Simulizi: Mimi na Boss Wangu

Simulizi: Mimi na Boss Wangu

Emotional instant gratification is the real problem to us. Just to hold them it become unbearable.
 
Tolu hajatoka kwa esthee au yupo kwenye proces za kumuozesha dada yake kwa bishoo aliyemtwanga
 
SEHEMU INAYOFUATA...............

Nilimpigia ESTA akapokea simu huku nikisikia makelele mengi sana sauti za wanawake wanaoonesha ni wengi.

Hello shemu, naona umenikumbuka vipi kwema,. aliongea ESTA Mara tu baada ya kupokea simu.

Mimi mzima, ila nilikuwa na maongezi na wewe, na ni vyema tungeonana tu maana hayatoshi kuongea kwenye simu. niliongea kwa sauti ya kiume na ya upole.

Mmh shemu mbona unanitisha salama kweli, ila si mbaya unaweza kuja japo sipo kule unakokujua saloon nimehamishia (akitaja sehemu ilipo)

Nilipajua aliponielekeza, ilikuwa ni sehemu palipochangamka sana, nikachukua Bajaj hadi eneo alilonielekeza, nilishuka huku nikimuona ESTA akiwa na kundi la wanawake wapatao kumi na mbili,
Wakiwa kama wanaagana hivi.

Baada ya kuniona Mimi aliwaruhusu wale wenzake huku akinikaribisha, Mimi,

Dah hongera sana yaani hii ni saloon ya kimataifa, congratulations my second wife. niliongea kwa kuipongeza ile saloon, ukweli niliona hata aibu kiukweli saloon ya Sasa ilikuwa na Kila kitu kwanza kilikuwa frem kubwa,likiwa na chumba kingine

Vioo vizuri na Yale yakukaushia nywele yakiwa ya kutosha.

Umeniitaje shemu, aliuliza huku akitabasamu.

Kwani wewe umesikiaje. huku nikimkazia uso.

Eti my second wife, una balaa wewe, alijibu huku akiniangalia kwa kuibiaibia.

Ila tuache masikhara,shemu unavutia sana, yaani tukipoteana siku tatu tu nakuona mpya , wakati wenzio wanazeeka we unarudi kwenye utoto, mtu ukimwambia una miaka 25 anakubali, nilimsifia kinafiki.

(Akicheka sana) uwwwwiiiiiiiiiiii
usinichekeshe, naona leo umekuja rasmi kwa kazi moja kunisifia, lakini mbona Mimi najiona kawaida?
aliongea kwa kudeka kisichana flani hivi.

Hapana unajua Nini, wewe una ule uzuri wa asili, akhi unanivutia sana shemu huwezi amini,natamani hata ungekuwa mke wangu wa pili, siyo kimada bali mke
niliongea huku nikijisemea liwalo na liwe.

Tulipanga kukutana kipindi kile lakini ulirusha,najua matatizo yalipelekea Ahadi yetu ikavunjika, lakini bado Kuna chance nyingi zilipatikana za kuweza kuongea au kufaidi uzuri wangu, siku nilizokaa kwako ndiyo kabisa, kabisaaaa hukuonesha hata dalili ya kuwa karibu na Mimi,

Nimetoka ukanipangia chumba, karibu kabisa na kwako lakini bado hukuniambia maneno hayo leo imekuwaje?
Makubwa mwenzangu.
alionesha kushangaa.

Sikia ESTA siyo tu unisikie Bali nisikilize, Mimi nayajua mapenzi, najua nahitaji kuwa na mwanamke kwa wakati gani, nisingeweza kukutongoza kipindi una matatizo yaani unapitia kwenye wakati mgumu, huo ni uonevu .

Unapomsaidia mtu, usitumie kilema au matatizo yake ili kujinufahisha mwenyewe, itakuwa si msaada Bali manyanyaso, Mimi nilijua kuwa ipo siku utakuwa sawa ukiendesha mambo yako, hapo ndipo nitakapokutamkia ya moyoni. na wakati wenyewe ni sasa.
niliongea kwa kumtega .

Mmmh haya bwana, wenzio wengi wanajua Nina ukimwi hata mkeo aliniambia live ile siku tuliyogombana. aliongea kwa unyonge ESTA.

Kwani ni kweli una ukimwi, na kama ni kweli umechukua hatua gani, maana ni vyema ukaitambua afya yako, ili tu ujijue na kama Kuna taratibu zitafuata basi utaishi tu, mbona watu wanaishi, kufa ni kufa tu, vifo vipi vya aina nyingi, Tena asilimia nyingi watu hawafi kwa VVU nikwambie.

Unajua baada ya kusikia watu walionisema pembeni kuwa nimeathirika, niliingiza uoga nikahisi ni kweli, nikaishi kwa hofu kwa kipindi kirefu sana, nadhani ile hofu ilipelekea kukonda sana.

Lakini hata mkeo aliamini sana kwamba Mimi nimeathirika, akapanga twende zahanati moja akinisihi kuwa ni Bora tukapate ushauri nasaha maana CD4 zinaweza kushuka nikawa hatarini Zaidi. nikamkatisha kidogo.....

Mke wangu naye, kazi ya udaktari alisomea wapi, nilisema nikitafuta kuungwa mkono

Nilishangaa!!
Nikawaza kuwa si mbaya pengine wananijua, lakini safari ilikufa baada ya wewe kuwa mahabusu . anasema ESTA

Sasa ile siku uliyonipangia chumba , ndiyo siku niliyokuwa nimejilipua na kwenda kituo Cha afya kucheki afya yangu, hata baada ya majibu kuwa negative sikuamini, nilitoka siku hiyo hiyo kwenda hospital ya mission ambapo nasikia hawabahatishi napo nikaambiwa Sina.

Sikuamini baada ya siku kama tatu nikaenda hospital ya (akiitaja hospital fulani ipo karibu na bahari)lakini licha ya kuwa foleni ilikuwa kubwa lakini nilifanikisha majibu yalikuja negative.
Pia juzi Kati Mimi na Nasra,na mama mchungaji (MADAM)walinishauri kuwa ni vyema kucheck afya ili kuwa na amani na kazi yako, kwakuwa safari hii nilikuwa na uhakika kwamba Sina nikaamua kwenda hospital binafsi anayoijua yeye bado majibu yalikuja negative.

Hivyo mama mchungaji baada ya kuona majibu yangu aliwaambia baadhi ya waumini kanisani kuwa, ESTA hayupo kama tunavyimfikiria hali iliyopelekea mwanaume fulani kuanza kurejesha mahusiano upya,

Ni yule ambaye uliamua ugomvi, yule aliniacha baada ya kusikia Nina VVU , hivyo hadi sasa yupo nguvuni hata Leo, alisema ESTA

Hebu niondoke Mimi asije kunikuta hapa ikawa balaa, maana nilimuona ni mtata. nilisema nikijifanya namuogopa yule jamaa.

Weweee hebu Kaa hapo, yule Mimi simtaki mwenzenu, tena sijawahi hata kumfikiria hata huo uchumba walikazimisha waumini wenzangu tu kipindi hicho ila si chaguo langu.

Aliongea ESTA kwa kujiamini sana huku akionesha kafurahi sana.

Tuachane na hayo, sasa tunafanyaje kwenye hili suala maana kiukweli wewe ni mwanamke uliyekuwa kwenye ndoto zangu kitambo sana . niliongea kwa tahadhari.

Ujue Daniel, mimi Sina tatizo na wewe ila mkeo, kwanza hatuelewani kihivyo akija kugundua je, si itakuwa balaa.halafu pia umekuwa wamoto sana Wala sikuamini kama ni wewe, sema nilimwelewa sana mwanamke mwenzangu, ulikuwa na haki baba kwa pale? Salute mwenzangu. aliongea huku nikijua anaongelea suala la Rose.

Huku nikijifanya sitaki kuongelea hayo lakini yeye aliendelea......

Huwezi amini kiroho Cha wivu kiliniuma sana, lakini nikajiuliza kwani Mimi ni mke wake. Nikaamua kupotezea, ila wewe ulimpata wapi yule mtoto, aliuliza na kunifanya nicheke.

Usije kujenga kuropoka kwa my wife nitakumaindi, nilitahadharisha huku nikijichekesha kwani nilisha ona Hana madhara.

Weweeeee(kwa sauti ya upole)
Hivi Daniel Mimi unanichukuliaje, yaani kabisa, nikae na mkeo nimusimulie kwanza naanzaje, ujue mwenzio huo uswahili hata Sina basi tu, ni maisha tu haya tumeona makubwa zaidi ya ya kwako lakini watu tulikaa kimya tu,, aliongea akionesha hajapenda nilivyomchukulia.

Basi basi nakutania tu kwanza Mimi nakuamini sana.nilimpoza baada ya kujiridhisha. tuliongea mengi huku yeye akiwa addicted na Mimi yaani macho yake tu yaliongea, kiufupi ESTA alikuwa akinielewa siku nyingi ila ni Mimi huwa nayeyusha

Wanaume wenzangu wanajua hili, mwanamke akikupenda Wala hutumii nguvu, ni kiasi Cha kubonyeza tu kama unavyoliendesha gari, Mara ukanyage accelerator, Mara brake yaani wewe tu.

Tuliagana na ESTA baada ya kuitwa na wafanyakazi wake akawape maelekezo. huku akiwa hapendi niondoke. Shemu nisubiri kwanza Nina maagizo kwa mkeo, aliniambia.

(Baada ya kurudi)
Unajua ilitakiwa nifike kwa mke Leo hii sema Nini, kwakuwa tumeonana naomba ukamweleze na umpe haya makaratasi akajaze,

Hebu kwa ESTA mke wangu hawezi kujaza kitu hakijui pia Mimi sijui hata makaratasi yanahusiana na nini,. niliuliza

Samahani sikukwambia ni kwamba Kuna shirika binafsi kutoka Uingereza linakuja kutoa msaada kanisani, kwahiyo Kuna vigezo lazima ujaze kwenye hizi form (akinionesha zile sehemu) na msaada utatoka kwa makundi , huku kila kikundi kikitakiwa kuwa na watu kumi na tano tu.

Hivyo kwa heshima yako, ulivyonipigania Hadi Mimi kuwa hivi nikaona, Bora mkeo awe sehemu yetu hivyo nilitaka niende Leo lakini kwakuwa tumeshaonana hakuna shida utampa ajaze huku hiyo karatasi ikiwa ndiyo utambulisho rasmi mwambie aitunze sana.aliongea kwa msisitizo huku tukiagana.

Kuna kitu nilishanote kwamba kumbe ESTA kwenda kwa mke wangu alikuwa na mambo yake sivyo navyofikiria. Nikawa na amani kiasi.

Nilifika home usiku wa saa mbili huku baada ya kusalimia nikatoa Yale maelekezo ya ESTA kwa mke wangu.

Ina maana siku hizi ESTA mmekuwa mkionana sana, maana aliniambia atakuja, lakini nashangaa hajafika na wewe ndiye umeleta hii ripoti.
aliongea mke wangu huku akinikazia macho.

Unajua Nini mke wangu, ESTA tangu agundue kuwa kwenye Yale mambo yake na MADAM, nilikuwa nafanya si kwa kumsaidia Bali kwa kujinufahisha alinuchukia sana, umesahau nilikwambia?

Eeeehh nakumbuka. alijibu mke wangu.

Sawa, hivyo Kaa ukijua kuwa ni kama katuchukia fulani hivi,hivyo baada ya wewe kuniambia kuwa anataka kuja hapa nilipata hofu, ikabidi nimzuie kuwa asije haupo , lengo nikutane naye nimsome na nijue ana lengo gani, baada ya kugundua ni kuhusu haya ya misaada ya watu wa ulaya ni nikaona si mbaya, nikimdanganya mke wangu.

Oooh very nice my husband, kumbe unatupenda eeh. aliongea huku akionesha kanielewa .

Ni kweli nawapenda sana, na ni jukumu langu kuilinda familia yangu. nilimalizia kwa tambo.

Usiku niliwaza namna nilivyocheza kete vizuri kwa ESTA ili kile alichokiona siku ile asijesema Wala kuropoka kwa mke wangu, lakini hata hivyo ESTA ni amemature hawezi kuwa na huo upumbavu. Na pia ESTA hajanikaa sana moyoni sijui kwanini, nikajikuta siwezi hata kusisimuka , tofauti na Rose ambaye nikiona tu anapiga moyo wenye tamaa za ngono unapiga paaaah.

Asubuhi ilinikuta ofisini, pia nikawa na siku nzuri sana, baada ya kusikia kuwa nitakuwa mmoja wa watu watakaokwenda Marekani ndani ya siku kumi zijazo, nikajisemea kwa maana hiyo Christmas na mwaka mpya nitakula nikiwa kwa Obama?
Furaha yake haikupimika.kila kitu nilichokifanya kilikuwa poa,

Hata Rose alikuwa akinipigia simu, akionesha yupo karibu na Mimi , nilikuwa na amani sana.

Itaendelea ................
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom