Litro
JF-Expert Member
- Nov 18, 2018
- 901
- 1,808
sante daktari mkuu wa zamu
sante daktari mkuu wa zamu
Asili yake ni neno SEGEMNEGE
Segemnege ni KIELEZI
Kielezi huelezea kitendo (KITENZI) jinsi kilivyo fanyika.
Mf.
Nourhan anatembea "taratibu"
Neno ANATEMBEA ni 'kitenzi' (kitendo)
Neno TARATIBU ni 'kielezi', kwa kwa mukhtadha husika anaelezewa jinsi Nourhan anavyotembea.
Msegemnege ni vivyohivyo kielezi, na maana yake kwa maneno mengine ni 'Shaghalabaghala', 'a~bila mpangilio', 'hovyo hovyo', nk.
---
Tangia alivyomuacha mke wake wa kwanza, mambo yake yanaenda segemnege.
---
Simulizi hii ni msegemnege
(m) hapo nimeongezea kuvunisha tu!
Kama vile baadhi ya watu wa Tanga, Mombasa na Zanzibar wavumishavyo maneno...
mf.
Meli => Jimeli...
Honda => Jihonda...
kama vile baadhi ya watu wa kanda ya ziwa wavumishavyo maneno...
mf.
Baiskeli => Libaiskeli
Moyo wangu umekudondokea => Limoyo langu limekudondokea
Kama vile watu wa kanda ya magharibi wavumishavyo maneno kwa kudunisha...
Hela => Kahela
Simu yake nzuri => kasimu kake kazuri.
Bila kuwasahau baadhi ya watu wa nyanda za juu kusini...
Sanduku => Gusanduku
Nyumba kubwa => Gunyumba gukubwa
Nk
___
Bila shaka umepata mwanga.
Watu wengine sijui wakoje ushasema sio simulizi ya kweli ya kutunga ameze tu hivyo hivyo 😂Meza hivyo hivyo mkuu.
Wanakaa woteHivi ifm Kuna hostel wanakaa wanaume? Nilijua wanakaa wadada tuu, anyway endelea na story mkuu
Sasa Kuna ubaya gani kuuliza swaliWatu wengine sijui wakoje ushasema sio simulizi ya kweli ya kutunga ameze tu hivyo hivyo
Kuwa makini unaposoma kuepusha maswali ya kijingaSasa Kuna ubaya gani kuuliza swali
Simulizi ya kubuni haina uhalisia hivyo kulikuwa hakuna haja ya kuuliza unasoma unamezea kwakua ni simulizi sio uhalisia.Sasa Kuna ubaya gani kuuliza swali
Jamii forum siyo mali yako kusema upangie nini watu Cha ku-comment, seat back and enjoySimulizi ya kubuni haina uhalisia hivyo kulikuwa hakuna haja ya kuuliza unasoma unamezea kwakua ni simulizi sio uhalisia.
Maisha ya uyatima ni tabu sana hususani wasimamizi wa mirathi wakiwa wenye kudhulumu.Happy Birthday.
Ukisoma unaona maisha ya watoto baada ya wazazi kufariki.
Hasa kifo kama hicho ambapo watoto wote walikuwa bado hawajaweza kusimamia kwa miguu yao.
Na usumbufu wa mahakama ni tatizo lingine
Nitarudi kuendelea kusoma.
Keki ni wapi huko?
😘
JBourne59 kwenye ubora wako haujawai koseaTupio la XI – The Jonathan Company Limited
Ilipoishia
Kikao kilihitimishwa kwa sisi kupewa ‘business card’ za Mheshimiwa Jaji, Gavana na Afande nasi tukawapa namba zetu ambapo walizisevu moja kwa moja kwenye simu zao na Hakimu alisisitiza baada ya wiki moja tusikose kufika NMB makao makuu kwani huku kuna kila kitu chetu na kwamba atafuatilia kujua kama kuna changamoto yoyote tutakayopata.
Sasa endelea…
Siku zilipita, na hatimaye ikafika Jumatatu ambapo ndio ilikuwa siku ya kwenda benki. Queen na Alex walikuwa wamejiandaa vyema kwa changamoto yoyote itakayo jitokeza kule benki na wote siku hiyo walikuwa wamevalia nadhifu baada ya Queen kumlazimisha sana Alex anunue nguo mpya na Queen alisimamia hilo.
Kutokea dawati la huduma kwa wateja, walipokelewa vizuri na kueleza shida yao ya kutaka kumuona meneja wa wateja, wakaambiwa wasubiri kwenye viti kwani wakati huo meneja husika alikuwa ana mgeni ofisini kwake.
Baada ya kusubiri kama nusu saa hivi tukaitwa.
Alex anaelezea…
Tukaoneshwa mlango wa kuinga na tukakaribishwa na meneja huyo kwa tabasamu zuri.
“Karibuni niwasaidie…” alisema yule dada Meneja
Queen tulikubaliana kuwa yeye ndiye atakuwa mzungumzaji mkuu hadi pale yeye akitaka mimi niongee ndipo niseme kitu…
“Ahsante dada, mimi naitwa Queen Jonathan na huyu hapa ni ndugu yangu anaitwa Alex Jonathan…” Alisema Queen.
“Oooh, karibuni sana, hebu subiri kidogo…” akaitikia yule meneja kana kwamba alikuwa anafahamu kitu kisha akainua simu yake ya mezani.
“…Boss, Jonathan Company is here…, Okay, okay, yes, in a second.” Akakata simu.
Aliongea yule Meneja kwa kunong’ona sana kiasi kwamba usipokuwa makini huwezi kujua hata ameongea kitu gani kisha akatuambia tumfuate naye akanyanyuka na kutuongoza katika ofisi nyingine…
Nilibahatisha kusoma mlangoni wakati tunaingia maana mimi nilikuwa wa mwisho kuingia tukitanguliwa na Meneja aliyetuongoza akitumia kitu kama kadi hivi kuruhusu milango kufunguka, tukapitia kwenye sehemu kuna ‘scanner’ ya mwili na kuturuhusu kuendelea…
“DCEO Corporate Banking” ni maandishi niliyoyasoma pale mlangoni. ..
“Karibuni..” Alisema yule dada Meneja aliyetuongoza…
“Sir, here is Mister Alex and Miss Queen...” aliongea tena yule dada meneja kisha akatugeukia na kutuambia suala letu litashughulikiwa hapo.
“Karibuni vijana, eee, mimi naitwa (akataja jina) ni msaidizi wa CEO …” akavuta droo na kutoa folder lenye mafaili kadhaa na kisha akawasha tarakilishi yake ya mezani na kuanza kubofya.
“Ahsante, mimi naitwa Queen Jonathan na huyu mdogo wangu anaitwa Alex Jonathan…”
“Nashukuru kuwafahamu, na habari zenu ninazo, karibuni sana.” Tukaitikia pale wote “Ahsante”
Sekunde chache mlango wa ofisi ile ukafunguliwa na akaingia dada aliyevalia sare maalum akituletea chai.
Ofisi ilikuwa kubwa, nzuri yenye hadhi ya kuitwa ofisi ya CEO.
“Karibuni, kuna chai, kahawa, maziwa, milo na cocoa…” alisema yule dada mhudumu huku akisubiri majibu yetu ili ajue ataandaeje…
“Nipatie Kahawa ya maji pekee…” alisema dada
“Nami nipatie maziwa yenye cocoa…” nilisema.
Tukamiminiwa viywaji vyetu pale na tukaanza kunywa tukisindikizia na sambuza ndogo ndogo nzuri na biskuti.
“Nipatieni vitambulisho vyenu vya Taifa…” alisema yule DCEO. Nikatoa changu na kumpa dada ambaye yeye ndiye akasimima kumpelea DCEO yule ambaye meza yake ilikuwa mita tatu hivi kutoka tulipokuwa tumeketi.
Hali ya ubaridi mkali mle ndani na utulivu uliokuwepo ilifanya nihisi njaa ya chai kuliko kawaida kitu kilichopelekea kujiongezea maziwa na kuweka milo na kahawa kwa pamoja safari hii.
“Queen, njoo uweke kidole hapo kwenye biometric (finger print reader)” alisema yule DCEO na pia ikawa hivyo ilipofika zamu yangu.
“Well well, sasa nimesha thibitisha kuwa ninyi ndio wahusika halisi katika suala hili,… malizeni kunywa chai kisha mnijulishe tuendelee…” alisema tena.
Kwa hamu tuliyokuwa nayo tukamaliza fasta chai na dada akasema…
“Tupo tayari baba”
DCEO akasimama na kutuamuru tumfuate ambapo tuliingia chumba kingine hapo hapo na ilionekana ni chumba cha mikutano kwa mandhari ya mpangilio wa meza, viti, sehemu ya ‘presentation display’ nk.
“Karibuni sana, hiki ni chumba cha mikutano yangu na wateja, hapa sasa tutaelewana vizuri…”
Akabofya kuwasha tarakilishi mpakato ilikuwepo pale meza kuu na ‘boom’, display ikaonekana kule kwenye ubao maalum ukutani.
DCEO akaanza kuongea…
“Eeee kuna mirathi yenu katika benki yetu lakini pia katika sehemu nyingine kama wosia unavyosema…”
“Awali ya yote poleni sana kwa kupoteza wazazi wenu…”
Aliendelea kuongea pale wee huku sisi tukisikiliza kwa makini, aliongea kwa kusoma wosia sentesi kwa sentensi na mgawanyo wa mali. Ajabu ni kwamba wasia ambao sisi tulisomewa mahakama ya mwanzo ulikuwa mfupi tofauti na huu ambao tulikuwa tunauona kwa macho yetu jinsi ulivyoandikwa kwa hati ya baba. Aidha mirathi kwa upande wa mama haukuwa mrefu zaidi ya mgawanyo tu wa hela zilizokuwa benki kwenye akaunti yake.
Sehemu ya wosia wa baba ilikuwa inasomeka hivi…
- Pesa zilizopo benki ya CRDB (TZS & UDS), NBC (TZS) , EXIM (USD) pamoja na STANBIC Bank (EURO & USD) zote zihamishiwe kwenye benki ya NMB, kisha zifunguliwe akaunti mbili (Corparate) moja ya Queen Jonathan Ngonyani na nyingine ya Alex Jonathan Ngonyani ambapo akaunti hizo ziwe za USD pekee. Jumla ya fedha hizo mpaka naandika wosia huu ni ka ifuatavyo:-
CRBDTZS - 79,xxx,xxx
CRDBUSD - 563,xxx
NBCTZS - 894,xxx,xxx
EXIMUSD – 270,xxx,xxx
STANBICUERO – 355,xxx
STANBICUSD – 350,xxx
-Pesa zilizopo benki ya NMB akaunti ya biashara zigawanywe nusu kwa nusu kisha wapewe Queen Jonathan Ngonyani na Alex Jonathan Ngonyani wafunguliwe akauti za biashara, hadi naandika wasio huu jumla ya yake zipo TZS 1,832,xxx, xxx/- pia washauriwe wafungue akaunt za akiba NMB ambapo waweke fedha kiasi.
Kuna hisa katika makampuni matatu ambapo hisa hizo zigawanywe nusu kwa nusu kisha umiliki uhamie kwa majina ya Queen Jonathan Ngonyani na Alex Jonathan Ngonjani :-
DCEO yule alikuwa anatusomea taratibu ili tuelewe na huku sisi wenyewe tukiona maandishi yenye hati ya baba yetu yakipita kwenye display iliyokuwepo mbele…
- Kampuni ya uwekezaji A 3%
- Kampuni ya mtandao wa simu A TZ 5%
- Kampuni ya uwekezaji B 1%
Wasio ulikuwa mrefu na wenye maelekezo na maelezo mengi, sote mimi na dada tulikuwa tunastaajabu utajiri ambao baba alikuwa nao na wala hatukujuwa wala hakuonesha kuishi katika hali ya ukwasi kiasi kile.
Moyoni tukiwa na furaha, lakini na maswali yasiyo na majibu pia kichwa tuliendelea kufuatilia maelezo ya DCEO.
“Eee kwa jinsi hiyo, yote hayo, kwa maana ya mgawanyo wa mirathi kwa upande wa baba yenu na upande wa mama yenu yameshafanyika, na akaunt zenu zitakuwa tayari punde si punde…” kisha akabofya kitufe fulani na baada ya dakika chake akaingia afisa mmoja wa benki, tulimtambua kwa sare zake, alikuja na camera na atakupiga picha kisha akaondoka.
Alituonesha pia pesa zilizokuwemo kwenye benki yake NMB, ambapo zilitofautiana kidogo na zile zilizomo kwenye wosia kwa kuongezeka kila akaunti. Pia akapiga simu kwenye benki zingine zenye akaunti za marehemu na kuomba apatiwe statement kwa mujibu wa amri ya mahakama kama tulivyomsikia akiongea, ambapo punde si punde zilikuja ‘printout’ kutoka kwenye printer na soft copy zilionekana kwenye display, nako hapakuwa na mabadiliko ya viwango vya fedha kama ilivyooneshwa kwenye wosia.
“Received, reeived received… proceed with bank transfer as ordered by BoT, you may check authentic of the source…, okay, …, Okay, transfer confirmed…”
Aliongea yule DCEO kwa lugha zao za kibenki wakifanya miamala ambayo sasa tulijuwa inaingia kwenye akaunt zetu.
“Kama mnavyosikia, hela zenu zote zinahamishiwa hapa, kisha ninyi mtakuwa huru kufungua akauti sehemu nyingine katika benki yoyote, lakini kwanza tulitaka kulimaliza zoezi hili mara moja ili muanze umpya mkiamua, lakini itakuwa vyema tukiendelea kufanya kazi nanyi Jonathan Company.
Siku hiyo ndio tulijua kuwa marehemu baba alikuwa ana ‘Private Company’ iitwayo Jonathan Company Ltd iliyokuwa inajishughulisha na mambo mbalimbali kama tulivyoonesha Memorandum and Article of Association ya kampuni hiyo na hisa zote za kampuni hiyo iliamriwa na wosia ziende kwa dada Queen.
Hadi inafika saa tisa alasiri tulikuwa tayari tumeshakabidhiwa kadi zetu za Corporate, fedha kiasi tulihamishia kwenye akaunti za akiba ambazo sote mimi na dada Queen tulikuwa nazo za hapo NMB na zoezi la uhamishaji umiliki wa kampuni Queen aliambiwa aende Brela kwa ajili ya kukamilisha utaratibu, na kuhusu hisa za uwekezaji katika kampuni alizowekeza baba ilibakia kipengele cha kuweka sahihi tu.
Alituruhusu kwenda mapumziko mafupi lakini alitutaka turudi tena benki baada ya saa moja…
“Saa kumi mrudi hapa, milango itakuwa imefungwa kwa wateja waliopo nje lakini mkifika waonesheni walinzi hizo kadi zenu mpya mtafunguliwa, kuna sehemu nataka niwasindikize…”
Tulitoka mle ndani tukiwa hatuna hata njaa, sijui kwa sababu ya ile chai nzito ama kwa sababu ya utajiri wa ghafla ili mradi tulikuwa na furaha na tulitembea kuelekea restaurant ya jirani kupata chakula cha mchana.
“Dada mimi sisikii njaa hata!” Nilisema wakati tunaingia cafeteria fulani iliyopo kwenye kituo cha kuuzia mafuta.
“Hata mimi Alex, sisikii njaa japo nilionja tu ile kahawa na sambusa kidogo” tukacheka kiasi na kuketi mle mghahawani.
Itaendelea Jumamosi panapo majaaliwa.