Simulizi:Penzi lisilo Na Mwisho


Shunie

Shunie

JF-Expert Member
Joined
Aug 14, 2016
Messages
110,121
Points
2,000
Shunie

Shunie

JF-Expert Member
Joined Aug 14, 2016
110,121 2,000
Sehemu ya 18

“Kuna nini?”
“Hakuna kitu mpenzi...”
“Ila umebadilika ghafla, hauna furaha, niambie tatizo nini,” aliuliza Aisha.
Razak hakutaka kujibu swali hilo, alichokifanya ni kumzugisha kwa stori nyingine huku akiulazimisha uchangamfu, baada ya hapo, akamwambia ajiandae kwani ilikuwa ni lazima ampeleke kwa wazazi wake kwa ajili ya kumtambulisha.

Baada ya kujiandaa, hawakutaka kupoteza muda, wakaingia ndani ya gari na safari ya kuelekea Masaki kuanza. Njiani, Razak alijitahidi kuwa muongeaji, hakutaka Aisha afahamu kitu chochote au kuona mabadiliko yoyote kwake, waliongea na kucheka sana na baada ya dakika kadhaa wakawa wamekwishafika nyumbani, wakateremka na kuelekea ndani.

Aliwakuta wazazi wake wote, alikaribishwa, wazazi hao walibaki na maswali mengi kuhusu msichana aliyeingia na Razak alikuwa nani na kwa nini alikuja naye nyumbani hapo?
Kwa kumwangalia, alikuwa msichana mrembo, aliyevutia lakini bado kwa mbali ilikuwa ni rahisi kujua kwamba hata mavazi aliyokuwa amevaa ilikuwa ni kama kulazimishwa.

Wazazi hao hawakutaka kuzungumza kitu, walijua kwamba iwe isiwe huyo msichana aliyeletwa kwao alikuwa mpenzi wa Razak ila swali pekee lililowajia vichwani mwao ni msichana Sabrina tu, alikuwa wapi? Na kwa nini Razak aliamua kuja na msichana mwingine?

Walikula na kunywa, walifurahia maisha, kwa Razak, siku hiyo hakutaka kumtambulisha Aisha kama mpenzi wake, aliwaambia kwamba alikuwa rafiki yake kipenzi aliyekuwa akiishi Magomeni, wazazi wake walifurahia, hawakuonyesha chuki yoyote ile.

Ilipofika saa kumi na moja jioni, wakaaga tayari kwa kuondoka kwani Razak aliwaambia wazi kwamba aliamua kuishi Kijitonyama kwa kuwa kulikuwa na mambo mengi binafsi alitaka kuyafanya, wazazi hawakuhoji, walikubaliana naye. Aisha alipoelekea kwenye gari tu, wakamvuta Razak.

“Razak, hebu tuambie ukweli, huyu Aisha ni nani kwako?” aliuliza baba yake.
“Ni mchumba wangu...”

“Tangu lini?” aliingilia mama yake.
“Kama wiki hivi mama...” alidanganya.
“Na vipi kuhusu Sabrina?” alidakia baba yake.

“Ni stori ndefu....”
“Ipi? Haisimuliki?”
“Inasimulika, ila inaumiza...”
“Hebu njoo huku.”

Huko, Razak alianza kuwahadithia wazazi wake kile kilichotokea, aliwaambia kila kitu tangu mapenzi yao yalipoanza kuyumba, alipokuwa akimbeleza msichana huyo kwa kumtumia meseji na hata kumpigia simu lakini msichana huyo hakuonyesha mabadiliko yoyote yale.

Hakuishia hapo, kwa kuwa alikuwa na meseji, akawapa wazisome, wote walihuzunika, hawakuamini kama msichana Sabrina ndiye yule aliyemfanyia vile kijana wao, wakatokea kumchukia sana Sabrina ila hiyo haikuwa sababu ya kumwamini sana Razak, walichokifanya ni kumpigia simu msichana huyo.

Kile walichoambiwa ndicho kilichotokea, Sabrina alibadilika, aliwajibu kiburi na mwisho kabisa kumalizia kwamba hakutaka kuwa na kijana wao kwani hakuwa chaguo lake tena.

Je nini kitaendelea......
 
Shunie

Shunie

JF-Expert Member
Joined
Aug 14, 2016
Messages
110,121
Points
2,000
Shunie

Shunie

JF-Expert Member
Joined Aug 14, 2016
110,121 2,000
Sehemu ya 19

Walisikitika lakini hawakuwa na jinsi, walitamani kumuona kijana wao akiwa na furaha hivyo kile alichoamua kuwa na msichana Aisha, kwao waliona sahihi kabisa.

“Ni lazima umuoe huyu Aisha, tena haraka iwezekanavyo...huyu Sabrina si binadamu, ni mnyama...” alisema baba yake huku akionekana kuwa na hasira mno.

“Nashukuru kwa ruhusa yenu, nitafanya hivyo mwaka huuhuu...” alisema Razak huku akiachia tabasamu pana, baada ya hapo, huyo akaondoka zake na Aisha huku moyo wake ukiwa na furaha mno, hata Aisha aliligundua hilo.

*****
“Tatizo nini Sabrina?” ilisikika sauti ikiuliza.
“Nimekuja kwako...”
“Kufanya nini tena?”
“Kulala...nyumbani wamenifukuza kwa ajili yako...”
“Umefukuzwa nyumbani kwa ajili yangu?”
“Ndiyo!”

Sabrina aliamua kwenda nyumbani kwa kina Sharifu, aliamua kukimbilia huko kwani ndipo kulipokuwa kimbilio lake. Alichanganyikiwa, kitendo cha kukataliwa kuwa na mwanaume huyo kilimuudhi na kitu pekee alichoona kustahili kukifanya ni kukimbia na kuelekea nyumbani kwa mwanaume huyo.

Moyo wake ulichanganyikiwa, alikuwa kama kichaa, wakati huo, hakuingia ndani bali alisimama getini na alikuwa akizungumza na Sharifu kwa kutumia kimashine kidogo kilichopachikwa ukutani ambapo kwa huko ndani kulikuwa na simu maalumu kwa ajili ya kuzungumza na mtu aliyekuwa ndani.

“Subiri nakuja...” alisikika Sharifu.
Sabrina alibaki akiwa amesimama nje ya geti, ilikuwa usiku sana na kila sehemu kulikuwa na ukimya mkubwa, ni sauti za mbwa ndizo zilizokuwa zikisikika kwa mbali.

Alibaki akitetemeka pale aliposimama, baridi lilimpiga ila akawa hana jinsi, ilikuwa ni lazima asubiri ili afunguliwe mlango. Wala hazikupita dakika nyingi, Sharifu akatokea mahali hapo, akalifungua geti na Sabrina kuingia ndani.
“Karibu sana...” alisema Sharifu.
“Nashukuru...”

Wakatoka mahali hapo na kwenda ndani ya nyumba hiyo. Sharifu alionekana kutokujiamini, alionekana kuwa na wasiwasi mwingi huku akiwa mtu wa mawazo mengi, macho yake hayakutulia sehemu moja, aliyapeleka huku na kule kama mtu aliyekuwa akikitafuta kitu fulani, ila alipotazamwa na Sabrina, uso wake akauwekea tabasamu pana.

Wakaingia mpaka sebuleni ambapo wakapitiliza mpaka chumbani. Sabrina alionekana kushtuka hasa macho yake yalipotua kitandani. Kilikuwa shaghalabaghala, huku kwa mbali chumba kukinukia manukato ya kike.

“Mmh!” alijikuta akiguna.
“Nini tena?”
“Mbona nasikia harufu manukato ya kike?”
“Wapi? Humu?”
“Ndiyo!”

Je nini kitaendelea.....
 
Shunie

Shunie

JF-Expert Member
Joined
Aug 14, 2016
Messages
110,121
Points
2,000
Shunie

Shunie

JF-Expert Member
Joined Aug 14, 2016
110,121 2,000
Sehemu ya 20

“Mmh! Manukato ya kike? Mbona ni yangu yanaitwa The Prince...”
“Hapana! Ni manukato ya kike, yanaitwa Cleopatra...” alisema Sabrina huku akionekana kuwa na wasiwasi mno.

“Hapana! Utakuwa umechanganya! Hebu niambie, mbona usikuusiku, imekuwaje huko?” aliuliza Sharifu huku akiwa ameingizia ishu nyingine kabisa na kuipotezea ile ya manukato.

“Nimekimbia nyumbani kwa ajili yako,” alijibu Sabrina.
“Kisa?”
“Wazazi hawakufurahia mimi kuwa nawe...”

“Haiwezekani! Kwa nini?”
“Sijui, ila hawakufurahi kabisa...nimeona bora niondoke...” alisema Sabrina.
Kwa kumwangalia tu alionyesha kuchanganyikiwa, kila alipomwangalia Sharifu, alimpenda zaidi ya alivyokuwa akimpenda hata kipindi cha nyuma.

Mwanaume huyo, kwake alikuwa kila kitu, hakutaka kumkumbuka Razak, aliuona moyo wake ukiwa na chuki juu ya mwanaume wake huyo aliyepita, mtu ambaye aliona kupanga naye maisha alikuwa huyu aliyesimama mbele yake, Sharifu.

Kwa Razak, bado alionekana kuwa na wasiwasi, hakuwa mtu huru kama ilivyokuwa kipindi wanapokuwa pamoja, kila wakati alikuwa mtu wa kuangalia huku na kule hali iliyomtia wasiwasi hata Sabrina mwenyewe.

Akahisi kulikuwa na kitu kilichokuwa kikiendelea na kitu pekee kilichokuja moja kwa moja kichwani ni kwamba mpenzi wake huyo aliingiza mwanamke ndani ya chumba hicho.
“Mbona upo hivyo?” aliuliza Sabrina.
“Nipoje?”

“Hujiamini, unaonekana una wasiwasi...una nini?”
“Hakuna kitu!”
“Umeingiza mwanamke?”
“Nani? Mimi? Hapana! Niingize mwanamke wa nini?” aliuliza Sharifu huku akijifanya kushtuka.
“Mmh! Sawa! Naomba nikaoge kwanza...”
“Hakuna tatizo...”

Sabrina hakuwa na amani, kitu pekee alichohisi ni kwamba mpenzi wake huyo alikuwa ameingiza mwanamke ndani ya nyumba. Alitaka kujua ukweli na ndiyo maana akamwambia kwamba alitaka kwenda bafuni kuoga lakini ukweli ni kwamba alitaka kufahamu kilichokuwa kikiendelea.

Alipokwenda bafuni, hakujimwagia maji bali alifungua bomba na kusimama pembeni, hapo ndipo aliposikia mlango wa chumbani ukifunguliwa, kwa harakaharaka akatoka, Sharifu hakuwepo, alikuwa ametoka.

Hakutaka kubaki chumbani, naye akatoka na kuanza kwenda sebuleni ili kuona nini kiliendelea, alipofika huko, napo hakukuta mtu. Hakukata tamaa, alichokijua ni kwamba lazima Sharifu aliingiza mwanamke ndani ya nyumba hiyo, hivyo akaenda nyuma ya nyumba hiyo ambapo huko akaanza kusikia minong’ono.
“Nusrat...nenda kwanza....” aliisikia sauti ya Sharifu.

“Ila nani ameingia?”
“Mama...”
“Usiku wote huu mpenzi...”
“Wewe nenda, nitakutafuta kesho...chukua hii hela, itakusaidia katika usafiri....” alisikika Sharifu.

Sabrina pale alipokuwa, alihisi miguu yake ikikosa nguvu, mapigo ya moyo yakaanza kumdunda kwa nguvu, hakuamini kile alichokisikia, yaani mwanaume aliyempenda, aliyempa moyo wake, leo hii aliingiza mwanamke mwingine ndani ya nyumba.

Je nini kitaendelea.....
 
Shunie

Shunie

JF-Expert Member
Joined
Aug 14, 2016
Messages
110,121
Points
2,000
Shunie

Shunie

JF-Expert Member
Joined Aug 14, 2016
110,121 2,000
Sehemu ya 21

Hapo ndipo akapata jibu sababu iliyomfanya Sharifu kuchelewa kuufungua mlango alipokuwa akipiga hodi.

Akahisi moyo wake ukiwaka kwa hasira, hakuweza kuvumilia pale ukutani alipojificha, kwa kasi ya ajabu akachomoka, akawafuata kule walipokuwa, hawakuwa wamemuona, ile ghafla, msichana Nusrat akashtukia akikabwa roba kali na kuanza kushambuliwa kwa ngumi mpaka kuanguka chini.

“Sabrinaaa....” alijikuta akiita Sharifu, hata kumtoa Sabrina alishindwa kwani alikuwa na nguvu mno, alimkalia Nusrat juu huku akimpiga mfululizo.
*****
Mapenzi yakawa motomoto, kila walipokuwa, walikuwa pamoja, hakukuwa na kitu ambacho kingeweza kuwatenganisha kutoka katika penzi zito walilokuwa nalo zaidi ya kifo tu.

Kila mmoja alichanganyikiwa, kwa Aisha, hakuamini kama kweli maisha yote aliyoishi kipindi cha nyuma yalibaki na kuwa historia, yaani asingeweza kurudi tena mitaani, kuombaomba na kutafuta mabaki ya chakula katika hoteli mbalimbali zilizokuwa Kariakoo.

Maisha yake yalikuwa mapya kabisa, alitakiwa kusahau kila kitu, alitakiwa kujua kwamba kwa kipindi hicho yeye alikuwa mpenzi wa mtoto wa bilionea, hivyo shida zote alizokuwa nazo kipindi cha nyuma alitakiwa kuzisahau.

Aisha hakutaka kuwaacha mapacha ambao ndiyo walionekana kuwa sababu ya yeye kukutana na Razak, alihakikisha nao wanapata maisha bora kama aliyokuwa akipata, hilo, kwa Razak wala halikuwa tatizo, kwa sababu umri wao haukuwa mkubwa sana, akawahamisha katika nyumba hiyo na kuwapeleka katika nyumba nyingine nzuri iliyokuwa Sinza, walitakiwa kuishi huko, wakawekewa mfanyakazi na kupewa kila kitu walichokihitaji.

Yote hayo aliyafanya kwa kuwa alitaka kumuona mpenzi wake akiwa na furaha tele, hakutaka ayakumbuke maisha aliyopitia kipindi cha nyuma, kila kitu kilichopita, alitaka kiwe historia ambayo isingeweza kujirudia tena maishani mwake.

“Unapenda nikufanyie nini katika maisha yako?” aliuliza Razak huku akiwa amemlaza Aisha miguuni mwake.
“Ninataka unioe...” alijibu Aisha huku akiachia tabasamu pana.
“Hilo tu?”

“Yapo mengi, ila hilo ndilo la kwanza!”
“Usijali mpenzi, nitahakikisha nakuoa haraka iwezekanavyo...” alisema Razak huku akiachia tabasamu pana.

Razak alikuwa na fedha, hilo kwake halikuwa tatizo hata kidogo, mara kwa mara walikuwa wakitoka na kuelekea sehemu mbalimbali kula maisha, walikwenda Zanzibar, katika Visiwa vya Komoro na Shelisheli, kote huko alitaka kumuonyesha Aisha jinsi maisha ya kuwa na fedha yalivyokuwa.

Kwa jinsi walivyopendana, kusikilizana na kujaliana, hakukuwa na aliyefikiri kwamba wakati mwingine kwenye mapenzi kuna kugombana na kufarakana, kwao, mapenzi yalikuwa motomoto.
Razak hakutaka kumkumbuka Sabrina, alitaka kumfuta kabisa kwenye akili yake.

Moyoni mwake alihisi kwamba kuna kitu kingeweza kutokea, hivyo alichokifanya ni kujihami mapema kabisa.
Akamwambia Aisha kuhusu msichana huyo, jinsi alivyokuwa naye na mapenzi kuja kuyumba na hatimae kuachana kabisa.

Kwa Aisha, hilo halikuwa tatizo, alifurahi kupewa taarifa na hivyo akajiandaa kwa lolote ambalo lingeweza kutokea.

Je nini kitaendelea....
 
Shunie

Shunie

JF-Expert Member
Joined
Aug 14, 2016
Messages
110,121
Points
2,000
Shunie

Shunie

JF-Expert Member
Joined Aug 14, 2016
110,121 2,000
Sehemu ya 22

Siku zikakatika, alichokifanya Razak ni kuanza mikakati ya kufunga ndoa na Aisha. Hakutaka kuchelewa, alitamani kumfanya mpenzi wake kuwa na furaha zaidi ya mwanamke yeyote chini ya jua.

Hakutaka kuchelewa, kwa kuwa yeye mwenyewe alianza kusimamia biashara mbalimbali za baba yake, akamnunulia Aisha gari la kifahari kwa ajili ya kufanyia mizunguko yake ya huku na kule.

Yule msichana mchafumchafu, aliyekuwa akiomba mitaani, hakuwa huyu wa kipindi hiki, huyu alikuwa Aisha mwingine kabisa, aliyependwa na kupendeka, aliyepanda thamani ambaye kila alipokanyaga, alipewa heshima na watu wengine.
“Hili ndinga kakununulia?” aliuliza Mohammed huku akionekana kulishangaa gari la Aisha.

“Ndiyo! Ni zuri au baya?”
“Ni zuri sana, aiseee...una bahati sana Aisha...”
“Bahati ya nini?”

“Kuwa na huyu Razak, anakupenda kweli...sasa itakuwaje? Mwambie basi na sisi atufanyie mchongo tupate ndinga...” alisema Mohammed huku macho yake yakiliangalia gari lile.

“Hakuna tatizo...kwanza mnahitaji nini katika maisha yenu?” aliuliza Aisha.
“Kwanza tuwe na hela za kula bata tu,” alijibu Mohammed.

“Hapana! Bata za nini kwanza? Cha kwanza tufanye biashara...” aliingilia Ahmed ambaye alikuwa kimya kwa kipindi kirefu.

“Hapo umeongea Ahmed....”
“Cha kwanza ni biashara, fedha zitapatikana tu, bata haziishi Moody, ni lazima tufanye kitu,” alisema Ahmed.

Hakukuwa na kipingamizi, kwa sababu Ahmed alishauri kwamba ni lazima wapewe hela ya kufanya biashara, hilo halikuwa tatizo, kesho yake tu Aisha akarudi mahali hapo huku akiwa na zaidi ya milioni kumi na kuwakabidhi, ilikuwa ni lazima wafanye biashara.

Biashara ambayo waliichagua ni kununua nafaka mikoani na kuyapeleka jijini Dar es Salaam. Hiyo ilionekana kuwa biashara nzuri ambayo iliwafanya kutokutulia jijini Dar.

Mara kwa mara walikuwa watu wa kusafiri, walikuwa vijana wadogo lakini maisha waliyoishi hapo kabla yalizifanya hata akili zao kukomaa na kufanya mambo kama watu wazima.

Huku Dar, bado mipango ilikuwa ikiendelea, watu wakapewa taarifa kwamba miezi miwili ijayo kungekuwa na harusi kubwa kati ya mtoto wa bilionea, Razak na msichana mrembo, Aisha.

Kutokana na baba yake Razak kujulikana sana na wafanyabiashara kutoka sehemu mbalimbali katika nchi za Kiarabu, watu wengi wakaahidi kuhudhuria harusi hiyo ambayo ilitarajiwa kutikisa kuliko harusi zote zilizowahi kutoka nchini Tanzania.
“Hivi kweli unanioa?” aliuliza Aisha huku akionekana kutokuamini.

“Ninakuoa mpenzi...unakwenda kuwa mke wangu...” alisema Razak huku akitoa tabasamu pana lililokuwa na matumaini kwamba iwe isiwe ilikuwa ni lazima harusi ifungwe.
****

Ulikuwa usiku sana, sehemu kubwa ilikuwa kimya lakini katika nyumba moja tu ndiyo kelele kubwa zilikuwa zikisikika, wanawake wawili walikuwa wakipigana huku mwanaume mmoja akiwa pembeni, alijaribu kuwagombelezea lakini hawakuachiana.

Sabrina alionekana kuwa na hasira kali, hakutaka kukubali hata mara moja kuona mwanaume wake aliyempenda akichukuliwa na mwanamke mwingine, hasira zilimpanda na kila alivyomwangalia Nusrat, alijikuta akiendelea kumshambulia pale chini.

Japokuwa Nusrat ndiye aliyefumaniwa na kuleta upole mwingi, alishindwa kuvumilia, hakutaka kuona akishambuliwa pasipo kurudisha mapigo, naye akaanza kumshambulia Sabrina.

Ulikuwa ugomvi mkubwa, uliosababisha kelele nyingi, hakukuwa na aliyekuwa radhi kumuachia mwenzake na hata Sharifu aliyekuwa pembeni alishindwa kabisa kuwagombelezea.
“Hebu achianeni kwanza....” alisema Sharifu huku akijaribu kuwatenganisha.

“Simuachiiii...yeye si anajifanya bingwa wa kuchukua wanaume za watu, simuachiii...” alisema Sabrina huku akiendelea kumng’ang’ania Nusrat.
“Wewe Sabrina hebu muachie mwenzako...nitakupiga...”

“Unipige mimi...wewe wa kunipiga mimi...kwa nini usimpige malaya wako?” aliuliza Sabrina, hasira zilimpanda kichwani, hakutaka kusikia lolote lile.

Je nini kitaendelea....
 
Shunie

Shunie

JF-Expert Member
Joined
Aug 14, 2016
Messages
110,121
Points
2,000
Shunie

Shunie

JF-Expert Member
Joined Aug 14, 2016
110,121 2,000
Sehemu ya 23

“Unipige mimi...wewe wa kunipiga mimi...kwa nini usimpige malaya wako?” aliuliza Sabrina, hasira zilimpanda kichwani, hakutaka kusikia lolote lile.
Alichokifanya Sharifu ni kutumia nguvu kumvuta Sabrina na kumuweka pembeni kisha kumsogelea Nusrat na kuanza kumpeleka nje ya nyumba hiyo.

Sabrina hakuwa na cha kufanya, alibaki akiwa amesimama, machozi yalilowanisha mashavu yake, hakuamini kile alichokiona, yaani mwanaume aliyekuwa akimpenda, aliyempa moyo wake, leo hii aliamua kuingiza mwanamke mwingine.

“Sharifu...kwa nini unanifanyia hivi?” aliuliza Sabrina huku akilia, Sharifu hakujibu kitu, alipohakikisha Nusrat ameingia ndani ya gari lake na kuondoka, akaingia ndani huku akimwacha Sabrina pale nje.

Moyo wake ulikuwa kwenye maumivu makali, hakuamini kile alichokiona, mwanaume yuleyule ambaye rafiki yake, Minah alimfuata na kumwambia kwamba alikuwa akimpenda na ndiye mwanaume huyohuyo ambaye leo hii aliamua kumuingiza mwanamke mwingine, alipouliza, hakujibiwa zaidi ya kuingia ndani.

Hakutaka kubaki pale nje, alihisi moyo wake ukiwa kwenye hasira kali, hakutaka kukubali kabisa, alichokifanya ni kuingia ndani, moja kwa moja akamfuata Sharifu aliyekuwa chumbani na kuanza kumuuliza maswali kwa sauti kali.

“Sikiliza Sabrina, sipendi kelele kabisa, tena unyamaze....nitakubabua...” alisema Sharifu huku akionekana kumaanisha alichokisema.

“Sharifu...kwa nini unanifanyia hivi?”
“Nimekufanyaje? Yaani unamvamia mtu na kugombana naye, humjui yeye ni nani, hujauliza, unaanza kumpiga, hivi unajua yule ni nani?” aliuliza Sharifu huku akionekana kukasirka.
“Unanifanyia hivi Sharifu...kweli unanifanyia hivi?”

“Unajua yule ni nani? Unajifanya una hasira sana, unajifanya una wivu sana, unadhani wewe ndiye mwenye hasira peke yako humu duniani? Unafikiri wewe ndiye mwenye wivu kuliko watu wote humu duniani?” aliuliza Sharifu huku akiendelea kumkaripia Sabrina.

Kilichofuata ni Sabrina kuanza kuongea maneno yake huku akimlaumu sana Sharifu lakini mwanaume huyo hakutaka kuzungumza tena, alibaki kimya huku akigeukia upande wa pili wa kitanda chake.

Sabrina alijuta, mwanaume ambaye alijitolea moyo wake wote kumpenda ndiye aliyeamua kumuumiza kwa kumuingiza mwanamke ndani ya chumba chake.

Hakulala usiku mzima, alibaki akilia pembeni ya kitanda cha Sharifu. Mwanaume huyo alipoamka asubuhi, akabaki akimwangalia Sabrina, hakumuonea huruma, kwake, alimuona mwanamke mpumbavu ambaye alifanya jambo la kipumbavu kumvamia msichana na kumshambulia pasipo kuhoji alikuwa nani.

“Naomba unisamehe mpenzi...” alianza kuomba msamaha Sabrina.
“Kwa lipi?”
“Kumpiga mtu pasipo kujua alikuwa nani...”

“Wewe si umejifanya mjanja...”
“Hapanna! Sikujua mpenzi, naomba unisamehe, ni hasira na wivu tu ndiyo vimeniponza....” alisema Sabrina.

Hicho ndicho alichokuwa akikitaka Sharifu, alijua kwamba yeye ndiye alikuwa na makosa lakini kamwe hakutaka kuonyesha kwamba kweli alikosea, hakutaka kujishusha kwa kuona kwamba msichana huyo alikuwa akimpenda, hivyo yeye ndiye aliyetakiwa kumuomba msamaha.

Sabrina hakuwa na jinsi, hakutaka kumuacha Sharifu, alimpenda hivyo hata kumuomba msamaha ilikuwa ni sehemu ya mapenzi mazito aliyokuwa nayo kwake.
“Usirudie tena, umesikia?” alisema Sharifu huku akimwangalia Sabrina kidharau.

“Nimesikia, sitorudia mpenzi...” alisema Sabrina huku akitokwa na machozi tu, moyo wake ulikuwe kwenye maumivu makali ambayo hakuhisi kama kuna siku angeweza kuumia namna hiyo.
*****
Je nini kitaendelea.....
 
Shunie

Shunie

JF-Expert Member
Joined
Aug 14, 2016
Messages
110,121
Points
2,000
Shunie

Shunie

JF-Expert Member
Joined Aug 14, 2016
110,121 2,000
Sehemu ya 24

Shamsiaa Othman: Huyu alikuwa msichana mrembo, kwa kumwangalia, ungehisi kwamba umekutana na malaika.

Alivutia machoni na hata umbo lake lilikuwa zuri, kila mwanaume aliyemwangalia, alitokea kumpenda mno.
Nilimpa moyo wangu wote, anipende kama nilivyompenda, pamoja na mapenzi yote niliyompa, akaondoka Dubai na kuniachia upweke.

Alikwenda nchini Oman, aliporudi, akaniambia kwamba amepata mwanaume mwingine, mzuri zaidi yangu na hivyo angeolewa na huyo.

Niliumia sana, kuanzia siku hiyo, nikajiapiza kwamba nisingependa tena, yaani ningekuwa natembea na wanawake na kuwaacha kwenye maumivu makali kama alivyonifanyia Shamsiaa.

Khadija Rahman: Baada ya Shamsiaa, nikaona ni bora nitafute kimbilio hukohuko Dubai. Moyo wangu ukaangukia kwa msichana huyu mrembo mwenye asili ya Yemen.

Kwa kumwangalia, alikuwa mrembo lakini kitendo cha mimi kwenda kwake, hakikuwa mapenzi, bali nilitaka nilipe kisasi kile nilichofanyiwa na mwanamke mwenzao.

Kweli akanipenda sana, alinipa nilichotaka lakini sikutaka kumpa mapenzi kwa asilimia mia moja, baada ya kutembea naye ndani ya mwezi mmoja, nikaachana naye.

Je nini kitaendelea.....
 
Smart911

Smart911

JF-Expert Member
Joined
Jan 3, 2014
Messages
23,821
Points
2,000
Smart911

Smart911

JF-Expert Member
Joined Jan 3, 2014
23,821 2,000
Sabrina hana akili, mkataa pema pabaya panamuita...

Aisha mwenzako huyooo... hujafanya hujaumbika...


Cc: mahondaw
 
Shunie

Shunie

JF-Expert Member
Joined
Aug 14, 2016
Messages
110,121
Points
2,000
Shunie

Shunie

JF-Expert Member
Joined Aug 14, 2016
110,121 2,000
Sehemu ya 25

Catherine Gozbert: Huyu alikuwa Mkristo safi. Mara ya kwanza kukutana naye alikuwa akitoka kanisani. Alikuwa msichana mrembo, mkononi alishika Biblia, nikaamua kumfuata na kumuomba nimpe lifti.

Alikuwa na usafiri wake, ilikuwa vigumu sana lakini nikahitaji nimsindikize, kweli akanikubalia, gari lake likawa mbele, langu nyuma. Alipofika kwao, akaliingiza gari kisha mwenyewe kuja nje.
Nilizungumza naye, alionekana kuwa mchangamfu.

Nilikuwa nikimuogopa ila baada ya kuona kwamba alikuwa mtu wa kawaida, nikazoeana naye, akanipenda, nikampenda ila kama kawaida yangu, sikuwa na moyo wa kupenda, moyo huo aliondoka nao Shamsia, hivyo nikamuacha, alilia na kulia, ila sikuweza kurudi kwake.

Farha Majeed: Nilisoma naye kitambo, baada ya kupotezana naye kwa kipindi kirefu, hatimaye nikaonana naye na ghafla tukatokea kuwa wapenzi.

Nilidumu naye kwa kipindi cha mwezi mmoja kama kawaida yangu, baada ya hapo, nikamuacha katika maumivu makali kwa kuamini kwamba ningempenda mpaka ndoa.

Sikuwa na historia ya kupenda na kufa kwa msichana, hivyo nilivyomtumia, nikamtupa kama ilivyokuwa kwa wengine. Akalia, akajuta kuwa na mimi ila sikutaka kusikia. Baada ya hapo, nikaamua kuelekea nchini Tanzania.

Je nini kitaendelea.....
 
Shunie

Shunie

JF-Expert Member
Joined
Aug 14, 2016
Messages
110,121
Points
2,000
Shunie

Shunie

JF-Expert Member
Joined Aug 14, 2016
110,121 2,000
Sehemu ya 26

Nusrat Twaha: Tulikutana katika Ukumbi wa Maisha Basement, akatokea kunipenda sana lakini hakujua ni kwa namna gani angenipata, hivyo akamtumia rafiki yangu wa kike, Minah ambaye naye nilimkosakosa.

Minah akanifuata na kuniambia kwamba nilikuwa napendwa, nikakubali, nikawa na Nusrat, tukafanya mengi, akapagawa nami ila ndiyo hivyo, muda wangu wa mwezi mmoja umetimia, hivyo nitammwaga kama wengine.

Sabrina Seif: Nilipomuona kwa mara ya kwanza, nilimpenda kidogo, nilimtaka niwe naye katika miezi yangu miwili ya kuwa hapa Tanzania kabla sijarudi Dubai. Sikujua ningempata vipi hivyo nikamtumia Minah, akanirekebishia na hivyo nipo naye.

Kama kumpenda, nampenda ila kwa asilimia tano tu. Nimemchezea kama wengine, nimemfanya ninachotaka kumfanya na sasa hivi nimemchoka, kama ilivyokuwa kwa wasichana wengine, hata naye huyu Sabrina nitamwaga japokuwa anapenda sana ndoa, kila nikikaa naye, anazungumzia ndoa tu.

Kashanifumania na Nusrat, nimemzugazuga tu, hivyo nammwaga kama kawaida kisha kurudi zangu Dubai. Kwa kifupi, siwezi kupenda, yule Shamsia ndiye aliyeharibu kila kitu. Baada ya kummwaga huyu, mwingine atakuja tu. Nafanya haya yote kama kisasi cha kuumizwa zamani.

Je nini kitaendelea.....
 

Forum statistics

Threads 1,284,196
Members 493,978
Posts 30,816,893
Top