SEHEMU INAYOFUATA......
Tuliagana na Shedy huku kukiwa hakuna maelewano, ni kwamba kila nililoliuliza sikujibiwa ipasavyo,
Majibu yalikuwa mepesi, tuliachana huku wakiingia, kwenye gari lao Toyota RAV4 wakiwa kwenye Mabishano makali hasa kile alichokisia mkewe tayari aligundua jambo,
Niliwasindikiza kwa macho, huku gari yake ikiwa inapandisha kilima fulani inatoa moshi na muungurumo mkubwa sana.
Nilicheka peke yangu,nikajisemea
Yaani huyu kuwa na hii gari ndiyo imekuwa fimbo ya kuweza kutuumiza sisi, kwahiyo anapita majumbani mwetu akitongoza wake wa watu kisingizio hii gari.
Kwa gari gani, hii ambayo inaonekana CC zimeshuka, halafu rejeta yenyewe inachemsha si kafika hapa kafungua boneti naona mvuke umetanda,
Gari hii ukute walitaka kupima chuma chakavu akajikuta anafunikwa na udalali wake wa pupa , nikitaka kununua gari hata leo nanunua hata kwa mtu , kwanza Nina uzoefu mkubwa wa magari nishaendesha sana siwezi kuuziwa mkweche Mimi baada ya muda fulani alinipigia simu akiniomba radhi nikiwa bado nipo palepale waliponiacha.
Nikaipokea .
Ila we Shedy nitakutafuta nishajua ukweli wote malaya mshamba wewe usiyejua kutongoza, unadhani mwanamke gani angekukubalia wakati unaenda kumvunjia heshima mumewe ,hivi wewe wa kumtongoza shemeji yako wewe?
Hapana kaka, hata Mimi nilimshangaa mkeo kunidhuru ila sikuwa na lengo baya.
Muongo wewe,acha upuuzi nimekustahi mbele ya mkeo ili asijue mengi lakini jua kuwa tukikutana Mimi na wewe hakuna maelewano umenikosea sana. Nikakata simu
Hapa Sasa sikuwa na masihara hata mke wangu sikuwa na Imani naye moja kwa moja,
Nikafika nyumbani pitiliza Hadi chumbani,mke wangu kuona ujio wangu alikuja .la kuniuliza aliuliza akajibiwa,
Mke wangu hiyo laki moja aliyoitoa Shedy iko wapi,niliuliza huku wangu ukimtisha mke wangu,
Mmmmh makubwa,hiyo hela ipo Mimi sikuipokea, anayo dada wa kazi vipi nimuite ailete, aliuliza.
Hapana, subiri kidogo hata hivyo Nina maswali kwako nadhani uliniambia ila sikukujibu kwakuwa sikuwa na maelezo ya pande mbili lakini pia hili suala sitaki mama yangu alijue liishie hapa hapa chumbani.
Nilisema.
Mume wangu kama nilivyokwambia ,kwanza hakuna maelezo zaidi ya niliyokupa,
Alijibu mke wangu.
Sasa we ulijuaje kuwa ana nia ya kukutongoza na yule ni shemeji yako,niliuliza,
Hey baba mbona maswali yako siyaelewi, kwahiyo Mimi ningeshindwaje kuelewa Hilo Jambo,kubwa zaidi ,aliongea mengi lakini nikamjibu kuwa kama nahitaji kupumzika,bado alikaa sebuleni,halafu wakati hayo yakiendelea dada wa kazi hakuwepo nikagundua kuwa yule pale ,kajificha makusudi huenda anajua kinachoendelea
Nikamtoa shem shedy kwa nguvu, lakini sababu iliyopelekea nimpige ni baada ya kunishika mkono eti niingie kwenye gari lake tuongee zaidi.
Nilimsifu mke wangu kimoyomoyo,ila nikajifanya sijaridhika na majibu yake.
Nikatoka nje,nikaongea na mama mambo fulani akikazana kuwa yeye anataka kuondoka,hata hivyo wao walienda huko nje ya mji wao na dada walienda kuchukua dawa fulani ili nioge,
Mwanangu wewe bado siku mbili tu ukaripoti huko kwa maboss wako wapya tumeona si vyema ukaenda kazini Ukiwa mwepesi.
Haaaaaa mamaaaaa mtakuja kutapeliwa bure ,nyie si wenyeji wa mji huu mmemjuaje huyo mtu mama yangu,niliuliza kivivu.
Tunamfahamu tangu aje hapa ana miaka mitatu tu,we humfahamu yule baba ambaye alikuwa anapata kifafa miaka ile Ukiwa unasoma shule ya msingi,walimpeleka hospitali za kila aina lakini ilishindikana hadi pale walipompeleka kwa mganga wa jadi ikaonekana ana majini/maruhani ya kiganga anatakiwa afunguliwe ,ili awe mganga na yeye,
Tangu hapo ugonjwa wake alipona na akaendelea na utaalamu wake huku akiwa na wateja sana hata hivyo Kuna miaka mitatu au minne alichukuliwa na tajiri mmoja aje aizindike nyumba yake,ndipo alipokwama huku kwakuwa aliona Kuna wateja zaidi,na hata namba zake za simu tunazo siku nyingi ndiyo maana ikawa rahisi,mama alisema.
Nikaishia kushangaa tu,kwanza huyu jamaa namjua tangu kijijini kwetu, na pia sifa za uwepo wa mtaalamu mkubwa pale pembeni ya mji nilikuwa nazo Ila sikujua kuwa ni yeye hasa ukizingatia Mimi si muumini wa hao watu.
Kumbe Ukiwa na maruhani mtu unaweza kupiga hela eeeh,niliuliza kiutani,
Ndiyo huoni anasaidia watu,mama alijibu
Sasa mama kama haya yanasaidia mbona mkiwa makanisani huwa mnayakemea yamtoke muhusika?
Hebu toka zako huko yaani we Dani hata hukui yaani tukaishia kucheka tu,
Sasa hii dawa mama,naifanyaje?
Hiyo ukaoge,ukienda ukienda kuoga nuizia kabisa mambo unayohitaji na usiyoyahitaji yaani kemea vitu vyote vibaya ni Mara moja tu Haina kurudia,alisema dada yangu.
Nikarudi chumbani nikaiweka mahali safi kabisa kwenye droo,nikarudi sebuleni,kwakuwa huko nje watu walikuwa bize na mambo yao nikaona ni wakati wa dada wa kazi kuongea na mimi nikamwita.
Naomba kujua kipindi Nina matatizo,mke wangu alipiga mtu.
Yaani Mimi Nina matatizo na yeye anatafuta matatizo,hebu nieleze ilikuwaje maana aliyepigwa ni rafiki yangu.niliuliza
Kiukweli shemu, yule rafiki yako sijui yupoje,alikuja hapa mchana akamuulizia dada,nikasema hayupo.
Lakini baada ya nusu saa,
Alirudi Tena,nikamuuliza unamtaka wa nini akasema, wewe una matatizo kwahiyo anataka waende wote ili wakusaidie,akaniachia laki moja kwamba nimpe dada akirudi Kisha akaondoka.
Baadaye akarudi Tena ,Mara ya tatu ilikuwa saa moja jioni dada akiwa hajarudi ,safari hii akawa anashuka kwenye gari, anataka kuingia ndani
Nikamzuia nikimwambia dada anakataza watu kuingia na Sasa ni usiku hutakiwi kuingia humu ndani.
Lakini alinitolea lugha Kali kwamba ,
Yeye hapa ni kama kwake,alisimamia nyumba hii kipindi inajengwa, kuanzia tofali na vifaa vyote alileta yeye,akanitukana nikajimbilia chumbani kwangu,
Baada ya muda kidogo dada akarudi, wakasalimiana, wakawa wanaongea vizuri tu,lakini dada nilimsikia akisema yule rafiki yako kaja usiku kufanya Nini kwetu,
Akajibu atulie kwanza atamwambia,
Ndipo dada alipoanza kumsukuma atoke nje, na walipofika nje nikasikia yule rafiki yako akilalamika ameumizwa ,akaondoka.
Siku hiyo dada nilimtengea Chakula hakula huku akiwa anatukana sana ,na akawa anaongea peke yake.
Ningekuua malaya wewe, kwahiyo kama umetembea na ESTA, unadhani utanipata na Mimi kwanza nilikuwa nakuheshimu sana kumbe wewe ni bure kabisa, alimalizia dada huku akienda kulala chumbani bila hata kuoga,
Asubuhi ilipofika,nilimpa hela nilizopewa Jana na yule rafiki yako,alizikataa huku akinilaumu nilipokea za nini nikamwambia nililazimishwa tu,
Akasema nikae nazo mpaka mwaka utakaporudi.
Inaendeleaa........
Bado mbichi hii