Simulizi: Sister Murcia

Simulizi: Sister Murcia

NO. (19).
ILIPOISHIA.
Baada ya kifo cha paulo wanafunzi wake
waliendelea kulitangaza neno la bwana kwa
kushirikiana na Sister murcia ambaye kwa kipindi
hicho alikuwa anangoja kujifungua mtoto ambaye
angekuwa mkombozi wa kijiji hicho.
SONGA NAYO.
kijiji kiliendelea kuwa na amani, mpaka muda huo
hakukuwa na dalili za kuwa kuna wachawi
wanaoishi, ingawa walikuwepo lakini hawakuweza
kufanya chochote. Kipindi hicho kumbe hata wao
walikuwa wakifanya mipango yao. Baada ya
mwenyekiti wa kijiji hicho kujitoa katika kikundi
hicho cha kishirikina wachawi wa pande zote mbili
waliamua kuungana na kuwa kitu kimoja. Wakiwa
chini ya uongozi wa padre joseph. Hapo ndipo
walipoamua kujipanga upya kwa ajili ya kukifanya
kijiji kile kirudi katika mikono ya kishetani. Wachawi
walijipanga vya kutosha. tageti yao kubwa ilikuwa
siku akizaliwa mtoto ambaye alikuwa tumboni mwa
sister murcia ndio na wao walianzieshe. Kwa imani
zao waliamini kabisa kuzaliwa kwa mtoto huyo,
ambaye hata wao tayari walikuwa washapata taarifa
kuwa ndiye atakaye kikomboa kabisa kijiji hicho na
kuwa kijiji cha kumtumikia bwana, hapo walijua siku
akizaliwa watu wote watakuwa wazubaifu na
kujisahau kisha watawafanyia mbinu zao za kichawi.
Safari yao ya maandalizi ilianza, kwakuwa walikuwa
wanajua kabisa hata mwezi hutoisha Sister Murcia
atajifungua mtoto huyo, wachawi walianza
kujichomeka katika kundi la watu waliokuwa
wanamtumikia bwana. Walifanya hivyo kwa taratibu
kabisa bila kugundulika, hata watu wiliokuwa
wanawaona waliamini ni miongoni mwao, kwani
tayari watu walikuwa washaokoka na kumtumikia
bwana mungu wao walikuwa ni zaidi ya mia tatu.
Hao ni wale ambao walikuwa wakilitumikia kanisa
la bwana. Mamia mengine ya watu bado yaliendelea
kuamini katika ushirikina, wakiamini kabisa kuwa
bila uchawi na miungu yao maisha hayawezi
kwenda, mizimu itawaangamiza. Mpaka zinasalia
kama siku mbili Sister murcia kujifungua wachawi
zaidi ya amsini walikuwa waisha jichomeka katika
watu wa mungu.
*****
Siku iliyokuwa imengojwa kwa hamu siku ya
kumpokea mtoto wa kiume ambaye ameandikwa
kwenye kitabu kuwa yapaswa azaliwe kwa ajili ya
kukikomboa kijiji cha Shimo la moto ilifika. Usiku
mida ya saa saba Sister Murcia alijisikia mabadiliko
mwilini mwake. Alikuwa akisikia maumivu
makubwa mwilini mwake, maumivu ambayo
hakuwahi kuyasikia, alikuwa kalishikilia tumbo lake
huku akiihemea juu juu na miguno ya maumivu
ikiwa imkatiki. Kwa bahati mbaya kwenye chumba
chake alikuwa amelala peke yake. Toka kupotea
kwa wanafunzi wake wa mwanzo wa kike sister
murcia aligoma kabisa kulala na watu chumbani
kwake. Kwa kujing'ang'aniza alitoka inje na kwenda
kwenye nyumba nyingine kubwa iliyojengwa kwa
ajili ya wageni na watumishi wengine wa kanisa.
Ndani ya nyumba hio walikuwemo watumishi wa
kike na wakiume tofauti iliyokuwa ikiwatenganisha
vilikuwa ni vyumba. Baada ya kugonga mlango,
mlango ulifunguliwa. Mtu wa kwanza kuufungua
mlango alikuwa bint mzuuri, bint huyo baada ya
kuufungua mlango na kuiona hali ya Sister murcia,
aligundua kuwa ndio wakati ambao waliungoja. Bila
kuchelewa bint yule aligeuka huku na kule kuangalia
kama kuna mtu. Alipoona kuwa hakuna mtu, bint
yule aliurudisha mlango na kumwambia sister
murcia Waongozane kurudi chumbani kwake.
Kwa kujikaza huku bint huyo akimsaidia, sister
Murcia alikubali kurudi chumbani kwake. Akiwa
anaomba kabisa kimoyo moyo baada ya kufikishwa
chumbani kwake Sister murcia alikarishwa chini yule
bint akamwambia.
"Ndio wakati wenyewe sasa, unaenda kujifungua,
kwahio jikaze na kusukuma kwa nguvu ili upate
kujifungua. Lakini ghafura ndani ya muda mfupi
upepo mkari uliokuwa umeambatana na kimbunga
ulivuma. Upepo huo ulisababisha hata madilisha ya
chumba cha Sister murcia kufunguka. Bint yule kwa
kujifanya kuwa naye anashangaa aliisogelea Switch
ya taa yao ya sorah na kuizima. Ndani ya chumba
lilibaki giza nene limetanda. Sister murcia alijaribu
kuomba msaada taa iwashwe bila mafanikio
hakajikaza kuelekea ilikokuwa taa ili awashe, kabla
hajafanya chochote alishitushwa na mianga mingi ya
mishumaa imetanda, tena yumo ndani ya poli
kubwa, poli ambalo lilikuwa linepakana na msitu wa
kutisha wa kutolea kafara. Yeye akiwa katikati huku
kundi kubwa la watu zaidi ya mia mbili likiwa
limemzunguka. Sister murcia aliogopa sana,
kilichokuwa kimebaki kwake ni imani yake tu
kumkomboa. Alijitahidi kuomba labda mungu wake
angeweza kumtoa katikati ya kundi hilo lakini
haikuwezekana. Muda huo uchungu uliongezeka
sana. Wachawi walipoona hivyo wakacheka sana,
kisha mkuu wao akasimama, akawatolea salamu
yao ya kichawi kisha akasema.
"Yule aliyekuwa akingojwa kwa hamu tunaye. Bila
shaka atakuwa miongoni mwetu wala hatokuwa
upande wa mungu wao"
Mchawi yule alisema, huyo ndiye alikuwa padre
joseph. Padre ambaye sister murcia alisimuliwa
habari zake na Murcia wa kwanza.
"Tunangoja kula nyama ya mama na mtoto. Wote
wawili inasemekana kuwa ni watu wa bwana mungu
wao, lakini sisi ni wakubwa na tunanguvu nyingi
kuliko hata huyo mungu wao, ndio maana
kashindwa kuwaokoa kutoka katika mikono yetu"
Padre joseph aliendelea kuropoka. Wachawi
wenzake walikuwa wakimshangilia sana na vigerere
kwa juu. Kumbe muda huo Sister Murcia alikuwa
anajisukuma kujifungua. Wachawi wakiwa wanapiga
makelele walishitukia kelele za mtoto akilia. Lakini
walipo tazama hawakuona kitu, hakukuwa mtoto
wala sister murcia, zaidi walikuwa wakisiki kelele za
mtoto tu akilia. Ghafra bado wakiwa wanashangaa
ulizuka tena upepo mkali pale pale ikatokea kitu
kama ukuta umewazunguka, hapo ndipo wachawi
walijawa na uhoga wa ajabu, akuna aliyejiamini kwa
uchawi wake, hata padre joseph naye alitafuta njia
ya kutokea lakini hakuiona. Kila walipokuwa
wanajaribu kukimbilia walikutana na ukuta huo.
Bado wakiwa wanaangaika, ilitokea nuru kama taa
iliyokuwa ikimulika alipokuwa Sister murcia na
mwanaye, akiwa kampakata mwanaye kwenye
miguu yake huku akimwangalia kwa furaha ya ajabu,
wachawi nao walibaki kushangaa.
"Imekuwa vipi ndani ya dakika mbili mtoto kazaliwa
kawa mchangamfu" kila mchawi aliyekuwa anaona
kitendo kile alikuwa anajiuliza hivyo hivyo, ilikuwa ni
ajabu kubwa sana kwao. Si kawaida hata kwa
maisha ya kawaida haijawahi kutokea. Kweli mtoto
yule alionekana kama ni mtoto wa miezi saba. Jinsi
alivyokuwa anafanya fanya mikono yake huku yupo
mapajani mwa mama yake. Ni muda huo huo
wachawi wale wakiwa wanashangaa kitendo kile
ilisikika sauti ikiwasemesha.
"Hakika ufalme wa bwana utukuzwe, mbinguni na
Duniani. Huu ni uthibitisho tosha kwenu nyinyi
wanadamu mliokuwa na imani haba kuwa bwana
mungu wenu yupo na anafanya kazi usiku na
mchana. Hakuna mwenye nguvu wala mwenye
mamlaka kama si yeye. Basi yapaswa kumtukuza
yeye na kufuata mamlisho yake mpaka pale
atakapo uchukua uhai wako"
Maneno hayo yalikuwa ya sauti ambayo ilikuwa
ikisikika kwa wachawi wale. Kwakuwa wao
walikuwa hawajui lakini yule alikuwa ni malaika
mwema wa bwana.
Muda huo tayari padre mchafu, ambaye aliyatumia
mamlaka ya bwana kwa ubaya alikuwa kaisha kufa.
Japo Sauti ile walikuwa wakiiogopa lakini wachawi
walijikaza na kusogea alipokuwa Sister Murcia na
mtoto wake ili kumshika. Mpaka muda huo kila
aliyekuwepo pale aliamini kabisa kuwa uchawi si
chochote mbele za mungu. Baada ya kuona
wachawi wale wakimsogelea sister Murcia
alisimama ilikuwa kama vile anajua nini kinaenda
kutokea kwa muda huo. Bila fujo wachawi wale
walijikuta wanapanga mstari wao na kuanza mmoja
mmoja akimsogelea Sister Murcia pale alipokuwa
na kumshika mtoto yule mkono, kisha
wanainamisha vichwa vyao chini kuonesha ishara ya
Eshima na kuondoka. Uwezi amini mpenzi msomaji
kila watu walivyokuwa wanaongezeka kumsogelea,
mtoto yule alikuwa akitabasamu, kisha akaanza
kuwapa mkono yeye mwenyewe hata alikuwa angoji
kuguswa. Hayo ndiyo yalikuwa maajabu ya siku hio
mpaka usiku kucha.
******
Kanisani watu, walipoamka walifanya kama kawaida
yao, wenye kuingia kanisani na kusali walifanya
hivyo. Wengine walikuwa wanaendelea na Shughuri
zingine. Lakini nao pia walianza kushikwa na
wasiwasi baada ya kutomuona Sister Murcia. Hio
ilikuwa ni mida kama ya saa mbili asubuhi.
"Jamani sister murcia mbona haonekani au
kachukuliwa na wachawi?"
Kijana mmoja aliuliza.
Bado wakiwa wanajiuliza walishangaa kuona kundi
kubwa la watu kuzidi hata wale ambao tayari,
walikuwa washabadilika na kumfuata bwana mungu
wao.
Kwakuwa kundi lile la watu lilikuwa limevaa mavazi
ya kichawi chawi. Moja kwa moja watu kanisani
wakajua wanavamiwa, waliokuwepo wote
wakakimbilia mapanga yao tayari kwa kupambana.
Bila kutegemea watu wote kanisani walistaajabu
baada ya kumuona Sister murcia kabebwa juu
mfano wa watu wa pwani kwa machifu wao. Hali
hio iliwafanya kujua kabisa kuwa mkombozi
waliyekuwa wakimngoja kaisha zaliwa. Nao pia
waliamua kwenda kuwapokea watu wale.
Toka muda huo kijiji kizima cha zima moto
kilizizima kwa kufurika watu katika viwanja vya
kanisa lao, lengo kumtazama mwana aliye zaliwa.
Huo ndio ulikuwa ukombozi wa watu wale. Baada
ya mwezi mmoja tangu Kujifungua Sister murcia
naye alifariki na kumwacha mtoto wake ambaye
bado alikuwa mchanga katika mikono salama ya
watu wa kanisani. Mtoto yule alilelewa lakini
alikuwa wa ajabu. Kiujumla alikuwa mtenda miujiza,
wagonjwa waliokuwa na imani ya bwana mungu
wao, waliweza kupona kwa kushika mikono yake.
Toka hapo kijiji cha shimo la moto kiligeuka kikawa
shamba la Mungu.
Mwisho.

Safi sana... Simulizi nzuri...

Chapter Closed...


Cc: mahondaw
 
Habari mambo naitwa Mr Equator Nimeandika ujumbe huu kuku omba swala moja tu!
Mimi nimetengeza website ya ku share story ambayo ni http://www.equatorstory.com/
Je umekuwa ukipata tabu kupost story zako hapa?
Hili ndo suluhisho lako.
Mimi nataka nkupe nafasi ya kuwa mmoja wapo wa kwanza kutumia hii website
unda account yako na uweze kupost story yako mpya.
 
Back
Top Bottom