Nyumbani kwangu huwa hatuna utaratibu wa kuandaa keki kwa ajili ya birthday ingawaje huwa zinaandaliwa kama kiburudisho kingine kiliwacho.Nimesoma.yote mzee
Bibi hamida hajaandaa kekj?
ngoja nitulize fuvu langu rasmi nianze kusomaDada, angalia post #33
thnx my G nimefika acha nianze mdogo mdogo
Sawasawa 😊🤗Tupio la VIII – John Mutalebwa
John Mutalebwa, ni kijana mtanashati mwenye mwili wa mazoezi na majigambo mengi. Ana gari aina ya Harrier alilonunuliwa na baba yake Mzee Mutalebwa ambaye ni kiongozi wa kisiasa na mwenye nguvu kwenye chama chake akiwakilisha wananchi katika moja ya wilaya za kanda ya Ziwa. Kiongozi huyu wa kisiasa ametuhumiwa mara kadhaa kwa utakatishaji fedha na biashara haramu lakini hapakuwa na ushahidi wa kumtia hatiani.
John, ambaye sasa anaingia mwaka wa tatu katika chuo cha usimamizi wa fedha IFM ndiye aliye mshawishi Emmy kwa kumnunulia Iphone 14 na kumuahidi maisha mazuri akimuacha Alex. Lakini John kama ambavyo inajulikana kwa wanafunzi wenzake wengi wa darasa lake, ni mtu wa kubadilisha wanawake sana kwa kutumia nguvu ya kifedha aliyo nayo.
Neema, Rachel, Margareth, Lidya, Zaituni na Laura hawa wote walijuwa kuwa urafiki wa Emmy na John hauwezi kudumu kwani John akipata mwanamke mwingine mzuri kuliko Emmy, atamfuata huyo na kumsahau Emmy kama alivyowaacha Catherine, Rebeca, Pauline, Martha, Pendo, Zubeda, Zainabu, Khadija na Lucy ndani ya miaka miwili ya chuo. Na hao ni wanafunzi wenzake, sijui huko kwingine hali ikoje.
Baada ya Emmy kushawishika kwa ‘outing’ katika hoteli kubwa kubwa na sehemu zingine mbalimbali za starehe, Emmy aliamua kuvunja uhusiano wake na kipenzi chake cha utotoni Alex mbele ya hadhara tena kwa maneno ya kashfa na aibu. Hakuna aliyependa kitendo kile cha Emmy kumfanyia Alex vile…
Zaituni bado alikuwa na simu aliyoitupa Alex, siku hiyo aliamua kumkabidhi Alex simu yake.
“Alex, mambo?!” alisema Zai huku akimkaribia Alex.
“Poa Zai, vipi shwari?” Alex alijibu vizuri tu kama kawaida yake. Alex pale chuoni alikuwa maarufu sana kwa kuuza vocha za kurusha za mitandao yote, biashara iliyomsaidia kujenga urafiki na wanafunzi wenzake na kujikimu kiaina.
“Nimekuletea simu yako, nimeibadilisha na kioo tachi (touchscreen) maana siku ile ilipasuka…” alisema Zai huku akimkabidhi ile simu Alex, Alex akaipokea na kuiangalia kisha akasema…
“Ahsante Zai, wewe ni mwema sana, una roho nzuri, Bwanaako atafaidika sana…” kisha wote wakacheka…
“Kwanza jamaa yako mwenyewe yuko wapi…” aliuliza Alex
“Yule palee kwenye…” alijibu Zai huku akionesha upande alipo boy friend wake.
“Ni yeye aliyenipatia hela ya kubadilishia kioo hiki…” aliongezea Zai.
“Ooh, basi twende nikamshukuru naye pia…” alisema Alex.
Baada ya hatua chache wakafika alipo Jafari, boyfriend wa Zaituni…
“Oyaa Jeff vipi?” alisalimia Alex
“level kama kawa..” alijibu Jafari.
“Nakushukuruni sana kwa ukarimu wenu wa siku zote na wa kuitengeneza simu hii…” Alisema Alex.
“Usijali babu, sio kitu, mbona kawaida tu!...” alijibu Jafari.
“Nawashukuruni sana, lakini hata hivyo naomba uridhie simu hii nimpatie Zai iwe yake moja kwa moja…” alisema Alex.
“Vipi kwani hujaipenda, au kioo kimebandikwa vibaya?!...” aliuliza na kushangaa Jafari.
“Hapana, hii niliyonayo infinix inanitosha, hata hivyo hiyo Samsung ina kumbukumbu nisiyopenda kubaki nayo, Zai pokea simu hii iwe yako, kuwa huru nayo…”
“Shukran Alex…” Alisema Zaituni kisha naye Jafari akamalizia..
“Haina noma jomba, basi tukapate chakula pamoja …” ilikuwa mida ya lunch.
Wakawa wanaelekea sehemu ya kupata chakula na Jafari hakuacha kuchagiza…
“Ila mwanangu Alex, ulimnunulia simu kali demu wako, sema hana shukrani tu, Samsung latest kabisa!...”
“Yote maisha tu mwana! Ila nini, atajuta! Maana alipoangukia sio penyewe…” Alex akajibu na wote wakaangua kicheko…
Jafari na Zaituni wapo kwenye uhusiano takribani miezi kumi sasa na wapo vizuri maana Jafari hana ‘mambo mengi’ wala Zaituni hayupo ‘macho juuu juu’
---
Alex akapata ‘text msg’ akialikwa nyumbani kwa dada yake Qeen jioni ile.
“…Jitahidi leo chakula cha jioni uje kula nyumbani Tabata…” ilisomeka sehemu ya ujumbe ule.
Ilipotimia saa kumi na mbili na nusu jioni, Alex alifika nyumbani kwa dada yake, akakaribishwa vizuri na kukutana na rafiki wa dada yake aitwaye Maurine ambaye ndio wamepanga nyumba nzima pamoja ila wamegawana upande kila mmoja anajitegemea.
“Karibu sana Alex, hapa ndipo ninapojifichaga, na huyu hapa ni Mourine, rafiki yangu kwa muda mrefu sasa…” alisema Queen akimkaribisha Alex.
“Karibu sana Alex…” alidakia Maurine na akamsogelea na kumkumbatia…
“Ahsanteni, nimeshakaribia…” alijibu Alex na kujitoa kwenye kumbatio ambalo lilianza kumpa hisia tofauti.
Maurine ameumbika, ni mrembo kuliko Queen kwa macho ya wengi, ila Queen ni smart sana kichwani kuliko Maurine. Wote wana maumbo mazuri yenye kuweza kushawishi wanaume…
Maurine, kahaba mwenzie na Queen, alikuwa ana muonekano mdogo kuliko Queen kimaumbile ingawaje walikuwa wamepishna mwaka mmoja tu kuzaliwa, unaweza kusema Maurine alikuwa ‘portable’ zaidi kuliko Queen.
“Alex jisikie huru, hapa ni nyumbani, natoka kidogo kuchukuwa kitu dukani kisha narudi…” Alisema Queen kisha akakazia…
“Mourine, mkirimu mdogo wangu kwa kinywaji apendacho, ‘usimkomaze’ narudi sasa hivi…”
“Hahahha dada jamani, mie wa ‘kukomazw’ na huyu!...” nilijichekesha pale kuonesha uchangamfu lakini nilikuwa najuwa nia ya dada kwamba niwe makini asije akanishawishi ujinga.
“Simkomazi da Queen, utamkuta salama salmin…” alijibu Maurine huku akitabasamu.
Nyumba waliyopanga ilikuwa mbali kidogo na huduma za maduka, hivyo ilitarajiwa kamuda fulani kangepita kidogo kabla ya Queen kurudi. Ni kwamba Alex aliwahi kufika kabla ya dada yake kuandaa mambo ya msosi, hivyo ilibidi aende barabara kuu kuangalia kitoweo alichopanga kukitumia siku hiyo na nduguye wakati wakijadili mambo yao.
“Sikujuwa kama da Queen ana kaka ‘handsome’ hivi…” aliachombeza Maurine wakati Alex akiwa bize na simu yake…
“Unapenda kinywaji gani Alex…” Alimuuliza
“Eeee nipatie sprite baridi…” alijibu.
“Soda?! Kwani upo kwenye dozi au?...” alishangaa Maurine
“Hapana, situmii kilevi tangu zamani…” Alex alijibu.
“Makubwa! Queen ana kaka mlokole!...” alisema huku akimfungulia soda na kummiminia kwenye glasi.
“Kwani walokole peke yao ndio hawanywi pombe?..” Alex aliuliza ili kunogesha stori…
“Najuwa sio walokole tu, je sigara unavuta?!...” aliuliza swali chokonozi…
“Hapana dada, sinywi pombe wala sivuti sigara…” Alex alijibu
Maurine akacheka kicheko cha kimbea kisha akasema…
“Niite tu Mourine bhana, na nimeshajuwa kilevi chako heheeee…”
Basi mazungumzo ya ‘kuchangamsha genge’ yaliendelea bila madhara kwa Alex hadi dada yake aliporudi na kuwakuta wakiendelea kuongea wakiwa wote wachangamfu…
Chakula kiliandaliwa, wakala wote watatu kwenye sebule ya Queen, lakini baada ya kula tu, Maurine aliaga kuwa anawahi kazini…
“Dada utanikuta, natangulia pale pa siku zote pa kuanzia…” alisema Mourine.
“Sawa, mie nitachelewa kidogo, nina mazungumzo na Alex kwanza.” Alijibu Queen na Maurine akaingia upande wa vyumba vyake kujiandaa na mtoko.
---
“Eee nimekuita hapa ili kwanza upafahamu nyumbani ninapoishi pia kujadili mawili matatu kuhusu kikao cha kule hotelini siku ile na tatu kukuambia kuhusu ujumbe mfupi wa maandishi kwa njia ya simu kwenye ile line niliyoipotezea…” Alisema Queen.
“Karibu sana Alex, hapa ndio nyumbani, maisha yanasonga kama hivi, lakini muda si mrefu tutabadilisha maisha yetu mdogo wangu…”
“Kuna lile swali nilitaka kumuuliza Afande siku ile kule hotelini ukanikataza, mimi naona kama kuna kitu hakija kaa sawa…” aliendelea Queen
“Inakuwaje katika tukio la mauaji kama yale Polisi ishindwe kufikisha upelelezi mwisho na hatimaye ikajulikana nini kilitokea…”
“Nilitaka anijibu pale pale ili roho yangu itulie, nilikuheshimu tu lakini wala sikuona mantiki ya wao kusema busara ilikuwa ni kuacha jambo liishie kama lilivyoishia, haina maana hata kidogo…”
Hatma ya hili jambo ikawa wafanye vikao na watu watatu kila mmoja kwa wakati wake, yaani Kamanda, Jaji na Gavana, lakini kwanza wasubiri wakabidhiwe mirathi yao kisha walianzishe kimya kimya wapate mwanga wa kauli zile za Kamanda kwamba busara iliwapelekea waache suala lile liishie kama vile.
Aidha kuhusiu ile ‘text msg’ aliyopokeaga Queen, Alex alihitimisha kuwa asiipuuzie, wafuatilie baada ya mambo ya mirathi kukamilika maana watakuwa na fedha za kutosha, ingawaje hadi wakati huo hawakujuwa kwenye mirathi kuna nini na nini zaidi ya akaunt za benki.
Itaendelea Jumamosi ijayo panapo majaaliwa.
Tupo pamoja MkuuMeza hivyo hivyo mkuu.