SIMULIZI: Nilipanga Nyumba Moja na Majini

SIMULIZI: Nilipanga Nyumba Moja na Majini

Nilipanga Nyumba Moja na Majini -MWISHO

"Lini umeniambia?"
"Wewe sijawahi kukupigia simu kukwambia? Tena ukasema kama vipi nihame lakini sitarudishiwa kodi ya nyumba na mimi nikakujibu niko tayari kwa hilo…"
"Sasa wewe ulikuwa ukiteswa kwa lipi, weka ushahidi hapa kwamba ulikuwa ukiteseka sana."
"Sina haja, mimi ndiyo najua."

Wakati tukijibizana hivyo, wale waombaji walikuja juu kwa kuomba. Walipaza sauti sana wakisema moto uteketeze kila hila na jambo lolote ambalo linakwenda kinyume na mimi ndani ya nyumba ile.

Ghafla, nilimwona yule dalali akianza kuyumba kama mlenvi, alikwenda kulia, kushoto, akasimama, akawa

kama ananijia mimi, nikamkwepa, akaenda kushoto na kuanguka puu!
Kwangu ilikuwa ni furaha kwani nilipata picha kwamba, yule dalali alikuwa anahusika moja kwa moja na matukio yote ya ajabu mle ndani. Niliwaita wale watu wanaofanya maombi na kuwataka washuhudie ambapo walipomwangalia dalali waliongeza mkazo wa maombi yao.

Mwisho, dalali aliamka akiwa kama hana ufahamu, alikalishwa chini na kuhojiwa ambapo alisema mambo ya ajabu sana. Alisema mwanaume aliyekuwa akiishi ndani ya vyumba vile ni yeye na mkewe, akasema mkewe ni jini kwa asilimia mia moja ila yeye si jini bali mkewe alimfanya awe na uwezo wa kutoonekana wala kujulikana na mtu.

Alipoulizwa kama alikuwa anapata faida yoyote kwa kitendo cha kugeuka kuwa jini alijibu hakuna ila alikuwa anasikia raha.

"Mfano, huyu bwana tangu ameishi humu hajawahi kutuona kwa macho lakini sisi tulikuwa tunamuona siku zote, tulikuwa tunaingia chumbani mwake na kumfanyia mambo yetu yeye hajui."
Jambo lingine ambalo lilinishangaza sana ni pale dalali huyo aliposema yeye alikuwa na uwezo wa kujua anachokusudia kukifanya mtu hata akiwa Dodoma na akakizuia mapema. Ila, anashindwa kujua endapo mtu huyo atakuwa anakusudia kufanya jambo kwa kuliwaza moyoni mwake bila kulisema kwa mtu.

Nilimuuliza mfano, akajibu mfano ni mimi na mfanyakazi mwenzangu tulipokuwa tumepanga kutumia bangi kuwaangamizi yeye na mkewe, walijua kwa sababu tulijadili kwa sauti ndiyo maana wao walijua. Akaongeza hata nilipoingia ndani na yule mzee aliyeshindwa akatimua, walijua tumepanga ndiyo maana wakawahi kwa kuchukua simu na kufanya mahoka mengine.

Yule mzee mkubwa wa wale waombaji akamuuliza: "Ina maana mkeo jini kwa sasa yuko wapi?"

Yule bwana akajibu atakuwa amerudi ujinini kwa sababu wakati wanaanza kuomba mkewe ndiye aliyekuwa wa kwanza kuhisi anaungua moto na kuanza kulia kwa sauti mpaka ndugu zake wakajitokeza kumtwaa kwenda naye ujinini.

Yule mzee mkubwa wao akauliza swali jingine ambalo na mimi nilitaka kuuliza. Alimuuliza hivi: "Sasa watu wanasema majini wana uwezo mkubwa, wanaweza kupata fedha na mali yoyote ile, sasa kama wewe ulikuwa mume wa jini kweli ni kwa nini aliamua uwe dalali?"

Dalali akajibu: "Mimi sikuwa dalali, bali nilijifanya dalali ili nipate mtu wa kumpangisha ndani kwa sababu mimi na mke wangu tulipenda kuwachezea watu wanaoishi ndani.

"Mimi nina eneo Ilala la kuuza magari, pia nina duka kubwa sana Mnazi Mmoja, sina shida ya maisha wala ya fedha."

Kwa maneno yake hayo nilikubaliana na yeye kwani ni kweli hali yake haikuwa ya kuchoka. Hata siku ya kwanza nilipokutana naye nilishangaa dalali gani ana mwonekano wa kibosibosi ingawa hakuwa na gari. Hapo na mimi nikapata nguvu ya kumuuliza swali:

"Sasa bwana dalali wa bandia, uliwezaje kusababisha mimi nipate namba yako ya simu kwa rafiki yangu anaitwa Mohamed Kombe na akasema wewe ni dalali unaitwa Yusuf Mwamba?"
"Sikia bwana Humuli. Nimeshasema sisi tuna uwezo wa kujua kile kinachojadiliwa mahali na kukifanyia kazi.
Dalali anayeitwa Yusuf Mwamba yupo, huyo rafiki yako tulimchezesha ulimi wakati wa kutaja namba, akazitaja zangu badala ya za Yusuf."

Nilichoka kabisa, yule mzee mkuu akasema tumwingize ndani maana watu waliokuwa wakipita walianza kukodolea macho pale nje.

Kule ndani, dalali aliendelea kuzungumza mambo mengi sana lakini kuna wakati alijipinda na kujishika mgongo akidai anahisi maumivu makali ya moto. Alisema sehemu hiyo ipo kama kuna mtu amebandika jiko la mkaa.

"Mungu amekuponya sana labda kama hutajutia matendo yako ya nyuma," alisema yule mzee aliyenisaidia.
"Mimi sitaki tena, kwanza najuta kwa nini niligeuka adui na kufanya vile kwa watu wengine. Naomba mniombee sana kwa huyo Mungu wetu."

Yule mzee alimwelekeza kanisa lake ambalo halikuwa mbali na pale nyumbani, yule dalali akasema atakwenda kesho yake mapema.

Mimi pia nilialikwa, nikakubali kwenda kesho yake. Walipoondoka, nilibaki na dalali. Wasiwasi ulinishika lakini

nikawa nasikilizia. Kila baada ya dakika tano dalali aliingia chumbani kwangu na kuniomba nimsamehe kwa yote yaliyopita.

Usiku nililala usingizi mzuri hadi kunakucha kiasi kwamba sikuamini kama ni kweli ile nyumba ilikuwa vile. Kesho yake nilikwenda kazini, jioni nilikwenda kwenye lile kanisa ambapo nilimkuta dalali ameshafika.

Tulianza kuwa waumini wa kanisa hilo. Baada ya wiki mbili, dalali alimleta mke wake na mtoto mmoja ndani, kumbe alioa na familia yake ilikuwa Dodoma. Baada ya mwezi mmoja na mimi nilihamia Buguruni ambapo nilioa lakini bado nasali kulekule Magomeni na yule dalali.

Namshukuru sana Mungu kwa kunipigania. Ile mikono ilikuwa si salama bila neema ya Mungu. Nadhani shetani alipanga nife lakini ameshindwa katika jina la Mungu. Amina.

MWISHO.
 
Mzizi Mkavu stori umeichukua gazetini tena Ijumaa (imemlizika muda si mrefu)je umewaomba au umeamua kuitoa humu bila kupata haki?otherwise ni nzuri na kiboko ya shetani ni Yesu hata kama ana nguvu vipi kwa imani anashindwa.
 
Hadithi na imani kama hizi ndio zinawafanya watanzania wanaangamia katika lindi la ushirikina linalopekekea baadhi ya watu wajinga kuua albino, kuchoma vikongwe, kuchuna ngozi za watu na sasa kukata vichwa vya watu. Pathetic.
 
Eee! Hi story nimeiona fesbuku kwa jamaa anaitwa Binshiwawa kama sikosei tena kama 2 weeks nyuma ivi
 
ila huyu jamaa ana roho ngumu bana khaaaaaa..........Mzizi mkavu huyu jamaa alikuwa apata usingizi kweli au alikuwa analala kazin? mh.... hapana kabisa yani ninge....:bolt::bolt:
 
Kuna wakati utadhani wanatumia sana neno dotikom, lakini ukisema usikilize zaidi unasikia wakisema sana kotoko au kiburate, wakati mwingine sauti ya kike ilisema kaunto, ya kiume ikarudia hivyohivyo, kaunto.

Haya mazito sana
Jamani najua kuna wenyeji wa Tanga Sumbawanga Pemba Zanzibar na Bagamoyo pamoja na kwengineko embu tililikeni mzidi kutufungua masikio kwa haya yalimkuta Humuli,,Maana majini nao ni viumbe kama binadamu utata unakuja wao wamepewa uwezo mkubwa na binadamu nae ana uwezo wake upi na jinsi gani ya kuutumia ndipo unapokuja ulakini
 
Mimi sio mpenzi wa haya mahadithi yenu lakini hii imenivutia sana embu leta nyingine, nimecheka sana hasa yale maeneo anayojisemea alafu anasikia vicheko. yaani mpaka hapa ofisini wameniona kituko, kumbe wasoma hadithi mnafaudugu sana
 
kamanda bado hujaonana na shigongo maana hiki kitabu
watu wanaweza kwiba wakatoa kabla yako
asante kwa promo
 
Haaaa haaaa ukivuta bangi humu tunaenda kushtaki police haiwezekani mtu uvute bangi hovyo hovyo haa haa haa maneno ya jini hayo
 
Back
Top Bottom