Simulizi: Msegemnege

Nimesoma.yote mzee
Bibi hamida hajaandaa kekj?
Nyumbani kwangu huwa hatuna utaratibu wa kuandaa keki kwa ajili ya birthday ingawaje huwa zinaandaliwa kama kiburudisho kingine kiliwacho.

Siku za kumbukumbu za kuzaliwa huwa tuna utaratibu wa kufanya ibada ya kumshukuru Mola kwa umri na afya na kujumuika pamoja kwa chakula cha jioni.

Alhamdullilah, jana jioni ilikuwa siku nzuri sana nyumbani.

Baadaye leo waliofanikiwa kufika nyumbani watatawanyika.

Ni furaha sana kujumuika na familia nzima na amani moyoni bila kujali hali ya maisha.
 
Tupio la VI – Hakimu mfawidhi

Ilipoishia

Nikamhadhithia historia nzima ya jinsi alivyonipiga kibuti.

“Kha!, Emilia ndio amekuwa na kiburi kiasi hicho!” dada alishangaa, maana Emmy aliyekuwa anamjuwa yeye wakati ule alikuwa mdogo na leo hii amenipiga kibuti.

Stori za hapa na pale ziliendelea na wakati tunaanza kula mara simu yangu ikaita…

“Hakimu hapa, leo saa moja jioni tukutane Serena Hotel upande wa Restaurant tupate dinner pamoja, muhimu sana, usikose” alisema kisha akakata simu.

Sekunde kadhaa baadaye simu ya dada ikaita na Hakimu yule yule akamwambia da Queen kama alivyo niambia.

---

Alex anendelea kusimulia…

Tukiwa ndani ya eneo la mapokezi pale Serena Hotel, nilipokea simu kutoka kwa Hakimu, namba yake sasa niliihifadhi kwenye simu yangu…

“Mko wapi..?” Sauti ya hakimu.

Nikamjibu “Ndio tumefika mapokezi na sasa tunaingia upande wa restaurant.”

“Ok, sisi tutachelewa kidogo, agizeni chochote muendelee wakati mnatusibiri..” Aliongea na kukata simu.

Nikamjulisha dada kuhusu ile simu na ikawa Hakimu ametuachia maswali, kwani tulijuwa tunakutana naye yeye peke yake lakini inavyoonekana kama kutakuwa na timu ya watu, du!

Restaurant tulipokelewa na mhudumu aliye valia nadhifu na mwenye tabasamu la ukaribisho…

“Karibuni…” alisema huku akituangalia usoni kama vile alikuwa anasubiri tuseme kitu.

Kuingia katika hoteli kubwa kama hii kwa bahati nzuri haikuwa mara yetu ya kwanza, wakati wa uhai wa wazazi tulishafanya ziara za kula katika karibu hoteli zote yenye hadhi kama hii hapa Dar na dada yeye alikuwa mzoefu zaidi maana katika kunisimulia maisha yake baada ya kutoka pale Manzese kisha kuhamia Sinza halafu Tabata, amekuwa akitembelea sana hizo hoteli nyakati tofauti.

Kwakuwa sikuwa na hela za kutosha mfukoni na kwa kuwa sikujuwa nguvu ya fedha ya dada nilijikuta nimesema…

“Eeeee tuletee maji makubwa 1 na soda sprite mbili…”

Mimi na dada tangia zamani tunapenda sprite hivyo nilijuwa hawezi kupindua chaguo. Nisijue kuwa kumbe dada yupo vizuri mfukoni na kwa kuwa hadi muda huo alikuwa hajapata kileo (pombe) basi alitumia mwanya huo kuagiza whisky…

“Ongezea Jacky Daniels kwenye hiyo oda” dada alisikika.

Nilimuangalia dada wala sikummaliza, yeye alikuwa anatabasamu tu.

Tuliletewa vinywaji vyetu na tulianza kunywa mdogo mdogo huku nikishangaa dada yeye akipiga ile whisky kavu-kavu bila kuchanganyia na maji au soda, ingawaje alikuwa anainywa kidogo kidogo taratibu sana.

Tuliendelea na maongezi ya kawaida baina ya kaka na dada huku tukitafakari ujio wa Hakimu na watu tusio wafahamu na kwa kweli hata hatukuweza kubashiri ni akina nani wanaweza kuwa wameambatana naye.

Saa mbili kasoro usiku ndipo Hakimu na watu wengine watatu waliingia na kusogea katika meza yetu kujumuika nasi.

Mavazi yangu tangia nilivyoanza kujisomesha yalikuwa ni yale ya kawaida tofauti na wakati wa uhai wa wazazi wetu, hivyo kwa kuniangalia kwa mavazi ilikuwa rahisi kujua hali yangu ya uchumi, na hapa ule usemi wa “Don’t judge a book by its cover” haukuchukuwa nafasi, maana jalada la kitabu kwa upande wangu lilikuwa linasadifu hali yangu ya uchumi moja kwa moja tofauti na dada Queen yeye alikuwa amevalia nadhifu vazi la kuendea ofisini hivyo alionekana ana hadhi fulani kulinganisha na mimi.

“Ooooh, poleni kwa kutusubiri, lakini sasa timu imetimia hivyo hakutakuwa na jambo litakalo haribika…” alisema hakimu.

“Eeee, Alex na Queen, kutaneni na Kamanda wa upelelezi wa makossa ya jinai…”, akamtaja jina na tukapeana mikono na kusalimiana… kisha akaendelea…

“Pia fahamianeni na Gavana wa benki kuu…” akamtaja jina na tukapena mikono…

“Na huyu hapa anaitwa Mheshimiwa Jaji (akamtaja jina)..” naye tukapeana mikono.

Hakimu yule mchangamfu aliendelea na utambulisho akiwaelekea aliokuja nao, “…eee bila shaka mnawafahamu hawa vijana…”

Akajibu yule kamada wa Polisi kuwa alituona mara moja tu miaka mitatu nyuma na kama angetukuta njiani asingetutambua…

Gavana na Jaji wao walikiri kutufahamu, nasi tulikuwa tunawafahamu, siyo kwa kuwaona kwenye magazeti ama runinga bali walishawahi kuja nyumbani Masaki mara kadhaa wakati wa uhai wa wazazi wetu.

“Queen umebadilika, umekuwa mkubwa sana, umenawiri na naona siku hizi unatumia vitu vikali…(akimaanisha pombe kali)” Jaji alisema kwa kumtania Queen

“Alex hujabadilika sana, vipi ulishamaliza masomo yako ya urubani?!” Alidakia Gavana…

Kabla sijajibu swali la Gavana, Hakimu yule akakatiza, “…eee nadaiwa shilingi ngapi maana nimekuta mmeshaanzisha sasa nataka ‘niklie’ ili tuanze moja…” alisema huku akitoa kadi yake ya CRDB na kuweka mezani na mhudumu alikuja na bill kwenye kasha maalum na kumkabidhi, naye akampatia kadi yake ya benki aka swap kwenye POS, risiti ikatoka kisha mhudumu yule akapatiwa oda mpya ambayo sasa ilijumuisha chakula.

“Bado sijamaliza masomo, kule NIT niliahirisha, nimedahiliwa IFM na sasa naingia mwaka wa pili…” nilimjibu swali lake ambalo sasa lilifungua kikao rasmi kiaina.

“Eeee, Alex na Queen, tumewaiteni hapa ili mpate kujuwa nini kinaendelea kuhusu mirathi yenu na hapa tupo na watu muhimu waliofanikisha shauri lenu kifikia tamati….” Alianza kuongea yule Hakimu kisha akamkaribisha Jaji kuongea…

“Karibu Mheshimiwa Jaji…” alimkaribisha.

Jaji aliongea kwa kuanza kutoa historia ya urafiki wake na baba yetu, na kwamba miezi michache kabla ya ajali za marehemu wazazi wetu alifuatwa ofisini kwake na baba yetu akiambatana na mama kuja kuhifadhi wosia ambao ulikuwa umeandikwa na kwa hati ya mkono na kusainiwa na baba.

Wakati Jaji anapata funda la kinywaji chake alichoagiza, Gavana naye akapata mwanya wa kupenyeza maneno…

Siku hiyo hiyo asubuhi na mapema, wakati naingia ofisini, niliwakuta wageni wawili katika orodha ya wageni waliokuwa wananisubiria, si wengine bali walikuwa ni wazazi wenu ambapo baada ya mazungumzo ya kawaida ndio akanikabidhi hati ya wosia kwa ajili yenu endapo ikitokea amefariki.

Gavana alipoona Jaji ameweka glasi chini naye akaamua apige pafu kinywaji chake…

Jaji akaendeleza historia…

Wakati huo wote Kamanda alikuwa akisikiliza kwa makini huku ‘akipiga vitu’ na yule Hakimu aliendelea kuwa msikilizaji pia.

“Wasia niliuhifadhi vizuri sehemu maalumu pale ofisini kwangu na maisha yaliendelea hadi siku nilipopata taarifa ya tukio la ujambazi lilopelekea kupoteza wazazi wenu…”

“Baada ya maziko, kwa bahati mbaya kulitokea fatiki za kusafiri mikoani kwa muda mrefu hadi nikasahau suala la wosia wenu nikawa bize na mambo mengine ya kazi.” Akashika glasi ili apige funda kadhaa kulegeza koo…

Gavana naye akapata nafasi ya kuongea…

Wakati huo wote mimi na dada tunasikiliza kwa makini ambapo sasa tukawa watu wanne ambao ni wasikilizaji wakiwemo Hakimu na Kamanda.

Stori ikawa ileile tu kwamba kila mtu alisahau kwa kutingwa na mambo mengi.

Lakini Jaji katika kufafanua kwake, alisema kuwa kuna siku alikuwa na kikao katika Hotel ya Sea Cliff na alipopita maeneo ya nyumbani pale ndipo akamkumbuka marehemu baba yetu na akakumbuka suala la wosia ambapo chini ulionesha nakala ya wosia huo ipo kwa Gavana pia.

Kesho yake ndipo Jaji alifika ofisini kwa Gavana na kufanya mazungumzo naye ili kutaka kujuwa mirathi husika iliendaje. Gavana naye alikiri kusahau na kwamba hajui kilichoendelea tangia wakati ule na hata wakati huo alikuwa hajui kinacho endelea, ndipo kwa pamoja wakaazimia kulifuatilia suala hili kujuwa liliendaje, wakakumbushia na suala la upelelezi juu ya ujambazi ule ambako nako waliazimia kufuatilia kesi ile na kuishia kukutana na Kamanda.

Ilipofika kipande cha upelelzi wa kesi ile, Kamanda aliweka glasi chini na kuanza kuzungumza…

“Eee poleni sana vijana kwa kupoteza wazazi wenu katika tukio lile, jalada la upelelezi lilifika ofisini kwangu na vijana wangu walifanya kazi yao kwa weledi hadi kufikia hatua ambayo walikuwa hawawezi kuendelea tena ndipo upelelezi wa kesi ile ukaachwa kama ulivyo…”

“Lakini baada ya ujio wa Mheshimiwa Jaji na Gavana ofisini kwangu, ilibidi nifufue upelelzi ule kwa kutumia njia shirikishi ya maafisa wengine kutoka Intelijensi kuu Polisi ndipo tukagundua ambayo hatukupaswa kuyajuwa na baada ya vikao kadhaa vyetu, ilionekana ni busara tuache kama ilivyo maana hakuna wa kumtia hatiani wala hakuna ambalo tungeweza kufanya zaidi, hivyo busara yetu kuwaenzi marehemu ikawa suala hilo tuliache kama lilivyo lakini tukazanie warithi wapate urithi wao na stahiki zao zote…”

Dada Queen alitaka kama kuuliza swali hivi lakini nikamzuia na kumwambia, ngoja, sisi tuwe wasikilizaji tu leo, maswali tuyahifadhi tutauliza siku nyingine tukipata nafasi.

Hakimu alitabasamu na kisha akaanza kusema.

“Wiki moja iliyopita nilipata memo kutoka kwa Mheshimiwa Jaji akitaka taarifa juu ya mwenendo wa shauri la mirathi ya Jonathan baba yenu ‘in-person’…”

“Nikaandaa na kuwasilisha kwa Mheshimiwa Jaji, katika kikao kifupi tulichofanya ofisini kwake, kisha akaniamuru nifanye haraka kuhitimisha shauri hilo na warithi wapate haki zao vinginevyo ningepoteza kazi mimi pamoja na wote walioshiriki kuchelewsha shauri lile…”

Akatulia kidogo kupata funda za kilevi kisha akaendelea…

“Kusema ukweli wanangu sisi watendaji wa mahakama ya mwanzo tuliingia tamaa baada ya kuona mali zilizokuwa kwenye mirathi ile kiasi cha kuanza kupiga danadana ili angalau ‘mjiongeze’ tuingie makubaliano ili tuweze kufaidika na mali ile sisi sote kitu ambacho ni kinyume kabisa na maadili ya kazi zetu na hata kidini pia…”

Hakimu alisema kwa unyonge na akapiga funda kadhaa za kilevi pale kama akiondoa kitu kilichomkaba kooni kilichokuwa kinamzuia asiongee vizuri…

“Kikao na Mheshimiwa Jaji kilinijenga upya na tangia muda ule nimebadilika na kuwa Hakimu bora,… nimefanya ujinga mwingi sana katika kutoa haki za watu, nimedhulumu wengi naomba Mungu anisamehe, na kwa kuwa hiki ni kikao rafiki, naomba tena kwako Mheshimiwa Jaji unisamehe na wote mliopo hapa mnisamehe, mnipe nafasi nyingine kuweza kusaidia wananchi katika njia iliyo bora kwa kufuata sheria na haki….”

Hakimu aliongea kwa uchungu sana huku kama anataka kulia hivi…

Wakati huo mhudumu naye alifika akiwa na wahudumu wenzake ambapo walituletea nyama nyingi zilizo ‘seviwa’ na udambwi-dambwi mwingi kiasi cha kufanya mpenda nyama yeyete atokwe na udenda.

“Karibuni…” sauti nyororo ilisikika kutoka kwa mhudumu wa kike akiwa amesimama sambamba na wahudumu wenziwe wawili wa kiume kama vile walikuwa wakisubiria tuanze kula wapate mrejesho…

Mimi niliinuka na kwenda kunawa mikono, lakini dada Queen na wale wengine wote walibaki pale ka kutumia nyenzo zilizoletwa kwa ajili ya kutumia kulia chakula kile…

Tulianza kula na wote tuliridhika kuwa chakula kipo sawasawa ndipo wale wahudumu wawili wa kiume wakaondoka na akabakia mmoja wa kike lakini naye alipewa ishara ya kuondoka na Hakimu ambapo wakati sisi tunaendelea kula yeye alikuwa anaendeleza historia ya yaliyojiri hadi siku hii kwenye kikao hiki.

“Niliporudi ofisini kwangu, niliitisha jalada la shauri lenu na kuanza kulipitia hatua kwa hatua na hatimaye sikuona sehemu ambayo ilikuwa na mapungufu isipokuwa sahihi zenu na ndio ikawa sababu ya kuwatumieni ujumbe mfupi wa maandishi kwenye simu zenu ambapo namba za simu zenu niliziona kwenye nyaraka zilizokuwepo, na ndio ikawa sababu ya kikao hiki, kwa upande wangu kuja kuwaomba radhi ninyi watoto wa marehemu na Mkuu wangu wa kazi Mheshimiwa Jaji na kwa Jamhuri kwa ujumla, lakini pia kutaka kuwakutanisha na waheshimiwa hawa (akawageukia wenzake wale) ili mfahamiane lakini kwa bahati nzuri leo siyo mara yenu ya kwanza kuonana nao isipokuwa Kamanda pale…”

Alimaliza Hakimu, macho yake yakarudi kwenye nyama na kilevi kisha mazungumzo mengine ya kawaida yakaendelea.

Kikao kilihitimishwa kwa sisi kupewa ‘business card’ za Mheshimiwa Jaji, Gavana na Afande nasi tukawapa namba zetu ambapo walizisevu moja kwa moja kwenye simu zao na Hakimu alisisitiza baada ya wiki moja tusikose kufika NMB makao makuu kwani huko kuna kila kitu chetu na kwamba atafuatilia kujua kama kuna changamoto yoyote tutakayopata.

Tuliwaaga kwa kupeana mikono na sisi tukaaanza kutoka lakini kabla hatujavuka mlango, Hakimu akatuuliza, mmekuja na usafiri gani…

Tukaangaliana pale na dada, kisha dada akajibu, tulikuja kwa daladala…

Mara Afande yule akasimama na kusema, ngoja niwapatie usafiri…

Alitusindikiza hadi nje kisha akamwamuru dereva wake atupeleke popote tutakapo kisha aende kupumzika maana yeye atapata usafiri mwingine.

“Tuanzie kwako dada…” nilisema wakati gari lilivyoanza kuondoka. Na kwa jinsi ile nikapata kupafahamu anapoishi dada.
----

Saa tano za usiku nilifikishwa nyumbani kwangu Manzese. Kutokea kule Hotelini hadi nafika nyumbani, sikuwa mwenye kuzungumza lolote kwa dereva, wala dada hakuwa na mazungumzo nami, kila mmoja alijawa na mawazo kutokana na kikao kile ambacho bado kilituachia maswali kadhaa.

Nilimjulisha dada kuwa nami nimefika salama, na kumuaomba kesho tutafutane ili tupate kujadili mambo kwa kuyachambua.

Asubuhi kama kawaida niliwahi chuo kuangalia kama matokeo mitihani yametoka ili nione kama ‘nimekamatwa au vipi’ ingawaje sikuwa miongoni mwa ‘vilaza’ chuoni lakini lolote humkuta yeyote pasipo kutarajia kwa sababu mbalimbali.

Kwa bahati nzuri baada ya kufika chuo, nilikutana na Bony ambaye alinipongeza kwa kufanya vizuri na kunijulisha kuwa yeye ana supplementary moja. Nilifurahi kisha nikamtia moyo Bony.

Inaendelea…
 
Tupio la VII – Mama Mchungaji

Mama Mchugaji, kama watu walivyo zoea kumwita ingawaje yeye mwenyewe ndiye mchungaji wa Kanisa la ‘kilokole’ maeneo ya Kihonda Morogoro, alikuwa anasifika sana kwa huduma zake nzuri za maombezi. Kanisa lake lilijaa waumini wengi wanawake na wanaume kiasi.

Alikuwa ni msomi wa theolojia na mwenye nguvu katika huduma yake ya maombezi ambapo alikuwa akitoa watu mbalimbali mapepo na kufanya huduma za ufunguzi wa vifungo mbalimbali.

Ilikuwa siku ya Jumatano jioni, siku tatu baada ya kufanya maombi pale KKKT, ndipo tulipofika katika Kanisa la mama Mchungaji. Tukiwa pamoja na waumini wengine, na sisi wageni tukiwa tumekaribishwa kwenye viti vya mbele kabisa, ghafla mtoto Junior alianza kulia, alilia sana isivyo kawaida mara tu mama mchungaji alivyofika pale madhabahuni.

“Nikawa sina jinsi, ikanibidi nitoke nje kwa muda maana kelele zilikuwa zinaharibu utulivu uliokuwepo mle kanisani…” alisema Vailet.

“…Nilivyotoka naye nje ya kanisa tu Junior akaacha kulia, nikajuwa labda nilivyo mbembeleza ndio ametulia hivyo nikarudi ndani ya kanisa na kuketi kwenye kiti changu cha awali…”

“Junior alivyo angalia mbele tu pale madhabahuni akaanza kulia tena kama mwanzo, ndipo mama mchungaji akaamuru apelekewe mtoto…”

“Mlete huku kwangu…” alisema yule mchungaji kisha kukatisha somo alilokuwa ameanza nalo na kuanza kuomba…

“Baba katika JJina la Yesu…...” aliombea weeee huku akiwa amemshika mtoto, lakini Junior hakuonesha hali ya kutulia akawa anarukaruka mikononi mwa mchungaji kwa nia ya kutaka amuachie…

Mchungaji alizidi kumg’ang’ania lakini naye mtoto alizidi kufurukuta, kukukuruka hadi ikabidi amweke chini…

Maombezi yaliendelea na waumini wengine wakapokea kila mmoja akikemea kwa mtindo wake, lakini mtoto hakukoma kulia na kuanza kufanya kama anataka kutambaa hadi ikapelekea kulala kifudifudi akitapatapa kama anaogelea kwenye maji.

Mara sauti tofauti kutokea mlango wa kanisa ikasikika, ikiimba wimbo wa kubembeleza mtoto kwa kilugha na binti kigoli akawa anatembea huku akiimba kuelekea madhabahuni.

Alikuwa ni binti mgeni kanisani mule hakuna aliye mjua, waumini waliendelea kukemea lakini sauti kama zilishuka hivi kutokana na mrindimo wa mpangilio wa sauti ile nyororo kwa lugha kama ya Kigogo hivi isiyoendana kabisa na namna ya ukemeaji mle kanisani.

Binti yule alikuwa kama darasa la saba hivi kwa kumuangalia, lakini akiwa katika mavazi ambayo yanadhihirisha kuwa ni kutoka katika familia masikini, alikuwa amevaa gauni lililofubaa ingawaje lilionekana safi.

Alielekea moja kwa moja kwa Junior pale madhabahuni huku akiendelea kuimba kilugha wimbo wa kubembelezea watoto na alipomshika tu Junior aliacha kulia, akamnyanyua na kumbeba kifuani, kisha akawa anaelekea upande wa mama Junior.

Kanisa zima likatulia na sauti ile nyororo ikasikika waziwazi na ikajulikana ni Kikaguru. Hakuacha kuimba hadi alipomkabidhi mtoto kwa mama yake kisha yeye akawa anatoka kanisani huku akiimba wimbo mwingine wa kuabudu…

“Yua Yaweh…eheheee, x2

“You are Yaweh… Alpha na Omega…”

Ulikuwa wimbo uliochanganyika Kiswahili na Kiingereza, binti alikuwa akirudia maneno hayo hayo huku akitembea tarabitu kuelekea mlango wa kutokea Kanisani…

Kanisa zima likaanza kufuatisha wimbo ule na sauti za mitetemo zikasikika wengine wakaanza kulia kwa hisia mbalimbali kasoro Mchungaji tu ambaye alikuwa mapegwa na butwaa…

Yule binti alitoka mle kanisani, huku ndani waumini waliendeleza ule wimbowa kuabudu hadi pale mama Mchungaji alipo ingilia kati kwa yeye naye kuitikia kwa sauti ya juu huku akinyoosha mkono kuashiria waache kuimba.

Ghafla akatoka mle kanisani kukimbilia nje kuangalia labda atamuona yule binti lakini haikuwa hivyo. Binti alishatokomea kusiko julikana.

Akarudi ndani ya kanisa na kuuliza kama kuna muumini anamfahamu yule binti…! Kimya kilitawala kuashiria hakuna aliyekuwa anamfahamu.

“Yule binti ana upako sana!”… Alisema mama Mchungaji.

“Natamani nijue anatoka wapi ili nimualike aje tena kanisani…” aliongea kwa kutetemeka.

Mama mchungaji hakuwa na nguvu tena ya kuendelea na misa, bali wasaidizi wake wakashika hatamu kumalizia pale mchungaji alipoachia somo wakati mtoto alipoanza kulia.
---

Wakati wa kutoka mule kanisani baada ya ibada ile ya jioni kuisha minong’ono ilianza kama kawaida ya binadamu.

Ibada iliisha mapema kuliko kawaida maana siku hiyo hakukuwa na huduma za ufunguzi kama ilivyo kawaida baada ya mama Mchungaji kutoonekana tena pale mbele madhabahuni maana aliingia chumba cha mapumziko papo hapo kanisani na kujilaza.

“Yule binti ni mtoto wa nani!?..” aliuliza mama mmoja

“Inaonekana hakuna anaye mfahamu katika sisi…” alijibu mama mwingine

“Sijui kwanini hatumfuatilia kujua anaelekea wapi pale alipokuwa anatoka…” Alisema baba mmoja

“Inaelekea ana nguvu za kuliko mchungaji…” alisikia dada mmoja akisema

“Shiiiiii, nyamaza wewe chawa wa mchungaji watatusikia….” Alisema mama mmoja kwa sauti ya chini akimkanya yule dada asiropoke.

“Kwanza alijuwaje kama mule kanisani kuna mtoto analia…” Alihoji yule dada…

“Halafu alikuwa anaimba Kikaguru, hivi si tuna waumini wakaguru humu!!?” aliuliza mama mwingine

“Eee tunaye mmoja lakini yule ni chawa wa mama Mchungaji, hatuwezi kumuuliza…”

“Sasa yule binti mbona alitoka hakuendelea kubaki kwenye ibada…?” aliuliza mama mwingine

Wakati huo kikundi hicho cha waumini kilikuwa kinaelekea eneo moja la makazi ndio wakajikuta wanapiga soga namna hiyo, kwa upande mwingine pia makundi ya waumini walijadili suala lile huku wakielekea makwao.

“…Ni kama vile alikuja kutoa yule mtoto pale mbele na kumpeleka ma mama yake kisha kuondoka, kama vile alikuja kumuokoa, si ndiyo…” alisema yule dada na wote wakaangaliana pale kisha wakaguna.

“Msigune, ndio hivyo, mimi najua hata wale wanaotoa ushuhuda ni ushuhuda wa uongo, wameandaliwa wale…” alisema tena yule dada

“We mwana we!, hebu funga domo lako!” yule mama aliye mkanya awali akarudia kumkataza asiropoke.

Majadiliano yaliendelea hadi watu walipopungua na kubadi wachache kisha hao wachache wakashika njia tofauti na njia ya mama Onesno Junior na mama Rose, wao wakawa na njia yao peke yao iliyo wapeleka moja kwa moja hadi nyumbani kwao.

“Mama Rose, wewe umejifunza nini?!” aliuliza Vai

“Mmh, Mwenzagu, makubwa!, hebu tuwe tunaudhuria haya maombi kuna mengi ya kujifunza…” Mama Rose hakujibu swali ila alipendekeza jambo.

“Tuwe kila siku jioni tunawaita wale wana maombi na wa kule kkkt kwa pamoja tufanye maombi hapa nyumbani labda tutang’amua jambo.”

Wazo lile likapita bila kupingwa na nyumba ya Vai sasa ikawa kama Kanisa, kila siku jioni kuna watu wane hadi watano walikuwa wanakuwepo kwa ajili ya maombi.

Zoezi la maombi lilipelekea kuchelewa kulala na kufanya lile tukio la mtoto kubadilishwa nepi usiku kila siku kujirudia na kuwa kama la kawaida.

“Inawezekana ni yule mtoto ndio anakuja kumbadilisha Junior nepi” Mama Rose alisema alipo shirikisha jambo lile ambalo sasa limekuwa kama la kawaida.

“Labda, lakini ngoja nifunge na kuomba kwa siku tatu ili nione kama Mungu atanionesha anayekuja kumbadili mwanangu nepi…” Vai alisema.

Baada ya siku tatu za maombi, usiku wake alishtuka usingizini na kukuta mtoto amebadilishwa nepi, nyingine zimefuliwa na mlango ulitoa sauti ile ya kufungwa kitu kilichomstua Vai.

Ni kwamba, tangia siku ile watoke kule kanisa la mama Mchungaji, Vai aliamua kutofunga mlango wake ili iwe rahisi kupata msaada kama kuna jambo limetokea. Sasa siku hiyo alipostuka usiku wakati mlango unafungwa ndipo akakimbilia kuangalia nani anayetoka mle ndani…

Kwa mbali aliona mtu mzima mwamamke akiwa amejitanda khanga akitoka, lakini aliona mgongo tu na wala hakusikia vishindo vya nyao za kutembea, na kabla ya yule mtu tupotelea mlangoni aligeuka nyuma na wakakutanisha macho…

Inaendelea…

Tupio la VIII – John Mutalebwa

John Mutalebwa, ni kijana mtanashati mwenye mwili wa mazoezi na majigambo mengi. Ana gari aina ya Harrier alilonunuliwa na baba yake Mzee Mutalebwa ambaye ni kiongozi wa kisiasa na mwenye nguvu kwenye chama chake akiwakilisha wananchi katika moja ya wilaya za kanda ya Ziwa. Kiongozi huyu wa kisiasa ametuhumiwa mara kadhaa kwa utakatishaji fedha na biashara haramu lakini hapakuwa na ushahidi wa kumtia hatiani.

John, ambaye sasa anaingia mwaka wa tatu katika chuo cha usimamizi wa fedha IFM ndiye aliye mshawishi Emmy kwa kumnunulia Iphone 14 na kumuahidi maisha mazuri akimuacha Alex. Lakini John kama ambavyo inajulikana kwa wanafunzi wenzake wengi wa darasa lake, ni mtu wa kubadilisha wanawake sana kwa kutumia nguvu ya kifedha aliyo nayo.

Neema, Rachel, Margareth, Lidya, Zaituni na Laura hawa wote walijuwa kuwa urafiki wa Emmy na John hauwezi kudumu kwani John akipata mwanamke mwingine mzuri kuliko Emmy, atamfuata huyo na kumsahau Emmy kama alivyowaacha Catherine, Rebeca, Pauline, Martha, Pendo, Zubeda, Zainabu, Khadija na Lucy ndani ya miaka miwili ya chuo. Na hao ni wanafunzi wenzake, sijui huko kwingine hali ikoje.

Baada ya Emmy kushawishika kwa ‘outing’ katika hoteli kubwa kubwa na sehemu zingine mbalimbali za starehe, Emmy aliamua kuvunja uhusiano wake na kipenzi chake cha utotoni Alex mbele ya hadhara tena kwa maneno ya kashfa na aibu. Hakuna aliyependa kitendo kile cha Emmy kumfanyia Alex vile…

Zaituni bado alikuwa na simu aliyoitupa Alex, siku hiyo aliamua kumkabidhi Alex simu yake.

“Alex, mambo?!” alisema Zai huku akimkaribia Alex.

“Poa Zai, vipi shwari?” Alex alijibu vizuri tu kama kawaida yake. Alex pale chuoni alikuwa maarufu sana kwa kuuza vocha za kurusha za mitandao yote, biashara iliyomsaidia kujenga urafiki na wanafunzi wenzake na kujikimu kiaina.

“Nimekuletea simu yako, nimeibadilisha na kioo tachi (touchscreen) maana siku ile ilipasuka…” alisema Zai huku akimkabidhi ile simu Alex, Alex akaipokea na kuiangalia kisha akasema…

“Ahsante Zai, wewe ni mwema sana, una roho nzuri, Bwanaako atafaidika sana…” kisha wote wakacheka…

“Kwanza jamaa yako mwenyewe yuko wapi…” aliuliza Alex

“Yule palee kwenye…” alijibu Zai huku akionesha upande alipo boy friend wake.

“Ni yeye aliyenipatia hela ya kubadilishia kioo hiki…” aliongezea Zai.

“Ooh, basi twende nikamshukuru naye pia…” alisema Alex.

Baada ya hatua chache wakafika alipo Jafari, boyfriend wa Zaituni…

“Oyaa Jeff vipi?” alisalimia Alex

“level kama kawa..” alijibu Jafari.

“Nakushukuruni sana kwa ukarimu wenu wa siku zote na wa kuitengeneza simu hii…” Alisema Alex.

“Usijali babu, sio kitu, mbona kawaida tu!...” alijibu Jafari.

“Nawashukuruni sana, lakini hata hivyo naomba uridhie simu hii nimpatie Zai iwe yake moja kwa moja…” alisema Alex.

“Vipi kwani hujaipenda, au kioo kimebandikwa vibaya?!...” aliuliza na kushangaa Jafari.

“Hapana, hii niliyonayo infinix inanitosha, hata hivyo hiyo Samsung ina kumbukumbu nisiyopenda kubaki nayo, Zai pokea simu hii iwe yako, kuwa huru nayo…”

“Shukran Alex…” Alisema Zaituni kisha naye Jafari akamalizia..

“Haina noma jomba, basi tukapate chakula pamoja …” ilikuwa mida ya lunch.

Wakawa wanaelekea sehemu ya kupata chakula na Jafari hakuacha kuchagiza…

“Ila mwanangu Alex, ulimnunulia simu kali demu wako, sema hana shukrani tu, Samsung latest kabisa!...”

“Yote maisha tu mwana! Ila nini, atajuta! Maana alipoangukia sio penyewe…” Alex akajibu na wote wakaangua kicheko…

Jafari na Zaituni wapo kwenye uhusiano takribani miezi kumi sasa na wapo vizuri maana Jafari hana ‘mambo mengi’ wala Zaituni hayupo ‘macho juuu juu’
---

Alex akapata ‘text msg’ akialikwa nyumbani kwa dada yake Qeen jioni ile.

“…Jitahidi leo chakula cha jioni uje kula nyumbani Tabata…” ilisomeka sehemu ya ujumbe ule.

Ilipotimia saa kumi na mbili na nusu jioni, Alex alifika nyumbani kwa dada yake, akakaribishwa vizuri na kukutana na rafiki wa dada yake aitwaye Maurine ambaye ndio wamepanga nyumba nzima pamoja ila wamegawana upande kila mmoja anajitegemea.

“Karibu sana Alex, hapa ndipo ninapojifichaga, na huyu hapa ni Mourine, rafiki yangu kwa muda mrefu sasa…” alisema Queen akimkaribisha Alex.

“Karibu sana Alex…” alidakia Maurine na akamsogelea na kumkumbatia…

“Ahsanteni, nimeshakaribia…” alijibu Alex na kujitoa kwenye kumbatio ambalo lilianza kumpa hisia tofauti.

Maurine ameumbika, ni mrembo kuliko Queen kwa macho ya wengi, ila Queen ni smart sana kichwani kuliko Maurine. Wote wana maumbo mazuri yenye kuweza kushawishi wanaume…

Maurine, kahaba mwenzie na Queen, alikuwa ana muonekano mdogo kuliko Queen kimaumbile ingawaje walikuwa wamepishna mwaka mmoja tu kuzaliwa, unaweza kusema Maurine alikuwa ‘portable’ zaidi kuliko Queen.

“Alex jisikie huru, hapa ni nyumbani, natoka kidogo kuchukuwa kitu dukani kisha narudi…” Alisema Queen kisha akakazia…

“Mourine, mkirimu mdogo wangu kwa kinywaji apendacho, ‘usimkomaze’ narudi sasa hivi…”

“Hahahha dada jamani, mie wa ‘kukomazw’ na huyu!...” nilijichekesha pale kuonesha uchangamfu lakini nilikuwa najuwa nia ya dada kwamba niwe makini asije akanishawishi ujinga.

“Simkomazi da Queen, utamkuta salama salmin…” alijibu Maurine huku akitabasamu.

Nyumba waliyopanga ilikuwa mbali kidogo na huduma za maduka, hivyo ilitarajiwa kamuda fulani kangepita kidogo kabla ya Queen kurudi. Ni kwamba Alex aliwahi kufika kabla ya dada yake kuandaa mambo ya msosi, hivyo ilibidi aende barabara kuu kuangalia kitoweo alichopanga kukitumia siku hiyo na nduguye wakati wakijadili mambo yao.

“Sikujuwa kama da Queen ana kaka ‘handsome’ hivi…” aliachombeza Maurine wakati Alex akiwa bize na simu yake…

“Unapenda kinywaji gani Alex…” Alimuuliza

“Eeee nipatie sprite baridi…” alijibu.

“Soda?! Kwani upo kwenye dozi au?...” alishangaa Maurine

“Hapana, situmii kilevi tangu zamani…” Alex alijibu.

“Makubwa! Queen ana kaka mlokole!...” alisema huku akimfungulia soda na kummiminia kwenye glasi.

“Kwani walokole peke yao ndio hawanywi pombe?..” Alex aliuliza ili kunogesha stori…

“Najuwa sio walokole tu, je sigara unavuta?!...” aliuliza swali chokonozi…

“Hapana dada, sinywi pombe wala sivuti sigara…” Alex alijibu

Maurine akacheka kicheko cha kimbea kisha akasema…

“Niite tu Mourine bhana, na nimeshajuwa kilevi chako heheeee…”

Basi mazungumzo ya ‘kuchangamsha genge’ yaliendelea bila madhara kwa Alex hadi dada yake aliporudi na kuwakuta wakiendelea kuongea wakiwa wote wachangamfu…

Chakula kiliandaliwa, wakala wote watatu kwenye sebule ya Queen, lakini baada ya kula tu, Maurine aliaga kuwa anawahi kazini…

“Dada utanikuta, natangulia pale pa siku zote pa kuanzia…” alisema Mourine.

“Sawa, mie nitachelewa kidogo, nina mazungumzo na Alex kwanza.” Alijibu Queen na Maurine akaingia upande wa vyumba vyake kujiandaa na mtoko.
---

“Eee nimekuita hapa ili kwanza upafahamu nyumbani ninapoishi pia kujadili mawili matatu kuhusu kikao cha kule hotelini siku ile na tatu kukuambia kuhusu ujumbe mfupi wa maandishi kwa njia ya simu kwenye ile line niliyoipotezea…” Alisema Queen.

“Karibu sana Alex, hapa ndio nyumbani, maisha yanasonga kama hivi, lakini muda si mrefu tutabadilisha maisha yetu mdogo wangu…”

“Kuna lile swali nilitaka kumuuliza Afande siku ile kule hotelini ukanikataza, mimi naona kama kuna kitu hakija kaa sawa…” aliendelea Queen

“Inakuwaje katika tukio la mauaji kama yale Polisi ishindwe kufikisha upelelezi mwisho na hatimaye ikajulikana nini kilitokea…”

“Nilitaka anijibu pale pale ili roho yangu itulie, nilikuheshimu tu lakini wala sikuona mantiki ya wao kusema busara ilikuwa ni kuacha jambo liishie kama lilivyoishia, haina maana hata kidogo…”

Hatma ya hili jambo ikawa wafanye vikao na watu watatu kila mmoja kwa wakati wake, yaani Kamanda, Jaji na Gavana, lakini kwanza wasubiri wakabidhiwe mirathi yao kisha walianzishe kimya kimya wapate mwanga wa kauli zile za Kamanda kwamba busara iliwapelekea waache suala lile liishie kama vile.

Aidha kuhusiu ile ‘text msg’ aliyopokeaga Queen, Alex alihitimisha kuwa asiipuuzie, wafuatilie baada ya mambo ya mirathi kukamilika maana watakuwa na fedha za kutosha, ingawaje hadi wakati huo hawakujuwa kwenye mirathi kuna nini na nini zaidi ya akaunt za benki.

Itaendelea...
 
Itaendelea Jumamosi ijayo panapo majaaliwa.
Sawasawa 😊🤗
 
Back
Top Bottom