Shunie
JF-Expert Member
- Aug 14, 2016
- 153,008
- 453,977
- Thread starter
- #41
Sehemu ya 09
“Mohammed, sahau kuhusu taa za gari...mbona nishawasamehe tu,” alisema Razak huku akionekana kutokujali sana.
“Unahitaji nini?” aliuliza Aisha.
“Nakuhitaji wewe...”
“Kwa hiyo unampenda?” alidakia Mohammed kwa kuuliza swali lililomfanya Razak kuachia zaidi tabasamu.
“Twendeni sehemu kwanza...” alisema Razak.
“Wapi?” aliuliza Aisha.
“Sehemu fulani!”
“Hatuwezi kwenda mpaka utuambie wapi!”
“Aisha...mimi si mtu mbaya kwenu, niamini, naomba mnichukulie kama mtu wa kawaida,” alisema Razak kwa sauti ya kubembeleza iliyoonyesha kumaanisha alichokuwa akikisema.
“Unataka nini kwetu?”
“Niwe karibu nanyi...nimeguswa na maisha mnayoishi...”
“Kwa hiyo?”
“Nataka kuwasaidia...”
Wote watatu wakaangaliana, hawakuamini maneno aliyokuwa akizungumza Razak, kwao walimuona muongo ambaye alikuwa na jambo lake pembeni ambalo hakutaka kuliweka wazi.
Hawakukubaliana na suala hilo, walikuwa mitaani kwa miaka mingi, leo hii mtu aje na kuwaambia kwamba alitaka kuwasaidia, kukubaliana naye lilikuwa jambo gumu.
“Hapana...” alisema Aisha.
Razak alikuwa kwenye wakati mgumu, hakuweza kuaminika, ilimbidi atumie nguvu za ziada kuwaambia watu hao kwamba aliposema kuwa anataka kuwasaidia, alikuwa akimaanisha kufanya hivyo.
Je nini kitaendelea...