ndoa kwa ajili ya mtoto ilikuwa
ishawaingia miyoni mwao. Hata usiku ulipita siku
nyingine ikaingia kama ilivyokuwa kawaida ya Sister
murcia alikuwa akiamka mapema na kuanza
maombi yake, siku hio hata paulo naye aliamka
mapema na kuingia ndani ya Sakarastia kwa ajili ya
kufanya maombi. Ndani ya sakarastia alikuwemo
Sister murcia naye akifanya maombi. Walikaa mule
kila mmoja akiomba maombi yake. Hatimaye saa
ya kutoka ilifika, walipojaribu kuufungua malango
mlango uligoma kufunguka, haukufunguka hata
walipotumia nguvu mlango wa chumba kile chema
ulishindikanika kufunguka.
"Bila shaka ni wakati wenyewe aliouchagua bwana,
wakukitafuta kile kizazi chema kwa ajili ya
kukikomboa kijiji hiki" paulo alitamka.
Baada ya kuyatamka maneno hayo mlango
ulifunguka. Sister murcia akuamini akamwangalia
tena paulo macho yake yakakutana na ya paulo
ambaye kipindi hicho yeye alikuwa amejawa na
tabasamu, waliangaliana kwa muda kama dakika
tano Kisha paulo akamshika sister murcia na
kuongozana naye kutoka ndani ya Sakarastia kisha
inje ya kanisa na kuelekea katika chumba
alichokuwa anakitumia sister murcia. Lilikuwa ni
zoezi gumu sana kwao lakini ilikuwa amna jinsi
iliwapaswa walifanye ili litimizwe agizo la bwana
mungu wao. Baada ya kukifanya kutendo kile siku
hio ndio ilikuwa ni ngumu kwao kwani hakuna hata
ambaye alitamani kuwa karibu na mwenzake. Sister
murcia alipomaliza kuoga alirudi chumbani kwake
akakaa, paulo yeye kidogo alikuwa na ujasiri
alifanya maandalizi ya chakula na kumpelekea sister
chumbani kwake kisha yeye akarudi kanisani na
kuendelea na maombi. Moyoni mwake paulo
ilikuwa ni kukiombea kizazi kitacho zaliwa kiwe
chini ya namlaka ya bwana. Paulo akusahahu
kwakuwa alijua kabisa wakati wake wa kufa
unamkaribia kama alivyo sema sister murcia,
aliomba maombi ili ikifika siku hio apokelewe
salama. Alizikumbuka dhambi zake, machozi yakiwa
yanamtoka paulo aliomba sana toka mida ya
asubuhi kama saa nne mpaka jioni hakuweza kula
chochote alikuwa akiomba tu.
Hali hio haikuwa kwake tu Sister murcia naye
alikuwa na wakati mgumu, mawazo yalikuwa
hayamuishii alitambua kabisa baada ya kukifanya
kitendo hicho, zimebakia siku chache tu za kuwa na
paulo siku za kumtazama katika macho yake,
machozi tu ndio yalikuwa yakimtoka.
"Sijui nitaishi vipi bila uwepo wake, nitaishi vipi
nikimwangalia huku najua wakati wake wa kuniacha
ndio huu. Muda wowote tangu sasa ataniacha. Eeeh
mungu kwanini umeyaruusu haya yanikute?" Sister
murcia alijisemea moyoni. kweli inauma inauma. Ni
bora hata wengine wangekuwepo basi kidogo faraja
ingekuwemo lakini atabaki peke yake katika kijiji
hicho cha shimo la moto endapo paulo akiondoka.
ITAENDELEA.
 
NO. 18
ILIPOISHIA.
Sijui nitaishi vipi bila uwepo wake, nitaishi vipi
nikimwangalia huku najua wakati wake wa kuniacha
ndio huu. Muda wowote tangu sasa ataniacha. Eeeh
mungu kwanini umeyaruusu haya yanikute?" Sister
murcia alijisemea moyoni. kweli inauma inauma. Ni
bora hata wengine wangekuwepo basi kidogo faraja
ingekuwemo lakini hatabaki peke yake katika kijiji
hicho cha shimo la moto endapo paulo akiondoka.
Songa nayo.
Siku nzima ilikuwa ni kilio kwa sister murcia. Hata
siku iliyofuata alijikaza kutoka ndani kwake kuja
kanisani kusali. Kwa bahati mbaya ama nzuri kwake
alimkuta paulo yumo ndani ya kanisa akiendeleza
maombi. Sister Murcia alishindwa hata kufanya
maombi alisimama, akalishika tumbo lake ambalo
alitegemea kubeba mimba muda si mrefu, pale pale
machozi yakamtoka. Kumbu kumbu zikamrejea
akatoka kanisani kurudi chumbani kwake.......Baada
ya sister murcia kuondoka paulo naye alitoka nyuma
na kumfuata huko huko chumbani kwake. Alipofika
akamkuta sister murcia amekaa kitandani machozi
tu yakimtoka.
"Sister Murcia tafadhali naomba usilie kwani bwana
hawezi kukuacha wewe katika mateso. Si wewe tu
hata mimi inaniuma tena sana tu kukuacha wewe
ukiwa na kizazi changu tumboni mwako bila hata
kukiona, lakini kwasababu ni agizo la bwana
yanipaswa mimi nife ili huyo azaliwe na huyo
atakaye zaliwa yeye ndiye atakaye kikomboa kijiji
hiki. Usife moyo na kukata tamaa, usioneshe
udhaifu juu ya jambo hili, imani yako itashuka....na
imani ikisha shuka tu, tayari shetani anapata nafasi
ya kukiingilia hata kile unachokitarajia kutunga
tumboni mwako. kitashambuliwa na jeshi la
shetani. Nakuomba ujipe Ujasiri twende ukasali.
Mungu yu pamoja nasi hawezi kabisa kukuacha
ukateseka"
Paulo alisema. Baada ya kusema maneno hayo kwa
ujasiri kabisa wa hali ya juu paulo alimbusu Sister
murcia kwenye paji la uso kisha akamnyanyua
kitandani kwake wakaongozana kurudi kanisani kwa
ajili ya maombi.
Mida kama ya saa mbili ndio walimaliza kuomba.
Wakiwa wanatoka ndani ya kanisa kuja inje
walikutana na vijana wawili mlangoni mwa kanisa.
Vijana wale walikuwa ni miongoni mwa walinzi wa
kijiji hicho. Si kwamba walikuwa na mapanga
hapana walikuwa wao na miili yao pamoja na miguu
na mikono yao huku ikiwa mitupu kabisa. Sister
murcia aliogopa sana baada ya kuwaona. Paulo
alikuwa tayari kaisha jipanga kwa ajili ya kuwakabiri.
Hata kabla paulo hajafanya maamuzi yoyote
alishangaa kuwaona vijan wale wakipiga magoti
mbele yao kisha wakasema.
"Sisi ni wenye dhambi tunaomba tusamehewe
dhambi zetu"
Hakuna aliyeamini paulo na sister Murcia kila
mmoja alimgeukia mwenzake na kumwangalia kwa
muda kama wa sekunde thelathini kisha paulo
akaawambia vijana wale wanyanyuke kisha
akawaruhusu waingie kanisani.
Sister murcia alikuwa na wasiwasi nao, alishindwa
kuwaamini kwani alilikumbuka tukio la Josephina na
Nyamumwi ambaye mpaka kipindi hicho walikuwa
tayari washakufa kwa uwezo wa nguvu za bwana.
Akiwa mwenye wasiwasi alimuita paulo pembeni na
kumwambia.
"Paulo umesahau tukio la kutekwa kwangu, mi
siwaamini tena watu hawa?"
"Si kwa mamlaka yako bali kwa mamlaka ya mungu
wako, je mimi ni nani kwako?"
Paulo alimuuliza Sister murcia.
"Wewe ni mkuu kwangu, umepewa mamlaka na
nafasi kubwa moyoni mwangu. Wewe ni mume
wangu"
Kwa upole Sister murcia alisema.
"Basi bwana kakisikiliza kilio chako, wala hutobaki
kwa mateso na hii ni dalili za kweli, ya kuwa tayari
kile alicho ahidi bwana kimeanza kutunga ndani ya
tumbo lako"
Paulo alisema. Baada ya paulo kuyasem maneno
hayo, sister murcia aliliangalia tumbo lake ambalo
mpaka kipindi hicho lilikuwa halioneshi kama kuna
kiumbe ndani yake. Alitumia kama dakika moja
kuliangalia tumbo lake machozi yakamtoka
akamgeukia tena mpenzi wake akamwangalia kisha
akamuuliza.
"Wanitazama vipi hali yangu kwa sasa?"
Swali hilo paulo alilijibu kuwa.
"Moyo wako unaonekana una majeraha mengi,
majeraha ambayo yanapelekea imani yako kushuka.
Mtumainie bwana kwa kila jambo kwani yeye
anaujua wakati ulionao"
Paulo alisema maneno hayo kisha akamfuta
machozi Sister murcia ambaye hata kwa kipindi
hicho alisha kuwa npenzi wake kwasababu tu ya
kukikamilisha kile kilicho toka kwa bwana.
Baada ya Zoezi hilo alimshika wakarudi kanisani na
kuanza kuzungumza na wageni wao. Vijana
waliokuwa wachawi leo wamejileta wao wenyewe
kutubia dhambi zao. Walizungumza nao kwa kina,
nao vijana wale wakakiri kwa kina juu ya madhambi
yao.
"Mmesamehewa dhambi zenu, kwani mungu wetu ni
mwepesi wa kusamehe madhambi yetu. Kila anaye
muomba kwa imani thabiti mungu umpa kwa muda
muafaka, umlinda katika wakati mgumu. Kwa
mungu hakuna kinachoshindikanika" paulo alisema.
Kisha akawakaribisha wale vijana kuwa nao pamoja.
Siku ilikuwa ni siku ya ajabu wao waliita. Kumbe
watu waliokuja kutubu dhambi zao waliongezeka
hata mwenyekiti wa kijiji hicho, ambaye alikuwa
mchawi mkubwa, aliongozana na Familia yake kuja
kanisani kuomba kusamehewa dhambi zake. Paulo
hakuamini kabisa, kumuona mchawi yule ambaye
alikuwa akitisha kabisa, aliyekuwa hapendi
masihara, aliyekuwa anauwa, akaifanya ardhi ya kijiji
kile kama ya kwake. Kwa hakika lilikuwa ni jambo
la kushangaza. Hata kabla hajafanya chochote akiwa
kasimama mlangoni mzee yule alisema.
"Mungu wako kaniokoa, hakika nalikumbuka tukio
langu la mwezi nyuma. Nilikaa nikilitafakari sana.
Nimekuwa mshirikina kwa zaidi ya miaka ishirini
sikuwahi kuiona nguvu ya ajabu kama ile tena kwa
maneno tu. Hakika nitasimulia na kuwafundisha
watu wote duniani juu ya nguvu za mungu wako"
mzee yule akiwa kabisa na familia yake ya watoto
watano alipiga magoti mlangoni mwa kanisa huku
machozi yakimtoka. Kila mmoja kanisani alishindwa
kuamini. kwakeli lilikuwa ni tukio ambalo hakuna
ambaye angelitarajia. Paulo alijinyanyua pale
alipokuwa amekaa na kuwafuata watu wale na
kuwambiwa.
"Hakika mmesamehewa dhambi zenu, mungu wetu
ni mwepesi wa kusamehe hata kama ulikuwa na
dhambi kama mlima mkubwa" baada ya kusema
hivyo paulo aliwambia watu wale wasimame na
kuingia kanisani waungane na wenzao ili wamsome
bwana mungu wao na kumjua.
*****
Hatimaye siku zilienda, miezi ikakatika. Mpaka
ikawa hata miezi saba tangu Sister murcia akiwa na
mjamzito, bado paulo alikuwepo. Watu walizidi
kuongezeka kuja na kuja katika kanisa la bwana.
Kipindi hiki kijiji kile cha kichawi kilibadilika na
kuwa cha kulitangaza neno la bwana kila sehemu,
hakukuweko tena na kuwaponda waliokuwa
wanakitangaza neno la bwana. Ingawaje wengi bado
waliamini mila zao lakini kiujumla watu wale
walikuwa wakilitangaza neno la bwana bila
matatizo.
*****
Zikiwa zimesalia kama mwezi tu kuzaliwa yule
waliyekuwa wanamtarajia kuja kukikomboa kijiji
hicho, hapo ndipo siku za paulo zilifika tamati, yule
aliyekuwa shujaa wa kijiji hicho cha shimo la moto
aliwaacha watu katika maumivu makubwa maumivu
ambayo kamwe miyoni mwao haikuwa Rahisi
kuyasahau. Ulikuwa ni msiba mzito. Inasemekana
kuwa Sister murcia alizimia kwa wiki kwasababu ya
uchungu aliokuwa nao. Kweli duniani tunapita, huo
ndio ulikuwa mwisho wa mtu mwema, mwenye
nguvu aliyepigania uhai wa watu wenye haki na
kulipigania neno la mungu liweze kusimama na
kuwabadilisha watu wa kijiji kile. Mpaka mazishi ya
paulo yanaisha Sister murcia bado alikuwa
amezimia.
Kipindi hicho kiujumla kilikuwa ni kigumu sana kwa
wanafunzi na watu wote waliokuwa katika kijiji
hicho. Lakini kilichoacha mshangazo na
kusitaajabisha kwa kila mmoja katika msiba wa
paulo, ulitokea mng'alo wa ajabu katika jeneza lake
mpaka anaenda kuzikwa bado hata kabri lake
lilikuwa na mwanagaza au nuru ya pekee, nuru hio
iliwatatiza wengi hata baadhi ya wachawi walijaribu
kulisogelea karibu lile wakiamini kuwa watapata
hata kuichukua nuru hio kiuchawi, walipigwa kwa
nguvu na kuanguka huko. Inasemekana kuwa ni
zaidi ya wachawi ishirini waliolisogelea kaburi lile
wote walitoka pale na majeraha ambayo
yalisababisha hata baadhi kufa kwa muda wa siku
chache baadaye.
Baada ya kifo cha paulo wanafunzi wake
waliendelea kulitangaza neno la bwana kwa
kushirikina na Sister murcia ambaye kwa kipindi
hicho alikuwa anangoja kujifungua mtoto ambaye
angekuwa mkombozi wa kijiji hicho.
 
NO. (19).
ILIPOISHIA.
Baada ya kifo cha paulo wanafunzi wake
waliendelea kulitangaza neno la bwana kwa
kushirikiana na Sister murcia ambaye kwa kipindi
hicho alikuwa anangoja kujifungua mtoto ambaye
angekuwa mkombozi wa kijiji hicho.
SONGA NAYO.
kijiji kiliendelea kuwa na amani, mpaka muda huo
hakukuwa na dalili za kuwa kuna wachawi
wanaoishi, ingawa walikuwepo lakini hawakuweza
kufanya chochote. Kipindi hicho kumbe hata wao
walikuwa wakifanya mipango yao. Baada ya
mwenyekiti wa kijiji hicho kujitoa katika kikundi
hicho cha kishirikina wachawi wa pande zote mbili
waliamua kuungana na kuwa kitu kimoja. Wakiwa
chini ya uongozi wa padre joseph. Hapo ndipo
walipoamua kujipanga upya kwa ajili ya kukifanya
kijiji kile kirudi katika mikono ya kishetani. Wachawi
walijipanga vya kutosha. tageti yao kubwa ilikuwa
siku akizaliwa mtoto ambaye alikuwa tumboni mwa
sister murcia ndio na wao walianzieshe. Kwa imani
zao waliamini kabisa kuzaliwa kwa mtoto huyo,
ambaye hata wao tayari walikuwa washapata taarifa
kuwa ndiye atakaye kikomboa kabisa kijiji hicho na
kuwa kijiji cha kumtumikia bwana, hapo walijua siku
akizaliwa watu wote watakuwa wazubaifu na
kujisahau kisha watawafanyia mbinu zao za kichawi.
Safari yao ya maandalizi ilianza, kwakuwa walikuwa
wanajua kabisa hata mwezi hutoisha Sister Murcia
atajifungua mtoto huyo, wachawi walianza
kujichomeka katika kundi la watu waliokuwa
wanamtumikia bwana. Walifanya hivyo kwa taratibu
kabisa bila kugundulika, hata watu wiliokuwa
wanawaona waliamini ni miongoni mwao, kwani
tayari watu walikuwa washaokoka na kumtumikia
bwana mungu wao walikuwa ni zaidi ya mia tatu.
Hao ni wale ambao walikuwa wakilitumikia kanisa
la bwana. Mamia mengine ya watu bado yaliendelea
kuamini katika ushirikina, wakiamini kabisa kuwa
bila uchawi na miungu yao maisha hayawezi
kwenda, mizimu itawaangamiza. Mpaka zinasalia
kama siku mbili Sister murcia kujifungua wachawi
zaidi ya amsini walikuwa waisha jichomeka katika
watu wa mungu.
*****
Siku iliyokuwa imengojwa kwa hamu siku ya
kumpokea mtoto wa kiume ambaye ameandikwa
kwenye kitabu kuwa yapaswa azaliwe kwa ajili ya
kukikomboa kijiji cha Shimo la moto ilifika. Usiku
mida ya saa saba Sister Murcia alijisikia mabadiliko
mwilini mwake. Alikuwa akisikia maumivu
makubwa mwilini mwake, maumivu ambayo
hakuwahi kuyasikia, alikuwa kalishikilia tumbo lake
huku akiihemea juu juu na miguno ya maumivu
ikiwa imkatiki. Kwa bahati mbaya kwenye chumba
chake alikuwa amelala peke yake. Toka kupotea
kwa wanafunzi wake wa mwanzo wa kike sister
murcia aligoma kabisa kulala na watu chumbani
kwake. Kwa kujing'ang'aniza alitoka inje na kwenda
kwenye nyumba nyingine kubwa iliyojengwa kwa
ajili ya wageni na watumishi wengine wa kanisa.
Ndani ya nyumba hio walikuwemo watumishi wa
kike na wakiume tofauti iliyokuwa ikiwatenganisha
vilikuwa ni vyumba. Baada ya kugonga mlango,
mlango ulifunguliwa. Mtu wa kwanza kuufungua
mlango alikuwa bint mzuuri, bint huyo baada ya
kuufungua mlango na kuiona hali ya Sister murcia,
aligundua kuwa ndio wakati ambao waliungoja. Bila
kuchelewa bint yule aligeuka huku na kule kuangalia
kama kuna mtu. Alipoona kuwa hakuna mtu, bint
yule aliurudisha mlango na kumwambia sister
murcia Waongozane kurudi chumbani kwake.
Kwa kujikaza huku bint huyo akimsaidia, sister
Murcia alikubali kurudi chumbani kwake. Akiwa
anaomba kabisa kimoyo moyo baada ya kufikishwa
chumbani kwake Sister murcia alikarishwa chini yule
bint akamwambia.
"Ndio wakati wenyewe sasa, unaenda kujifungua,
kwahio jikaze na kusukuma kwa nguvu ili upate
kujifungua. Lakini ghafura ndani ya muda mfupi
upepo mkari uliokuwa umeambatana na kimbunga
ulivuma. Upepo huo ulisababisha hata madilisha ya
chumba cha Sister murcia kufunguka. Bint yule kwa
kujifanya kuwa naye anashangaa aliisogelea Switch
ya taa yao ya sorah na kuizima. Ndani ya chumba
lilibaki giza nene limetanda. Sister murcia alijaribu
kuomba msaada taa iwashwe bila mafanikio
hakajikaza kuelekea ilikokuwa taa ili awashe, kabla
hajafanya chochote alishitushwa na mianga mingi ya
mishumaa imetanda, tena yumo ndani ya poli
kubwa, poli ambalo lilikuwa linepakana na msitu wa
kutisha wa kutolea kafara. Yeye akiwa katikati huku
kundi kubwa la watu zaidi ya mia mbili likiwa
limemzunguka. Sister murcia aliogopa sana,
kilichokuwa kimebaki kwake ni imani yake tu
kumkomboa. Alijitahidi kuomba labda mungu wake
angeweza kumtoa katikati ya kundi hilo lakini
haikuwezekana. Muda huo uchungu uliongezeka
sana. Wachawi walipoona hivyo wakacheka sana,
kisha mkuu wao akasimama, akawatolea salamu
yao ya kichawi kisha akasema.
"Yule aliyekuwa akingojwa kwa hamu tunaye. Bila
shaka atakuwa miongoni mwetu wala hatokuwa
upande wa mungu wao"
Mchawi yule alisema, huyo ndiye alikuwa padre
joseph. Padre ambaye sister murcia alisimuliwa
habari zake na Murcia wa kwanza.
"Tunangoja kula nyama ya mama na mtoto. Wote
wawili inasemekana kuwa ni watu wa bwana mungu
wao, lakini sisi ni wakubwa na tunanguvu nyingi
kuliko hata huyo mungu wao, ndio maana
kashindwa kuwaokoa kutoka katika mikono yetu"
Padre joseph aliendelea kuropoka. Wachawi
wenzake walikuwa wakimshangilia sana na vigerere
kwa juu. Kumbe muda huo Sister Murcia alikuwa
anajisukuma kujifungua. Wachawi wakiwa wanapiga
makelele walishitukia kelele za mtoto akilia. Lakini
walipo tazama hawakuona kitu, hakukuwa mtoto
wala sister murcia, zaidi walikuwa wakisiki kelele za
mtoto tu akilia. Ghafra bado wakiwa wanashangaa
ulizuka tena upepo mkali pale pale ikatokea kitu
kama ukuta umewazunguka, hapo ndipo wachawi
walijawa na uhoga wa ajabu, akuna aliyejiamini kwa
uchawi wake, hata padre joseph naye alitafuta njia
ya kutokea lakini hakuiona. Kila walipokuwa
wanajaribu kukimbilia walikutana na ukuta huo.
Bado wakiwa wanaangaika, ilitokea nuru kama taa
iliyokuwa ikimulika alipokuwa Sister murcia na
mwanaye, akiwa kampakata mwanaye kwenye
miguu yake huku akimwangalia kwa furaha ya ajabu,
wachawi nao walibaki kushangaa.
"Imekuwa vipi ndani ya dakika mbili mtoto kazaliwa
kawa mchangamfu" kila mchawi aliyekuwa anaona
kitendo kile alikuwa anajiuliza hivyo hivyo, ilikuwa ni
ajabu kubwa sana kwao. Si kawaida hata kwa
maisha ya kawaida haijawahi kutokea. Kweli mtoto
yule alionekana kama ni mtoto wa miezi saba. Jinsi
alivyokuwa anafanya fanya mikono yake huku yupo
mapajani mwa mama yake. Ni muda huo huo
wachawi wale wakiwa wanashangaa kitendo kile
ilisikika sauti ikiwasemesha.
"Hakika ufalme wa bwana utukuzwe, mbinguni na
Duniani. Huu ni uthibitisho tosha kwenu nyinyi
wanadamu mliokuwa na imani haba kuwa bwana
mungu wenu yupo na anafanya kazi usiku na
mchana. Hakuna mwenye nguvu wala mwenye
mamlaka kama si yeye. Basi yapaswa kumtukuza
yeye na kufuata mamlisho yake mpaka pale
atakapo uchukua uhai wako"
Maneno hayo yalikuwa ya sauti ambayo ilikuwa
ikisikika kwa wachawi wale. Kwakuwa wao
walikuwa hawajui lakini yule alikuwa ni malaika
mwema wa bwana.
Muda huo tayari padre mchafu, ambaye aliyatumia
mamlaka ya bwana kwa ubaya alikuwa kaisha kufa.
Japo Sauti ile walikuwa wakiiogopa lakini wachawi
walijikaza na kusogea alipokuwa Sister Murcia na
mtoto wake ili kumshika. Mpaka muda huo kila
aliyekuwepo pale aliamini kabisa kuwa uchawi si
chochote mbele za mungu. Baada ya kuona
wachawi wale wakimsogelea sister Murcia
alisimama ilikuwa kama vile anajua nini kinaenda
kutokea kwa muda huo. Bila fujo wachawi wale
walijikuta wanapanga mstari wao na kuanza mmoja
mmoja akimsogelea Sister Murcia pale alipokuwa
na kumshika mtoto yule mkono, kisha
wanainamisha vichwa vyao chini kuonesha ishara ya
Eshima na kuondoka. Uwezi amini mpenzi msomaji
kila watu walivyokuwa wanaongezeka kumsogelea,
mtoto yule alikuwa akitabasamu, kisha akaanza
kuwapa mkono yeye mwenyewe hata alikuwa angoji
kuguswa. Hayo ndiyo yalikuwa maajabu ya siku hio
mpaka usiku kucha.
******
Kanisani watu, walipoamka walifanya kama kawaida
yao, wenye kuingia kanisani na kusali walifanya
hivyo. Wengine walikuwa wanaendelea na Shughuri
zingine. Lakini nao pia walianza kushikwa na
wasiwasi baada ya kutomuona Sister Murcia. Hio
ilikuwa ni mida kama ya saa mbili asubuhi.
"Jamani sister murcia mbona haonekani au
kachukuliwa na wachawi?"
Kijana mmoja aliuliza.
Bado wakiwa wanajiuliza walishangaa kuona kundi
kubwa la watu kuzidi hata wale ambao tayari,
walikuwa washabadilika na kumfuata bwana mungu
wao.
Kwakuwa kundi lile la watu lilikuwa limevaa mavazi
ya kichawi chawi. Moja kwa moja watu kanisani
wakajua wanavamiwa, waliokuwepo wote
wakakimbilia mapanga yao tayari kwa kupambana.
Bila kutegemea watu wote kanisani walistaajabu
baada ya kumuona Sister murcia kabebwa juu
mfano wa watu wa pwani kwa machifu wao. Hali
hio iliwafanya kujua kabisa kuwa mkombozi
waliyekuwa wakimngoja kaisha zaliwa. Nao pia
waliamua kwenda kuwapokea watu wale.
Toka muda huo kijiji kizima cha zima moto
kilizizima kwa kufurika watu katika viwanja vya
kanisa lao, lengo kumtazama mwana aliye zaliwa.
Huo ndio ulikuwa ukombozi wa watu wale. Baada
ya mwezi mmoja tangu Kujifungua Sister murcia
naye alifariki na kumwacha mtoto wake ambaye
bado alikuwa mchanga katika mikono salama ya
watu wa kanisani. Mtoto yule alilelewa lakini
alikuwa wa ajabu. Kiujumla alikuwa mtenda miujiza,
wagonjwa waliokuwa na imani ya bwana mungu
wao, waliweza kupona kwa kushika mikono yake.
Toka hapo kijiji cha shimo la moto kiligeuka kikawa
shamba la Mungu.
Mwisho.
 
Back
Top Bottom