SEHEMU INAYOFUATA...........
Nilitulia ofisini huku tayari nikiwa nimevurugwa si kidogo,
Sasa itakuwaje kumbe yule dogo ana ukaribu na madam, Sasa hospital tenaaaaa..... Nilipanga na kupangua huku nikishindwa kupata jibu kamili, hata muda wa lunch ulipofika sikuweza hata kula maana tayari nilikuwa na hofu kubwa.
Niliomba ruhusa ya masaa mawili ili nielekee hospital ya taifa ambako niliambiwa na MADAM tukutane,
Nilipofika nilikuta baadhi ya ndugu wa yule kijana, wakiwa naye nje kabisa tayari kwa kuondoka naye, nilichogundua ni kwamba dogo Wala hakuumia lengo ilikuwa anitengenezee msala.
Niliwasalimia wote huku wengine wakiitikia kwa sauti ya chini, lakini Kuna mama mmoja alianza kunitolea lugha chafu.,
Yaani umeshindwa kumuua jana, ukasikia bado yuko hai na anapumua ukaona Bora uje ummalizie kabisa,
Haya muue huyo hapo. Fanya lolote mwanaume wewe. alibwata sana yule mama huku kama mjuavyo umati kwenye ile hospital nikaona Bora niondoke tu, wakati najiandaa, kutoka nilidakwa na maaskari waliovaa kiraia huku vitambulisho vyao vikiniaminisha.
Hivi kumbe ni huyu jamaa, mbona hata hafanani na kupiga mtu , ujue kidogo nibishe yaani Wala huwezi kumdhania,
alikuwa ni afande mmoja ambaye alikuwa akimuuliza mwenzake kama ni Mimi.
Sasa bwana Daniel, tunaomba utwambie tairi za gari ya jamaa ulipeleka wapi, maana tulichogundua ni kwamba Kuna watu uliwapanga mje mmvamie dogo, halafu mkamwibia, maana wakati wewe ukimburuza Kuna vijana uliwaandaa kwaajili ya kukamilisha mpango wenu, haya tuambie vifaa viko wapi.
aliuliza afande aliyekuwa anaendesha gari ndogo hivi vi crown.
Kwa uzoefu wangu sijawahi kuulizwa maswali njiani nyie tufike kituoni Kisha mengine yatafuata, niliwajibu kijeuri huku simu yangu ambayo tayari waliichukua wao, ikaita.
Afande Ommy, hii simu ya hiri jambazi inaita huenda ni majambazi wenzie wanampigia, alisema Afande ambaye tulikaa siti za nyuma Mimi na yeye, kucheck jina la mpigaji ni Rose, aisee moyo ukiniuma sana
Yule afande akapokea simu huku akiweka loud speaker na kuniamrisha niongee.............
Hello my vipi tena, nasikia Kuna maaskari wamekuja hapo ofisini kwako wakikuulizia, inaonekana hawana Nia njema na wewe , kwani Kuna Nini kimetokea , unaniumiza ujue, aliongea Rose bila hata salamu.
Tayari wameshani arrest ila tutaongea, baada ya kugundua Niko nao akakata simu.
Huyu unamwitaje kwanza maana anavyoongea ni kama mke wako, na ulivyomsevu ni tofauti.
Atakuwa ni malaya wake tu huyo, au anashirikiana naye kwenye wizi, waliongea kwa kupokezana wale maafande huku wakiwa wameniudhi pakubwa.
Hatimaye tulifika kituo fulani ambacho sikujua kwanini wamechagua kituo kile, tulishuka kwenye Lile gari huku ukali wa majamaa ukiongezeka (Wana sifa Hawa maaskari basi tu)
Kushuka nilimkuta MADAM akiwa na wapambe kadhaa , pamoja na wale ambao niliwaacha hospital pamoja na yule kijana niliyempiga, nikagundua kumbe ndiyo maana walikuwa wananizungusha lengo lilikuwa Hawa watangulie kufika.
Haya vua mkanda, vua viatu halafu una viatu vya gharama kweli, ulivipiga wapi maana we una mbinu sana kwenye kuiba. aliongea yule afande niliye sikia akiitwa Ommy, au Omari
Hapana naomba nimsikilize kwanza akiongea upuuzi namwacha hapa hapa , aliongea madam ambaye kwa uzito wake anaheshimika sana kwahiyo akasikilizwa,.
Enhee hebu tuambie ilikuwaje maana Mimi ninavyokujua nimeshangaa, tumefanya mambo mangapi wewe tolu, Hadi imefikia tunaishi kirafiki sana , kwanini ulimpiga huyu mtoto sisemi kwakuwa yupo na Mimi, ni kwamba hata angekuwa mtu hapaswi kujichukulia Sheria mkononi.
aliweka kituo.
Kwanza samahani madam kwa usumbufu wote, lakini pili nikushukuru kwa kuweza kunipa nafasi ya kusikilizwa Kabla sijawekwa lockup, story iko hivi.. nikawasimulia yote kuanzia uwepo wa dada yangu Hadi anauzoea mji na kuanza kurubuniwa sisemi kwamba lilikuwa ni kosa dada yangu kuwa na mwanaume tatizo ni utaratibu uliotumika,
Kama huyu kijana angekuwa anamtaka Dada yangu kiheshima yasingetokea yote haya...
. Kabla sijamaliza
Lakini wewe jamaa unasema Dada yako aliaga anaenda mkoani ila yeye Ndiye akaenda kwa huyu jamaa hivyo Mimi sioni kosa lake huyu, kifupi alifuatwa mwenyewe, aliongea mmoja wa maaskari akimtetea yule dogo kwamba Hana kosa.
Kipande hiki madam alikielewa sana, inaonekana alivyoelezwa ni tofauti na maelezo yangu.
Ni kweli ulikuwa na mwanamke kwa kipindi Cha wiki nzima, aliuliza MADAM akimgeukia yule Dogo.
Akajibu kwa kutingisha kichwa.
Jamani ndugu zangu naombeni Hawa niwasuluhishe mwenyewe, maana wote wapo upande wangu maana mzizi nimeshaupata , alizungumza madam, akiwaambia wale maaskari.
Sasa mama sisi tumeshamuweka kwenye detension , kuhusu shambulio na wizi wa vifaa vya gari la mlalamikaji, Sasa unavyosema utamaliza mwenyewe naona si vizuri maana, kweli inaonekana bwana Daniel alikasirika kuhusu dada yake, lakini swali, kwanini achukue sheria mkononi? Huoni hii ni jinai mama, aliongea afande Fulani ambaye alikuwa na cheo Cha koplo Huku akijichekesha chekesha kwa kumuogopa Mama.
Hapana afande naomba nieleweke hivyo, aliongeza MADAM Kisha tukaondoka.
Safari iliishia kwenye mgahawa Mmoja Huku tukifika kwa mafungu maana wengine walipanda daladala kwakuwa gari ya MADAM ilitosha watu wachache, tulisuluhishana Huku ikionekana gari ya dogo walifungua ni wale marafiki zake, lengo siyo wamuibie lengo wanizidishie kosa, kwa hiyo ikaonekana wazi tairi zote zipo hivyo Madam akaamrisha zikarudishiwe .
Tuliagana huku madam akinionya sana, kuhusu kudhibiti hasira zangu akidai tungekuwa hatujuani mimi na yeye tungeongea mengine.na pia kama yatajirudia ataweka ujuwani pembeni
Nilifurahi yale matatizo kuisha huku nikitazama saa ikionekana ni saa tatu usiku, nikampigia mke wangu ambaye huwa anakereka sana kuhusu kurudi usiku.huku nikimsimulia kwa kifupi mkasa wangu.
Nilifika nyumbani, siku hiyo nikipokelewa vizuri sana na mke wangu, licha ya kuwa alikuwa bado kanuna kutokana na vibao nilivyomzaba Jana yake, lakini kusikia nilikuwa polisi, alihuzunika sana,.
Yaani Leo mke wangu, kama asingekuwa yule boss wangu, mngesikia Niko mahabusu, yaani mbona ingekuwa balaa.
Mmmh mume wangu ujue nafsi yako tayari imejenga urafiki na vituo vya polisi, naiona hiyo evil spirit ikikuandama tayari, hebu jaribu kufanya hata maombi mume wangu Kuna roho si nzuri kwa upande wako, tatizo hata kanisani mume wangu umekuwa mvivu, lakini pia nilikuonya Jana kuwa unalotaka kufanya utapoteza haki hako bure tu.
Hebu fikiria baada ya kugundua kuwa dada yako yupo, sehemu fulani wewe ungeripoti polisi huku ukiwasaidia kuwajulisha mahali alipo mtuhumiwa huoni kama ingekuwa heko kwako yaani hao maaskari unaosema walikuwa wakikukejeli Leo pengine ungekuwa nao Jana mkimfuata huyo mtuhumiwa.
Pole sana mume wangu, ulinipiga Jana umeniumiza, ni mzazi nahitaji UPENDO na ukaribu wako, lakini bila kujiuliza Mimi ni nani ulirusha kibao hadi nilishangaa ni huyu huyu mume wangu kweli, ona Sasa yaani umeponea kwenye tundu la sindano sijui ingekuwaje, yaani Mimi tena na mtoto mgongoni, mahot pot na chupa za chai huku nikitafutiza wadhamini eti upate dhamana hivi unajisikiaje mume wangu!
Unanionea sana halafu mume wangu ni mpole, mcheshi mnyenyekevu yaani hata marafiki zangu Kuna muda wanakumwagia sifa Hadi naweka wivu lakini unaanza kubadilika mambo ambayo ulitakiwa kuyafanya ujanani unafanya ukubwani , si umechelewa tu kupata watoto wewe pengine ungekuwa na mjukuu. aliongea mke wangu huku nikiwa simpingi kwa lolote, aliongea kweli tupu, japo nilitamani niwajue hao marafiki zake wanaonimwagia sifa.maana nilishakuwa wa moto.
Kesho asubuhi ya Jumanne nilipiga suit fulani ya kijivu huku nikipiga tai fulani , hata nilivyopanda kwenye daladala Baadhi ya abiria wasiowavumilivu wakasema hata wewe kiongozi unapanda humu , au unaigiza movie.
Nilishuka huku nikisindikizwa na kejeli, mnamuona Boss eti sababu kavaa hiyo suti Hawa ni matapeli wa mjini huenda, hata anapolala hapajulikani, wengine wakiniita Yahya wakifananisha alivyoimba Lady Jay Dee, walimwengu bwana.
Nilifika ofisini huku, yule dada ambaye niko naye ofisini akinishangaa,
Mr, yaani hata siamini Jana Kuna PT(yaani gari la polisi) lilikuja hapo nje waliingia ndani wakakukosa , yaani nilikosa amani kabisa, mbaya Zaidi sikuwa na salio nikupigie, ili nikustue , bahati nzuri Da Rose alinitafuta ikabidi nimuelekeze kuwa akupigie ili akustue kuwa unatafutwa,.
Lakini alinipa jibu kuwa umeshakamatwa, hatukuwa na namna Mr,. yaani ingekuwa huna mke tulipanga tukutafute tungejua tu upo kituo gani ila tulihofu tusijegongana na mke wako. tutasema sisi ni akina nani, alisema yule Binti.
Sasa na wewe , si mngekuja tu mnamwambia kuwa sisi tunafanya kazi ofisi Moja, kifupi ni heshima tu kwake kwani kungekuwa na ubaya gani, nilimtega .
Weweee mwenzangu hatungeweza sisi,. Aliongea yule Binti huku nikifikiria jambo kuwa kwani dada yake kashamwambia kuwa yuko karibu na Mimi, ila huwenda maana hata umri hawajaachana sana pengine huwa wanaambizana .
nilijisemea.
Halafu Mr Daniel uliwasiliana na Dada maana tangu jana hata leo asubuhi alinipigia, akiulizia maendeleo yako, hebu mtafute mtoe hofu basi, aliongea yule Binti almaarufu kwa jina la Janet. ni la Binti Fulani kana nyodo sana na utoto mwingi sana , hata waliomleta kwenye ofisi yangu walilenga apate uzoefu fulani.
Nikapiga simu baada ya kuona nishafanya setup ya mambo yangu.
Haloo my, habari za asubuhi. nilimsabahi kwa uchangamfu Rose.
Hata siamini kama ni wewe haya nambie imekuwaje, aliuliza
Nilimwambia mwanzo mwisho huku nikimdanganya kwa asilimia tisini , sikutaka ajue mambo yangu hasa suala la kumpiga mtu maana ningejishushia heshima yangu.
Basi Sawa , usiku wa jana nilikuwa zamu hata hivyo leo niko free tunaweza kuonana baada ya kazi ili nikupe pole? aliongea Rose
Huku mwili ukinisisimka kutokana na ile kauli niliyoambiwa,
Haina shida Haina shida, nilimkatisha ili mdogo wake asielewe mambo yetu,
Nilipiga kazi huku Kila saa nikimuwaza Rose, namna atakavyonipa pole kutokana na misukosuko ya jana iliyonipata.
Kiufupi Rose alishanipenda tayari.
Siyo kupendwa bure lakini, ni kwamba Mimi ni mhongaji mzuri nikiwa nazo , hizi miatatu mianne kwangu kawaida.
Mida fulani ya mchana nilipokea simu toka kwa mke wangu, akiniagiza vitu fulani,
Sasa mume wangu, Leo uwahi kidogo Nina mazungumzo na wewe , lakini pia Kuna muda ESTA alinipigia simu eti ana mazungumzo na Mimi, hata sijui anataka kuongea Nini na miye nilitaka anipe hata utangulizi kidogo ila kadai atakuja hapa hapa, alimalizia Mke wangu.
Nilikauka kama nimepigwa electric shock maana baridi si baridi na joto si joto, sikumjibu kitu mke wangu.
Nikakata simu yake ili nimpigie ESTA huku nikiwa nusu kwa nusu nimchane kuwa ole wake nisikie kile alichokiona siku ile, au nimtongoze, yaani nimwambie tukutane somewhere, sikuweza kuopt kitu muda ule. Nilikuwa njia panda.
Itaendelea.............................